Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, April 5, 2012

Hujafa hujaumbika-18
‘Hapa ndio sehemu ya kucheza karata yako ya maisha, ...’akaniambia mke wangu tukiwa chumbani, baada ya wazee kuondoka, walipoondoka, nilijikuta mwili ukianza kuogopa, ni kama vilekinga fulani imeondoka,na huji nini kitatokea baadaye. Wakati nawasindikiza mjomba aliniambia;

‘Kama ungelikuwa na akili ungelifuata ujumbe niliomuachia mkeo huyo uliye naye sasa,..lakini naona bado upo gizani, samahani sana, nikisema kuwa mke ana walakini,...siku ile nipofika akaniona kama ombaomba..akaniangalia kwa jicho la dharau kama hanijui, nikajua hapo hakuna ubinadamu...jaribu kuwa mwangalifu...’akasema mjomba.

‘Lakini mjomba huyo sasa ni mke wangu nimeshamuoa....itabidi nijarabu kumuelimisha, najua atabadilika tu, ..’nikasema.

‘Ni kweli, hayo ni maswala ya mke na mume, lakini samaki hakunjiki akiwa mkavu...ulitakiwa upanue masikio yako kabla,usikie nini zaidi, hasa kwa sie tuliowahi kuiona dunia, ulitakiwa uweke akili yako chini utafakari, upime  na uchanganue, faida na hasara...wewe msomi hayo ulitakiwa kuyajua,...nini maana ya elimu yako... lakini hukutaka kuyafanyia kazi...sio biashara zote zinauzika mjomba, sio vyote ving'aavyo ni dhahabu mjomba..’akasema mjomba.

‘Mjomba nimekueelwa, tatizo ni kuwa nimeshafulia nguo maji, sina budi niyaoge,  nita-oa na na kuacha mpaka lini....kosa lilishafanyika, sasa naona nijirudi kwa kukaa na mwenzangu atanielewa tu, yeye ni binadamu....’nikasema huku nikiaangali nyuma, mke wangu alikuwa akijaribu kuwa karibu na sisi kusikiliza tunayoongea.


‘Mimi sina zaidi, ila fundisho, ukioa, usitazamie kuwa kila kitu unachotaka utakipata mara moja, sisi hadi tunafikia uzeeni, yapo mambo mengi mpaka leo unatamani yawepo kutoka kwa mwezako, au unataka mwenzako ayafuate, lakini bado, na bado hatujachoka kufundishana, ndoa ni nusu ya imani, ndoa ni maisha yenu...jitahidini kuelekezana, msichoke, ...ila ndoa kama haina kuaminiana,kuelewana, na kushauriana, na adabu na kuwajali wazazi, mtaishia kubaya.....’akasema mjomba alipoona mke wangu anatusikiliza.

‘Nimekuelewa mjomba, tutajitahidi sana...’nikasema.

‘Sawa, ila ujumbe wangu ni muhimu sana, ....utakuja kuniambia siku yake...ni bora kizingiti kiwe imara hata kama hakivutii, lakini kitaimarisha nyumba, kuliko kizingizi cha mvuto, .......kisicho imara...’akasema mjomba wakati waning akwenye gari.

‘Niliwapungia mkono,na mamaalionekana hana raha kabisa, isigelikuwa uzee, angeliangusha chozi...nilimtizama baba, yeye hakutaka hata kuniangalia....wakanondoka, na kuniacha nikiwa kamabua lililokauka.

‘Mjomba wako bwana, ....yule mtu simuamini, ....hata ukimwangalia anakuwa kama anakuosma kwenye moyo wako, anakujua ulivyo....namchukia, na akipita kweney anga zangu, sijuikama nitambakiza...yeye ni kikwazo.., twende zetu nyumbani, kwani tuna mengi ya kuongea...mengi sana....sasa ni mimi na wewe...’akasema mke wangu akinisihika mkono.

