Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, April 18, 2012

Hujafa hujaumbika-23‘Tunahisi kuwa huenda wewe ndiye shahidi unayetakiwa kusimama keshokutwa  wanataka kukusimamisha wewe kama shahidi, …sijui wana lipi jipya, kama ulivyoona,hakuna lolote walilotoa ambalo linaweza kukutia wewe hatiani na hawo wanaosema wapo nyuma yako…wameshindwa kutoa ushahidi,  sasa wewe unategemewa kuwa shahidi wao na tegemeo lao la mwisho…najua nia yao ni kukusimamisha na kukutega kwa maswali….uwe makini …..’akasema wakili huku akimwangali mke wangu kwa makini.

‘Umeshaongea na mume wako kuhusu hali halisi, ….natumai kutakuwa hakuna ubabaishaji, maana kama atakubaliana na matakwa ya hawo watu, hakuna jinsi….natumai unampenda kama ulivyodai…’akasema wakili.

‘Nimeshaongea naye, ….’akasema mke wangu huku akiniangalia machoni, kwa leo alionekana mnyonge sana, kiasi kwamba nilimuonea huruma, licha ya chuki nilizokuwa nazo juu yake, kuwa yote hayo yametokea kwa jili yake, sikujua kwanini anaonekana mnynge hivyoo tofauti na jinsi anavyokuwa siku zote. Huwa anajiamini, na mkakamavu….

‘Mke wangu….’nikataka kusema kitu, lakini mke wangu alinionyesha ishara ya kutokuongea lolote na wakili akamwangalia kwa makini na kusema;

‘Kwani kuna jingine ambalo mimi silijui…?’ akauliza.

‘Hapana muheshimiwa wakili…’akasema mke wangu, lakini mimi nilijua kuwa lazima lipo jambo,na  jambo lenyewe litakwua kubwa…lakini sikuwa an jinsi ya kulijua, nikatulia ….

*******

Ni karibu miezi sita sasa imepita kesi hii ikiendelea na kila siku watu wamekuwa wakijumuika kwa wingi, na hata wengine kutoka nchi za jirani, ambao kwa namna moja au nyingien kesi hii iliwagusa, na vyombo vya habari vimekuwa vikiandika kwa wingi, …kwao umekuwa msimu wa biashara..

Niliinama chini nikiwaza, nikikumbumbuka mengi,na kila hatua ya hii kesi nimekuwa nikiahidiwa mengi, nakumbuka hata siku kadhaa nyuma niliomba kuwa kesi hii ikiisha mapema, nipewe mtaji wa maana niondoke hapa mjini, nikajiunge na wazee wangu kijijini, ….nikajiunge na ushirika wa mke wangu wa kwanza ambaye nasikia wamempendekza kugombea udiwani kwenye eneo lao….namtakia kila laheri na mimi nikaomba kama ikiwezekana katika kura zitakazopigwa ya kwangu iwe mojawapo…lakini je itawezkena iwe hivyo.

‘Hilo tu unahitaji kisai gani…?’ akaniuliza wakili wetu.

‘Milioni ishirini tu…’nikasema na huyo wakili akaniangalia kwa mshituko, halafua akasema ;

‘Ni pesa nyingi kidogo, lakini nitawauliza wahusika, sizani kuwa kwao itakuwa pesa nyingi, na nakuahidi kama utashirikina vyema na kesi hii ikaisha vyema, pesa hiyo utaipata….nikuahidi hilo,…..’akasema huyo wakili.

‘Kwa vipi, maana wewe ni wakili tu, na watoaji hiyo pesa ni wengine….?’nikauliza.

