Nikiwa nimeshika ile picha mkononi, niliinua kichwa na
kumwangalia Yule wakili mwanadada, ambaye alikuwa kipita na gari,…. akanikuta
nikiwa nimekaa kwenye jiwe, na hapo nimeishikilia ile picha. Tulisalimiana na
akaniuliza habari za maisha yangu tukaongea kidogo na akanialika kwenye chakula
cha mchana, nikashukuru kwa ofa hiyo.
Tulipomaliza kula, akaniuliza hiyopicha nimepata wapi,
na hapo nikamhadithia kisa cha huyo
mwanamama chotara wa kizungu mweney nywele nyingi, na kisa hicho kikamvutia
sana, na alikuwa anataka kuondoka, lakini nikaona ana hamu kusikia mengi kuhusu
huyo chotara wa kizungu.
Nilipomaliza kumhadithia yaliyonikuta, akaingalia ile picha
ambayo kwa muda huo nilikuwa nimeiweka mezani ,akaniangalia kwa makini halafu
akasema;
‘Sasa mbona umebakia na hiyo, ina umuhimu gani tena, maana
kama umesemahuyo mwanamama akikuona anakimbia, na hiyo picha umesema haifanani
kabisa na yeye, unanini na hiyo picha,maana unavyoiangalia ni kama vile
unamfahamu huyo aliyepo kwenye hiyo picha.. au umependa hiyo picha maana kweli
mweney hiyo picha anaonekana ni mrembo….hebu niambie kulikoni…?’
.
‘Kiukweli namfahamu sana mwenye hii picha, …na inanikumbusha
mbali sana, mbali kulko maelezo,,cha kujiuliza ni je huyu mwanamama kaipataje
hii picha, au ana uhusiana gani na huyo binti, mwenye hii picha, maana sijawahi
kumuona huyu mwanamama huko kijijini, ….hapo sijaelewa…’nikasema.
‘Huenda ndio hawo mawakala wa kutafuta mabinti na kuwarubuni
kwa matajiri….’akasema huyo wakili.
‘Inawezekana,…. maana haiji akilini awe na picha yake,na
sizani kama huyu binti yupo hapa nchini, na nionavyo mimi labda atakuwa
keshaolewa au yupo nchi za nje, kaolewa na wazungu,…kwani ni kipindi
kirefu…nakumbuka siku anapiga hii picha nilikuwepo, alinipa kopi moja,….kopi
yangu nilikuwa sibanduki nayo , lakini ilikuja kupotea.
‘Kama ni hivyo mbona ni muda mrefu sana….hatakuwa hivyo
anavyoonekana, isije ikawa ni binti wa huyo mwenye hiyo picha….maana mimi
ninavyo hata kama huyu mwanamama ni wakala, hawezi akatafuta huyo binti,
kwasababau hatafaa kwa hiyo kazi,najua wao wanatafuta mabinti
wadogowadogo..sijuii unanipata hapo…?’ akasema huyo wakili.
‘Na kweli,labda kuna jambo….na ndio maana nawaza sana, na
nitafanya kila njia nikutane tena na huyo mwanamama, hasa kwa jili ya hii picha
sio vinginenvyo….’nikasema
‘Natamani nisikie kisa chako na huyo mwenye hiyo picha, mmh,….sijui
kama nina muda,…naona maisha yako yanavisa vingi na vingi ni vya kusikitisha,
una damu gani wewe …?’akasema huyo wakili huku akicheka na kusubiri asikie nini
nitasema, nami hapo hapo,kwanza nikaangalia juu na kutabasamu, halafu kumbukumbu
zangu za utotoni zikanijia na kuaanza kumhadithia huyu wakili kisa changu na
huyo anayeonekana katika hiyo picha;
***********
‘Hawa watoto wanapendana sana,….utafikiri ni ndugu, wakiwa
wakubwa kama wataoana natumaifamilia
yaoitakuwa na raha, …..’akasema mama mmoja.
‘Nikuambia ukweli mama Nanhii,ni nadra sana kwa watoto
wanakuwa hivi kuja kuoana, maana mwanaume anachelewa sana kukua na kuanza maisha,
mpaka ahangaike ajiweke sawa, binti atakuwa kesahakuwa mkubwa, na wakiacahaan
kidogo tu,kunatokea mabadiliko, na hata wasijuane tena,…..’akasema mama
mwingine waliyekuwa naye,na kauli kama hizo tulishazisikia sana.
‘Hivi kweli tukiwa wakubwa si tutaoana..?’ nikamuuliza
mwenzangu.
‘Kwani kuoana ni nini,mimi naona raha tukiwa hivi hivi
milele..sijui nitaishije kama tutatengana tusionane tena…kweli tukiwa wakubwa,
uahidi kuwa hutaniacha, utanioa mimi...’akasema .
‘Naahidi kwa mungu, wewe utakuwa mke wangu,…hata itokee
nini, au tuoane sasa hivi kabisa..’nikasema na ikawa kama mzaha, maana
tulitafuta vitu tukajiandaa kama bwana ba bibi harusi, na baadaye tukaulizana;
‘Sasa nanai atautufungisha hii ndoa, siunaona wakati
wakifunga ndoa kunakuwa na mtu wa kufungisha ndoa, ..?’ tukaulizana.
