Kesi iliendelea katika hatua nyingine, maana mwanzaoni walianza kutoa vielelezo kuonyesha kuwa huyo marehemu hakufa kwa ugonjwa moyo ,kuna shinikizo nyumba yake....na mimi nilikuwa mmoja wa wahusika, ....na ili kuthibitisha hilo, wakatoa vielelezo vya picha, lakini walitakiwa pia watoe ushahidi wa watu,....
Ilionekana walishindwa, kwani wengi wa mashaidi waliowasimamisha, walikataa hata pale waliposhinikizwa kwa maswali, ukumbuke hiyo hotel kulikotokea hicho kifo inamilikiwa na mama Docta,na wafanyaakzi wa humo ni watiifu wakubwa wa huyo mama, alichofanya ni kuhakikisha anawalipa vyema mishahara yao....
Jingine ambalo liliwashindakuthibitisha hayo madai yao,ni kuwa mwili wa huyo marehemu ulikutwa ukiwa ndani yagari haukukutwa hapo, ulikutwa ukiwa ndani ya gari lake mbali kidogo na hiyo hoteli.
Walichoona baadaye ni nikunisimamisha mimi kama shaidhi kwa upande wa
washitaki,lakini kwa namna ambayo hata hakimu alishangaa, na hakutaka kuuliza
sana, licha ya kutulia kwa muda na kusema;
‘Lakini huyu ni mshitakiwa,….’akasemana baadaye akatulia na
kusema niendelee, baada ya kuteta na wenzake na kuwaita mawakili wa pande zote mbili, ambao wote walikubali kuwa haina shida, na utaratibu wote ulipokamilika nikaanza kuulizwa maswali…..Jamani usiombe kusimamishwa kizimbani na kuhojiwa na watu kama hao...inafikia mahali unatamani uropoke ovyo, ...lakini nilijaribu sana kuwa makini.
‘Wewe unafanya kazi gani?’akaniuliza wakili mwanadada.
‘Nafanya kazi mbalimbali, sehemu tofauti-tofauti, ….za
kuajiriwa na za muda…’nikasema baada ya kumwanglia wakili wangu kwa makini,
alitingisha kichwa kuniashiria nijibu, kwani alishanielekeza jinsi ya kujibu maswali
kama hayo.
‘Hebu niambie kuhusu hizo kazi za muda ni zipi…?’ akaniuliza
huyo mwanadada
‘Kama kuuuza duka, au kuwa mhudumu wa hoteli….’nikajibu kwa
mkato
‘Ni hizo tu au kuna kazi nyingine za muda…?’ akaniuliza huku
akinikazia macho. Hutaamini kuwa ni mwanadada,akikuangalia macho yake utafikiri
yanakuona ndani ya ubongo wako na kujua nini unachofikiria, lakini nilishamzoea
na sikuwa na shaka na yeye.
‘Kazi za muda huwezi kutabiri, leo unaweza ukapata kazi hii
kesho kazi hii, mimi kwasababu natafuta pesa sichagui kazi ipi…’nikasema.
‘Huchagui kazi ipi, au sio hata kama utaambiwa kufanya kazi
ambayo hupendelei utafanya tu kwasababu unatafuta pesa ….’akauliza
‘Naweza kufanya ilimradi isiniumize….’nikasema
‘Kazi gani inayoumiza?’ nikaulizwa
‘Kazi zakuumiza zipo nyingi,mfano kubeba zege,…kubeba vitu
vizito…’nikasema
‘Ulishawahi kufanya kazi ya uwakala…?’akaniuliza.
‘Uwakala upi…?’ nikauliza na mimi.
‘Wewe unajua uwakala upi na upi…?’akaniulzia tena swali juu
ya swali
‘Upo uwakala wa kutafuta viwanja, vyumba…nk,
‘Wewe ulishawahi kufanya yoyote kati hizo kazi za uwakala
unazozijua…?’
‘Ndio…siwezi kukataa kwasbabu natafuta pesa nimeshawahi
kufanya…’nikasema huku nikwamwangalia wakili wangu.
‘Kama kazi ipi ya uwakala uliyowahi kufanya…?’ akaniuliza
‘Nyingi tu, kutafutia watu vyumba, viwanja….ni nyingi sijui
ipi hasa unaulizia…’nikasema nikujaraibu kukwepa mtego wake.
‘Katika kipindi hiki cha karibuni, tuseme mwezi mmoja kabla
hujakamatwa uliwahi kufanya kazi y uwakala, kufanya kazi ambayo …’kabla
hajamaliza wakili wangu akaingilia kati.
Hakimu naye akaniokoa na kulizua hilo swali kuwa halina
msingi wa kesi na anachotaka ni kunilzimisha nijibu vile anavyotaka yeye…
‘Wewe kwa kisomo chako, umekuwa ukifanya kazi za uhudumu,
kuuza maduka…unaweza kutuambia ni kwanini ukajishusha kiasi hicho wakati
ulitakiwa uwe ofisini, kama meneja…?’ akaniuliza.
‘Kazi siku hizi hamna nimejaribu kutafuta kazi sawa na
kisomo change sijapata., ..’nikasema kwa kujitetea, na wakati huo wakilii wangu
alitaka kunizuia lakini nilikuwa nimeshajibu.
