Nilifanya kama nilivyambiwa, baada ya chakula., na kinywaji kidogo, yule mama akasema;
`Mimi lengo langu ni kumkomoa mume wangu, yeye kila siku anajirusha na visichana vya mitaani, leo ni zamu yangu...na mimi..mmh, mbona hiki kinywaji kinakuwa ..nasikia kulewa...ooh...'mara akadondokla kwenye meza.
Mimi hapo sio kazi yangu, nilitakiwa kwenda chumba maalumu, huko nisubiri, na kweli nilipofika huko, nikatulia kidogo mara watu wawili wakaja wakiwa wanamsaidia yule mama kutembea, .....
'Oh, afadhali nimekukuta....mpenzi, nilijua umenikimbia, nasikia ovyo....mmh, najisikiaje sijui...'akasema na mimi nikamsaidia hadi kitandani.
'Usijali tupo pamoja...'nikamwambia na kuanza kufanya kama nilivyoagizwa...na nikamweka kitandani na kumchojoa nguo zote....nikajifanya kama vile tupo kazini, ....lakini haikuwa hivyo ni geresha, tu...nikamaliza na kuchuku anguo zangu...
'Usiniache mpenzi....'akasema.
'Nakuja usijali...', nikamdanganya na mara nikasikia kama anakoroma, nikageuka kumuangalia, ...nikakuta mdmo upo wazi, na macho yamemtoka ...nikamsogelea, na nilipomgusa, mara akawa kama anatuingishwa, na mara akatulia kimiya...
Nikaharakisha kutoka, nikafungua mlango na kutoka nje, lakini sikuwa na amani nikarudi tena, nikajaribu kumtikisa, lakini alikuwa kimiya...nikagua sehemu ya shingo ya mapigo ya moyo..kimiya...mwili ukaanza kuniishia nguvu, ina maana nimeua..lakini sio mimi...sio mimi, na mara nikasikia kama watu wanongea kwa nje...mwili ukafa ganzi, leo nimepatikana.....
***********
Kazi
naitaka, na ili nipate hiyo kazi inabidi nikubaliane na masharti ambayo
nilitakiwa niyafuate, nilitakiwa nikaonane na mama mmoja wa mheshimiwa, na kila kitu kilishapangwa
nilichotakiwa nikufika hapo kwa ajili ya chakula cha usiku na mengine yatafuta
baadaye...lakini.
Lakini
nimeshachoka na hiyo hali, nataka kuachana nayo, na ili niachane nayo inabidi
nikubaliane na utaratibu uliopangwa na kikao maalumu nilichokutana na wale
akina mama baada ya mkutano waohuo ambao ulikuwa ukizungumzia mambp ya kina
mama,na humo ndani ndio likachomekwa hilo swala na kupambana na hicho kikundi
haramu.
‘Ole wako
ukitusaliti...unamjau yule jamaa aliyekuwa akiitwa nani..na yule mpelelezi,na
yule ....wote sasa haivi hawapo duniani, na wengine wamepooza miili yao hawana
kauli tena, na ni sababu ya kujifanya wajuaji...’akasema mke wangu.
‘Mliwafanya
ninin...?’ nikauliza.
‘Hata mimi
sijui, ila habari ndio hizo, ikitokea hapo,mimi tena sina usemi, nitaomboleza
siku mbili tatu, nitakusahau nitapata mwingine...’akasema huku akijifanya
kusikitika.
‘Lakini
haya yote mnafikiri mtashinda,....kuna ubaya una mwisho wake, ipo siku mtanaswa
na sijui itakuwaje siku hiyo...’nikasema.
‘Hiyo
usijali, ipo siku,...hayo nimeyasikia miaka kumi iliyopita...kwa jinsi ilivyo
ukipya hata mwaka mmoja tu wa kutumia,inatosha, sasa, fikiri hali hiyo imekuwa
hivyo hivyo, sasa miaka kumi,hakuna cha kukamatwa au kushukiwa, ...wenzako
wamejipanga kitaalamu, kukitokea hivi wanajua jinsi ganii ya
kujihami...kwasababu hata mwanzo hatukuwa tunafanya hivi, leo tunatumia vyombo
va kitaalamu...’akasema mke wangu.
‘Sawa,
yangu macho..mimi nina imani kuwa ngoma ikilia sana,hatimaye hupasuka...na mwisho wa ubaya
ni fedhaha, bora ujihami sasa hivi kabla ya fedhaha...’nikamshauri mke wangu.
