‘Samahani
kwa kukusumbua asubuhi hii ndugu muheshimiwa....’ Ilikuwa sauti iliyomshitua
muheshimiwa katika usingizi mtamu, ....alishawaambia walinzi wake hataki
kusumbuliwa na simu zote alikuwa kazima, kasoro hiyo ambayo anayeijua ni mke
wake tu...alishanga kabisa kusikia sauti nyingine,sauti ambayo hakupenda
aisikie tena katika maisha yake.....
‘Nyie watu
situlishamalizana na nyie,...niliwalipa hela yote mliyotaka, na mkaahidi kuwa
sitawasikia tena katika maisha yangu..ina maana ndivyo mlivyo, hapa sisi mnanitafuta
ubaya, sitashindwa kufanya lolote baya hata kama
niku....’akaongea kwa hasira.
‘Sikiliza
muheshimwa, tunalozungumzia hapa sio kuhusu lile swala lako, lile
tulishamalizana kabisa,....na sisi tunatunza ahadi zetu, hili ni swala
jingine,kabisa ni kuhusu mkeo..’ile sauti asiyoitaka kuisikia ikasema na
aliposikia kuwa ni kuhusu mkewe, aliinuka haraka kitandani na kujiweka vyema,
alimtizama yule aliyekuwa kalala naye pembeni na moyo ukamsuta ...
‘Kafanya
nini mke wangu...?’ akauliza kwa sauti kali.
‘Tatizo
lenu inavyoonekana, nyie wawili, wewe na mkeo, mlikutana,wote ni kunguru haufugiki..samahani
kuwaita hivyo, muheshimiwa...’ile sauti ikasema.
‘Nauliza
kafanya nini mke-wa-wangu...?’ ikauliza tena kwa hasira.
‘Kwanza jiulize tumeipata wapi hii namba, ambayo anayeijua
ni mke wako tu...’ile sauti ikasema.
‘Kama hamtaki kuniambia kafanya nini, nitakata hii simu na
baada ya muda wa nusu saa mtaona nini nitakifanya...hamuniji mimi eehe, lile
swala la kwanza, nimkubali hivy hivyo tu, lakini sio kila muda mnataak
kunipanda kichwani,...hivi nyi...’akasema kwa hasira.
‘Tutashukuru
sana ukifanya hivyo muheshimiwa, maana hata mkuu
sana angelifurahi kusikia hivyo, kwani lengo lake ni safi kabisa, kutaka
kupata viongozi bora wasaidizi,utakuwa umemrahisishia kazi yake ya kuwachuja, ...ukumbuke
mpo wengi ambao wote wanagombea hiyo nafasi, kwahiyo...kwa mtindo huo utakuwa
makapi,,’ ile sauti ikatulia kidogo.
‘Hayakuhusu
hayo...’akasema mheshimiwa.
‘Ukumbuke,
tulishakuabaliana kuwa tutajaribu kuweka njie yako iwe safi,
sisi ni moja ya wafadhili wako, je upo tayari kuzalilika,.... wewe unafikiri wenzako
hawafuatilii nyendo zako,hasa wale wabaya wako, wakigundua kosa dogo
watahakikisha wanakumaliza kisiasa...unajua hilo...’simu ikasikiak ikisema.
‘Kwanini
hauniambii....’mheshimiwa akauliza kwa hasira.
‘Mkuu sana,
keshakuwekea alama ya kuuliza, ndio unachapa kazi sana, lakini madoa doa
kamahayoyanaharibu utawala bora, na akisikia mambo kamahayo,moja kwa moja
atakuona hufai kabisa kuwa kiongozi, ni kiongozi gani ambaye haijali ndoa
yake....’ile sauti ikasema, na mheshimiwa akageuka kumwangalia yule kimwana
aliyelala pale kitandani,...akajiuliza hawa watu wamejuaje mbali kote huku...
alitamani kumfukuza yule mwanamke mle ndani,lakini kwa muda ule
haingeliwezekana....
‘Lakini
tulishakubaliana kuwa hatutafutana-fuatana tena, hasa maswala yanayohusu misha
yangu, nyie jukumu lenu ni...mbona..’akalalamika.