‘Mungu anatosha,…mungu ndiye atatufungisha hii ndoa na ndiye
shahidi wetu. …’nikasema na kweli tukakaa vyema na kuanza kusema yale maneno
tuliyosikia wakisema wakati wanafungisha ndoa, na toka siku ile tukawa
tunaitana mke na mume.
Ulikuwa ni utoto,
maana tulipoanza kusoma, akili zileza kitoto zikawa zinapotea,lakini kukweli
ndani ya nfasi zetu,tulikuwa tumejenga upendo wa dhati, tulikuwa karibu na hata
tukienda na tukirudi tunakuwa pamoja.
Nilipofika darasa la saba, ndipo nikaanza kuwa na utundu
kutokana na vile vitabu nilivyokuwa nikisoma kwa
Mjomba, na hapo ndipo nikawa
na akili ya kujua kuwa kuna mahusiano ya mume na mke,kutokana na hivyo vitabu,
lakini sikuwa na akili ya kikubwa kihivyo, ni utundu tu. Utundu wangu ulikuwa
kwa wasichana wengine, sio kwa huyu binti,….’nikasema huku nikiwa nimeshika ile
picha mkononi.
‘Binti huyu nilimuheshimu sana, licha ya kuwa moyoni
nilimpenda, lakini kwa viletulikuwa pamoja muda mwingi ikawa namuona kama dada
yangu zaidi. Hata yeye aliniona kama kaka yake, maana alija kwetu anauliza kaka
Msomali yupo wapi,…na hata mimi nikienda kwao naulizia kama dada, sio mke au
mume, kama tulivyoahidiana tukiwa watoto.
Urafiki wangu na huyo binti ulianza kuingia sura mpya,pale
mini nilipoanza masomo ya sekondari,na kutokana na vile vitabu nilivyosoma vya
mapenzi, nikawa naanza kuvutika zaidi, na kwa vile sekondari ilikuwa ni ya bweni, basi nilikiwa shuleni kila mara
namuandikia barua huyo binti, na sasa tunaitana wapenzi, …kaka mpenzi na dada
mpenzi.
Nakumbuka nilikuwa na
boksi zima laa barua nilizoandikiana na huyu binti, na kwakweli alikuwa akijua kuandika barua za
kimapenzi, hata kipindi nilipokuw mkubwa, na nikiwa nikizipitia, nilitambua
kuwa huyu binti atakuwa na kipaji Fulani cha mambo hayo, kama sio uandishi basi
akisomea fani zinazoendana na mambo haya atafanaikiwa sana.
‘Huyu kweli akiwa mpenzi wangu sitakuwa na shida, nitampenda
sana….kwasababu anajua kupenda…’nilikuwa nikisema hivyo.
Mambo yakaanza kubadilika pale walipohama na kwenda kuishi
Kenya, akawa ansomeahuko, lakini mara kwa mara walikuwa wakija likizo, na mimi
nnikiwa likizo, tunakutana, na huwa tunaongea sana,….hutaamini nikiwakaribu
naye, siwezi kumchezea, au kumfanyia chochote, tunaheshimiana kama kaka na
dada, ila tunaongeza kimoyoni `mpenzi’….nilikuwa naogopakumuuzi,au kumfanyao
jambo litakalo mkasirisha.
‘Hivi unakumbuak wakati tukiwa wadogo,unaikumbukaile ndoa
yetu ya kitoto…’akaniuliza huyu binti, na mimi nikacheka sana,na kucheka kule
alikutafsiri vibaya,maana nilimuona akikunya uso kwa hasira, akaniangalia kwa
makini halafu akauliza;
‘Ina maana wewe umeshabadili ile ahadi yetu…?’ akaniuliza
‘Ule ulikuwa utoto, hivi unaweza kukubali kuwa wewe ni mke
wangu?’ nikamuuliza.
‘Ndio ulikuwa utoto, lakini ndio ulikuwa mwanzo wa maisha ya
kikubwa….nakuuliza ina maana wewe yale hayapo tena moyoni mwako, unakumbuka
barua tulizokuwa , unakumbuka kila mara nilikuwa nakikuuliza kuhusu ahadi
yetu…?’ akaniuliza.
‘Nakumbuka sana,…lakini mengi ni ya utoto, au sio, na sio
kwamba nasema sikupendi, nakupedna sana,na kama ningelikuwa na uwezo
ningelikuambia tufunge ndoa , lakini sisi bado wadogo, bado tunasoma,… na
sipendi wewe nikuharibie maisha yako, kwa mambo ya kimpanzi, wewe nakuheshimu
sana, nitaumia sana nikifanya jambo litakalokuumiza baadaye….’nikasema hivyo,
lakini nakumbuka tika siku ile nilimuona akiniangalia kwa jicho la hasira .
Hata kipindi kimoja
tulikutana na maongei yetu yakafikia huko huko, aliniambia wazi kuwa, kama
nitakuwa nimevunja ahadi yetu hatanisamehe hadi kufa kwake. Niliwaza sana kuhusu
huo usemi,lakini ndio utoto, bado tulikuwa vijana na sikujua kuwa mwenzangu
alikuwa kadhamiria kweli, ….na kipindi
kile ndio damu ilikuwa ikichemka, utundu wangu kwa wasichana wengine ulikuwa
mkubwa sana, hadi kesi zinaletwa nyumbani kuhusu huo utundu….