‘Kwanini usipate wakati sifa zote unazo…?’ akaniuliza
‘Siwezi kujua kwanini….’nikasema
‘Kwa mara ya mwisho ulitafuta wapi kazi na ukaambiwaje…?’akaniuliza
‘Nilitafuta kwenye kampuni moja ya vifaa vya magari,
wakaniambai nisubiri…
‘Usibiri mpaka lini…
‘Walisema wataniita….na ndio ikatokea hii kesi…
‘Hukuwahi kuuliza kabla kwanini hawo ambao hawakuwahi
kukubali kukuajiri,….kwenye kampuni nyingine yoyote uliyokataliwa ilikujua kwasababu
gani kwani vyetu na elimu unayo..?’akauliza na wakili wangu akaingilia kati,
hakimu akazuia hilo swali labda liulizwe vinginevyo. Akauliza kivingine lakini
halikuwa mbali na lile swali la kwanza na wakili wangu alitaka kulizuia mimi
nikajibu kwa haraka;
‘Nilipohojiwa kwenye kazi niliyowahi kukataliwa, niliuliza
kwanini nisubiri,wakasema mpaka wanihakiki kwakupitia wanadhamini
wangu….’nikasemabaada ya kuulizwa swali hilo kivingine.
Maswali yaliulizwa mengi mpaka nikaanza kuchanganyikiwa,
nilijikuta kama naulizwa maswali yale yale kwa kugeuzwageuzwa tu na mwisho
akauliza swali ambalo nilijibu haraka-haraka kabla sijamwangalia wakili wangu
wangu ambaye kumbe alitaka kunizua nisijibu.
‘Ndio kazi za usiku nilishawahi kufanya….kwasababu kazi ni
kazi iwe mchana au usiku…’nikasema.
‘Kazi ipi ya usiku uliyowahi kufanya…?’ akaniuliza.
‘Kazi ya uhudumu wa hoteli….’nikasema.
‘Uhudumu gani huo, mapokezi au kazi ipi hasa….?’ Akauliza.
‘Unapoitwa kwenye kazi hizoo za kibarua huchagui kazi gani,
unaweza kupangwa popote pale…..
‘Je siku ya tarehe hiyo ya tukio ..umedai kuwa ulikuwa
ukihudumu kwenye hoteli hiyo ambayo mara kwa mara ndipo uanpofanyia kazi,lakini
nina ushaidi kuwa ulikuwepo kwenye hoteli kubwa ya kitalii…na nitawaita
mashahidi kusibitisha hilo….’kabla hajamaliza wakili wangu akadakia
kuzuia,lakini hakimu akaomba hilo swali lijibiwe, hata pale wakili wangu
alipoweka pingamizi.
‘Ningejigawaje,…. Nilishakuambia kuwa nilikuwa hotelini
kwangu ninapofanyia kazi,…waite hawo mashahidi walioniona…..’nikasema huku nikimwangalia
wakili wangu ambaye hakufurahishwa na jinsi ninavyojibu maswali kabla
hajaniruhusu.
‘Nitawaita muda ukifika, sio kazi yako kuniamrisha, je siku
hiyo ya tukio,uliwahi kukutana na mkeo….
‘Ndio nilikutana naye…..
‘Sasa hapo uligawaje….?.
‘Kuna muda wa mapumziko, na kwa vile kazini kwake sio mbali na kwangu
tunapeana taarifa kuwa tukutane mahali, …na mara nyingine namuita mke wangu
kupata chakula cha mchana…au cha usiku….
‘Kwahiyo siku hiyo ya tukio ndivyo ulivyofanya..?’akaniuliza.
‘Ndio..’nikasema huki nikijitahidi kumwanglia wakili wangu,
lakini huyu mwanadada akawa kasimama mbele yangu nasikuweza kumuona vyema
wakili wangu, ambaye alishasimama kuingilia kati.
‘Je ulikuwausiku wa saa ngapi..?’ akaniuliza.
‘Usiku wa saa ngapi, …ukumbuke huyo ni mke wangu…naweza
kumuita wakati wowote…’nikasema na watu wakaguna.
‘Jibu swali langu ,siku hiyo ya tukio ulimuita mke wako,
kama ulivyosema, je ulikuwa usiku wa saa ngapi ambao ulimuita mkeo mkapate
chakula cha usiku…’akasema na watu wakacheka.
‘Siwezi kukumbuka….
‘Je kazini mnaruhusiwa kufaya hivyo…?’ akaniuliza.
‘Ndio kwa muda wa chakula tunaruhusiwa kufanya
hivyo…’nikasema.
‘Kwahiyo upo muda maalumu wa chakula,unaojulikana na kila mtu…?’
akaniuliza.
‘Ndio…..’nikajibu na wakili akatabasamu, halafu akaniuliza.
‘Je mlikutana usiku wa saa ngapi na huyo mkeo…?’akaniuliza
tena hilo swali.
‘Nilishakuambia sikumbuki..’nikasema na huyo mwanadada
akamuangali hakimu akiandika jambo na baadaye akaniuliza swali jingine.
‘Je mlikutana wapi ….?’
Wakili wangu akaingilia kati, hilo swali, lakini hakimu tena
akaamrishwa lijibiwe, na nilipojibu hapo ikawa ni mlolongo wa maswali mengine ambayo nia ilikuwa kuniweka katika eneo la tukio,
lakini wakili wangu alikuwa mjanja kupita kiasi, na maswali yalivyoendelea
nikajikuta naanza kujikanyaga, na wakili wangu alipoona hivyo akaomba
mapumziko…ili nikirudi yeye ndiye ataniuliza kuziba mapengo ya majibu yangu.