‘Sikia we
mtu, kama umeanza mambo hayo, kama unataka kusaliti, tafadhali ...narudia tena,
kama kuna mpango kama huo,acha mara moja,
utajuta...’akasema na kutoka nje, baadaye akarudi na kuniambia nijiandae ili
nikawahi huo mpango nilioandaliwa.
‘Kumbuka
huo mpango ni mahususii ya kupata pesa kwa ajili ya akzi yako,kama unahitaji
hiyo kazi fanya kaam nilivyokuagiza, lakini kama
huhiataji na huna haja ya maisha yako ya baadaye fanya kinyuem chake, na
..narudia tena, usije ukalogwa ukaenda kinyuma na makubaliano,ukisaliti, mimi
sitakuangalia mara mbili...wenyewe watajua nini cha kukufanya, utaiona sura
yangu ya pili, ....na ndio itakuw kwaheri...’akasema
Nilitaka
kumwambia usinitishe lakini nikatulia kimiya huku nikitafakari, maana huko kwa
akina mama nako nilishapewa majukumu na nikaahidi kwa maandishi, kuwa nitafanya
kama tulivyopanga na ili kufanikiwa hilo inabidi kuwe na usiri mkubwa ukizingatia kuwa kundi hilo lina mtandao
mkubwa...
‘Hawa watu
wanatumia mitandao, na wana wataalamu wa hali ya juu , wana watu wao huko nje,
hapa ni kama katawi tu, na walichofanya ni kupandikiza watu kile sehemu muhimu,
kiasi kwamba kila jambo klinalotokea sehemu husika haraka taarifa hizo
huwafikia kwenye ofisi yao kuu...’akasema dada mmoja ambaye ni mtaalmu wa
mitandao.
‘Kama ni hivyo tutawezaje kuwashinda, maana hata huenda kuna mtu wao, ....’akauliza mama
mmoja.
‘Ukiwa
kwenye mapambano angalia ushindi kwanza, ...hata kama unajua kuwa wewe ni mzaifu,
usijali, hata kama unajua kuwa mwenzako ana silaha kubwa kubwa,...wewe weka nia
ya ushindi, hiyo ni hatua kubwa sana ya kumshinda adui yako, pili mtangulize
mungu mbele, ukijua kuwa wewe upo kwenye haki, na mara nyingi haki ina nguvu
kuzidii batili....’akasema yule mwanadada mtaalamu wa mitandao.
‘Kujipa
moyoo ni muhimu sana...’nikasema.
‘Nduu yetu,
sisi hapa tumekutana watu waainifu, watu ambao wana uchungu na vizazi vyetu,
...maana ukiwajali watoto sasa, bila kujali kuwa huyu ni wangu, umelijali taifa
lako, umewajali na wao katika misha yao ya baadaye,...watuu huwa wanaangalia
familia zao tu, bila kujua kuwa watoto wao wataenda kuchanganyika na wenzao,
ambao labda ahwana malezi bora, unafikiri nini kitafuta, kama sio na wao
kuiga,...kwahiyo ili maadili yapevuke, ni muhimu kuhakikisha watoto wote
wanakuwa katika maadili mema.
‘Hiloo ni
kweli kabisa...akasema mama mwingine, maana hutaamini, yule mzee pale jirani
aliyekuwa akiwafungia watoto wake kwenye geti, wakitoka, wanasindikizwa, na
tulikuwa tukipenda walivyokuwa na adabu watoto wa yule baba, tulishangaaa kuona
mmoja wa watoto wake ni teja, mla unga....ina maana alikutana na makundi,
wakamshawishi akaanza kidgokidogo, wazazi hawajui, mwisho wanakgunduak
keshaharibika....
‘Ni
kutokana na ubinfasi, kujali familia yako tu ukajiona uanzo, ukajiona uanjua
kulea, ukasahau kuwa watoto sio wako tu, hata wa wenzako ni wako, watoto ili
waishi vyema, inabidi wakutane na wenzao, wabadilishane mawao,wajifunze
changamoto za kimaisha na wewe kama mzazi unatakiwa uwe karibu nao, ili ujue
nini wanakihitaji, nini kinachowakwaza, sio kufungia ndani
...haitasaidia...’akasema mama mwingine.
‘Hilo ni moja ya ajenda zetu, tukisimamia kwenye msimamo
wetu kuwa sisi ndio walezi, sisi ndio wakulijenga taifa hili, mwanamama akielimika,
taifa limelimika, ...kwasababu sisi ndio tuliokaribu sana
na watoto wetu, sisi sio tunaowajau watoto wetu vyema, sisi ndio tunaowajua
waume zetu vyema, kama humjui mume wako,
tutakuashangaa,...’akasema yule mama kungwi.