‘Kama wakili najua ipi inawezkana na ipi haiwezekani,nimeshapendekeza hilo kwa wahusika na wao walishaliweka katika bajeti zao, …kilichohitajika ni kiasi kiyakachokufaa…na kukubali kwako kuwa mshirika mwema katika kesi hii….najua unajua umuhimu wa maisha ya baadaye, walishasema kuwa ulishapata kazi mahali, lakini hiyo nafasi inaweza isisubiri hadi kesi hii itakapoisha, ila kama ikiisha vyema na kama upo tayari kwa kazi wanaweza kukutafutia sehemu nyingine…’akasema wakili.

‘Yote hayo kwa ajili yangu..au ndio ili nishirikiana nao nyie kweney hii kesi..?’nikauliza.

‘Sio kwa hilo, ila ni kwa ajili ya kuwa mtu wao wa karibu, umefanay kazi nyingi kwao, na wao wamkuwa wakitunza fadhia zako, na wameona kuwa ni vyema kesi hii ikiisha iwe ni sehemu ya kukulipa fadhila zako…kumbuka na wewe unahitaji kutulia na kuwa na maendeleo yako, sio kuwa tena mtumwa wa wengine…’akasema wakili.

‘Ili niyaamini hayo nahitaji hiyo hundi ….kesho….’nikasema na wakili akahisi kuwa atahakikisha kuwa inapatikana na yeye kama wakili atahakikisha kwua hundi hiyo ni ya ukweli na mkataba wa kieshria unakuwepo utakaohakikisha haki yangu..na kweli kesho yake kila kitu kikatayarishwa na hiyo hundi ikaanadikaila haikuweka tarehe,….

‘Tarehe itaandikwa siku kesi ikiisha…’akasema wakili…

‘Kwanini……?’ nikauliza.

‘Kwasababu bado upo kwenye kesi, …ndio kesi inaendelea vyema, lakini lolote linaweza likatokea, je hundi hiyo itakuwa na manufaa gani…ngoja ukitoka ndio hudni hiyo ianze kufanya kazi…’akasema wakili na mimi nikakubaliana na hilo wazo.

*********

‘Kesi hii ni ya kudai haki, ….haki ya wanyonge, haki ya wanaudhulumiwa na kufanywa kama watumwa ndani ya nchi yao huru….ukiwa huna uhuru wa kuamua mambo yako mwenyewe,ukawa umefungwa mikono yote miwili , una njaa, una shida, …huku unaambiwa ufanye hivi ili ulishwe…..una nini tena hapo duniani, utakubali …’akaseme Yule mwanadada wakili.

‘Dunia hii imetufunga sisi wakinamama,…tumefungwa mikono yote yote miwili….tuna njaa, tuna shida, huku tukiahidiwa kulishwa vinono…hatuna mikono,hatua kauli, kila tunachoongea kinatumiwa kama wimbo wakuburudisha wakubwa, sasa kama njia ya matangazo kwa manufaa ya matajiri…..miili ytu inatumika kama bidhaa  na matangazo,  kwa kupewa majina na sifa kebekebe…..lakini nini tunachokipata mwisho wa siku…’ akasema wakili na kuwaangalia wazee wa baraza.

‘Ndio maana nasema sisi ni watwana ndani ya hii dunia….sasa tunahitaji haki…kwasababu haki ipo, haki ipo kisheria, na hata kidini,….mengine ni mambo yaliyotungwa na hawo wanaojiona matajiri,….., na kesi hii ndiyo itakayobadili mtizamo huu kama sheria ilivyo na tunaomba haki ishike mkondo wake, na wahusika wawezekuchukuliwa hatua zitakazoweza kukomesha haya yote.

‘Ni wangapi wasiojua kuwa hawo akina dada mnaowaita majina mabaya wengine wanatumiwa kujiuza kwa mslahi ya wachache, wanajitosa mabarabarani bila ridhaa yao, wengine wamejengewa nyumba za kukodi na kutumiwa miili yao kama bidhaa za kuzalishia mali kwa ajili ya wakubwa….ni nini wanachopata mwisho wa siku…..’akasemahuyo mwanadada.

