Ilikuwa muda wa saa sita za usiku, eneo lote lilikuwa
kimiya, kilichokuwa kikisikia na sauti za mingurumo ya wafungwa, mimi sikuweza
kupata usingizi kabisa, kama nilivyokuambia nilitakiwa nipambane kiume,
nilikuwa nasubiri huyo mtoa roho aje tukutane naye…lakini kulikuwa kama siku
nyingine nami nikakata tamaa na kujua kuwa huenda hakimu hakufikishiwa ujumbe
wangu…..nikajibanza pale nilipokuwa nimejificha.
Nilikumbuka jinsi nilivyohangaika ili nimuone hakimu, lakini
haikuwezekana, na matokea yake nikakutana na Yule wakilianayetetea akina mama,
na hata yeye alikuwa kama haniamini tena, nikakumbuka jinsi alivyokuja wakati
nikiwa nimepiga magoti mbele ya Yule askari.
‘Vipi huyu jamaa ana matatizo gani mbona anapiga magoti kama
anatubu dhambii zake…?’ .
‘Eti anataka kuonana na hakimu…?’ akasema Yule askari kwa kebehi.
‘Unataka kuonana na hakimu,…? Mbona muda mwingi ulikuwa naye
ndani ya mahakama, una lipi jipya la kuonana naye, na wakili wako yupo wapi
maana yeye ndiye njia yako ya kufika kwa hakimu…’akasema huyo wakili.
‘Ni muhimu nionane naye, na hili nataka niongee naye
mwenyewe, sio kwa kupitia kwa wakili, …maana hakuna ninayemuamini kwa sasa….’nikasema.
‘Kuna jambo gani unataka kumwambia hakimu, ….na kwanini
usimwamini wakili wako?’ Akauliza na baadaye akamgeukia Yule askari na
kumwambia ampe nafasi aongee na mimi. Yule askari akasema muda wa kuondoka
umefika hakuna nafasii tena ya maongezi…aongee harakaharaka..’akasema afande.
‘Unasikia anavyosema afande, hata wao sio kosa lao wanafuta
sheria,kama kuna kitu muhimu wewe niambie harakaharaka, nitajitahidi nifikishe
huo ujumbe kwa hakimu…kuna jambo gani sema haraka gari linawasubiri
nje…;akasema huyo mwanadada.
‘Ni kuhusu usalama wangu, ….sizani kama nitaweza kufika kesho,
sihitajiki tena kusimama mahakamani , sina amani tena, nimeonekana msaliti…nimesikia
kwa amsikio yangu wakili akipigiwa simu….’Nikasema.
‘Tulishakuambia hilo hukutuamini, sasa unaona….lakini usiwe
na wasiwasi, hayo tunayajua, na tunayafuatilia kwakaribu sana…na kuhusu huko
mahabusu,tutaangalia jinsii usalama wako utakavyokuwa, lakini wewe sio mtu
wetu, tunaogopa kukuingilia….’ Akasema na halafu aakmgeukia Yule afande;
‘Afande hili ni muhimu sana, kama hutaliweza tunaomba
utuitie muhusika, huyu mtu ni muhimu sana katika kesi yetu na huko gerezani
anahitajika awekewe ulinzi mkubwa…’akasema huyo mwanadada.
‘Mbona huko kuna ulinzi wa kutosha…hakuna shida kabisa, hata
mimi naweza kufuatilia hilo kuhakikisha kuwa hakuna matatizo,mbona ndio kazi
zetu….’akasema huyo afande.
‘Kama unatuhakikishia tunaomba utuhakikishie
kimaandishi…maana kama litatokea lolote wewe utakuja kujibu mahakamni…’akasema
huyo mwanadada.
‘Kama ni hivyo ngoja nikaonane na mkuu wa huu
msafara….’akasema Yule afande na baadaye akaja na mkuu msafara,wakaongea na huyo
mwanadada kwa siri pembeni, sikujua wameongea nini, na baadaye tukaondoka hapo
mahakamani.
Tulipofika gerezani, tukaendeela na shughuli zetu kama
kawaida na muda wa kulala ulipofika, kila mmoja alikwenda mahali pake, lakini
nilipofika chumba ambacho nilikuwa nalala…nikashikwa na butwaa, kwani kulikuwa
na mtu mpya…labda ni mfungwa mgeni..labda,labda..zikawa nyingi, lakini sikuwa
na amani.Nikaingia ndani….
