Siku hiyo
kabarua karibu kiote majani, maana nilifika kazini mapema, nikawajibik ipasavyo,
na kumaliza kazi zangu mapema kama kawaida yangu, nikaona kwa vile nimemaliza
kazi mapema, ngoja nikamuone huyu Muhindi anipe mshiko wangu,nikahangaike kwingine....
Nikafika
ofisini, huko mara nyingi sisi vibarua haturuhusiwi kufika labdakwa dharura au
kuja kulipwa posho yako , mimi sikujali, nikaenda tu, na bahati mbaya nikamkuta
mkewe, mwenyewe alikuwa katoka;
‘Weye mbona
hufanyi kazi....wakuja huku kufanyia nini..?’ akaniuliza huyo mke wa bosi
akiniangali akwa makini.
‘Nimemaliza
kazi yangu, nataka malipo na kama ipo nyingine naweza kufanya maana bado muda
upo, lakini ukimaliza kazi yako unalipwa kwanza, kabla ya kuanza kazi nyingine...’nikasema.
‘Unajua
kazi sana weye, nitakupelaka kwenye duka yangu...na weye nasikia ni mume wayule
dada mrembo....?’ akaniuliza.
‘Dada yupi,
maana wapo dada wengi..?’ nikadadisi.
‘Yule
anaitwa Kimwana....anakuwa pale mapokezi...?’ akauliza huku akisinisogelea.
‘Aaah, ndio
ni mke wangu...’nikasema.
‘Unaju
akuna jambo nataka kukwambia,....mkewako hana tabia nzuri....nimemfumamara
nyingi akiwa na mume wangu, sikujali sana...maana inatakiwa uwe na
ushahidi...nimepanga siku nikimfuma, nammaliza kabisa....atajua mimi ni baniani
au muhindi...’akasema huku akiniangalia machoni.
‘Mimi sijui
hayo....’nikajitetea,na mara akawa ananishika shika,....ooh, nikasema yale
yele....nikarudi nyuma na kumwangalia machoni , nikiwa na wasiwasi, na kabla
sijasema kitu akasema ;
‘Kamamkewako
ananiibia mume wangu na mimi nitamuibia mume wake, unasikia...utakuja kufanya
akzi kwangu,...’akanisogelea na kutaka kunishika, na mara mlangoukafunguliwa,
wakaingia mume wa huyo mwanamke namkewangu.
‘Wewe
unafnya nini huku ofisini,nilishawaambi mje huku kwa taarifa maalumu....’akasema
huyu bosi huku akituangalia kwa mashaka, na hata mke wangu naye alikuwa kaduwaa
pale mlangoni.
‘Huyu
nimemuita mimi, nataka anisaidie kazi kwangu, kule dukani, hapa keshamaliza mpe
helayake halafu tunakwenda kule dukani kwangu...’akasema mkewa wahuyo bosi.
‘Kazi bado,
ipo kazi mingi hapa ya kufanya, ...’akasema huyo bosi.
‘Kamaipo
kazi atafanya mtu mwingine, huyu namchukua mimi, umenisikia vyema, na huyo
dadamrembo anakuja kufanya nini huku ofisini...?’ akauliza huku akimwangalia
mke wangu.
‘Kuna kazi
nataka akaifanye....unajua wiki inayokuja itakuwa ya biashara, sasa lazima ajue
jinsi y akuwapokea wageni ...’akasema huku akitoa jarida kubwa lenye picha.
‘Simtaki
humu ....sitaki awe anaingia humu, unanisikia, ....weye mwanamke, sitaki uwe
unaingia humu ofisini, kama unataka kumpa kazi kampe huko mezani kwake,na nakuonye tena, kama siku nikiwakuta
tena na mume wangu....utajua mimi ni nani...’ akasemahuyo mama.
‘Mimi
nafuta maagizo, kaniita kama bosi wangu ningelifanyaje mama mimii sina nia mbaya...’akajitetea
mke wangu.
‘Ni hapo
nikiwafuma, sitajua kuwa ulikuwa an nia mbaya au nzuri, utakayeumia ni wewe...’akasemana
kunishika mkono tuondoke naye, nikasema sijalipwa hela yangu ....
‘Mpe hela
yake nataka kuondoka na huyu mtu...’akasema huyo mwanamama,na mumewe akafanya
haraka kunilipa pesayangu, na hapo ndipo nikajua kumbe yule mwanamkendiye
mweney mamlaka yote ya kazini hapo.