‘Sio kwamba natumia nafasi hii kuhutubia siasa, muheshimiwa hakimu, bali nataka koti yako hii tukufu ione hali ilivyo kabla sijamuita shahidi wangu muhimu….’akasema huyo mwanadada pale alipolalamika wakili mtetezi.

‘Ninachotaka kuonyesha ni mnyororo ambao kutokana nawo hili tkio limetokea, na kama tusipotambua gilo chimbuko,hakuna atakayeweza kuona kwanini wanawake wakajiingiza katika matendo haya,na kutokana na mtendo hayo, watu wanapoteza maisha ….chanzo ni huo mnyororo…lakini umefungwa kitaalamu kiasi kwamba hakuna anayeweza kugundua…’akasemana wakili mwenzake akalalamika tena

‘Wanawake  ndio waliounganishwa katika huu mnyororo, nitakuja kutoa ushidi kamili kwanini nasema hivyo, …ila hapa natoa kama muhutasari ili muda ukifika koti yako tukufu iweze kuunganisha haya niliyozungumza na matukio kamili likiwemo hili kwenye hii kesi….’akasema mwanadada.

Kesi iliahirishwa ….

**********
Kesi ilipotajwa tena,watu walifuria kama kawaida, na mashaidi mmbali mbali walitwa toka sehemu zote mbili, na kila hatua huyu mwanadada aliweza kutoa maelezo ambayo wakili mwenzake alikuwa akiyapinga mara kwa mara kuwa wakili huyo anatumia mahakama kama eneo ya kisiasa badala ya kutoa hoja au ushahidi unaoendana na hiyo kesi…

‘Hawa wanawake wanaotumiwa kama chombo chakuwastarehesha mbwana wakubwa, moja kwa moja utasema wamejitosa wenyewe kufanya hivyo, lakini sio kweli, kuna nguvu ya kiuchumi, kua nguvu ya kisaikolojia na kuna nguvu ya kimtego ambayo hawa watu wanaondesha hizi biashara, ama kwa kutokana na pesa zao na ujanja wa kitaalmu wameweza kuwanasa hawa wanadada na wakajikuta hawawezi tena kufanya lolote zaidi ya kuitikia kile walichoagizwa…..’akasema huyo mwanadada.

‘Ndugu muheshimiwa hakimu, natoa mfano mmoja ulio wazi kuhusiana na hawo waitwawo warembo,….vimwana, au ….angalia jinsi wanavyotumiwa kwa manufaa ya matajiri, na nini wanachokuja kupata mwisho  wa siku ni ukandamizaji wa hali ya juu….picha zao zinatumiwa kama matangazo ya biashara .ukizingatia kuwa mwanamke mwili wake wote ni kivutio, na pasi na kulijua hilo, wanawake wamekuwa wakinyinywa, na ili hali wao ndio masikini wa kutupwa.

Kama nilivyoanza kuonyesha katika ushahidi wetu mwa mwanzo, waanwake wamekuwa wakitumiwa katika ngono, na pica zao zinachukuliwa kama silaha, mapicha ya uchi yanasambazwa, kwa vitisho , kuwa usipofanya hivi tutazifikisha sehemu Fulani, tutaziweka kwenye magazeti, na kama ushahidi ulivyoonyesha ni kuwa picha hizo zimeuzwa ncho za nje, kwa ajili ya maslahi ya hawo ambao wamtufikisha hapa tulipo….’akasimama pale wakili mwenzke aliposimama na kulalamika, kuwa wakili mwenzake badala ya kuelezea kuhusu hiyo kesi anaingili mambo mengine yasiyohusika.

‘Wakili tunakuomba uwe katika mpangilio wa kesi hii na kuonywa kwa mara nyingine, kama hayo unayoongea yanahusiana na hii kesi tunaomba uweke katika msingi uliokubalika…’akasema mheshimwa hakimu na wakili akaomba mashama na kuanza kuongea kwa njia nyingine.

