‘Hapa ndio
sehemu ya kucheza karata yako ya maisha, ...’akaniambia mke wangu tukiwa
chumbani, baada ya wazee kuondoka, walipoondoka, nilijikuta mwili ukianza kuogopa,
ni kama vilekinga fulani imeondoka,na huji nini kitatokea baadaye. Wakati
nawasindikiza mjomba aliniambia;
‘Kama
ungelikuwa na akili ungelifuata ujumbe niliomuachia mkeo huyo uliye naye sasa,..lakini naona
bado upo gizani, samahani sana, nikisema kuwa mke ana walakini,...siku ile nipofika akaniona kama
ombaomba..akaniangalia kwa jicho la dharau kama hanijui, nikajua hapo hakuna
ubinadamu...jaribu kuwa mwangalifu...’akasema mjomba.
‘Lakini mjomba huyo sasa ni mke wangu nimeshamuoa....itabidi nijarabu kumuelimisha, najua
atabadilika tu, ..’nikasema.
‘Ni kweli,
hayo ni maswala ya mke na mume, lakini samaki hakunjiki akiwa mkavu...ulitakiwa
upanue masikio yako kabla,usikie nini zaidi, hasa kwa sie tuliowahi kuiona dunia, ulitakiwa uweke akili yako chini utafakari,
upime na uchanganue, faida na
hasara...wewe msomi hayo ulitakiwa kuyajua,...nini maana ya elimu yako... lakini hukutaka kuyafanyia kazi...sio biashara
zote zinauzika mjomba, sio vyote ving'aavyo ni dhahabu mjomba..’akasema mjomba.
‘Mjomba nimekueelwa, tatizo ni kuwa nimeshafulia nguo maji, sina budi niyaoge, nita-oa na na kuacha mpaka lini....kosa
lilishafanyika, sasa naona nijirudi kwa kukaa na mwenzangu atanielewa tu, yeye
ni binadamu....’nikasema huku nikiaangali nyuma, mke wangu alikuwa akijaribu
kuwa karibu na sisi kusikiliza tunayoongea.
‘Mimi sina
zaidi, ila fundisho, ukioa, usitazamie kuwa kila kitu unachotaka utakipata mara moja, sisi hadi
tunafikia uzeeni, yapo mambo mengi mpaka leo unatamani yawepo kutoka kwa mwezako, au unataka mwenzako ayafuate,
lakini bado, na bado hatujachoka kufundishana, ndoa ni nusu ya imani, ndoa ni
maisha yenu...jitahidini kuelekezana, msichoke, ...ila ndoa kama haina
kuaminiana,kuelewana, na kushauriana, na adabu na kuwajali wazazi, mtaishia kubaya.....’akasema mjomba
alipoona mke wangu anatusikiliza.
‘Nimekuelewa
mjomba, tutajitahidi sana...’nikasema.
‘Sawa, ila
ujumbe wangu ni muhimu sana, ....utakuja kuniambia siku yake...ni bora kizingiti kiwe imara hata kama hakivutii, lakini kitaimarisha nyumba, kuliko kizingizi cha mvuto,
.......kisicho imara...’akasema mjomba wakati waning akwenye gari.
‘Niliwapungia
mkono,na mamaalionekana hana raha kabisa, isigelikuwa uzee, angeliangusha
chozi...nilimtizama baba, yeye hakutaka hata kuniangalia....wakanondoka, na
kuniacha nikiwa kamabua lililokauka.
‘Mjomba wako bwana, ....yule mtu simuamini,
....hata ukimwangalia anakuwa kama anakuosma kwenye moyo wako, anakujua
ulivyo....namchukia, na akipita kweney anga zangu, sijuikama nitambakiza...yeye
ni kikwazo.., twende zetu nyumbani, kwani tuna mengi ya kuongea...mengi
sana....sasa ni mimi na wewe...’akasema mke wangu akinisihika mkono.
‘Sasa ni
muda wa kucheza karata yako ya mwsiho....’akasema mke wagu
‘Karata
yangu ya mwisho kivipi,...kwanza niambie maswala ya nyumba....’
