‘Kimwana
namba moja, nimekuita hapa kwa jambo moja kubwa ambalo nahisi wewe peke yake ndiye unaliweza, wenzako wanaweza wakaogopa...najua ulishaniambia kuwa
wewe umeamua kubadilika,na hata umeolewa..safi kabisa maana najua huyo mume
ataishi maisha ambayo ilitakiwa wake wawe hivyo....’akasema Mama D, kama
wanavyomuita, wengine humuita Docta tu.
‘Mimi
nilipenda kusikia nini huyo mume wako angesema baada ya kukutana na mtu kama
wewe...najua kuwa kuna taarifa za kuwazalilisha kuwa mnajiuza na vitu kaam
hivyo, lakini hiyo ni kawaida na ni chamgamoto kwenu....na hili nilijua
litatokea ,lakini ndio gharama za hii kazi...’akatulia na kuangalia nje.
'Hiyo kwangu ilikuwa hatua ya kwanza, maana nilikuwa na malengo, kuwa ikifika hapa, kukitokea hiki nichukuea hatua gani...sasa hatua inayofuata inahitaji ujasiri na...
Na mara
akaingia dada mmoja ambaye ni mmoja wa walinzi akamnong’oneza Docta na docta
akatoa macho kuonyesha kuwa alichoambiwa ni jambo la kutisha kidogo,
akawaeukai mabinti aliowaita na kusema kwa sauti ya haraka;
‘Kuna jambo
limetokea....juzi, na hili sikutegemea kuwa litawahusu nyie naona kumbe kuna
miongoni mwenu wamehusika na hilo...nilishawaonya kuhusu mambo hayo,kuwa katika
kazi yetu hatutaki kutumia nguvu,...hauhitaji silaha, sisi wenyewe ni silaha, kama ukitumia akili...na mambo kama haya yanavuruga mpangilio wangu. Nakumbuka ndio
niliwafundisha ujasiri, na jinsi gani ya kujihami, lakini sio kutumia
silaha...sasa naona miongoni mwenu kuna mmoja kajihusisha na
ujambazi....’akasema na wale mabinti wakaguna.
‘Ndio huo
ni ujambazi, kama mlitumia silaha, kumtisha yule Mhindi ili atoe pesa, na
kumjeruhi mlinzi, ina maana gani, huo ni ujambazi, na wahusika wameshabainika,na kibaya zaidi wananihusisha na mimi, eti wakisema mabinti zangu...hilo
halipo, maana mimi sina mabinti....nyie ni watu walioamua kukodi majengo yangu
kwa kazi zenu ambazo mimi sizijui...’akasema na kuangalia nje.
‘Hilo ndilo
nataka wote mliweke akilini na mseme hivyo....vinginevyo, mimi sitahusika na
yoyote yule atakayewekwa ndani kwa uzembe wake....mimi niliwafudisha kuwa mkono
wa mwanamke muda wote ni laini...kivutio...au sio, sio mkavu wa kutisha, kumbe
wengine hawakunielewa na hilo somo...sasa ..ooh, ngoja nikaongee na hawo
maaskari kwanza nisubirini hapa...’akasemana kutoka.
‘Ina maana
ndilo alilotuitia huyu mama au kuna jingine...?’ akauliza mmoja wa wasichana.
‘Lipo
jingine lakini hili la polisi naona limeharibu utaratibu ...’akasema msichana ambaye yupo
karibu sana na huyo mwanamama.
‘Lipi hilo..?’
wakauliza wengine.
‘Atawaambia
mwenyewe...mimi siruhusiwi kuongea jambo ambalo sijaambiwa niseme...
Mara
Kimwana akakumbuka jambo, na haraka akainuka pale alipokuwa kakaa na kusema
anataka kuondoka kuna jambo muhimu analifuatilia huko kwake..
‘Huwezi
kuondoka ..subiri mpaka mama arudi...’akasema mmoja wa walinzi.
‘Hapana
kuna jambo muhimu sana, akija mama mwambieni nina zarura...’akasema na kuondoka
haraka.