‘Mheshimiwa hakimu, kutokana natoa vielelezo hivi hapa ambavyo vinaonyesha hawa akina dada na poicha zo ambzo zimekuwa zikitumika kama vitisho,…na hizi hapa zimekuwa zikitumika katika maswala ya kibiashara watu wanafaidika nazo bila hata weneywe kujua au kupata chochote na hata kama watakipata ni sehemu ndogo tu ya haki yao…’akasema huyo mwanadada.

‘Je hivi vinahusika je na hii kesi yetu..?’ akauliza hakimu

‘Muheshimiwa hakimu, hizi ndizo silaha za vitisho, ambazo huchukuliwa wakati mhusika hajijui, ama kwa kupewa madawa yaliychanganywa kwenye kinywaji na kutokana namadawa hayo anafikia hatua anafanya mambo ambayo akiwa katika hali halisi asingeliweza kuyafanya…’akasema wakili.

‘Mambo kama yapi…?’ akauliza hakimu.

‘Kutokana na hali iliyopo, tusingeliweza kuyaweka yote hayo hadharani ndio maana tumetumia vielelezo vya picha zilizchukuliwa na hawa watu, tunaziwakilisha kwako kama ushaidi….’akasemawakili.

Kukatokea mabishano ya kuitaalamuu wa kisheria kuhsuiana na hizo picha mpakahkimu akaingili kati na kusema picha hizo zitachukuliwa kama ushaidi na ili ziwe na nguvu kunahitajika hawo watu walitendewa hivyo wafike wenyewe mahakamani kama mashahidi ili ushaidi huo uwe na nguvu.

‘Ndugu hakimu, wengi wa waliotendeewa hivyo wamekuwa wakiogopa , kutokana na kutishiwa uasalama wao, na wengien walishapoteza maisha kwa kujiua au kupatwa mashinikizo ya moyo hasa baada ya kuonyeshwa hayo waliyoyafanya kinyume na matakwa yao…’akasema wakili.

Kukatokea mabishano mengine ya kisheria wakili wa utetezi akisema hayo anayozungumza mwenzake ni ubunifu tu, hayana msingi na hauhusiana na hiyo kesi,…wakabishana  hadi hakimu alipoingilia kati na kumtaka wakili awalete hawo mashahidi ambao wanatumiwa na ushahidi huo uwe unahusianan na hiyo kesi,

‘Kuhusu usalama wako utahakikishwa unakuwepo kwani wapo watu wa uslama kuhakiksiha kuwa hilo linatekelezwa…..tunataka uwalete hawo mashahidi ….’akasema muheshimiwa hakimu baada ya kunong’onezana na wazee wa baraza na wasaidizi wake.

‘Nduhu muheshimiwa tutasimamisha baadhi ya mashahidi ambao wamajitolea kusema ukweli ambao ni miongoni mwawaathirika wa haya mathila, ya haya mapicha …..na kutokana na hayo mapicha , au maonyesho mbalimbali, baadhi ya vyombo vya habari, wamekuwa wakizitumia hizo picha zao,…na utaona jisni gani mtu anavyodhalilika…

‘Isitoshe muheshimiwa hakimu pia wapo baadhi ya wafanyabiashara wanazitumia picha hizo kwa ajili ya kutanagza biashara zao, hata bila ya ridhaa ya hawa akina dada, je kuna uwiano upi au haki ipi au makubaliano yepi ambayo yalimhusisha huyu mwanadada, au kuna makuablaino yepi, yatamlinda huyu mwanamke aliyetumika hapo, zaiid ya kudhalilika na kuendelea kuwa masikini,…?’ akauliz ahuyo wakili.