Bahati tulipotoka kukaja wageni wa huyo mama,
ikabidi zoezi hilo lisahaulike, na baadaye akaniambia niondoke tutaonana kesho,
basi nikarudi nyumbani mapema.
Nikiwa na
vijisenti vyangu, nikapitia gengeni kununua chochote na kila nilivyopiga
amehsabu helaikawa haitoshi, nikajiuliza hivi wanawake wanawezaje maana ukimpa
pesa, anaweza kununu akitu ambacho mimi nimeshindwa, nikaishia kanunua bamia na
nyanya kidogo ili siku ipite, nikazunguka huku na kule kutafuta kingine
chochote kwa bei ndogo lakini vitu vingi bei hazikamatiki,...
‘Kweli
maisha magumu, wakati nipo ofisini hali kama hii nilikuwa siioni, ukipita
sehemu kama hizi unanunua hata kuuliza bei,....leo kitu kidogo tu, nabishana na
hawa kina mama, ambao nao wanatafuta riziki yao, kweli maisha ni kupnda na
kushuka..’nikajikuta nikiongea mwenyewe kama mtu aliyechanganyikiwa.
Nilipofika
nyumbani niliwakuta wazee wamekaa nje,,kwakuwaanglia tu usoni, niligundua kuna
jamabo,..kwani mimi niliondoka mapema kabla ya mke wangu, kwahiyo inawezekana
kulikuwa na kutoelewana kati ya mke
wangu na wazazi wangu,moyoni nikasema, hivi hali hii itaisha lini, ina maana
mke wangu haoni kuwa hawa ni wazazi wetu, anatakiwa kuwatendea wema, kwanza
wamechoka wanastahili kupumzika, lakini sio kuwafanyisha kazi kama vijana.
‘Shikamooni
wazazi wangu, mbona mpo hivi, ....?’ nikauliza
‘Hilo sio
la kuuliza, ulipondoka hapa mlipanaga mtuseme ili tuondoke wenyewe....?’
akasema baba.
‘Mbona mimi
sielewi hilo baba, mimi nifanye hivyo nimechanganyikiwa au ....kwani kulitokea
nini huku nyuma?’ nikauliza.
‘Huoni tupo
nje, tumeambiwa mgeni siku zake ni tatu, sisi tumeshakaa zaidi ya mwezi, nab
ado hatufanyi kazi, kazi ni kusubirii kula tu...maneno mengi, sasa tukaona
ngoja tukusubiri hapa nje, ili tukuage, hatutakosa sehemu ya kukaa....’akasema
baba.
‘Hapaan
hapana twendeni ndani, hilomimi sikubali,kwanini awafanyie hivyo,kwani hapa ni
kwake, .....twendeni tukaongee ndani, na haondoki mtu hapa,kamanikuondoka
aondoke yeye...’nikasemakwa ukali.
‘Aondoke
yeye wakati kasema nyumba hii ni ya kwake, wewe upo upo tu,umeshindwa kulipia
deni, yeye keshalipia na hati miliki inayoonyesha umiliki wa nyumba katuonyesha....ina
jina lake na kila kitu chake....wewe umelala tu,ina maana hujui hilo...?’
akauliza baba.
‘Huyo
anatania tu,...eti hati miliki ina jina lake,mbona itakuwa maajabu...’ nikasema
huku moyo ukinienda mbio, maana kweli hatii miliki ya nyumba yangu haionekani
kabisa,....ina maana aliichukua yeye akaenda kuibadili, lakini kwa
vipi....haiwezekani.
‘Huyo
anatania tu, tulikuambia mwenzako yupo hapa kwa malengo, na inavyoonyesha lengo
lake ilikuwa hii nyumba,sio wewe,hebu jiulize kwanini akugande wewe, una nini
cha zaidi kuwashinda matajiri,kuwashinda wanaume wengi anaokutana nao....akili
yakoimeganda, hata kuwaza huwezi, unachowaza ni tama zako za kimwili,na huo ni
ugonjwa....’akasema mama.
‘Mama hivi
kweli mnaamini kuwa mimi na akili zangu nikubali kuiandikisha nyumba hii kwa
mke wangu, kwanini nifanye hivyo, wakati nipo hai, ....ndio ni kweli nyumba hii
ipo kama rehani,kwani walishakuja wapiga mnada kuinadi....na walinipa notisi ya
miezi ....mmh, ikawa imepita, lakini sikuwaona tena wakija, hili lilinitia
wasiwasi....’nikasema.