Chumba hicho tulikuwa
wawili nilipofika mara ya kwanza,..lakini siku mbili hivi za karibuni ,
nilikuwa nalala peke yangu kwani mwenzangu ambaye tulikuwa naye hapo
alihamishwa baada ya kusikilizwa kesi yake na kuonekana ana hatia. Sasa leo
nafika hapo namkuta mtu mgeni,na huyo mtu akawa kalala sehemu yangu. Kwasaabbu
nilishakuwa mwenyeji nikauliza kwa ukali.
‘Mbona umekuja kulala mahali pangu….?’ Nikauliza.
‘Wewe una kwako hapa, hebu ishia huko nisije nikakumaliza…kila
mahali kuna mtu,mimi nitakaa wapi…kwanza utoke humu ndani, humu nalala peke
yangu, sitaki usumbufu, au nikuonyeshe kuwa mimi ni nani, huko nje wananijua,
hata hivyo sizani kama nitamaliza siku mbili hapa….’akasema huyo jamaa na yeye
kwa ukali, na mimi kwa kuogopa purukushani, na kwa vile nilikuwa bado na
wasiwasi wa kuuliwa usiku, nikatafuta sehemu nyingine, …nikjabanza kwa shida
shida, nikiwaza jinsi ya kupata sehemu nyingine kamaile.
Kwa hali ilivyo, usingizi haukuja kabisa, kwani sehemu hiyo
niliyojibanza,sio sehemu rasmi, na ukakaa kama hakuna chumba maalumu, ni hapo
hapo kwenye hicho chumba, lakini ni kwa nje kando kidogo, na sio sehemu nzuri,
lakini nikaona nijibanze hapo hadi kesho, na nilipapenda kwasababu watu hawakuoni
wakipita kwa nje, nikajifunika vipande vya godoro,….
Hata hivyo kwa shida shida usingizi ukanijia na mara
nikajikuta nikitembea pembeni mwa ukingo, ni kama njia nyembamba….ipo kama daraja,
lakini ni njia, upande mmoja ni ukingo wenye shimo refu ajabu.
Nilikuwa naangalia kwa kujiiba, maana hata kuangali lile
shimo unaogopa,unaweza ukapatwa na kizunguzungu ukatumbukia, na kwa kujiiba
huko nilijaribu kuangalia urefu wa lile shimo , lakini sikuweza kuona mwisho
wake,lilikuwa ni shimo refu ajabu, na pana sana, ina maana huko mbele
lilipoishia kwa upana huwezi kuona, ilikuwa ndio kama mwisho wa dunia.
Ilivyo nilitakiwa kupita pembezoni hadi mwisho wake, ili
nifike barabara inyokwenda huko ninakotakiwa nifike,na walasijui ni wapi, na
upande mwingie ambao nilikuwa sijauona, kulikuwa mto wenye mamba na kila aina
ya wadudu , ….na ukijsogeza karibu na ukingo wa huo mto, harufu yako ikiwafikia
hawo wadudu , mamba na mijoka wanaweza kukurukia, kwahiyo hutakiwi ukaribie
huko ukingoni,….
‘Huku ni kuzimu nini…..?’nikauliza.
‘Unauliza jibu,…’sauti nyingine ikanijibu, lakini sikumuona
aliyenijibu, huenda alikuwa nyuma yangu,na huwezi kujigeuza, unaweza ukakosea
mguu ukakanyaga kusipofaa ukateleza, kwahiyo wewe unachotakiwa ni kuangali
mbele..
Mara ukasikika upepo,….na kelele zikaanza kusikika kwa
nyuma,ina maana ilikuwa ni vilio, labda ni kwa wale waliokosea wakadondoka, au
walikamatwa na mamba, ….mikoromo ya watu wakikata roho, huwezi kugeuka, wewe
unatakiwa kwenda mbele, na muda tulipangiwa unaanza kuisha….
‘Mkichelewa kiza kikiingia wadudu kama mamba wanatoka mtoni,
mtashindwa kupita…kwani watakuwa wameziba njia wakisubiri mawindo….’tuliposikia
hivyo, tulianza kusukumana, na hapa watu wakaanza kudondoka huku na kule, na
hata aliyekuwa nyuma yangu akawa anhema na kukoroma kwa uwoga, nikamwambia
asinisogelee karibu kwasababu anaweza kunisukuma,lakini hakusikia akawa anakoroma
kama samba…
‘Bwana wee acha
kukoroma, unawaita simba….’nikasema, lakini hakusikia, na ile sauti ya kukoroma
ikazidi hata ikanitisha, nikasema huyu asije akawa ni samba yupo nyuma yangu,
ngoja nimwangalie, nikageuza kichwa, na pale ikawa ni kosa, maana nilipogeuza kichwa,
mguu wanguukakosea njia, na haukukanyaga sehemu inayostahili, nikajikuta
nimekanyaga hewa na niliojaribu kujiweka sawa huyu jamaa anayekoroma
akanisukuma…..
