Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, September 7, 2012

Mbio za sakafuni huishia ukingoni-sehemu ya pili-3



  Sijawahi kufika Dodoma, ilikuwa ni mara yangu ya kwanza, na ingawaje nilikuwa na mzigo wa kuuza, lakini hilo halikuwa akilini kwangu kabisa, kwani kichwani kulijaa mawazo , chuki , hasira na wivu. Vitu hivyo vilinifanya nishikwe na jaziba, ambayo sijawahi kuwa nayo kabla, na  kila dakika iliyokuwa ikipita kwangu ilikuwa kama mtu anayepigilia msumari wa moto kwenye akili yangu, na hasa pale nilipokuwa nikiikumbuka ile video nilyoiona kwa yule mwanadada.

Niliangalia huku na kule kama ninaweza kumuona mume wangu, lakini hakukuwa na dalili yoyote, nikageuka kumwangalia mwenzangu ambaye alikuwa haonyeshi dalili yoyote ya wasiwasi, yeye alishaanza kuongea na wateja wake. Baadaye akanijia na kunishika bega, akasema;

‘Haya maswala hayataki hasira, na lolote utakaloliona huko liwe akili kichwani mwako, maana ukitumia nguvu, ukaweka hasira yako mbele, utakosa kila kitu, hii iwe sehemu ya uchunguzi tu,…kumbuka maelekezo yangu, huku tumekuja kwa ajili ya biashara na si vinginevyo….haya twende makaoni,….’akaniambia yule mwanadada, na tukachukua taksii hadi huko makaoni.

‘Lakini mimi bado siamini, maana nimemuliza mume wangu kakataa kata kata, na hata kuniapia kuwa yeye hawezi kufanya jambo kama hilo, …’nikakumbuka nilivyomwambia, na huyu mwenzangu hakutaka kunijibu lolote.

Tukiwa kwenye gari simu yake ikaita, akachukua ule mkoba wake, na hapo nikajikuta nikishikwa na wasiwasi, …ule mkoba, nikakumbuka kile kitu...nikageuka haraka kuangalia nje, na kuyaondoa hayo mawazo haraka kichwani, sikutaka kuwazia mabaya zaidi. Nilichofanya ni kuanza kuwaza maisha yangu na mume wangu, ili kuondoa mawazo hayo mengine kichwani. Kwa ujumla, sikutaka mawazo mengine yaniteke akili yangu, na ili nifanikiwe hilo nikajikuta nikiwaza siku ile mume wangu aliporejea  toka Dodoma .

Siku ile nilikuwa sina raha , nilikuwa nimeshaanza kuathiriwa na mawazo, hasa baada ya kupata hizi taarifa kuwa mume wangu naye ni miongoni mwa hawo wenye nyumna ndogo, …nilijitahidi sana kutokumuonyesha hasira nilizo kuwa nazo, kwani bado nilikuwa sijaamini.  Lakini nahisi aligundua mabadiliko fulani.

*****

‘Mke wangu mpenzi vipi mambo ya hapa, nimekumisi sana, kila siku huko kwenye kikao nilikuwa nikikuwaza wewe, nilitamani nikatishe kikao nije nikuone…’akaniambi huku akinikumbatia, na mimi nilikuwa kama mti,  mwili mzima ulikuwa wa baridi, na kitendo kile kilifanya fundo nilililokuwa nalo moyoni litake kupasuka, nikajitahidi kujifanya na mimi nipo naye, nikasema kinafiki;

‘Hata mimi mume wangu, na nashangaa siku mbili hizi nimekuwa nikiota kuwa naibiwa, maana nasikia huko Dodoma kuna wanawake warembo, ambao kazi yao kubwa kuwaburudisha wanasiasa wanaokwenda huko, wakijua kuwa mna pesa nyingi za kutumia…’nikamwambia.

‘Hayo ni yao, na kama wapo watu wa namna hiyo, wanafanya hivyo kwa tamaa zao. Siwezi kukukatalia kwasababu watu tunatofautiana, na mambo kama hayo yapo, lakini kila mmoja ana akili zake, kama una mke unayempenda kama mimi ninavyo kupenda wewe kwanini nijiingize kwenye tamaa hizo’akaniambia huku akijaribu kuyakwepamacho yangu.

‘Ni kweli ni tamaa, na tamaa za wanaume hazina mpaka…na uwongo wenu hauna dini, maana unaweza hata kuapa, wakati ni kweli umefanya hivyo,…’nikaanza kumwambia, na yeye akageukia dirishani na kusema;

‘Mimi, nifanye mambo hayo…hapana, nani wa kukuzidi wewe, hilo usidanganyike,na kama kuna mtu kakudanganya hivyo ujue ana lake jambo’akasema.

