‘Wakati
mwingine mambo yako yananishanagza sana, sasa huu mkanda unaofundisha utapeli
wa dunia utanisaidia mimi kitu gani, mimi sio mwizi na sipendi niwe
hivyo....nataka kazi halali, unajua nimejifunza, jambo kubwa sana katika maisha
ni vyema uishi kutokana na kipato chako, kama hakitoshi jibane hivyo hivyo,
usiwe na tamaa,unaona hapa nilipofikia....’nikawa namwangalia Kimwana.
Kimwana
macho yake yalikuwa kwenye ule mkanda, huku akitikisa kichwa kukubali kitu
fulani, akageuka kuniangali na kusema;
‘Sikiliza
wewe wakuja...hebu angalia ile akili iliyotumika pale,....ukiitumia kwa hawa
matajiri wetu ambao wana pesa za kamari...maana naziita pesa zao za kamari,...wewe huwajui
vyema hawa watu , ...pesa zao nyingi sio za halali, kama sio za halali, kwanini
na wewe usichukue kidogo...kidogo tu,... kwa mbinu kama ile...’akarudisha nyumaili
nione vyema.
‘Umeona
hiyo.. wakati mwingine shule sio lazima uingie darasani,hii mikanda
waliyotuletea ina mafunzo, inawezekana yakawa mema au mbaya, ni akili kichwani
mwako...mimi nina akili najua lipi baya na lipi zuri, usinione hivi.....hapo
ni utapeli wa dunia, mtu anapata pesa kilaini,hutumii nguvu...
‘Unanitia
mashaka wewe naon haupo sawa kabisa, yaani wewe hapo ulipo unawaza kutapeli...mara ulikuwa changu....utabisha kuwa haukuwa changu wewe.... sasa
unataka kuwa tapeli...hapana sijui kama nitakuweza wewe....’nikasema huku
nikaangalia mlangoni.
‘Sikiliza
mume wangu dunia hii usipotumia akili utakufa njaa, nishakuambia hilo, na wakati
mwingine kuna shule zipo kwenye hii mikanda sio swala la kuangalia tu,
unaangalia unajifunza jambo,...juzi ulivyokuja na kunivamia chumbani na visu
mkononi, nilikushangaa sana,.....nilikuwa darasani...eti nilikuwa changu, unajua uchangu wewe...uliwahi kuniona barabarani najiuza...nyi watu wa ajbu kweli...`i am professional...training,.....ooh, naona nikiongea na wewe hutanielewa,ilajua kuwa mimi sio changudoa.....’akasema huku akiwa anaangalia ule mkanda kwa
makini.
‘Haya ipo siku utaumbuka tu....siku ile hata
angelikuwa nanii angafanya kama nilivyofanya....wewe unaangalia mikanda ya video michafumichafu,isiyofaa...umeweka
sauti kubwa, ambayo mtu akiwa nje anajua kabisa kuna watu wanaongea huku....nyie
watu, mbona mnaiharibu hii dunia, hawo wanaigiza tu, ili wapete pesa, sio hali
halisi ile,mnaharibiwa vichwa vyenu bure...uelewe hilo ....’nikamwambia.
‘Kuigiza
hawaigizi vitu ambavyo havipo....ni kama unapotunga hadithi, unaitoa kichwani,
lakini ni kutokana na matendo yaliyopo miongoni mwa watu, ndio unapata
kisa....halikadhalika hii mikanda ya video, wanaigiza maisha ya watu....na ili
uhakikishe angalia kama ule ulionikuta naangalia, umehakikiwa na madocta ambao pia wamehusika kuelezea mambo hayo kitaalamu, ...sio hivi hivi tu...nyie watu mumeenda shule gani...’akasema
huku akiinuka pale kitandani.
‘Hamna kitu
pale, mimi sitapoteza muda wangu kwa mambo hayo, ....sina tabia ya kuangalia mapicha ya watu walioigiza ili wapate pesa, ...mimi sina pesa badi nikae kuangali hayao mapicha, kwanini badala ya
kuangalia wanavyoigiza, nisiingie mitaani nikachakarika...’nikasema.
‘Safi kabisa, haya
chakarika basi, ...sana sana ni utaishia kutoa mijasho,unakuja hapa unanuka mijasho tu, hakuna hata sento moja mfukoni. ..kuharibu soli..hakuna
unachokuja nacho..kwasababu unachakarika bila malengo....mimi asilimia kubwa ya
shule yangu ni kwa kupitia hizi video...na kama ungeliniweka darasani
ningelikuwa docta....' akasema huku akiniangalia machoni.
'Najua mtu kama wewe huwezi amini,..maana kusoma nyie ni kufaulu darasani, ....unaweza kuamini mimi nilifeli darasa la saba,lakini kinamna nimesoma hadi chuo kikuu..huamini....lakini wenzako wananiamini, hata likitokea jambo linalohitaji utaalamu naitwa...naitwa hata na madocta..sio madocta hawo wa hospitalini..nielewe lakini....nielewe naongelea nini...mambo yapo mengi ya kujifunza....wenzako wanajua..'akasema huku akiwa kama anachukia kwani nilionyesha kutokumsikiliza kabisa.