Walipokuja safari
nyingine,baada ya miaka kadhaa, huyo binti alikuwa sio Yule niliyemjua tena,
alikuwa kabadilika kweli, msomi wa nguvu, akili imepevuka, unajua tena wenzetu
huko Kenya, Kiingereza ni kama lugha yao ya taifa, kwahiyo huyu binti alikuwa
akiongea kiingereza kama mzungu, na alitawaliwa zaidi na maisha na tabia za
kizungu, nahali hiyo ilitufanya tuanze kuwa mbali mbali,hasa kutokana na maisha
na tabia za familia yetu.
Na hata hivyo sio sisi kama familia yetu tu tuliokuwa
tukiwaangalia kwa jicho jingine, lakini hata wavulana wengi, waliogopa kuongea na
huyu binti, kwasababu muda mwingi alikuwa akiongea Kiingereza na tukamuona kama
ana dharau fulani hivi ,unajua wivu unaweza ukaijengea hoja…Pamoja na hayo huyu
binti alijitahidi sana kuwa karibu na mimi, ila mimi nikawa na hisia zilezile
za wenzetu, na familia yangu ilianza kunipiga marufu nisewe najuana na huyo
binti, eti ataniharibu tabia na kuiga tabia za kigeni.
‘Ataharibiwa kitabia ipi hiyo aliyo nayo ambayo ni nzuri,….
wakati mwenyewe keshaharibika, hivi huoni tabia ya motto wako ilivyo, kila siku
kesi za kuwachezea wasichana wa watu,halafu unamkataza kuwa eti siwe karibu na
huyo binti,mbona binti wa watu hana
tabia mbovu kama za mwanao….au unamkataza ili asiwe kama mzungu…’akasema mama
aliposikia baba akinikanya kuhusu huyu binti.
‘Wewe hayo hayakuhusu, huyu licha ya tabia zake hizo….lakini
ni mwanaume,huwezi ukamwambia asiwe na mrafiki wa kike, …ila kuna tabia zingine
za kifamilia,huyu binti na familia yao wanaojifanya wazungu wataiweza….haya
maswala tunajua sisi tunao-ona mbali,…’akasema baba.
‘Haya,tutaona na huko kuona mbali kwenu..’akakubali mama kwa
shingo upande.
Kwa maneno ya baba nikapata kisingizio, sio kwamba nilikuwa
napenda iwe hivyo,…moyoni ilikuwa ikiniuma sana, nilikuwa siishi kumuwaza,
lakini kila nikikutana naye, nakuwa kama najigonga gonga, nahisi kuna kizuizi
fuklani,…..
Yule binti akagundua kuwa nimeanza kujenga umbali kati yangu
mimi na yeye na hili hakuweza kuvumilia, siku hiyo akaniita, akasemaakribu ni
wataondoka, anaomba tukapige picha ya pamoja,tulipiaga picha, ya pamoja, halafu
akapiga picha ya peke yake, ndio akanipa nakala moja na nyingine akabakia nazo
mwenyewe.
Tukiwa tunatembea ndio akaniuliza hilo swali nalikumbuka
hadi leo, aliniuliza hivi;
‘Hivi kwanini siku hizi nakuona hunipendi kama zamani …unakuwa
kama unanikwepa,….niambie ukweli bado nipo moyoni mwako,au ndio umeshakua, nay
ale ya utoto hayana thamani tena kwako….?.’siku hiyo akaniuliza.
‘Sio kwamba sikupendi, lakini nakuona kama wewe ni tofauti
na mimi sasa, unaonekana umesoma zaidi yangu, upo kama mzungu, na unavyongea
kiingereza, wanaume wengi wanakuogopa kuwa utawaabisha…na hata familia yangu
inadai kuwa huendani na maadili yetu…..hutaweza kufuatilia mambo yetu ya
kimila,ambayo ni muhimu sana kwa wazee wangu….’nikasema
‘Usitafute visingizio, kiingereza ni lugha tu, kama lugha
nyingine,haihusiani kabisa na makubaliano yetu, mimi sioni hilo kama ni tatizo,
mbonanaongea Kiswahili kama kawaida tu,….kumbuka sana ahadi yetu ya utotoni,
mimi kwangu ni kitu muhimu sana, ….kwasaabbu nakupenda toka ndani ya moyo
wangu, sio kuhusu mambo mengine ya nje….’akasema na kuniangalia akionyesha uso
wa huzuni.
‘Hata mimi nakupnda hivyo hivyo….ila, mambo ya
familia…..’nikasema
‘Kuhusu familia yenu ,kwani utaishi na wao milele, wao wana
maisha yao, na njua kabisa ipo siku utaachana nao,utakuwa na familia yako,
unatakiwa uaanze kulielewa hilo, pia mambo mangapi ya kifamilia unayokwenda
kinyume nayo…yapo mengi, lakini huo ni utaratibu wako,…..mimi ninawasiwasi na wewe,nahisi
umepata mwinginemoyoni mwako….’akasema na kuonyesha kuona aiabu Fulani.