‘Sasa ni muda wa kucheza karata yako ya mwsiho....’akasema mke wagu

‘Karata yangu ya mwisho kivipi,...kwanza niambie maswala ya nyumba....’
Sikiliza wewe mwanaume....sina muda wa mchezo, kila kitu kinajieleza kwenye ile katarasi uliyoikuta hapa kitandani. Hapa tunangea jambo jingine muhimu sana, achana na hilo kwanza. Nilipofika pale ofisini nilipowakuta na yule mama Mhindi, niligundua kuwa anakutaka, ...hilo nina uhakika nalo...’akasema mke wangu.

‘Haya mawazo yako bwana....,kwanza umeshanichanganya...sikuelewi unaongea nini...’nikaanza kuwa mkali.

‘Ukali hausaidii kitu, maana hutaweza kubadili maji kuwa maziwa,vinginevyo uchanganye na maziwa ya unga...na hilo linahitaji vifaa, ..pesa..nikiwa na maana kuwa kwa sasa hivi huna ujanja, huna pesa, ...utafanya nini...kila kitu nimeshakiweka sawa, nenda kokote huwezi kitu....’akasema na kuniangalia kwa makini.

‘Tutaona,.... kama kweli ni haki yangu,tutaona...’nikasema huku nikiwa nimeinama chini.

‘Hahahahahaki yako, ulijenga kwa mkopo au sio, uliwahi kulipa huko mkopo, hujalipa, umelipwa na wengine, hiyo ni haki yako kweli...’ akawa anagusa kwa kidole kwenye sehemu ya kichwa.

‘Wewe mwanaume, kuhusu nyumba hiyo sahau,...nyuma hii ilitakiwa kupigwa mnada,...hukuniambia, lakini mimi nilikuwa najau mapema,...jamaa wakaja hapa wakakutia jambajamba...ukawakatia vijisenti, wakaondoka, mimi niwajua, na najua hiyo...nikaenda ofisini kwako, wakawekwa sawa, na mambo safi...ukiwa na pesa unaringa....’akasema huku akihesabu pesa alizokuwa nazo mkononi.

‘Mimi nakuambia  utaishia kubaya...ipo siku ....tupo...’nikasema kwa chuki na hasira...

‘Wameshasema wengi,..ngoja nikufungue macho na masikio, haya hayakuanzia leo au jana, siku unatoka huko Ulaya, tulishaanza kukusoma, mimi nakujau toka huko kijijini, najua uzaifu wako...ulipomuoa Bintii Yatima, tukasema tumekukosa, ....lakini mwenyewe ukajileta, kilaini ..'akasema huku akicheka.

'Mimi nilishasema tumekukosa, ila wenzangu wataalamu wakasema vuta subira, ..kosa limeanzia pale pale wanapokosea wenzako, kutokuijua misingi ya ndoa yenu, kosa,.... uzaifu wako kosa...na kosa hilo ni kwa wanaume wengi....unaoa unalemaa,   huku natamba mimi nimeoa, au nimeolewa...hata wanawake, wanaona wameolewa basi tena...' akaongea huku katizama pembeni, mimi nilikuwa namsikiliza huku hasira zikinipanda.

'Hilo ni kosa kwa wanandoawengi, .ukioa au kuolewa iwe ni mwanzo wakuijenga ndoa,...iwe kama nyumba, kila mara inahitaji uangalizi, ....vingenavyo litakuwa hema tu...sisi ndio makazi yenu kwenye hayo mahema, ...hayo tulishayajua...ndipo hapo tukaona kuna  mwanya wa kufanyia vitu vyetu,...ndani ya mahema, ... sasa tupo kazini....ukishituka tushamaliza..’akasema na kunisogelea akijaribu kunikumbatia, nikamsukumia mbali na kusogea pembeni mbali na yaye, yeye akacheka na kuniangalia, halafu akasgeuka upande mwingine na kusema;