Nilijikuta nikielea hewani,…ina maana nilikuwa nikizama
kwenda huko kuzimu, kwenye shimo lisilolokuwa na mwisho,nikaanza kupiga ukulele….
‘Wewe mbona unasumbua watu…mikelele ya nini..’sauti
ikasikika, kwa muda ule sikujua ni ya nani, haraka haraka nikainuka..ooh, kumbe
ilikuwa ni ndoto…nikakumbuka kuwa nipo mafichoni,nikajibanza vyema,nikitafuta
usungizi tena.
Mara wakaja majamaa wanne, mmojawapo alikuwa mku wa wafungwa
hapo gerezani, akasogea hadi pale alipolala Yule jamaa, ambapo nilitakiwa
nilale mimi, akagonga na rungu lake, kwa
nje kwenye nondo zinazotuzunguka,maana vyumba hivyo vimezungukwa na nondo,
ukitaka kuotoka unafunguliwa na afande, wakamuamusha Yule jamaa na mazungumzo
yao nikayasikia wakiongea
‘Wew Unaitwa chumba cha wageni…’nikasikia sauti ikisema,huku
Yule msemaji akiwa kashika ufunguo, kuonyesha kweli anaweza kuufungua huo
mlango,lakini nikajiuliza usiku kama huu kuna nini hado mtu aitwe chumba cha
wageni. Nikasubiri kusikia zaidi….
‘Chumba cha wageni usiku huu…?’akauliza huyo mfungwa kwa
hasira.
‘Ndio…usiki huu,wewe unaujua usiku hapa ….unasikia afande anakuita….’akasema Yule mkuu wa wafungwa.
‘Mimi huko siendi…’akasema Yule mfungwa.
‘Unaleta ubishi sio…unafikiri bado upo uraiani, hapa ni amri
amri….hujajifunzamisha ya haa muda wote huu, au kwa vile hatukuwahi kuja
kukukaribisha ulivyofikahapa..sasa tutakukaribisha rasmi,…..’akasema huyo mkuu
wa wafungwa, alikuwa pande la jitu, na pembeni yake wapo wasaidizi wake na wao
ni mijitu inatisha, …..
‘Mimi huko siendi na kama ni mgeni mwambieni nitaonana naye
kesho..’akasema Yule mfungwa naye alionekana ana mwili, sio haba, lakini huwezi
kuwalinganisha na hawo jamaa wengine.
‘Sio mgeni ni afande anakuita..hujatusikia au huna masikio,
..ngoja tuingie huko tukuzibue hayo masikioa’akasema huyo jamaa huku akifungua
mlango.
‘Nimesema huko siendi kama ni kuniua niulieni hapahapa…maana
nyie mna lenu jambo…hata hivyo nimeshachoka na maisha, ila ole wenu, nitakwena
na mmojawenu…’akasema huyo jamaa akijiweka tayari.
‘Nani kasema anataka kukua wewe,…unaleta uzushi hapa ndani..’akasema
huyo mkuu wa walinzi.
Mara akaja afande mmoja, akauliza kuna tatizo gani, yule
mfungwa akajitetea kuwa hawo jamaa wanamwambia kuwa kuna mgeni wake chumba cha
wageni,usiku kama huo,na ahwaamini kuwa kweli kuna mgeni, huenda wanataka
kumfanyia kitu kibaya….
‘Tumemwambia unamuita afande,….lakini analeta ubishi..’akasema huyo
mkuu wa wafungwa na Yule afande akawaangalia kwa hasira wale jamaa na baadaye
akamgeukia huyo mfungwa na kumwambia;
‘Ina maana hukusikia ujumbe wangu kuwa ninakuita….?’
Akauliza huyo afande
‘Lakini afande muda kama huu ni wa kulala, mnaniamusha usiku
usuki, kuna nini cha muhimu,….mbona ni kinyume cha sheria,sio kwasababu tupo
hapa ndio mchukue sheria mkononi mwenu,sio wote wenye makosa hapa, wengine
tumeshikwa kimakosa…kuna nini unaniitia muda kama huu?’ akauliza.
