Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, April 2, 2012

Hujafa hujaumbika-15



 ‘Wakati mwingine mambo yako yananishanagza sana, sasa huu mkanda unaofundisha utapeli wa dunia utanisaidia mimi kitu gani, mimi sio mwizi na sipendi niwe hivyo....nataka kazi halali, unajua nimejifunza, jambo kubwa sana katika maisha ni vyema uishi kutokana na kipato chako, kama hakitoshi jibane hivyo hivyo, usiwe na tamaa,unaona hapa nilipofikia....’nikawa namwangalia Kimwana.

Kimwana macho yake yalikuwa kwenye ule mkanda, huku akitikisa kichwa kukubali kitu fulani, akageuka kuniangali na kusema;

‘Sikiliza wewe wakuja...hebu angalia ile akili iliyotumika pale,....ukiitumia kwa hawa matajiri wetu ambao wana pesa za kamari...maana naziita pesa zao za kamari,...wewe huwajui vyema hawa watu , ...pesa zao nyingi sio za halali, kama sio za halali, kwanini na wewe usichukue kidogo...kidogo tu,... kwa mbinu kama ile...’akarudisha nyumaili nione vyema.

‘Umeona hiyo.. wakati mwingine shule sio lazima uingie darasani,hii mikanda waliyotuletea ina mafunzo, inawezekana yakawa mema au mbaya, ni akili kichwani mwako...mimi nina akili najua lipi baya na lipi zuri, usinione hivi.....hapo ni utapeli wa dunia, mtu anapata pesa kilaini,hutumii nguvu...

‘Unanitia mashaka wewe naon haupo sawa kabisa, yaani wewe hapo ulipo unawaza kutapeli...mara ulikuwa changu....utabisha kuwa haukuwa changu wewe.... sasa unataka kuwa tapeli...hapana sijui kama nitakuweza wewe....’nikasema huku nikaangalia mlangoni.

‘Sikiliza mume wangu dunia hii usipotumia akili utakufa njaa, nishakuambia hilo, na wakati mwingine kuna shule zipo kwenye hii mikanda sio swala la kuangalia tu, unaangalia unajifunza jambo,...juzi ulivyokuja na kunivamia chumbani na visu mkononi, nilikushangaa sana,.....nilikuwa darasani...eti nilikuwa changu, unajua uchangu wewe...uliwahi kuniona barabarani najiuza...nyi watu wa ajbu kweli...`i am professional...training,.....ooh, naona nikiongea na wewe hutanielewa,ilajua kuwa mimi sio changudoa.....’akasema huku akiwa anaangalia ule mkanda kwa makini.

‘Haya ipo siku utaumbuka tu....siku ile hata angelikuwa nanii angafanya kama nilivyofanya....wewe unaangalia mikanda ya video michafumichafu,isiyofaa...umeweka sauti kubwa, ambayo mtu akiwa nje anajua kabisa kuna watu wanaongea huku....nyie watu, mbona mnaiharibu hii dunia, hawo wanaigiza tu, ili wapete pesa, sio hali halisi ile,mnaharibiwa vichwa vyenu bure...uelewe hilo ....’nikamwambia.

‘Kuigiza hawaigizi vitu ambavyo havipo....ni kama unapotunga hadithi, unaitoa kichwani, lakini ni kutokana na matendo yaliyopo miongoni mwa watu, ndio unapata kisa....halikadhalika hii mikanda ya video, wanaigiza maisha ya watu....na ili uhakikishe angalia kama ule ulionikuta naangalia, umehakikiwa na madocta ambao pia wamehusika kuelezea mambo hayo kitaalamu, ...sio hivi hivi tu...nyie watu mumeenda shule gani...’akasema huku akiinuka pale kitandani.

‘Hamna kitu pale, mimi sitapoteza muda wangu kwa mambo hayo, ....sina tabia ya kuangalia mapicha ya watu walioigiza ili wapate pesa, ...mimi sina pesa badi nikae kuangali hayao mapicha, kwanini badala ya kuangalia wanavyoigiza, nisiingie mitaani nikachakarika...’nikasema.

‘Safi kabisa, haya chakarika basi, ...sana sana ni utaishia kutoa mijasho,unakuja hapa unanuka mijasho tu, hakuna hata sento moja mfukoni. ..kuharibu soli..hakuna unachokuja nacho..kwasababu unachakarika bila malengo....mimi asilimia kubwa ya shule yangu ni kwa kupitia hizi video...na kama ungeliniweka darasani ningelikuwa docta....' akasema huku akiniangalia machoni.