‘Hahaha
kama huyo mama Docta wenu sio ehe hebu niambia kuhusu yeye, huyo mama Docta...?' nikasema kama nauliza vile
‘Mama yetu,
mama yetu yupi huyo.....?’ akashituka na kuniuliza
‘Unajifaanya
hujui au sio....mimi sio mtoto mdodgo
nimekwsiha kujua ....’nikasema huku nikimwangalia.
‘Sikiliza
hapa nipo darasanai kama unataka kaa hapa pembeni tuangali huu mkanda, kama
unahitaji kuwa na mimi nitakufundisha, kamahuhitaji, basi wewe kaa hapa
nyumbanimwanaume nikatafute pesa, lakini hii ni gharama,malipo yake
...hahaha....utaona mwishowe.
‘Mimi
sinamuda huo, ule wa mwanzo nimeutupia jalalani...’nikasema na hapo akainuka
kwa ahsira na kusema;
‘Yaani ile kitu nimenunue kwa hela yangu, wewe
unaitupa, ....ndio maana nimeutafuta siuoni, nautaka mkanda wangu,la sivyo hapa
kutachimbika....’akasema na kuinuka kitandani.
‘Wa nini ule, uchafu tu, hebu niambia una faida
gani...’ikabidi nimpoze maana huyu mwanamke akianza visa kweli kutachimbika.
‘Wewe hukuona, ilikuwa inanifundisa maswala ya
ndoa, jinsi gani wanandoa wanatakiwa kuishi, kutendeana, ....’akatulia
nilipomuonyesha ue mkanda wake ulipo.
‘Unaona hapa nje, umeidhinishwa na madakitari
bingwa...hawa walisaidia kukamilisha huu mkanda, walipochunguza na kugundua kuwa
wanandoa wengi hawatimizi sharti muhimu landoa yao, kwasababau hawajui, ....wao
walijua ndoa ni ndoa tu,umeoa umeolewa...’akatuliana kuniangalia kwa makini.
‘Ndoa ina mambo mengi, lakinikuna jambo moja
muhimu na wengi wanaliita `la ndoa...’ huajsikia kupika au kufagia kukaitwa
`kazi zandoa’hapana, ....kwasababu ungeliweza kuzifanya mwenyewe, au
ungelitafuta mfanyakazi wa ndani akakufanyia, ....au sio...?’ akaniambia huku
akikunja uso alipoona simsikiliza.
‘Tatizo lako ndio hilo, hutaki kunielewa....nyie wanaume mnazarau yale mambo muhimu na matokeo yake
mtaoa,mtaacha na mwishowe mtaokota garasa...hilo nikuambie ukweli....huu mkanda
ni mahususi kwa wanandoa unafundisha mambo ya kimaumbile...kuna mambo mengi
nyie wanaume hamuyajui, na na kama hamuyajui, na hamutaki kujifunza, ....basi
ukimpata mke mwenye akili kama mimi anayekujali na kujali ndoa yake, anakuletea
mambo kama haya,...’akauchukua ule mkanda na kuuweka kwenye kabati.
Ila leo ni tofauti, leo tunajifunza jisni ya
kutafuta pesa.....njoo hapa tuangali halafu nitakufundisha jisi gani inatakiwa
iwe..ndio ni utapeli kama inavyoonyeshwa, lakini ukitumia akaili ..unatafanya
akzi, na utafanikiwa, ...acha mambo ya wivu,..hahah eti siku ile mtu huyu na
kisu mkononi, wewe...kisu ni silaha gani....’akasema na kunifanya nikumbuke
siku ile ambayo nilifika nyumbani nikawa nasikia kelele za ajau akabu ndani....
Siku ile
nilifika nyumbani nikiwa na mawazo, nikiwa nimehamaki, baada ya kumjua kuwa mke
wangu miongoni mwa hawo wanawake wanafanya
bishara haramu za kujiuza na sasa ananitumia kamachambo au sijui kwa maslahi
gani, nia na lengo lngu nikifika niongee naye vyema, kama ikibidi tuachane kwa
amani, ...
Nikiwa
sijui nichukue uamuzi gani maana akiondoka hapo na mimi itabidi nianza kazi ya
kuomba omba, maana sina kitu, kwa asilimia kubwa namtegemea yeye. Nikawaza kwa
undani mwishowe nikaoana hakuna jinsi, lazima nibakie naye kwa muda huku
nikitafuta jinsi ya kuishi hapa Dar.