‘Usinichukie,mpenzi..eeh,...hata hivyo, kazi na dawa, usijli ,maneno ya watu, kama maneno yangelikuwa yanaua mara moja, ningelishakufa siku nyingi..lakini bado muda wangu, najua ipo siku zamu yangu itafika , lakini sio kama utakavyo wewe....hapa tulipo, kuanzia sasa tunaonekana ,....jitahidi kuwa mwangalifu....’ akaonyesha kidude fulani kipo juu...hakikuwepo kabla, akasema;

‘Hicho ni moja ya vitu vya ulinzi, badoo vipo vingine visivyoonekana....hii sio kazi ndogo, wenzako wamejiimarisha kimataifa...hii nyumba sio yako tena, na mimi ni...wapo wenyewe...ipo siku utakutana nao...’akacheka na kunitizama machoni.

‘Usipoteze pumzi yako, na uhai wako kabla ya wakati, ...kuanzia sasa mimi ni bosi wako, utafanya lile ninalotaka ufanye....vinginevyo nitakufukuza kama mbwa...na hutachukua siku mbili utakutwa kwenye mtaro...ipo mijibwa ikiamrishwa, itakufanyia kitu mbaya...hutatamaani tena kuishi kwenye dunia hii...’akasema huku akiniangalia kwa uso ambao sijawahi kuuona kabla.

‘Usinitishe kabisa..mimi mtoto wamjini, tutapambana humuhumu...utaona ...’nikajipa matumaini

‘ Sawa, ila nisikiliza kwa makini,  yule mama Muhindi anaoekana anakutaka na mimi, na cha ajabu mumewe naye toka siku nyingi ananisololea mimi, lakini namtolea nje, kiama chake kishafika ....kwetu sisi yote ni sawa, tunawahitaji sana watu wa namna hiyo...sisi ni mshetani....kazi yetu ni kusubiri, ukijileta tunakufanya ile unayaotaka...’akasema huku anaonyesha meno nje, kama wafanyavyo mashetani.

‘Hivi wewe...unafikiri utaishi dunia hii milele...’nikasema huku nikimshangaa. Nikainuka palekitandani ni kukaa mbali na yeye,na yeye hakujali akagukia upande mwingine, huku akiwa kashikwa kichwa kama kukiegemezana mkono huku akiwa hanitizami, na mimi namwangalia kama mtu ambaye sijawahi kumuona kabla...

‘Muda huo huo mfupi, tunautumia....sasa nisikilize kwa makini, hapa ni mjini, ukizubaa utakufa njaa, ...wewe upo na mimi, kama pete na kidole, utalijua hilo baadaye kwanini nasema hivyo....kwasasa kila mtu anajua wewe ni mume wangu....lakini kuanzia sasa kisiri....unanielewa kisiri...’akawa kama ananing’oneza  masikioni.

‘Mimi ni bosi wako....utafanya kama nitakavyokuagiza...’maneno hayo yalikuwa yakijirudia kichwani mwangu wakati wote, utafikiri aliyagandisha kwenye ubongo wangu, na hata pale nilipokuwa nikimsubiri mama wa bosi ambaye alishaniambia nifike kwake kwani kuna kazi natakiwa kufanya, maneno hayo yalikuwa yakijirudi akichwai kwangu  mara kwa mara....`mimi ni bosi wako.....’

               *********

Siku hiyo niliamuka mapema sana,na cha ajabu nilipoamuka sikumuoma mke wangu, wala sijui aliamka saa ngapi na wala sikujua wapi amekwenda. Hata hivyo jana aliniambia kuwa yeye atakuwa anafanya mambo yake kivyake na nisiwe namuuliza kwanini labda kama ni mambo ya kawaida ya ndani.

‘Ujue sisi ni mke na mume, hilo litabakia hivyo usoni mwa watu...lakini mengine ni siri yetu...’aliniambia.