‘Hilo
tulishakubaliana...sawa kabisa , na tukasema tutahakikisha kuwa hakuna
anayekusumbua tena, ili ufanikiwa kupanda ngazi katika maswala yako ya kisiasa,....na
tetesi zilizopo ni kuwa huenda ukateuliwa kuwa ....siunajau tena hilo, nchi hii
haina siri, lakini kwa mtindo huo sijui,...unajua mheshimiwa sisi tunajitahidi
kukulinda,tukijua kuwa ukishika usukani na sisi hatutasumbuliwa tena,...’ile
sauti iksema.
‘Ndivyo
tulivyokubaliana....sawa kabisa, ... na mimi nimewaahidi kuwa nikishika hiyo
nafasi sitavunja ahadi yangu...mbona nyie mnavuja ahadi..’akaanza kulalamika.
‘Sio sisi,
hili linamhusu mkeo...na tunafnaya kazi yetu ya kuondoa uchafu utakaokuharibia
....licha ya kuwa wewe mwenyewe hujatulia muheshimiwa, ...tunakuomba ili hizi
habari zisivuje,maana ikipita nusu saa waandishi wa habari wataipata hiyo
skeno, watamkuta mkeo hapo hotelini...’ile sauti ikasema.
‘Watamkuta
mke wangu...unasema wapi, ...hotelini ,anafanya
nini....haiwezekani...’akalalamika.
‘Wanasema
kuwa dhambi kama hiyo, adhabu yake huanzia
hapa hapa duniani, ukizini wake za wenzako, ukizini watoto wa wenzako na wewe
pia utafanyiwa hivyo hivyo kwa mkeo na kwa watoto wako..huyo aliye naye hapo ni
nani, sio mke wa mtu, unajua kuna usemi usemao,` titi fo tati’, au uovu kwa
uovu.’ile sauti ikasema.
‘Mke wangu
huko hotelini alifuata nini.....niambieni haraka....?’ akauliza kwa hasira huku
akiangalia kule kitandani kwa wasiwaasi.
‘Kwanza tumbukiza kwenye akaunti yetu milioni ishirini
haraka, kwa ajili ya hizi gharama...hatutaki malimbikizo zaidi, kumbuka milioni
ishirini, ...hiyo ni gharama ya kazi tunayokufanyia ya kukuondolea mauchafu
yako, na pili, hakikisha unafika mwenyewe hapo hotelini, na kuondoa mwili wa
mkeo,... ‘
‘Eti nini
mwaili wa mke wangu...’sauti ya muheshimiwa ikauliza kwa wasiwasi, na mpiga
simu hukujali hilo
swali akaendelea kusema;
‘Na hakikisha
kuwa hakuna kinachojulikana, na futa nyayo zako usijulikane kuwa ulifika mahali
hapo, kama huwezi sema usaidiwe, lakini ujue ni gharama...tunakupa dakika tano
za kutuambie tufanye weneywe au utafanya wewe ....na kama tutafanya sisi pamoja
na kutaka kujua kwanini mke wako alifika hapo tutahitaji shilingi milioni kumi nyingine...kwaheri..
‘Fanyeni
nyi...nyi....ooh, mungu wangu nimekwisha...’mheshimiwa alijikuta akikosa nguvu
, giza likatanda usoni,....kitu kikali kiachoma kifuani, ...akainua mkono
kujishika kutokana na yalemaumivu, mara uso ukatanda giza akadondoka sakafuni
na kupoteza fahamu....
*********
‘Mke wangu
kwanini mnanifanyia hivi...?’ nilimuuliza mke wangu nikiwa nimechanganyikiwa.
‘Hebu
sikiliza kwanza.., wewe hutakiwa kuwa hapa,....’akasema mke wangu akiwa
kasimama mlangoni na khanga moja, sikuwa na najali, nikijua mke wangu alikuwa
peke yake humo ndani, kama nilivyomuacha.
‘Ngoja
niingie ndani maana, huko...’nikasema nikisukuma mlango ili niingie ndani.