Nilipofika
mlangoni ndio palenikaitizama nyumba kwa makini,nikiwa najilaumu kwanini
nilisitisha yalemakato ya kulipia deni, maana kamaningelikwenda kamamakubaliano
yalivyokuwa deni lingelikuwa dogo sana, naingekuwa rahisi kumalizia kwa njia
nyingine,lakini sasa deni ni kubwa ukujumlisha na riba. Nikashika kitasa na
kukizungusha.
Nikiwa na
kisu mkononi, niliingia chumbani huku kichwa kimejaa mawimbi,hapo hasira zote
zilikuwa kumalizana na huyo binti,kama ndio kaamua kuniingizia wanaumehumo
ndani, basi liwalo na liwe, ni bora nikafungwe tu...nikajisemea huku moyoni
nikiwaza maisha ya jela, nilionja mara moja nikajuta, ....hapana, huyu lazima
nimfanye kitu mbaya.
Wakati bado
Kisu kikiwa mkononi, niliusukuma ule mlango,na zile hasira na chuki
nilizotamani kuzificha zikawa zimevumbuka na hapo sikuwa na simile tena, lengo
langu ni kufanya jambo ambalo hawatalisahau nikajitosa ndani...
‘Oh, ndio
utaratibu gani huo wa kuingia bila hodi huoni nipo shuleni hapa....’akasema
Kimwana, akiwa kajilaza kitendani na mbele yake kaweka runinga ikiwa na video
akiangalia picha, na nilipoptisha macho ya haraka niligutukana kuagalia
pembeni..
‘Ni vitu
gani unaangalia hivyo na umefungulia kwa sauti kubwa kiasi kwamba watu
wanafikiri mpo na...na...
‘Naju hata
wewe ulikuwa ukifikiri hivyo, ndio umechukua kisu ili umchinje huyo mwanaume niliyemuingiza
humu, ....hahaha..haya kamchinje yule jamaa, huoni aanavyofanya, ...pale ni
shule tosha,....shule ya kukurizisha wewe mwanaume wangu...’akasema Kimwana.
‘Hembu
ondoa uchafu wako hapa.....’nikasema huku nikikaa kitandani na kuangalia
pembeni.
‘Uchafu,...hahaha.....uchafu
wakati ulimuacha mkeo kwasababu ya mambo hayo...hivi ndivyo mkeo alitakiwa
akufanyie, hukumfunda....ilitakiwa kama hajui ungelimnunulia vitu kama
hivi...huu mkanda umeidhinishwa kitaalamu kuna madocta wazungu na waafrika,
wamefanya utafiti na kugundua nini kilichopo ndani ya hisia za kibinadamu...na
kwanini ....tatizo lako hutaki kuelewa, au hutaki kinielewa....’akawa anaongea
lakini sikuwa namsikiliza kwani hapo nilishahakikisha kuwa huyu ni changuduo.
‘Sikiliza wewe
mwanamke hapa nilipo nawaza jinsi ya kupata pesa, jinsi ya kupata kazi, ....sifurahii
kabisa hii hali ya mimi kuwa nalishwa na wewe, ....wewe naona badala ya
kunisaidia kwa hilo unaleta mambo ya mchezo, eti jinsi ya mume na muke waishi sijui wafanye
nini,ili iweje,...hayo hata bila kufundishwa yanajileta yenyewe tu,...hivi
mkiwa na njaa kweli mambo hayo yanafanyika....?’ nikamuuliza.
‘Hahaha...eti
mkiwa na njaa,...nani ana njaa hapa, kwani hujashiba,....ujue kuwa kama akili
haijatulia katu huwezi kufikiri....hili linatuliza akili, linatuliza
mihamaniko,....ndio maana mke au mume anatakiwa ailijulie kwa ajili ya
mwenzake, ili muweze kutulizana......vinginevyo macho yatakuwa wayu wayu,
kutizama wapiti njia,...kutamani vya wenzenu, ..akili zenu
hazitatulizana....nikuulize,ukiwa na njaa, hutaweza kuwatamani mabinti au wake
za wenzako...?’ akaniuliza.
‘Swali hilo
niliwahi kuwauliza wazazi wangu kipindi kile....unakumbuka, maana unatoka
kazini,una njaa ya mkeo...una ....huna na kwasababu huko maofisini, kuna
mabinti waliojaliwa hawana aibu, wanakutamanisha, ....sasa unakimbili anyumbani
ukijua ...mke yupo ....lakini ukifika duuuh,....mke anasema subiri, usiku
uiingie, na hata ukiingia ni kwa mbinde...kumbe ndio maana mnatunasa
kirahisi...?’ nikasema na mara mlango ukagongwa.....
‘Ni nani
tena huyo wakati kama huu...hapa tupo darasani, tupo faragha....watu hawajui maana
ya nyumba za watu, kila mara hodi, hodi...hawatambu huu ni muda wa faragha kwa
wanandoa..., hatutakiwi kubugudhiwa...’akalalamika kimwana.
‘Lakini
muda huu ni mchana....huenda ni wageni muhimu wanaweza wakawa watu wa kutuletea
pesa...’nikasema.