********
Nikiwa
njiani huku nikiwaza nilichokifanya, nikakaribia nyumbani,....akilini nilikuwa sijaamini nilichokiona mlendani,..nakilanililowaza, sikuweza kupata picha. Nilipoufikia mti wenye kivuli nikajipumzisha
kidogo, maana jua lilikuwa likichoma hadi mfukoni,
....nikaangalia kule nyumbani kwangu,na mara nyingi nikiingalia nyumba yangu kwa
mbali, moyo unaniuma sana, nikijua kuwa siku yoyote itakuwa sio yangu tena.
‘Hivi
kunaweza kukatokea miujiza gani nikalilipa hiloo deni...sijui, hata nikipata kazi
leo, sio rahisi benki kukubali kunivumilia tena, na nikawa nalipa kidogokidogo...namuomba
mungu hawa wapiga mnada waendelee kusahahu sahau....’nikajikuta nikiongea peke
yangu.
Mara macho
yangu yakagundua gari ambaloo halikuwa mbali sana na pale nyumbani lilikuwa hatua chache kutoka nyumbani kwangu, lakini kwa muonekano lilikuwa ni gari la polisi, hapo mwili ulisisimuka,
utafikiri nimefanya uhalifu fulani, nikajiuliza moyoni, kwanini nimefanya hicho
nilichokifanya, kwanini ninakuwa na huruma na mtu asiyejihurumia....
‘Ningelikaa
kimiya nione mwisho wake ni nini, lakini je....mara nikaona pale mlangoni kwangu
akitoka askari...Kumbe askari wapo nyumbani kwangu, kwanini wameliweka gari
mbali na nyumbani kwangu, au walifanya hivyo makusudi, ili waliopo hapo wasijue kuwa wanakuja maaskari. Janja yao.
******
‘Mnasema
wenyeji wametoka, na hamjui watarudi muda gani, ina maana nyie tangu mfike
hawow wenyejiwenu wakiondoka hawasemi wanakwenda wapi, au watarudi saa ngapi?’
akauliza askari mmojawapo.
‘Kuna siku
wanatuambia, kuna siku hawasemi, ....hatuna muda mrefu tangu tufike
hapa....kwani kuna tatizo gani?’ akauliza baba.
‘Kuna
maswali machache tunataka kuwauliza, hasa kuhusiana na mke wa mwenye nyumba
hii...’akasema askari.
‘Mimi
nilisema huyu mwanamke atamuingiza mtoto wetu hatiani,....sasa
unaona...’akalalamika mama.
‘Kwani
umeambiwa kuna hatia....huyo ni mwanaume na matatizo kama hayo ni kawaida
katika maisha, hebu tuambieni kuna tatizo gani, maana sisi ni wazazi wa huyo
mwenye nyumba..’akauliza baba.
‘Ni vyema
tukawauliza wao wenyewe, msiwe na wasiwasi,wakija waambieni tunawahitjai
kituoni...wafike haraka, vinginevyo tukija wenyewe litakuwa swala
jingine...’akasema askari na kuondoka.
********
‘Hebu
niambie kuna tatizo gani mpaka maaskari wanafika hapa, ...wamekuja hapa ukiwa
haupo na lengo lao kubwa ni wewe....hasa baada ya kupokea ile simu, hebu
niambie ilikuwa simu ya nani, na jinsi ulivyoondoka hapa jana,uliondoka bila
kuaga,ina maana ile simu ilikuwa ya matatizo gani?’ nikamuuliza.
‘Hayo
hayakuhusu, nilishakuambia kuna mambo yangu ya kimasiha hutakiwi kuyajua, na
nafanya hivyo kwa nia njema....’akageuka na kuangalia kwenye droo ya kitanda,
na kusema;
‘Kwanza
niambie pale kwenye droo, kulikuwa na pesa na vitu vyaagu vingine,...niliondoka
bilakufunga,sasa hivi naona droo haina kitu, pesa na vitu vyangu vingine vipo wapi?’
akauliza Kimwana akiniangalia machoni.
‘Pesa zako
hizi hapa...., nilipoona droo zipo wazi na afunguo haupo, nikaona
nikuhifadhie...’nikamwambia na kumkabidhi zile pesa, alizipokea na kuanza
kuzihesabu, na alipomaliza akauliza tena;.
‘Na vitu
vingine...?’ akauliza kwa ukali.