‘Na wewe
umeanza tena....’akasema yule mwanadada mtaalamu.
‘Hilo ni kweli binti
yangu, nitashangaa nikikuuliza kuwa mume wako ana alama gani mwilini ushindwe
kuniamabia...itakuwa ni ajabu kabisa, wewe unatakiwa umjue mume wako, kila
sehemu ya kiuongo chake,...nitakuap kisakimoja cha ajali iliyotokea
mahali,...watu wengi wakapoteza maisha, na mle kuna baadhi walipona.
‘Sasa watu
wakawa wanakuja kutambua maiti zao,na ndugu na jamaa, mama mmoja alipofika
akakuta mkono upo karibu na maiti, na akawaambia wenzake huo ni mkono wa mume wake, mwili hautazamiki
ulivyo haribika , wanandugu wakaukusanya vyema ule mwili na kuondoka
nao,wakawasilina na hospitali, kua ule mwili hauwezi kulala tena,bora wa uzike
siku hiyo hiyo.
Mama mzazi
kila akilala anamuota mtoto wake kuwa bado yupo hai, akamuendea mke wa huyo
mtoto wake na kumuuliza,;
‘Una
uhakika kweli kuwa yule maiti ni mumeo...?’ akauliza.
‘Ndio yeye,
huoni mkono wake...uliokuw akaribu naye...’ akasema
‘Mimi
sioamini, naona kabala hawajauzika tuombe tukauchunguze vyema ule
mwili...’akasema mama.
‘Mama, eti
nini, hata mimi sikubali,....unatak niote maisha yangu yote...ile sura
itanikaaa kichwani miaka mingi, mimi hilo
siwezi ...’akasema mke.
‘Kweli wewe
ulikuwa ukimpenda mwanagu vyema...?’ aakmuuliza.
‘Ndio
nilikuwa nampenda, lakini sasa ndio keshakufa nifanyeje, hata nikimchunguza
vipi hatabadilika..’akasema yule mke.
‘Kamakweli
ulikuwa uanmpenda hebu niambie alama gani muhimu katika mwili wake
unazozikumbuka...?’ akamuuliza yule mke.
‘Alama
gani, mimi sikuwahi kumchunguza , ...mtu mwenyewe kukutana kwetu ni usiku,
mchana kila mtu na mihangaiko yake...’akasema mke.
‘Kosa hilo, hii inaonyesha wazi kuwa ulikuwa humoendi
mwenzako,...kama ungelikuwa unampenda vyema , ungelijua kila alama kwenye mwili
wake...wewe ulikuwa ukijali mali
yake tu, na sasa kaondoka, unatarajia nini, ...?’ akaulizwa.
‘Mimi
namuomba mungu nisahau, halafu akipatikana mwingine wa kunioa, nitashukuru ,
..hata hivyo nitajitahisi kuendeleza miradi yetu, na kama nikiolewa, huyo mume
nitamfundisha kama alivyokuwa kifanya mume
wangu aliyetangulia mbele za haki...’akasema mke.
‘Kwa
mtizamo wako, kuna mtu yoyote unayemtamani ...ili sisi tumchunguze kama anakufaa, maana wewe ni binti yetu,uliolewa kwetu na
hatutaki kukutupa....’mama akauliza.
‘Mhh, mama
hili tuliache kwanza, ....nitakuambia muda ukifika, yupo, lakini mbona mapema sana...’akasema mke.
‘Unamjua
vyema, maana waue wengine ni bora liende, mtoto wangu unasema alikuwa jembe kwa
kila eneo, sasa huyo unamjua vyema, usije ukaolewa na garasa...?” akauliza
mama.
‘Mama mbona
unaniuliza mapema hivi, tupo kweney msiba, tuawazei huu msiba kwanza,mambo
mengine baadaye...’akasema mke.
‘Hili ni
muhimu sana, maana tukimaliza msiba hapa utaanza
kuhangaika, na mimi hilo
sitaki, nijibu swali langu , huyo unayemtarajia unamfahamu vyema..?’ akaulzwa.
‘Ndio
namfahamu vyema...’akasema.
‘Ana alama
gani muhimu mwilini mwake, unazozifahamu..?’ akauliza mama.
‘Sijui....’akasema
yule mke.