‘Hutakiwi
kukanyaga ndani, utaharibu kila kitu,... kumbuka wewe upo kazini,... nenda moja
kwa moja kazini kwako, huko ndipo unatakiwa uwepo, ...ulikuwa kwenye zamu ya kazi
za usiku...kwanini hufuati masharti, nilishakuamabi usije huku nyumbani,...haya
ingia kwenye gari twende nikukimbize huko kazini...’akasema mke wangu bila
kujali kuwa kavaa khanga moja, akaingia kwenye gari na kunifikisha sehemu ambayo
huwa napofanyia kazi za usiku.
‘Kama ...ikibidi
utasema ulichomoka mara moja tukakutana sehemu,...mimi na wewe,..yule mlinzi
atakuwa shahidi...’akasema huku akinivutia kwake, tukashikana kwa muda, halafu akasema;
‘Haya nenda
haraka, ukajitahidi kufanya kazi..., mengine yaache kama yalivyo...yatasawazishwa...ili
mradi uwe umefanya kama nilivyokuambia....’akasema
mke wangu bila ya kuonyesha wasiwasi.
**********
Ilipofika
asubuhi nilikuwa wa kwanza kuangalia magazetini,...lakini sikuona taarifa
yoyote ninayoihitaji, nikasubiri taarifa ya habari ya asubuhi, sikusikia
lolote, nikashangaa, ..
‘Ina maana
yule.... hakuwa kafariki...haiwezekani....’nikasema
‘Nani kafariki...?’akauliza
mmoja wa wafanyakazi.
‘Kuna mtu
mmoja alikuwa akiumwa sana,..tulikuwa tunamsikilizia, lakini nasikia bado anadunda...’nikadanganya.
‘Ndio
kuumwa sio kufa...mungu ana miujiza yake, wapo watu wabaya, wanaua,..wanafanya
machafu, mungu anawahifadhi tu, utajiuliza kwanini hawo watu wabaya wasife...kwa
uoni wangu, nafikiri Mungu anafanya hivyo kuwapa hawa watu nafasi huenda
watatubia na kuwa watu wema...’akasema huyo jamaa.
‘Kweli ...huenda
wakajijua na kuja kutubia...maana madhambi yamezidi duniani...inahitajika kila
mtu atubie kwa dhambi zake, kwani kwa ahli ilivyo, kila mtu ana dhambi zake..ingawaje
zinazidiana,.....’nikasema nikijaribu kujitetea.
‘Tena
haraka sana, usisubiri hadi kesho,maana dunia hii imekwisha,...kama umefanya
kosa, ukajijua ni mwanzo mzuri, vyema ukatubu haraka iwezekanavyo, kabla
hujachelewa, maana machafu ni kama kuonja asali, ....utapenda urudie tena na
tena, na ukizoea , basi utaoana ni jambao la kawaida, nafasi inakuwa haiogopi
tena,...bora kama mtu umejigundua ..acha mara moja, tubu kiukweli na usirudie
tena, kwani ukirudia utakuwa unamchezea mungu. ...’Akasema yule mlinzi, na
kabla sijamjibu akaongezea kusema;
‘Unajua
rafiki yangu, sasa hivi watu wanafanya
machafu kila kona,...kutokana na kazi hii ya ulizni, nimeona mambo ya ajabu
sana usiku.... usiku kunaharibika, ...unatamani ukimbie, maana gharika ikitokea
sijui hiyo ghadhabu ya mungu ita....maana nikuambie ukweli, usiku unaficha
mengi sana..’akasema huku akipiga miayo ya usingizi.
‘Kweli
....’nikasema na kutaka kuondoka, lakini yule mfanyakazi mwenzangu ambaye
hupenda sana kuongea akaendelea kuniongelesha akasema;
‘Nimesikia
kuna watu wanauza mili yao kwa uchafu wa ngono,....sio kusikia tu ,nimeshuhudia
hayo...hata wanaume wanarubuniwa, ....na eti kazi hiyo wanalipwa hela nyingi
sana, hizo ni pesa chafu hazina hata baraka...sasa fikiria huo
uchafu...wanafikiri kwa kufanya hivyo hawataadhibiwa,...adhabu yake inaanzia
hapahapa duniani, kwani ukizini mke wa mwenzako na wa kwako atafanyiwa hivyo
hivyo...’akasema huyo jamaa.
