‘Tunahisi kuwa huenda wewe ndiye shahidi unayetakiwa
kusimama keshokutwa wanataka
kukusimamisha wewe kama shahidi, …sijui wana lipi jipya, kama ulivyoona,hakuna
lolote walilotoa ambalo linaweza kukutia wewe hatiani na hawo wanaosema wapo nyuma
yako…wameshindwa kutoa ushahidi, sasa
wewe unategemewa kuwa shahidi wao na tegemeo lao la mwisho…najua nia yao ni
kukusimamisha na kukutega kwa maswali….uwe makini …..’akasema wakili huku
akimwangali mke wangu kwa makini.
‘Umeshaongea na mume wako kuhusu hali halisi, ….natumai
kutakuwa hakuna ubabaishaji, maana kama atakubaliana na matakwa ya hawo watu,
hakuna jinsi….natumai unampenda kama ulivyodai…’akasema wakili.
‘Nimeshaongea naye, ….’akasema mke wangu huku akiniangalia
machoni, kwa leo alionekana mnyonge sana, kiasi kwamba nilimuonea huruma, licha
ya chuki nilizokuwa nazo juu yake, kuwa yote hayo yametokea kwa jili yake,
sikujua kwanini anaonekana mnynge hivyoo tofauti na jinsi anavyokuwa siku zote.
Huwa anajiamini, na mkakamavu….
‘Mke wangu….’nikataka kusema kitu, lakini mke wangu
alinionyesha ishara ya kutokuongea lolote na wakili akamwangalia kwa makini na
kusema;
‘Kwani kuna jingine ambalo mimi silijui…?’ akauliza.
‘Hapana muheshimiwa wakili…’akasema mke wangu, lakini mimi
nilijua kuwa lazima lipo jambo,na jambo
lenyewe litakwua kubwa…lakini sikuwa an jinsi ya kulijua, nikatulia ….
*******
Ni karibu miezi sita sasa imepita kesi hii ikiendelea na
kila siku watu wamekuwa wakijumuika kwa wingi, na hata wengine kutoka nchi za
jirani, ambao kwa namna moja au nyingien kesi hii iliwagusa, na vyombo vya
habari vimekuwa vikiandika kwa wingi, …kwao umekuwa msimu wa biashara..
Niliinama chini nikiwaza, nikikumbumbuka mengi,na kila hatua
ya hii kesi nimekuwa nikiahidiwa mengi, nakumbuka hata siku kadhaa nyuma
niliomba kuwa kesi hii ikiisha mapema, nipewe mtaji wa maana niondoke hapa
mjini, nikajiunge na wazee wangu kijijini, ….nikajiunge na ushirika wa mke
wangu wa kwanza ambaye nasikia wamempendekza kugombea udiwani kwenye eneo
lao….namtakia kila laheri na mimi nikaomba kama ikiwezekana katika kura
zitakazopigwa ya kwangu iwe mojawapo…lakini je itawezkena iwe hivyo.
‘Hilo tu unahitaji kisai gani…?’ akaniuliza wakili wetu.
‘Milioni ishirini tu…’nikasema na huyo wakili akaniangalia
kwa mshituko, halafua akasema ;
‘Ni pesa nyingi kidogo, lakini nitawauliza wahusika, sizani
kuwa kwao itakuwa pesa nyingi, na nakuahidi kama utashirikina vyema na kesi hii
ikaisha vyema, pesa hiyo utaipata….nikuahidi hilo,…..’akasema huyo wakili.
‘Kwa vipi, maana wewe ni wakili tu, na watoaji hiyo pesa ni
wengine….?’nikauliza.
