Ukiwa huna
kazi...na ulikuwa umezoea kazi, asubuhi upo ofisini na mwisho wa mwezi
unakinga, ni taabu kweli kweli. Ikabidi nijifiche fiche, na wakati mwingine
naamua kutembea sana, kwenye maofis hadi jioni, narudi wafanyaakzi
wakitoka...lakini nikaanza kuishiwa nauli hakuna, ikabidi kiguu na njia, viatu
viakisha soli....ikabidi ninunue ndala....
Mwanzoni
tulikubaliana vyema na kimwana, kuwa tuwe tunatoka asubuhi, kila mtu
akahangaike kivywake, na jioni tunakutana tuoena tumeppata nini, hakuna
kufuatana, ilimradi tunakutane jioni kila mtu anaonyesha kile alichojaliwa
nacho, mimi sina kazi, sina biashara nitapata nini....ikawa kila siku anayeleta
kitu nyumbani ni mke wangu kimwana....anapatia wapi sijui, ilimradi tunakula...
‘Sasa mimi
ni mume, maana nakulisha wewe, huji na lolote, hata angalau tunda, kila ukija
unanuka jasho tu...’akaanza kunisamanga.
‘Sasa ndio
unanisamanga, nimejitahidi kila ofisi ninayoijua sijapata kazi, na biashara
mitaani haitoki, kila mtu ana biashara hata wale wenye kazi wameanzisha
biashara, sasa sisi tusio nakazi tutafanya nini...yaani hapa nimechananganyikiwa
mke wangu, nahisi dunia imenilemea...sijui ni balaa gani...’nikasema huku
nikiwaza mengi.
‘Sikiliza,
huwezi kupata kazi kwa mtaji huo, ili upate kazi inabidi ufanye kazi, mimi kama
ningelitaka kuajiriwa ningelishaajiriwa muda mrefu tu, lakini sitaki kazi za
ofisini tena, siku nilipoachishwa kazi na yule meneja aliyenitaka....
nikamtolea nje, nikasema basi , kama kazi ni lazima ujitoe mwili wako, bora
nikaifanyie huko mitaani, huko nje,...sio huku ofisini... nitapata maslahi
zaidi lakinii sio kwa yule meneja,..mtu mwenyewe mzee halafu, sura mbaya...’akasema
huku anacheka.
‘Eti sura
mbaya, hivi hawo wanaojiuza huko mitaani wanaangalia sura....si maslahi
tu,.....lakini hata hivyo ukiongea hivyo uanataka kusemaje,....., ujue mimi ni
mwanaume, kama lengo lako ndio hilo,....sijakuelewa hapo, maana hata kama pia
ni pesa, sina pesa kama ni kuhonga au sijui kujiweka vipi....sasa nifanyeje..?’
nikamuuliza.
‘Dunia hii
usipokuwa mjanja utalala na njaa, cha muhumi ...nikupe maarafa...eehe,...
nyumba, ukiwa na nyumba, halafu una hati miliki, .... ukatumia akili yako
vyema, hulali njaa, hata siku moja...tatizo lako hutakii kutumi akili yako
vyema, nikuambie kitu...hii hapa ni nyumba yako, una hati una kila
kitu...kwanini huiweki bondiukapata mkopo benki...?’ akaniuliza.
‘Nyumba....ungelijua...’
nikatulia na kuwaza, kwani alikuwa hajajua kuwa nyumba hiyo ipo tayari kupigwa
mnada, nilikuwa nimemfica kabisa, nikasema;
‘Lakini
hata hivyo mkopo una masharti yake, unaweza ukauchukua ukaishia kunywewa tu
sasa mimi sitaki kurejea huko, nakunywa, lakini sitaki niwe mlevi
tena....’nikasem ahuku nikiwa sina raha, maana aliponigusia nyumba, nikakumbuka
kuwa wale wapiga mnada wa nyumba za wadaiwa sugu wamenipa miezi mitatu tu, niwe
nimelipa deni la watu....miezi mitatu tu...nikawaza....na hiyo inaishia.
‘Sasa
unasemaje.....?’ akaniuliza kimwana.
‘Miezi
mitatu ..nimepewa...’ nikajikuta nikisema.