‘Hapa unafuta sheria hata kama ni saa ngapi ukiambiwa kuja
unakuja mara moja…hujaja kulala hapa kamaulikuwa unataka kulala ungelilala huko
nyumbani kwako, ….’akasema huyo afande.
‘Sasa mimi huko siendi afande,…fanyeni lolote mnalotaka
kufanya….’akasema huyo mfungwa.
Wale jamaa
waliposikia hivyo, wakamuiingilia humo ndani na kuanza kumbeba juu, juu, na
jamaa hakukubali, kukatokea mapigano,….ilikuwa vurumai, lakini kwa vile wao
walikuwa wengi wakamdhibiti, na ilichukua nusu saa, Yule jamaa akawa chini
sakafuni,na mara wale jamaa wakato mbio,na kukimbia, na Yule afande akasogea
pale alipolala Yule mfungwa na kumgusa kwenye shingo, nafikiri ilikuwa ni
kuhakikisha kuwa kafa au vipi.
Baadaye Yule afande
akaondoka..humo nilipokuwa nikawa natetemeka kwa uwoga, nikazidi kujibanza,
maana kesi ianweza kunigeukia mimi kuwa ndiye niliyeua, lakini mara Yule afande
akarudi na maafande wenzake wakamchukua huyo mfungwa,akionekana kabisa hayupo
hai,….moyoni nikashukuru mungu, nikijua kuuwa huenda lile lengo lilikuwa kwa
ajili yangu sasa sijui ilipangwa, au ni mungu mwenyewe kajalia ikatokea hivyo.
Siku ya pili yake nikashikwa na homa kali sana, ikabidi
nipelekwe hospitalini, huko nikapata mapumziko chini ya ulinzi, hadi jioni
nikajikuta hali ina nafuu, na kuruhusiwa kurudi gerezani, nilipofika huko
gerezani nilijaribu kuuliza wenzangu kama wakili yangu alifika, wakasema
hawajamuona, nami sikujali sana, na kwa vile nina kibali cha kazi ndogo ndogo,
nikawa nimepumzika ndani ya gereza hadi usiku ukaingia.
Sikulala kabisa ile sehemu yangu ya kawaida,nikichelea
kukutana na hawo jamaa waliommaliza mwenzetu, na cha ajabu sikusikia lolote
kuhusu huyo mwenzetu, na hata nilipowauliza wenzangu, hawakutaka hata
kuliongelea, kama vile wanaogopa kuliongelea hilo jambo , kuwa wakiongea na wao
litawakuta. Nami nikaona haina haja ,ni bora nijikalie kimiya nisubiri nini
kitatokea baadaye. Nilitafuta sehemu nyingine na kuifanya ndio mako yangu
mapya, hadi kesho yake asubuhi.
Majina ya wanaokwenda kwenye kesi zao kwa siku hiyo
yakaitwa,lakini cha ajabu sikusikia kabisa jina langu likitajwa,nikashangaa
maana nilikuwa na uhakikakabisakuwa siku hiyo ndiyo siku ya kesi yangu,licha ya
kutokuoenekana kwa wakili wangu,….nikaona hapo kuna jambo,nikasubiri hadi kila
kitu kilipokuwa tayari nikaenda kukutana na mkuu wa msafara.
‘Afande mimi nina uhakika leo ndio siku yangu ya kesi,
lakini jina langu sijalisikia likitajwa…’nikasema.
‘Labda kesi yako imeahirishwa, jina lako nani maana mimi nimekabidhiwa hii
orodha leo asubuhi nilikuw akituo kingine, na mwenzangu ambaye ni mweneyji hapa
kapatwa na dharura, kwahiyo sina uhakika zaidi na mambo ya hapa.
‘Naitwa Mtoto wa Msomali…’nikasema na huyo afande akaangali
majina na alipofika sehemu ya jina langu akakuta limepigiwa msitari mwekundu,
akaniangalia kwamakini, na muda huo huo dereva akawa anapiga hino,kwani
tulikuwa tunachelewa.
