Nilikuwa hata sijui nifanye nini ili niweze kuishi, maana
tangu niachiwe huru, nimekuwa mtu wa kuzunguka huku na kule kuwatafuta marafiki
wa zamani lakini sikuwahi kumpata mtu ninayemfahamu na wa kuaminika, na hata
Yule anayenifahamu kidogo, akaniona ananikwepa na hata kunikimbia, ….sijui ni kwanini.
Basi nikaona nihamie maeneo ambayo nitaweza kuishi, huku
nikifanya bishara ya kuokota chupa na kuuza,ili angalau niweze kuishi,na siku
nyingine nakosa pesakabisa na kugeuka kuwa omba omba, sina mbele wala nyuma,na
hapo nikakumbuka na kujijutia ile hundi niliyoahidiwa, ambayo hata hivyo nisingeliweza
kuipata tena, kwa jinsi mambo yalivyokuwa. Walishaniona mimi ni mbabaishaji,….
Siku hiyo nilikuwa na
mawazo sana, nikawa nakoswa koswa na magari,…na mwishowe nikaona nisije
nikaambulia kilema, ni aheri ningeligingwa nakufa,lakini naweza kuambulia
ukilema, na hali niliyo nayo nitaozea Mumhimbili, nikaona ni bora niingie
kwenye jengo moja, ambalo tulizoea kuliita kijiweni, siku hizo labla sijawekwa
ndani.Humo kweneye hilo jengo tulizoea kukutana baada ya kupigika kwenye
vibarua, …ukiwa ni vijisenti vyako kidogo,aah, utapata supu ya ngozi, ukoko,na
vyakula vya bei ndogokutoka kwa mama Ntilie, ambao wanauza kwa kujiiba
wakiwakwepa watoto wa mjini, au wengine huwaita `cite’ au watoto wa mkuu
wamkoa. Ukiingia hapo unachojali ni kujaza tumbo hujali usafi au ubora wa
chakula.
‘Ohh, mshikaji, upo, ….’jamaa mmoja akanisalimia akiwa
anaharakisha kuingia ndani, utafikiria anakimbilia kuingia kwenye daladala,
lakini nilijua kabisa ni njaa, inayomkimbiza, nami wala sikumjibu, nikijisogeza
malngoni,….palishaanza kubadilika , naona usafi umeboreshwa,….nikashangaa, ina
maana hiyomiezi niliyokuwa nasota jela, kuna maendeleo kidogo.
Nilikuwa nayaangali haya wakati naingia mlangoni, huku
nikiangaza angaza wapi nikajibanze, natembea huku macho yangu yako huku na
kule, na wakati natemba eneo lamlango,
kwa bahati mbaya nikapigana kikumbo na mwanamama mmoja,aliyekuwa akitoka nje.
Niligeuka kumwangalia huku nikitafuta lugha ya kuongea,maana humu ndani
hakunalugha safi, kila neon linamatusi ndani yake, watu humo utazani
wamechanganyikiwa, au hawana adabu.
Yule mwanamama, au mwanadada, alikuwa na nywele ndefu ajabu,nafikiri ni za bandia,
maana zilikuwa ndefu kiasi cha kumfunika
sehemu kubwa ya kichwa hadi mebagi, sikashuka hadi nyuma mgongoni, na
usoni zilikuwa kama mtu kajifunika khanga ya nywele, na kuachia sehemu ndogo tu
ya macho.
