Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, April 20, 2012

Hujafa hujaumbika-25



Kesi ilianza kama kawaida nikasimamishwa na sasa nikihojiwa na wakili wangu, ilichukua muda mrefu kunihoji, nikiwa niulizwa maswali najibu,na hapa na pale kunatokea ubishani wa kisheria, na inafikia hatua wakili Yule mwanamama anaomba kuniuuliza maswali tena na baadaye anaikuja wakili wangu mtetezi, na ikawa kama mimi ndio mpira unaochezwa na sehemu zote mbili, na ikaonekana dhahiri kuwa mimi ndiye nitakuwa ufunguo wa kushinda au kushindwa na baadaye ikafika muda wa mapumziko.

‘Vipi mbona unajibu tofauti na nilivyokuambia, kuna tatizo gani,huoni ulivyoniweka katika wakati mgumu, ilikuwa kazi rahisi tu, sasa wewe umaifanya imekuwa ngumu, kuliko maelezo, kuna tatizo gani…?’ akasema wakili wangu kwa hasira.

‘Mbona mimi nimjibu itakiwavyo….wewe ni wakili, na wakili unahitaji nini toka kwa mshitakiwa,…unahitaji ukweli au uwongo, ….ndani ya mhakama unatakiwa useme ukweli kwasababu ya kiapo, ….na ndivyo nilivyojaribu kusema ukweli….naomba unielewe hivyo,mimi sio mtaalamu wa uwongo….na hasa sehemu kama hii ambayo ina kiapo….’nikasema.

‘Kiapo….,ndio nakubaliana na wewe, lakini tangia mwanzo tulikuwa yuankwenda vizuri, kwa maslahi yako, na ndio jukumu langu kukutetea, au sio…?’ akasema na kuniangalia, na mimi nikawa kimiya nikiwa nimetingwa na mawazo tele kichwani, nilikuwa nimechoka kutokana na akzi hiyo ngumu.

‘Sikiliza mimi nipo hapa kwa ajili yako,kukutetea, na ndio kazi yangu, ….kama ulivyoona, nimekuwa nikijaribu humo ndani kukuweka sawa, lakini tunakuwa watu wawili tofauti, ….nikumabie ukweli ilishafikia sehemu nzuri,…leo tungemaliza mambo,  kesi hii haina miguu,haina ushaidi, wanakutegemea wewe tu, wengine wote hawana la kusema …sasa wewe umeshajitia doa mwenyewe,sijui nikimwambia bosi wako atasemaje….’akasema huku akikuna kichwa.

‘Nikuulize kitu muheshimiwa,…hivi wewe umesomea nini…?’ nikamuuliza na swali hilo lilimshitua na akageuka kuniangalia kwa muda.

‘Swali gani hilo, huoni nini ninachokifanya hapa….’akasema huku akikuna kichwa kuonyesha kuwa ana mawazo mengi kichwani.

‘Wewe ni wakili , na unajua kuwa ukiuliza swali unatakiwa ujibu, ….kama ulivyokuwa ukifanya ndani ya ulingo, ..au ukitoka nje uwakili unakuwa hauna maana, …mbona unakwepa swali langu….?’nikamwambia.

‘Haya ….unataka nikujibu, sawa, mimi nimesomea sheria…’akajibu

‘Sheria ambayo inakutaka useme ukweli au uwongo, utetee haki, au uwongo…?’nikamuuliza

‘Nimesomea sheria, ….unanielewa, mimi ni wakili, na hapa niwakili mtetezi, … kutetea haki yako, …uelewe hilo…sasa haki ipi ,  inategemea wewe mwenyewe, …unaweza ukatenda kosa, lakini kwa kutokujua sheria, ni haki yako kutetewa,hapo sijatenda uwongo unaodai….kwanza nikuulize kwanini umeniuliza hilo swali?’ akaniuliza.

‘Kwasababu wewe unajua kabisa kuwa unachotetea ni uwongo,…mambo wanayodai hawo akina mama na serikali ni kweli tupu,…tuseme ukweli tuwe wapenzi wa mungu,  wewe unayapinga, unasaidia huo uovu…huoni kuwa unakiuka miiko ya sheria..?’ nikamwambia kama nauliza.