‘Umeanza kutekwa na maneno ya kusikia ….hapa mitaani
waananisingizia mambo mengi, lakini hata hivyo, ni kawaida,mvulana lazima
uchukue mazoezi, ili nikikuoa wewe niswe na taabu ya masisha, kama unaniona
nipo na wasichana wengine, ni kupteza muda tu,lakini moyo wangu upo
kwako….’nikaaema
‘Hivi maneno gani hayo unayoyaongea, una akili kweli, hivi
na mimi nikifanya hivyo utajsikiaje ukiniona, sitapasuka kwa wivu na
hasira,….nikuambia kitu, …ni vyema ukajenga hisia za kumfikiria mwenzako,kuwa
je nikifanay hili mwenzangu atajifikiriaje, na je kama ningelifanyiwa mimi
nitasikiaje, huo ndio upendo wa kweli, kuthaminiana, ….lakini wewe unajifikiria
mwenyewe, hunijali mimi hisia zangu….’akasema na mimi nikabaki akukuna
kichwa,nilikuwa na tabia mtu akiniambia kitu kamasina jibu la kumpa, najikuna
kichwa.
‘Kwahiyo wewe unasemaje…nianze utundu kama ninavyowafanyia
wasichana wengine…mimi sipendi kukuharibu, nataka tukioana ndio tuanze mapenzi
….au wewe unaonaje…?’ nikasema nikiwanamwangalia na yeye akacheka kwa dharau,
na kicheko chake cha dharau kilikuwa sikipendi,na wavulana wengi walikuwa
wakiliongela hilo.
‘Unajua mambo hayo mnayofanya nyie…., kwa umri huo, sio
wakati wake kabisa,mimi ninachoongelea hapa ni urafiki wa kweli, ambao hatima yake
ni kuwa mke na mume, sio mapenzi ya kimwili,….bado muda wake…’akasema na
kuniangalia kwa makini.
‘Hivi wewe siunaishi maisha ya kizungu….mimi najua wazungu …kwa
mambo hayo ndio wenyewe, mmmh…’nikajiuma uma, na sikusema kitu, ila yeye
akasema;
‘Unajua nyie wavulana mnajidanganya sana mkikutana, mna
tabia mbaya sana,… nimeshasikia tabia yako…ya kuwaharibu wasichana wa familia
zawatu wengine,…na hivi mnafikiri wazungu wao sio wastaarabu,….ndio wapo waliharibika
kama nyie, lakini wengine wanajiheshimu, kujiheshimu ni ubinadamu wa kila mtu,
awe mzungu au mwafrika…..’akasema na kuniangalia machoni.
‘Hapo hujaniambia kitu…..’nikasema.
‘Tatizo ni kwa vile mnachukulia mapicha mnayoangalia, au
hawo wanaorudi huku wakiwa wamechanganyikiwa ndio mnachukulia kuwa wote wapo
hivyo….wenzenu kwanza elimu, na mengine yanafuata baadaye, lakini nyie,
mnayachanganya mapema,kwanza starehe,elimu itakua yenyewe, hutafika namna
hiyo…’akasema.
‘Usinidanganye, usione kwa vile na kuheshimu ukafikiri sijui
maisha ya kizungu,….lakini ipo siku..’nikasema.
‘Wewe, usione na mimi nakuangalia unavyofanya ukafikiri
sitaweza kumtafuta Yule atakayenipenda, …huko wananibembeleza lakini sikubali
kwa ajili yako,……kwa ajili ya kukupenda, kwa ajili ya ahdi yetu…lakini
mwenzangu naona hata hunifikrii kabisa…’akasema.
‘Usinidanganye, ….najua huko Kenya unao wengi tu, hasa
wazungu…ukirudi huku unajifanya huna mtu….lakini yote hayo ya nini,
nimeshakuambi kuwa wewe niye tegemeo la moyini mwangu, hwo wengine wanakuwa
wakupotezea muda,….’nikasema.
‘Hiyo kauli,…..kama ungelijiua nisivyoipenda,….hebu
nikuulize hivi dada yako akifanyiwa hivyo utafurahi, ninavyokujua usingekubali
kamwe….kama hupendi, kwanini sasa unawafanyia watoto wa wenzenu, ….nakukanya
kuhusu hiyo tabia,sio nzuri….. ukumbuke tulivyoahidiana tulivyokuwa wadogo kuwa
tutapendana….lakini hatutaharibiana hadi tukiwa wakubwa, hadi tukifunga ndoa,
yale yalikuwa na maana sana, ina maana ahadi yetu ilikuwa ya uwongo….?’akasema
kwa masikitiko.
‘Sio kwamba sikupendi,..na ahadi yetu ipo moyoni….na,
na…ndio maana wewe nakuheshimu sana, siwezi kukufanyia mambo ninayowafanyiwa
wasichana wengine…’ nikasema na yeye akainuka na kuniangalia kwa hasira na
kusema
‘Mimi kauli yako hiyo siipendi,….kwanini hujali hisia za
wenzako, …eti mambo ninayowafanyia wasichana wengine, ina maana una wasichana
wengine unawafanyia …nini sijui, unao sio…..?’ akaniangalia kwa hasira,…..