‘Wewe huoni nini….unatembe ahuku nanihii yako mbele kama …..’akasema
na lugha ile ninayoijua ikafuata …..akainama kuchukua mkoba wake uliodondoka
chini, nami wakati huo huo nilikuwa nimeinama kumsaidia kuukota, akauwahi kabla
yangu,na kama vile anaogopa kuwa nitamuibia akaushikilia barabara mkononi. Na
kunifyoza…..sikujali ndivyo palivyo hapo, kama unahasira utaumia mwenyewe bure
,maana humo hakuna kupigana, ukipigana unamwagiwa maji au matakataka…olewako
ujifanye mwamba….matusi yote yatakuangukiwa wewe…
‘Saamhani dada yangu, ni njaa tu inatufanya hata tusione
mbele,…ukiniazima elifu mbili tu nitashukuru sana…kwanini nanhii….’nikasema
namimi nikaporosha neon linalolingana na humo ndani, ambalo nisigeliweza
kulitamka sehemu nyingine zaidi ya humo ndani....
‘Elifu mbili kwa kazi gani uliofanya…ukiwa an nguo zako
hivyo hivyo…. ,wewe unafikiri pesa ni za kuokota tu hivihivi,…. dume zima huna
hata haya, kuombaomba pesa…halafu uanomba mwanamke pesa, kawaombe wanaume
wenzako wakuonyeshe mji….’akasema na likafuata tusi la nguoni, na mimi sikujali
nikacheka, maana ndio lugha za hapo.
‘Na wewe hutekenywi au shemeji kakuchoka, hujui
mapenzi….nipe hiyo elifu mbili, nikaongeze …..’nikatamka tusi na Yule mwanadada
akasema kwa lugha ile ile ya mle ndani, lugha ta matusi...
‘Haya chukua hizi hapa usije ukanipa nuksi ya bure maana
wewe nina mashaka na wewe, sizani kama….’akasemanalikafuata tusi la nguvu,na
mimi nikacheka na kuipokea hiyo pesa huku nikashangaa nikikabidhiwa pesa ambayo
sikutegemea,nikaipokea huku siamini macho yangu, nikijua atadai chenji yake, na
hapo tukakutanasha macho yetu na Yule mwanamama…akaurudisha mkono wake haraka, utafikiri
alishika kaa la moto, ….lakini kwa muda huo nilishaichukua ile noti ya shilingi
elifu tano…..
Nilishikwa na mshangao,maana macho yetu yalipokuatana na yule
mwana mama ilikuwa kama kaona kitu cha
kumshitua, kwanza aliniangalia mara moja, halafu ikawa kama vile kuna kitu
kimepanua macho yake , akayakodoa kwa usoni akaonyesha wazi kuwa anaogopa,kama
vile mtu aliyeona kitu cha kutisha,halafau akarudi kinyume nyumehuku akiwa
kakodoa macho yam domo,kama vile anataka kupiga yowe,lakini sauti haitoki, na
mara akageuka nyuma na kuangalia mlango upo wapi,mbio akatoka akikimbia…
‘Ahsante dada yangu…naku….oh, vipi…’nikasema, na kushikwa na
butwaa,na vile vitendo, name nikawa natoa macho kwa mshangao, nikimwangalia
huku sijui kimemsibu kitu gani,yule mwanamama, siwezi kumuita mwanadada, labda
nimuite mwanamama,ingawaje mwili wake kauweka kiafya, hajajiachia kiasi cha
kuonekana mwanamama inaonekana ni mtu wa mazoezi, au ni mtu anayeujua mwili
wake vyema, na kuutunza ipasavyo.
‘Oooooooh…..’ndiyo sauti aliyota huku akiishia mlangoni.
Cha ajabu hata ile pochi yake akaiodondosha tena, kwa jisni
alivyoshituka, nami nikaikota haraka na kushikilia mkononi, huku nikiwa namfuatilia
kwa nyuma,….ulikuwa nimikoba hii ya akina mama, wanayopenda kutembea nayo, lakini
ilionekana ni ya bei mbaya, haiendani kabisa na sehemu kama hiyo, nikajiuliza
moyoni, kuwa huyu mwanamama, na huu mkoba mbona haviendani,ukiangalia na sehemu
yenyewe, au kauiba na alikuja humu kuwakoga wenzake.