‘Miiko ipi, niliyoikiuka….tatizo lako huelewi sheria,….hilo niachie mimi….nia na lengo langu ni kukutetea wewe, na kwa vipi, ni mambo ya kisheri ambayo huyajui,…nikuambie ukweli,watu wengi hufungwa, kwasababu hawajui sheria, na hawataki kututumiwa sisi, tukawatetea,…unanielewa lakini…’akasema wakili huku akionyesha kuwa nampotezea muda wake.

‘Zipo sheria zipo wazi hata kama hujasomea sheria….zinaonekana katika upeo wakibinadamu….utu wa mtu ni muhimu sana,na unatakiwa ulindwe, mambo ya kiutu,kibanadamu mambo yapo dhahiri….yaliyotendendeka haya utu,hayana ubinadamu, ndio maana mtu anashindwakuvumilia, hakutarajia,…..inafikia hatua mapigo ya moyo wake yanashindwa kuvumilia….’nikasema huku nikiwa ndani ya hisia.

‘Nataka uelewe nafasi yangu kama wakili mtetezi, ….imefikia hatua uanze kuamua moja, unataka kutoka jela au uanataka kufungwa,maana kama utajibu kinyume na nilivyokueleza,hakuna jinsi ni lazima utafungwa….’akasema na kuniangalai kwa makini.

‘Na je na wewe hutachukuliwa hatua kwa kutetea uwongo, katika kazi zenu hazina miiko hiyo…maana ikifikia hatua hiyo nitasema ukweli kuwa hata wewe ulijua hilo, lakini ukawa upande wa mteja wako,ukitafuta pesa badala ya ukweli…niambie ukweli, unafanya hyo kwaajili ya maslahi au unafanya kuangalia ukweli na haki..?’nikasema na huyo wakili akaniangalia kwa makini na kusema;

‘Tatizo lako hujui sheria…nakuuliza tena, unataka nikutetee utoke jela, au niache, maana natapoteza muda wangu kwa mtu ambaye hana ushirikiano na mimi….,mimi kazi yangu ni kukutetea, na si vinginevyo, kama haki na ukweli, sheria itaamua,…hiyo ni kazi ya hakimu, ila mimi kama wakili mtetezi natimiza wajibu wangu, …maswal ya maslahi ni mengine, ….nakuuliza tena,upo tayari nikutetee au hutaki..?’ akaniuliza.

‘Kwani mimi nimekataa usinitete…..sijakataa, kabisa, …kunasehemu nimesemakuwa sikutaki unitetee? ’nikauliza huku nikionyesha uso wa kuchoka.

‘Hujasema kwa kauli ya moja kwamoja, lakini umekuwa ukijibu maswali kinyume na makubaliano, wakati nakuelekeza jinsi ya kujibu maswali unajibu tofauti….tunakuwa hatuna makubaliano…kwamatindo huo unampa mwanya mwenzangu kunishinda….sijui unanielwa hapo?’ akauliza na kuniangalia machoni.

‘Nakuelewa,na mimi nataka unielewe pia…’nikasema.

‘Hebu nikuulize kuna ninii kimekupata,hadi ukabadilika kipindi hiki muhimu, niambie ili nijue nini cha kufanya, kwaninii umebadilika wakati tulikuwa tunakwenda vyema…?’ akaniuliza.

‘Ndugu muheshimiwa…mimi ni binadamu na nina hisia sawa na binadamu wengine, sitaweza kujibu uwongo, ambao matokeo yake ni kuangamiza vizazi vyetu..hebu fikiri wewe mtoto wako afanyiwe hayo tunayoyatetea,..utajisikiaje….tuwe binadamu wenye hisia na kuwajali watu wengine hata kama lengo letu nikutafuta maslahi…’nikasema

‘Una maana gani kusema hivyo….kwani hayo niliyokuelekeza ujibu, tena nakuelekeza mbleya mhakama, ni uwongo, je ina maana ulihusika katika kifo cha huyo muheshimiwa…nimabie kamakuna amblo mimi silijui, ili nijue jinsi gani ya kukutetea?’ akaniuliza