‘Kama wakili najua ipi inawezkana na ipi
haiwezekani,nimeshapendekeza hilo kwa wahusika na wao walishaliweka katika
bajeti zao, …kilichohitajika ni kiasi kiyakachokufaa…na kukubali kwako kuwa
mshirika mwema katika kesi hii….najua unajua umuhimu wa maisha ya baadaye,
walishasema kuwa ulishapata kazi mahali, lakini hiyo nafasi inaweza isisubiri
hadi kesi hii itakapoisha, ila kama ikiisha vyema na kama upo tayari kwa kazi
wanaweza kukutafutia sehemu nyingine…’akasema wakili.
‘Yote hayo kwa ajili yangu..au ndio ili nishirikiana nao
nyie kweney hii kesi..?’nikauliza.
‘Sio kwa hilo, ila ni kwa ajili ya kuwa mtu wao wa karibu,
umefanay kazi nyingi kwao, na wao wamkuwa wakitunza fadhia zako, na wameona
kuwa ni vyema kesi hii ikiisha iwe ni sehemu ya kukulipa fadhila zako…kumbuka
na wewe unahitaji kutulia na kuwa na maendeleo yako, sio kuwa tena mtumwa wa
wengine…’akasema wakili.
‘Ili niyaamini hayo nahitaji hiyo hundi ….kesho….’nikasema
na wakili akahisi kuwa atahakikisha kuwa inapatikana na yeye kama wakili
atahakikisha kwua hundi hiyo ni ya ukweli na mkataba wa kieshria unakuwepo
utakaohakikisha haki yangu..na kweli kesho yake kila kitu kikatayarishwa na
hiyo hundi ikaanadikaila haikuweka tarehe,….
‘Tarehe itaandikwa siku kesi ikiisha…’akasema wakili…
‘Kwanini……?’ nikauliza.
‘Kwasababu bado upo kwenye kesi, …ndio kesi inaendelea
vyema, lakini lolote linaweza likatokea, je hundi hiyo itakuwa na manufaa
gani…ngoja ukitoka ndio hudni hiyo ianze kufanya kazi…’akasema wakili na mimi
nikakubaliana na hilo wazo.
*********
‘Kesi hii ni ya kudai haki, ….haki ya wanyonge, haki ya
wanaudhulumiwa na kufanywa kama watumwa ndani ya nchi yao huru….ukiwa huna uhuru
wa kuamua mambo yako mwenyewe,ukawa umefungwa mikono yote miwili , una njaa,
una shida, …huku unaambiwa ufanye hivi ili ulishwe…..una nini tena hapo duniani,
utakubali …’akaseme Yule mwanadada wakili.
‘Dunia hii imetufunga sisi wakinamama,…tumefungwa mikono
yote yote miwili….tuna njaa, tuna shida, huku tukiahidiwa kulishwa vinono…hatuna
mikono,hatua kauli, kila tunachoongea kinatumiwa kama wimbo wakuburudisha
wakubwa, sasa kama njia ya matangazo kwa manufaa ya matajiri…..miili ytu
inatumika kama bidhaa na matangazo, kwa kupewa majina na sifa kebekebe…..lakini
nini tunachokipata mwisho wa siku…’ akasema wakili na kuwaangalia wazee wa
baraza.
‘Ndio maana nasema sisi ni watwana ndani ya hii dunia….sasa
tunahitaji haki…kwasababu haki ipo, haki ipo kisheria, na hata kidini,….mengine
ni mambo yaliyotungwa na hawo wanaojiona matajiri,….., na kesi hii ndiyo
itakayobadili mtizamo huu kama sheria ilivyo na tunaomba haki ishike mkondo
wake, na wahusika wawezekuchukuliwa hatua zitakazoweza kukomesha haya yote.
‘Ni wangapi wasiojua kuwa hawo akina dada mnaowaita majina
mabaya wengine wanatumiwa kujiuza kwa mslahi ya wachache, wanajitosa
mabarabarani bila ridhaa yao, wengine wamejengewa nyumba za kukodi na kutumiwa
miili yao kama bidhaa za kuzalishia mali kwa ajili ya wakubwa….ni nini wanachopata
mwisho wa siku…..’akasemahuyo mwanadada.