Sikiliza wewe
mwanaume....sina muda wa mchezo, kila kitu kinajieleza kwenye ile katarasi
uliyoikuta hapa kitandani. Hapa tunangea jambo jingine muhimu sana, achana na
hilo kwanza. Nilipofika pale ofisini nilipowakuta na yule mama Mhindi,
niligundua kuwa anakutaka, ...hilo nina uhakika nalo...’akasema mke wangu.
‘Haya
mawazo yako bwana....,kwanza umeshanichanganya...sikuelewi unaongea
nini...’nikaanza kuwa mkali.
‘Ukali hausaidii
kitu, maana hutaweza kubadili maji kuwa maziwa,vinginevyo uchanganye na maziwa
ya unga...na hilo linahitaji vifaa, ..pesa..nikiwa na maana kuwa kwa sasa hivi
huna ujanja, huna pesa, ...utafanya nini...kila kitu nimeshakiweka sawa, nenda
kokote huwezi kitu....’akasema na kuniangalia kwa makini.
‘Tutaona,....
kama kweli ni haki yangu,tutaona...’nikasema huku nikiwa nimeinama chini.
‘Hahahahahaki
yako, ulijenga kwa mkopo au sio, uliwahi kulipa huko mkopo, hujalipa, umelipwa
na wengine, hiyo ni haki yako kweli...’ akawa anagusa kwa kidole kwenye sehemu
ya kichwa.
‘Wewe
mwanaume, kuhusu nyumba hiyo sahau,...nyuma hii ilitakiwa kupigwa
mnada,...hukuniambia, lakini mimi nilikuwa najau mapema,...jamaa wakaja hapa
wakakutia jambajamba...ukawakatia vijisenti, wakaondoka, mimi niwajua, na najua
hiyo...nikaenda ofisini kwako, wakawekwa sawa, na mambo safi...ukiwa na pesa
unaringa....’akasema huku akihesabu pesa alizokuwa nazo mkononi.
‘Mimi
nakuambia utaishia kubaya...ipo siku
....tupo...’nikasema kwa chuki na hasira...
‘Wameshasema
wengi,..ngoja nikufungue macho na masikio, haya hayakuanzia leo au jana, siku
unatoka huko Ulaya, tulishaanza kukusoma, mimi nakujau toka huko kijijini,
najua uzaifu wako...ulipomuoa Bintii Yatima, tukasema tumekukosa, ....lakini
mwenyewe ukajileta, kilaini ..'akasema huku akicheka.
'Mimi nilishasema tumekukosa, ila wenzangu wataalamu wakasema vuta subira, ..kosa limeanzia pale pale wanapokosea wenzako, kutokuijua misingi ya ndoa yenu, kosa,.... uzaifu wako kosa...na kosa hilo ni kwa wanaume wengi....unaoa unalemaa, huku natamba mimi nimeoa, au nimeolewa...hata wanawake,
wanaona wameolewa basi tena...' akaongea huku katizama pembeni, mimi nilikuwa namsikiliza huku hasira zikinipanda.
'Hilo ni kosa kwa wanandoawengi, .ukioa au kuolewa iwe ni mwanzo wakuijenga ndoa,...iwe
kama nyumba, kila mara inahitaji uangalizi, ....vingenavyo litakuwa hema
tu...sisi ndio makazi yenu kwenye hayo mahema, ...hayo tulishayajua...ndipo hapo tukaona kuna mwanya wa kufanyia vitu vyetu,...ndani ya mahema, ... sasa tupo kazini....ukishituka tushamaliza..’akasema na kunisogelea
akijaribu kunikumbatia, nikamsukumia mbali na kusogea pembeni mbali na yaye, yeye akacheka na kuniangalia, halafu akasgeuka upande mwingine na kusema;
‘Usinichukie,mpenzi..eeh,...hata
hivyo, kazi na dawa, usijli ,maneno ya watu, kama maneno yangelikuwa yanaua
mara moja, ningelishakufa siku nyingi..lakini bado muda wangu, najua ipo siku
zamu yangu itafika , lakini sio kama utakavyo wewe....hapa tulipo, kuanzia sasa
tunaonekana ,....jitahidi kuwa mwangalifu....’ akaonyesha kidude fulani kipo
juu...hakikuwepo kabla, akasema;
‘Hicho ni
moja ya vitu vya ulinzi, badoo vipo vingine visivyoonekana....hii sio kazi
ndogo, wenzako wamejiimarisha kimataifa...hii nyumba sio yako tena, na mimi
ni...wapo wenyewe...ipo siku utakutana nao...’akacheka na kunitizama machoni.