Watu wa
kutuletea pesa hahahahaee, pesa njoo, hivi wewe huna akili ya kufikiria...nina
uhakika watu wanaokuja saa hizi sio wa kuleta pesa,hawo ni watu wa shida, ni
watu wasio na pesa,wanakuja kuomba...eti kutuletea pesa...pesa hailetwi
kirahisi hivyoi...umelala ijilete yenyewe ni ya mashetani au ...sijui nenda
kuwaafungulie...
*******.
‘
Oooh...’nilijikuta niguna pale nilipofungua mlango,
‘Mwanetu
umtusahau...’ilikuwa kauli ya mama,....nikawaangalia wazaziwanhu hawa kwa muda
hata bila kusema kitu, maana ni muda mrefu sijawa na mawasiliano nao,
ningewasiliana no vipi wakati sina pesa, sina kazi...
‘Au hata
ndani hutaki kutukaribisha...?’ akasema baba.
‘Aaah sio
hivyo wazazi wangu,...baba, mama...ooh, mbona mpo hivi....kumetokea nini, karibuni,shi-shi
kamooni...mbona mumechoka hivi?.‘
‘Unatushangaa
leo, ushukuru tupo hai, na umshukuru sana mke wako wa kwanza isingelikuwa yeye
sijui ungeweza kusema baba au mama...’akasema baba huku akijikongoja kuingia
ndani.
Hali zao
zilionyesha kuchoka, na ilivyoonyesa sio kwasababu ya uzee, kama sio ugonjwa
basi kuna jambo kubwa limetokea huko kijijini.
‘Wanasema
kuna tatizo limetokea katika ukoo wetu, ingawaje tatizo sio kwa ukoo wetu tu,
hili tatizo ni maeneo yote, mvua hazinyeshi, hakuna mazao, mifugo yote
imekufa....hebu fikiri familia yetu ambayo kipindi cha njaa ndio inategemewa
safari hii tumekuwa hatuna kitu...’akasema mama.
‘Na mjomba
yeye yupo wapi naona umekuja na ndugu zangu wengine tu....?’ nikauliza.
‘Mjomba
wako alisafiri na familia yake kwenda kwa mtoto aishie huku Dar, ina maana
hamjawasilina naye mbona yupo hapa Dar?’ akauliza.
‘Kwakweli
sijawahi kuwasilinana naye...’nikasema.
‘Nakumbuka
kuna mzee mmoja alikuja hapa siku moja, akakuuliza, ...ooh, nimemkumbuka ndio
yule mlikuja naye siku ile, nilimsahau kabisa, maana alikuwa kakonda sana,mimi
nikajua ni ombaomba tu, nikampa pesa kidogo nikamwambia iishie zake, nakumbuka
aliniambia ....akija mjomba wangu mwambie hiki kizingiti hakifai kabisa
katika nyumba....’akasema Kimwana.
‘Mbona
hukuniambia, inawezekana ndio mjomba wangu huyo...unasema alisema nini?’
nikauliza nikitafakari.
‘Swala hapo
sikujua alisema nini...swala hapa ni hiki kijiji kitaishije hapa , siunajau
tena mambo ya bajeti, na leo sijatoka kabisa, leo nilikuambia nipo mapumziko....yule Mhindi anafanya mahesabu ya vifaa vyake, nami nikasema tukae
tujifunze maisha, sasa mara huuuh kijiji ndani ya nyumba...sasa hiki kijiji kitaishije hapa...?’ akasema mke wangu
akiwaonyosha vidole wazazi wangu.
‘Hiki sio
kijiji, hawa ni wazazi wangu...elewa Kimwana, wazazi ni kitu kingine, kikiharibika hapa wakakasirika mimi ninaweza kuokota makopo, bila wao nisingelikuwepo duniani, kwahiyo
tungalie tutawasaidiaje, tutafanyaje...’nikasema huku nikiwaangalia wazazi wangu
walivyochoka. Moyoni nikaingiwa na moyo wa huruma, maana ni kipindi kirefu sijawasilina nao,
sijawahi kuwatumia hata senti moja, hasa baada ya kuachana na mke wangu wa
kwanza.
‘Sasa hamna
chochote huko, mwanangu maana tangu jana hakijaingia kitu tumboni....’akasema
baba, na baba ninavyomjua ni mtu walishe..nikamwangalia Kimwana, Kimwana
akacheka, akasema;
‘Unaona....watu wanaagiza kama hotelini....kwamtaji huo hapa hakuna cha bajeti tena, sasa hivi ...oh, kashughulike huko jikoni, mimi
ngoja nitoke nikaangalia hiki kijiji kitaishije hapa na nikirudi nataka tuongee
vyema, ukumbuke na mimi nina familia yangu, na wao wana njaa hivihivi, mimi
nimewaambia hali ngumu,....wamenisikia... sasa wewe..huwezi kusema hivyo au sio.....`anyway', tutaonge baadaye anikirudi,...na kuongea kikweli kweli...' akawa keshafikamlangoni,halafu kaam vile kasahau kitu akageuka na kusema;
'Angalia huko jikoni kama kuna chochote wapikie wanakijiji, wasija wakatufia hapa...’akasema
kimwana akichukua na kutoka nje akiwa na kimfuko chake.