‘Wewe dada umedondosha mkoba wako….’nikawa namkimbilia
nikimpigia ukelele, lakini ilikuwa kama ndio namfukuza,akawa anakimbia huku
anaangalia nyuma, na kila akiniona namfuatilia ndio naye anaongeza mbio, ikafikia
mahali akawa anakimbia kabisa kama mtu aliyechanganyikiwa na mimi
nikasema,hapana, … dada mwenye huruma kama huyu, hastahili apoteze mkoba wake,
na humo ndani ilionekana kuna simu na vitu vyake vingine….nikamfuatilia huku
nikimuita kwa sauti kuwa asimama ili achukue mkoba wake…hakusimama,….
Alipofika upande mwingine wa bara bara,akaona
bajaji,akaisimamisha na kuondoka nayo,nami nikjaitahidi kumuita kuwa kadondosha
mkoba wake,lakini hata hakujali , akaondoka na ile bajaji, nikabakia nimeduwaa,
nakujiuliza ina maana haunisikia,na kwanini anakimbia, ina maana ananikimbia
mimi,na kwanini anikimbie mimi,…..nikasimama kwa muda nikiwaza, na mara ikaja
bajaji na kusimama mbele yangu…..
Sijui kwanini nilifanya hivyo, kwani pale palenikaingia
ndani ya ile bajaji, nikamwambia mwenye bajaji anisaidie kuifukuzia ile bajaji
iliyoondoka,…kwani Yule abiria mle ndani nina mzigo wake, ..hapo moyoni nikijua
sitalipa pesa nyingi zaidi ya ile niliyopewa,
na hata kama nikilipa pesa nyingi, huyo mwanamama, anaoenekana ni mtu
mwema, ataniongeza chochote, kwa wema niliomfanyia,….basi Yule jamaa akakubali
tukaifutilia hiyo bajaji mpaka tukafika maeneo ya nyumba za wakubwa……wenye
nazo….
Ile bajaji aliyokuwa nayo Yule mwanamama, ikasimama na Yule
mama akatoka mbio, nakuingia ndani ya nyumba tuliyokuwa tumesimama mbele yake.
Kwani na sisi tulikuwa tumeshafika na kusimama karibu na hiyo bajaji,….nafikiri
Yule mwanamama, hakujua kuwa nimemfuatilia nyuma na hiyo bajaji ,kwani nikipindi
namlipa huyo mwenye bajaji pesa yake ndipo Yule mwanamama aliyeingia ndani ya
lile jengo akawa anatoka nje, akiwa na pesa mkononi,akamlipa Yule mwenye bajaji pesa yake,na mimi nikawa namsogelea,….
Akageuka kuondoka akiwa na haraka na kukimbilia ndani , na
mara akaniona…alipanua mdomo na kutaka kupiga yowe, na alichofanya ni kusema;
`mungu huyu hapa tena….ooh’....
Alikurupuka na kukimbilia ndani haraka,na mimi nikasema
lazima nikamtoe hofu kuwa mimi sio mtu mbaya,nikaelekea kule kwenye mlango wa
hilo jengo. Lilikuwa ni jengola bei mbaya, mageti yenye alama za ulinzi na
maneno ya kutisha kuwa kuna ulinzi mkali,mimi sikujali, nikalifikia lile geti
na kugonga mlangoni....
‘Wewe ni nani, na unataka nini….?’ Akauliza mlinzi huku
akiwa kafungua nusu upenyo wa mlango.
‘Mimi nina taka kumuona huyu mwanamama aliyeingia hapa sasa
hivi….’nikasema
‘Hapa haparuhusiwi mtu yoyote kuingia,na huyo mwanamama
uliyemuona hana mamlaka ya kuruhusu mtu kuingia hapa,….unasikia ….tunakuomba
uondoke haraka, kabla hatujakushughulikia,unaijua jela wewe,utaenda kuozea huko
jela sasa hivi…ondoka mara moja eneo hili….’akasema huyo mlinzi.