‘Usipoteze
pumzi yako, na uhai wako kabla ya wakati, ...kuanzia sasa mimi ni bosi wako,
utafanya lile ninalotaka ufanye....vinginevyo nitakufukuza kama mbwa...na
hutachukua siku mbili utakutwa kwenye mtaro...ipo mijibwa ikiamrishwa,
itakufanyia kitu mbaya...hutatamaani tena kuishi kwenye dunia hii...’akasema huku
akiniangalia kwa uso ambao sijawahi kuuona kabla.
‘Usinitishe
kabisa..mimi mtoto wamjini, tutapambana humuhumu...utaona ...’nikajipa
matumaini
‘ Sawa, ila
nisikiliza kwa makini, yule mama Muhindi
anaoekana anakutaka na mimi, na cha ajabu mumewe naye toka siku nyingi
ananisololea mimi, lakini namtolea nje, kiama chake kishafika ....kwetu sisi
yote ni sawa, tunawahitaji sana watu wa namna hiyo...sisi ni mshetani....kazi
yetu ni kusubiri, ukijileta tunakufanya ile unayaotaka...’akasema huku
anaonyesha meno nje, kama wafanyavyo mashetani.
‘Hivi
wewe...unafikiri utaishi dunia hii milele...’nikasema huku nikimshangaa.
Nikainuka palekitandani ni kukaa mbali na yeye,na yeye hakujali akagukia upande
mwingine, huku akiwa kashikwa kichwa kama kukiegemezana mkono huku akiwa
hanitizami, na mimi namwangalia kama mtu ambaye sijawahi kumuona kabla...
‘Muda huo
huo mfupi, tunautumia....sasa nisikilize kwa makini, hapa ni mjini, ukizubaa
utakufa njaa, ...wewe upo na mimi, kama pete na kidole, utalijua hilo baadaye
kwanini nasema hivyo....kwasasa kila mtu anajua wewe ni mume wangu....lakini kuanzia
sasa kisiri....unanielewa kisiri...’akawa kama ananing’oneza masikioni.
‘Mimi ni
bosi wako....utafanya kama nitakavyokuagiza...’maneno hayo yalikuwa yakijirudia
kichwani mwangu wakati wote, utafikiri aliyagandisha kwenye ubongo wangu, na
hata pale nilipokuwa nikimsubiri mama wa bosi ambaye alishaniambia nifike kwake
kwani kuna kazi natakiwa kufanya, maneno hayo yalikuwa yakijirudi akichwai
kwangu mara kwa mara....`mimi ni bosi
wako.....’
*********
Siku hiyo
niliamuka mapema sana,na cha ajabu nilipoamuka sikumuoma mke wangu, wala sijui
aliamka saa ngapi na wala sikujua wapi amekwenda. Hata hivyo jana aliniambia
kuwa yeye atakuwa anafanya mambo yake kivyake na nisiwe namuuliza kwanini labda
kama ni mambo ya kawaida ya ndani.
‘Ujue sisi
ni mke na mume, hilo litabakia hivyo usoni mwa watu...lakini mengine ni siri
yetu...’aliniambia.