‘Nilishakumbia usitetereke, mimi nipo nyuma yako, hakikisha
kila swali kabla hujajibu unaniangalia mimi kwanza, nikikupa ishara ya kujibu
jibu, kama nikiwa kimiya na wewe kaa kimiya, na nitajua nini cha kufanya….unasikia,
nashukuru hata hivyo umejitahidi sana, na najua kwa hali ilivyo tunaweza
tusiendelee leo…' akasema wakili wangu.
'Kwahiyo nitaendelea kusota rumande...'nikasema kwa uchungu.
'Haina jinsi...na nitakuhoji mimi kuziba mapengo yaliyojitokeza, Yule motto
mdogo sana kwangu…hakuna kesi hapa….’akasema wakili wangu kwa kutamba, na kweli
tuliporudi ndani ya mahakama, hakimu akasema kwasababu muda umekwisha kesi hiyo
itaahrishwa na kusikiliza tena siku ya pili yake,na mimi nikarudishwa rumande.
*********
Ilikuwa muda ambao hairuhusiwi hata wageni kunitembelea nikawa
natafuta usingizi, na mara nikasikia jina langu likiitwa na askari mlinzi,
nikasogea mlangoni na huyo askari akaja kufungua mlango, nikaingwa na wasiwasi,
isije ikawa mbinu nyingine za kunimalizia huku huku jela,…lakini sikuwa na
jinsi ilibidi nifuate maagizo, aliniambia nielekee chumba cha wageni, na mimi
nikiwa na mshangao …ni mgeni gani muda kamahuo, nikaharakisha kufika sehemu
tunapokutania na wageni…
‘Subiri hapo kidogo..’akasema Yule askari na mimi nikasubiri huku nikiwa
nimesimama, kujiandaa kwa lolote lile, nilishahisi kunaweza kukatokea mtafaruku,
kwahiyo kama nikufa nife kiume, nitapiagana hadi muda mwa mwisho,nikaomba dua ,
nikamuomba mungu, anisaidie kama ni janga nipambana enalo kiume, na ikibidi
nisfe kabla sijakutana na wazazi wangu, …
Mara nikahisi mtu akija kwa nyuma yangu, nikajiandaa nikitutumua
misuli,nikageuza kichwa kwa hasira nikiwa tayari kwa mapambano, uso wangu
ulipotua kwa huyo mtu….nilihisi mwili ukinyong’o’nyea sikujua kwa nini, lakini
hali hiyo ilinikumbusha kipindi kile cha nyuma wakati natafuta mke…..
‘Umenisahau nini..?’ akauliza huyo mgeni ambaye alikuwa
kasimama kwanza, akiniangalia na mimi nikiwa nimegeuza kichwa tu nikamwangalia, mgeni huyu mwanadada alikuwa kavalia mavazi ya kitenge, ya heshima,….akasimama kama vile anataka kupigwa picha, nafikiri alitaka nimuone vyemaalivyopendeza, mkono mmoja kashika kiuno na mwingine kaweka mfukoni, ...nikitabasamu, na
kabla sijajibu akaongezea kusema;
‘Pole sana na masahibu yaliyokukuta….’akanisogelea na
kusimama mbali kidogo na mimi.
‘Siwezi kukusahau wewe hata siku moja, hongera kwanza kwa kupendeza…unajua nikuambie ukweli.upo kichwani mwangu
na akilini mwangu, sema ndio hivyo, ilibidi yatokee hayo ili mabadiliko yawepo…ni
jambo pia la kushukuru, nimesikia juhusi zako, hongera sana….’nikasema.
‘Sawa nashukuru, hizi ni moja ya kazi zetu,...akasemahuku akiwa kama ananionyesha vazi alilovaa, kama wafanyavyo wanamitindo, ...tunajituma kweli akina mama siku hizi, mungu anajua zaidi…' akasema halafu akaniangalia machoni akasema;
'Ila mimi sina muda
mrefu, kama nilivyoagizwa na askari kuwa nisikae muda mrefu….nilifika hapa DAR kwa ajili ya kikao maalumu cha
akina mama, na nikakutana na wakina mama w ahapa Dar, ni moja ya mipangilio
yetu ya maendeleo, na nimejifunza mengi, …kulikuwa na ajenda nyingi, ila moja
ambayoo sijui ….sina uhakika kama ndivyo ilivyo…ni hali iliyopo has ahuku
mjini, na hata huko kijijiniimeanza kuingia ya wanawake kutumiiwa
kamabidhaa….’akawa anaongea harakaharaka…
‘Usisikilize hayo maneno….achana nayo kabisa, fuatlia
maendeleo yako na kilichokuleta, hayo mengine hayana maana….kwani umeletwa na hayo, au ...!’nikasema kwa
hasira.
‘Nisikilize basi, sina muda mrefu wa kuongea na wewe…’nikasema.
‘Nakuomba usijiingize kwenye haya maswala, kama wamekuambia
kitu kushusiana na mimi,usiwakubalie kamwe….kama wamekutuma,waambie waniachie
mambo yangu mwenyewe, najua jinsi gani ya kujietetea….ni hatari, usije
ukakubali kujiingiza…’nikasema lakini yeye hakunsikiliza akawa anaendelea
kuongea.