'Najua mtu kama wewe huwezi amini,..maana kusoma nyie ni kufaulu darasani, ....unaweza kuamini mimi nilifeli darasa la saba,lakini kinamna nimesoma hadi chuo kikuu..huamini....lakini wenzako wananiamini, hata likitokea jambo linalohitaji utaalamu naitwa...naitwa hata na madocta..sio madocta hawo wa hospitalini..nielewe lakini....nielewe naongelea nini...mambo yapo mengi ya kujifunza....wenzako wanajua..'akasema huku akiwa kama anachukia kwani nilionyesha kutokumsikiliza kabisa.

‘Hahaha kama huyo mama Docta wenu sio ehe hebu niambia kuhusu yeye, huyo mama Docta...?' nikasema kama nauliza vile

‘Mama yetu, mama yetu yupi huyo.....?’ akashituka na kuniuliza

‘Unajifaanya hujui  au sio....mimi sio mtoto mdodgo nimekwsiha kujua ....’nikasema huku nikimwangalia.

‘Sikiliza hapa nipo darasanai kama unataka kaa hapa pembeni tuangali huu mkanda, kama unahitaji kuwa na mimi nitakufundisha, kamahuhitaji, basi wewe kaa hapa nyumbanimwanaume nikatafute pesa, lakini hii ni gharama,malipo yake ...hahaha....utaona mwishowe.

‘Mimi sinamuda huo, ule wa mwanzo nimeutupia jalalani...’nikasema na hapo akainuka kwa ahsira na kusema;

‘Yaani ile kitu nimenunue kwa hela yangu, wewe unaitupa, ....ndio maana nimeutafuta siuoni, nautaka mkanda wangu,la sivyo hapa kutachimbika....’akasema na kuinuka kitandani.

‘Wa nini ule, uchafu tu, hebu niambia una faida gani...’ikabidi nimpoze maana huyu mwanamke akianza visa kweli kutachimbika.

‘Wewe hukuona, ilikuwa inanifundisa maswala ya ndoa, jinsi gani wanandoa wanatakiwa kuishi, kutendeana, ....’akatulia nilipomuonyesha ue mkanda wake ulipo.

‘Unaona hapa nje, umeidhinishwa na madakitari bingwa...hawa walisaidia kukamilisha huu mkanda, walipochunguza na kugundua kuwa wanandoa wengi hawatimizi sharti muhimu landoa yao, kwasababau hawajui, ....wao walijua ndoa ni ndoa tu,umeoa umeolewa...’akatuliana kuniangalia kwa makini.

‘Ndoa ina mambo mengi, lakinikuna jambo moja muhimu na wengi wanaliita `la ndoa...’ huajsikia kupika au kufagia kukaitwa `kazi zandoa’hapana, ....kwasababu ungeliweza kuzifanya mwenyewe, au ungelitafuta mfanyakazi wa ndani akakufanyia, ....au sio...?’ akaniambia huku akikunja uso alipoona simsikiliza.

‘Tatizo lako ndio hilo, hutaki kunielewa....nyie wanaume  mnazarau yale mambo muhimu na matokeo yake mtaoa,mtaacha na mwishowe mtaokota garasa...hilo nikuambie ukweli....huu mkanda ni mahususi kwa wanandoa unafundisha mambo ya kimaumbile...kuna mambo mengi nyie wanaume hamuyajui, na na kama hamuyajui, na hamutaki kujifunza, ....basi ukimpata mke mwenye akili kama mimi anayekujali na kujali ndoa yake, anakuletea mambo kama haya,...’akauchukua ule mkanda na kuuweka kwenye kabati.

Ila leo ni tofauti, leo tunajifunza jisni ya kutafuta pesa.....njoo hapa tuangali halafu nitakufundisha jisi gani inatakiwa iwe..ndio ni utapeli kama inavyoonyeshwa, lakini ukitumia akaili ..unatafanya akzi, na utafanikiwa, ...acha mambo ya wivu,..hahah eti siku ile mtu huyu na kisu mkononi, wewe...kisu ni silaha gani....’akasema na kunifanya nikumbuke siku ile ambayo nilifika nyumbani nikawa nasikia kelele za ajau akabu ndani....

Siku ile nilifika nyumbani nikiwa na mawazo, nikiwa nimehamaki, baada ya kumjua kuwa mke wangu  miongoni mwa hawo wanawake wanafanya bishara haramu za kujiuza na sasa ananitumia kamachambo au sijui kwa maslahi gani, nia na lengo lngu nikifika niongee naye vyema, kama ikibidi tuachane kwa amani, ...

Nikiwa sijui nichukue uamuzi gani maana akiondoka hapo na mimi itabidi nianza kazi ya kuomba omba, maana sina kitu, kwa asilimia kubwa namtegemea yeye. Nikawaza kwa undani mwishowe nikaoana hakuna jinsi, lazima nibakie naye kwa muda huku nikitafuta jinsi ya kuishi hapa Dar.