Kuanzia pale na nikaanza kumchukia, na hasa
aliponionyesha ile sura ya ukatili...nilimuona kama shetani fulani, na kama
ningelipata silaha kwa muda ule,nisingesita kuitumia. Basi sikujali nikaamuka
na kujiandaa kwenda kibaruani, nikijua sasa ninalo, na cha muhimu
nikutokuogopa, maana nikiazna kumuogopa huyu mtu atanifanya mtumwa wake. Lazima
nipambane naye hadinione mwisho wake...nikaahidi hivyo.
Nilipofika
kazini, nikasubiri maana sikuwa mzoefu wa eneo hilo, ingawaje nilishwahi kufika
mara kwa mara tukiwa tumetumwa kuchukua bidhaa hapo dukani. Nikasubiri hadi
bosi alipofika, na alipofika tu akaniita ofisi kwake,...nikamfuata huko ndani
ya ofisi.
Kichwani nilikuwa
nimevaa kofia pana, ambayo nilipewa namkewangu, niliambiwa niingia ndani ya
hiyo ofisi, niivue ile kofia niiweke sehemu ya juu,, kama ni kabati au sehemu
yoyote iwe ya juu, na chombo kama cha kuskilizia mzika nitakuwa nacho, hataweza
kujua ni chombo maalumu, kumbe hicho kiliunganishwa moja kwa moja kwenye simu
yangu.
Nikakumbuka
kwanini mke wangu aliniazima simu muda faulani nyuma, na tangu siku ile kila
kinachotendeka nyumbani anakijua, kumbe.....hapo sasa akili ikaanza kutambua
kuwa huyu mke sio kamaninavymjua mimi, ni jambazi sugu....hata nilipojaribu
uichunguza simu yangu sikuona kitu kipya, ilikuwa ileile, isipokuwa huo waya wa
kuskilizia mziki, ambao ni wa kawaida tu..
‘Na weye
unapenda kusikiliza miziki kama vijana....mimi wakati naongea nataka
unisikilize mimi tu..kwanza njoo huku ndani....’akasems yule mama wa Kihindi,
name nikamfuata kutoka kwenye ofisi na kuingia kwenye chumba cha
ndani,nikashangaa, kumbe huku ndani kuna chumba kidogo, ambacho kilikuwa na
sofa kubwa, ambalo unaweza kulikunjua na kuwa kitanda, kuna jokofu la kuhifadhi
avinywaji, kuna kabati la vitabu, na vifaa vya ndani kama chumba cha msela.
Nikakumbuka
siku moja jamaa yangu aliniambia kuwa
huko kwa bosi alipokuwa akifanyia kazi mwanzoni, kuna ofisi ya ndani kwa
ndani hapo ndipo alipokuwa akifanyia mazambi yake na akiandada waliokuwa
wakitaka pesa za harakaharaka...ni hadi mkewe alipokuja na yeye akahamishiwa
huku kiwandani...
‘Unaona
hii,...ofisi ndogo ya kumpumzikia, hii
ni kazi ya mume wangu,...nimeijua mengi alikuwa kifanya humu, .sasa
nataka nifanyie na yeye kama alivyofanyia mimi....wajua nataka nini weye...kwanza
penda umbile oko...?’akasema huku akianza kunishika shika....
‘Bosi vipi.
hapana..mbona..aah, ...ooh, hujui mume
wako akinishika hapa...itakuwa taabu ....’nikaanza kulalamika, na yeye akasema
mume wake hawezi kuja hapo mpaka kuwa na mawasilino kuwa anakuja,.....
‘Akikushika
shika ujifanye kama hutaki-wataka, lakini hakikisha lengo lake linafikia sehemu
ambayo inathibitisha kuwa mnafanya tendo...unanielewa ....hili nataka
lifanyike, jinsi ninavyokuelekeza ...vinginevyo bwana hatutaelewana, nitakutupa
barabarani uchi, ....huna nyumba hapa, huna pesa....unataka ukalale
vichochoroni, kama hutaki hilo fanya lile nitakalokuambia ufanye...’ nikawa
nayakumbuka maneno ya mke wangu Kimwana.