‘Ni mambo ya aibu sana, na niliposikia kuwa na wewe
umehusishwa nayo, kwanza sikuona ajabu,kwani namjua mkeo vyema, lakini hadi
kufikia kufungwa, hadi kufikia kuua, nikashituka sana ….najua kabisa chanzo kitakuwa
ni mkeo, ‘akasema huku akiniangalia machoni.
'Kwahiyo...huoni nipo jela,mnataka ninii zaidi...'nikasema kwa hasira.
‘Mtoto wa Msomali, wewe umetoka kwenye familia bora, familia
inayojali tabia njema, eti unakubali kushirikishwa katika mambo hayo, na
aliyekukokota ni Yule Yule kule kijijini anajulikana historia yake…hebu niambie
nini umuhimu wa elimu yako….nini unatafuta katika dunia hii kupata sifa,…uwe
mushuiakmkuu kwenye mapicha hayo, ili wakuone dunia nzima kuwa wewe ni mwanaume
, je familia yako, watoto wako watajisikiaje wakijua kuwa wewe ulikuwa mmoja wa
….inatia aibu hata kuongea…’akasema huyo mgeni.
‘Najua na wengi watanilaumu sana kwa hili, lakini hakuna
anayejua nini kinaendelea ndani yake, ni kwanini nayafanya haya yote….ni rahisi
kwa mtu asiyejua kutoa wazo, au kushutumu, lakini kwa mimi amabey nipo ndanii
ya haili tatizo najua ni kwanini nafanya hivi…nawaomba mniachie wenyewe, na naogopa
sana familia yangu, wazazi wangu wakihusishwa na hili….na nimetishiwa
hivyo..naogopa isije ikafika huko…’nikasema.
‘Wahusishwe mara ngapi..!’akasema huyo mgeni.
‘Kwani kuna nini kimetokea,wamehusishwaje..hapana,
hawajahusishwa, niambie kuna nini kimetokea, na kwanini upo hapa, usiniambei
kuna jambo baya limetokea huko…?’ nikauliza nikiwa nahaha kutaka kujua.
‘Inawezekana umefichwa kasababu upo huku jela, na huenda
imefanywa hivyo makusudii ili usiumie zaidi , hivi nikuulize hii kesi inahusu
nini hasa, au ndio hayo niliyosikia akina mama wakiongea, maana kama ni hayo na
unatumiwa kihivyo, kwakweli unaiabisha familia yenu,….sikuwa na uhakika na hilo
kwani hata wao hawakukutaja wewe kuwa muhusika, walisema kiujuma na kuwa kuna
watu wameshakamatwa na wangekubali kushirikiana nao, mambo hayo yangeisha
kabisa…’akasema huku akiniangalia kwa makini.
‘Kwahiyo wakakutuma uje unione…?’ nikauliza.
‘Wewe mtoto wa Msomali, ni nini kimetokea hadi ubadilike
kiasi hicho na kwanini mapicha mabaya kama yale yatumwe kwa wazazi wako, na
hayo yaliyoandikwa kwenye hiyo barua ndiyo yaliyomuumiza hata mama yako, ujue
mama ni mama,uchungu kwa mwana hauishi hata uwe mkubwa kiasi gnai,….alishindwa kabisa
kuvumilia, ingawaje kwa sasa hali yake inaendelea vyema ….’akatulia.
‘Ni nini kimetokea huko hebu niambie vyema, mapicha gani
hayo yaliyotumwa huko, habue niambie vyema,maana unanichanganya sasa, kwani mama
anaumwa…wazazi wangu wamefanya nini..hapana, naomba isiwe hivyo ninavyofikiria,
hapana, nitaua mtu….wanataka nijiue mwenyewe sio, hapana, kabala sijajiua
mwenyewe, nitahakikisha anayehusika na hilo naye keshakufa….naapa….?’nikawa
kama mtu aliyewehuka, nilirukaruka kwa hasira.
‘Mama yako alipatwa na mshituko alipoletewa hiyo barua
zikiwemo hizo picha chafu chafu...ambazo hazifai hata kuangalia, ni kama yale
mapicha yao ya video, nakumbuka uliwahi kunileeta video moja, ingawaje hiyo
picha…mmmh, imezidi….lakini ….kwanini watu wajizalilishe kiasi hicho, na
kwanini uchafu wenu, muwaletee hadi wazazi,…jamani,hiyo ni adabu gani, yaani ni
aibu, eti ulikuwa na ….mke wa muheshimiwa …na ndani yake kulikuwa na ujumbe wa
vitisho…'akasema huyo mgeni.
'Ujumbe gani...?'nikajikuta nikiuliza
'Sikuweza kuusoma wote,....maana mama alipoona hayo mapicha ndio mambo yakaharibika....lakini nakumbuka kuna sehemu inasema kuwa usipofanya watakavyo, hizo picha zitafika mbali….'akasema huyo mgeni.
'Mbali wapi waongo wakubwa hawo...'nikajitetea.