Nilipofika mlangoni ndio palenikaitizama nyumba kwa makini,nikiwa najilaumu kwanini nilisitisha yalemakato ya kulipia deni, maana kamaningelikwenda kamamakubaliano yalivyokuwa deni lingelikuwa dogo sana, naingekuwa rahisi kumalizia kwa njia nyingine,lakini sasa deni ni kubwa ukujumlisha na riba. Nikashika kitasa na kukizungusha.

Nikiwa na kisu mkononi, niliingia chumbani huku kichwa kimejaa mawimbi,hapo hasira zote zilikuwa kumalizana na huyo binti,kama ndio kaamua kuniingizia wanaumehumo ndani, basi liwalo na liwe, ni bora nikafungwe tu...nikajisemea huku moyoni nikiwaza maisha ya jela, nilionja mara moja nikajuta, ....hapana, huyu lazima nimfanye kitu mbaya.

Wakati bado Kisu kikiwa mkononi, niliusukuma ule mlango,na zile hasira na chuki nilizotamani kuzificha zikawa zimevumbuka na hapo sikuwa na simile tena, lengo langu ni kufanya jambo ambalo hawatalisahau nikajitosa ndani...

‘Oh, ndio utaratibu gani huo wa kuingia bila hodi huoni nipo shuleni hapa....’akasema Kimwana, akiwa kajilaza kitendani na mbele yake kaweka runinga ikiwa na video akiangalia picha, na nilipoptisha macho ya haraka niligutukana kuagalia pembeni..

‘Ni vitu gani unaangalia hivyo na umefungulia kwa sauti kubwa kiasi kwamba watu wanafikiri mpo na...na...

‘Naju hata wewe ulikuwa ukifikiri hivyo, ndio umechukua kisu ili umchinje huyo mwanaume niliyemuingiza humu, ....hahaha..haya kamchinje yule jamaa, huoni aanavyofanya, ...pale ni shule tosha,....shule ya kukurizisha wewe mwanaume wangu...’akasema Kimwana.

‘Hembu ondoa uchafu wako hapa.....’nikasema huku nikikaa kitandani na kuangalia pembeni.

‘Uchafu,...hahaha.....uchafu wakati ulimuacha mkeo kwasababu ya mambo hayo...hivi ndivyo mkeo alitakiwa akufanyie, hukumfunda....ilitakiwa kama hajui ungelimnunulia vitu kama hivi...huu mkanda umeidhinishwa kitaalamu kuna madocta wazungu na waafrika, wamefanya utafiti na kugundua nini kilichopo ndani ya hisia za kibinadamu...na kwanini ....tatizo lako hutaki kuelewa, au hutaki kinielewa....’akawa anaongea lakini sikuwa namsikiliza kwani hapo nilishahakikisha kuwa huyu ni changuduo.

‘Sikiliza wewe mwanamke hapa nilipo nawaza jinsi ya kupata pesa, jinsi ya kupata kazi, ....sifurahii kabisa hii hali ya mimi kuwa nalishwa na wewe, ....wewe naona badala ya kunisaidia kwa hilo unaleta mambo ya mchezo, eti  jinsi ya mume na muke waishi sijui wafanye nini,ili iweje,...hayo hata bila kufundishwa yanajileta yenyewe tu,...hivi mkiwa na njaa kweli mambo hayo yanafanyika....?’ nikamuuliza.

‘Hahaha...eti mkiwa na njaa,...nani ana njaa hapa, kwani hujashiba,....ujue kuwa kama akili haijatulia katu huwezi kufikiri....hili linatuliza akili, linatuliza mihamaniko,....ndio maana mke au mume anatakiwa ailijulie kwa ajili ya mwenzake, ili muweze kutulizana......vinginevyo macho yatakuwa wayu wayu, kutizama wapiti njia,...kutamani vya wenzenu, ..akili zenu hazitatulizana....nikuulize,ukiwa na njaa, hutaweza kuwatamani mabinti au wake za wenzako...?’ akaniuliza.

‘Swali hilo niliwahi kuwauliza wazazi wangu kipindi kile....unakumbuka, maana unatoka kazini,una njaa ya mkeo...una ....huna na kwasababu huko maofisini, kuna mabinti waliojaliwa hawana aibu, wanakutamanisha, ....sasa unakimbili anyumbani ukijua ...mke yupo ....lakini ukifika duuuh,....mke anasema subiri, usiku uiingie, na hata ukiingia ni kwa mbinde...kumbe ndio maana mnatunasa kirahisi...?’ nikasema na mara mlango ukagongwa.....

‘Ni nani tena huyo wakati kama huu...hapa tupo darasani, tupo faragha....watu hawajui maana ya nyumba za watu, kila mara hodi, hodi...hawatambu huu ni muda wa faragha kwa wanandoa..., hatutakiwi kubugudhiwa...’akalalamika kimwana.

‘Lakini muda huu ni mchana....huenda ni wageni muhimu wanaweza wakawa watu wa kutuletea pesa...’nikasema.