‘Weye una
umbo zuri, hebu toa shati yako..taka ona kifua yako....’akaamurisha huyo mama,
nami nikajifanya kukataa, akanijia na kuanza kunito akwa nguvu, ...na baaaye
akasema nivue suruali...ooh, hapo nikaona imezidi mpaka, na nilipokataa
akanijia na kunivua kwa nguvu....mwisho nilibakia
kamanilivyozaliwa...nilijisikia vibaya....
‘Sasa kweli
una umbo safi weye, kuja hapa sasa,....vua na mimi hii nguo....’akaamurisha,
nami nikawa nafanya kama anavyotaka yeye, akili pale ishachanaganyikiwa, damu
inanichemka, kilichofuata hapo tena
sikuweza hata kuhadithia, ilikuwa ni sikio la kufa hakisikii dawa, kwani
sikuweza kuvumilia , kama ujuavyo damu yangu inachemak kweli...na nilishituka nikiwa
nimeshavuka mpaka wa makubaliano na mke wangu, alivyotaka;
‘Hakikisha
hamfanyi tendo lenyewe,ikifia hatua hiyo ya tendo mtolee nje,... ili akuhitaji
tena na tena....unanielewa,... ole wako uvunje masharti, najua tamaa yako
ilivyo, itawale kwa hilo, ukitawaliwa na
tamaa zako hapo utajuata....unisikilize kwa makini, kwani zaidi ya hapo tamaa yako
itakutokea puani mwenyewe...’nilikumbuka alivyosema mke wangu.
‘Oh, mungu
wangu nimefanya nini tena....ume....oh’nikajikuta nikilalamika.
‘Usijali
mimi nitakupa pesa mingi,na nitakufungulia duka lako menyewe,kwahiyo utakuwa
uankuja kufanya kazi hapa kwangu kila siku...napenda weye sana...’akasema huyo
mama, na baadaye nikaonyeshwa akzi ya kufanya,lakini akili yangu haikuwa hapo,
nilikuwa natafuta njia ya kuharibu ile simu,maana najua mambo yote yamerokodiwa
hapo.
‘Kama
maliza kuja huku...’nikasikiasauti ya bosi wangu ikiamrisha.
‘Sawa
Bosi...’nikasema huku nikikurupuka na kumfuata huko ndani na huko nilionyeshwa
kazi nyingine ya kupanga maboksi ya bidhaa mpya zilizofika , kuzitoa kwenye
maboksi yake na kuyaweka kwenye maboksi mengine,ili yaonekane ni kutoka Ulaya...nchi hii bwana ...ukiuziwa kitu
unaambiwa hii mali toka Ulaya, kumbe imetoka huko wapi sijui....mjini hapa, ...bongo
ya wenyewe.
Ilipofika
saa sita nilikuwa hoi, maana hapa kazi haina makadrio , ni kufanya tu, mara
hiki mra kile...na baadaye ikafika muda wa mchana,...nikajua hapa bosi ataagiza
msosi wa maana,...na kweli akaja pale nilipokuwa napanga panga maboksi,kwanza
akaniangalia kwa makini, halafu akanituma nikamnununulie chakula kwenye hoteli
ya jirani...nilijua na mimi nitanunuliwa chakula change, lakini haikuwa hivyo.
Nikasema
haina shida, ....nikakimbili hiyo sehemu niliyoagizwa kuwa ndipo anaponunulia
chakula chake, nilipofika hapo nikakutana na msichana mmoja namfahamu
tukasalimiana naye kidogo akaniuliza nafanyia wapi kazi nikamwambia, alishangaa
kidogo, kwani hakutegemea kuwa nitakuwa huko na baadaye akaniuliza;
‘Hivi
nasikia umemuoa yule binti Kimwana....?’
‘Ndio mbona
siku nyingi tu...’nikasema.
‘Haya wee,....unajua
niliskia kuwa Kimwana anaolewa,, nikasema kama nikimjua huyo mume anayetaka
kumuoa nitamtonya.... maana ningelijua mapema kuwa ni wewe ningekushauri
vinginevyo, uachane naye....lakini ndio hivyo ukipenda kitu sio rahisi
kushauriwa....’akasema.