‘Aisee...hapa naona hakuna amani...mwanangu ndio imefikia hivi..vipi kazi lakini...?’
akauliza baba.
‘Wazazi
wangu hayo tutayaongea baadaye, ngoja niangalia kipoza njaa...’nikasema na
kuinuka, na mama akanifuta huko jikoni, nikashukuru kwa hilo,ingawaje
nilimwambia atulie tu wao ni wageni,laikini hakukubali akasema;
‘Mwanangu
mimi siwezi kukuona ukiingia jikoni wakati mimi nipo, hata kama mimi ni mama yako,
ilihali nguvu ninazo, acaha niifanye hiyo kazi, wewe nionyeshe vitu vya kupika
vipo wapi, nitafanya hiyo kazi wala usiwe na wasiwasi....wewe nenda akongee na
baba yako, kwani mnatumia majiko ya umeme au ya kawaida...?’ akaluliza mama
‘Mama siku
hizi tunatumia majiko ya kawaida , hali imebadilika mama...tutaongea kwa kirefu baadaye...’nikasema
nikideka kwa mama, mama ni mama hata uwe mtu mzima....
‘Mwanangu
mbona na wewe umekonda kiasi hiki,...mwanangu hali hii hapa inanitia
wasiwasi... usiniambie ni hiyo njaa ya kijijini ndio imefika hadi huku,...
lakini inawezekana maana kama sisi
tusipolima mtakula wapi,...mazao yote yanatoka kijijini, huku mjini hakuna
mashamba , mashamba yapo wapi huku mjini, haya mazo huko hakuna...sijui
tutakimbilia wapi, mungu mwenyewe ndiye anajua....
‘Mama hiyo
isikutie wasiwasi...ilimradi tupo hai, tutaishi tu...kwakweli iannisikitisha
sana, ....hapa nilipo najuta, najuta kwa mengi, umesema aliyewasaidia ni Binti
Yatima yupo wapi ...mbona hamkuja naye?’ nikauliza kwa shauku.
‘Yupo kwa
mume wake....mlivyoachana tu,wanaume wengi alimfuata kumuoa, na mwisho wake
akaolewa na mume mmoja tajiri,ambaye familia yao inaishi Kenya, ...walikaa kwa
muda na muda walipokuwa huku nchii, ndio walikuwa wakitusaidia hata alipohamia
Kenya bado alikuwa akituma pesa za amtumizi...kwakeli mungu amemjalia sana yule
binti...umefanya kosa sana kumuacha...’akasemamama.
‘Lakini
mama ujue kila kitu kinafanyika kwa mpango wa mungu, je ningekaa naye
angeliweza kuolewa na huyo tajiri, je angelifikia hatua hiyo
aliyofikia....asingeliweza, lakini yote haya yametokea kama sababu ili nimuache
aende kuishi sehemu anayostahili...kwakweli, kila mara namuwaza sanamke wangu
wakwanza...na hapa nakumbuka ukweli kuwa sio vyote ving’aavyo ni
dhahabu....natamani kama enzi hizo zingelirejea nikajisahihisa...’nikasema
nikimuangalia mama akihangaika jikoni.
‘Nenda
kaongee na baba yako ana hamu sana na wewe...hayo yameshapita tena...maji
yakishamwagika hayazoleki...mwenzio yupo Kenya na nasikia anasoma, karibuni
kuingia chuo kikuu....’akasema mama.
‘Mpaka
kaamua kusoma, kweli ameamua, kweli kampata aliyemshiba...haya ngoja nikaongee
na baba,najua baba ataishia kunilaumu na mwisho tutaishia kugombana,....haya
mama kila kitu kipo hapo kwenye kabati, leo tutakula, sijui ya
kesho...’nikasema na kutoke jikoni na kwenda kuongea na mama.
‘Ya kesho
hatuna mamlaka nayo anajua Mungu...’akasema mama akiwa hajui nina maana gani.
Nikatoka pale eneo la jiko na kuingia varandani na kumkuta baba akiwa kashikwa
na kausingizi...
‘Baba vipi
umeshikwa na usingizi,uchomvu wa safari au njaa...?’ nikamtania baba.
‘Yote.....oooh’akasema
huku akipiga miayo.
Poleni
sana,nasikitika sikuweza kufanya lolote sio kwamba niliwasahau, bali hali
yenyewe ilikuwa ngumu na nilipowaona na nyie mpo kimiya nikajua hakuna
shida...’nikajitetea.