 Kuanzia pale na nikaanza kumchukia, na hasa aliponionyesha ile sura ya ukatili...nilimuona kama shetani fulani, na kama ningelipata silaha kwa muda ule,nisingesita kuitumia. Basi sikujali nikaamuka na kujiandaa kwenda kibaruani, nikijua sasa ninalo, na cha muhimu nikutokuogopa, maana nikiazna kumuogopa huyu mtu atanifanya mtumwa wake. Lazima nipambane naye hadinione mwisho wake...nikaahidi hivyo.

Nilipofika kazini, nikasubiri maana sikuwa mzoefu wa eneo hilo, ingawaje nilishwahi kufika mara kwa mara tukiwa tumetumwa kuchukua bidhaa hapo dukani. Nikasubiri hadi bosi alipofika, na alipofika tu akaniita ofisi kwake,...nikamfuata huko ndani ya ofisi.

Kichwani nilikuwa nimevaa kofia pana, ambayo nilipewa namkewangu, niliambiwa niingia ndani ya hiyo ofisi, niivue ile kofia niiweke sehemu ya juu,, kama ni kabati au sehemu yoyote iwe ya juu, na chombo kama cha kuskilizia mzika nitakuwa nacho, hataweza kujua ni chombo maalumu, kumbe hicho kiliunganishwa moja kwa moja kwenye simu yangu.

Nikakumbuka kwanini mke wangu aliniazima simu muda faulani nyuma, na tangu siku ile kila kinachotendeka nyumbani anakijua, kumbe.....hapo sasa akili ikaanza kutambua kuwa huyu mke sio kamaninavymjua mimi, ni jambazi sugu....hata nilipojaribu uichunguza simu yangu sikuona kitu kipya, ilikuwa ileile, isipokuwa huo waya wa kuskilizia mziki, ambao ni wa kawaida tu..

‘Na weye unapenda kusikiliza miziki kama vijana....mimi wakati naongea nataka unisikilize mimi tu..kwanza njoo huku ndani....’akasems yule mama wa Kihindi, name nikamfuata kutoka kwenye ofisi na kuingia kwenye chumba cha ndani,nikashangaa, kumbe huku ndani kuna chumba kidogo, ambacho kilikuwa na sofa kubwa, ambalo unaweza kulikunjua na kuwa kitanda, kuna jokofu la kuhifadhi avinywaji, kuna kabati la vitabu, na vifaa vya ndani kama chumba cha msela.

Nikakumbuka siku moja jamaa yangu aliniambia kuwa  huko kwa bosi alipokuwa akifanyia kazi mwanzoni, kuna ofisi ya ndani kwa ndani hapo ndipo alipokuwa akifanyia mazambi yake na akiandada waliokuwa wakitaka pesa za harakaharaka...ni hadi mkewe alipokuja na yeye akahamishiwa huku kiwandani...

‘Unaona hii,...ofisi ndogo ya kumpumzikia, hii  ni kazi ya mume wangu,...nimeijua mengi alikuwa kifanya humu, .sasa nataka nifanyie na yeye kama alivyofanyia mimi....wajua nataka nini weye...kwanza penda umbile oko...?’akasema huku akianza kunishika  shika....

‘Bosi vipi. hapana..mbona..aah, ...ooh,  hujui mume wako akinishika hapa...itakuwa taabu ....’nikaanza kulalamika, na yeye akasema mume wake hawezi kuja hapo mpaka kuwa na mawasilino kuwa anakuja,.....

‘Akikushika shika ujifanye kama hutaki-wataka, lakini hakikisha lengo lake linafikia sehemu ambayo inathibitisha kuwa mnafanya tendo...unanielewa ....hili nataka lifanyike, jinsi ninavyokuelekeza ...vinginevyo bwana hatutaelewana, nitakutupa barabarani uchi, ....huna nyumba hapa, huna pesa....unataka ukalale vichochoroni, kama hutaki hilo fanya lile nitakalokuambia ufanye...’ nikawa nayakumbuka maneno ya mke wangu Kimwana.