‘Kwani ana
nini kikubwa...?’ nikauliza kwa mshaka.
‘Hata
nikikuambia sasa hivi utaamini, mtu umeshalamba asali na kuiona utamu wake,
wewe jichunge tu, ...maana unaweza ukaingizwa mkenge....huyo ni mtaalamu wa
kitu kinachoitwa `mlungula’ au kwa lugha ya wenzetu wanaita `blackmaili ‘
akasema na kunifanya nitake kuangusha kile chakula nlichonunua.
‘Hapana sio
kwasasa, ...labda kama ilikuwa hivyo ni zamani, ulishakutana naye siku hizi za
karibuni, mbona katulia, kaamua kubadilika kabisa baada ya kuolewa...hayo mambo
ni ujana, baadaye unajuata unaamua kujituliza...nina imani tabia hiyo
keshaisahau...’nikamwambia.
‘Ndio maana
nasema kwa hivi sasa hakuna kitu utasikiliza,... ila ninachoweza kukuambia ni
kuwa wewe sio mume wake wa kwanza, wenzako walisema hivyo hivyo, sasa wanajuta
na wengine hawapo duniani,...nisikutishe sana, ila nakushauri sana uwe
mwangalifu...’akaniambia.
‘Ahsante
ngoja nimpelekee huyu bosi chakula chake...’nikasema.
‘Bosi wako
ndio huyo mke wa bosi ambapo mkeo anafanyia kazi,...au sio?’ akauliza
‘Ndio ...nani
kakuambia hyo,....’ kablahajanijibu nikamwambia `...baadaye basi...’nikasema nikaharakisha
kurudi kule kazini, kwani niliona nimetumia muda kidogo kuongea na huyo binti,
na mimi nsingelipedna kuonekaan mzembe wa muda. Na wakati natembea kwa haraka,
akili yangu ilikuwa ikinituma niiharibu ile simu.
Nilipofika hapo
dukani nikampa chakula chake na akakigawa mafungu mawili, na kunipa sehemu
mojawapo, nikashangaa kwanini asingelenininunulia chakula changu mwenyewe,
ananunua chakula cha mtu mmoja halafu anakigawa mara mbili, huo ubahili wa hali ya juu sana...nikamwangalia
machoni
`Kula hiyo
chakula,...kula sasa hivi...’ kwasabbu nilikuwa na njaa nikaanza kukila kwa
pupa tu, nay eye akatabasamu na kuchukua chakula chake na kundoka.
Nikala kile chakula,....na baadaye akaniita tena kule
kwenye kile chumba, safari hii sikukubali kirahisi, nikawa nasita kwenda, lakini
baadaye nkawaza nakusema bora niitikie wito kwanza, ...mengine nitajua hukohuko
ndani, maana ndio bosi tena....., ikabidi nimfuate huko ndani, tulipofika
nikakuta anaanza mambo ni yale yale, safari hii sikukubali,....nilifanya kama
nilivyoagizwa na mkewe wangu,...siju kamaitasaidia....
‘Sikia mimi
nataka ufanye ninavyotaka mimi, ...kama unaleta jeuri nitafukuza kazi weye......nasema
nitakupa pesa mingi na kukufungulia duka...sikia eeh, ...fanya hii siri....’akasema
na mara simu yake ikaita, akapokea na kuanza kuongea na mume wake. Waliongea
kwa muda, na ilionyesha kuwa mume wake alikuwa akidai pesa nyingi ambazo mkewe
hakupenda zitolewe. Mimi najua jua Kihindi....nilikipatapata kidogo.
‘Lazima
uniambie zakazi gani,pesa yote hiyo ya nini....?’akauliza mkewe
Baadaye
wakawa wanakuja wageni, na lile zoezi likakwama had muda wakuondoka ukafika, na
hapo nikshukuru mungu. Nilipotoka hapo nikafika hotelini,maana nilipewa hela
nyingi kidogo, nikaagiza chakula, na wakati nakula mara mtu mmoja akanishiak
begani.