‘Duuh,
mwanangu siku hizi wewe ndio mama wa nyumbani, au nisemeje, maana ile kauli ya
mkeo imenichefua kweli, isingelikua hii shida....,nisingelikaa hapa, yaani
sijui nisemeje...mkeo anakuambia uingie jikoni...ukapike yeye anafanya nini...au
ndio hivyo anakwenda kazini, na kazi gani hiyo siku ya leo...na muda kama
huu...mwanangu angalia sana...’akaanza kusema baba.
‘Baba naomba
ya hapa uyaachie hapa hapa....mimi najua nini ninachokifanya...hujui naumia
kiasi gani, lakini wakati mwingine inabidi ukubali ukweli...vinginevyo
ungelinikuta nipo mitaani naomba, au....sijui ningelikuwa nafanya kazi gani
sijui, baba...hapa nilipo sina kazi...naishi kwa kumtegemea huyo binti....akihangaika
huko anapokwenda ndio tunapata riziki ya kutufanya tuishi, kazi hakuna
kabisa....’nikasema bila aibu.
‘Eti
nini....haiwezekani, wewe siulituambia kuwa kampuni yenu ilikupeleka kusoma, imekusomesha hadi Ulaya,....halafu ndio imeamua
kukufukuza kazi, haioni hiyo ni hasara, haiwezekani,...nahisi kuna jambo
umetenda ....ina maana wao hawana akili wakufukuze
hivi hivi tu..au ndio huyo mke kakufanya hivyo..., au ni laana ya mkeo wa
kwanza maana hivi vitu sio mzaha....’ akasema baba huku akipiga miayo ya njaa.
‘Baba naona
una njaa hebu nikakununulie angalau ndizi mbivu uzibe njaa kidogo...’nikasema huku
nikiinuka kutoka nje.
‘Aaah,
chochote kwangu sawa maana ukiwa na njaa huchagui kipi cha kula, yaani hata
vile vya kuwekea maji yawe baridi,naitaje ile mashine....iko wapi ,naona vitu
vingi vilikuwemo humu ndani havipo, ina
maana umeuza vyote au uliibiwa nini....naona hata yale masofa ya
kifahari ukikaa unazama hakuna, mwanangu vipi kulikoni....?’ akawa anaongea
wakati mimi nimeshatoka nje.
Nilipofika
nje nikaonana na muuza genge ambaye ananidai vitu vingi nilivyokuwa nachukua,
na aliponiona tu akaanza kulalamika; kwake bila kulipa, nikimuahidi kuwa
nitamlipa mwisho wa mwezi, lakini ikawa ndio kazi nimefutwa.
‘Deni langu
broo, ...mimi kamtaji kangu unakaona kakubahatisha sasa ukikaa na hela yangu
muda wote huo unafikiri nitaendeshaje biashara,naoma unilipe leo broo....’akalalamika.
‘Sikiliza
bwana mdogo hata nchi kubwa kama Marekani inadaiwa madeni makubwa, sembuse wewe
na mimi...kudaiwa ndio moja ya biashara,...biashara ni kuuza, kudai na
kudaiwa...sasa sikiliza nina wageni wamekuja ghafla, naomba ndizi mbivu za
elifu, ....chukua hii hapa,... silipi deni kwa leo...nitakulipa tu, na
kukuunganishia....nataka siku moja uwe na duka, sio kigenge kama hiki....’nikampa
na kweli akanipa ndizi mbivu,nami nikarudi ndani.
***********
‘Haya
chakuala tayari, hebu tule huku tunaongea, maana kama tulivyosikia kijiji kipo
hapa na kipo mkononi mwako, kuna usalama hapa maana tusikae hapa huku
tunasimangwa, kama wewe huna kazi, unalishwa na mke, ..na sisi tumekuja hapa
kwa huyu ambaye tulimkana, huoni hapa tutaishi kwa kusimangwa tu.
‘Sasa
wazazi wangu tutafanyaje, mimi ndio hivyo sina kazi, ...bila kuwafichai huyu
binti ndiye anayeniweka hapa mjini, vinginevyo ningelishakuja huko
kijijini....na yapo mengi...,hata hii nyumba yenyewe nilijenga kwa mkopo, deni
halijalipwa na benki wanataka kuipiga mnada hii nyumba ili warudishe deni lao....naishi
hivyo hivyo, siku yoyote wanaweza kufika hapa na kuipiga mnada hii nyumba, sina
jinsi,....nimetumia mbinu za kuongea na hawo wanaonadisha, ....angalu kuvuta
muda, .....’nikaongea huku nikiangalai huku na kule, maana sikutaka kabisa mke
wangu alijue hilo.
‘Kama ni
hivyo ...turudi kijijini, wewe una minguvu bado, una akili za shule, unaweza
ukawekeza huko, kilimo bora cha kumwagilia...ukatuongoza kama alivyowahi kufanya
mjomba wako....mjomba wako kachoka siku hizi , lakini ujanani mwake, alikuwa
akija kijijini anatufundisha mbinu nyingi za kilimo bora, kufuga kwa mpangilio,
lakini safari hii kachemsha mwenyewe kakimbilia kwa mwanae huku mjini..’akasema
baba.