‘Basi labda
walikuja wakakutana na huyo mkeo akaongea nao, na huenda keshalipa hilo deni na
nyumba imechukuliwa na yeye...’akasema mama.
‘Haiwezekani
maana kila jambo linautaratibu wake, hati zote huko benki, huko halimashauri
zote zimeandikishwa kwa jina langu...naili zihamishwe kwenda kwa mtu mwingine
ni lazima mimi mwenyewe niwepo, ...itakuwa maajabu basi...’nikasemanakuingia chumbani.
Nilipoingia
tu nikakuta karatasi ipo kitandani, ilikuwa nakala ya hati miliki ya nyumba,
nikaichukua na kuisoma, kweli ilikuwa na jina la mke wangu, kuwa ndiye mmiliki
halali wa nyumba...nakulikuwa na kiambatishi cha wapiga mnada, kuonyesha wao
walipiga mnadahiyo nyumba baadaya mimi kushindwa kulipa deni na aliyweza
kushinda huo mnada na mke wangu ambaye alilipa pesa taslimu sawa na hilo deni
la nyumba....
‘Mungu
wangu......’mwili mzima mzima ukaisha nguvu
*******
Nikawa
naongea na wazazi wangu maana sikuwa na la kufanya, kama kweli mke wangu
kanunua hiyo nyumba sio mbaya, ni kama helakutoka mfuko huu kuingia mfuko wa
pili, nikajipa matumaini
‘Mwanangu
sisi tumeshindwa,...maana tulijua pamoja na hii shida ya njaa, tungeliweza
kukusaidia kuondokana na mnaso ulionaswa nao, lakini kila tulivyojaribu kukusaidia
tunaona hunasuki, ...iliyobakia tunamuachia mungu...’akasema mama.
‘Kwani
wazazi wangu vipi...?’ nikauliza nikiwa na wasiwasi, ..ndio najua kuwa wazazi
wangu hamuishi inavyotakiwa wazazi watendewe, lakini nina matumaini kuwa hali
hiyo itaisha tu, na hata hivyo hali yangu itakuwa njema tu, nitapaat kazi tu,
sizani kuwa nina mkosi wa kutopata kazi. Nilisema huku nikiwaangalia wazazi
wangu;
Wazazi
wangu afya zao zilishabadilika, sio kama walivyokuja, angalau sasa wanaonekana
akmawatu, jamani msiombee njaa, ....hali iwe vipi, lakini njaa haina muamala,
mwili unapukutika na kamaulikuwa kijana unakuwa mzeekablaya umri wako. Wazee
wangu walipokuja walikuwa wamechoka sana, nakuzeeka isivyo sawa na umri wao,
sasa wanaafadhali licha ya manyanyazo yaliyopo....
‘Mtoto
wetu, ndio tumetokea huko kijijini kwa kukimbia njaa, lakini kwa hali iliyopo
hapa imetushindwa,....sisi ni wazee, sisi ni wazazi wako, hatupo na umri sawa
na nyie tena hata nguvu zetu sio sawa na nyie, kwa umri huu tulitakiwa tukae
tufaidi matunda yenu...’akasema mama.
‘Na ndivyo
ninavyotaka mama iwe, najitahidi sana, tatizo ni kuwa sina kazi kazi
hazipatikani, lakini hiki kibarua ninachofanya kitatusaidia kidogo na kama
ikiwezekana nikipata pesa kidogo tu tunafungua genge,...na hata hivyo mwenzangu
naye anajitahidi, tunachotakiwa ni kumvumilia, kama mjuavyo kakulia mazingira
tofauti na sisi...’nikasema huku nikijitahidi kuficha machozi.
‘Najua
unavyojisikiamtoto wetu, lakini yote yanategemea wewe, tulikuwa na matumaini
kuwa utazindukana, utajua wapi ulipo, lakini kila tulivyojitahidi haikusaidia kitu
,mwenzako kakuzidi akili, hujijui na hujui wapi unapokwenda na tuna wasiwasi
siku ukizindukana utakuwa umechelewa...na hata hivyo umeshachelewa, angalia
alivyokufanyia....’akasema baba.
‘Kwa vipi
wazazi wangu, nyie ni wazazi wangu hamtakiwi kunitupa,...kama mnaona nipo katika
hatari kwanini hamuniambii, na ni hatari gani hiyo....kwasababu kama ni huyu
mwanamke , keshaamua kujirekebisha, na hatua liyofikia inatia matumaini,
....tuzidi kumsaidia ...kama ni nyumba, haina shida, kuinunua yeye ni kama
kunisaidia tu, isichukuliwe na mtu mwingine...’nikasema.