‘Vitu gani
vingine....mimi nimekuambia ni pesa ndizo nilizoziona ,lakini sikuona kitu
kingine...’nikasema huku nikimkazia macho.
‘Sikiliza...wewe mwanaume, mimi sio mjinga kukuambaia kulikuwa
na kitu kingine, usijifanye mjanja , unaweza ukafanya jambo ukaja kujijutia
baadaye, hicho kitu kilichokuwa hapo ni hatari, ni bora ukanirudishia nikajua
mwenyewe jinsi ya kukihifadhi...’akasema huku akikagua mle kwenye droo.
‘Mimi
sijaoan kitu kingine...zaidi ya hizo pesa..’nikasema huku nikimwangalia kwa
makini.
‘Tusitaniane...nakuambia
ukweli hicho kitu kitakuletea matatizo....mimi mwenyewe nimekabidhiwa tu... na
kama polisi wakija hapa, na wakakiona umekwenda na maji, usije ukasema
sijakuambia.....’akasema huku akitafuta kila kona ya chumba.
‘Kitu gani
hicho, ...mpaka polisi wahusike,....mbona husemi kulikuwa na kitu gani
humo...mimi sijaona kitu zaidi ya pesa, kama kuna kitu kingine ambacho mimi
sikijui niambie....’nikasema na baadaye wazazi ambao walikuwa njewakaingia, na
kutupa taarifa kuwa polisi wanatuhitaji kituoni haraka iwezekanavyo.
‘Haya ndio
mambo tuliyowahi kukukanya....unaona jinsi unavyojiingiza kwenye matatizo ambao
kamaungelitusikiliza mapema yasingelikukuta...’akasema mama.
‘Mama
usijali hakuna tatizo hapa,....’nikasema nikijipa moyo.
‘Msijali
wanakijiji,...haya ni mambo ya mjini...tumeshazoea matatizo kama hayo...nyie
endeleeni na
shughuli, maana wanasema asiyefanya kazi asile....sasa hata vikazi
vidogo vidogo vya hapanyumbani mpaka mtu aambiwe....sio kwamba nawaamrisha
mfanye, lakini ni swala la....’nikamkatiza kabla hajaongea zaidi.
‘Kimwana,
unataka nini kwa hawa wazazi, unataka wafanye nini,mama kila siku ndiye
anafanya kazi zote za hapa nyumbani utafikiri ndiye mfanyaakzi wa hapa nyumbani,
ulitaka akufanyie nini zaidi....au unataka baba naye afanye nini...?’ nikauliza
kwa ukali.
‘Kuna usafi
wa nje, angali majani yalivyoota nje....kwasababau wapo hapa wanaweza
wakasaidia...aah, ngoja ninyamaze maana ulishasema antakiwa kuji....kufnaya
nini vile, maana sijui kuigiza mambo hayo, haya twende huko polisi
ukajichanganye huko, na ole wako kama ulichukua hicho kifaa na ....ole...wako
kamaunataka kwenda Segerea, jifanye mjanja...’akaniamb huku akininyoseha
kidole.
‘Twende ,
mimi sina wasiwasi, tutayajulia huko mbele...’nikasemana tukaondoka kuelekea
kituoo cha polisi.
Tulifika
kituoni tulikutana na huyo askari aliyekuja nyumbani na moja kwamoja
tukaingizwa kwenye chumba maalumu, na kuanza kuhojiwa kwa saa nzima, na
hatimaye tukaongozana nao hadi nyumbani ili kufanya msako...mimi sikuwa
nakipingamizi,ingawaje mke wangu aliwapinga kwa nguvu zote,
'Hakuna kupekua humu ndani, .....kwa uhalifu gani, ...'akasemamke wangu, na hata hivyo ilibidi akubali baadaye alipoona
mimi sina kipingamizi akakubali shingo upande huku akiniangalia kwa wasiwasi,
na msako ukafanyika kila kona ya nyumba, wakitafuta silaha inayosaidikiwa kuwa
imehusika katika ujambazi na silaha hiyo aliporwa kutoka kwa mmoja wa maaskari
akiwa kazini..
‘Na
waliompora na hawo machangudoa....’akasema askari mwingine.
‘Kwani huyu
askari alikuwa wapi, kama hakuwa na hawo machangudoa...?’akauliza jamaa mmoja
aliyekuwa karibu akisikiliza.