‘Weye una umbo zuri, hebu toa shati yako..taka ona kifua yako....’akaamurisha huyo mama, nami nikajifanya kukataa, akanijia na kuanza kunito akwa nguvu, ...na baaaye akasema nivue suruali...ooh, hapo nikaona imezidi mpaka, na nilipokataa akanijia na kunivua kwa nguvu....mwisho nilibakia kamanilivyozaliwa...nilijisikia vibaya....

‘Sasa kweli una umbo safi weye, kuja hapa sasa,....vua na mimi hii nguo....’akaamurisha, nami nikawa nafanya kama anavyotaka yeye, akili pale ishachanaganyikiwa, damu inanichemka,  kilichofuata hapo tena sikuweza hata kuhadithia, ilikuwa ni sikio la kufa hakisikii dawa, kwani sikuweza kuvumilia , kama ujuavyo damu yangu inachemak kweli...na nilishituka nikiwa nimeshavuka mpaka wa makubaliano na mke wangu, alivyotaka;

‘Hakikisha hamfanyi tendo lenyewe,ikifia hatua hiyo ya tendo mtolee nje,... ili akuhitaji tena na tena....unanielewa,... ole wako uvunje masharti, najua tamaa yako ilivyo, itawale kwa hilo,  ukitawaliwa na tamaa zako hapo utajuata....unisikilize kwa makini, kwani zaidi ya hapo tamaa yako itakutokea puani mwenyewe...’nilikumbuka alivyosema mke wangu.

‘Oh, mungu wangu nimefanya nini tena....ume....oh’nikajikuta nikilalamika.

‘Usijali mimi nitakupa pesa mingi,na nitakufungulia duka lako menyewe,kwahiyo utakuwa uankuja kufanya kazi hapa kwangu kila siku...napenda weye sana...’akasema huyo mama, na baadaye nikaonyeshwa akzi ya kufanya,lakini akili yangu haikuwa hapo, nilikuwa natafuta njia ya kuharibu ile simu,maana najua mambo yote yamerokodiwa hapo.

‘Kama maliza kuja huku...’nikasikiasauti ya bosi wangu ikiamrisha.

‘Sawa Bosi...’nikasema huku nikikurupuka na kumfuata huko ndani na huko nilionyeshwa kazi nyingine ya kupanga maboksi ya bidhaa mpya zilizofika , kuzitoa kwenye maboksi yake na kuyaweka kwenye maboksi mengine,ili yaonekane ni  kutoka Ulaya...nchi hii bwana ...ukiuziwa kitu unaambiwa hii mali toka Ulaya, kumbe imetoka huko wapi sijui....mjini hapa, ...bongo ya wenyewe.

Ilipofika saa sita nilikuwa hoi, maana hapa kazi haina makadrio , ni kufanya tu, mara hiki mra kile...na baadaye ikafika muda wa mchana,...nikajua hapa bosi ataagiza msosi wa maana,...na kweli akaja pale nilipokuwa napanga panga maboksi,kwanza akaniangalia kwa makini, halafu akanituma nikamnununulie chakula kwenye hoteli ya jirani...nilijua na mimi nitanunuliwa chakula change, lakini haikuwa hivyo.

Nikasema haina shida, ....nikakimbili hiyo sehemu niliyoagizwa kuwa ndipo anaponunulia chakula chake, nilipofika hapo nikakutana na msichana mmoja namfahamu tukasalimiana naye kidogo akaniuliza nafanyia wapi kazi nikamwambia, alishangaa kidogo, kwani hakutegemea kuwa nitakuwa huko na baadaye akaniuliza;

‘Hivi nasikia umemuoa yule binti Kimwana....?’

‘Ndio mbona siku nyingi tu...’nikasema.

‘Haya wee,....unajua niliskia kuwa Kimwana anaolewa,, nikasema kama nikimjua huyo mume anayetaka kumuoa nitamtonya.... maana ningelijua mapema kuwa ni wewe ningekushauri vinginevyo, uachane naye....lakini ndio hivyo ukipenda kitu sio rahisi kushauriwa....’akasema.