‘Je
alikuambai huo mpango, alikuhusisha, .....?’ akauliza mama
‘Hapana,
labda alipitiwa...au sijui hawa watu walifika lini hapa kupiga huo mnada..’nikasema
nikiwa na wasiwasi .
‘Ndio hapo
tunasema umezidiwa ujanja, maana hujijui, hasa inapofikia kwa huyo mwanamke wako....hatutaki
kukuharibia uhusiano wenu, lakini kila tukiangalia mbele kuna giza...sisi ni
wazazi wako, na kama ulivyosema siku ile, wewe sasa sio mtoto mdogo tena,
unajua nini unachokifanya, na kweli tunaona jinsi unavyoishi na mkeo,mnajua
nini mnachokifanya...’akasema baba na mama akadakia nakusema;
‘Sio kwamba
kazi za hapa ni ngumu, mbona ni kazi ndogo tu, za kawaida, hatuoni ajabu
kufanya kazi zote hizo, kwasababu tumezoea kazi, lakini heshima ni kitu muhimu
sana....mimi mama yako katika umri huu nisimamiwe kama mtoto mdogo....hapa
hujafagiai vyema, vyombo hukusafisha vyema, chakula hiki hujapika vyema....sio
kauli nzuri,lakini sio kosa lake....’akasema mama.
‘Mama hilo
nitawalinda hadi mwisho, nilishaongea na mwenzangu na amesema hatawafanyisha
kazi tena,...kama hataki nitajua nini cha kufanya maana hapa ni kwangu...’nikasemanikionyesha
kujiamini.
‘Hapa ni
kwako....ina maana hujaamini kuwa hapa sio kwako tena, wewe subiri,kama
hatakuja mwenzako mwingine mwenye sharubu kama wewe, ukaambiwa ishia, kama
alivyoambiwa mjomba wako,....aliambia haya chukua msaada huu na
ishia...hahaha,jamani kizazi hiki mbonamna vituko...’akasema mama.
‘Mama hii
ni nyumba yangu kamani haki yangu nitaipigania mapka hatu aya mwisho..mtaona
tu..’nikasema nikijipa moyo.
‘Hayo ni
maneno tu mtoto wetu, kauli yako inakushitaki, hata ulivyoitamka, umeitamka
kimashaka, tuna wasiwasi, kama ulivyosema nyumba hii uliijenga kwa mkopo,na hukuweza
kuulipia tena, ina maana katokea mtu kainunua,ili mkopo huo ulipwe, kwahiyo ni
mali yake, sio yako tena,....hapo huoni kuwa mwenzako ni mjanja kuliko
wewe.....tulishakuambi kuwa kuwepo kwake hapa ni kwa malengo ambayo mwisho wake
yatakuumiza...ndio hayooo’akasema mama.
‘Hapana
mama,haniwezi mimi...hilo lisiwatie shaka...huyo namjulia mimi,...haiwezekani,
nitaongea naye na nitaona nini lakufanya...’nikasema huku nikiwaza akilini kuwa
je hiyo itawezekana vipi wakti sina pesa, sina kazi, asilimi kubwa tunamtegemea
mke wangu.
‘Tutafutie
nauli, kesho au keshokutwa tunaondoka, tumeshawasiliana na mjomba wako, na yeye
yupo mbioni kurudi kijijini, tuna mpango wa wazee ambao keshaufanyia kazi,
hatutakufa njaa, na tunakushauri kwa ahtu ailiyofikia ni bora tukaondoka pamoja
kabla hujaumbuiwa, ....kama upo tayari tuondoke pamoja,...tuondoke kabla mambo hayajawa mabaya zaidi...’akasema baba.
‘Baba na
mama naona nyie mumeshapanga iwe hivyo, na kama mumewasiliana na mjomba siwezi
kuwazuia, lakini lengo langu nilitaka tukae pamoja mpaka hapo mambo
yatakapokuwa mazuri,...na naona sio jambo jema kwa nyie kuondoka haraka hivi,
.....Basi ngoja akija mwenzangu tutaongea naye tuone jinsi gani tutafanya, ili
hata mkirudi nyumbani mpate nini cha kuanzia...’nikasema.