‘Hata kama
alikuwa nao,alikuwa akitimiza majukumu ya kikazi....kwanini unaingilia hapa,
kwanza wewe haikuhusu ..hebu ondokeni hapa...’askari wakaanza kutimua watu
wasiohusika, lakini ujumbe ulishafika. Kwani inavyosadikiwa askari huyu na
mwenzake walikuwa eneo hilo wanakopenda kukaa hawo wasichana wanaoitwa
machangudoa. Wasichana wale walipogundua kuwa maaskari wanawafukuza eneo
hilo,wakapanga mbinu za kuwahadaa hwo maaskari kimapenzi, na walipowanasa, ndipo
wakachukua silaha mbili bastola na bunduki....bunduki ilipatikana
baadaye,lakini bastola haikugunduilika wapi ilipo.
‘Sasa
kwanini mje kwa huyu mke wangu...?’nikauliza.
‘Kuna
taarifa kuwa silaha hiyo ilikuja kufichwa hapa...na kwa taarifa yenu, hizo
silaha zilipochukuliwa zilitumika kufanyia ujambazi....mnaona hatari iliyopo
hapo...naomba mlifikirie hili kwa makini....’akasema askari.
‘Mimi
nauliza kwanini mhusi kuwa hiyo silaha imeletwa kufichwa hapa, ...ina maana mke
wangu alikuwa huko kwa hawo machangudoa,au anashirikina nao...?’ nikauliz akwa
hasira.
‘Sikiliza
sisi tumewakamata washukiwa na tulipowabana sana mmoja akasema silaha hiyo
walimpa dada mmoja akaifiche, na akasema
ni huyu mkeo, ...kwahiyo tunaomba kwa usalama wake kama anayo aitoe, vinginevyo
tukihakikisha kuwa ni kweli alipewa, atahusishwa na huo ujambazi,....’akasema askari
mmoja.
‘Lakini
mumetafuta kila kona hakuna, ...endeleeni kutafuta mpaka mjirizishe
wenyewe...’nikasema huku nikigeuka kumwanglia mke wangu ambaye alikuwa katulia
akivuta sigara. Huwa kukiwa na jambo linalomkera sana hupendelea kuvuta sigara,
na tabia hii nimejaribu kumkanya kuwa sigara sio njema kwa afya yake, lakini
haambiliki.
‘Usituvutie
sigara hapa....’akasema askari kwa ukali.
‘Hapa ni
nyumbani kwangu, kama sigara inakukera ondoka,... nani aliyekuambia uje
nyumbani kwangu, ..sio kwasababu wewe ni askari
ndio unituingilia hadi sheria za nyumbani kwangu, ..kwanza nyie
maaskari, mtatumwaje na hawo wasichana wenu kuja kwangu kuwa eti wamenipa
silaha, na muwaamini, hamjuii hawo wanaweza kusema hivyo ili kuniharibia maisha
yangu ...mimi ni mke wa mtu nina heshima zangu, au mnalenu jambo....?’ akauliza
mke wangu kwa hasira.
‘Hatuna
maana hiyo kwako,... ila siku hizi kuna mtindo umezuka, ...Hawo wanaohusika,
siku hizi hawakai barabarani,wanachofanya
ni kukodi nyumba kwa siku, wiki au mwezi, wanawasiliana na wateja wao
muda wakukutana...’akasema
‘Mimi nimeshakuambia
kuwa mimi ni mke wa mtu,...unanielewa ...tokalini mke wa mtu akafanya mambo
hayo, au nikuulize wewe mke wako anaweza kufanya mambo kama hayo?’ akase mke
wangu na yule askari akakunja uso kwa hasira, na kusema;
‘Hatuzungumzi
habari za mke wangu hapa, usiharibu mada, unataka kuharibu jambo la msingi...’
‘Jambo la
msingi ni lipi, hilo maana sikuelewi elewi mimi ....?’ akauliza mke wangu.