‘Nani
wewe....?’nikauliza nakugeuka nyuma kwa hasira, nikiwazia vibaka wa Dar, ambao
wanaiba kwa mtindo huo, uitwaoo `mdudu’ ukishikwa bega ukigeuka, wanakuchomolea
pesa iliyopo mfuko wa shati....
‘Tulia..wewe..
hata mkono wa mkeo huukumbuki, naomba hii simu yako....mara moja’ akasema na kuichukua
haraka, kwani kwa muda huo simu yangu ambayo ilikuwa pale juu ya meza,
nilishaanza kuifungua, nikiwa na malengo ya kuiharibu, lakini bado nilikuwa nasita
maana simu yangu naipenda sana.
‘Simu yangu
ya nini bwana...’nikasema na kutaka kuichukua...
‘Sikiliza
...tulikubaliana nini....na mambo yote yapo humu, usiwe na shaka, kila kitu
niachie mimi, wewe huna tatizo lolote...ilimradi uwe umefanya kama nilivyokuagiza..nikuambie
kitu, kwanza mambo mengine yameshaanza, sasa hivi nasubiri kupokea pesa nyingi
kidogo, tatizo ya hizo pesa zina mikono mingi na sehemu kubwa inakwenda kwa...mama....’akasimama
hapo huku akitoa kitu fulani kwenye ile simu yangu.
‘Haya
chukua simu yako, na kesho nitaichukua tena kurudishia hicho kidude...ki...’akasema
na wakati huo alikuja muhudumu wa ile hoteli, yeye akanilipia chakula na
akashikana mkoo na yule mhudumu , na yule mhudumu akanondoka, ...sikujua
kwanini wameshikana mkono. Baadaye tukaondoka kurudi nyumbani huku kichwa
kikiniwanga.
‘Ukifuata
ninavyokuagiza , hutaamini, umasikini wote utausikia kwenye bomba, ila
ukivurunda, utaniona sura yangu iliyojificha, mimi nina sura mbili, ya kike na ya
kiume, hiyo ya kiume inaonekana mara moja tu, na anayeiona hataiona tena hadi
mwisho wa dunia...wanasema nina shetani dume, likitokea kuondoka kwake mpaka
linywe damu ya mtu,.....natumai unanielewa...’akasema.
‘Una maana
gani...usinitishe kabisa, kwanini mnataka kuniingiza kwenye majaribu ya
mlungula, hamjui hiyo nikinyume cha sheria na yule ni mke wa mtu, unafikiri
mimi ni jiti eeh, sina hisia ...wengine hisia zetu hazina subira, siwezi
kuvumilia kiasi hicho..’nikasema.
‘Sio
tatizo,....kama uliisaliti ndoa yako, utajuata...unajua hisia zako zisizo na
mpaka, zitakuponza, ...sawa, lakini tatizo ni kuwa hicho chombo kinaenda
kuangaliwa na mama na kundi la wataalamu, hivi utajisikiaje ukiwa unaangaliwa
na watu hawo, na wakati huo wewe ni mume wangu, na mimi natakiwa niwepo hapo,
....ndio maana sikutaka utende zaidi ya nilivyokuagiza...’akasema.
‘Mungu
wangu, hebu kilete hicho chombo,....usikipeleka....’nikasema
‘Umeshachelewa,
huyo dada aliyekuja kuchukua pesa ya chakula ulichokula ni mmoja wa wasichana wa
mama, na kazi yake ndio hiyo kupeleka hivyo vifurushi kwa mama....kama
ulivurunda huko shauri lako..ukiniabisha tutakuja kupambana wenyewe.....’akasema
na kunifanya nitamani dunia ipasuke nizame.