'Hayo sijui…lakini kwa kweli, fanyeni
mfanyalo, na huo uhuru wenu wa kufanya mpendavyo, lakini waacheni wazee wa watu
watulize miili yao,…wameshawatumikia vya kutosha,....wamewalea, wameteseka kwa ajili yenu, wamewasomesha, ....sasa hiyo ndio fadhila
mnayowalipa wazazi wenu…?’ akaniuliza huku akiniangalia kwa makini.
‘Siamini….hapana siamini…’nikajikuta naweweseka huku nikitamani
dunia ipasuke nitumbukie ardhini, na hapo nikakumuka walivyoniambia, kuwa
wengine hufikia hatua ya kujiua, kutoakana na mambo hayo ya aibu yanayowakuta,
wanashindwa kuvumilia….
Kwa jinsi nilivyojisikia, hata mimi hapo, kama kungelikuwa na sumu karibu uniambie
niinywe, ningeinywa chapu chapu, niondokane na hizo aibu...hebu wewe fikiria familia yetu ni moja ya familia inayoheshimika huko kijijini,leo inasikika taarifa kama hiyo na mapicha machafu kama hayo yanaonekana kila kona, ..hutaweza kuvumilia, utauweka wapi uso wako....
‘Jamani, hamumuogopi hata mungu….aaah, natamani hadi
kukukimbia, maana ina tia aibu….lakini nikaona ni vyema nije nikuone, ili
nisikie kauli yako, je unahusikaje na hayo machafu…na je kesi yako inahusiana
na hayo machafu, au ni kubambikiwa kuua kama ile ya kule kijijini? .’akaniuliza
huku akiniangalia kwa macho ya huruma.
‘Haiwezekani….eti nini, nani kanifanyia hivyo, ….. sasa
nimejua kabisa hizi ni mbinu za hawa akina mama…. ni mchezo umechezwa na hawa akina mama ili niwe upande wao, kwanini
hawanipi nafasi nikafanya nijuavyo mimi…kwanini na wao waandiriki kunifanyia
hayo ambayo najaribu kupambana nayo, hawajui nini mbinu yangu....sikubali
nitapambana nao mpaka haua ya mwisho….
‘Akina mama wapi hao….,hayo sio ya akina hawo mama wa watu…usiwapake
matope kabisa… , unawasingizia bure….Nikushauri kitu, usije ukagombanishwa na hawo akina mama,
kwani kwenye kikao hicho nilichohudhuria, moja y a ajenda yao ilikuwa kupiga
vita mambo kama hayo,….na mara nyingi walengwa wakubwa ni akina mama,
wanatumiwa kudhalilishwa…. haitawezekana wao wapige vita mambo hayo, halafu
ndio wao wawe msitari wambele kuyafanya hayo, hakuna mzazi mwenye akili zake timamu
atafanya hayo, wale waliokuwepo wote pale kikaoni ni wazazi….’akasema huyo mgeni.
‘Sasa unafikiri ni nani,….maana hawa watu nilio nao pia ni wazazi, na ndio
wameniwekea wakili na tulishakubaliana kuwa baaada ya hii kesi hawataniagiza
kwenye mambo yao tena,hawatanihitaji tena kwenye mambo yao, watanipa mtaji nije huko
kijijini tuwe pamoja….na aliyenihakikishia hilo ni wakili na kauli ya wakili inakubalika kokote…unafikiri
wanaweza kunifanyia kitu kama hicho…?’nikauliza huku nikiwaza.
'Yeye kama wakili anaweza asifanye na wala asijue kuwakimefnayika kitu kama hicho, na kama alijua, pengine walikuja kumwambia baadaye, na ndipo akawashauri wahakikishe kuwa hiyo barua haipo...inawezekana kwa biandamu...'akasema mke wangu ambaye alionekana sasa ameiva kielimu...
'Haiwezekani...'nikajikuta nikisema.
‘Nikuambie kitu….kwanini basi siku ya pili yake alikuja mtu
toka huku akisema mnafanya kazi na yeye na katumwa kuwa kuna barua ilitumwa kwa
wazazi wako kimakosa, inaombwa haraka, irudishwe ilipotoka, na wazazi walikuwa
wameshaichoma kwa hasira,lakini mimi nilichomoa picha moja haraka na….na
nakumbuka huyo mtu alisema kuwa wewe umeshakubali kushirikiana na wao, na ya kuwa
kesi uliyo nayo inakwenda vyema….’akasema huyo mgeni.
‘Tulipomuuliza kesi gani, alisema ni mambo madogo tu ya
ofisini, hakutaka kusema ni kesi gani na alipohakikisha kuwa kweli hiyo barua
imechomwa moto, akawakabidhi wazee pesa na zawadi nyingine, akisema zimetoka
kwako, na wazee wakachukua hizo pesa wakijua zimetoka kwako na kutoa ujumbe ukifikie
kuwa pesa nyingine zilizokuwa zikitumwa na wewe wanazipata…hivi kweli ulikuwa
ukiwatumia pesa za matumizi kwa vipi na
wewe nasikia upo huku jela karibi miezi
sita sasa…?’ akauliza kwa mshangao.
‘Yupoje….huyo mtu aliyekuja huko kijijini…?’ Akauliza na
nilipoambia wasifa wake , nikamgundua mara moja kwani ni mmoja wa watumishi wa
mama Docta, nikagwaya, nikajikuta jasho likinitoka na hasira zikanipanda, ….