‘Baba mimi
hali kama hii nitaweza kushika jembe, na hata hivyo kama mumedai kuwa kuna
njaa, nitaenda kufanya nini, ufike mahali kuna kianzio, sasa hakuna hata
chakula...hata mbegu mnasema mumekula, nitaanzaje mimi, au elimu itasaidia
nini...tubanane hapa hapa, tuone itakuwaje, ngoja akirudi mwenzangu tutaangalie
nini la kufanya....’nikasema huku nikiwa na wasi wasi na kweli mara mlango
ukafunguliwa....
‘Haya
wanakijiji hamjambo...maana leo nimefika kwa Mhindi ikabidi nimpigie magoti,
nimemwambia nyumbani kuna kijiji kimefika kuanzia mjumbe hadi balozi, ....sina
pesa ya kula, na sijui tutalalaje humu, maana kitanda tulicho nacho ni
kimoja....’ akasema na kuniangalia kwa makini mimi nikamminyia jicho na
kumwambia
‘Wife eeeh,
njoo huku kwanza tuongee, ....’nikasema kwa haraka, nilipomuaona haniangalii,
au aliniangalia akazarau, akanifuata tukaingia chumbani kuongea. Tulipofika
akawa wa kwanza kuongea akasema;
‘Sikiliza
zamani tukisoma shule ya msingi kuna wimbo ulikuwa ukiimbwa, mgeni siku ya
kwanza mpe wali na samli...lalalala....si ndio, siku ya pili, ugali eeh, hivyo hivyo...nimesahau kidogo, na siku ya tatu
mpe jambe akalime, ...akishindwa, ...utaajza mwenyewe, sasa nakumbia hivi, leo
tutawakarimu ipasavyo, wale washibe,....’akasema huku akitoa pesa kwenye pochi
lake, nilishangaa pesa zote hizo kazipata wapi, lakini niliogopa kumuuliza.
‘Sasa....eeh,
kesho tutaangalia jinsi ya kufanya
lakini kesho kutwa, aah...wataanza kumuona kimwana, ..anga zangu zitaanza
kuwaka... sijui,...kwanza watu wenyewe walishaniambai sifai kuingia kwenye
familia yao, leo hii nawalisha mimi....sikiliza siku tatu, sio zaidi , hata
mimi nina wazazi wangu...lakini nimewatolea nje, ...nimewaambia wapo akina
kaka...sijui kinachoendelea huko...wananijua mimi , wananiogopa, kwani
sikopeshi mtu....’akasema na kuziweka pesa kwenye droo ya kitanda.
‘Sikiliza
mke wangu, umezungumzia wageni, hawa sio wageni hawa ni wazazi wangu na nikupe
ushauri,hapa ndipo mahali pa kuwaonyesha
kuwa wewe ni mkwe mwema, au unasemaje .....ndio sehemu ya kuingia kwenye
familia yetu bila shaka...kilaini...’niksema huku nikitabasamu.
‘Hahahaa...ngoja
nicheke...kuingia kwenye familia yenu, ina maana nyie mnajioan wa maana sana,
kwa vile kule kijijini mnatambulika kuwa ni familia ya maana,familia tajiri,
familia yenye maadili mema....hahaha...’ akacheka mpaka anashika mbavu.
‘Sasa
unacheka nini kwani sio kweli hiyo....’nikasema huku nikimwangalia kwa
mshangao.
‘Kwa vipi,
jione mwenyewe, hapa nani bora.....wewe au mimi, ..haya , mbona hawo wanakijiji
wanakuja kuishi na mtu anayetoka kwenye familia mbovu, familia yenye maadili
machafu...wewe. nyie acheni hayo..maisha hayana muamana, leo kwangu kesho
kwenu....’akashika kiuno huku akihesabu hela alizobaki nazo mkononi, halafu
akatoa noti mbili akanikabidhi.
‘Nimkuelewa,
mpenzi ,leo kwako kesho kwangu....’nikasema huku naziangalia zile noti
mbili....na aliponiona naziangalia akaangua kicheko na kusema kwa kuyarudia
maneno yangu kwa dharau;
‘Kesho
kwako....hahahaha..sasa usiku tutakula nini,... hiyo ni bajeti ya kesho...leo
kama nilivyokuambia mgeni siku ya kwanza, unamkarimu, mimi sina noma, nijua
kuwakarimu wageni, unaonaje tuwatoe ....kwenye hoteli saafi wanapata chakula na
kinywaji, safi kabisa, pesa leo ipo...swafi kabisa, kama ulivyosema
nijipendekeze...au sio’ akaniangalia kwa jicho la pembeni akacheka.
