‘Ndio kosa kubwa ulilo nalo, ubinfsi, na mfumo
dume…..sikulaumu sana, ila ninachokuambi ani kuwa peke yako hutaweza , huko ni
kujidanganya, huko ni kujipa moyo kusiko na msingi, ujue wenzako wapo wengi
wamekamilika kila idara, wamejiandaa kwa muda mrefu, ….na sio kiubabe, kutumia
miguvu, hapana wenzako wanatumia akili, sio kiujunja-ujanja tu wa kuongea
mdomoni, bali kwa utaalamu, kisheria na kisaikolojia…unasikia sana….’akasema
huyo mwanadada.
‘Ili iweje….?’ Nikajikuta
nauliza swali la kijinga.
‘Ili iweje…unanichekesha kweli, ….wewe mwenyewe umeamini
kuwa wao watakutafutia kazi, au sio, ina maana wana uwezo wa kuwashawishi
waajiri wakuchukue, waajiri ambao mwanzoni ulipoenda mwenyewe walikukataa…wao
wanaweza kumfanya muheshimiwa akasalimu amri, na kutoa kiasi kikubwa cha pesa
ambacho hakikuwa katika bajeti yake…halafu unauliza ili iweje, unaniuliza swali
kama hilo…nikujibuje….?’Yule mwanadada akaniangalia kwa mshangao.
‘Lilikuwa sio swali kwako,ila nilikuwa najiuliza
mwenyewe…’nikajitetea
‘Kwahiyo sasa umepata jibu...?’akaniuliza.
‘Unajua…mpendwa hujanisaidia katika hili
linalonikabili,unachofanya hapa ni kuniogopesha tu,…nini lengo lako la kuja
hapa, kunilaumu kuwa sijatekeleza hilo
tulilokubaliana au umekuja kunisaidi kama
wakili…?’ nikauliza.
‘Yote hayo yapo ndani ya uwezo wako, kwasababu tunaogopa
hata kukuamini tena, maana wewe tuliona ni seehmu muhimu ya kuwanasa hawa
watu,lakini bado hukutaka kushirikiana na sisi,inaonyesha una tamaa, tamaa ya
kazi, ….sawa kazi ungelipata, lakini je ingekuwa ndi mwisho wa yote
hayo…’akasema huyo mwanadada.
‘Kwanini….isiwe ndio mwisho, ulishawahi kukaa bila kazi
ukaona jinsi gani unavyozaraulika, unavyodhalilika…?’ nikamuuliza.
‘Tatzi lako hujajiamini…ndugu yangu, ina maana unafurahia
hiyo hali ….hujijui kuwa wewe ni mtumwa…..wewe unatumiwa kwa ajili ya
kuwatajirisha wenzako,na kujiweka hatarini…unawajua hawa watu vyema, wanakujali
kama utakuwa ni faida kwao, wakigundua kuwa wewe ni mzigo kwao,….watakumaliza
bila huruma…?’ akaniuliza.
‘Kwa hivi sasa siogopi, hata kama
wanataka kuniua waniue tu…mimi nina fadia gani tena, nimeshawekwa uchi mbele ya
wakwe..mbele ya watu ninaowaheshimu, sina maana tena….iliyobakia ni kutembea
uchi tu mitaani…kama punguani ’nikasema huku
nikionyesha uso wa huzuni.
‘Mwanzoni nilikuwambi wewe ni mwanaume au sio….hukujiuliza
kwanini nimesema hivyo…sio kwamba nyie wanaume mna ujasiri sana wa kupambana na
hatari…sio kwamba ndio maana wanakutumia kama dume la mbegu, …hapana, ila
niachotaka kukuambia hapa ni kuwa wakati mwingine sisi wanawake tunakuwa na
ujasiri zaidi yenu …..Je wewe unalikataa hilo,au
hujajua kuwa mfumo dume, unawakweza hata pale msipostahili kukwezwa….?
Akaniangalia machoni.
‘Inategemea,…huo ujasiri ni wa kitu gani, lakini mume ni
mume tu…na mke ni mke tu…kutoakana n hilo
unalopambana nalo….’nikasema huku nikiwaza hiyo kauli ya huyo mwanadada.
‘Mimi hapa ni mwanamke, na nipo tayari kukabiliana a hilo
kundi….licha ya kuwa najua hatari iliyopombele yetu, ni kama kujiingiza ndani
ya mdomo wa mamba, ili ukaukate ulimi wake….wewe unaweza kufanya hivyo,…?’
akaniuliza na kuniangalia machoni.
‘Kwanini nisieweze kama inawezekana….’nikasema kwa kujiamini,maana
hapo unatetea udume wako, hata kama
haiwezekani inabidi ukubali tu, kufa na tai shingoni.