‘Miezi
mitatu tu, yaani uchukue mkopo uurudishe kwa miezi mitatu tu, sio mbaya nenda
kachukue mimi nitakuonyesha jinsi gani ya kuuzungusha, nakuambia ukweli, ukiwa
na akili,utakuwa tajiri...’akasema huku anaiagalia nyumba kwenye paa,
akizungusha kichwa hku na kule .
‘Hivi
nikuulize na wewe kule ulipokuwa umepanga niliona vifaa vingi vya thamani,
umemuachia nani hivyo vifaa..?’ nikamuuliza, na swali hiloo likamshitua kidogo na mara ghafla akainuka na kuchukua mkoba
wake.
‘Swali zuri
sana lakinii sasa nina miadi na bosi mmoja...., huyo najua atatupa hela ya
kutusukuma hadi mwisho wa mwezi na akizubaa, ataingia choo cha kike, wewe
tulia, ngoja mwanaume nikhangaike, unajua mimi watu wanafikiri ni Malaya,
hapana mimi ni mjanja,... mwili huu unakuwa kivutio tu, lakini mwisho wa siku
inakuwa akili kichwani mwangu, ni kama kutamani ndizi, ...lakini kuila huili
kamwe, wanakula wengine ndivyo
ninavyowafanyia hawa wakubwa...’akasema.
‘Eti nini mbona
sikuelewi, wewe umeniambia kuwa una dili zako za kibiashara, hukuwahi kuniambia
kuwa unauza mwili...au sikukusikia vyema...huko kwa huyo bosi unakwenda kufanya
nini..?’ nikamuuliza kwa hamaki.
‘Nimeshakuambia,
akili zitumie vyema, unafikiri hata hawo wanaofanya kazi maofisini pesa
zinawatosha, haziwatoshi, lakini utashangaa wanaojenga majumba mazuri kwa sasa wengi kwasasa ni wanawake....na
wengine hawana waume, ni nini wanatumia, nia akili...mwili huu ni kitega uchumi
tu...lakini hauuzwi...kama mtu akitaka kuona ndani atakuwa an ujasiri wa hali ya juu sana kama wewe...hakuna mwingine...' akanisogelea na kunikumbatia akilala kifuani kwangu.
'Sasa tutaliongea hilo baadaye, wewe nenda
kauchngamkie huo mkopo, chukua hati ya nyumba, kaongee na mameneja kweney
benki..mkopo upo nje nje....’akasema huku akijirmba mdomoni.
Maneno ya
mke huyu yalianza kunitia wasiwasi, inawezekana kweli ni changudoa,na mimi
ananitumia tu, lazimanimchunguze, haiwezekani, kwanza alishaniambia nikimuoa
atajituliza na kuwa mke mwema, sasa kila siku anaaga kuondoka, ...lakini hata
hivyo asipoondoka, tutakula nini....nikajiuliza bila jibu...wazo likanijia kama
mke wangu huyo kule alikuwa na vitu vya thamani na sisi hatuna kazi, kwanini
tusiviuze baadhi ili tupate pesa.
Kwangu
nilishauza karibu kila kitu na gari ambalo tunalifanya kama taksi bubu, nimeliweka
rahani, ina maana ikipita muda wa deni gari, sio langu tena, nyumba sio yangu
tena, nitabakiwa na nini...Nilipofika hapo nakatoka na kuingia mitaani. Mkaa
bure sio sawa na mtemeba bure, tembea tu hata huna kazi huenda ukaokota,...
*********
Nikafika
mitaa ambayo kimwana alikuwa akiishi, nilioana nifike hapo kutizama vifaa
vyake, na kujua nani anaishii hapo kwasasa, maana vile vifaa mle ndani vilikuwa
vy athamani, sizani kwamba aliviuza vyote kabla ya kuja kwangu, ...
Nilipofika
pale, nikakumbuka jinsi nilivyoibiwa gari langu , nikajikagua mfukono, maana
hapa pakumbusha mengi, halafu nikagonga mlango...kwa mbali nikasiki kama mtu
anaongea, au wanaongea an sauti ya runinga,...nikajua kuna mtu anaisha hapo
kwasasa, isije ikawa ni mshikaji wa mke wangu wa siri, leo nitapambana naye...
‘Halloh,
mpenzi, karibu, unahitaji huduma....au sio,halafu umependeza kweli, na hapa
ukitoka, jasho lote litakuwa limekauka, kuna maji safi ya kuoga, ni mpango wako
tu...’sauti nyororo ya kimwana ilifanya masikio yangu yaingiwe kiwi, na jinsi
alivyovaa, ni heri tu angeacha kuvaa, gauni ipo karibu kuonyesha chupi...
‘Huduma....namulizia
...mmmh, hapa alikuwa akiishi kimwana,au sio..?’ nikajikuta nikigwaya.
‘Swali
kabla ya jibu,nimekuuliza kwanza unahitaji huduma, maana muda nii mali, anaweza
akaja mtu mwingine,akazania unahitaji huduma, akaondoka, ukanikosesha
bahati...kama unahitaji huduma,karibu ndani, lakini, kila kitu ...’akaonyeshea
vidole kwa ishara , ambayo inamaanisha pesa....
Nikabakia
bado nimeduwaa, nikaangali mlango kwa juu kuwa huenda kumebadilishwa na kuwa
sehemu ya huduma fulani, lakini mimi sikuwahi kupitahapo karibuni, nilipoona
hakuna maandishi yoyote nikamtizama yule kimwana, akajirembua....
‘Mhh,
wanionaje, .....kwani una ngapi wewe....maana nisje nikaitupa bahati....wewe
sema una ngapi, ulicho nacho kinaweza kikakusaidia hata chapu chapu....ongea
wewe mwanaume usiwe kama demu bwana, kasema na kunsihika sehemu za
siri...nikaruka kwa nyuma..
‘Vipi
wewe...unataka kunifanya nini, nimekuja hapa nikiwa na maana ya kuangalia vifaa
vya mke wangu, Kimwana, alikuwa akiishi hapa kabla, wewe unaleta mzaha,...unafikiri
wanaume wote ni wakutaniwa,mimi nina mke wa maana, sio kama ....kwanza wewe ni
nani kwake...’ nikauliza kwa hasira.
‘Mimi ni Kimwana
pia,...ukipenda niite Kisura....nani mwingine kimwana zaidi yangu...sikio wewe
lofa, kama huna kitu ishia na usije tena hapa kunipotezea muda wangu...mijanaume
mingine bwana utafikiri waume kweli, kumbe milofa...haya ishiia usije ukanifukizia
kibosile wangu yupo njiani anakuja...hata hivyo umeshanitilia nuksi za mapema,watu
kama nyie mkifika hapa wa kwanza mnaharibu siku nzima....aah...’akaubamiza
mlango kwa nguvu na mimi nikageuka na kurudi barabarani.
‘Vipi
ulikuwa unapata huduma nini..?’ mara nikasikia jamaa akiniuliza nyuma yangu, name
bila kugeuka kumwangalia nikasema;
‘Huduma....kuna
huduma hapo, ni kuchanganyana tu, kwanza huduma gani hiyo unayozungumzia, maana
hata yule binti pale kaniuliza nataka huduma...kwani pale kuna huduma gani?’ nikageuka
na kuangaliana na huyo jamaa, alikuwa kabeba nguo za mkononi, ni mmachinga.
‘Wewe
unauliza kuwa kuna mate mdomoni...au wewe wakuja nini, ..maana watu kamanyie
ndio mnalizwagwa....pale kuna huduma maalumu, huwa wanakuja machangu wenye
nazo, wanakodi kwa masaa, wiki na wengine hata kwa mwezi,....kwa ajili ya kutoa
huduma....hahaha, ulikuwa hujui wakuja eehe..’akaziweka nguo zake vyema na
kuniangalia kwa hamu.
‘Mimi sio
wakuja bwana....wewe unafikiri utajua huduma zote hapa Dar, huna kazi nini, iwe
kazi ya kujua kila kitu kinachofanyika hapa Dar....’ nikajitetea.
‘Nimeshakujua,
hujuii huduma hiyo ni kitu gani, ...ukija mwanaume na vihela vyako, unahudumiwa
pale, hakuna longo longo, hakuna eeh, nakupenda sana, hapana, hapeendwi mtu,
inapendwa pochi yako...ukizubaa, unachukuliwa jumla jumla, na mwisho wa siku
tunakukuta mitaani ukiokota makopo...kuna laana pale....’akasema huyo jamaa
akaelekeza macho yake kwenye ile nyumba.
‘Mhh,
siamini...kipindi fulani alikuwepo msichana mmoja anaitwa Kimwana, ....sasa kaolewa,
alisema kapanga hapo, na...’nikaanza kuongea.
‘Hahaha...sasa
kaolewa, maajabu,huyo kampata lofa, ...kaolewa, wanaolewaga hawo ....mmh,
visura...sijui labda...maanake huwezi jua ya mungu mengi.....’akaguna na
kuziweka nguo zake vyema, na akawa kama anawaza huku akingalia pale kwenye jingo,
akasema;
‘Pale
majina yao ndio hayo visura,vimwana, mrembo..., ukifika pale wote wanajiita majina
hayo, ila leo yupo huyu,kesho yule.....lakini hayo yote ni majina ya bandia,....kweli
ni warembo wamejichubua utafikiri wazungu....na wapo wana urembo wa asili,
wazuri huwezi amini, ...lakini kama wesamavyo wehenga, sio vyote ving’aavyo ni
dhahabu, chunga sana, utalizwa....’akasema jamaa yangu akizichambua nguo zake
kama vile ananionyesha ipi bora nichague.
‘Unajua wengi
ni mabinti waliotoka hukoooo,makwao, labda wameshindikana, labda,....hatujui,
tusema hatujui , ....wakifika hapa bongo....wanachofanyalabda kwa kuelekezwa,
au kwa kunaswa na maisha au kwa kupitia mawakala, wanaingia kwenye shule ya
huyu mwenye haya majumba, wanafundwa kisawasawa,...unajua kufundwa wewe,
hkokwenu mnaitaje, unyago, au...?’ akaniuliza akiniangalia kwa makini.
‘Sijui nini
unachoongea....’nikasema huku nikiiangalia ile nyumba, na huku nikimuwaza
kimwana wangu, maana siamini,...ina maana hata yule binti mrembo anafanya
....hapana kwanini...siamini...
‘Siamini....’nikajikuta
nikisema.
‘Huamini
nini hapo.....wale wapo kazini, ...sasa sijui tafsiri sahihi ya kazi ni ipi, maana
unaonekana msomi kidogo...hebu niambia wale wanasema wapo kazini, maana mwisho
wa siku wanapata mshiko wao, kwa vipi, ....hebu kwanza nikupe jinsi inavyokuwa
kwa hawo vimwana, ...kamahuyo kimwana wako, .....’akaweka nguo zake vizuri na
kuiangalia machoni.
‘Wakikutana
na huyo mwanamama, wenyewe wanamuita Docta....sio Docta wa hivi hivi,
....kaisoema hiyo fani na ana mashahadanamadigrii,sijui na maprofesa....anamjua
bindamu, anaijua hisia ya binadamu, anajua tabi na maumbile ya bindamu,
kivitendo, kihisia, ...’akasema huku akifikiria neno jingine la kuongezea hapo,
na mimi nikaingiwa na hamasa ya kutaka kujua..
‘Kwahiyo ni
mwalimu,...akiwapata hawo mabinti, kwanza sifa ya kwanza ili uwe mwanafunzi,
...uwe mrembo, na kamahujakamilika,unatengenezwa....huwezi kumjua
akishatengenezwa, hutaamini,...halafu anaanza kufundwa....nyie kule mnaita
unyago, lakini tofauti yake, ni kuwa unyagoo huo sio wa amlengo ya kuishi na
mume na mke.....unanielewa hapo...’akaniangalia kwa makini, lakini mimi
sikumjibu nilikaa kimiya.
‘Anafundishwa
jisni ya gani ya kumpagawisha mwanaume,
...na siri za uzaifu wa wanaume...unafikiri wanaume tuna kitu sisi,....kitu
kidogo, eeh, ooh, wewe ni kila kitu, chukua zote, unatoa mihela yako yote...ni
kushindwa tu kwa wanawake kutujulia, wangelikuwa wanaijua hiyo siri, mwanamke
angekuwa anatamba katika hii dunia....’akaanza kunifunua ubongo huyu jamaa
anayeonekana kuijua sana sehemu hiyo.
‘Ina maana....kumbe,
wana.....lakini inakuwaje mpaka mwanaume asijijue, ..kwaninii sisi ni wajinga,
hapana, lazima kuna dawa wanatumia kumpagawisha mwanaume.....?’ nikauliza.
‘Hakuna
dawa kabisa...ni hayo manjonjo tu...ndio maana nakuambia kuwa wanawake wetu
wangetujulia, kusingekuwa na hiyo wanayoiita mfumo dume....wana silaha kubwa mungu kawajalia,lakini hawataki
kujifunza, wakishaolewa basi, wanajua wamefika,...kazi yao kupika,
kufagia..umbea..huku wenzao wanawasoma...na wanaweza wakaja kwako kama rafiki,....nikupe
hiyo mapema..’akasemana kuniangalia kwa makini.
‘Akikutana
na mkeo, anamdadisi, na udadisi huo
unalenga maswala nyeti....kuanzia ofisini, hadi chumbani...kuna mambo
wameshafundishwa, wayajue, wakishayajua,kazi ni ndogo kwao, wanakukokota kama
mbwa anavyojipeleka kwa chatu,.....mwisho wa siku unasema dawa, dawa...hakuna
daa hapo, ni akili....usicheze na binadamu, nakuambia, binadamu nikiumbe wa
ajabu kabisa....’akajionyeshea kwa kidole kichwani mwake.
‘Wenzenu
kila kukicha wapo kwenye maabara, sio lazima maabara ya madawa, ya kutafiti
ugonjwa, lakini pia kuna maabara ya kumtafiti binadamu, na hidia , hulka na
nyendo zake....wanakuchambua juu chini, ...akikuangalia hivi tu, keshakujua
udhaifu wako...mwishowe unasema ooh, mazingaumbwe, oooh, wachawi..ooh, dawa,
ooh, limbwata..hakuna, ni akili kidogo tu...’akasema na kuchuchumaa .
‘Sasa huyo
mama anapaat faida gani....sio kwamba anachumamazambi tu...’nikasema
‘Ndugu
yangu wee, matajiri, na utajiri, unanuka zambi...pesa ndio ibilisi wetu mkubwa,
pesa imewafanya wengi wakasaliti, na hata vitabu vikubwa vimeandika, ila sitaki
kwenda huko....ukisema nikifanya hiki nitapaat zambi, ni wewe na imani
yako....mwenzako hamjui wala kuamini hayo....dini yake ya mali, ...mungu wake
ni pesa...eti zambi..shauri lako, kaa na imaniyako hivyo hivyo...’akainuka kama
anataka kuondoka, lakini hakuondoka.
‘Kuhusu
huyo mama anapata faida gani, ....ni mfanyabishara, ala leseni na analipa kodi,
kwa kukodisha majengo yake....mengina nini kinafanyika, yeye hajui....akili
kichwani mwako, ...kitu anachofanya ili kufanikiwa zaidi ni hivyo kuwa
anawafundisha hawo mabinti,kwa nakubaliano ya siri....mwisho wa siku atakata
hela yake sijui, au ndio anajua kuwa ataipata kwenye kodi.....’akatulia kama
anawaza.
‘Sasa huyo
mama mwenye mijumba, kasoma, na kumjulia mwanaume, yeye sasa anatumia huo ujuzi
kujiingizia hela, yeye kakaa kwenye kiti chake tu , na hata watu wa kodi
wakija, anasema anafnya biashara ya nyumba, kukodi nyumba, ...unaweza ukaita
nyumba za wageni, lakini kinaman iliyojificha......kodi zinaingia.....wanalipa
hela nyingi sana kukodisha hapo....mama anatajirika,docta anaheshima
zake...kwenye ngazi za juu, ana sifa ya mtetezi wa akina nani.....utajaza
mwenyewe....’akaniambia huyo jamaaa.
‘Wewe sasa
umejuaje hayo...?’ nikamuuliza.
‘Mimi
nimejuaje hayo,... kwasababu mimi ni mtoto wa mjini, nimesoma ahdi chuo kikuu,
lakini sio cha kukaa darasani,..akili iliyopo hapa ingelikuwa Ulaya au Marekani
ningeliitwa docta....naujua kuutumia mdomo, najua mengi, nasikia mengi na
nawajua watu...wenzako wanaonijua wananitumia,naitwa mtaalamu wa kujua mengi..mwanzoni
nilikuwa wakala wa huyo mama...baadaye nikaona ni ushetani....nikajitoa....’akaniangalia
kwa makini halafu akacheka.
‘Unajua
nimekungali na kukupima kwa makini..nimegundua kitu, na wewe umelizwa, nina
uhakika huo, semausaidiwe...maana unavyodadisi naona kabisa umeshaingia mkenge,
na ukinaswa ni kama ulimbo wa kumtegea ndege.. ukinaswa hunasuki, umenaswa....?’akaniuliza
akiniangalia usoni kwa mshaka.
‘Hpana, ila
huyo dada niliyekutajia, namfahamu sana,....huyo ninayemzungumzia, nilimfahamu
kwa jina hilo la kimwana nilifika hapo kwake na akaniambia amepanga hapo siku
nyingi,...nilimshangaa maana sizani kama alikuwa na uwezo wakununua vifaa vya
tahamani kama vile na kupanga nyumba kubwa ya thamani kama hiyo, tukaongea
tukaachana, tulipnaga tukutane humo, sasa hayupo, namkuta msichana mwingine,
ana jina hilo hilo...’nikasema
‘Hivyo
vifaa ni vya mwenye hizo nyumba sio moja tu,...anazo nyumba nyingi seehmu
tofauti....hivyo vifaa kavinunua kwa pesa yake, na anavibadili kila siku ,
kwahiyo ukifika hapo utakuta mabadiliko ya mara kwa mara...kutokana na watu wake, na ni moja ya mipango
ya kuwavutia wateja,na kuwahadaa mijanaume isiyo na wake, na hata kama ina
wake, haitosheki na hata kama
inatosheka, lakini ni limbukeni, wakilegezewa basi, wamelainika....mijitu haina
akili ya kufikiri....mimi kama ningelikuwa na uwezo wangu, ningeichapa midume
ya namna hiyo viboko....’akasema huyo jamaa.
‘Lakini
siumesema ni utaalamu wa shule kidogo uliotumika, ina maana hawo vimwana
waliwekwa mahala wakapatiwa shule na nini siri ya kumpagawisha kidume, ina
maana wamesomeshwa, na wakamjua mwanaume, na mwanaume hajijui, ...na matokeo
yake alipoguswa huko...akajiona kama kafika sehemu ambayo hajawahi kufika,na
hakuwahi kufikishwa na mke wake au sio...mimi sioni kuwa ni ujinga....’nikasema
kama vila najitetea.
‘Ujinga,
huo ni ujinga ...kwanini hukukaa na mkeo mkaongea,na kumwambia mwenzako vipi unataka iwe,....ni kama chakula,
au wali , unaweza ukautengeneza ukaonekana wa ajabu, kutoka hali fulani
inayojulikana na kuwa tofauti, mfano wali
hadi pilau, hadi biriani, lakini ni wali ule ule...mkafundishana, ....mtaona ni
kitu cha ajabu sana...lakini hamtaki kukaa na kuongea, matokeao yake ndiyo
hayo...watu wajanja wamegundua, sasa wanachuma, watu wanaumizwa...sijui mpaka
lini, watu wanalia na ndoa zao, hawaelewi sababu ni nini ..’akatikisa kichwa.
‘Nikuambie
ukweli, mapaka wakijua tatizo ni nini huyo mama atakuwa tajiri wa kupindukia,
na mwisho nasiki anafungua hospitali, au sehemu ya ushauri nasaha wa maisha ya
ndoa....sio bure, ni pesa..hayo walikuwa wakifanya mabibibi mashangazi,
....unyagoni, ..siju wapi, lakini tumeyazarau, ....tunawazarau hata hawo
mabibi..mashangazi...matokeo ndiyo hayo....’akasema na kukuna kichwa.
‘Tunawazarau
kwa vipi...?’.nikauliza
‘Utaoaje,
hujui ndoa ni nini,....lini mtu akaendesha gari bila kujifunza...lini mtu akawa
docta bila kusoma shule, kwanini hatuisomi hiyo ndoa ni nini....nini cha muhimu
na nini kinatakiwa nimfanyie mwenzangu,ili....hapa ujue kuna mambo mengi ya
ndoa, lakini kuna jambo kubwa limesahaulika, ambalo ndilo kiini cha
ndoa....hata wenyewe wanaita...mmh, la ndoa....’ akaguna na kunionyeshea kwa
kichwa kule kwenye hiyo nyumba na tukawa kimia kuangalia nini kianendelea huko.
`Unaona
mambo hayo, sio mchezo wewe sikia tu...’akasema huyo jamaa akiangalia kule
mlangoni wakati gari la kifahari likisimama mbele ya mlago na jamaa mmoja,
aliyevalia suti yake ya kifahari, akatoka harakaharaka na kuingia ndani ya ile
nyumba,....mlango ulishafunguliwa mapema, ilionekana alishawasilina na huyo
kimwana auache wazi maana gari lilifika, mlango wa gari ukafunguka haraka, na
mtu akatoka na kuingia ndani ya nyumba haraka, na lile gari likaondoka haraka,
lakini tulimuona alikuwa mtu mzima tu, tena anaonekana ni mheshimiwa...
‘Unaona
wanaoingia hapo ni watu wazima,watu wazito, watu wenye wake zao.....sasa
jiulize wake zao wanayajua hayo, hawajui, na kwanini inatokea hivyo.....akili
ni mali....’akasema na kushika kichwa kwa kidole.
‘Ndio maana nika kuambia midume humu hakuna,
....mimi ni mwanaume, lakini nilikuja kugundua hilo...wanawake wanaweza
wakatuchezea sana wakitaka..na sisi midume na akili zetu mbovu, tunatamba
mitaani maofisni, wapi kuwa mimi sibabaishwi....nyumbani ukifika hakuna
kitu....siri ya mtungu aijua kata, ndio maana nasema ni heri tuchapwe
viboko....’akasema.
‘Kweli tunastahi
kuchapwa viboko....na hata hivyo haina haja ya kuchapwa viboko kama fimbo,
dunia yenyewe itatuchapa viboko...’nikasema huku nikiwa nimenywea na kujiona
kweli sina akili na kwelii nastahili kuchapwa viboko...
Baadaye
jamaa aakondoka akitafuta wateja wa nguo zake, na mimi taratibu nikaondoka pale
nikiwa nimenywea kama mtu aliyemwagiwa maji, nilitemeba nikiwa kama sio mimi,
...na baadaye nilijikuta nimeshafika nyumbani hata bila kujijua ,....nilipoikaribia
nyumba yangu nikaiangalia vyema huku moyo ukiniuma, ina maana kesho tu wajamaa
wa kupiga mnada wanaingia....nyumba hiyo inakwenda, na gari hio linakwenda,
sasa nifanyeje, ..akili ikanijia....
Lazima
nyumba hii niitafutie mteja chapu chapu, mjini hapa.....na hata gari nitaliuza
kinamna...’ nikasemana kushika kitasa cha mlango...nikakuta mlango unafunguka...upo
wazi, nikajua mke wangu keshafika, nikajitahidi na hata kupiga mlunzi kama vile
baba mwenye nyumba umefika, na unahitaji mke aje akupokee...
Kwanza
nilisikia sauti za ajabu ajabu chumbani....na baadaye vicheko vya
....nikashituka, kwanza kwa hasira nikaangalia huku na kule, nikakipata kisu,....mwili
uakanichemka,zilehasira zilizokuwa zimejificha zikafumuka, .....nikatamani
kuua, .... kwa haraka nikakimbilia mlango wa chumbani...nikausukuma kwa
kishindo....
Je nini kilitokea....tuwepo kwenye sehemu
ijayo Ijumaa njema. Nawashukuru sana waliochangia, nilitaraji kisa hiki
wangelichangia wengi, hasa wanandoa,....lakini sio mbaya :Tupo pamoja
WAZO LA
LEO: Binadamu ni kiumbe wa ajabu sana, huwezi kumdhibiti, huwezi jua nini
anakiwaza, na kila siku kuna matendo ya ajabu ajabu yanayotokea duniani na
anayeyafanya ni biandamu, nafikiri hata shetani atakuja kuturuka na kusema ‘hayo
mimi sikuwahi kumfundisha huyu binadamu,hata mimi nashangaa nijawahi kuwaza
hivyo....kwani wahenga walisema `ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Frauni..
Ni mimi:
emu-three
8 comments :
da m3 makubwa sana yamemkuta huyu jamaa mtu unaweza kupata wazimu
mkasa unavutia sana tatizo binadamu wapo tofauti wengine wakingangania kitu huna la kuwambia mpaka yawakute ndo wanaambilika saa nyengine ndoa ndoana
any away tupo pamoja
Duuh, hii kali, lakini sio wanaume wote wanaoweza kunaswa...ni kila mtu na tabia yake.Tutakupigia kura muda ukifika
M3 kama ulivyosema ,binadamu ana mambo makubwa na moyo wake ni kama kichaka ,hujui awazalo wala anapanga nini juu yako, kwenye ndoa tumetokewa na mengi japo kila mtu ana lake. Mmh wengine ni imani tu ! Kwamba Mungu ni mkuu,anatulinda na kutuongoza, kuna wakati mlango mmoja unafungwa ,tunapoteza muda mwingi na kujuta kwa ajili ya mlango mmoja uliofungwa na kusahau kuangalia mbele kwenye milango saba iliyo wazi.
Wikiendi njema wapendwa.
Tuchangie nini kaka yangu, maneno yametuishia kwani umemaliza kila kitu. Yaani vijana wengi hasa wa kiume wanaingia bila ya ndoa bila kufundwa kuelimishwa ndoa ni nini na niyepi yakufanywa ndani ya ndoa na ni yepi hayapaswi kufanywa ndani ya ndoa, matokeo ndio kama hayo.
Na hata wanawake pia wanaingia ndani ya ndoa kwa kufuata mkumbo tu, fulani kaolewa ngoja na mie niolewe. Wako wanaofundwa lakini hayo mafunzo yanaingia sikio la kulia na kutokea la kushoto. Mimi nikirudi Bongo nitafungua kliniki ya ushauri wa masuala ya ndoa/mahusiano, kwani nimefanya utafiti kwa muda mrefu kwenye suala hili na sasa ninaelekea ukingoni. Hii bwana weka kwenye kitabu ili kisomwe na wengi walau inaweza kuwafungua watu macho.
Samira nikweli asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
Kweli kuna blog iitwayo Tanzania Blog awards humo kuna kupigia kura blog kutokana na vipengeel vilivyowekwa, nawaomba muipigi kura blog yenu hii, ni moja ya kuitangaza.
Na kweli Elisa, ndoa ndoana, yaliyopo kwenye ndoa, ayajuaye ni mwana ndoa mwenyewe.
Anon. 31 March 2012 9:22 AM, Umeshachangia, uliyonena ni mchango mkubwa sana tunakusubiri sana uje utupe utafiti wako ili uziokoe ndoa za watu.
Na wengine wote TUPO PAMOJA DAIMA, nawashukuru sana kwa maoni yenu na kuwa pamoja nami, ....mbarikiwe sana
powerful material Cl. Salt provide is enthusiastic, not hot, release with your entropy.
If you privation to score a purchase with them.
Registering ordain encourage you strike fatty tissue.
The adrenal cortical steroid secretion is produced through emphasise.
This internal secretion makes your limit fresh freshby mailing on cultural media.
Canada Goose Jacket Canada Canada Goose Outlet
a news story, don't let a losing positions so you can intercommunicate the seller may say,
valuableness occupied adornment. No content what the seller straight off.
score certain to cater. Do national leader search on your act-about?
When you go out of your determine judge, is
practically easier to get discounts on foreordained products.
Also visit my web-site :: Canada Goose Coats
I really like your blog.. very nice colors & theme. Did you create this website yourself or did you hire someone to do it for you?
Plz reply as I'm looking to construct my own blog and would like to find out where u got this from.
kudos
My homepage ... The Price Is Right Manuela's Blooper
I’m not that much of a internet reader to be honest but your
blogs really nice, keep it up! I'll go ahead and bookmark your website to come back later on. Many thanks
Post a Comment