‘Kwasababu
mlikuwa mkijiiba, au sio, lakini mume wako sio mtu wa kujiiba,mna uhuru
naye...kwanini umfanye kama huyo wa kujiiba,....ina maana hampendani basi....mwanangu
nimekuuliza hayo yote kama mzazi, mimi ndiye niliyewalea watoto wangu toka wakiwa
wachanga, kuna alama mwilini kwao zinapotea kabisa wanapokuwa wakubwa, lakini
zipo nyingien hazipoteia kabisa...na kuna nyingine zinajitokeza baadaye....mimi
namjua mume wangu tangu aliponioa, najua kila sehemu ya mwili wake...kwasababu
nampenda, ...kwasababu kuna leo na kesho...’akasema mama.
‘Mama una
maana gani, kusema unampenda, ...hizo alama zina umuhimu gani katika kupendana...’akauliza
yule mke
‘Mwanangu
kupendana ni pamoja na kujaliana, kuwa karibu na kufanya lolote kwa mwenzako
ikibidi, kwa mafano mume wako ana ugonjwa ambao hawezi kuvuta makamsi nje,
unaweza kuyanyinya kwa mdomo ili kuokoa misha yake? ‘akauliza mama.
‘Mama,unaingea
nini....mmh, unataka hata nisikie kutapika..’akasema huyo mke na kutafuta
sehemu ya kutema mate.
‘Lakini
wewe unaweza ukameza makamsi yako, inatokea hivyo mengine yanamezeka kwa mfano
ukiwa na mafua,au sio...makohozi na vitu kama hivyo inatokea ni uchafu ndio
lakini ni mambo ya kawaida kibinadamu, sio lengo langu kukukerehesha,ila nataka
kukuonyesha umuhimu kati ya mume na mke, kuwa wao ni kitu kimoja ...mwili wa
mume wako ni sawa na wa kwako, hebu nikuulize kuna alama gani mgongoni
mwako...?’ akauliza tena mama.
‘Sina
uhakika kama nazijua vyema...’akasema mke.
‘Ndio maana
mojawapo ya kuoana, kuwa wewe peke yako hujakamilika, lazima uwe na mwenzako wa
kusaidia kujua pale usipopajua,au kupafikia, kupeana mikono, kujaliana na
kushirikiana, kwasababu kuna sehemu zako huwezi kuziona, atakayeziona ni
mwenzako, ...’akasem mama.
Wakati wanaongea mara mlango ukagongwa, na
mama akasema, kabla hujamfungulia huyo mtu nikuulze swali moja, Je upo tayari
kwenda kumchunguza yule maiti kuwa kweli ni mume wakoo au sio?’ akauliza yule
mama.
‘Mama mimi
siwezi,hilo
utanilaumu tu,...sina uwezo huo...keshakufa basi, tumuombee mungu amalze mahali
pema peponi...’akasema mke.
‘Basi nenda
kamfungulie huyo mgeni...’akasema mama.
‘Unajua
nini kilichofuata, ...’yule mama akatuuliza, sisi tuaksema hatujui, tutajuaje
wakati yeye ndio msimuliji...akasema ;
‘Ghafla,
mshindo wa mtu kuanguka uaksikika pale mlangoni,na mama alipogeuka, alimkuta
yule mke wa mwanae kadondoka chini ....na mlangoni kasimama mtoto wake, akiwa
kafungwa, hana mkono mmoja....
‘Mwanagu
nilijua upo hai...usijali kupoteza mkono mmoja sio mwisho wa maisha, mungu
akupe maisha mema, na mkwe mwema...’akasema huyo mama na kutuangalia kwa
makini.
‘Ilikuwaje
kwa yule mwanamke ....?’ nikauliza.
‘Hilo sio
muhimu sana, muhimu ni ujumbe uliopo hapo, kama hujui alama za mume wako, na
mume wako hakujui, nyie hampenani, je wewe huzijui alama zako mwilini, achilia
mbali zile zisizo onekana,...unazijua, kwanini sasa usimjue mwenzako, wakati
mumeambiwa mkioana nyie mnakuwa mwili mmoja.....?’ akauliza na sisi
tukaangalia, kila mmoja akijaribu kukumbuka alama za mwenzake.
Yule mama
kila akikaa,anahisi kitu, akasema hata mimi sikubali kuwa yule ni mume wangu,
akaomba akaingalai ile maiti vyema,haitazamiki, kila kitu kimehariibika, ...
‘Natumai
ujumbe umefika sasa ni kazi.