Watu wa kutuletea pesa hahahahaee, pesa njoo, hivi wewe huna akili ya kufikiria...nina uhakika watu wanaokuja saa hizi sio wa kuleta pesa,hawo ni watu wa shida, ni watu wasio na pesa,wanakuja kuomba...eti kutuletea pesa...pesa hailetwi kirahisi hivyoi...umelala ijilete yenyewe ni ya mashetani au ...sijui nenda kuwaafungulie...

                                    *******.

‘ Oooh...’nilijikuta niguna pale nilipofungua mlango,

‘Mwanetu umtusahau...’ilikuwa kauli ya mama,....nikawaangalia wazaziwanhu hawa kwa muda hata bila kusema kitu, maana ni muda mrefu sijawa na mawasiliano nao, ningewasiliana no vipi wakati sina pesa, sina kazi...

‘Au hata ndani hutaki kutukaribisha...?’ akasema baba.

‘Aaah sio hivyo wazazi wangu,...baba, mama...ooh,  mbona mpo hivi....kumetokea nini, karibuni,shi-shi kamooni...mbona mumechoka hivi?.‘

‘Unatushangaa leo, ushukuru tupo hai, na umshukuru sana mke wako wa kwanza isingelikuwa yeye sijui ungeweza kusema baba au mama...’akasema baba huku akijikongoja kuingia ndani.

Hali zao zilionyesha kuchoka, na ilivyoonyesa sio kwasababu ya uzee, kama sio ugonjwa basi kuna jambo kubwa limetokea huko kijijini.

‘Wanasema kuna tatizo limetokea katika ukoo wetu, ingawaje tatizo sio kwa ukoo wetu tu, hili tatizo ni maeneo yote, mvua hazinyeshi, hakuna mazao, mifugo yote imekufa....hebu fikiri familia yetu ambayo kipindi cha njaa ndio inategemewa safari hii tumekuwa hatuna kitu...’akasema mama.

‘Na mjomba yeye yupo wapi naona umekuja na ndugu zangu wengine tu....?’ nikauliza.

‘Mjomba wako alisafiri na familia yake kwenda kwa mtoto aishie huku Dar, ina maana hamjawasilina naye mbona yupo hapa Dar?’ akauliza.

‘Kwakweli sijawahi kuwasilinana naye...’nikasema.

‘Nakumbuka kuna mzee mmoja alikuja hapa siku moja, akakuuliza, ...ooh, nimemkumbuka ndio yule mlikuja naye siku ile, nilimsahau kabisa, maana alikuwa kakonda sana,mimi nikajua ni ombaomba tu, nikampa pesa kidogo nikamwambia iishie zake, nakumbuka aliniambia ....akija mjomba wangu mwambie hiki kizingiti hakifai kabisa katika nyumba....’akasema Kimwana.

‘Mbona hukuniambia, inawezekana ndio mjomba wangu huyo...unasema alisema nini?’ nikauliza nikitafakari.

‘Swala hapo sikujua alisema nini...swala hapa ni hiki kijiji kitaishije hapa , siunajau tena mambo ya bajeti, na leo sijatoka kabisa, leo nilikuambia nipo mapumziko....yule Mhindi anafanya mahesabu ya vifaa vyake, nami nikasema tukae tujifunze maisha, sasa mara huuuh kijiji ndani ya nyumba...sasa hiki kijiji kitaishije hapa...?’ akasema mke wangu akiwaonyosha vidole wazazi wangu.

‘Hiki sio kijiji, hawa ni wazazi wangu...elewa Kimwana, wazazi ni kitu kingine, kikiharibika hapa wakakasirika mimi ninaweza kuokota makopo, bila wao nisingelikuwepo duniani, kwahiyo tungalie tutawasaidiaje, tutafanyaje...’nikasema huku nikiwaangalia wazazi wangu walivyochoka. Moyoni nikaingiwa na moyo wa huruma, maana ni kipindi kirefu sijawasilina nao, sijawahi kuwatumia hata senti moja, hasa baada ya kuachana na mke wangu wa kwanza.

‘Sasa hamna chochote huko, mwanangu maana tangu jana hakijaingia kitu tumboni....’akasema baba, na baba ninavyomjua ni mtu walishe..nikamwangalia Kimwana, Kimwana akacheka, akasema;

‘Unaona....watu wanaagiza kama hotelini....kwamtaji huo hapa hakuna cha bajeti tena, sasa hivi ...oh, kashughulike huko jikoni, mimi ngoja nitoke nikaangalia hiki kijiji kitaishije hapa na nikirudi nataka tuongee vyema, ukumbuke na mimi nina familia yangu, na wao wana njaa hivihivi, mimi nimewaambia hali ngumu,....wamenisikia... sasa wewe..huwezi kusema hivyo au sio.....`anyway', tutaonge baadaye anikirudi,...na kuongea kikweli kweli...' akawa keshafikamlangoni,halafu kaam vile kasahau kitu akageuka na kusema;

'Angalia huko jikoni kama kuna chochote wapikie  wanakijiji, wasija wakatufia hapa...’akasema kimwana akichukua na kutoka nje akiwa na kimfuko chake.