‘Naapa kuwa
nitawafanyia jambo ambalo hamtakuja kunisahau...’nikasema huku nikiwa na hasira
ambayo haijawahi kuniingia moyoni mwangu. Na hata tuulipoangaliana mimi na yeye
aligundua hilo, akaniangalia kwa macho makavu, halafu akageuka pembeni na
kusema;
‘Usiape,...maana
wapo walioapa kabla yako na kiapo chao hakikuwasaidia kitu na wengine kiapo
chao kiliwapeleka kuzimu, waliamua kujiua,....haisaidii kuapa, kinachotakiwa ni
matendo, fanya unaloona ni sahihi kwako, ...usichelewe, ukichelewa wenzako
wanawahi, utaapa haya umeapa, kipo wapi .... sisi mwisho wa siku tunajitwalia
mshiko, ...lengo letu linatimia, unavohaha hivyo ndio tunacheka,....’ na kweli
akacheka sana.
‘Unacheka,
unafikiri mimi hapa napendezewa na mambo hayo, unaniumiza sana,na sio siri
chuki niliyonayo kwako sijawahi kuipata kabla....’nikasema kwa hasira.
‘Natumai
umenielewa, usifikiri hata mimi napenda kukuumiza, hapana, lakini inabidi iwe
hivyo, kimaslahi na kiusalama wangu, ....ipo siku utajua kwanini, nikuambie
uwkeli, nimekutana na wanaume wengi, katika kazi hii, lakini wewe umekuwa wa
pekee katika moyo wangu,..hata hivyo moja ya masharti yetu, ni kazi kwanza,
mengine baadaye, kwahiyo...kama unataka uendelee kukaa na mimi ufuate
ninavyokuagiza, ukijifanya kichwa ngumu, ukakiuka, utakutana na mume
mwenzako,sura yangu ya pili....’akasema.
‘Sawa
tutaona...’nikasema huku nikishika kichwa na kuwakumbuka wazazi wangu,....na
sura ya mke wa kwanza ikanijia ikinitizama kwa masikitiko na ile kauli ya mjomba ikawa inasikika kwa mbali na neo lililosikika vyema ni `kizingiti '....
NB: Nawashukuru sana wale wote wanaosoma visa hivi, wengine wanaona labda ni hadithi za kubuni tu,lakini kama kweli uliwahi kujichanganya mitaani, vijijini ukaishi na watu, haya yanatokea sana....na hata mkichunguza ndani ya ndoazetu, matatizo haya yapo, tunajenga ndoa lakini hatuzijali, zinakuwa kama nyumba iliyohamwa, zinakuwa mahema....
Naomba ushirikiano wenu, kwa maoni na ushauri, na kama hamtojali, nipendekezeni kwa wingi kwenye blog ya:
WAZO LA LEO: Mambo yakutuzidi hasa wanandoa, tujaribu kuomba ushauri kwa wazee wenye busara, sio kwa kila mtu, ukumbuke mambo yandani ya ndoa ni siri za ndoa, huruhusiwi kuzisema kwa kila mtu, ukiwa mpayukaji wa mambo yako ya ndani ya ndoa, kwanza unavunja miiko ya ndoa, pili wasiokutakia mema watachuku mwanya huo kukuharibia, siri ya ndoa ni kwa wanandoa wenyewe.
Ni mimi:
emu-three
4 comments :
Jamani ,sijui nisemaje! Ila kwa sisi wenye imani Mungu yupo ,inatakiwa tusali sana ...huyu jamaa alifungwa kabisa !haambiliki wala haelewi !
Haya mambo yapo sana kwenye maisha yetu ya kila siku. Tuko pamoja M3 tutakupigia kura kwa wingi mpk Blog yetu ishinde kwa kishindo.
This is the perfect site for аnybody who wіsheѕ to
understаnԁ thiѕ tοpic. You reаlize a
whole lоt its almost tοugh to argue with you (not that I rеаlly would want to…HaHa).
You сertainly put a frеsh spin on a subject which has
beеn discussed for yеars. Eхcellent stuff,
just wondeгful!
mу blog post - angielski
What's up to every body, it's my first visit of this blog; this website consists of awesome and truly good material designed for visitors.
My website: very midsummer
Post a Comment