‘Kwani ana nini kikubwa...?’ nikauliza kwa mshaka.

‘Hata nikikuambia sasa hivi utaamini, mtu umeshalamba asali na kuiona utamu wake, wewe jichunge tu, ...maana unaweza ukaingizwa mkenge....huyo ni mtaalamu wa kitu kinachoitwa `mlungula’ au kwa lugha ya wenzetu wanaita `blackmaili ‘ akasema na kunifanya nitake kuangusha kile chakula nlichonunua.

‘Hapana sio kwasasa, ...labda kama ilikuwa hivyo ni zamani, ulishakutana naye siku hizi za karibuni, mbona katulia, kaamua kubadilika kabisa baada ya kuolewa...hayo mambo ni ujana, baadaye unajuata unaamua kujituliza...nina imani tabia hiyo keshaisahau...’nikamwambia.

‘Ndio maana nasema kwa hivi sasa hakuna kitu utasikiliza,... ila ninachoweza kukuambia ni kuwa wewe sio mume wake wa kwanza, wenzako walisema hivyo hivyo, sasa wanajuta na wengine hawapo duniani,...nisikutishe sana, ila nakushauri sana uwe mwangalifu...’akaniambia.

‘Ahsante ngoja nimpelekee huyu bosi chakula chake...’nikasema.

‘Bosi wako ndio huyo mke wa bosi ambapo mkeo anafanyia kazi,...au sio?’ akauliza

‘Ndio ...nani kakuambia hyo,....’ kablahajanijibu nikamwambia `...baadaye basi...’nikasema nikaharakisha kurudi kule kazini, kwani niliona nimetumia muda kidogo kuongea na huyo binti, na mimi nsingelipedna kuonekaan mzembe wa muda. Na wakati natembea kwa haraka, akili yangu ilikuwa ikinituma niiharibu ile simu.

Nilipofika hapo dukani nikampa chakula chake na akakigawa mafungu mawili, na kunipa sehemu mojawapo, nikashangaa kwanini asingelenininunulia chakula changu mwenyewe, ananunua chakula cha mtu mmoja halafu anakigawa  mara mbili, huo ubahili wa hali ya juu sana...nikamwangalia machoni

`Kula hiyo chakula,...kula sasa hivi...’ kwasabbu nilikuwa na njaa nikaanza kukila kwa pupa tu, nay eye akatabasamu na kuchukua chakula chake na kundoka.

Nikala  kile chakula,....na baadaye akaniita tena kule kwenye kile chumba, safari hii sikukubali kirahisi, nikawa nasita kwenda, lakini baadaye nkawaza nakusema bora niitikie wito kwanza, ...mengine nitajua hukohuko ndani, maana ndio bosi tena....., ikabidi nimfuate huko ndani, tulipofika nikakuta anaanza mambo ni yale yale, safari hii sikukubali,....nilifanya kama nilivyoagizwa na mkewe wangu,...siju kamaitasaidia....

‘Sikia mimi nataka ufanye ninavyotaka mimi, ...kama unaleta jeuri nitafukuza kazi weye......nasema nitakupa pesa mingi na kukufungulia duka...sikia eeh, ...fanya hii siri....’akasema na mara simu yake ikaita, akapokea na kuanza kuongea na mume wake. Waliongea kwa muda, na ilionyesha kuwa mume wake alikuwa akidai pesa nyingi ambazo mkewe hakupenda zitolewe. Mimi najua jua Kihindi....nilikipatapata kidogo.

‘Lazima uniambie zakazi gani,pesa yote hiyo ya nini....?’akauliza mkewe
Baadaye wakawa wanakuja wageni, na lile zoezi likakwama had muda wakuondoka ukafika, na hapo nikshukuru mungu. Nilipotoka hapo nikafika hotelini,maana nilipewa hela nyingi kidogo, nikaagiza chakula, na wakati nakula mara mtu mmoja akanishiak begani.