‘Nakuona umeshasita,…kama unaweza kwanini tulikuagiza
mengine, umefanya mengine….huoni ulivyoukana udume wako,…sisi tunataka kuleta
mageuzi, kwasababu athari kubwa ni kwetu sisi wakina mama na watoto, nyie
mnatumiwa kama chambo tu, hamjali familia,
hamjali athari kwasababu nyie ni madume…..’akasema huyo mwanadada.
‘Lakini huyo …anyeendeleza haya ni mwanamke….’nikajitetea.
‘Tuyaache hayo,….maana naona hujanielewa,bado kichwa chako
kimetawaliwa na mfumo dume, tafakari haya kwa makini na angalia athari zake,
kwako na kwa vizazi vijavyo,…..Nakuomba ujue kuwa mbele yako kuna kesi, na kesi
hii kama itafuta sheria bila kupindishwa, utakuwa hatarini, …lakini najua kundi
hilo litakusaidia na huenda ukaonekana huna hatia, kama kawaida yao, ila safari
hii hatutakubali,hata kama utajiua…’akasema na kuangalia saa yake.
‘Kwanini nijiue…sasa kwahiyo..?’nikauliza.
‘Kwahiyo ni akili kichwani mwako,..je upo na sisi…ufe kiume,
au bado upo nakundi lako ukaendelee
kuishi kama mtumwa…hilo
nakuachia wewe mwenyewe ulitafakari….’akasema Yule mwanadada na kutaka kundoka,
na baadaye akasema;
‘Sisi kwa hivi sasa tuna ushahidi wote tunaouhitaji, na
itafika muda tutakuhitaji wewe kama shahidi…na
hapo hutakuwa na ujanja tena, na tunachogopa ni kuwa ikifikia hatua hiyo,
huenda ukasimama mahakamami mara moja na baada ya hapo tunaweza tusikuone
tena…..’akasema huyo mwanadada.
‘Kwa vipi..?’
nikauliza
‘Kwa vipi, …kama tungelijua ni kwa vipi, ingesaidia sana,
lakini wengi tuliwashauri hivyo, na pale walipokubali kuwa watashirikiana na
sisi, sijui ni kwanini, hawakuweza kusimama mahakamani mara ya pili yake…..….’akasema
huyo mwanadada.
‘Walifanya nini….?’nikauliza
‘Walijiua….’akasema huku akionyesha uso wa kutafakari na
kunifanya na mimi niwe mwenye mawazo mengi kichwani, nikijiuliza kwanini watu
wafikie hatua hiyo,na mara huyi mwanadada akaangalia saa yake, na kabla
sijauliza swali akainuka na kuondoka na alipofika mlango akasema;
‘Wewe ni mwanaume au sio…? ‘ akauliza na kuniangalia
machoni. Na mimi nikamwangalia kwa makini halafu nikatingisha kichwa kukubali.
‘Basi pambana kiume,….’akatabasamu na kuondoka.
‘Mume wangu usijali,
wakili wetu keshafanya vitu vyake, unachotakiwa wewe ni kutokujibu
maswali yoyote utakayoulizwa na askari au mtu mwingine yoyote pasipo na wakili
wetu…unanielewa ninalokuambia..?’akaniambia mke wangu.
‘Nimekuelewa,…lakini nina maswali nataka kukuuliza…’nikasema
‘Maswali mengine hayana msingi hapa, kama ni kuhusu hiyo
kesi yako utamuuliza wakili wetu, lakini kama ni maswala ya nyumbani,au sijui
ya nini,…ya kazi, huu sio muda wake….utafanyaje kazi na wakati umeshikiliwa
huku,…..cha muhimu wekeza fikira zako katika kukabiliana na hawa watu,maana inavyoonekana
safari hii wanajaribu kupenya kweney ukuta wetu,..nawasikitikia kwani hawajui
ndani kuna nini..’akasema mke wangu.
‘Wakina nani hawo….?’nikauliza.
‘Kuna makundi mawili, moja ni hawo wanaojiita serikali, hawa
htunajua jinsi gani ya kufanya, lakini kuna kundi jingine limeibuka, eti
watetezi wa haki za akina mama na watoto…wao wanajifanya wanajua sana, ngoja
tuwaone, …wanadai eti huyo mke wa muheshimiwa, kauwawa, wakati mazingira yote
yanaonyesha kafa kwa mshituka wa moyo, ….’ Akatulia na kuniangalia kwa makini.
‘Ndivyo ilivyokuwa lakini…..’nikasema, na bila kujali
akaendelea kuongea
‘Na wamefikia kusema eti, kutokana na hicho kifo cha mke wa muheshimiwa
ndio maana hata muheshimiwa mwenyewe kapatwa na kiharusi, …na sasa hivi hawezi
hata kuongea…’akasema mke wangu.