‘Sijahusika…sijasema nimehusika, ila najibu yale ambayo ni sahihi ninapoulizwa, lakini ukiniuliz a kuwa nimehusika, jibu la mkato nii kuwa sijahusika, kwasababu kweli sikuhusika,…ila kama sababu ya mtendo yangu, yalifikia hatua hiyo , hapo ukiniuliza nitasema yale matendo sahihi niliyoyafanya….je hilo ni kosa ndugu muheshimiwa…?’nikauliza

‘Matendo yapi,… na hujui ukisema hivyo unajihusisha moja kwamoja na kifo chake, pili unajidhihirisha kuwa kweli unatumiwa….na…tatu…wewe mtu, hivi nikuambieje, ndio maana nataka uniachie mimi, ufanye vile ninavyokuelekeza, tatizo lako hujui sheria, ndio maana watu kama sisi tupo, ili kukulinda uisije ukaumia…utaozea jela wewe…..’akasema huku akingalia saa yake.

‘Hilo nakubaliana nalo, nisilokubaliana nalo ni kusema uwongo , uwongo ambao upo dhahiri, moyo wangu unanisuta, na nitashindwa kuishi kwa amani, nitashindwa hata kuwaangali watoto wangu, nikijua kuna watoto wa wengine, nilishindwa kuwatetea mahakamani , ….huoni hawo wanaoathirika ni watoto wa wengine, sawa na watoto wako….?’nikasema kama nauliza huku namwangalia machoni. Na yeye akawa naniangalia kwa mashaka.

‘Kwahiyo utajibu kinyume na makubaliano yetu…au sio,… na kwa msingi huo hatupo pamoja, basi haina haja ya mimi kukutetea, ngoja niongee na bosi wako,kama inawezekana amtafute mtu mwingine unayemkubali…maana nitakuwa napoteza muda wangu na mwisho wa siku nitaonekana sijui kazi….’akasema.

Akaitoa simu yake huku akisita sita, na kabla hajampigia huyo anayetaka kumpigia, mara akaja askari na kusema huyo wakili anaitwa na hakimu. Cha ajabu aliiweka ile simu palemezani, na kuondoka haraka bila ya hiyo simu,….

*****

Nilibakia peke yangu kwenye chumba maalumu cha kuongelea na mara simu ya Yule wakili ikaita, nikaiangalia inavyoita,mpaka ikanyamaza, ikaita tena….na safari hii nikaingiwa  na hamu ya kujua ni nani anayepiga nikaisogelea na pale nikaona jina la Docta Mama,  nikacheka,…

Iliita mpaka ikanyamaza tena, ukapita muda , halafu ikaanza kuita tena, hapo nikatizama kule mlangoni,mlango ulikuwa umefungwa, nakaichukua ile simu na kuibonyeza kupokea na kuiweka sikioni.

‘Nakuambia hivi, chelewesha chelewesha hiyo kesi,  maana huyo mtu hatutaki aonekane tena …tutajua nini la kufanya…maana nimepata taarifa kuwa hana ushirikiano,na tukimuachia anaweza kutukaanga, umenielewa…fuata ninayokuagiza, …umenielewa lakini…?’akauliza huyo mwanamama,nikatulia kimiya…

‘Umenielewa…au …’nikakata ile simu na haraka nikatafuta sehemu ya kufuta simu hiyo iliyoingia na kuhakikisha haipo kabisa hata kwenye sehemu ya kumbukumbu ya simu zilizofutwa,halafu nikairudisha pale mezani ….na wakati naiweka wakili akaingia…

‘Huyu hakimu anataka kuleta mambo mengine…anataka kesi hii imalizwe haraka iwezekanavyo,nahisi keshaona jinsi ulivyo jibu hayo maswali leo. Ilikuwa ifanyike haivyo, lakini sasa nimeshindwa nifanyeje,kwani nikisema sawa, basi hakuna jinsi, utakwenda jela…

‘Hata hivyo bado una nafasi hawajui mtego wangu,ila yote yanategemea wewe…upo tayari nikutetee, au una nini cha zaidi,hebu niambie…?’akauliza na kuniangali, halafu akaichukau simu yake na kuangalia kama kuna simu iliita,hakuona kitu ,akanigeukia na kusema;

‘Hapa kuna simu iliita,….mmmh,ok, haian shida…’akasema na kunigeukia

‘Umefikia wapi, maana nataka kumpigia bosi wako ili nimfahamishe nini kinachoendelea, na ili anipe jibu, ili nikionana na hakimu nijue nini la kusema....yaani umaniweka katika wakati mgumu sana,..hii kesi ilikua yetu, haikuwa na kipingamizi, sasa sijuu hata nifanyeje, lakinii bado una nafasi,mimi nipo kwa ajili yako…je upo pamoja na mimi au nini uamuzi wako…?’ akaniuliza.