‘Aisee...hapa naona hakuna amani...mwanangu ndio imefikia hivi..vipi kazi lakini...?’ akauliza baba.

‘Wazazi wangu hayo tutayaongea baadaye, ngoja niangalia kipoza njaa...’nikasema na kuinuka, na mama akanifuta huko jikoni, nikashukuru kwa hilo,ingawaje nilimwambia atulie tu wao ni wageni,laikini hakukubali akasema;

‘Mwanangu mimi siwezi kukuona ukiingia jikoni wakati mimi nipo, hata kama mimi ni mama yako, ilihali nguvu ninazo, acaha niifanye hiyo kazi, wewe nionyeshe vitu vya kupika vipo wapi, nitafanya hiyo kazi wala usiwe na wasiwasi....wewe nenda akongee na baba yako, kwani mnatumia majiko ya umeme au ya kawaida...?’ akaluliza mama

‘Mama siku hizi tunatumia majiko ya kawaida , hali imebadilika mama...tutaongea kwa kirefu baadaye...’nikasema nikideka kwa mama, mama ni mama hata uwe mtu mzima....

‘Mwanangu mbona na wewe umekonda kiasi hiki,...mwanangu hali hii hapa inanitia wasiwasi... usiniambie ni hiyo njaa ya kijijini ndio imefika hadi huku,... lakini inawezekana  maana kama sisi tusipolima mtakula wapi,...mazao yote yanatoka kijijini, huku mjini hakuna mashamba , mashamba yapo wapi huku mjini, haya mazo huko hakuna...sijui tutakimbilia wapi, mungu mwenyewe ndiye anajua....

‘Mama hiyo isikutie wasiwasi...ilimradi tupo hai, tutaishi tu...kwakweli iannisikitisha sana, ....hapa nilipo najuta, najuta kwa mengi, umesema aliyewasaidia ni Binti Yatima yupo wapi ...mbona hamkuja naye?’ nikauliza kwa shauku.

‘Yupo kwa mume wake....mlivyoachana tu,wanaume wengi alimfuata kumuoa, na mwisho wake akaolewa na mume mmoja tajiri,ambaye familia yao inaishi Kenya, ...walikaa kwa muda na muda walipokuwa huku nchii, ndio walikuwa wakitusaidia hata alipohamia Kenya bado alikuwa akituma pesa za amtumizi...kwakeli mungu amemjalia sana yule binti...umefanya kosa sana kumuacha...’akasemamama.

‘Lakini mama ujue kila kitu kinafanyika kwa mpango wa mungu, je ningekaa naye angeliweza kuolewa na huyo tajiri, je angelifikia hatua hiyo aliyofikia....asingeliweza, lakini yote haya yametokea kama sababu ili nimuache aende kuishi sehemu anayostahili...kwakweli, kila mara namuwaza sanamke wangu wakwanza...na hapa nakumbuka ukweli kuwa sio vyote ving’aavyo ni dhahabu....natamani kama enzi hizo zingelirejea nikajisahihisa...’nikasema nikimuangalia mama akihangaika jikoni.

‘Nenda kaongee na baba yako ana hamu sana na wewe...hayo yameshapita tena...maji yakishamwagika hayazoleki...mwenzio yupo Kenya na nasikia anasoma, karibuni kuingia chuo kikuu....’akasema mama.

‘Mpaka kaamua kusoma, kweli ameamua, kweli kampata aliyemshiba...haya ngoja nikaongee na baba,najua baba ataishia kunilaumu na mwisho tutaishia kugombana,....haya mama kila kitu kipo hapo kwenye kabati, leo tutakula, sijui ya kesho...’nikasema na kutoke jikoni na kwenda kuongea na mama.

‘Ya kesho hatuna mamlaka nayo anajua Mungu...’akasema mama akiwa hajui nina maana gani. Nikatoka pale eneo la jiko na kuingia varandani na kumkuta baba akiwa kashikwa na kausingizi...

‘Baba vipi umeshikwa na usingizi,uchomvu wa safari au njaa...?’ nikamtania baba.

‘Yote.....oooh’akasema huku akipiga miayo.

Poleni sana,nasikitika sikuweza kufanya lolote sio kwamba niliwasahau, bali hali yenyewe ilikuwa ngumu na nilipowaona na nyie mpo kimiya nikajua hakuna shida...’nikajitetea.