‘Mambo ya hapa bwana,…mimi nhukulia juu kwa juu, kuwa
nitakuwa mkuu wa msafara lakini dereva anajiona yeye ndiye mwenye mamlaka,….na
mambo mengine sijakabidhiwa, lakini hakujaharibika kitu tutatumia uzoefu,…haya kaingie
kwenye gari twende, tutajua hukohuko….’akasema
na mimi nikaingia kwenye gari.Na Yule mkuu wa msafara akaomsogelea mwenzake na kuchukua nyaraka za kumbukumbu akawa
anaziangalia na baadaye akawa anateta na mwenzake, na wakawa wanaonyeshana lile
daftari na nyaraka lenye majina na mara wakageuka kuniangalia.
Baadaye kukawa na mambo mengine mengi ya kufuatilia, na kwa
vile Yule afabde alikabidhiwa mambo mengi juu kwa juu, hakuwa anayajua ilibidi
kila mara kwenda kuuliza na kufuatilia na baadaye tukaondoka kwenda mahakamani.
Tulipofika mahakamani Yule mkuu wa msafara akanichukua hadi chumba maalumu,
wanapowekwa watu ulinzi mkali, akasema;
‘Wewe uje huku,maana mambo yako yana utata, ni kweli kuwa
leo ni siku yako ya kesi,lakini maelezo yaliyopo hapa yanaonekana kunichanganya, cha ajabu inaonekana kuwa wewe haupo hai…..sasa
sijui nini kinaendelea,….itabidi nifuatilie swala lako kwa karibu,na kwahiyo utakuwa kwenye ulinzi mkali mpaka
nionane na wahausika….’akasema na kuniangalia kwa makini,akachukua jaridalenye
picha yangu,akalitaizama na karatsi iliyoweka hapo akaisoma na kuniangalia
machoni. Akasema.
‘Sawa wewe utakaa hapa na usije ukajidanganya kwa lolote
lile, upo kwenye ulinzi mkali,….tusubiri maelezo zaidi…wewe kaa hapa….nitakuja
baadaye .’akasema huku akiondoka
kufuatlia maswala mwengine.
Siku ikaanza na kesi yetu ilikuwa ndiyo ya kwanza,na watu
walijazana kama kawaida, ingawaje kilechumba kilikuwa sehemu ambayo huwezi
kuona vyema nje, hata hivyo nilijitahidi hadi nikapata sehemu yenye upenyo na
kuweza kuona nje.Pale nilipokuwa nimewekwa ni sehemu ambayo mawakili hukutana
kwa dharuara labda kwa kujadli jambo au kuhifadhiwa wafungwa hatari.
‘Huyu ni nani….mbona hakuna orodha ya wafungwa hatari…?’ Akauliza
mwendesha mashitaka, na wakili wa mshitaka akaniangali a kwa makini,halafu
akageuka upande wa pili,…akiwa kashikwa na mshangao, na wakati huo Yule mwanadada
wakili alikuwa akiingia ndio anaingia hapo kwenye chumba, ilionekana walikuwa
na kikao chao maalumu,…akaingia moja kwa moja pale tulipokuwa, akasalaimiana na
wenzake, na kusema;
‘Unajua hapa nilipo nimechanagnyikiwa, na bado nasikitika
sana moyoni, na najuata sana, maana siku ile ya mwisho wakesi hii,Yule mshitakwa
namba moja,aliniambai kuwa ana wasiwasi na uaslaam wake kuwa watamua hawo
wenzake, na mbinu hizo zitafanyika huko gerezani, ….sikumwamini sana, kama mjuavyo
kuwa ni mtu niliyemtegemea mwanzoni , lakini alikuja kunigeuka….sasa’ Akasema na
akaingiwa na wasi wasi na mimi, maana alichotaka kuongea pale huenda
hakikutakiwa kusikiwa na mtu mwingine, kwanza, aliangalia saa yake.
‘Kwahiyo kama ulivyonielezea jana, tutaendelea kama kawaida,
bila hata ya yeye….si kila kitu kipo sawasawa,
?’akauliza mkuu wa mashitaka.
‘Ndio kwasababu ushahidi wa kutosha tunao,ila Yule mwanamama
ambaye ndiye kiongozi,wa haya yote, na kuwatumia watu wengine, katoweka kinamna,….
tangu jana haonekani alipo,licha ya kupokea amri ya mahaka kuwa awepo leo hapa mahakamani
kama shahidi…hatukuweza kumkamata moja kwamoja, kutokana na kesi yenyewe
ilivyo,…lakini kwa mtindo huu inabidi atafutwe na akamatwe,….’akasema Yule mwanadada.