‘Sio kwamba natumia nafasi hii kuhutubia siasa, muheshimiwa
hakimu, bali nataka koti yako hii tukufu ione hali ilivyo kabla sijamuita
shahidi wangu muhimu….’akasema huyo mwanadada pale alipolalamika wakili
mtetezi.
‘Ninachotaka kuonyesha ni mnyororo ambao kutokana nawo hili
tkio limetokea, na kama tusipotambua gilo chimbuko,hakuna atakayeweza kuona
kwanini wanawake wakajiingiza katika matendo haya,na kutokana na mtendo hayo,
watu wanapoteza maisha ….chanzo ni huo mnyororo…lakini umefungwa kitaalamu
kiasi kwamba hakuna anayeweza kugundua…’akasemana wakili mwenzake akalalamika
tena
‘Wanawake ndio
waliounganishwa katika huu mnyororo, nitakuja kutoa ushidi kamili kwanini
nasema hivyo, …ila hapa natoa kama muhutasari ili muda ukifika koti yako tukufu
iweze kuunganisha haya niliyozungumza na matukio kamili likiwemo hili kwenye
hii kesi….’akasema mwanadada.
Kesi iliahirishwa ….
**********
Kesi ilipotajwa tena,watu walifuria kama kawaida, na
mashaidi mmbali mbali walitwa toka sehemu zote mbili, na kila hatua huyu
mwanadada aliweza kutoa maelezo ambayo wakili mwenzake alikuwa akiyapinga mara
kwa mara kuwa wakili huyo anatumia mahakama kama eneo ya kisiasa badala ya
kutoa hoja au ushahidi unaoendana na hiyo kesi…
‘Hawa wanawake wanaotumiwa kama chombo chakuwastarehesha mbwana
wakubwa, moja kwa moja utasema wamejitosa wenyewe kufanya hivyo, lakini sio
kweli, kuna nguvu ya kiuchumi, kua nguvu ya kisaikolojia na kuna nguvu ya
kimtego ambayo hawa watu wanaondesha hizi biashara, ama kwa kutokana na pesa
zao na ujanja wa kitaalmu wameweza kuwanasa hawa wanadada na wakajikuta
hawawezi tena kufanya lolote zaidi ya kuitikia kile walichoagizwa…..’akasema
huyo mwanadada.
‘Ndugu muheshimiwa hakimu, natoa mfano mmoja ulio wazi
kuhusiana na hawo waitwawo warembo,….vimwana, au ….angalia jinsi wanavyotumiwa
kwa manufaa ya matajiri, na nini wanachokuja kupata mwisho wa siku ni ukandamizaji wa hali ya juu….picha
zao zinatumiwa kama matangazo ya biashara .ukizingatia kuwa mwanamke mwili wake
wote ni kivutio, na pasi na kulijua hilo, wanawake wamekuwa wakinyinywa, na ili
hali wao ndio masikini wa kutupwa.
Kama nilivyoanza kuonyesha katika ushahidi wetu mwa mwanzo,
waanwake wamekuwa wakitumiwa katika ngono, na pica zao zinachukuliwa kama
silaha, mapicha ya uchi yanasambazwa, kwa vitisho , kuwa usipofanya hivi tutazifikisha
sehemu Fulani, tutaziweka kwenye magazeti, na kama ushahidi ulivyoonyesha ni
kuwa picha hizo zimeuzwa ncho za nje, kwa ajili ya maslahi ya hawo ambao
wamtufikisha hapa tulipo….’akasimama pale wakili mwenzke aliposimama na
kulalamika, kuwa wakili mwenzake badala ya kuelezea kuhusu hiyo kesi anaingili
mambo mengine yasiyohusika.
‘Wakili tunakuomba uwe katika mpangilio wa kesi hii na
kuonywa kwa mara nyingine, kama hayo unayoongea yanahusiana na hii kesi
tunaomba uweke katika msingi uliokubalika…’akasema mheshimwa hakimu na wakili
akaomba mashama na kuanza kuongea kwa njia nyingine.