‘Duuh, mwanangu siku hizi wewe ndio mama wa nyumbani, au nisemeje, maana ile kauli ya mkeo imenichefua kweli, isingelikua hii shida....,nisingelikaa hapa, yaani sijui nisemeje...mkeo anakuambia uingie jikoni...ukapike yeye anafanya nini...au ndio hivyo anakwenda kazini, na kazi gani hiyo siku ya leo...na muda kama huu...mwanangu angalia sana...’akaanza kusema baba.

‘Baba naomba ya hapa uyaachie hapa hapa....mimi najua nini ninachokifanya...hujui naumia kiasi gani, lakini wakati mwingine inabidi ukubali ukweli...vinginevyo ungelinikuta nipo mitaani naomba, au....sijui ningelikuwa nafanya kazi gani sijui, baba...hapa nilipo sina kazi...naishi kwa kumtegemea huyo binti....akihangaika huko anapokwenda ndio tunapata riziki ya kutufanya tuishi, kazi hakuna kabisa....’nikasema bila aibu.

‘Eti nini....haiwezekani, wewe siulituambia kuwa kampuni yenu ilikupeleka kusoma,  imekusomesha hadi Ulaya,....halafu ndio imeamua kukufukuza kazi, haioni hiyo ni hasara, haiwezekani,...nahisi kuna jambo umetenda ....ina maana wao hawana  akili wakufukuze hivi hivi tu..au ndio huyo mke kakufanya hivyo..., au ni laana ya mkeo wa kwanza maana hivi vitu sio mzaha....’ akasema baba huku akipiga miayo ya njaa.

‘Baba naona una njaa hebu nikakununulie angalau ndizi mbivu uzibe njaa kidogo...’nikasema huku nikiinuka kutoka nje.

‘Aaah, chochote kwangu sawa maana ukiwa na njaa huchagui kipi cha kula, yaani hata vile vya kuwekea maji yawe baridi,naitaje ile mashine....iko wapi ,naona vitu vingi vilikuwemo humu ndani havipo, ina  maana umeuza vyote au uliibiwa nini....naona hata yale masofa ya kifahari ukikaa unazama hakuna, mwanangu vipi kulikoni....?’ akawa anaongea wakati mimi nimeshatoka nje.

Nilipofika nje nikaonana na muuza genge ambaye ananidai vitu vingi nilivyokuwa nachukua, na aliponiona tu akaanza kulalamika; kwake bila kulipa, nikimuahidi kuwa nitamlipa mwisho wa mwezi, lakini ikawa ndio kazi nimefutwa.

‘Deni langu broo, ...mimi kamtaji kangu unakaona kakubahatisha sasa ukikaa na hela yangu muda wote huo unafikiri nitaendeshaje biashara,naoma unilipe leo broo....’akalalamika.

‘Sikiliza bwana mdogo hata nchi kubwa kama Marekani inadaiwa madeni makubwa, sembuse wewe na mimi...kudaiwa ndio moja ya biashara,...biashara ni kuuza, kudai na kudaiwa...sasa sikiliza nina wageni wamekuja ghafla, naomba ndizi mbivu za elifu, ....chukua hii hapa,... silipi deni kwa leo...nitakulipa tu, na kukuunganishia....nataka siku moja uwe na duka, sio kigenge kama hiki....’nikampa na kweli akanipa ndizi mbivu,nami nikarudi ndani.

                                                 ***********

‘Haya chakuala tayari, hebu tule huku tunaongea, maana kama tulivyosikia kijiji kipo hapa na kipo mkononi mwako, kuna usalama hapa maana tusikae hapa huku tunasimangwa, kama wewe huna kazi, unalishwa na mke, ..na sisi tumekuja hapa kwa huyu ambaye tulimkana, huoni hapa tutaishi kwa kusimangwa tu.

‘Sasa wazazi wangu tutafanyaje, mimi ndio hivyo sina kazi, ...bila kuwafichai huyu binti ndiye anayeniweka hapa mjini, vinginevyo ningelishakuja huko kijijini....na yapo mengi...,hata hii nyumba yenyewe nilijenga kwa mkopo, deni halijalipwa na benki wanataka kuipiga mnada hii nyumba ili warudishe deni lao....naishi hivyo hivyo, siku yoyote wanaweza kufika hapa na kuipiga mnada hii nyumba, sina jinsi,....nimetumia mbinu za kuongea na hawo wanaonadisha, ....angalu kuvuta muda, .....’nikaongea huku nikiangalai huku na kule, maana sikutaka kabisa mke wangu alijue hilo.

‘Kama ni hivyo ...turudi kijijini, wewe una minguvu bado, una akili za shule, unaweza ukawekeza huko, kilimo bora cha kumwagilia...ukatuongoza kama alivyowahi kufanya mjomba wako....mjomba wako kachoka siku hizi , lakini ujanani mwake, alikuwa akija kijijini anatufundisha mbinu nyingi za kilimo bora, kufuga kwa mpangilio, lakini safari hii kachemsha mwenyewe kakimbilia kwa mwanae huku mjini..’akasema baba.