‘Hakimu akataka kumuuliza swali, lakini baadaye akaghairi na kumuonyeshea kuwa andelee …

‘Utaona kuwa mwanamke ananyonywa, kwa kutumiwa mwili wake kama kitega uchumi cha matajiri, kwani pegine kunaweza kukawa na mkataba uliotengenezwa kinamna kwa maslahi yahawo matajiri, na lakini picha hizo hazitaishia hapo, zitakwenda mbali zaidi kutegemeana na hilo tangazo au jarida au tangazo,na wengine watazitumia kwa maslahi yao na huyu mwanamke aliyetumiwa hatafaidikia lolote na hilo….’akasema wakili.

‘Je muheshimiwa hilo linahusiana vipi na hii kesi .’akalalamika wakili mwenzake.

‘Kama nilivyosema toka awali, kuna mambo yanahitajika kufahamika kabla, ambayo ni chimbuko la haya yote, ndio chimbuko la hii kesi….na ukiichukulia kijuu juu hutaweza kuligundua hilo, ndio maana nilianza na mashahidi wale waliotumika kama chambo, na mapicha hayo machafu….wao walitumiwa kufanikisha yale makusudio kwa watu mbali mbali, na kama mlivyoona picha hizo za ukahaba zilitumika kama silaha, …na baadaye nitakuja kuonyesha jinsi kesi hii ilivyohusika na hili…’akasema huyo mwanadada.

‘Onyesha ili kuthibitisha hilo…liwe linahusu hii kesi….’akadai wakili mtetezi.

‘Sio kazi yako kumuamrisha hivyo…’akasema hakimu na kumuonyeshea ishara wakili aendelee kuongea

‘Tumezitoa hizo kama ushahidi kwenye mahakama yako hii tukufu, picha hizo zilitumika kwa kutishiwa hawo walengwa kuwa zitaonyeshwa kwa wakwe, kwa mabosi wao……na hizo hizo ndizo zilizotumika kwa hawo waheshimiwa kuwa wasipotoa pesa zitasambazwa kwenye vyombo vya habari…..’akasema Yule mwanadada na hapo hapo wakili wa utetezi akalalamika kuwa wakili mwenzake anaongea mambo yasiyohusiana na hiyo kesi.

‘Ndugu muheshimiwa hakimu, tunatarajia kumsimamisha shahidi wetu wa mwisho ambaye tunatarajia kuwa ataiwezesha Mahakama yako hii tukufu kugundua mengi yaliyojificha kutokana na kesi hii hii, shahidi huyu amekuwa akitumika kama dume la mbegu lisiloruhusiwa kuzalisha…’akasema huyo wakili na watu wakaguna nawengine kucheka.

‘Hatatuaki kelele…tumeshawaambia kama hamtutulia hamtaruhusiwa tena kuhudhuri hii kesi hapa ni sehemu ya utulivu,hapa ni mhakamani kuna sheria zake…’akasema hakimu kwa hasira.

‘Narudia tena kwenu mawakili kuwa humu sio sehemu ya siasa tunachohitaji hapa ni ushahidi….,’akasema Hakimu, na kuwaangalia mwakili wa pande zote mbili,halafu akasema tena kwa ujumla.

‘Sawa kesi inaahirishwa hadi keshokutwa, na hakikisheni mna ushahidi wa kutosha na tutamsimamisha huyo shahidi wenu wa mwisho kama mlivyosema siku hiyo ya kesho kutwa ya tarehe….’ akasema hakimu na kesi ikaahirishwa tena.

‘Huyo shahidi ni nani….?’ Nikasikia mtu mmoja akiuliza.

‘Hatujajua bado, …..?’ akasema wakili wa utetezi.Moyoni nikawa nawazo kuwa ni mimi kama walivyoniamba,lakini bado nilikuwa sijaamua nifanye nini, maana mimi nipo kwa washitakiwa nikiwa mshitakiwa namba moja, na hawa wanaotaka kunisimamisha kama shahidi ndio miongoni mwa wanaonishitaki,…

‘Ingia kule….’mara nikaamrishwa niingie kwenye gari, huku nikiwa sina nguvu , mwili ulishachoka kusubiri, …na nimekuwa nikilalamika kwa kutokupewa dhamana, lakini niliambiwa kutokana na kesi ilivyo siruhusiwi kupewa dhamana, wapo washitakiwa wengine walioungwanishwa kweney kesi hii lakini wao meruhusiwa kupewa dhamana isipokuwa mimi tu.