Kauli yangu hiyo ilikuwa ikimvunja sana moyo,na akawa kaninunia
na yeye akaanza kujenga umbali fukani na mimi, ingawaje kila mara nikikutana
naye nilimgundua akiwa akiniangalia kwa jicho la kujiiba,na nikikutanisha macho
yangu na yake huangalai pembeni kwa haraka, hakutaka macho yetu yakutane.
Na mimi hapo nikaona
ni bora nisijitese kwa ajili yake, nikawa sijifichi tena kuwa na wasichana
wengine, na akitokea akinikuta nikiwa nao,nilimuona kabisa akikunja uso wa
hasira, na nilijua kabisa namuumiza moyo wake,lakini nikawa najifanya
sijali,ila sikupenda kumuumiza, kwanii mara nyingi nilikuwa nikijitahidi
asionione , lakini wasichana wa pale kijijini walikuwa wanataka kama kumkomoa
vile, wakamuona wanajionyesha kuwa mimi na mpenzi wao.
Nakumbuka safari moja,ambayo nilimuumiza sana huyo binti, ni
siku moja alipokuja nyumbani, akiwa na malengo ya kuniaga kuwa wanaondoka,
akaniifumania na msichana mmoja, tukiwa
chumbani kwangu, kitandani,…maana kule kijijini nilikuwa nimepewa chumba
changu cha uwani, ….sitasahu siku hiyo.
Alifungua mlango, sikujua kwa waakti huo, maana nilikuwa
mbali,nilipogeuzakichwa change na kumuona akiwa kasimama mlangoni,nilishikwa na
aibu ya mwaka, nikumbuka niliziba macho kama afanyavyo mtoto mdogo, aili
sionekane, wakati unaonekana….na yule msichana tuliyekuwa naye mlendani akawa
ananishikilia, na mimi nikawa namsukumambli na mimi…..
‘Hivi kwanini wewe unanifanyai hivyo….?’ Akasema akiwa
analia ….niliondoa mikono machonii na kumwangalia kwamasikitiko, niliumia sana
moyo wangu sikuu ile, sikutarajia kuwa angelikuja. Na hapo hapohapo akageuka na
kuondoka.
Toka siku ile hatukuonana tena, liondoka kurudi Kenya,na
huko walikaa sana, na hata walipokuja mara moja, hakuweza kuja kuniona,
nilipata ujumbe tu, kuwa walikuja, na ujumbe huo ulisema kuwa yeye bado
anatunza ileahadi yetu, na kama nimeamua kuivunja, …ipo siku nitajuta…ilikuwa
karatasi ambayo hakuwa na maneno mengi kinyume na alivyokuwa akiniandikia
zamani, mwishoni aliandika na hivi;
‘Ulinichonifanyia sitakisahau maishani , lakini ipo siku
utajuta na utanikumbuka…..
Kimiya kikatawala
*******
‘Kauli hiyo,….,huenda ndio inanitafuna hadi leo….’nikasema,na
kutulia kidogo , halafu nikayarudia yale maneno kwa sauti ya taratibu
nikayasema tena;
‘Ulinichonifanyia sitakisahau maishani , lakini ipo siku utajuta na
utanikumbuka…..’ na kweli najuta na namkumbuka sana huyo binti. Wakali
akaniangalia kwa makini, na baadaye akatabasamu, hakusema kitu kwa muda natumai
huyu wakili alikuwa akiwaza yake,au alikuwa akiwaza yale niliyomwambia, na baadaye
akasema;
‘Pole sana, inaonyesha huyo binti alikupenda sana,lakini
wewe ulikuwa kinyume chake….na ndivyo mlivyo wanaume wengi, mkipendwa hamjali,
huwa hamjali hisia za wenzenu, sijui kwanini..’akasema nafikiri na yeye kuna mambo
yalitokea katika maisha yake, …sikumuuliza, nikafuta uso wangu na kusema;
‘Hiyo ndio habari ya huyu mwenye picha hii,….’nikaiangalia
kwa makini, na kusema tena;
‘Sasa sijui kwanini ilifika kwenye huo mkoba wa huyu mwanamama
mwenye manywele mengi anayenikimbia kama akaona jinamizi, mama sikumbuki kabisa
kumuona huyu mwanamama huko kijijini, ni sura ngeni kabisa, tena aonekana
kabisa ni mchanganyiko wa damu za wazungu na kiafrika…Yule ni chotara…’nikasema.
Yule mwanadada wakili aliniangalia machoni kwa makini,
halafu akasema; ‘Siku hizi kuna madawa yanabadili sura za watu,ukimeza vidonge,
unabadilika kabisa na kuwa mweupe,…lakini weupe huo sio mnzuri, ngozi inakuwa
ya namna namna….Sijui kwa huyo mwanamama unavyosema ana sura kama ya chotara wa
kiafrika na mzungu,kama ningelimuona karibu ningelijua kuwa ni rangi ya asili
au ndio hawo wanaomeza madawa…’
‘Sina uhakika na hilo, na wala hilo halinisumbui kichwa
changu, …..maana nilimuona mara moja, na nywele zilikuwa zimefunka sana usoni
mwake, na mara ya pili nilimuona kwa mbali, akiwa uso wazi kidogo, ,lakini
nywela kaziachia na kufunika sehemu kubwa ya uso, nafikiri ndio mtindo wake
huo….lakini anaonekana kabisa kama ni mweupe kama mzungu…’nikamwambia wakili
huyo
Wakili huyo alitabasamu na kutaka kuondoka, nilimshukuru ka
chakula hicho alichoninunulia name nikamwambia kuwa naahidi kuwa safari
nyingine na mimi nitamnunulia chakula….akasema nisijali sana, nakabla
hajaondoka akaniulizia kama nimeshapata taarifa yoyote kuhusu alipo mke wangu
au Yule mama Docta.