‘Mpigie bosi wako…...najua nini atakuambia,…hilo lilishapangwa, hata kama kesi hii itakwishamtakavyo, lakini uamuzi ulishapitishwa kuhusu mimi na huyo bosi, bosi wako…., nawajua sana hawa watu,  lakini mjue nyie sio mungu,..’nikasema

‘Unajua usipokuwa muwazi kwangu mimi sitaweza kufanya kazi yangu vyema, niambie tatizo lipo wapi ili nione jinsi ya kusaidia, na huyo sio bosi wangu, ni bosi wako….’akasema huku kakunja sura, halafu aaktabasamu.

‘Usiwe na wasiwasi bwana …unaona jinsi ninavyopambana kwenye ulingo wa kisheria, …ina maana ukinielewa vyema hutashindwa hii kesi, lakini kwanza nijue undani wa tatizo lenyewe, ili nijue vipi tutalitatua, kwani kuna nini kimetokea mpaka usiniamini mimi….?’akasema

‘Sio kwamba sikuamini wewe, lakini je hawo waliokutuma wana lengo gani kwangu, …huenda hujui au unajua lakini kwasababu ya maslahi au kwasababu ya wito wa kazi yako utajifanya hujui…kwasababu ya mslahi au misingi ya kazi yako….sawa utajifanya hujui, lakini yote ni kwasababu ya mslahi, tusidanganyene, nia hapo mnataka mimi niseme uwongo,kwa manufaa yenu, au sio….?’ nikauliza

‘Useme uwongo upo, mbona sikuelewi, …hakuna uwongo  hapa, sisi tunafuata sheria, wapi tumekwenda kinyume cha sheria ili uitwe uwongo, mimi ninaangali sheria inasema nini kuhusiana na hilo tatizo, kwa jili ya kukutetea….je kuna sehenu umekiuka sheria, kama umekiuka, tutaangalai kwa vipi,na utetewe vipi….lakini kwa kesi yako hujavunja sheria, ila watu wanataka ukubali kuwa umevunje sheria ili kufanikisha malengo yao, ndivyo ilivyo sasa, sasa sisi tunaujua sheria lazima tuwatetee nyie msioijua...natumai umenielewa…’akasema huku akiangalia saa yake.

‘Sasa huko mumeongea nini na hakimu….?’ Nikamuuliza na yeye akacheka na kuniangalia kwa muda akasema;

‘Hayo ni mambo ya kisheria hayakuhusu….ila la muhimu ni kuwa hakimu anataka kesi hii iishe haraka maana inavuta hadhira , kila siku watu wanaongezeka, na mtokeao yake inaweza ikageuzwa na kuwa mambo ya kisiasa,na inaweza ialeta vurugu ….kwahiyo anataka haki itendeke,kesi hii imalizike haraka iwezekanavyo….’akasema wakili.

‘Haki itatendeka kweli….je itatendeka kweli,  wakati nyie mnataka kuufuta ushahidi na ukweli upotoshwe…’nikasema

‘Ufutwe kwa vipi….kwa vipi tuupotoshe….mmh,..?’akauliza na mara simu yake ikalia, akaniangalia kwa muda kabla hajaipokea, halafu akasogea pembeni, akageuka tena kuniangalia na safari hii uso wake ulibadilika,sio ule wa tabasamu tena, alionyesha makunyazi usoni,sikuelewa kwanini na akasogea mbali na kuipokea hiyo simu.