‘Kwani huo si ndio ukweli wa hilo, ….na kwanini haya yote….?’nikauliza
‘Ndio maana nakuambia utulize kichwa chako,na mambo yote
muachie wakili, ukianza kuropoka, utaozea jela, …..na usipende kuuliza uliza ….kwanini,
kwanini….ukijua kwanini ndio utafanya nini…’akasema mke wangu.
‘Hivi mimi mnanionaje kuwa sijasoma, kuwa sijui kuongea
kuwa…yaani mnanvyonifanya mimi ni kama zezeta tu, kila kitu nafanyiwa au
kuelekezwa tu fanya hivi, usifanye hivi….mnanifanya kama
mtoto au mtu asiye na akili,kwanini nisijue nini kinachoendelea, kwanini
mnanifanyia hivyo….’ Nikakunja uso kwa hasira huku nimemkazia machoo mke wangu.
‘Hasira hasara…..’akasema huku akitabasamu.
‘Hasira hasara,…..tutaona, …sasa nikuambie ukweli, mambo
yamefika kikomo… sasa nimeshindwa kuvumilia, hamuwezi mkanifanya mimi chombo
chenu cha….’nikasema kwahasira na kablasijamaliza, mke wangu akaniwekea kidole
chake mdomoni.
‘Kama umeshindwa kuvumilia,
njia ni rahisi, nitakuleeta tindikali,…..unakunywa mwenyewe….’akasema mke wangu
huku akiniangalia machoni.
‘Sikiliza wewe mwanamke, mimi sio hawo waheshimiwa, unajua
kwanini wanafikia hapo, kwasababu wameweekza huko, wanaogopa kuumbuka,…mimi
naogopa nini…nitakosa nini….usinitishe,na kama
ni kunywa hiyo tindikilai utakunywa wewe….’nikasema huku moyoni nikiwa na
wasiwasi.
‘Unajifanya jasiri sana,mume
wangu unajua nakupenda sana, naogopa hicho
unachojiringia nacho…mimi sitaweza kukutetea ikifika muda huo,…na hata hivyo kama nilivyosikia, huenda …’akatulia na kuangalia nje.
‘Huenda nini…sema usinitishe kabisa…’nikasema.
‘Wameshachoka na wewe, na wanasema ukiendelea kuwepo unaweza
ukawa kikwazo…’akasema mke wangu akwia na wasiwasi.
‘Kwahiyo….?’ Nikauliza.
‘Nisikilize kwa makini,….sikiliza nikupe ushauri wa
bure….wewe usisumbue kichwa chako bure kwa hivi sasa, wapo watu wanalipwa pesa
nyingi kwa mambo hayo, wanajua nini wanachokifanya, wewe hutaweza kufanya
lolote, ila kama umechoka na maisha, sikukatazi, ingawaje nakupenda sana, na ni
wewe peke yake ambaye niliona tunaweza kuishi na kuwa na familia yetu,….’akasema
huku akiangalai pembeni.
‘Familia yetu…nimechoka na lugha yako hiyo ya
hadaa….sikuamini tena, nikuambie kitu,….wewe umetumwa kunimaliza na kufikia
malengo yenu, sizani kama hayo unayoongea
yanatoka moyoni, ..na kama
hayo ni mapenzi ni yenu sio mapenzi halisi…’nikasema huku nikimwangalia
Kimwana.
‘Jamani….ndio uansema hivyo….hivi jiulize nani angelikubebe
katika hiyo hali kama sio mapenzi…kuna wanauem
wangapi, lakini nimekuja kukuchagua wewe…kwalipi bora…kaam sio kwamba
nakupenda, tatizo lenu wanume mkiambiwa mnapendwa mnaringa…’akasemamke kwangu
nakuniangalia machoni.
‘Hebu tuacheni na hizo hadaa, mimi nitafanya hicho msichokitaka, na tutaona
nini mwisho wake, tindikali sinywi, na wala sumu gani,labda mninywishe wka
nguvu….’nikasema huku nikiwa na wasiwasi.
‘Wewe….jifanye unajau sana….usifikiri
hata mimi napenda kuishi haya maisha ….kama kungelikua na njia ya kuyakwepa
ningelishayakwepa zamani, lakini sina ujanja, niliingia kilaini sana nikijua hapa
nitaukata, lakini…haya nikasema ngoja niachane nao, mungu wangu…najuta kwanini
siku ili niliongea hivyo, ….’nakasimama na machozi yakawa yanaonekana machoni.
‘Ilikuwaje….?’ Nikamuuliza kwa wasiwasi.