‘Mheshimiwa hakimu, kutokana natoa vielelezo hivi hapa
ambavyo vinaonyesha hawa akina dada na poicha zo ambzo zimekuwa zikitumika kama
vitisho,…na hizi hapa zimekuwa zikitumika katika maswala ya kibiashara watu
wanafaidika nazo bila hata weneywe kujua au kupata chochote na hata kama
watakipata ni sehemu ndogo tu ya haki yao…’akasema huyo mwanadada.
‘Je hivi vinahusika je na hii kesi yetu..?’ akauliza hakimu
‘Muheshimiwa hakimu, hizi ndizo silaha za vitisho, ambazo
huchukuliwa wakati mhusika hajijui, ama kwa kupewa madawa yaliychanganywa
kwenye kinywaji na kutokana namadawa hayo anafikia hatua anafanya mambo ambayo
akiwa katika hali halisi asingeliweza kuyafanya…’akasema wakili.
‘Mambo kama yapi…?’ akauliza hakimu.
‘Kutokana na hali iliyopo, tusingeliweza kuyaweka yote hayo
hadharani ndio maana tumetumia vielelezo vya picha zilizchukuliwa na hawa watu,
tunaziwakilisha kwako kama ushaidi….’akasemawakili.
Kukatokea mabishano ya kuitaalamuu wa kisheria kuhsuiana na
hizo picha mpakahkimu akaingili kati na kusema picha hizo zitachukuliwa kama
ushaidi na ili ziwe na nguvu kunahitajika hawo watu walitendewa hivyo wafike
wenyewe mahakamani kama mashahidi ili ushaidi huo uwe na nguvu.
‘Ndugu hakimu, wengi wa waliotendeewa hivyo wamekuwa
wakiogopa , kutokana na kutishiwa uasalama wao, na wengien walishapoteza maisha
kwa kujiua au kupatwa mashinikizo ya moyo hasa baada ya kuonyeshwa hayo
waliyoyafanya kinyume na matakwa yao…’akasema wakili.
Kukatokea mabishano mengine ya kisheria wakili wa utetezi
akisema hayo anayozungumza mwenzake ni ubunifu tu, hayana msingi na hauhusiana
na hiyo kesi,…wakabishana hadi hakimu
alipoingilia kati na kumtaka wakili awalete hawo mashahidi ambao wanatumiwa na
ushahidi huo uwe unahusianan na hiyo kesi,
‘Kuhusu usalama wako utahakikishwa unakuwepo kwani wapo watu
wa uslama kuhakiksiha kuwa hilo linatekelezwa…..tunataka uwalete hawo mashahidi
….’akasema muheshimiwa hakimu baada ya kunong’onezana na wazee wa baraza na
wasaidizi wake.
‘Nduhu muheshimiwa tutasimamisha baadhi ya mashahidi ambao
wamajitolea kusema ukweli ambao ni miongoni mwawaathirika wa haya mathila, ya
haya mapicha …..na kutokana na hayo mapicha , au maonyesho mbalimbali, baadhi
ya vyombo vya habari, wamekuwa wakizitumia hizo picha zao,…na utaona jisni gani
mtu anavyodhalilika…
‘Isitoshe muheshimiwa hakimu pia wapo baadhi ya wafanyabiashara
wanazitumia picha hizo kwa ajili ya kutanagza biashara zao, hata bila ya ridhaa
ya hawa akina dada, je kuna uwiano upi au haki ipi au makubaliano yepi ambayo
yalimhusisha huyu mwanadada, au kuna makuablaino yepi, yatamlinda huyu mwanamke
aliyetumika hapo, zaiid ya kudhalilika na kuendelea kuwa masikini,…?’ akauliz
ahuyo wakili.
‘Hakimu akataka kumuuliza swali, lakini baadaye akaghairi na
kumuonyeshea kuwa andelee …
‘Utaona kuwa mwanamke ananyonywa, kwa kutumiwa mwili wake
kama kitega uchumi cha matajiri, kwani pegine kunaweza kukawa na mkataba uliotengenezwa
kinamna kwa maslahi yahawo matajiri, na lakini picha hizo hazitaishia hapo,
zitakwenda mbali zaidi kutegemeana na hilo tangazo au jarida au tangazo,na
wengine watazitumia kwa maslahi yao na huyu mwanamke aliyetumiwa hatafaidikia
lolote na hilo….’akasema wakili.
‘Je muheshimiwa hilo linahusiana vipi na hii kesi
.’akalalamika wakili mwenzake.
‘Kama nilivyosema toka awali, kuna mambo yanahitajika
kufahamika kabla, ambayo ni chimbuko la haya yote, ndio chimbuko la hii kesi….na
ukiichukulia kijuu juu hutaweza kuligundua hilo, ndio maana nilianza na
mashahidi wale waliotumika kama chambo, na mapicha hayo machafu….wao walitumiwa
kufanikisha yale makusudio kwa watu mbali mbali, na kama mlivyoona picha hizo
za ukahaba zilitumika kama silaha, …na baadaye nitakuja kuonyesha jinsi kesi
hii ilivyohusika na hili…’akasema huyo mwanadada.
‘Onyesha ili kuthibitisha hilo…liwe linahusu hii kesi….’akadai
wakili mtetezi.
‘Sio kazi yako kumuamrisha hivyo…’akasema hakimu na
kumuonyeshea ishara wakili aendelee kuongea
‘Tumezitoa hizo kama ushahidi kwenye mahakama yako hii
tukufu, picha hizo zilitumika kwa kutishiwa hawo walengwa kuwa zitaonyeshwa kwa
wakwe, kwa mabosi wao……na hizo hizo ndizo zilizotumika kwa hawo waheshimiwa
kuwa wasipotoa pesa zitasambazwa kwenye vyombo vya habari…..’akasema Yule
mwanadada na hapo hapo wakili wa utetezi akalalamika kuwa wakili mwenzake
anaongea mambo yasiyohusiana na hiyo kesi.
‘Ndugu muheshimiwa hakimu, tunatarajia kumsimamisha shahidi
wetu wa mwisho ambaye tunatarajia kuwa ataiwezesha Mahakama yako hii tukufu
kugundua mengi yaliyojificha kutokana na kesi hii hii, shahidi huyu amekuwa
akitumika kama dume la mbegu lisiloruhusiwa kuzalisha…’akasema huyo wakili na
watu wakaguna nawengine kucheka.
‘Hatatuaki kelele…tumeshawaambia kama hamtutulia
hamtaruhusiwa tena kuhudhuri hii kesi hapa ni sehemu ya utulivu,hapa ni
mhakamani kuna sheria zake…’akasema hakimu kwa hasira.
‘Narudia tena kwenu mawakili kuwa humu sio sehemu ya siasa tunachohitaji
hapa ni ushahidi….,’akasema Hakimu, na kuwaangalia mwakili wa pande zote mbili,halafu
akasema tena kwa ujumla.
‘Sawa kesi inaahirishwa hadi keshokutwa, na hakikisheni mna
ushahidi wa kutosha na tutamsimamisha huyo shahidi wenu wa mwisho kama
mlivyosema siku hiyo ya kesho kutwa ya tarehe….’ akasema hakimu na kesi
ikaahirishwa tena.
‘Huyo shahidi ni nani….?’ Nikasikia mtu mmoja akiuliza.
‘Hatujajua bado, …..?’ akasema wakili wa utetezi.Moyoni
nikawa nawazo kuwa ni mimi kama walivyoniamba,lakini bado nilikuwa sijaamua
nifanye nini, maana mimi nipo kwa washitakiwa nikiwa mshitakiwa namba moja, na
hawa wanaotaka kunisimamisha kama shahidi ndio miongoni mwa wanaonishitaki,…
‘Ingia kule….’mara nikaamrishwa niingie kwenye gari, huku
nikiwa sina nguvu , mwili ulishachoka kusubiri, …na nimekuwa nikilalamika kwa
kutokupewa dhamana, lakini niliambiwa kutokana na kesi ilivyo siruhusiwi kupewa
dhamana, wapo washitakiwa wengine walioungwanishwa kweney kesi hii lakini wao meruhusiwa
kupewa dhamana isipokuwa mimi tu.
‘Wewe huwezi kupewa dhamana kwasababu wamedai kuwa eti ni
kwa usalama wako na kesi ilivyo…’akaniambia wakili wetu.
‘Na weweumekubali iwe hivyo….?’ Nikauliza.
‘Sio swala la mimi kukubali, …dhamana ni haki yako lakini
kuna mambo ya kisheria ambayo wameyatumia wao,na huwezi ukalazimisha,
tumejitahidi , lakini mwisho wa siku tukaona tuache tu , kwani watatufikiria
vinginevyo….je umefikiria vipi kuhusu ushauri tuliokupa..?’ akaniuliza.
‘Ushauri upi…?’ nikauliza nikijaribu kuwaza….
‘Huenda wewe ni shahidi wao mkuu, kama walivyodai, na kesi
kama unavyoiona, watakachofanya ni kukubana kwa maswali,…na kamanilivyokuambia
usiongee nao lolote au kukubali mashinikizo yao…nia yao ni kutaka ionekane wewe
una kosa na ulikuwa ukitumiwa….kwahiyo kwa vyovyote vile ukiwa upande wao
utakuwa hatiani….’akaniambia huyo wakili.
‘Kwahiyo wakiniuliza maswali ya mtego nitafanyaje…?’
nikauliza.
‘Hilo niachie mimi, nikisema huwezi kujibu, usijibu lolote,
na kila akiuliza swali tuliao kwanza uniangalie mimi nitakuambiaje….’akasema
wakili.
‘Na hundi yangu umpe nani..?’ nikauliza.
‘Wewe unataka nimpe nani,..sema yoyote tutampa, lakini
itakuwa inafanya kazi baada ya kesi kuisha, kwavyovyote iwavyo…ila ikiwa upo
upande wetu…wewe unasemaje…?’akaniuliza na kunianglia machoni.
Akilini nilikuwa nawaza kuhusu mambo ya akina mama,
waliniomba sana, wakataka niseme ukweli mtupu, kwa maslahi ya vizazi vyetu, kwa
mslahi ya watoto wetu….sasa je nijitoe mhanga,nikasweke jela kwa ajili ya
maslahi ya vizazi vijavyo,wakati mimi sio mkosaji,wakosaji wapo na wapo nje
wanatesa….kwanini,kwanini na mimi nisitoke nje nikashughulika na mambo yangu,
pesa ndio hiyo mtaji wa kutosha…..
WAZO LA LEO: Vyovyote iwavyo, jaribu kusimamia kwenye haki, hata kama kwa kufanya hivyo wengine wataumia, watakuona mbaya, lakini ipo siku watakuona wa maana wakiijua hiyo haki ...kwani upo usemi usemao haki ya mtu haipotei bure
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
Swadakta ndugu wa mimi wazo limenigusa sana!!Mmmmhh kazi nzuri ndugu yangu daima mbele haturudi nyuma,Mungu azidi kukusimamia,Pamoja sanasana sana daima!!!!!!
Ninafikiria kuanza kuweka AUDIO VERSION ya hizi hadithi.
Kwa sasa nimechelewa, lakini naamini "next ijayo" ntajaribu ku-catch up nawe
Ndugu wa mimi na mzee wa changamoto,mubarikiwe sana...TUPO PAMOJA.
Mzee wa changamoto,hujachelewa sana, mambo kidogokidogo, na huo utalamu utumegee kidogo....
Post a Comment