‘Nani wewe....?’nikauliza nakugeuka nyuma kwa hasira, nikiwazia vibaka wa Dar, ambao wanaiba kwa mtindo huo, uitwaoo `mdudu’ ukishikwa bega ukigeuka, wanakuchomolea pesa iliyopo mfuko wa shati....

‘Tulia..wewe.. hata mkono wa mkeo huukumbuki, naomba hii simu yako....mara moja’ akasema na kuichukua haraka, kwani kwa muda huo simu yangu ambayo ilikuwa pale juu ya meza, nilishaanza kuifungua, nikiwa na malengo ya kuiharibu, lakini bado nilikuwa nasita maana simu yangu naipenda sana.

‘Simu yangu ya nini bwana...’nikasema na kutaka kuichukua...

‘Sikiliza ...tulikubaliana nini....na mambo yote yapo humu, usiwe na shaka, kila kitu niachie mimi, wewe huna tatizo lolote...ilimradi uwe umefanya kama nilivyokuagiza..nikuambie kitu, kwanza mambo mengine yameshaanza, sasa hivi nasubiri kupokea pesa nyingi kidogo, tatizo ya hizo pesa zina mikono mingi na sehemu kubwa inakwenda kwa...mama....’akasimama hapo huku akitoa kitu fulani kwenye ile simu yangu.

‘Haya chukua simu yako, na kesho nitaichukua tena kurudishia hicho kidude...ki...’akasema na wakati huo alikuja muhudumu wa ile hoteli, yeye akanilipia chakula na akashikana mkoo na yule mhudumu , na yule mhudumu akanondoka, ...sikujua kwanini wameshikana mkono. Baadaye tukaondoka kurudi nyumbani huku kichwa kikiniwanga.

‘Ukifuata ninavyokuagiza , hutaamini, umasikini wote utausikia kwenye bomba, ila ukivurunda, utaniona sura yangu iliyojificha, mimi nina sura mbili, ya kike na ya kiume, hiyo ya kiume inaonekana mara moja tu, na anayeiona hataiona tena hadi mwisho wa dunia...wanasema nina shetani dume, likitokea kuondoka kwake mpaka linywe damu ya mtu,.....natumai unanielewa...’akasema.

‘Una maana gani...usinitishe kabisa, kwanini mnataka kuniingiza kwenye majaribu ya mlungula, hamjui hiyo nikinyume cha sheria na yule ni mke wa mtu, unafikiri mimi ni jiti eeh, sina hisia ...wengine hisia zetu hazina subira, siwezi kuvumilia kiasi hicho..’nikasema.

‘Sio tatizo,....kama uliisaliti ndoa yako, utajuata...unajua hisia zako zisizo na mpaka, zitakuponza, ...sawa, lakini tatizo ni kuwa hicho chombo kinaenda kuangaliwa na mama na kundi la wataalamu, hivi utajisikiaje ukiwa unaangaliwa na watu hawo, na wakati huo wewe ni mume wangu, na mimi natakiwa niwepo hapo, ....ndio maana sikutaka utende zaidi ya nilivyokuagiza...’akasema.

‘Mungu wangu, hebu kilete hicho chombo,....usikipeleka....’nikasema

‘Umeshachelewa, huyo dada aliyekuja kuchukua pesa ya chakula ulichokula ni mmoja wa wasichana wa mama, na kazi yake ndio hiyo kupeleka hivyo vifurushi kwa mama....kama ulivurunda huko shauri lako..ukiniabisha tutakuja kupambana wenyewe.....’akasema na kunifanya nitamani dunia ipasuke nizame.