‘Ina maana hawa watu wameamua kunivua nguo hadi kwa wazazi
wangu, ili niazirike…..hapo wamegusa pabaya…hapo sasa wamenipandisha hasira
nilizokuwa nimezificha, …..tutapambana nao hadi nione mwisho wake…’nikasema kwa
hasira .
‘Ina maana wewe ndio walikuwa wakikutumia kufanya hayo
mapicha, mbona hiyo picha nilipompa shemeji yangu alisema hizo ni mbinu za
mitandao, ….maana yeye ni mtaalamu wa mitandao, amenifundosha kutumia `komputa’
najua jua….yeye alisema imegushiwa kiujanja, …kwa hiyo picha niliyobahatisha
kuichukua, sijui kwa hizo nyingine ambazo wazazi wako walizichomamoto, sina
uhakika nazo…’akasema huyo mgeni.
‘Nakuhakikishia sikuwahi kufanya huo uchafu, niliambiwa
nijifanye nataka kufanya hivyo, lakini nisifanye tendo lenyewe, ni kiasi cha
kumkaribia tu, nilishajifunza, sikutaka kurudia kosa…..na walisema mengine
watajua wao weneywe, unayo hiyo picha hapa….?’ Nikauliza na mara huyo mgeni
akanipa hiyp picha, nilipoiona karibu nidondoke kwa kuzimia….niliitizama bila
kuamini macho yangu.
‘Mungu wangu….mimi nifanye kitu kama hiki, ….hapana, hawa
watu ni wabaya sana, ndio nilivua nguo nakubali kama walivyoniagiza,
nikajifanya kama namkaribia halafu nikamuacha pale alipojaribu kuning’ang’ania,
alijaribu kunishika kwa nguvu,lakini sikukubali, nikamuacha, ….sikuwahi kabisa
kutenda tendo hilo, naapa, na tendo lenyewe la kifrauni kama hivyo…hapana,….hawa
watu ni wabaya sana…ni wabaya kupita maelezo…..’nikajikuta nikipiga ngumi
ukutani.
‘Ndio maana nakuambia huyo shemejii yangu alisema kuna
sehemu ya hiyo picha imegushiwa, kinamna, haijakamilika…sasa sijui kwa vipi…wanajua
wenyewe hawo wataalamu, au sijui alikuwa akijaribu kutuficha jambo…’akasema
huyo mgeni.
‘Ngoja nitaitumia hii, ….ingawaje sijui kama itafaa, lakini
ikibidi nitaitumia kama ushaidi muda
ukifika, lakini, hapana nitakuwa najizalilisha, mwenyewe,…na kwanini ukamuonyesha
huyo shemeji yako, huoni kwamba unazidi kuniweka uchi kwa jamii,….usijali hata
hivyo, … ila nitaifanyia kazi hii picha, wewe niachie ….nakuhakikishia kuwa
sikuwahi kutenda tendo kama hilo, nilikuwa na akili zangu timamu, nakumbuka
kabisa,sikuwa katu….’nikawa najitetea.
‘Mimi nakuamini,kwasababu nakujua, ndio maana nikajiuliza
hivi kweli umebadilika kiasi hicho au ndio maana uliamua kuniacha kwasababu
siwezi uchafu huo…sikuamini na mapaka sasa siamini hivyo….mungu akusamehe sana
, na kama wanakubambikia huo uchafu, achana nao haraka, kama ni kazi huna njoo
kijijini kuna kazi nyingi za kiamendeleo….’akasema huyo mgeni.
Nilijilaumu moyoni nakusema kwa sauti, `Nilishawafikiria
vibaya hawa akina mama kumbe nazungukwa na hawa hawa watu wanaojifnaya ni wema
kwa kuniwekea wakili….’nikajikuta nikisema.
‘Hilo limetokea kwa nguvu za mungu ili uone ni jinsi gani
hawo watu walivyo, ni kwamba wao wanachojali ni maslahi yao, na ukionyesha
dalili ya kuwakana, wanaweza hata kukuua, hebu angalia athari gani
walizomsababishia mama yako, na je nini hatima ya yote hayo…je una uhakika gani
kuwa ukimaliza hiyo kesi mambo yako yatakwenda vyema…usijidanganye, muonja
asali haonji mara moja…’akasema huyo mgeni
‘Kwahiyo umakuja hapa kwa kutumwa au umekuja hapa mwenyewe
kuja kuniona kuwa bado nipo hai…au umekuja kwa kwalengo gani..?’nikamuuliza kwa
hasira.
‘Sijatumwa na mtu,….nimefika hapa Dar kwa shughuli zetu za
akina mama, na isngelikuwa ni vyema nirudi bila kukuona, na nilipofika hapo
nyumbani nikaona mabadiliko makubwa…ile nyuma ndio umeiuza au ndio umeamua iwe
ya kupangisha, nakumbuka ulisema nyumba hiyo hutaipangisha kamwe, maana kweli nimewaona
wapangaji mle ndani na wengi ni akina
dada…..?’akaniuliza.
‘Hayo hayakuhusu…yaache kama yalivyo…..’nikasema huku moyo
ukiniuma.
‘Sawa hayanihusu ni kweli..uonavyo wewe,…. ila pia nilifika
kukusalimia, kujua hali yako…nakuonea sana huruma, maana mikosi haikuachi, mimi
kwa ujumla nilishakusamehe na kila mara nakuombea kwamungu uzishinde hizo tamaa
za kishetani, na uzindukane na ikiwezekaan uachane na huyo rafiki yangu, maana
namfahamu sana, najua tabia yake , hamtaivana kamwe, na atazidi kukutia
matatani…’akasema huku akiniangali kwa macho ya huruma.