‘Mimi hawo watu sijawahi kukutana nao, na hata nilipoulizia
wapi walipo, hakuna hata mtu mmoja anayejua, ni kama wamepotelea hewani, na
hakuna anayejali kujua wapi walipo….’nikasema
‘Inasemekana huyo Docta Mama yupo hapa nchini, na kipindi
kile cha kesi alikimbilia Kenya,na huko akawa anafanya yale yale aliyokuwa
akiyafanya huku, kule ana kibali, na anatambulika kama docta wa akina mama,…
ila hilo kuwa wanamshuku huenda ana biashara nyingine zaidi ya hiyo
inyotambulikana….’akasema huyo wakili.
‘Biashara gani hizo…?’ nikauliza.
‘Yeye ana kazi yake yenye kibali inayojulikana kuwa ni
mtaalamu wa ushauri wa ndoa na
mahusiano, na pia ni dakitari bingwa wa akina mama, kwa ushauri nasaha,na hata
matibabu ya uzazi. Kiujumla ni mtaalamu kweli, huko Kenya anatambulikana sana,
…lakini hapa nchini, hatambulikanani kihivyo na pia hapa nchini sio raia,
anakuja kwa kibali hicho cha muwekezaji…’akasema huyo wakili.
‘Aaah,kumbe ndio maana hata Kiswahili chake ni cha shida…,
na nchi hii itaharibiwa na hawa wawekezaji,tusipoangalia tutakwenda wengi kwa
migongoo ya hawa wawekezaji wakigeni…’nikasema
‘Unajua tulishaligundua hilo na mara nyingi tulikuwa
tukijaribu kutafuta mwanya wa kumshitaki huyu mwekezaji, hasa tulipogundua kuwa
anajihusisha na bishara hiyo haramu ya kuwarubuni akina dada, tukajaribu
kulifikisha ngazi zinazostahili, lakini kila vielelezo vilipopatikana, tukakuta
tunagonga mwamba, sijui kulikuwa na kikwazo gani,lakini nimegundua haya kupitia
kweney hii kesi yako..’akasema.
‘Uligundua nini…?’ nikauliza.
‘Na kipindi cha hiyo kesi yako, ikagundulika kuwa yeye ndiye
yupo nyuma ya hayo yote,na alitakuwa ashikwe na kufikishwa mahakamani, sijui
alijuaje akawa keshaondoka mapema, na hata kipindi kesi yako ikifanyika alikuwa
hayupo hapa nchini….’akasema huyo wakili.
‘Kwanini asishitakiwe huko huko alipo, akakamatwa…?’nikauliza.
‘Sheria zinatubana,na hatuna ushahidi wa moja kwa moja, na
utambue kuwa Yule ni mjanja sana, mambo yote hayo alikuwa kiyafanya kwa kupitia
watu wengine, yeye anakuwa kama mshauri tu…na hata huyo mwanasheria uliyekuwa
akikutetea wewe, hakuwekwa na yeye moja kwa moja, alitumiwa mtu mwingine
kabisa, ambaye kwa sasa ni marehemu….
‘Yule mwanamama kafariki….?’ Nikauliza kwa mshangao..
‘Ndio alikufa kwa shinikizo la moyo….na utakuta yeye ndiye
alishika kila kitu kwa hapa nchini, na
yule wakili aliyekuwa akikutetea hayupo hapa nchini, aliondoka siku ile ile ya
mwisho wa kesi yako, ….alikuwa keshakata tiketi ya kuondoka,…..anakwenda
masomoni huko Ulaya, na hata hivyo alitusaidia sana kufichua mambo mengi
yaliyokuwa yamejificha.
‘Yule mtu nilikuwa simuamini,ina maana alikuwa akiuma huku
na kule….?’ Nikauliza
‘Hayo tuyaache kwa sasa…kuna jingine maana nataka
kuondoka…?’ akaniuliza
‘Mhh, ni shukurani tu,ila….mmmh, nikuulize kitu,…kuna kitu kimoja nakishangaa
sana,…mpaka sasa nakuwa na wasiwasi ….sijui kuna nini kimetokea, nashindwa hata kuamini…’nikasema na kuangalia chini.
‘Kitu gani hicho, niambie ……kama ni kuhusu maisha yako,
nitakuasaida lakini sio sasa, ni mpaka mwakani, ambapo kampuni yangu itakuwa
tayari kuajiri watu,nimeamua kujiajiri…na wewe nimekuweka katika watu nitakao
wachukua, kwa sasa bangaiza hapa na pale ili uweze kuishi, mimi sina la
kukusaidia kwa sasa….maana mshahara wangu ni mdogo na una mikono mingi,mara
nyingi tunategemea wafadhili ….’akasema huyo mwanamama.