‘Jambo la
msingi ni hilo tukio lililotokea,...na ni kawaida kukitokea uhalifu lazima
tuufanyie uchunguzi, na hapa ni moja ya
kazi zetu, kutafuta ukweli na kufichuka ukweli ulipo, kujua chanzo cha uhalifu
huu, hatujakunyoseha kidole wewe moja kwa moja kuwa unahusika,ila ninachotaka
kusema ni kuwa uhalifu umefanyika, na kama umefayika ni lazima tutafute
wahusika, ....na ndani ya uhalifu huo kuna silaha ye polisi iliyochukuliwa...je
mnajua lolote kuhusiana na sil’akasema askari huyo akiwa kamkazia Kimwana macho.
‘Je huo
uchunguzi umelengaje hapa kwangu, na isiwe kwa mtu mwingine....?’ akauliza
Kimwana.
‘Kutokanana
vyenzo vyetu vya habari na mahojiano kati ya mmoja wa wahusika tukaeleekzwa
kuja kwako....ni moja ya taratibuu na wewe kama raia mwema unatakiwa
ushirikiane na sisi...ni kawaida, huna haja ya kujishuku....’akasema polizi.
‘Sina haja
ya kujishuku wakati nyie mumeshanishuku...ina maana kinachotakiwa ni mimi
kujitetea, siwezi kukaa kimiya tu....mwisho wa siku mnaweza mkamshika asiye na
hatia, ....imeshatokea hivyo....’akasema na kabla hajaendelea mara akaingia
askari mmoja.
‘Afande,
unaitwa huku na mkuu ...’akaja askari mmoja,na kuondoka na huyo askari na
baadaye akarudi na kusema;
‘Bahati
yako, hiyo silaha imepatikana,lakini hatujamalizana na wewe unaweza ukahitajika
kituoni muda wowote , kwasabbu kwanini utajwe wewe...lazima kuna kuhusika kwa
namna yoyote ile,na nitahakikisha kundi lenu na huyo mwanamama, mnafikishwa
mbele ya sheria...’akasema yule askari.
‘ Ni mpaka....hahaha....umeshindwa
babu wee...hapa ni maji marefu, nakuambia hivi kama ni kwa matindo huo
yatakushinda....mjini hapa...’akasema mke wangu bila kujali.
‘Hivi wewe
huoni unawapandisha hasira hawa watu, wenzako wapo kazini,na kuna huo uhalifuu
umefanyika, wewe unaleta mzaha, hawo ni wanausalama, wanaweza wakakulinduika
ndani kwa usalama wa taifa...’nikasema.
‘Sio rahisi
hivyo, tatizo lenu na Wananchi wengi ni uwoga,...hakuna sheria ya kumshika mtu
ovyo ovyo, bila kuwana ushahidi kamlifu kuwa ni mhalifu..ukiwaogopa hawa watu
watakunyanyasa...na mara nyingi uwoga ni dalili mbaya sana ya kutokujiamini...’akasema
mke wangu.
‘Hebu
niambie hicho ulichokuwa ukitafuta kwenye hiyo droo ni hiyo silaha....?’
nikamuuliza.
‘Wewe
mwanaume, sema ukweli ulikwenda kuiweka wapi, maana umevuruga mambo ya watu,
unafikiri hawo wanye nao wakija kuniuliza nitasema nini hapa...aah, watu
wengine bwana..waoga...’akasemabila kujali.
‘Yaani
badala ya kushukuru kuwa umeokoka na hilo janga, ...unafikiri wangeikuta hiyo
sailaha hapa ungelikuwa wapi sasa hivi...na mbona kila hatua inaonyesha wewe
kuwepo kwenye makundi hatarishi...kumbe na hata silaha unajua kutumia?’nikamwambia.
‘Silaha,
ina maana wewe hujui kutumia silaha,....tuachane na hayo, hebu tuangalia jinsi
ya kusihii na hiki kijiji, maana mambo ndio hayo yameharibika, kwa mtaji huu
hakuna sehemu ya kufanya dili la pesa, hata huyo Muhindi atakuwa
mbendembende...hiki kijiji kitakuwa hapa mpaka lini?’ akauliza.
‘Nilishakuambia
hiki sio kijiji, hawa ni wazazi wangu wanahaki ya kukaa hapa hadi hapo
watakapoamua kuondoka wenyewe....’nikasema.