‘Inawezekana
kweli... eti eeeh...inawezekana ni kweli, eeh, hata mimi nakubaliana na wewe...’nikasema,
halafu nikasogea pembeni nikaishika simu yangu, nikiwaza, ...baadaye nafsi
ikasema ngoja nihakikishe, nikasogea mbali kidogo na yule mfanyakazi,ambaye
aliongeza maongezi ili tu tuwe naye, asipatwe na usingizi,maana kazi za usiku
zinachosha....
Nilipohakikisha
nipo mbali na yule mfanyakazi nikampigia simu mke wangu, nia hasa ni kutaka
kujua nini kinaendelea huko, licha ya kuwa niliambiwa nisubiri mpaka saa tatu,
lakini moyo haukuwa na subira tena, nikapiga simu kwa mke wangu...kuhakiki...
Simu iliita
kwa muda bila kupokelewa, na kila nilipokuwa nikisubiri, nikiwa nimeweka simu
sikioni na wimbo wa simu ukiwa unaendelea kuimbwa masikioni mwangu, kuashiria
kuwa mpokeaji hajapokea,na hapo moyo ukawa unajaa mawimbi ya hasira, wivu, na
chuki....na baadaye ikapokelewa;
‘Halloh,
nani...ooh, ...nimekuambia usinisumbue,...unataka nini asu..su..buhi ooh, .....’akapiga
miayo na halafu akasema;
‘Nimeshakuambia
kuwa wewe unatakiwa ubakie huko huko hadi saa tatu...unataka nini asubuhi
hii....’sautiya mke wangu ikasema ikionyesha bado yupo usingizini,..lakini kwa
mbali kwenye simu nilisikia sauti ya kiume ikiuliza ‘Ni nani huyo...’
‘Mke
wangu..na nani huyo anauliza huko...’kabla sijamalizia kuongea simu ikakatwa,
na kuniacha nikighazibika,na hata nilipojaribu kupiga tena ikawa
haipatikani,....
Mwili
ulinisisimuka,kwa hasira ,na wivu..kweli tenda mtendee mwenzako, ukitendewa
wewe kinauma,... ama kweli mkuki kwa nguruwe...nimesahau kuwa muda uliopita na
mimi nilikuwa na mke wa mtu, nikifanya hayo hayo anayofanyiwa mke wangu,
niliwaza hivyo, ...ingawaje sikuwa na uhakika wa moja kwa moja, lakini uhakika
gani wakati nimesikia kabisa sauti ya mwanaume ikiuliza...huyo mwanaume atakuwa
kafuata nini asubuhi hiyo kama sio alilala na mke wangu.
Kila hatua iliyopita, mawazo yakawa yananitesa
moyo wangu, ikafikia hatua najihisi kuwa mimi ni mtu mwenye bahati mbaya, ibu
kuwaza kosa limetokea wapi, labda kuna kitu nimekifanya ambacho hakikutakwia
kiwe hivyo, inawezekana ni kwasababu wazazi wangu hawajafurahiwa na mkehuyo
niliye naye, inawezekana...
Pia
inawezekana ni kwasababu ya jinsi nilivyomfanyia mke wangu wa kwanza,
nilitakiwa nimtendee haki, lakini sikujali hata pale alipokiri kosa lake na
kuahidii kuwa atajirekebisha. Lakini mwishowe alikuwali ukweli , akaona
hatutaivana, na sasa yupo katika hali nzuri, kwahiyo hilo
halina nguvu sana, kwasaabbau kama
tungeliendeela kuishi naye, huenda hiyo hali asingeipata, sasa kosa lipo wapi..
Labda ni
kwasababu ya haya mchafu ninayoyafanya, lakini haya mchafu yamekuja kwasababu ya
hali ngumu. Kwasababu..ya ooh, labda ni kweli kwasababu ya huyu mke wa pili...hapo
nikakanywea, nikaanza kuhsii jambo kwenye nfasi, lakini sikutaka liingie
akilini na kukubali moja kwamoja kuwa ni kwasababu ya huyu mke wangu...