‘Nilikuwa na mko…kibegi,…..’kabla sijamaliza mlango
ukafungwa usoni mwangu na sauti ikasema;
‘Sitaki nikuone hapo nje,….nenda zako, hatuhitaji chochote
kutoka kwako…..’akasema na mimi nikaona haina haja, nikageuka na kuondoka
zangu,huku nikiwaza hilo tukio , maana huyo mwanamama, alionekana kabisa
ananiogopa mimi,hasa nilipomuona kwa mra ya pili, mwanzoni sikuwa na uhakika
huo, lakini safari hii ya pili, nikajua mara moja kuwa ni mimi anyenikimbia.
‘Kwanini anikimbie, ninatisha nini….hapana,sizani kukaa
jelamiezi hiyonimebadilika kiasi cha kutisha watu, huyu ana lake jingine,
‘nijajikuta nikiongea mweneywe huku nimeushika ule mkoba mkononi, sikujua
niufaye nini….
Nikiwa natembea mbali ya lile jengi nikawa nawaza kuhusu haya
maisha maana tangu nitoke jela, imekuwa mimi kama kioja fulani, maana huyo sio
wa kwanza kuonyesha dalili ya kunikimbia, kila nikikutana na mtu anayenifahamu
kidogo,, mtu huyo hunikimbia,na wala hataki kuongea na mimi, nikajiuliza kuna
nini,au nimekonda sana,au nina nini cha ajabu cha kuwafanya watu wanikimbie.
Kwa maisha kama haya nikajikuta nikilala kwenye majengo
wanayolala wachuuzi au wafayabiashara wanaoleta mizigo toka mkoani,na wakati
mwingine nafanya akzi ya kupakua hiyo mizigo na kupata chochote, na siku
zinakwenda.
Niliwaza sana, nilipotokea, maana nilikuwa mtu wa watu,
nlikuwa na nyumba yangu nzuri, kazi nzuri, lakini sasa nipo mitaani ,
ombamba,…kweli hujafa hujaumbika, na hapo hapo nikaumbuka siku ile nilipotoka
kwenye huo mkasa ulionifanya nisweke jela kwa miezi zaidi ya sita....
*******
Siku ile nilipotoka jela, nilitokea mhakamani, ….moja kwa
moja niliongoza kiguu na njia hadi mahali pale palipokuwa na nyumba yangu,
nikitarajia nitamkuta mke wangu, ingawaje ni siku nyingi sijamuona, tangu kesi
ianza, hakuweza kukanyaga mahakamni, nikajau labda anaumwa, na hata
nilipomuuliza wakili wangu, hakunipa jibu la maana, ….alisema hajui mke wangu
alipo , mimi nisimuwaze yeye, niwazie kesi yangu.
Nilipotoka jela, sikuwa na mahali pakwenda, zaidi huko
nyumbani kwangu,nikatumia pea kidogo aliyonipa Yule mwanadada wakili. Alinigaia
hiyo pesa, pale aliponiona nikiwa nimeduwaa, aliponiambia kuwa kuwa,nipo huru,
sina hatia, kamamahakailiviyosema, kwahiyo naweza kuondoka.
‘Naweza kuondoka….?....., ina maana haina haja ya mimi kurudi
kule gerezani…?’nikauliza.
‘Haina haja, hukusikia hakimu alivyosema, ….wewe nenda
nyumbani kwako , kajipange vyema, uachane na hawo watu , hasa huyo mke
wako,…’akaniambia.
‘Ni kweli sijui yupo wapi maana sijamuona akija kweney
kesi….’nikasema.
‘Achana naye, chukua nauli hii,nenda nyumbani kwako,
kamuommbe mungu wako….maana huko ulipokuwa ukienda sio mahali pema…nakutakia
maisha mema,na kama utakuwa na tatizo chukua kadi yangu hii hapa
nitakusaidia…’akasema na kunipa kadi yake na pesa ya nauli.