‘Sio kuhusu hilo, …ni ….ni….’ nikasita kidogo halafu
nikasema;
‘Unajua tangu nitoke jela, watu wengi wanaonifahamu ….’ Nikatulia tena
kidogo na kutingisha kichwa, halafu nikasema;
‘Hii ni ajabu kabisa, hata kumsimulia mtu nashindwa, ….watu
wanaonifahamu, nikikutana nao wananikimbia….kabisa, wengine wanatimua vumbi
kabisa….kama sijui naonekanaje…’nikamwangalia huyu mwanadada usoni, ili
aniangalie vyema, yeye kwanza alionyesha uso wa kujiuliza na baadaye
akatabasamu na kuniacha niendelee kuongea.
‘Na ningelisema labda ni kwa huyo mwanamama pekee, lakini sio
huyu mwanamama tu peke yake, huyo ninayemzungumzia eehe,…huyo mwenye manywele
mengi, ….., hata wengine….wakiniona tu, wakinigundua kuwa ni mimi wanakimbia,
hivi nipoje usoni, nimkonda sana..au…. kwanini….unajua inanipa shida sana hiyo
hali…huko sio kunyanyapaliwa kwa hali ya juu…au, sijui kwakweli...’nikasema
huku nikionyesha uso wa huzuni.
‘Mbona mimi nakufahamu sijakukimbia…huoni kuwa hizo ni hisia
zako tu,….kuna jingine labda ambalo hujaniambia…maana hapo sioni kuwa kuna
tatizo ni hisia zako tu….’akaniangalia na aliponiona nipo kimiya akasema;
‘Labda ulikuwa na watu wengi unaowadai,wakikuona wanakumbukia
deni, na kwasababu hawakutarajia kukutana na wewe, na kwa vile ulikuwa jela,
basi wanajua wewe ni mtu hatari, unaweza ukawatolea hasira kwao, au kuna kule
kukuona kuwa huna kitu, wanaogopa utawaomba…huo ni utani tu, usije ukaona nakuzarau….’akasema
na kucheka.
‘Sio kunizarau,huo ni ukweli usiopingika kuwa kweli sina
kitu, nimepigika, nimefulia, nimeanikwa uchi….ndio maana inafikia hadi kuwa
omba omba,….lakini sio kwamba napenda iwe hivyo ,ni njaa, ndio maana wanasema aduo
yako muombee njaa, njaa sio mchezo jamani…’nikasemahuku nikijaribu kutabasamu.
‘Kwa ujumla….sina uhakika na hilo,ila….kuna tukio sijui kama
lina ukweli, kuna watu wamevumisha kuwa kuna ombaomba majini, au masehtani, wao
wakikuomba ,ukawaangalia machoni tu, umekwenda na maji,..kwani utawapa kila
kitu chako, na mwishowe wanakuchukua na wewe mwenyewe…’akasemahuyo dada
akaniangalia machoni.
‘Kukuchukua kukufanyaia nini….’nikasema huku nikiangalia
huku na kule kwa uwoga.
‘Kukunyinya damu….wana njaa ya damu za watu….’akasemana
aliponiona nikiangalia huku na huku nikionyesha uso wa uwoga,akasema;
‘Si unaona sasa,binadamu huwa tumejengwana hisia za uwoga,
na nyingi tunajijengea wenyewe, unaweza ukawaza na hisia za kumbukumbu Fulani,
au hisia tu zinakuja kichwani, ukajikuta mwili unasisimukwa kwa uwoga,…kumbe
hakuna kitu….’akasema huku akitabasamu, halafu akaniangalia kwa makini, na
aliponiona bado nipo kimiya nikiwa kwenye mawazo au wasiwasi, akasema;
‘Hebu naiomba hiyo picha, ninataka nikaifanyie kazi , kama
nilivyokuambia, wafadhili wetu wametupa kazi ya kupambana na madawa ya
kulevya,…’akasema.
‘Sasa hii picha inahusianaje na madawa ya kulevya….?’
Nikauliza nikimwangalia kwa mshangao.
‘Wewe umesema kwenye ule mkoba kulikuwa na mfuko wa plastiki,
ndani ya huo mfuko kuna vipakti vidogovidogo,vilivyojazwa vitu kama unga unga….au
sio, na nakushangaa kidogo, ina maana wewe katika ujanja wako wote hapa mjini, hujawahi
kuona madawa ya kulevya?’ akaniuliza.
‘Sijawahi,…kiukweli sijawahi, na kwanini nihangaike kuyajua,
wakati situmii , …. nayasikia tu, na kwa muda ule,sikuwa na wazo hilo kabisaaa,
ulivyoniambia sasa hivi ndio na mimi najaribu kuwazia hivyo, inawezekana ikawa
ni madawa ya kulevya…..nilijaribu kulamba nikizania ni `glucose’, lakini
nilitema haraka nilipoona ladha yake sio yenyewe, nikiogopa isije ikawa ni sumu…..’
nikasema huku nikijaribu kukumbuka ladha yake
‘Uivyoelezea inawezekana kabisa hayo ni madawa ya
kulevya,…na kwa mtaji huo, huyo mwanamama uliyemuona anaweza akawa mzungu wa
unga anayetafutwa sana hapa nchini,tukimpata huyo…kesi imekamilika….na tutakuwa
tumepiga hatua kubwa sana,…..kwahiyo ukiwahi kumuona tena,nipigie simu
haraka…..unasikia…? akasema akasema kwa sauti aliponiona nimetulia kuonyesha
kuwa nipo mbali sana kimawazo
‘Nimesikia…..nakusikia unafikiri,…licha ya kuwa nipo mbali
kimawazo,lakini tupo pamoja…..’nikasema huku bado naiangalia ile picha.