‘Kujipendekeza....duuh,
mbona hiyo kazi, nikuambie ukweli hii sio shepu ya kujipendekeza, mimi
najipendekeza kama kuna mslahi,kamakuna lengo, na nisema ukweli mimi
najipendeekzakwako tu kwako tu kwasababu....’akangalia juu ya paa, sijui alikuwa akiwaza nini.
‘Kwasababu
gani...?’ nikamuuliza kwa hamasa .
Akanisogelea
na kunikumbatia halafu kwa sauti ya kujilegeza akasema; `kwasababu nakupenda,
na huku kanikumbatia akiwa kaweka kichwa na kungalia upanda wa nyumba yangu, akabetua
mdomo wa dharau, hakujau kuwa namuona kwenye kiyoo cha kabati lililokuwepo humo
ndani, ...
‘Kimwana
naomba uniambie ukweli, nini lengo lako,...maana nahisi sio kweli unafanya hayo
kwangu bilamalengo, sizani unafanya haya kwasababu ya kunipenda kaam unvyodai,
..nimesikia mengi kuhusu wewe na wenzako mliokuwa mkifundishwa na huyo mama
mumuitaye Docta....na sijui kwanini upo na mimi maana lengo lenu ni kuwachuna
watu weney pesa, mimi sina pesa....’nikasema.
‘Unataka
nikuambie nini lengo langu,...nakusikitikia sana...?’ akaniachia na kuangalia pembeni.
‘Itakuwa
vyema, kuliko kuja kunishitukizia....’nikamwambia.
‘Hivi wewe
kwa muda kama huu una jeuri gani, hata nikikuambia sababu ...hicho kijiji hapo
utakipeleka wapi...sikiliza haya hayafai kwa sasa, jiandae na iandae hiyo
kamati ya kijiji twende tukatumie, tambia hii ni gharama, ipo siku ya kuipangia
bei,ambayo itafidia gharama hii na faida kibao...mimi nina malengo marefu..’akasema
huku akibadili nguo.
‘Sikuelewi
kimwana una malengo gani na mimi....?’nikamuuliza na mara simu yake ikalia na
akaichukua na kuniangalia kwa muda bila kuipokea, akasema;
'Nakuonea huruma sana, ...' huku simu ikiendeelakuitia, halafu akanibusu kwa mbali.
'Kwanini huipokei hiyo simu....?' nikamuuliza huku nikiwaza ni simu ya nani hiyo
‘Usijali
utakayoyasikia hapa nikiongea ni mambo ya kibiashara... mjini hapa ....’akaipokea
simu.
‘Sema
shosti kuna nini unataka kuniambia...nimeshakuambia tangu awali,mimi huku sipo
tena. Nimeolewa, ...unanielewa ,mimi nimke wa mtu,..eti nini ,mama Docta,...tulishamalizana
anye, vipi tena... ananihitaji, kuna nini....sasa hivi...hapana, ...eti
nini...siwezi,mimi nimeshajitoa,...eti nini...haiwezekani,....
Nilibaki
nimeduwaa, maana Kimwana alikurupuka, akaondoka hata bila kuaga sikujua kumetokea nini huko
anapokwenda, mimi nikatizama droo ya kitanda ambayo mara nyingi anaifunga na ufungua anatembea nao, leo
kaondoka bila kuifunga,...hamu ya kuchungulia nini kilichopo ikanijia, nikaivutakwa nje....zile pesaalizoweka,..nikazisogeza ili niangalie kwa ndani......ooh, moyo ukanidunda....macho yakaingiwa
na kwikwi, nikajikuta mwili mzima ukitetemeka, sio kwasababu ya zile pesa, ila
kile nilichokiona.....nikatamani na mimi nitoe humo nikimbie....
NB Hebu kisia , Je aliona
nini...tukumbuke kuwa kisa hiki na mahsusi kwa wanandoa...tutajaribu kugusia
gusia kamayalivyomkuta rafiki yangu, na kama kuna mwazao maoni,
tuambizane,maana mimi sio mtaalamu sana waammbo hayo, ila kisa ndivyo
kilivyokuwa;
‘WAZO LA
LEO: Wazazi ni watu muhimu sana katika maisha yetu, vyovyote wawavyo
tusiwanyanyase,kwani hakuna kama wazazi,...utayajua haya ukianza kulea...
huwezi hata siku moja kuwalipa fadhila zao kwani hakuna kama mama,hakuna kama
baba.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
mh m3 inachekesha yaani wazazi anawaita wana kijiji haya nasubiri nione itakuwaje
binadamu usife moyo kwani kila kinachotokea na mitihani tu ili ujuwe yupi mwema na yupi wa kukaa nae
Nashukuru sana Samira Tupo pamoja.
Kuna tatizo kidogo kwenye blog, najaribu kupambana nalo. Ilitakiwa sehemu hii ionekane kwenye blogs za watu, lakini inaonekana sehemu iliyopita!
Post a Comment