‘Nashkuru sana, na ubarikiwe sana, kweli wewe ni mtu mwema
sana….’nikasema huku nikimwangalia kwa uso wa huruma.
‘Usijali yote ni maisha….nia yetu ni kuwasaidia wote,…lakini
lengo letu hasa ni kwa akina mama,na nyie wanaume maliojikuta kwenye huu
mtego….’akatulia kwa muda, na baadaye akasema;
‘Nakushauri tena, …achana na hawo watu,… jipange kimaisha na ukijitahidi maisha
yatakuwa mazuri bila kutafuta njia za mkato, wengi ndipo wanapokosea,
….utatajirikaje kwa kutumia mgongo wa mwenzako, hali ujue kapataje mali aliyo
nayo…..kwaheri tukijaliwa tutaonana tena lkini iwe kwa heri, sio kwa shari, au
sio …?’akasemana kuingia kweney gari lake akaondoka zake.
Nikafika maeneo ya
ilipokuwa nyumba yangu, lakini nilipofika hapo nilikuta jengo limebadilika
kabisa na limekarabatiwa kivingine,…hutaamini kuwa pale ndipo ilikuwa nyumba
yangu,nilifikiri nimpotea, lakini nilipotizama vyema, nikawa na uhakika ni hapo
hapo,maana zipo alama nyingine zipo vile vile…..
‘Huyu mwenye hili jengo yupo wapi…?’ nikauliza.
‘Hatujui, yeye anakuja mara moja moja kwa mwezi kuchukua
pesa yake,na kuishia zake, hatujui wapi anapoishi,kwanza itatusaidia nini,kama
tunalipia kodi yake….mtu kama huyo huhitaji we anakuja mara kwa mara, anaweza
akakupandishia kodi,kwanza ukimuona moyo unalipuka paaah, unajau sasa kodi ya
watu inahitajika……’akasema jamaa mmoja mwenye duka kubwa la vifaa vya simu.
Nililiangalia lile Jengo
lilivyorabatiwa kwa muda mfupi,moyoni nikasema, kweli watu wana pesa, usiseme
hata siku moja, kuwa na kuwa la kibiashara, sio nyumba ya kuishi mtu tena,
sikukata tama nikajaribu kuwauliza watu mbali mbali hadi nikampta mtu mmoja
anayepajua vyema hapo mahali , ndipo akaniambia kuwa hilo jingo lilikuja kuuzwa
kwa muhindi mmoja,alaiyelipa pesa nyingi kwa dadammoja aliyekuwa akimiliki
hapo, na huyu dada hajaonekana tena hapa mjini tangu alipouza hilo jingo.
‘Huyo dada umafahamu vyema?’ nikamuuliza.
‘Kwanini nisimfahamu, Yule Malaya…alikuwa akijiita kimwana,
kumbe kazi yao ni kujiuza na akimpata bwege anamuweka ndani, na mwisho wa siku
anamuibia huyo bwege, …na hata hii nyumba ilikuwa ya bwege mmoja,aliyemchukua
huyo kimwana,…eti mpaka wakafunga ndoa, …mwisho wa siku, akatapeliwa…’akasema
huku akicheka.
‘Akatapeliwa nyumba nzima,….siamini…’nikajifanya kushangaa.
‘Unashangaa mjini hapa, kashangae juu, ndege inaelea hewani,….,
hapa mjini bwana, kama umekuja leo
utashangaa sana. Hii nyumba nakumbukakabisa ilikuwa na bwege mmoja, ambaye
alijenga kwa mkopo,nakumbuka kabisa,na huyo kimwana akafanya mambo yake, na
watu wao huko sijui wapi, na mwisho wa siku nyumba ikawa yake…’akasemahuyo
jamaa.
‘Kweli hapa mjini, ina maana huyo kimwana alikuwa na pesa
nyingi sana…au alizipata wapi?’ nikadadisi.