‘Wewe nipe hiyo picha inaweza ikasaidia jambo…siku hizi
utaalamu mkubwa,..na hata hivyo….,nahisi kuna kitu ndani yake, …nitakigundua
tu, nahisi hivyo,na hisia zangu mara nyingi zinanipeka kwenye ukweli…’akasema.
‘Lakini huyu mwanamama hafanani kabisa na wauza madawa ya
kulevya, ….hii sura ya huyu mwanamama,…..mmmh naiona kama sura ngeni sana
machoni mwangu….na kwanini alikuwa ndani ya kile kijiwe, na haonyeshi kuwa ana
hali ngumu….kile kijiwe ni cha watu waliopigika….uliwahi kuingia mle ? ’nikasema
nakumuuliza huku naiangalia ile picha.
‘Hafanani eeh….hahaha, wewe usijali kabisa, wamailiki
wakubwa wa hizo biashara, huwezi kuwajua kwa sura, ….huwezi kabisa kuwadhania
kuwa wanafanya hiyo bishara na wengine hawatumii kabisa, wao wanauza
tu…kwasababu wanajua madhara yake….tatizo inakuwa kwa hawa watumiaji,.….hasa
vijana wetu, na hasa akina mama ambao ndio nawapigania kwa nguvu zangu
zote….’akasema huyo mwanadada wakili.
Nikasita kumpa ile picha,niliona kama ni kitu cha thamani
nimekipata baada ya kunipotea, ni kilikuwa ni kitu cha thamani sana kwenye
maisha yangu, nikaiangalia kwa mara nyingine na kumkumbuka huyo binti
tulivukuwa naye utotoni ikawa inanichezea akilini..sijui sasa yupo wapi
natamani nikutane naye angalau mara moja, najua atakuwa keshabadilika sana na
huenda keshaolewa ana watoto au yupo huko Ulaya, au …sijui wapi…lakini
sijasahau mapenzi yetu ya kitoto…
‘Mbona unasita kunipa hiyo picha….inakukumbusha mbali sana,
au sio, nitakurudishia picha yako, nikishamaliza kazi yake, usijali….’akasema
na kuichukua mikononi mwangu.
‘Kweli hujafa hujaumbika,…nashindwa kuamini, kuwa kumbukumbu
kama hizo zingenijia tena na kunifanya nimuwaze sana huyo binti,…cha ajabu hata
kipindi natafuta mke, kila ninayemuona nilikuwa nikilminganisha na yeye, lakini
sikumpata, na hata niliyempata, hakunipa kile nilichokuwa nizani ningelipata
toka kwa huyo binti….’ Nikasema huku nikiwa bado nipo mballi kimwazao.
‘Unajua …mawazo yangu na yake yalikuwa kitu kimoja, na
kilichobakia sasa ni kumbukumbu za barua tulizakuwa tukiandikanana…kumbukumbu
hizo bado zipo akilini,i….natamani sana nikutane naye tena..hata kama
yupoje….angalau nimuone tu…’nikasema na Yule mwanadada wakili akacheka na
kuondoka zake.
NB Najua wengi wana kumbkumbu kama hizi, sijui kwamba kuna
waliobahatika na kufanikiwa kuifikia ndoto zao za utotoni, ya kuwa walipendana toka utotoni
hadi kuoana, na sasa bado wanaishi kama mke na mume, wapo kweli…kama wapo mungu
awabariki sana….
Kisa kinakifikia ukingoni, sina uhakika lini, ...maswali yaliyobakia kichwani, ni je kwanini watu wanamkimbia huyu jamaa, je hiyo picha imefikaje kwa huyo mwanamama, kwanza huyo mwanamama ni nani...na aliipataje hiyo picha...kuna siri ndani yake,...nikamwangalia msimuliaji anipe jibu, akasema tusubiri sehemu ijayo.....
WAZO LA LEO: Kukosana kwa binadamu ni jambo la kawaida, ni
vyema ikitokea sintofahamu kati ya wanandoa, marafiki,majirani, ndugu, na kukatokea
kukwaruzana, kwa hapa na pale, jengeni tabia ya kusameheana.
Kama ni wanandoa Kaeni chini na kuyajadili hayo yalisababisha kukosana au
kukwaruzana….ili yasijirudie tena, . huenda yalitokea hivyo ili kuiimarisha
ndoa yenu, na hata hivyo tukumbuke kuwa sote ni binadamu hatutaweza kukamilika
kwa kila kitu, mkamilifu ni muumba pekee.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Hongera sana, ukituona hatuandiki chochote, sio kwamba hatufurahii kazi yako, wewe ni kiboko, na kama ukiwekwa kwenye mashindano ya KUTAFUTA mtunzi bora wa visa, riwaya na hadithi, utawaacha wengine mbali sana...HONGERA SANA
Post a Comment