‘Baba mimi hali kama hii nitaweza kushika jembe, na hata hivyo kama mumedai kuwa kuna njaa, nitaenda kufanya nini, ufike mahali kuna kianzio, sasa hakuna hata chakula...hata mbegu mnasema mumekula, nitaanzaje mimi, au elimu itasaidia nini...tubanane hapa hapa, tuone itakuwaje, ngoja akirudi mwenzangu tutaangalie nini la kufanya....’nikasema huku nikiwa na wasi wasi na kweli mara mlango ukafunguliwa....

‘Haya wanakijiji hamjambo...maana leo nimefika kwa Mhindi ikabidi nimpigie magoti, nimemwambia nyumbani kuna kijiji kimefika kuanzia mjumbe hadi balozi, ....sina pesa ya kula, na sijui tutalalaje humu, maana kitanda tulicho nacho ni kimoja....’ akasema na kuniangalia kwa makini mimi nikamminyia jicho na kumwambia

‘Wife eeeh, njoo huku kwanza tuongee, ....’nikasema kwa haraka, nilipomuaona haniangalii, au aliniangalia akazarau, akanifuata tukaingia chumbani kuongea. Tulipofika akawa wa kwanza kuongea akasema;

‘Sikiliza zamani tukisoma shule ya msingi kuna wimbo ulikuwa ukiimbwa, mgeni siku ya kwanza mpe wali na samli...lalalala....si ndio, siku ya pili, ugali eeh,  hivyo hivyo...nimesahau kidogo, na siku ya tatu mpe jambe akalime, ...akishindwa, ...utaajza mwenyewe, sasa nakumbia hivi, leo tutawakarimu ipasavyo, wale washibe,....’akasema huku akitoa pesa kwenye pochi lake, nilishangaa pesa zote hizo kazipata wapi, lakini niliogopa kumuuliza.

‘Sasa....eeh,  kesho tutaangalia jinsi ya kufanya lakini kesho kutwa, aah...wataanza kumuona kimwana, ..anga zangu zitaanza kuwaka... sijui,...kwanza watu wenyewe walishaniambai sifai kuingia kwenye familia yao, leo hii nawalisha mimi....sikiliza siku tatu, sio zaidi , hata mimi nina wazazi wangu...lakini nimewatolea nje, ...nimewaambia wapo akina kaka...sijui kinachoendelea huko...wananijua mimi , wananiogopa, kwani sikopeshi mtu....’akasema na kuziweka pesa kwenye droo ya kitanda.

‘Sikiliza mke wangu, umezungumzia wageni, hawa sio wageni hawa ni wazazi wangu na nikupe ushauri,hapa ndipo  mahali pa kuwaonyesha kuwa wewe ni mkwe mwema, au unasemaje .....ndio sehemu ya kuingia kwenye familia yetu bila shaka...kilaini...’niksema huku nikitabasamu.

‘Hahahaa...ngoja nicheke...kuingia kwenye familia yenu, ina maana nyie mnajioan wa maana sana, kwa vile kule kijijini mnatambulika kuwa ni familia ya maana,familia tajiri, familia yenye maadili mema....hahaha...’ akacheka mpaka anashika mbavu.

‘Sasa unacheka nini kwani sio kweli hiyo....’nikasema huku nikimwangalia kwa mshangao.

‘Kwa vipi, jione mwenyewe, hapa nani bora.....wewe au mimi, ..haya , mbona hawo wanakijiji wanakuja kuishi na mtu anayetoka kwenye familia mbovu, familia yenye maadili machafu...wewe. nyie acheni hayo..maisha hayana muamana, leo kwangu kesho kwenu....’akashika kiuno huku akihesabu hela alizobaki nazo mkononi, halafu akatoa noti mbili akanikabidhi.

‘Nimkuelewa, mpenzi ,leo kwako kesho kwangu....’nikasema huku naziangalia zile noti mbili....na aliponiona naziangalia akaangua kicheko na kusema kwa kuyarudia maneno yangu kwa dharau;

‘Kesho kwako....hahahaha..sasa usiku tutakula nini,... hiyo ni bajeti ya kesho...leo kama nilivyokuambia mgeni siku ya kwanza, unamkarimu, mimi sina noma, nijua kuwakarimu wageni, unaonaje tuwatoe ....kwenye hoteli saafi wanapata chakula na kinywaji, safi kabisa, pesa leo ipo...swafi kabisa, kama ulivyosema nijipendekeze...au sio’ akaniangalia kwa jicho la pembeni akacheka.