Kwa muda ule sikujali kwasababu nilishajua ni nani kampigia na ataambiwa nini,tatizo ni hapo akaiulizwa je simu yake yakwanza aliipokea nani….sikujali…

‘Hapa nikuwaza jinsi gani ya kujiokoa na janga hilo…sasa inabidi nianza mapigano ya nafsi yangu,…’nikasema kwa sauti, huku nikakumbuka yale maneno ya mwanadada, ambaye ni wakili, licha ya kuwa walikuwa wakibadilishana na wenzake mara kwa mara ndani ya mahaka ,lakini yeye alisimamia katika kutetea haki za akina mama, yeye alipenda sana huo usemi kuwa `nipambane kiume’

‘Inabidi sasa nipambane kiume.’ Nikasema huku nikinyosha


‘Kwa uzoefu wangu, wewe ndiwe umeweza kuvumilia muda mrefu hadi hatua hii, kesi nyingi zilizopita zilikuwa hazichukui muda mrefu hivi, …’nikakumbuka meneno ya wakili wangu huyu anayenitetea

‘Kwanini zilikuwa hazichukui muda mrefu hivi, kwani zilihusu mauaji….?’ Nikadadisi.

‘Zilikuwepo za mauaji,na  nyingine lakini chanzo ni mambo haya haya, na cha jabu kesi za mauaji ndizo zilikuwa hazikuchukui muda mrefu, maana mshitakiwa anaamua kuchukua sheria mikononi mwake, anajihukumu mwenyewe kabla hajahukumiwa,…sijui kwanini hawa watu hawajiamini,nashukuru wewe unajiamini kidogo…’akaniambia kwani ilikuwa kipindi cha mwanzoni wakati najibu anavyotaka yeye.

‘Wanachukua sheria mikononi mwao kwa vipi, wakati wapo mahabusu ,ina maana wanajiua….?’ Nikauliza.

‘Nawashangaa sana, unakwedna nao vizuri, mwanzoni wanafuata unavyowaelekeza,  lakini mwishoni wanajikanyaga, halafu wanaona kujiua ndio njia ya mkato, hawajui kuwa huo ni uoga. Huweze ukajiua ukiwa vitani, pambana…., hata kama ni kufa ufe ukiwa unapambana, …huenda ungelishinda, na hii kesi ni yakushinda tu….’ Akasema akijiamini, hakujua nini kilichokuwepo kichwani mwangu.

Wakati nawaza haya Yule wakili akarudi, na alionyesha ule uso wake wa tabasamu, lakini sio kama ilivyokuwa mwanzoni,…kwa muda mfupi niliokuwa naye nimejifunza mengi kuhusu huyu mtu, sura yake inaweza kubadilika, lakini anajitahidi sana akikuangalia machoni,awe anatabasamu,…nahapo huwezi kujua ana lengo gani, …. akaniangalia kwanza kwa muda bila kusema kitu, akasogea  na kunishika begani akasema;

‘Watu wa zamani wanasema; mtoto akililia wembe mpe…..sijui nini kilichokusibu, na lengo langu lilikuwa jema kabisa, nia yangu ilikuwa kukusaidia, maana najua wewe ni mhanga wa mambo ambayo huna makosa nayo, inaonyesha kabisa wewe ni mtu mwema sana, lakini labda kwasababu ya hii shida ya kimaisha,umejikuta ukiingia katika msukosuko huu, kama wengine…. pole sana…’akawa kama ananiminya begani.

‘Pole ya nini…muheshimiwa…?’ nikauliza.

‘Kwasababu mimi sina la kufanya tena, tusubiri maana waanshauriana huko ndani,haijajulikana kama kesi itaendelea leo, …..kama msimamo wako ndio huo, mimi nitajitoa, labda iwe vinginevyo,kwasababu mimi nakwenda kwa mujibu ya matakwa yenu, kama bosi wako kasema kama hukubali kuwa pamoja nami , basi….sasa mimi nifanyaje…’akaniangalia machoni.

‘Lakini mimi sijakataa uwe wakili wangu…nimekuambia kuwa nimekataa?’ nikamuuliza.

‘Unaweza ukakataa kwa kauli au kwa vitendo, wewe umekataa kwa vitendo, na vitendo ndivyo nguzo ya hii kesi, nakuambia pita huku wewe unapita unapotaka wewe, nitafanyaje hapo, hebu chukulia wewe upo nafasi yangu ungelifanyaje?’ akaniuliza.

‘Ningelifuata misingi na masharti ya kazi yangu, …kusimamia sheria katika misingi ya haki….’nikasema.