‘Usiniuliza kazipata wapi, wakati nimekuambia kuwa kazi yao
ndio hiyo ya uatapeli, inawezekana kuna njia zao walitumia,au alimtapeli mtu
mwingine kinamna, kwasababu alipouz ahii nyumba akapotea kabisa, nakumbuka kuna
jamaa alikuja kufungua kesi na huyu mhindi akidai kuwa nyumba hiyoni yake,
lakini alishindwa kesi.
‘Ohh, kumbe basi hii nyumba ina hsitori
ndefu…’nikasema...huku nikigeuka pembeni ili asije akanijua huyu jamaa,ambaye
alikuwa akionge huku akaifanya shughuli zake.
‘Huyu bwege aliyekuwa akimiliki hii nyumba mwanzoni sasa
hivi yupo wapi…?’ nikauliza.
‘Sizani kamayupo hai, maana hawa akina dada akikutapeli
ukajifanya mjanja, utaondoka hii dunia,…sina uhakika kamayupo hai,na kamayupo
hai atakuwa jela, au kakimbilia kijijini kuogopakuumbuka…’akasema huyo jamaa.
‘Ukimuona unaweza kumtambua…?’nikamuuliza.
‘Kwanini nisimtambue…kama kweli yupo hai, maana wngi
walionaswa na hawo watu, utasikia mara kajiua ,mara kafa kwa shinikizao la damu,wengine wanakumbwa na
kiharusi,….kwakeli Yule jamaa siwezi kumashau,….’akasema na kuinua boksi
alilokuwa akijaza vitu.
Akatulia kidogo kama anawaza jambo, halafu akasema; ‘Hata
kama kabadilika kimaisha nikimuona tu nitamfahamu…unajua ndugu sasa hivi watu
wanahangaika na maisha, hakuna mtu anayejali kuhusu mwingine, unahangaika kuangalia maisha yako nay a
familia yako. Nikuulize kwanini unamuulizia huyo bwege,una shida na yeye…?’
akauliza na safari hii aliinua kichwa kidogo kuniangalia, na haraka nikageuza
uso upande mwingine,na kuanza kuondoka, huku nikisema;
‘Sina shida na yeye…..,nilikuwa natafuta sehemu ya kuweka
biashara …..sasa naona huku hapanifai tena…’nikasema na kujiondokea hapo
haraka, nisije nikaumbuka, na nilipogeuza
kichwa nikiwa mbali, nilimuona yule jamaa akiwa kaduwaaa akiwa ananiangalia, …nikageuza
kichwa haraka na kuangali huko ninapokwenda, na sikugeuka nyuma tena, na toka
siku hiyo nikawa sitembelei maeneo hayo.
**********
Nikiwa na ulemkoba wa Yule mwanamama nikaondoka hadi kwenye jingo
moja lililokuwa linajengwa, na nikatafuta sehemu yenye amani, nikakaa, hapo
nilipokaa, kulikuwa na shomo la maji taka, lilikuwa refu na naona lilikuwa
likitumika,….na lilikuwa refu sana, nikaachana nalo na kukaa juu yake, huku
miguu nimeiningiza kweney shimo,….nikawaza, sasa nifanyeje, nikakumbuka kuwa
sijala,….
‘Oooh,huku kukaa na njaa kutaniua, pesa bado , nikajipapasa,
na kujikuta nina elifu tatu,…kabla sijainuka, wazo la kuukagua huo mkoba
ukanijia,….sikupenda kufanya hivyo, jela ilishanifunza,..sitaki tena kureeja
huko,huko sio pa kwenda, jamani..