‘Kujipendekeza....duuh, mbona hiyo kazi, nikuambie ukweli hii sio shepu ya kujipendekeza, mimi najipendekeza kama kuna mslahi,kamakuna lengo, na nisema ukweli mimi najipendeekzakwako tu kwako tu kwasababu....’akangalia  juu ya paa, sijui alikuwa akiwaza nini.

‘Kwasababu gani...?’ nikamuuliza kwa hamasa .
Akanisogelea na kunikumbatia halafu kwa sauti ya kujilegeza akasema; `kwasababu nakupenda, na huku kanikumbatia akiwa kaweka kichwa na kungalia upanda wa nyumba yangu, akabetua mdomo wa dharau, hakujau kuwa namuona kwenye kiyoo cha kabati lililokuwepo humo ndani, ...

‘Kimwana naomba uniambie ukweli, nini lengo lako,...maana nahisi sio kweli unafanya hayo kwangu bilamalengo, sizani unafanya haya kwasababu ya kunipenda kaam unvyodai, ..nimesikia mengi kuhusu wewe na wenzako mliokuwa mkifundishwa na huyo mama mumuitaye Docta....na sijui kwanini upo na mimi maana lengo lenu ni kuwachuna watu weney pesa, mimi sina pesa....’nikasema.

‘Unataka nikuambie nini lengo langu,...nakusikitikia sana...?’ akaniachia na kuangalia pembeni.

‘Itakuwa vyema, kuliko kuja kunishitukizia....’nikamwambia.

‘Hivi wewe kwa muda kama huu una jeuri gani, hata nikikuambia sababu ...hicho kijiji hapo utakipeleka wapi...sikiliza haya hayafai kwa sasa, jiandae na iandae hiyo kamati ya kijiji twende tukatumie, tambia hii ni gharama, ipo siku ya kuipangia bei,ambayo itafidia gharama hii na faida kibao...mimi nina malengo marefu..’akasema huku akibadili nguo.

‘Sikuelewi kimwana una malengo gani na mimi....?’nikamuuliza na mara simu yake ikalia na akaichukua na kuniangalia kwa muda bila kuipokea, akasema;

'Nakuonea huruma sana, ...' huku simu ikiendeelakuitia, halafu akanibusu kwa mbali.

'Kwanini huipokei hiyo simu....?' nikamuuliza huku nikiwaza ni simu ya nani hiyo

‘Usijali utakayoyasikia hapa nikiongea ni mambo ya kibiashara... mjini hapa ....’akaipokea simu.

‘Sema shosti kuna nini unataka kuniambia...nimeshakuambia tangu awali,mimi huku sipo tena. Nimeolewa, ...unanielewa ,mimi nimke wa mtu,..eti nini ,mama Docta,...tulishamalizana anye, vipi tena... ananihitaji, kuna nini....sasa hivi...hapana, ...eti nini...siwezi,mimi nimeshajitoa,...eti nini...haiwezekani,....

Nilibaki nimeduwaa, maana Kimwana alikurupuka, akaondoka hata bila kuaga sikujua kumetokea nini huko anapokwenda, mimi nikatizama droo ya kitanda ambayo mara nyingi anaifunga na ufungua anatembea nao, leo kaondoka bila kuifunga,...hamu ya kuchungulia nini kilichopo ikanijia, nikaivutakwa nje....zile pesaalizoweka,..nikazisogeza ili niangalie kwa ndani......ooh, moyo ukanidunda....macho yakaingiwa na kwikwi, nikajikuta mwili mzima ukitetemeka, sio kwasababu ya zile pesa, ila kile nilichokiona.....nikatamani na mimi nitoe humo nikimbie....

NB Hebu kisia , Je aliona nini...tukumbuke kuwa kisa hiki na mahsusi kwa wanandoa...tutajaribu kugusia gusia kamayalivyomkuta rafiki yangu, na kama kuna mwazao maoni, tuambizane,maana mimi sio mtaalamu sana waammbo hayo, ila kisa ndivyo kilivyokuwa;

‘WAZO LA LEO: Wazazi ni watu muhimu sana katika maisha yetu, vyovyote wawavyo tusiwanyanyase,kwani hakuna kama wazazi,...utayajua haya ukianza kulea... huwezi hata siku moja kuwalipa fadhila zao kwani hakuna kama mama,hakuna kama baba.




Ni mimi: emu-three

2 comments :

samira said...

mh m3 inachekesha yaani wazazi anawaita wana kijiji haya nasubiri nione itakuwaje
binadamu usife moyo kwani kila kinachotokea na mitihani tu ili ujuwe yupi mwema na yupi wa kukaa nae

emuthree said...

Nashukuru sana Samira Tupo pamoja.

Kuna tatizo kidogo kwenye blog, najaribu kupambana nalo. Ilitakiwa sehemu hii ionekane kwenye blogs za watu, lakini inaonekana sehemu iliyopita!