‘Hilo ni tatizo langu, wewe umeshapata mume anayekufaa basi
shukuru mungu,…kwangu mimi hii naiona kama ni adhabu mungu kanipangia, na sina
jinsi lazima niitumikie, nashukuru kuwa wewe umenisamehe, kwahiyo najua sasa
tatizo lipo kwa wazazi, na nahisi, kinachosababisha haya yote kwa sasa ni
ujinga wangu, na ndio ukafikia hata wazazi kutokuwa radhi na mimi,….lakini
….lakini…’nikajikuta machozi yakinilenga lenga na huyu mgeni akahema kama vile
mtu aliyechoka na jambo, na kusema;.
‘Ndio maana nikaja kukuona ili hata nikirudi huko kijijini
wazee wakiniuliza nijue nini cha kuwaambia, licha ya kuwa baada ya kuona hiyo
mipicha michafu, hawataki hata kukuona, hwataki hata kusiki jina lako,….lakini
shemeji yangu alikuja kuwatoa hizo hasira na kuwaambia kuwa kuna michezo ya
mitandao inayoweza kugushi picha na kuonekana kinyume na ilivyopigwa na hiyo
picha ni moja ya michezo hiyo, …au …?’ akasema na kuniuliza huku akiniangalia
kwa makini.
‘Baba alikubalian na hiyo hoja…?’nikauliza bila kujali hilo
swali lake.
‘Unajua baba alivyo mdadisi, aliuliza ina maana hiyo picha
iliunganishwaje , lazima itakuwa ilipigwa ukiwa uchi….ndio iwezekane, kuunganishwa,
akasema kama nikuunganishwa ni lazima ulipigwa wapi ukiwa uchi….akasema lazima utakuwa
unavuta bangi au unga, ndio ukaweza kufanya uchafu kama huo, na kama ni kweli,
hawatakutambua tena kama mwanafamili wao….’akasema huyo mgeni.
‘Hiyo ndio laana ninayosema….na adhabu yake ndiyo hii
inayoniandama, ngoja niadhibiwe, ni haki yangu kuadhibiwa,…kwakweli najuta, sijui
kimenipata kitu gani, sijui ni mlaumu nani,hapana,hakuna wa kulaumiwani …kosani
langu mwenyewe, ….lakini lazima nipambane kiume,….hata kama watanimaliza,
lakini sitakubali kirahisi……..’nikajikuta nikiapa kwa kidole.
‘Sisi tulikuwa hatujui kabisa kuwa upo katika madhila
haya,….pole sana maana nakumbuka ulivyofungwa kule kijijini,na tena yamekukuta
haya,…pole sana na kama unahitaji msaadawetu tuambie, nitaongea na mume wangu
tuone jinsi gani tunaweza kukusaidia….’akasema huyo mgeni.
‘Hapana, msijihusishe kabisa na kesi hii, …hili niachieni
mwenyewe,sihitaji ndugu yangu yoyote kujihusisha, ….nisingependa kuja kujijutia
baadaye, na haina haja kuwajulisha wazazi wangu,….na kama inawezekana usiwaambie
lolote kuhusu hii kesi, …hata hivyo, najiuliza, ni nani alikuambia kuwa nipo huku jela…?’
nikauliza.
‘Hawo sijui ni wapangaji wako….waliniambia kuwa una kesi
mbaya,…kama nahitaji zaidi nionane na mke wako, lakini sikuwahi kumuona ,na
hata nilipohangaika kumtafuta mke wako sikuweza kumpata, nilitaka kujua kama
umekamatwa kwasababu gani, na nini kinachoendelea…kwani wengi niliowauliza
walikuwa wakinipa maelezo yasiyokamilika na wengine waliniambia jambo ambalo
lilinishitua sana na ndio nikakumbuka ile barua iliyokuja huko
kijijini….’akasema mgeni.
‘Hiyo barua tena….., hawa watu ni wanyama, lakini dawa yao
inachemka!’ nikasema kwa hasira
‘Mimi kesho naondoka, na nilichofanya nikujitahidi kutafuta
kila njia nikuone, ili nijue nini kinachoendelea, na pia ili ujue kuhusu hali
ya wazazi wako, mama kwa sasa hajambo, ila ukichanganya na uzee ha huo
mshituko, ametetereka kidogo, baba anadunda, mzee Yule nii chuma cha pua….’akasema
huyu mgeni na tukatulia kidogo na baadaye akashituka akikumbuakk kuwa muda
aliopewa umekwisha akasema;
‘Na hakuna anayejua kuwa nimekuja kukuona, kwasababu
hairuhusiwi, nilichofanya ni kuwa kati ya akina mama niliokuja nao kuna mmoja
mume wake yupo hapa gerezani, ni mkubwa kubwa Fulani, akaniunganishia na ndipo
nikapata muda wa kuja kukuona….huwezi amini kesi yako hii wazazi wako hawajui
kabisa….,wamejitahidi sana kuificha….’akasema.