Kwasababu
hiyo nimejikuta nikifanya yale ambayo hayafai, na matokeao yake na pata
adhabu,...ingawaje kwenye nafsi nilijitetea kuwa yote hayo nilikuwa nayafanya sio
kwa hiari yangu, ...lakini kwanini nikakubali, ...ama kweli ubaya utalipwa kwa
ubaya...nikajiona nitafute shughuli za kujisahaulisha huku nikiwaza nchukue
hatua gani, na ni nini hatima ya haya yote, na nikirudi nyumbani hiyo saa tatu
nichukue hatua gani, nifanyeje, maana siku zinavyozidi kwenda nazidi kudidimia
kwenye machafu, kwenye hatari....
‘Na
nikirudi nyumbani, kutachimbika, lazima nijitoe kwenye huu utumwa, ...kama kazi
yenyewe ili kuipata ni lazima nijizalilishe, ...sasa itanishinda, lakini hata
hivyo, nimeshatimiza kile walichokitaka, kwahiyo lazima niipate hiyo kazi
waliyoniahidi, maana nimitimiza kile walichokitaka, lakini kama watajifanya
wajanja zaidi, lazima niwachomee,...ndio hata kama wakiniita msaliti sitajali,
kama ni kufa, ...kila mtu atakufa tu...’nikawa najipa moyo kwa kuwaza hili na
lile, ilimradi saa ziende...
Saa mbili
ikafika, nikajua sasa nii muda wa kuanza kujiandaa kwa ajili ya kuondoka, nikijua
kamahakuna lolote mpaka muda huo, huenda kila kitu kipo shwari, nikamwangalia
mlinzi ambaye kwa muda huo anajifanya yupo kazini, ili mabosi wakiingia wamkute
anahangaika, ...ndivyo ilivyo, kazi za namna hii, unatakuwa umuonyesehe bos
kuwa unafanya kazi, ...
Nikiwa
nimuangalia huyu mlinzi nikakumbuka kipindi nilipokuwa ni bosi ofisini, ilikuwa
nikiingia tu ofisini, kila mtu anahangaika kwenye kazi yake,..utafikiri kweli
wanafnya kazi kwa bidiii, lakini ukiwapa
kisogo tu, wanafanya mambo yao mengine, wengine wanajisomea magzeti,...nilikuja
kugundua kuwa kipato na uwiano wa matabaka ya kipato nayo huchangia hiyo hali,
kipato hakirizishi kwahiyo huyo mfanyakazi anafanya kile ambacha anahisi ni
sawa na kipato chake na muda mwingie anaigiza tu kuwa anafanya kazi.
Nikiwa
ndani ya mawazo, nikainua kichwa kuangaliai dirishani, kwani nilisikia kama honi
ya gari, nikajiuliza ni bosi gani kawahi hivyo ofisini, maana kuingia kwao ni
kuanzia saa mbili na nusu, mara nikamuona yule mlizni akifungua geti, nikasubiri kwa hamu, na mara nikaona gari la
polisi likiingia,.... hapo mwili ukafa ganzi, miguu ikaisha nguvu,....macho
yakaanza kuona giza, nikajua sasa
kumekucha,...yale niliykuwa na wasiwasi nayo ndiyo hayo yamevumbuluka,.... ni
lazima watakuwa wamekuja kunikamata mimi...
‘Msomali,
....kuna maaskari wanakuulizaia huku nje......’ sauti ya mlinzi ikasema kwa
nguvu, sikuweza hata kumjibu. Nikajikongoja kutoka nje, kichwa kikiwa kikiwa
hakifanyi kazi..
Wazo la leo: Fanya mambo yako kwa malengo, usikate tamaa, jitahidi kila siku ufanya jambo katika mpangilio wako, hata kama ni kwa shida, hata kama ni kidogo maana kidogo kidogo hujaza kibaba
Ni mimi:
emu-three
4 comments :
Haya asante kwa ku update... Tulimis mwendelezo huu
Elisa nashukuru kwa kunimiss na wapendwa wengine mungu atajalia tu,
Hapa sasa naona utamu unakolea yaani nasubiri kwa hamu kuona /klusoma kinachoendelea...ama kweli mkuki kwa nguruwe...
Kweli dada yaNGU Yasinta Utamu kolea
Post a Comment