Lakini moyo uuitamani kitu, na kitu kikiwa karibu nawe,
unashindwa kuvumilia, nikauchukau ule mkoba na kuufungua,….nikakuta simu ya bei
mbaya…nikaiangalai,ilikuwa hewani, ina maana kulikuwa na mtu anapiga, lakini
mlio ulikuwa hautoki, ….na mara bila kutarajia nikakuta nimeshaipokea ile simu;
‘Ule mzigo nitakuletea huko huko kijiweni,uje na pesa yangu
taslimu,….ni mara mbili ya ule, na uwe makini maana mandata wamecharuka, ila
hapo kijiweni hawajapashitukia, watumie wale wale akina mama….’simu ikakata……
‘Mzigo gani huo….?’ Nikajiuliza.
‘Nikairudishia pale pale,na kukagua vitu vingine, nilichokuta
cha zaidi ni mfuko wa plastic, ndani kulikuwa na mfuko mwingine,una vitu vimefungwa
kama vibunda vya binzari, ni unga ungamweupe,sikuangalia zana,maana vilikuwa vingi
tu,….moyoni nikasema,ina maana huyu mwanamama na ujanja wake wote anafanya
biashara ya viungo vya kupikia,maana hii inaweza ikawa ni hamira....
Nikaufungua vyema, na kutoa kimoja…ulikuwa kama `glucose’
ulaini wake,…nikalamba…mmh,mbona haina aldha, nikatema, na kukirudishia
humo,sikuwa na wazo jingine lolote, na kwa vile nilikuwa na njaa,nikaona
nitafute kama kuna pesa.
‘Nitachukua pesa….siiibi, nachukua tu kwa gharama ya
kuhangaika kwangu,….nikikutana naye nitamwambia….nikachukua elifu kumi,…na mara
kwa pembeni nikaona pesa za kigeni,zilikuwa kwenye kimfuko cha pembeni….nikachomoa
dola mia,nikaichunguza, nikaiweka kwenye kiatu changu….
‘Ngoja nitaichunguza vyema, huyu mama anaweza akawa ana dola
za bandia, ukishikwa nayo unaishia jela….’nikatulia kwaza, nikiwaza…sikuahangaika
na huo mkoba tena, maana vitu vingine vilivyokuwa humo ndani vilikuwa
vikorokoro vya akina mama,nikaufunga ule mkoba, na kumbe kulidondoka picha
mbili za `pasipoti size’, nikaziokota, na kabla sijaitizama vyema, mara kwa
nyuma nikasikia sauti, na picha moja ikaniponyoka,nikabakia na moja, sikuweza
kuiokota tena, mawazo yangu yakawa kwa hawo watu wanaoongea….
‘Ndio Yule pale….ndio…. yule, Yule….yule pale….’nikageuka,….walikuwa
ni askari..’mmh,nikasema hapa ndio balaa la kurudi tena jela,nikauangalia ule
mkoba, nikajua hiki ni kidhibiti cha kuwa nimeiba, labda ndio wanaoutafuta….nikageuka
kule walipo wale maaskari….kabla hawajanikaribia nikaanza kurudi nyuma,
kutafuta upenyo wa kukimbilia.
`Wewe simama hapo hapo….’ Akaamrisha mmojawapo wa wake
maafande.
‘Kwanini bwana afande…?’ nikauliza
‘Kuna kitu ulicho nacho, ambacho sio mali yako,….’akasema.
‘Ni kitu gani afande na ni mali ya nani… bwana afande, ….maana…’nikasema
na kusogea mbali na wao, ….wakaja hadi pale nilipokuwa nimesimama, na kile
kimkoba nimekishika kwa uficho.
‘Ni mkoba wa mama Yule pale aliyesimama pale barabarani,anauhitaji
mkoba wake tu,hana haja na wewe,….tunauomba na uishie zako….’akasema huyo
afande.
‘Kama ni hivyo tu, haina shida, aje mwenyewe auchukue…lakini
sio nyie….’nikasema.
‘Anakuogopa….wewe tupe tumpelekee…’akasema huyo afande.