‘Siwezi kukuambai kwa sasa, ila ninaloweza kukuambia ni kuwa
hakuna njia,…. njia ni moja tu ambayo ni rahisi,…ambayo wengi waliamua
kuitumia, hatunao tena duniani, marafiki zangu wapendwa,….’akasema huku akiniangalia
usoni huku machozi yakiwa yametanda kwenye mboni za macho.
‘Ni wewe..lakini mimi siogopi hilo,
kufa ni kufa tu…hata kama upo humo au haupo,
ipo siku utakufa tu..sasa kwanini ufe kwa aibu, kwanini usife ukiwa unatetea
haki…..’nikasema kwa ujasiri.
‘Bravo…haya jitahidi ufe kwa ujasiri…unaijua tindikali
wewe…ukimwagiwa machoni itakuwaje, ..au ukitiliwa kwenye kinywaji ukainywa itakuwaje
huko tumboni…ni mifano tu midogo…wenyewe hawatumii nguvu sana,..wewe mwenyewe utachukua hiyo gilasi yenye
tindikali au chochote utakunywa,...'akasema huku akionyeshea kwa mikono.
Nikamwangalia anavyoonyeshea kwa mikono yake, na kukunja uso, na sikusema kitu kwa muda na yeye akaendelea kusema;
'Au utajimwagia hiyo tindikali mwenyewe usoni
…..bila hata mtu kukufanyia hivyo…hiyo ni mifano ya kujimaliza mwenyewe, lakini
sio lazima wafanye hivyo moja kwa moja, na sio lazima tndikali kama tindikali….’ Akasema huku akionyesha uso wa
kutahayari.
‘Hivi wewe unanionaje mimi, yaani, una akili zako timamu,
uchukue tindikali..ujimwagie..sikuelewi…? ’ nikauliza
‘Mimi mweneywe nilikuwa najiuliza hivyo,…lakini zipo njia
nyingine,…huoni hawo wanaushikwa na kiharusi,….walipenda iwe hivyo…mwili wa
binadamu upo upo tu, lakini kuna mambo ya kiingizwa kichwani,yakayumbisha akili
yako, huchukui muda, …..nimeona wengi na
mengi, ndio maana nasema ukiingia kwenye hili kundi ni rahisi tu, lakini
kutoka, njia ni moja tu,…..’akasema mke wangu nikamkatiza kwa kusema.
‘Kujiua…mumejidanganya …sio mimi…’nikajipa moyo.
‘Zipo njia nyingi, lakini muda utasema…kwani watu wanye
rongo nguvu, maaskari, wakubwa, waheshimiwa…unafikiri wao hawana ubavu, wana
kila njia ya kufanya , lakini waliasalimu amri….wenzako wanakujau kuliko
unavyojijua wewe…ndio fani yao…wamjiandaa….naona
wakili huyo anakuja , usije ukaropoka haya tuliyokuwa tukiongea….uwe mwangalifu
na kauli yako…’akaniambi mke wangu, na wakili akaja na mke wagu akaondoka.
‘Kesi imekaa vibaya kidogo, natakiwa kupamba na mawakili
wawili...sio hoja maana sio mra ya kwanza. Ila mengi yanategemea ushirikiano wako na mimi, ….kinachotakiwa ni kuwa mkweli,muwazi na mwepesi wa kuelekezwa….na cha mhimu kwa sasa, usiongee
na mtu yoyote kuhusu hii kesi kama mimi sipo….tatizoo ni kuwa huna jinsi ila
ukubaliane na hilo nitakalokuambia….’akasema wakili
‘Lipi muheshimiwa, maana umesema niwe mkweli,na bado unanipa
masharti…’nikasema na huyo wakili aakniangalia sana machoni akasema.
‘Unataka kufia jela, au kubakia uraiani….?’akaniuliza.
‘Hiyo ni kazi yako…’nikasema
‘Ndio maana nasema unatakiwa ukubaliane na huo ukweli,
….ushirikiane na mimi kwa kusema ukweli…na hilo litaweza kukusaidia vinginevyo…mtajuana
wenyewe, mimi kazi yangu nikuangalia ukweli na atakavyo mteja wangu….’akasema
huku akifungua `briefcase’ yake.
‘Haya ngoja tuanze kuongea jinsi ilivyo kuwa,….’akasema
wakili huku akifungua makabrasha yake, na mimi hapo nikajua kweli sasa
nimekamatika, ….
WAZO LA LEO: Ni vyema tukubali kuwa kama binadamu hatuwezi kujua kila kila kitu, wewe kama unajua hili mwenzako anajua lile cha muhimu ni kushirikiana.
Na pia tukubali kuwa kama binadamu kila mmoja ana udhaifu wake, hatuwezi sote tukawa wakamilifu, kwani unapomnyoshea mwenzako kidole, ukumbuke vidole vitatu vinakunyoshea wewe...
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment