Mke wangu
akawa keshaondoka kurudi kwao, na nilibakia na wazazi wangu, ambao hawakutaka
kabisa kunielewa, na hawakuamini kile kilichotokea na walitaka kujua kwanini
imetokea vile, ...kila sababu niliyowapa haikuwatosheleza, na mwishowe
wakanishauri kuwa nifike huko kijijini nikaombe msamaha yaishe, lakini mimi
niliwaambia waziwazi, kuwa sihitaji kumuomba msamaha mtu yoyote , kwasababu
yeye mwenyewe anajua kosa lake, nikasema bila aibu
‘Yeye ndiye
alinisukuma hadi nikafikia huko,....nimejaribu weee....hapana ,sasa nimempata
mtu angalau, hata kama hamtakubali hayo, ....basi ndio hivyo na iwe hivyo....’
nikajitetea hivyo.
‘Mwanangu
unakumbuka wakati unataka kumuoa huyu binti, nilikuambia wazi,...kwanza
hakulelewa katika mazingira mema, kama ulivyokuwa kumuona, anahitaji muda
kujifunza kila kitu unachokihitaji, na hatuelewi hizo sababu zako zina msingi
gani...hazina mshiko....ni aibu tupu kamawakisikiawazee kule kijijini...kwa
ufupo wewe ndiye uliyeshindwa majukumu..’akasema baba.
‘Mwanangu
tulikuambia na kujaribu kuzuia ndoa yako, hatukupenda kabisa mtoto wa watu aje
kuumia tena...unakumbuka, tulikuambia hakikisha kweli unamuhitaji, kwani yule
binti kaumia sana katika maisha yake, hatukupenda kabisa aishie kwenye maisha
maisha ya taabu tena...mimi nilibeba
hiyo dhamana toka kwa mrehemu mama yeke, na hapa nilipo nashika nafasi yake
kama mama yake...tafadhali mrudie ukamuombe msamaha...’akasema mama..
‘Kwani mimi
nilimfukuza, kila kitu anapata, chakula nyumba hiyo hapo , alikuwa anapata,...aje,
sijamfukuz amimi, lakini inavyoonekana anajitia kiburi, unaona alivyofanya katimukia
huko kwao, sijui kwenu au sijui kaenda wapi, au kwa mwanaume mwingine. Ili alipize
kisasi...sijui...yeye mwenyewe atalikoroga,...sina uvumilivu mimi,...kwa
mtizamo huo aspoangalia mimi nitaoa mke
mwingine...’nikasema bila kujali..
‘Umechanganyikiwa
mwanangu na nani huyo mke mwingine ndiye huyo uliyekuwa ukizini naye...?’
akasema mama kwa hasira.
‘Kwani
tofauti ipo wapi mama...mimi huyo naye nampenda,na anajua nini
ninachokitaka....mama unajua katika msiah haya ya ndoa nimejifunza mengi,mimi
sikuwa natakiwa nikurupuke kuoa, ilitakiwa nifanye uchunguzi wangu mwenyewe,...nifanye
majaribio kwanza, mwisho wa siku ningelijua yupi ananifaa...’nikasema bila aibu
na mama akaniangalia kwa chuki.
‘Usinichefue
wewe mtoto, unafikiri wanawake ni watu wa kufanyiwa majaribio, ina maana huyo
binti hafai...hapana, kuna kitu hapo....’akasema mama kwa hasira.
‘Mama sio
kwamba huyo mke wangu hafai,lakini tabia zetu zimekwua tofauti, hisa na
mapendeleo yangu yawe vipi, ...mama samhani kusema kuwa, yule amekaa kishamba
shamba sana, na mimi naishi mjini....unaoana alitakiwa kujifunza hivyo....lakini
mengine hataki mimi nifanyeje....’nikasema.
‘Haya
kamahutaki kwenda kumuomba mwenzako msammaha, sisi itabidi tukafanye hivyo,
maana taratibu na mila zetu, tendo ulilofanya ni baya na faini yake ni kubwa,
na inategemea huyo bintii atakusamehe au la...kwasababu ushahidi kila kitu
kimeoenekana wazi....’akasema baba.
‘Sikilizeni
wazazi wangu, kama mnataka kufanya hivyo, mimi siwakatazi, na mwambieni huyo
mke wangu, yupo huru kurudi hapa, mimi sijamfukuza....kama hataki basi, sina
jinsi....’nikasema na baadaye wazazi wangu wakaondoka.
*********
Nilibakia
ndani na kujiona mpweke, nikawaza mengi, na kun amuda akili inanijia na
kujialaumu, lakini sijui kwanini, mawazo tu yalipokwenda kwa huyu kimwana,
akili ikaruka na bila kupoteza muda nikakurupuka
mbio mbio nikamwendea huyo kimwana,...
‘Vipi mambo
yameendaje, mke yupo nyumbani....maana wanawake wa kijijini wavumilivu hata
uwatendeeje, hawabanduki, nakumbuka mama yangu alikuwa akiishii na baba, baba
alikuwa mlevi kupindukia, akirudi anafanya maajabu, anampiga mama....lakini
mama anakubali tu, na hata kumfulia matapishi,au awakati mwingine kwasababu ya
ulevi, anapitiwa na haja...aah, mimi siwezi kabisa..’akasema kimwana.
‘Ina maana
na mimi nikiwa hivyo utanikimbia.....?’ nikamuuliza.
‘Ikizidi sana ...., kulewa sio mbaya, hata mimi nakunwa, lakini sio ulewe na mipombe yako iwe kero,...iwe mipombe ya kupigana, .... uje unipige....hapana, tutapigana, mimi hilo ulijue wazi,....siwzi kuw
amtumwa, kama nikupendana tupendane,kama tunageuza mapenzi uwanja wa ngumi,
tutazichapa...ehe,,haya niambie imekuwaje..?’ akasema huyo kimwana.
Nikamuelezea
ilivyokuwa na jinsi nilivyopagawa nikamuelezea kila kitu,....sijui akili yangu
muda ule ilikuwaje,sikuwa hivyo kabla....nilikuwa kama mjinga fulani.
‘Sasa
unajua mimi name nimetafakari sana kuhus maisha yangu, ....nimejiuiza nitaishi
hivi mpaka lini,umri unakwenda, na msiha ndiyo hayo yanabadilika, nahitaji na
mimi kutulia na kuwa na watoto wangu, kwa mtaji huo, name nasema hivi...kama
unanipedna kweli, tufunge ndoa, na ndo aiwe ya haraka iwezekanavyo...’akasema
huyo kimwana.
‘Eti
nini...?’ nikashituka.
‘Eti
nini..nikuulize unanipenda au hunipendi....?’ akauliza.
‘Hiyo
umenishitukizia, nifunge ndoaa na wewe..hapana, sio kwa sasa, unajua ndoa
lakini wewe, ukiingia kwenye ndoa, kuna masharti yake, na wewe sizani kama
unaweza kutulia kwenye ndoa....tusubiri kwanza kidogo, kwanza sijaachana na mke
wangu...mambo hayajakuwa shwari....’nikamwambia.
‘Sikiliza
mimi sio Malaya, kama watu wanavyonisema, siwezi kukaa na wewe tu, huku najua mimi
sio mke wako, kwahiyo amua moja, tufunge ndoa, au uishie zako...’aaksema kwa
nyodo.
‘Sijasema
sitaki kufunga ndoa na wewe, lakini ni mapema sana,....huoni hali ilivyo, mke
yule tumesigishana, hatujakaa na kuamua kuachana na mara nafunga ndoa na
wewe...kwanza yule ni rafiki yako mtaangaliaan vipi...’nikajaribu kujijitetea.
‘Umenisikia,
lakini....kama hutaki ndoa, basi ishia,... umenikuta na maisha yangu, ....na
kama walivyonikuta wengine na nilipowagusia ndoa wakaukata na wewe unaweza
ukaukata vile vile, mimi sio jamvi la wageni na mimi nahitaji mume nitulie...nilee
watoto wangu, hayo ndio maamuzi yangu...kwaheri nenda kafikiria ukija hapa uje
na jibu,....’akasimamia kwenye msimamo huo na akasoegeela mlango akaufungua na
kunionyeshea niondoke.
***********
Mtu mzima
niliwaza sana,nikanywa mapaka nikapitiliza, nakumbuka siku hiyo nilijikuta
nimelala kibarazani mwanyumba yangu nikiwa bwiii...na kesho yake natakiwa
kazini. Nilifika kazini nikasingizia
naumwa, na kwenda kwenye barm huko nakiutwika kisawasawa...
Nilipofika
kwa kimwana akanifukuza akiwa na msimamo huo huko wakutaka ndoa,na hakutaka
kabisa kunifungulia na alinitishia kuwa nikiendelea kukaa hapo nje ya nyumba
yake ataniitia watu kuwa mimi ni mwizi.
Ikawa kila nikienda
kwake, ananitolea nje, na siku moja nikakuta mlango umefungwa kabisa, hayupo ,
hapo moyo ukaanza kuniuma,...wivu ukanijaa moyoni, ikabidi nihangaike kumtafuta, na nilipompata
akasema anajiandaa na safari ya kwenda kijijini kuna jamaa kaahidi kumuona, na
yeye anachotaka sasa ni ndoa, ...
‘Muda wa
kuolewa umefika, sitaki kuipoteza hii bahati....wewe umeshaoa unajua utamu wa
ndoa, mimi je...kwahiyo toka leo tusijuane, mimi ni mchumba wa
mtu...’akasema looh, nikamzaba kibao, na
yeye akanirudishia cha nguvu, nikabaki nimeduwaa....
‘Wewe
unanipiga kibao mimi,...koma, kama ulivyokoma ziwa la mama..ko... kampige
mkeo...toka humu ndani kwangu, sitaki hata kukuona....’akanifukuza kabisa,
ikabidi nitoke pale nikiwa nimenywea, nikafika kwangu na kesho yake nilipofika
kazini, nikakuta barua ya kusimamishwa kazi....
‘Huu sasa
mkosi...’nikasema na kwenda kumuona mkurugenzi ambaye aliniambi waziwazi kuwa
wamenivumilia sana, na wamenionya sana, sasa imefikia kikomo;
‘Unasikia
ndugu yetu, wewe umeamua kuishi maisha yako unayotaka, ...maisha ambayo
hayaendani na maadili ya kazi, unakuja umelewa, kazini hukai, una madeni
mengi,uanitia kampuni hasara ....sisi tumechoka kukubeba, kwahiyo hiyo ndio
zawadi yako, na ukiangalia hapo, madeni yako ni makubwa hata kuliko mafao yako,
lakini kampuni imeamua kukusamehe madeni yaliyozidi, .tutakachofanya ni kukata
madeni yetu kutokana na kiwango cha pesa ya mafao yako,...na hutakuwa na
chochote kutoka kwetu, zaidi ya .....barua hii....’akasema mkurugenzi.
‘Eti nini,
hapo niatawapeleka mahakaamni, sikubali, mnataka mkate kila kitu, nitaishije
mimi....’nikalalamika.
‘Sawa wewe
nenda huko mahakamani siunadai haki yako bwana, kama ipo tutakulipa,
....kwaheri bwana, tunakutakia maisha mema, kwakweli tumejitahidi vya kutosha,
....nenda kastarehe na kimwana wako...lakini kumbuka kuwa starehe ni
gharama......’akasema huyo mkurugenzi na kweli nikafukuzwa na walinzi nikaishia
zangu mitaani....
Nilipofika
nyumbani kwangu nikamkuta yule kimwana kajaa tele, akanipokea kwa bashasha,
utafikiri sio yule aliyenifukuza kwake, na aliponiona nilivyonywea akajua kuan
jambo;
‘Vipi
mpenzi mbona unakuwa kama umemwagiwa maji....?’ akauliza.
‘Sasa mzee
mzima nimeumbuka,kazi sina....’nikasema.
‘Kazi huna,
wewe mwanaume bwana, kwani kazi ipo moja hapa duniani, nikuambie ukweli, mimi
nilifukuzwa kazi siku nyingi sana, lakini naishi, natesa raha....hapa sin
akazi, lakini sijawahi kulala njaa, ni akili kichwani...bongo hapa, wewe tesa
maisha, ukiyapatia ....maisha yenyewe mafupi, unataka kuyawahisha kabla ya siku zake....sikiliza utanioa au
hunioi?’akasema bila kujali matatizo
yangu.
‘Sasa wewe
umeshasikia kuwa sina kazi....bado unataka tuoane, tutaishije?’ nikamuuliza.
‘Kwani mimi
naishi hivi nina kazi, kwani hawo waliopo mitaani wakihangaika wana kazi
zakuajiriwa hebu jiulizei wanaishije...tutajua jinsi ya kuishi wewe usijali
kabisa..hayo maisha ya mbeleni niachie mimi, ilimradi usiniingilie,....mimi nitakulipa
fadhila zako, ili ujue kweli nakupenda, unafikiri,...hebu jiulize kwanini
nisiwang’ang’anie vipoba wanaojigonga kwangu, nakuja kwako, kwasababu nimezimia
kwako, ....wewe namimi tunaendana....unasemaje mpenzi...’akasema
‘Sawa kama
upo tayari kuishi na mimi hata bila kazi, hapo najua kweli unanipenda....sasa unataka
tuoane vipi..harusi au juu kwa juu...maana pesa sina?’ nikauliza.
‘Eti nini, Juu
kwa juu, watu watajuaje kuwa na mimi nimeolewa....acha hiyo, ngoja nikuonyeshe
njia, tutayarishe kadi, nitawapelekea marafiki zangu na wewe wapelekee rafiki
zako, siulishawahi kuwachangia,.... sasa ....sasa ni wakati wao kulipa
deni...hilo litafanyika tu....’akasema baadaye tukakubaliaan hilo.
Kweli mambo
yalijipanga, baadhi ya marafiki zangu wakanichangia na pesa ikapatikana yakutosha harusi ikafanyika, bilakujali kuwa
nina mke mwingine kijijini, ndoa ikafungwa, ...na kimwana nikawa naishi naye
ndani, siku , miezi ikapita,....
************
Siku moja
nikapokea ugeni, walikuwa mjomba na mke wangu wa kwanza, na baadaye akaja baba
na mama, walikuja kwa mabasi tofauti, na wakanikuta nipo ndani na kimwana,
akawakaribisha vizuri tu, ...
‘Huyu ndiye
nani ...?’ akauliza mjomba.
‘Ni mke
wake...’akajibi kimwana
‘Hujaulizwa
wewe binti...’akasema mama.
Mimi
nikawaangalia kwa makini halafu nikamwangalia mke wangu wa kwanza, niakasema
kwa utaratibu;
‘Hivi ni
haki mke kuondoka kwa mumewe ikapita zaidi ya miezi mitatu...aah,ishafika
sita?’nikauliza huku nikiangalia kalenda ukutani.
‘Je wewe
kwanini ulimruhusu akaondoka, ...na ukumbuek huyu mke, ulimchukua kwa wazazi
wake, na ukaahidi kuishi naye ikiwemo ulinzi na usalama wake, je alivyoondoka,ulijitahidi
kumtafuta,je ulijuaje anaishi vipi huko alipo....?’ akauliza baba.
‘Najua
alikwenda wapi, ndio maana sikumtafuta na mlipoondoka hapa niliwapa maagizo
kuwa arudi, hakurudi, ina maana alionyesha kiburi, na....maisha yangu siwezi
kuishi bila mke, na ndio maana nikaamua kuoa mke mwingine, kama huyu yupo
tayari kuishi nami tena, anakaribishwa, isitoshe, huyu mke wangu mpya walikuwa
marafiki sana....mimi sijali...’nikasema.
‘Wewe nani
aishi na...’akataka kuongea kimwana wangu, lakini mke wangu wa kwanza akaanza
kuongea kwa huzuni. Kwanza aliziba macho yake kwamikono, nafikiri alikuwa akificha machozi, akawa ananiangali kwa jicho moja kupitia kwamkono aliyofunika machoni, na baadaye akaondoa na kuaniangalia moja kwa moja , sikuja ana maana gani.
‘Mama na
baba na mjomba, nyie ni wazazi wangu, na ninawaheshimu sana, ..hali ilivyo
sizani kwamba kuna ndoa tena hapa, mimi nimekulia maisha ya shida, nimeteseka
sana, na nilijua kuolewa ndio mkombozi wangu, lakini naona ni kama kuruka mkojo
na kukanyaga kinyesi....’akasemamke wangu wa kwanza kwa huzuni.
‘Wazazi
wangu, labda ndivyo mungu alivyonipangia kuwa maisha yangu yawe
hivyo...namshukuru sana mungu, ...mwenzangu naye ana hulka na maisha yake
ambayo labda nimeshindwa kuyafikia, ...je nikiishi naye hapa yatakuwa yamefikia
huko, kwasababu mimi ni yule yule, na tabia zangu ni zile zile...unafikiri
itakuwaje ....sio kugeuka mfanyakazi na mtumwa wa nyumba hii...hapana
nisingelipenda kuwa hivyo tena.....’akasema mkewangu huku machozi yakimtoka.
‘Mwanangu
tulia, huondoki hapa, wewe ni mke halali wa mtoto wetu, tumekuozesha kwa sheria
zote,...’ ...akasema mama halafu aaknigeukia na kusema ;
‘Hebu
tuambia huyu unayedai kuwa ni mke wako mpya ulimoa kwa sheria gani, nani mzazi
wako aliyeshuhudia hiyo ndoa,....huo ni uhuni wenu mumechukuana tu mitaani na
kujifanya mumeoana, haipo hiyo...hatuitambui hiyo ndoa kma kweli ipo...’akasema
mama.
‘Ndoa zipo
za namna nyingi, kuna ya kimlia ya dini na ya bomani,....sasa mama
unatakaje,sio lazima nioe kwa seheria za kimlia...mimi na huyu tumeoana bomani,
na ndoa inakubalika, na vyeti vyetu vipo, na huyu mke ....maana nashindwa hata
kumuita mke, kaondoka kwangu miezi mitatu,...ooh sita sasa....sna inaweza ikawa
zaidi kaka huko, nitamuaminije, huenda...alikuwa kwa bwana’ke....’nikasema kwa
hasira.
‘Niombe
tafdhali....niombe radhi kabisa, mimi sio Malaya kama huyo hawara yako....mimi
nimakulia kwenye maadili, siwezi kuuzalilisha mwili wangu kwa wanaume bila
ndoa...hilo nakuthibitishia na mungu wangu ni shahidi...kwahiyo kama umeamua
kumuoa huyo hawara yako, sawa, mimi naondoka, ila nataka talaka
yangu...’akasema mke wangu wa kwanza.
‘Hilo tu,
talaka yako ipo tayari nilishaitayarisha, nilikuw anasubiri tu hizi porojo
ziishe nikukabidhi, kingine unahitaji nini, sidhani kuwa kuna maliyoyote
tulichuma pamoja, sijachuma na wewe hata kitu kimoja....ulikuwa mfanyakazi tu
wa ndani...na kuhsu mtoto, mimi nitatoa matunzo yote, atasoma, ukitaka kukaa naye
sawa, kama hutaki nitakaa naye mwenyewe hakuna shida...’nikasema.
‘Mtoto
wangu nitakaa naye, hawezi kuja kuteseka, kama nilivyoteseka mimi, hilo
lisikutie shaka, na kuhusu mali , sihitaji mali yako, unakumbuka uliponitoa,
niliweza kuishii maisha magumu kuliko unavyozania, kwahiyo kwangu maisha ni
kawaida tu, ninachowatakia ni maisha mema, na nisema kuwa, ....mungu awabariki
sana...’akatuli na kuanza kulia.
‘Unalia
nini...kama umekubali yaishe basi...’akasema huyo mke mpya.
‘Wew tuli
kule, hayakuhsu haya, ...’akasema baba kwa hasira.
‘Yananihusu
sana baba, kama hayanihusu, kwanini huyu mwanamke mshamba, alikuwa akinitukana
na kuniita hawara, au mliona mimi ni jiti tu, sina mdomo wakuongea...sikilizeni
sana wazazi..wa-ngu,mimi nina heshima sana kwa wale wanaotaka heshima yangu,
lakini mtu akinikosea,ataikosa heshima yangu, sijali kuwa ni nani, waulizeni
wazazi wangu kijijini....’akasema na kutulia kimiya akisikilizia.
‘Kwa hilo
tu tunakujau sana, wapo ulipotoka, ndio maana hatutaki uishi na mtoto wetu
utatuharibia kizazi, hufai kabisa kuingia kwenye familia yetu, hatukukaribishi
kabisa huko...’akasema baba na mjomba ambaye muda mwingi alitulia akasema;
‘Jamani
hawa ni watoto wetu, kwa vyovyote iwavyo, na makosa yametokea, na hili ni
muhimu tulijue, kuwa kama tutaendeela hivi hatutaweza kulisawazisha hili
jambo,...huyu kijana bado anajioa mdogo, na hali niliyoiona hakuna jisni ya
kumrudisha nyuma, keshaamua hivyo...labda kuna sababu zake za msingi, lakini
hazijafuata utaratibu, na sioni kuwa kuna haja ya kufuata huo utaartibu tena,
...’akatuli amjomba na kuniangalia kwamakini.
‘Kuna usemi
usemao, mtoto akililia wembe, mpe, ukimkata atajifunza, sasa wewe umelilia
wembe, sawa huo hapo...’akasema na kumwangalia kimwana wangu, sikujlai,
...nikatulia kuskiliza tu, kwakweli akili ilifungwa kabisa, nilimuoa huyo
kimwana, ni kila kitu, ...
‘Nakuambia
mjomba, mimi maisha niliyapitia, ilifikia mahala niakasema nini natafuta dunia
hii, ...starehe zina mwisho wake, na maisha haya yapo, wapo waliishi wafanya
makubwa zaidi yetu, wapo wapi....huwezi kufanya lolote likaizidi hii
dunia...tunakushauri kama wazazi, kumbuka ulipotoka, kumbuka kuwa maisha ya
ndoa sivyo hivyo unavyzania, kuwa natamani hivi , nataka hivi, iwe hivyohivyo
mara moja, ....’akasema mjomba name nikampa nafasi maana mjomba namuheshimu
hata zaidi ya baba.
‘Kweli
umeonyesha kuwa damu yako inachemka,...na sasa unataka kusihi na wake wawil,
hatukukatazi, lakini ujue kuwa maisha ya wake zaidi ya mmoja yana masharti
yake....siotu kujiolea...masharti yake ni magumu ndio maana wengi wanashindwa
na hata walio-oa, waulize vyema, nini wanachokipata...hukatazwi oa wake
upendavyo, laini ukumbuke kuwa na wao ni biandamu,wanstahili zao, uwatendee
wema na adilifu, je utaweza hilo...?’ akauliza mjomba.
‘Mzee wangu
samahani kwa kuingilia, na huenda tukajadili haya mapaka kesho, wakati swala lipo wazi, kwanza ndio imeshafungwa, mimi ni mke halali, pili kwa kauli ya mume wangu,keshamuacha mke wake wa kwanza,kkwahiyo hapa tuzungumzie ndoa yangu sio ya wake wawili,...'akasema huku akitabasamu kwa dharau.
'Hivi wewe unaongea nini...'akasema mama.
'Ndio mama, huo ndio ukweli, ...ujue kuwa huyo mwenzangu keshaachika, na mimi ndiye mke halali....hukusikia alivyosema mume wangu ...au rudi vyema wasikie...sio nashnikiza iwe hivyo, hapana ila kauli ya mume wangu ndiyo ya msingi...’akasema mke
wangu huyo mpya.
‘Nani
kakuambia hayo wewe unafikiri ni rahisi hivyo....tulia kwanza wakubwa waongee,
na ujifunze kuishi na wakubwa, umeshasema kuwa uheshimiwe na wewe utaheshimu,
mbona wewe unakimbilia kuvunja heshima za wakubwa,kweli kwa mtindo huo utasheshimiwa...’akasema
mama.
‘Samhani
sana mama, nilikuwa naweka wazi, mimi nitafunga mdomow angu mpaka mniruhusu,
haya mmmmmh’akasema na kuufumba mdomo wake kwa vidole.
‘Kazi
ipo....’akasema baba.
‘Baba
msiumie kichwa, mimi haya niachieni mwenyewe kwanza, mimi ni mwanaume, na
nawaheshimu na kuwajali sana wazazi wangu, nitakuwa mtomvu wa fadhila kama
sitwashukuru kwa yote mliyonifanyia, ...wazazi wangu nyie mumeshatimiza wajibu
wenu,nawashukuru sana, ....lakini mimi sio mtoto tena, nimefikia mahala pa mamuzi
yangu...’ nikasema huku nwaangali kila mmoja kwa wakati wake.
‘Mimi hapa
ni mtu mzima,....namimi kuwa ninachokifanya ni kwa mslahi yangu,....natafuta
maisha yangu, na ili nifanikiwe natakiwa nimpate mwenzangu anayekubaliana na
matakwa yangu, umerudi kazini, unajihisi , unaburudishwa,hata uchiomvu wote
unapotea....si kweli mama, ndivyo wewe unavyomfanyia baba...’nikasema huku
namwangali mama kwa aibu kidogo.
‘Sio kwamba
binti Yatima alishindwa hayo, kwakweli alijitahidi, ilakuna mambo machache
ambayo kwang niliyaona ni muhimu kinaman fulani,..,kweli ana adabu, kweli ana sifa
zote za kijijini, kwenu anafaa sana,....lakini niligundua kuwa kwangu itaniwia
vigumu,hakubaliani na haendani nitakavyo mimi....hivi wazazi wangu mngelifurahi
kuniona natembea mitaani na machangudoa, ...au nivumile tu mpaka nipate vidonda
vya tumboni, au .....’nikasema na kucheka halafu nikasema;
‘Kama
haiwezekani sawa, lakini kama kuna mbadala, kwanini mtu uumie....kwanini....’kabla
sijamaliza kuongea Binti Yatima akanikatiza nami nikatulia kumsikilza nikiwa na
hamasa kusikia nini anachotaka kuongea.
‘Wazazi
wangu naona kitakachoendelea hapa ni kuzalilishwa tu, kauli hizo sio nzuri, na
nisingependa kuingia huko na kulumbana ksuiko na sababu....mimi nimeshakubali,
kama alivyosema mwenzangu, kuwa hapa tunaongelea ndoa moja,kuwa yeye keshapata
mimi nimeshindwa, ...yote ni heri, karibu sana rafiki yangu na mume huyo wako
wote...nawatakia maisha mema,....sina zaidi naomba hiyo talaka yangu,ili kesho
na keshakutwa, isije ikawa vinginevyo....na nina... ‘akasema kukatishwa na
kilio huku akiziba uso wake kwa mikono miwili, nahisi hakupenda watu wamuone akilia au ndio aibu ya kukaa pamoja na wakwe na kuongea aliyoyaongea..
‘Hivi nani
kakuambi umeachika...’akasema baba.
‘Hapana
baba mimi sipo kwenye ndoa tena, ndio ni ukweli usiopingika kuwa nilimpenda
sana mume wangu, hajui tu, ....nilimpenda tangu siku ile ya mwanzo tuliyokutana
naye, nilijua yeye ndiye muokozi wangu na yeye atachukua nafasi ya mama yangu,
maana mama yangu alikuwa kipenzi changu,... lakini mungu alimpenda
zaidi....lakini kumbe kwa mume huyu nilikuwa kama majaribio ambayo nimeyashindwa
na inabidi nikubali ukweli..’akasema huku akifuta machozi.
‘Pole
sana....’akasema rafiki yake kwa sauti ya upole, halafu akawa kama kashituka na
kuuziba mdomo wake..hakuna aliyemjali kwa muda huo.
‘Hapana
hilo kwetu kama wazazi halipo, sisi bado tunakutambua kama mke halali wa
mwanetu, kwasababuu taratibu hazijafuatwa,ilitakiwa wewe mtoto wetu, urudi huko
kijijini kwa wazee ili tuone tatizo ni nini, na kama inabidi iwe hivyo, basi
taratibi zingelifuatwa....’akasema baba.
‘Baba,
ukitaka hayo tutaumia wengi...tutaishije hapa...baba , na mama na mjomba
kubalini ukweli,najua mnanipenda sana,na nami nawapenda sana,lakini tukubali
ukwelil, kuwa kila jambo lina mwisho wake, na ukililazimsiha kuna kuumia hapo ,
na huenda ukakosa yote, kwani mkamia maji huyanywa...’akasema mke wangu wa
kwanza.
‘Hapo
umenena mtalaka wangu....na ndio maana nakupenda, ..unajua hali halisi...na
nashukuru sana ,na hata hivyo nasikitika, kuwa sikukutendea haki,... lakini hakuna
jinsi, inabidi iwe hivyo,...wewe mwenyewe unajua,...tutaishije hivyo...hapana,
.... nakuomba uvumilie tu, kwani wapo wengi wanakutafuta kule kijijini,
utampata anayekufaa....wewe ni lulu sana kule kijijini...wanakufahamu ,
wanakupenda na wanaikubali hiyo tabia, hulka, na mienendo yako...sawa eeh..’nikasema
huku nakwepa kumwangalia machoni.
‘Nimekusikia
na nashukuru kwa kauli yako hiyo, nami nasema hivi, nakushukuru sana, kwa wema
wako na mengi uliyetendea,maana ulinitoa kwenye makucha ya simba, isingelikuwa
wewe sijui ningelikuwa wapi, ...nakiri moyoni kuwa wewe ulikuwa kila kitu
kwangu,lakini kama nilivyosema awali siwezi kulazimisha hali iilivyo,....’akatulia
na kuhema kwa nguvu, baadaye akaendelea kusema;
Mimi
nimekubali kushindwa, nisamehe kama nilishindwa kutimiza yale uliyoyataka,
najua mwenzangu , ambaye alijifanya ni rafiki yangu, ndio kweli tulisoma anye,
na namjua vitimbwi vyake na tabia yake, lakini sikujua kuwa ana malengo hayo,
haina shida kabisa...kweli mwenzangu anayaweza hayo, ...lakini tukumbuke kuwa binadamu
wote hatulingani,....huyu anajua hili na mwingine hajui, lakini lipo analijua
kuliko mwenzake, tunazidiana...’akatulia an kumwangalia rafiki yake.
‘Siongei
haya kukubembeelza kuwa nataka turudiane,hapana,....moyo umeshachefuka.... na
baada ya hayo, naomba hiyo talaka yangu...niondeoke...’akasema huyo binti
akigeuka kuondoka na alipofika mlangoni, mama akamrudisha na kwambia arudi ake,
naye bila ajizi akafanya hivyo, akarudi na kukaa kwenye sehemu yake.
‘Mimi bado
kauli yangu ni ile ile...ndoa bado ipo, sisi huyu binti unayemuita mkeo hatumtambui,
na katu hatutamkaribisha kwenye familia yetu kama mke mwana....kwasababu
tumajua , tunakijua kizaizi chake,nini unataka kutuletea katika hii
familia....hapana, kama umeamua hivyo, basi jua kuwa sisi hatupo pamoja na
wewe....’akasema baba na mama akakubali kwa kichwa.
Na mimi
sikusubiri nikaingia ndani na kutoka na karatasi ya talaka, nikawa naisoma kwa
sauti kubwa huku natembea kuelekea sehemu yangu niliyokuwa nimekaa awali, na
kimwana akawa anatabasamu kwa mbali, na binti Yatima machozi yanamtoka,
...sikujali nikaisoma kwa mbwembe:
‘Mimi mtoto
wa Msomali kwahiari yangu mwenyewe, bila kushurutishwa , nimeamua kumuacha mke
wangu,kwa talaka zote .....sababu za msingi, kwanza hatuna mahusiano mema kama
mke namume, pili kaondoka nyumbani miezi mitatu bila kuaga, na hakuwahi kunipa
taarifa yoyote toka huko alipo,...pamoja na mambo mengine nimeamua kumuacha, yeye
sio mke wake tena, na yupo huru kuolewa na yoyote yule....hatudaiani...’Nilipofika
hapo nikatupa jicho kumtizama binti Yatima, ambaye alikuwa kafunika uso wake na
kitambaa akifuta machozi
‘Na kuhusu swala la mtoto yupo huru kuishi na
mzazi yoyote kati yetu wawili , na hata hivyo nimekubali kumhudumia kwa mambo yote muhimu, ....nimemaliza,aukunakipengele
nimesahau maana mimi mimisioo mtaalamu kwa mambo haya...’nikasema huku
namwangalia mjomba, utafikirii ni jambo la heri lililokubalika, nilipowaona
wapo kimiya, nikaweka saini yangu chini, na kumkabidhi binti Yatima ile
katarasi, ....
‘Hahaha...kweli
wewe mtoto umetushinda, yaani umekaa na huyu binti mkapanga muandike hiyo talaka,
eti kuwa hii ndio talaka, huo ndio
utaratibu gani,...lini mlikaa baraza la usuluhishi mkayaongea matatizo yenu,
hata ikashndikiana, ...hebu niambie, wapi mlikutana na wazazi mkayaongea
matatizo yenu, au kwasababu umeguswa mtima nyongo wako na hawo wanaojua wapi
ulipo na kuwazuzua wanaume....sikiliza tutakusubiri kijijini uje ufuate
taratibu zote, lakini talaka hii haikubaliki.....’baba akaichukua ile talaka na
kuichanachana vipande vipande.
‘Hata
ukiachana imeshapita hiyo...’nikasema hata bilakufikiria...’na wote
wakaniangali huku wananishangaa, hawakuamini kuwa kweli ndiye yule kijana, yule
mtoto waliyemtarajia kuwa atashika usukani wa familia kamaalivyo
mjomba....wakachoka na hatimaye baba akasimama nakusema;
‘Twendeni
zetu....huyu naona kuna lake jambo,...sio bure, .... bila kumkazania huyu
tutapoteza mtoto moja kwa moja....’akasema baba na kumgeukia mkewe ambaye
alionekana kujawa na huzuni usoni...mama na mtoto bwana,hata awe mkubwa vipi.
Na hata mjomba alivyotaka kuongea kitu, akasita na kumfuata baba nyuma, huku
kaweka kichwa chini. Mimi mwenyewe kuna muda hisia zilinijia na kutaka
kuwaambia wasubiri kidogo, lakini nilipomtizama kimwana, nikayeyuka,
nikatabasamu naye akatoa lile tabasamu lake, nikawa hao .....
Mara mlango
ukagongwa, tukaangaliana , kwasaabbu ni kwangu nikainuka kufungua mlango, na
nje niliona gari ambalo ni la wapiga mnada, nikawaza kuna nini leo hapa,
pembeni ya mlango kuna jamaa kashikilia daftari , akaniangali ahalafu akasema;
‘Sisi ni
watu wa mnada, hiki hapani kibali toka mahakamani, ...kazi yetu tuliyopewa ni
kuwafuatilia wadaiwa sugu, unakumbuka nyumba yako hii ulijenga kwa mkopo...’akawa
anaendelea kuongea, lakini sikuweza kumsikia, maana kichwa hapo kilikuwa sio changu,... nilishasahau kuwa
hiyo nyumba niliijenga kwa mkopo nadaiwa.....sasa itakuwaje, ...mungu wangu wee....
Je iltakuwaje,
na je ilikuwa rahisi hivyo kuwa nimempata kimwana ,ndio kila kitu saafiii...hebu
tuone yatakayoajiri...niwaulize kuna yoyote kati yenu aliyewahi kukutwa, au
kuwa jamaa yake aliyewahi kukutwa na
majanga kamahaya, je alisaidiwaje?
WAZO LA
LEO: Usione watu wapo kimiya, ukazani hawana shida, au matatizo kama yako, ...hapana...kila mtu ana shida au mataizo yake, ila wengine ni rahisi kuyaongea mataizo yao au shida zao na kujiona wao wamezidiwa.
Ni
kweli shida zipo na huenda zikazidiana, na tunatakiwa kusaidiana, na labda wengine wanafikiria kuwa kwa kuongea sana wanaweza kukapata misaada,...inwezekana sikatai, ila isiwe ndio sababu ya kujitangaza kwa kila mtu, kwani kwakufanya hivyo utafukuza baraka, na sio wote
wenye nia njema na shida zako. Hili nimejifunza,...sijui wewe,hata hivyo wahenga husema; subira yavuta heri
Ni mimi:
emu-three
9 comments :
Mmh inasisimua na kufundisha sana.
Elisa ulipotelea wapi mpendwa, mpendwa sana, karibu tena, na nashukuru kuwa nami tena...au na wewe uliamua kuwa `kimiya kimiya...'
Kuna mpendwa mwingine naye kaingia mitini...Samira, upo wapi, ...kwa mara ya mwisho kukusikia hapa kijiweni,ulisema unakuja huku bongo,umezamia wapi maana ukifika huku bongo, unachanganywa an maisha, hata kile ulichopangilia kinayeyuka....
Ni matumaini yangu upo na upo salama, na karibu hapa kijiweni kwetu, tunakupenda sana na kukuhitaji kwamawazo yako yeney hekima.
Hakika ina sisimua na kufurahisha ...Nimelipenda wazo la leo...Pamoja daima.
m3 mzima nipo dear nipo nimerudi na nashukuru kwa kunikumbuka nami nawapenda sana ila life na baadhi ya watu wa tz wamenichanganya sana sana huwezi amini nimemiss miezi miwili mikasa yetu hasa akufaae kwa dhiki tangu nimerudi about 2wk sasa nasoma zilopita vp mzima dear naona kuna mkasa mpya naufatilia japo mda mdogo
nimefurahi sana kunikumbuka nami nipo narejesha akili
love u m3
Wazo la leo lafundisha sana....na kweli mtoto akililia wembe mpe Mtoto wa Msomali ipo siku atamkumbuka Binti Yatima....Tuko pamoja M3 na wadau wote wa blog hii.
Tupo pamoja dada Yasinta ubarikiwe sana
Haya ndio maisha yetu mpendwa Samira. Vumbi,jua kudhulumiwa, kuonewa ajira hakuna,maisha ghali.
Huku kufa hatufi lkn cha moto tunakiona
Precious tupo pamoja,Mungu akupe baraka tele tuzidi kua pamoja
Nipo kabisa miram3,ila mara nyingi nasoma haraka haraka,hata comment nashindwa kuacha ,si unajua majukumu tena ya maisha ,ila tupo pamoja kabisa.
Post a Comment