‘Kwanini aniogope na nitakuwa na ushahidi gani kuwa nyie
mtamfikishia….’nikasema na huku nimesogea mbali na wao kama vile naeleeka kule
barabarani. Na kule alipokuwa Yule mama nilimuona akiwa kama anarudi kinyume
nyume….hasa pale aliponiona nikiwa namsogelea yeye….
‘Yule afande akatoa bastola, nakusema…lete huo mkoba au
nitakushughulikia kama jambazi…’akasema na mara akaja afande mwingine aliyekuwa
mwanzoni kasimama na yule mama akawaambia;
‘Msimuue,…..hakikisheni mnauchukua huko mkona tu na yeye muwacheni
aende zake,…‘ akasema.
Niliposikia hivyo kuwa kumbe hawana haja ya kuniua
mimi,nikaanza kuwachezea shere, walipokuwa wakinifuata huku, kwa kasi
wakitimiza amri ya bosi wao nakimbia upande mwingine kuwakwepa,…..wakija huku
napitia huku, na wakati nakimbizana nao, nikajikuta nimefika pale palipokuwa na
lile shimo la maji taka,.na muda huo wazo langu halikuwa limekumbuka hilo shimo tena,….tahamaki
nikajikuta nimekanyaga sehemu ya lile shimo, na kuporomoka kwenda ndani, ...nikazama, na bahati nzuri, mikono ikawahi kudaka chuma
kilichokuwa kimiejitokeza, nikabaki naelekea ndani ya hilo shimo….
‘Aaaah, nisaidieni, ....mungu wangu……’kukuru
kakara, ule mkoba ukaniponyoka na kutumbikia ndani ya lile shimo,na hata Yule afande
aliponikaribia naye huyo akaserereka,na kutumbukia…hata alipojaribu kuudaka ule
mkoba ikashindikana,tukawa tunauangalia ukizama,…huku tumeshikilia kile chuma, ….haraka
nikajikakamua na kupanda juu….nikatimua mbio…
‘Wewe mpumbavu kweli….’akasema huyo afande, ikajaribu kuutoa
mguu wake ulionasa, na mimi bila kusema kitu nikatimuka mbali kabisa na wao, …..nilipogeuka
kuwaangalia, niliwaona wakiwa wamejikusanya wakiangalia ndani ya lile shimo,na Yule
mwanamama alikuwa mmojawapo.
Wazo la kuwafuata likanijia, nilitaka nimuombe Yule mama
masamha ….nikawa nawajia, …yule mama akaniona akawaambia kitu wenzake….wenzake
wakasimama kuniangalia, ….wakaniona nawajia, ….mara wote wakawa wanarudi
kinyumenyume…mara wakageuka, wakwaza kukimbia alikuwa Yule mama, halafu mara
wale maafande na wao wakafuatia na kuanza kutimua mbio….
Nikabakia nikishangaa, ….vipi ina maana hata maafande
wananiogopa…kuna nini jamani…..nikakumbuka ile picha niliyokuwa nayo,….bado
ilikuwa mkononi,nikaigeuza sehemu inayoonyesha sura…..kwanza nikashituka,…nikakadoa
macho kuiangalia vyema…..mapigo ya moyo yakaongezeka…..
Je kwanini wanamuogopa huyo jamaa…na je huyo mwanamama ni
nani?
WAZO LA LEO: Kumbuka kumshukuru mungu kwa kila jambo, liwe la heri au la shari liwe jema au baya, kwani yote hutokea ili iwe sababu ya jambo fulani.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
m3 na mimi nafikiri ni kwa nini watu wanamuogopa jamaa huyu sipati jibu lolote
i cant wait kujuwa mungu akujalie kila kheri m3
Ndugu wa mimi kazi yako ni yakipekee, Mungu azidi kukufunulia, pia Ahsante kwa WAZO LA LEO!!!Pamoja Daima ndugu wa mimi!!!!!!
Post a Comment