‘Tutarejea mjadala ule ule na hautaleta tija…ila ninachokuambia ni kuwa tupo pamoja…..hata kama bosi wako anasema nikuache, lakini mimi nitakuwa na wewe….nafikiri muda umefika,muda ambao hata mimi nilikuwa nausubiri….’akasema na kunishika bega.

‘Mnaanza kugeukana nini…?’ nikasema kimoyomoyo.

‘Kazi hii ya uwakili, unaweza ukaifanya kwa malengo  mema kabisa, na kama kazi nyingine lengo ni kupata pesa kwasababu ni ajira….na nia na makusudio yetu ni kimlinda mteja wako, ili ashinde kesi yake,….ndio lengo letu kubwa ndio maana unaitwa wakili mtetezi…huwezi ukachukuliwa kama wakili mtetezi halafu uwe kinyume chake…nafikiri unanipata hapo…?’akasema huyo wakili.

‘Ina maana hata ukiona kuwa mteja wako ni mkosaji, yupo hatiani, utamteta tu, hata bila ya kumpa ushauri, utakubali tu hiyo kesi kwasababu ya maslahi…?’ nikamuuliza.
‘Kazi yetu kubwa unapopewa kazi ni kuhakikisha unaijua ile kesi,na kweli kesi nyingi za huyu mama zinautata, na mimi kama wakili wake,namshauri inavyowezekana,lakini lengo letu lipo pale pale, kumtetea na kumlinda mteja wako ….lakini..!’akatulia kwanza na kuangalia pembeni.

‘Lakini vipi muheshimiwa….ujue wewe bado ni wakili wangu, unatakiwa unitete kama inavyotakiwa, kama unaona nipo kwenye hatia nishauri,kama nipo kwenye kudhulumiwa naomba unisimamie na mungu atakulipa…’nikajikuta nikisema.

Yule wakili aligeuka na kuniangalia, akasogea karibu yangu na kunishika tena begani, hakusema kitu, akageuka na kuanza kuondoka, nikabaki nimeduwaa, nikijua ni yale yale….Lakini alipofika hatua mbili mbele akageuka na kusema;

‘Nikumabie kitu, usikate tamaa, upi sahihi, na tupo pamoja,ila kama nilivyokuambia mimi ni wakili mtetezi,…siwezi kugeuka kuwa kinyume chake,….pigana kiume, tukijaliwa tutaonana…na mungu atakulinda…’akasema na kuondoka.

Nilibakia peke yangu nikiwaza hili na lile na mara askari akaja na kusema mawakili wameshakubaliana kuwa kesi hiyo iahirishwe mpaka kesho kutwa, na wakili wangu kasema kuwa kapata dharura, hakuweza kuja kuniaga,ila yupo pamoja na mimi…

‘Sasa tafadhali naomba nionane na muheshimiwa hakimu..tafadhali nipo chini ya miguu yako…nakuomba sana…kwani ikipita leo,..sijui itakuwaje…nakuomba tafadahali….’nikapiga hata magoti.

‘Wewe huruhusiwi kuonana na hakimu….haitawezekana, ni wakili wako tu…na kwasababu maalumu…’akasema.

‘Hili halihitaji kusubiri, na kama litasubiri,kitakachotokea kitakuwa juu yako, nakuomba tafadhali, wewe timiza wajibu wako kafikishe huo ujumbe….ni muhimu sana…’nikasema huku nimepiga magoti, na wakati huohuo nikaona wakili yule mwanadada akitoka,na wasaidizi wake, akaniona nikiwa nimepiga magoti…

Je nini kitatokea, tuzidi kuwa pamoja, na hapa nifupisha sana kutokana na muda na hali halisi....

 WAZO LA LEO: Kusema uwongo imekuwa ni jambo la kawaida kwetu na hata kama mtu anajua kuwa anachose ni uwongo, ataahidi tu, ili watu wamuone, na haja yake itimie…na hata kutatafuta njia za kuhalalisha uwongo wake, tujue kabisa hizo ni dalili za unafiki,….
Jamani,jamani tukumbuke kuwa ahadi ni deni.


Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Kwanza nikupe pele kwa kazi kubwa unayoifanya ambayo sijui kama kuna malipo yoyote kipesa unayopata zaidi ya kukupongeza.
Sisi hatuna cha kukulipa ila nikukuombea kwa mungu akuzidishie kipato chako.