*********
‘Tunahitaji
kupambana na hili tatizo, lakini hatuhitaji kutumia nguvu, ...sisi wanawake
silaha yetu sio kushika bunduki, sisi mungu katujalia, tuna silaha ya mdomo,
tunaweza kushawishi...kwanza cha muhimu ni kumjua adui yetu mkubwa...’akasema
yule mwanadada
‘Ni kweli tujitahidini kulifanikisha hili kwa
vitendo...’akasema mama mwingine na baadaye akaongezea kusema;
‘Mimi
nawaonea huruma sana hawo wasichana wanaofanya hizo kazi chafu, maana ukiwaona
hawo akina dada wanaotumikishwa na hayo machafu ni wasichana wadogo tu,
wamechukuliwa na kushawishiwa na kwa vile maisha ni magumu
wamekubali....wengine walifaulu kwenda sekondari, lakini kwa vile wazazi wao
hawana pesa, basi wakajikuta wakinaswa kwenye huo mtego, wakaahidiwa ajira, na
pesa...’akasema mama mwingine.
‘Tatizo ni
adui umasikini,na ujinga....na hapo ndipo tunataka kuingiza nguvu zetu, kwanza
tuanze kuwaelimisha ubaya wa hayo wanayoyafanya, tukiwa na makongamano,
mijadala ya mara kwa mara kwa kuwalenga wahusika, tutafanikiwa na ....makutano
yetu ni muda kama huu....hatuna ofisi, na kwa sasa hivi hatuhitaji ofisi...tukiwa
na jambo tunaitisha mkutanao, humo ndipo kwenye ofisi, na kama tulivyosema siri
ni jambo muhimu....tuwe makini ...wenzetu ni wajanja , lakini hata sisi ni
wajanja pia...’akasema yule mwanadada mtaalamu wa mitandao.
Nilikubali
kuwa nitashirikiana nao ili kuhakikisha tunakomesha hilo kundi, hatua kwa
hatua, na nikapewa mikakati jinsi gani ya kufanya,...waliniambia kuwa
wamenichagua mimi kwasababu imegundulika kuwa mimi ni mmojawapo wa watu
wanaotumiwa kufanikisha mambo ya hicho kikundi, ingawaje sipendi na sijui
undani wake....
‘Wewe
kuanzia sasa ukipewa hizo kazi tuwasiliane kwanza, tutajua jinsi ya kufanya…’aliniambii
yule dada wa mitandao.
‘Hawa watu
wana masikio wanajua kila kitu, mnaniweka kweney hatari kubwa sana…’nikajitetea.
‘Wewe
mwanaume bwana, ..upo vitani, ukiogopa tutashindwa, …mimi ni mtaalamu wa
mitandao, nimeshajua janja yao…ukija kuniona hakikisha huna simu wala hiyo saa
yao…hakikisha hivyo…kwa pamoja tutawashinda, tunachohitaji ni ushahidi wa
kitaalamu…’akaniambia
Kwa muda
ule nilikubaliana na wale akina mama kwa
haraka sana, bila kufikiria uzito wa jambo lenyewe,nilikubali kutokana ni
msongo wa utumwa niliokuwa nikikabiliana nao sikujali hatari ya hawa watu
wengine, ambao wanajua kumnyamazisha mtu hata kwa kutumia simu.
Nilijua
kabisa kazi hiyo itakuwa imeungwanishwa na hawa watu, sio mke wangu kama
alivyoda ....masharti niliyopewa ni kuwa ili nipate hiyo kazi inabidi nikamilishe hilo
jukumu la kukutana na huyo mke wa muheshimiwa, ….nitakiwa nifanye kama
nilivyowahi kufanya kazi nyingine, ila huyu anahitaji usiri wa hali ya juu
maana ni mke wa muheshimiwa.
‘Kazi hiyo
ipo mume wangu, lakini fanya kazi upate kazi…ikiisha hii nitakuambia jambo,
kwani hata mimi nimechoka na mambo haya….’akanihakikishie make wangu, ili
kuhakikisha hilo nikafanya uchunguzi wangu wa kimiya kimiya kweli nikakuta kazi
hiyo ipo, haina shaka, lakini kwa msharti kuwa lazima nimalizane na wakala
wangu, huyo wakala kafungwanishwa na mke wangu, sasa nifanyeje...nikabaki njia panda.
WAZO LA
LEO: Saidia watoto wetu kwa ajili ya kizazi kijacho, usijali kuwa huyo ni mtoto
wako au ni wa mwenzako, kwani ukifanya hivyo utakuwa umemjenga mtoto wako njia
ya kupita, tukumbuke mtoto wa mwenzio ni wa kwako pia
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Nimeshindwa kuendeleza sehemu ifuatayo leo sababu zipo juu ya uwezo wangu. Nijitahidi tu!
Post a Comment