‘Naapa kuwa nitawafanyia jambo ambalo hamtakuja kunisahau...’nikasema huku nikiwa na hasira ambayo haijawahi kuniingia moyoni mwangu. Na hata tuulipoangaliana mimi na yeye aligundua hilo, akaniangalia kwa macho makavu, halafu akageuka pembeni na kusema;

‘Usiape,...maana wapo walioapa kabla yako na kiapo chao hakikuwasaidia kitu na wengine kiapo chao kiliwapeleka kuzimu, waliamua kujiua,....haisaidii kuapa, kinachotakiwa ni matendo, fanya unaloona ni sahihi kwako, ...usichelewe, ukichelewa wenzako wanawahi, utaapa haya umeapa, kipo wapi .... sisi mwisho wa siku tunajitwalia mshiko, ...lengo letu linatimia, unavohaha hivyo ndio tunacheka,....’ na kweli akacheka sana.

‘Unacheka, unafikiri mimi hapa napendezewa na mambo hayo, unaniumiza sana,na sio siri chuki niliyonayo kwako sijawahi kuipata kabla....’nikasema kwa hasira.

‘Natumai umenielewa, usifikiri hata mimi napenda kukuumiza, hapana, lakini inabidi iwe hivyo, kimaslahi na kiusalama wangu, ....ipo siku utajua kwanini, nikuambie uwkeli, nimekutana na wanaume wengi, katika kazi hii, lakini wewe umekuwa wa pekee katika moyo wangu,..hata hivyo moja ya masharti yetu, ni kazi kwanza, mengine baadaye, kwahiyo...kama unataka uendelee kukaa na mimi ufuate ninavyokuagiza, ukijifanya kichwa ngumu, ukakiuka, utakutana na mume mwenzako,sura yangu ya pili....’akasema.

‘Sawa tutaona...’nikasema huku nikishika kichwa na kuwakumbuka wazazi wangu,....na sura ya mke wa kwanza ikanijia ikinitizama kwa masikitiko na ile kauli ya mjomba ikawa inasikika kwa mbali na neo lililosikika vyema ni `kizingiti '....

NB: Nawashukuru sana wale wote wanaosoma visa hivi, wengine wanaona labda ni hadithi za kubuni tu,lakini kama kweli uliwahi kujichanganya mitaani, vijijini ukaishi na watu, haya yanatokea sana....na hata mkichunguza ndani ya ndoazetu, matatizo haya yapo, tunajenga ndoa lakini hatuzijali, zinakuwa kama nyumba iliyohamwa, zinakuwa mahema....

 Naomba ushirikiano wenu, kwa maoni na ushauri, na kama hamtojali, nipendekezeni kwa wingi kwenye blog ya:
http://www.tanzanianblogawards.com/ ili tuitangaze blog yenu hii kama mnaona haya ninayoandika yana faida kwa wengine pia. Tupo pamoja

WAZO LA LEO: Mambo yakutuzidi hasa wanandoa, tujaribu kuomba ushauri kwa wazee wenye busara, sio kwa kila mtu, ukumbuke mambo yandani ya ndoa ni siri za ndoa, huruhusiwi kuzisema kwa kila mtu, ukiwa mpayukaji wa mambo yako ya ndani ya ndoa, kwanza unavunja miiko ya ndoa, pili wasiokutakia mema watachuku mwanya huo kukuharibia, siri ya ndoa ni kwa wanandoa wenyewe.


Ni mimi: emu-three

4 comments :

elisa said...

Jamani ,sijui nisemaje! Ila kwa sisi wenye imani Mungu yupo ,inatakiwa tusali sana ...huyu jamaa alifungwa kabisa !haambiliki wala haelewi !

Precious said...

Haya mambo yapo sana kwenye maisha yetu ya kila siku. Tuko pamoja M3 tutakupigia kura kwa wingi mpk Blog yetu ishinde kwa kishindo.

Anonymous said...

This is the perfect site for аnybody who wіsheѕ to
understаnԁ thiѕ tοpic. You reаlize a
whole lоt its almost tοugh to argue with you (not that I rеаlly would want to…HaHa).
You сertainly put a frеsh spin on a subject which has
beеn discussed for yеars. Eхcellent stuff,
just wondeгful!

mу blog post - angielski

Anonymous said...

What's up to every body, it's my first visit of this blog; this website consists of awesome and truly good material designed for visitors.


My website: very midsummer