‘Wewe huwezi kupewa dhamana kwasababu wamedai kuwa eti ni kwa usalama wako na kesi ilivyo…’akaniambia wakili wetu.

‘Na weweumekubali iwe hivyo….?’ Nikauliza.

‘Sio swala la mimi kukubali, …dhamana ni haki yako lakini kuna mambo ya kisheria ambayo wameyatumia wao,na huwezi ukalazimisha, tumejitahidi , lakini mwisho wa siku tukaona tuache tu , kwani watatufikiria vinginevyo….je umefikiria vipi kuhusu ushauri tuliokupa..?’ akaniuliza.

‘Ushauri upi…?’ nikauliza nikijaribu kuwaza….

‘Huenda wewe ni shahidi wao mkuu, kama walivyodai, na kesi kama unavyoiona, watakachofanya ni kukubana kwa maswali,…na kamanilivyokuambia usiongee nao lolote au kukubali mashinikizo yao…nia yao ni kutaka ionekane wewe una kosa na ulikuwa ukitumiwa….kwahiyo kwa vyovyote vile ukiwa upande wao utakuwa hatiani….’akaniambia huyo wakili.

‘Kwahiyo wakiniuliza maswali ya mtego nitafanyaje…?’ nikauliza.

‘Hilo niachie mimi, nikisema huwezi kujibu, usijibu lolote, na kila akiuliza swali tuliao kwanza uniangalie mimi nitakuambiaje….’akasema wakili.

‘Na hundi yangu umpe nani..?’ nikauliza.

‘Wewe unataka nimpe nani,..sema yoyote tutampa, lakini itakuwa inafanya kazi baada ya kesi kuisha, kwavyovyote iwavyo…ila ikiwa upo upande wetu…wewe unasemaje…?’akaniuliza na kunianglia machoni.

Akilini nilikuwa nawaza kuhusu mambo ya akina mama, waliniomba sana, wakataka niseme ukweli mtupu, kwa maslahi ya vizazi vyetu, kwa mslahi ya watoto wetu….sasa je nijitoe mhanga,nikasweke jela kwa ajili ya maslahi ya vizazi vijavyo,wakati mimi sio mkosaji,wakosaji wapo na wapo nje wanatesa….kwanini,kwanini na mimi nisitoke nje nikashughulika na mambo yangu, pesa ndio hiyo mtaji wa kutosha…..

WAZO LA LEO: Vyovyote iwavyo, jaribu kusimamia kwenye haki, hata kama kwa kufanya hivyo wengine wataumia, watakuona mbaya, lakini ipo siku watakuona wa maana wakiijua hiyo haki ...kwani upo usemi usemao haki ya mtu haipotei bure


Ni mimi: emu-three

3 comments :

Rachel siwa Isaac said...

Swadakta ndugu wa mimi wazo limenigusa sana!!Mmmmhh kazi nzuri ndugu yangu daima mbele haturudi nyuma,Mungu azidi kukusimamia,Pamoja sanasana sana daima!!!!!!

Mzee wa Changamoto said...

Ninafikiria kuanza kuweka AUDIO VERSION ya hizi hadithi.
Kwa sasa nimechelewa, lakini naamini "next ijayo" ntajaribu ku-catch up nawe

emu-three said...

Ndugu wa mimi na mzee wa changamoto,mubarikiwe sana...TUPO PAMOJA.

Mzee wa changamoto,hujachelewa sana, mambo kidogokidogo, na huo utalamu utumegee kidogo....