‘Una uhakika na hilo, kuwa hakuna anayejua kuwa umekuja
kuniona …maana hawa watu ni hatari, kitendo hiki usingelikifanya kama
unegliwajua hawa watu ….unacheza na hatari , wakijua hawa watu wanaweza
kukukamaliza…’nikamwambia.
‘Hakuna, anayejua zaidi ya huyo mwanamama na huyo mume
wake….na hata hivyo mimi sio Yule mwanamama uliyemtoa kijijini kipindi kile,
….najua nini ninachokifanya…..usiogope kuhusu mimi….’akasema na baadaye
akaondoka akinisisitizia kuwa niachane na hayo mambo…
Kwakeli niliamini kuwa hakuhusishwa…..kwani alivyoongea
hapo, inaonekana kabisa hajui undani wa hiyo kesi, na nashukuru kuwa hakusema
zaidi kuwa niwasaidie akina mama kwenye hiyo kesi, hii ilionyesha wazi kuwa
kweli hakushawishiwa kuwa aje kuniona na wakili wa akina mama.
*********
‘Naomba nikuulize swali kabla kesi haijaanza….’nikamwambia
wakili wangu ambaye alikuwa kafika kuniandaa kwa jili ya kesi ya leo, na
ikizingati kuwa yeye ndiye atanihoji kwa
muda mrefu, hakujali sana kwa hilo, ila alihakikisha kuwa nipo nay eye
kimawazo.
‘Sikiliza kwanza, achana na mambo mengine yote, akili yako
itulize kwenye hii kesi, …sitaki tuaharibu mpangilio, fanya vile
nilivyokuelekeza, tushinde, utoke humo jela, tuanze mipangilio mingine ya
maisha, sifurahii wewe uendelee kusota huko jela,unatakiwa uwe uraiani,
ukajiendeleze, au vipi…?’ akaniuliza huku akitabasamu kiuongo.
‘Ni heri ya kauli yam domo,maana ndio kazi yake kusema,
lakini siri ya mtungi anayeijua ni kata,lakini kuna mambo mengi mnanificha na
mimi ilikuwa ni haki yangu kujua, ….’nikalalamika.
‘Mambo gani ….kama ni kuhusu hiyo hundi yako ipo tayari…hilo
niamini mimi, ujue mimi ni wakili ninjaali kazi yangu ambayo mojawapo ni kuwa
mwaminifu kwa mteja wangu, kwahiyo naomba uniskilize mimi, au kuna jambo
jingine kuhusuana na hii kesi….?’ Akaniuliza huku akiniangalia machoni, na hapo
hapo wazo la kutokumwambia lolote likanijai nikasema;
‘Hiyo hundi sio muhimu sana kwangu, ninachojali ni kuwa lini
nitatoka humu,maana mimi nimechoka, nateseka ile mbaya na pili mpaka sasa
sijajua kuhusu hali ya wazazi wangu, je wanajua kuwa nipo kwenye hii kesi mbaya
ya kubambikiwa….?’nikauliza kiujanja.
‘Tuliona ni vyema wasijue, na hata hivyo ili kuhakikisha kuwa
hawana matatizo tulimtuma mtu wetu awapelekee chochote, na kuangali hali zao,
na tunashukuru kuwa aliwakuta hawana shida….’akasema huyo wakilia.
‘Mbona hukuniambia na nakumbuka kuna siku nilikuulizia,
lakini hatukupata nafasi ya kuongea, unajau kuwa hawo ni wazazi wangu
wananihusu na muda mwingi na wawazia wao, nilikuwa na hamu sana nionane na wao…ni
muda mrefu sana, hatujaonana na wao, inaniuma sana…kwaninini mlinificha kuhusu
wazazi wangu, kwanini mkafanya hivyo…?’ nikauliza kwa hasira na uchungu.
‘Hayo yote tunajua, tulikuwa tukiwatumia pesa mara kwa mara
kuhakikisha kuwa hawayumbi,hilo lilikuwa halina haja yaw ewe kujua, kwani
wazazi wako ni sawa na wakwangu, …lakini hata hivyo , wao kule wamejitahidii
sana katika shughuli zao za kimaendeleo, naona kuna mwamko wa kumaendeleo,
akina mama wana vyama vyao,akina baba pia…kwa ujuma hawana shida….usijali kwa hilo…’akasema
huyo wakili..
‘Hawana shida eeh, hawajambo si ndio, ….una uhakika na hilo,…?’
Nikauliza nay eye akaniangalia machoni , na niliona kama anasita kuniambia
kitu, lakini baadaye akasema;
‘Hawajambo….mama yako kidogo alikuwa anaumwa, lakini
tulihakikisha kuwa anatibiwa vyema, na sasa hajambo kabisa, na tutahakikisha
kuwa anapata matibabau yote yanayostahili…’akasema huyo wakili.
‘Ninachoweza kusema kwa sasa ni kuwa nawashukuruni sana…sina
zaidi….’nikasema na yule wakili akaniangalia kwa mashaka na alitaka kusema kitu
lakini kabla hajafugua mdomo wake ,tukaitwa ndani kuendelea na kesi yetu…..
WAZO LA LEO: Kama itafikia hatua ya kukosana kwa mke na mume, hadi kutalikiana, kama ni lazima kufanya hivyo, achaneni kwa wema, ili mkikutana mkutane kwa wema, maana huwezi jua ya leo na kesho,....
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Tupo pamoja mkuku
Post a Comment