‘Kibali kila kitu si kipo tayari…sasa mnasema tena
haonekani,…jamani,muwe makini na hili, mimi sio kazi yangu kufuatilia kila
kitu, mimi nataka mkifika hapa kila kitu kipo tayari,tunaweka mambo sawasawa,…sasa
tuanza kuongea maana muda unakaribia….’akasema mkuu wa mashitaka.
‘Lakini jana tulikutafuta sana, ukawa na …’akasema halafu
mara akageuza shingo kuangalia uapnde wangu, kwani muda wote huo alikwua
hajaniangalia, akaniona…..’alaivyoshituka karibu adondoshe lile jarida
alilokuwa kalishikilia mkononi, akaniangalia kwa makini halafu akanisogelea na
kuniangalia usoni, akafungua jarida
alilokuwa kalishikilia na kuanglai kitu,halafu akawageukia wenzake, na baadaye
akanigeukia mimi wenzake wakafanya hivyo hivyo…
‘Wewe ..mbona, …..sielewi, usiniambie kuwa,…mpo
mapacha,maana dunia hii ina mengi…’akasema Yule mwanadada.
‘Kwani kuna nini…maana toka huko gerezani kuna utata,jina
langu halijaitwa, na kwenye orodha jinalangu limekatwa kwa wino mwekundu,na
mkuu wa msafara naye hajui zaidi…sasa kuna ninikinanendelea…?’ nikauliza.
‘Ahsante sana mungu, maana nilishaanza kujijutia, siku ile
nilimpakazi yuleafande kuwa ahakikishe kuwa upo salama, na siku hiyo hiyoi huyo
afande akapatwa na dharura na kwendakwao,….nilikuja kupata taarifa siku ya pile
yake wakati tukio lilishatokea,…’akasema huyo mwanadada.
‘Tukio gani…?’ akauliza mkuu wa mashitaka.
‘Mkuu huyu ndiye mshitakwa mkuu, ambaye tulipata taarifa
kuwa kajiua…kumbe haikuwa hivyo, nafikiri kuna makosa yalifanyika huko
gerezani,na wahusiak wa huo mpango wanajua kuwa imekuwa hivyo, ….inabdi
uchunguzi wa haraka ufanyike,na Yule mlinzi wa siku ile, akamatwe akahojiwe….’akasemahuyo
wakili.
‘Hiyo siyo kazi yako,ongea kuhusu kesi ya leo, ..’akasema
mkuu wa amshitaka.
‘Kesi ya leo, iendelee kama kawaida, na mengine tukatete
ndani..’akasema na wakachukuana huko ndani mimi nikabakia palenikiwa an ulinzi
mkali, huku moyoni nikijiuliza nini itakuwa hatima yangu, ….
WAZO LA LEO TOKA KWA MDAU: Hakuna jambo litamkuta mwanadamu isipokuwa limepangwa na Mwenyezimungu muweza wa kila jambo. Hivyo Utashi wa binadamu hauna nafasi, mbele ya makadrio ya mweneyzimungu. Kwani yeye kila alipngalo liwe huwa.
NB Shukurani kwako mdau,na wewe kama una wazo lako unataka liwe hewani litoe ili kunogeza kisa chetu, na kama inawezekana liendane na kisa cha siku hiyo.
Ni mimi:
emu-three
6 comments :
m3 ya leo kali inasikitisha lakini alipangalo mungu binadamu haliwezi na pahala popote ikisimama haki basi ushindi upo
huyu kaka yamemkuta nampa pole
nawe m3 unajitahidi kuwa na sisi
siku njema dear
Mmmmhh kazi nzuri ndugu yangu,pongezi tele,daima mbele.Pamoja sana sana ndugu wa mimi!!!!!
Ngoja mie niweke neno la leo, maana umetuacha juu ya mawe leo, yaani nilikuwa natamani kuendelea kusoma zaidi na zaidi mara ghafla vuum kimya.
Neno la Leo
Hakuna jambo litamkuta mwanadamu isipokuwa limepangwa na Mwenyezimungu Subhana wa Taala. Hivyo binadamu wanajisumbua tu sijui nimfanye nini nani sijui nimtoe roho nani hakuna anayeweza kuyafanya haya kama Mwenyezimungu hakupanga.
Nashukuru Samira tupo pamoja
Ndugu wa mimi tupo pamoja
Wazo la hekima hilo nitaliweka, shukurani sana
Post a Comment