‘Sawa sio
mbaya maana mama ni jembe, anavyopiga mzigo hapa nyumbani, nimemkubali,
....lakini baba mmmh, ananiboa, muda wote kakunja nne, anasubiri sahani mezani,
huyu tutakosana naye....wewe subiri..na leo tunaongozana hadi kwa huyo Muhindii
anahitaji kibarua wakubeba mizigo...’akasema huku akiangalia saa.
‘Mimi
nikabebe mizigo naelimu yangu hii...hivi wewe unanionaje mimi...?’ nikamuuliza.
‘Kula hiyo
elimu yako...elimu bila kazi ina maana gani, elimu ni jinsi ya kupata mahitaji
yako, elimu sio kufa na tai shingoni, umekaa ndani na makaratasi yenye mapambio
makubwa, eti shahada, au stashahada, au sijuii nini...lakinii mfukoni hakuna
kitu, hayo ni mkaratasi tu, yanastahili kutupwa shimoni..elimu ni
pesa,....elimu ni mipango, elimu ni kuwa na uhakika wa mkate wa kila siku....’akasema
huku akionyesha mkono mdomoni.
‘Unajua
sana kuutumia mdomo wako...’nikasema na mara
simu yake ikaita na alipokea bilakuiangalia
‘Kuna nini
tena Docta....?’ akauliza
‘Mimi
....hapana,huoni hali ilivyo huko nje...’akasema na kusogea mbali na pale
nilipo.
Mimi ni mke
wa mtu mama, kwanini usiwatumie wengine....najua sana, lakini wapo ambao ni
wajanja, wanaweza kuifanya hiyo kazi....oooh, mama,tafadhali...mbona hunitakii
mema, ...ooh,...mkuu wa usalama, hapana, huko tunakwedna
mbali...huko,...unamjua eti nini, uliwahi, ... haya nakuja ...’akakata simu na
kunigeukia.
‘Huyu mama
sasa ananipanda kichwani, lakini sina jinsi, maana ameshika mpini, ....haya
mimi natoka,ila kesho ujiandae tutakwenda kwa huyo Muhindi, lakini huko uwe
makini maana mke wake naye simuamini,....’akasema nakuchukua mkoba wake.
‘Sasa
unakwenda wapi?’nikamuuliza.
‘Kwa
wanaojua hii dunia, ....huyo ni mama, yeye ndiye alinilea, ..sio mama yule wa kijijini,
hapana huyu ni mama wa mjini, mama wa maisha, akikohoa unatetemeka....sina
jinsi, ila akijifanya kuniburuza, nitamuhesabia masiku, hata mimi nina data
zake...yeye anajifanya ana kila kitu chetu, hajui hata mimi ni
mjanja....tutaona mwalimu na mwanafunzi nani zaidi....’akasema na kuondoka.
‘Siamini
....’nikajikuta nikisema .
NB: Nimechelewa kuiweka sehemu hii kwasababu
ya matatizo ya blog, nashukuru mungu ile hali imetangamaa, tuzidi
kuwemo,ingawaje sehemu hii nimeiburuza kwa harakaharaka , lakini natumai ujumbe
utakuwa umefika.
WAZO LA
LEO: Mabaya yapo na watendaji wa ubaya ni hawo hawo wanadamu, tunaposikia jambo
tusizarau, tulifanyie uchunguzi kwanza, kwani lisemwalo lipo kama halipo laja....na
hata hivyo tusiwe na pupa na maamuzi , kwani maamuzi ya haraka yanaweza kuleta
majuto baadaye, kama walivyosema wahenga, haraka haraka haina Baraka na majuto
ni mjukuu.
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
wanakijiji what a name to call ur inlaws!!! wanawake sie hii ni aibu tujifunze kupitia hii story na kujirekebisha nina uhakika tupo wenye haya mapungufu haya na wandoa dawa ya tatizo ni kulikabili na si kulikimbia
thanks m3 kwa kutupa kitchen party ndoani...
Ujumbe umefika M3 na umeeleweka kabisa
Pam,...Kuna jamaa aliniambia kuwa wanawake ni watu wa ajabu sana, wao wana huruma sana, lakini wakibadilika wanakuwa wabaya zaidi ya mnyama...sin auhakika na hilo, nawasikiliza nyie.
Nashukuru Precious, tupo pamoja
Na wengineo mungu awabariki kwa kuendelea kuwa nami.
Post a Comment