‘Tunaomba
kama inawezekana, usimuhusishe huyo mwenzako kuhusu sisi, kama hutaweza kuipata
hiyo nauli, usisumbuke, sisi tutajua jinsi gani ya kuondoka, ...ila tulitaka
kukuambia yale yaliyopo moyoni mwetu, kama alivyosema mjomba wako, nyumba hii ....haina
kizingiti imara,....utakuja kujua baadaye, lakini yote ni wewe mwenyewe, hatutaki
kukulazimisha...hatutaki kuingilia maihs yako....wembe ulioulilia unaanza
kukukata...’akasema baba.
‘Usimwambie
mtoto hivyo, tunatakiwa tumshauri tuondoke naye, mabona tutakuwa tukiishi huko
kijijini kwa mashaka, kwa hali kama hii , ...hapana tundoke na mtoto wetu..’mama
akawa anamwambia baba kwa sauti ndogo
‘Msijali
wazazi wangu, kuhsu mimi, nimeshajifunza sana, ..naona sasa nitulie, na
nimeamua huyu mke nitajitahidi tuishi naye na hatua kwa hatua atabadilika
tu,...msiwe na mashaka kabisa na mimi...’nikasema.
‘Haya kama
ndivyo ulivyoamua sawa, wewe ni mtu mzima, ila ukishindwa maisha karibu sana
kijijini, tunataka maendeleo kutoka kwako, maisha ya mjini yana raha zake
lakini yana gharama zake,...ili uishi mjini kwa raha unatakiwa uwe na pesa,
kwasababu hakuna shamba....shamba la huku ni uwe na kazi, na kazi za hapa ni za
kuajiriwa, uwe mtumwa wa matajiri....vinginevyo unatakiwa uwe na biashara ya
maana , lakini hayo maisha ni yakwenu, sisi hatuyawezi....’akasema baba.
‘Ni kweli
haya ni maisha ya kwetu, nyie maisha yenu ni kijijini...wanakijiji mpo katika
kikao cha kijiji...safi sana, na hilo ni jambo jema kabisa....’sauti ikatokea
malngoni, Kimwana alikuwa kasimama huku kasika kiuno, akatizama huku na kule
akakunja uso, na akawaangalia wazazi halafu akasema;
‘Shikamooni
wazazi, ila kabla ya hiyo marahaba yenu, nakumbuka nilisema leo nitakuja na
wageni, sasa kama ningelikuja nao siingelikuwa ni aibu tupu, nje kuchafu, ndani
ndio usiombe...jamani mnataka nifanye kazi ngapi, niwalishe na bado hata vikazi
hivii vidogo nije nifanye mimi, ....haya nitafagia mwenyewe, haina shida, maana
nikisema hivyo naambiwa sina adabu...na sina shida ....’akasema na kuchuku
ufagio.
‘Usiwe na
wasiwasi binti, tunatarajia kuondoka karibuni, ...kesho tutaondoka tu...’akasema
mama.
‘Mnanishangaza,
muondoke, muache kuishi na mtoto wenu, yupo mjini,...hahahaha, maana mkiwa
kijijini mnatamba, tuna mtoto ana kazi, ana nyumba mjini...mumeiona kazi
yake...ndiyo hiyo,...nyumba sijui .... kwahiyo ni vyema mkasema ukweli, mkajua
ukweli kuwa yale ya zamani kuwa ukoo huu ni bora, familia hii ni bora, haupo
tena, yoyote anaweza kuwa bora....’akasema huku akimalizia kufagia.
‘Ubora wako
ni wa pesa za msimu, ambazo hazina uhalali, sio sawa na ubora unaojulikana huko
kijijini, ndio maana tunataka kuondoa hapa haraka, .....tusije tukajikuta
tunakula vile visivyoliwa na mwisho wa siku miili yetu itajaa sumu ya dhuluma...’akasema
baba.
‘Hahaha,
kama ni hivyo mbona mumeshakula...hamuoni mlivyobadilika...haya hiyo ndio
shukurani ya punda, nilijua tu, hata nijipendekeze vipi siwezi kuwatimiliza,
mimi mumeshaniweka kwenye kundi baya, lakini sijali, .....unafikiri,.... mimi
nina maisha na mtndo wangu, siyumbishwi na hisia za watu,ilimradi sili kwao...kuna
mtu nimekula chake hapa, hakuna...huyu mwanaume, sana sana namlisha mimi, asema
ukweli....’akasema huku akinigeukia mimi akaniangalia kwa macho tofauti na siku
nyingine.
‘Tusianza
kuchafuana....’nikajikuta nikisema.
‘Samahani
....samahani bwana mkubwa...’akasemana kucheka,halafu akawageukia wazazi wangu
na kuuliza;
‘Haya
mnataka kuondoka,nauli mnayo...mtaondokaje hapa,na huko kijijini mtaenda kusihi
vipi, maana huko ni njaa ya kufa mtu...nimewasilina na watu huko wanasema
wanaishi kwa msaada wa serikali,...’akasema huku akiwaangalia wazazi kwa makini.
‘Hilo
tumeshaongea na mumeo...’akasema baba.
‘Mumeo..leondio
nasikia hiyo kauli mumeo,siku zote mwanamke wako,....sio mke wako...leo mnaanza
kunitambua hahaha..haya yangu macho, ...’akasema halafu akanigeukia na kuniangalia kwa dharau;
‘Sawa labda
ana nauli, ya kuwapa....haya ngoja mimi nikajipumzishe kidogo....maana hakuna
kupumua hapa, huko kazini nako mambo
taabu tupu huyo Muhindi ananifanya kama kinyago chake cha bishara zake,
unarudi nyumbani badala ya kutulizwa kwa maneno matamu ya faraja, unakatishwa tamaa
na watu wasiotosheka....’akasonya na kupitiliza kuingia chumbani,na kabla
hajaingia chumbani akasema;
‘Ama kweli
kutegemewa ni mzigo mzito sana..na kila unavyojaribu kuweka mambo yawe sawa,
wengine wanaona wanaonewa...lakini tutafika tu...haya na wewe mwanaume, ukimalizana
na wazee wako njoo tuongee ndani...’akasema mke wangu maana siku hizi neno
mpenzi limeshafutika mdomoni, sasa naitwa wewe mwanaume.
‘Sawa
nakuja, nisubiri nimalizane na wazazi wangu...’nikasema huku moyoni nimejawa na
mawimbi, nikaiangalia nyumba kwa juu na kuangalai kona zote za nyumba,
nikasikitika, na nilipogeuza macho kuwaangalia wazazi wangu macho yakafunikwa
na machozi.
‘Mtu mzima
akilia kuna jambo...mjomba unalia mapemahivyo, bado...usideke kwa wazazi wewe ni mwanaume, angalia sana kizingizti cha nyumba yako....’ilikuwa sauti ya mjomba akiwa mlangoni.
'Una maana gani mjomba...?'nikauliza na mara mlango wa chumbani ukafunguliwa mke wangu alikuwa kasimama pale mlangonii huku kashika kiuno...
Je ni nini
kitaendelea...mambo ya kifamilia hayo....mnasemaje wenzangu?
WAZO
LA LEO: Mazoea yakijijenga hugeuka kuwa
ni tabia, ama iwe tabia njema au tabia mbaya, ni vyema ukapima matendo yako kwa
kuangalia faida na hasara za matendo yako. Na hasa mkiwa wawili mke na mume, ni
vyema, mkajaribu kuangaliana matendo yenu, kama hayaendi sawa, shaurianeni
mapema,kwani mkiachia tabia ikajijenga, mtashindwa kuelewana baadaye.
Ni mimi:
emu-three
5 comments :
Dah ! Nasoma naona kama ni hadithi za kufikirika,ila haya mambo yapo! Binadamu tuna mambo .....
Elisa inabidi nikukutanishe na huyo jamaa, ili uhakiki mwenyewe. Kuna mataizo mengi watu tunakutana nayo,ukiamua kuyaweka vizuri unaweza usiamini, ..hasa kama hujakutana na matatizo kama hayo.
Mimi aliponihadithia kuwa alikutana na mama wa Kihindi akamlazimsiha, nikaona hiyo ni ongeza chumvi, lakini baadaye nilikutana na jamaa ambaye anakijua hicho kisa vyema, akanithibitishia, hapo ndipo nikaamini kuwa ....duh, ni rangi tu, ndani sote tupo sawa.
Kwenye kitengo chako huna mpinzani, lbda watoe kura kwa kujuana, lakini kifani your best writer!
haya mambo yapo swali ivi huyu kaka ana elimu mpaka ulaya amefika alikuwa haelewe kama kuna kitu sio kawaida kwenye life yake au ndo kazidiwa maana yapo haya kuzidiwa na wajanja wa mjini
m3 big up dear uko juuuuu sana songa mbele
haki ya Mungu ni kama vile hadithi ...kweli UBINADAMU KAZI..
Post a Comment