‘Mumu wangu nakupenda sana, na sitavumilia kama nitagundua kuwa una mtu mwingine, na ukumbuke tulipotoka, ukumbuke uliponichukulia, wengi walinitaka na wewe pekee ndiwe uliyefanikiwa kunichukua, sasa isje ikafika mahali nikajuta na kusema aheri ningekwenda kwa yule mwingine…’nikamwambia na niliona akibadilika sura, akasema;

‘Lakini hayo yote yametoka wapi mpenzi wangu, ni nani mlikutana naye akaanza kukudanganya, ndio maana nakukunya usikae na marafiki, wengi wa marafiki ni waongo, na wanaweza wakatunga uwongo wenye sawa na ukweli, ukaamini, na kumbe hakuna kitu….chunga sana mashoga, hawo watu sio wema, na hawapendi wenzao wakiishi kwa upendo na amani’akaniambia huku akijbaragua kwa kushika hiki na kile.

‘Mume wangu, dunia sasa hivi haina siri, mambo ya mitandao , mambo ya kisasa, yanaweza yakaonyesha kila kitu, zamani wazee wetu walitumia ramli  wakajua ya ghaibu,lakini siku hizi kuna mitandao, inaweza ikaonyesha kila kitu…upo chumbani kumbe wenzako wameweka mitambo inaonyesha siri zako,…’nikasema na yeye akaniangalia kwa mashaka.

‘Mke wangu vipi, mbona unanitisha, mbona unakuja na hoja za kunipa wasiwasi, kuna nini kimetokea hadi ufike kuongea hayo, unataka kusema nini…..?’akaniuliza akiwa na wasiwasi.

‘Natumai umenielewa, nililotaka kusema ni hilo, kuwa uwongo una mwisho wake, na mbio za sakafuni maranyingi huishia ukingoni, ukumbuke tulipotoka, ukumbuke magonjwa, ukumbuke mungu wako, kuwa lolote utakalolifanya kwa siri, mungu analiona na ipo siku ukweli utadhihiri na kuishia kuumbuka’nikasema na yeye akatulia kimia.

‘Mume wangu kumbuka alivyosema dakitari kuwa mimi nina dalili za shinikizo la damu, la kushuka, na nijitahidi sana kutokupata mishituko au mashinikizo ya mawazo.Na hilo nimejitahidi sana, na mtu wakuweza kunisadia zaidi ni wewe…nakuomba tafadhali usije ukaniua….’nikasema na yeye akashika shavu, kuonyesha kuumia kwa namna fulani…

‘Mke wangu ina maana huniamini…?’ akaniuliza

‘Nakuamini ndio maana nakuambia hayo,….’nikasema na baadaye mazungumzo yalikatishwa na wageni, maana hayo mambo yao ya siasa hayampi mtu muda wa kuongea na mwenzake, simu, wageni, ilikuwa  ni kero.

*******

‘Halloh, mwanadada,ni mimi mke wa kiongozi, nilitaka kukuambia kuwa mume wangu kaondoka leo asubuhi, kwenye mambo yao ya kisiasa, sasa nimekaa nakuwaza sana, nikaona ili nisiumie na mawazo, ni bora nijirizishe,…’nikasema kwenye simu.

‘Hata mimi nina safari ya huko, na umefanya jambo la maana sana, maana huko kuna biashara msimu huu, nguo zako na vipodozi vinahitajika sana. Unajua hawa wakubwa, wakifika huko wanahitaji zawadi kwa washikaji zao, sasa hapo ndipo soko linapozaa matunda, nitakupigia simu nikuelekeze vitu gani vya kubeba..’akasema huku akikwepa kuongea lolote kuhusu madhumuni ya hiyo safari.

Baadaya alinipigia simu na kunielekeza nini chakubeba, aina gani za nguo, vipodozi na bidhaa zingine ambazo alisema zinahitajika sana huko.Na hata nilipotaka kuongea madhumini ya hiyo safari, yeye alikwepa na kuongelea maswala ya biashara tu.

Nilipokutana naye aliniambia kwanini hakupenda kuongea lolote kuhusu madhumuni ya hiyo safari,kwenye simu akaniambia;

‘Kumbuka haya mambo yanahitaji usiri mkubwa, simu siku hizi zinasikilizwa, na kumbukumbu za mazungumzo zinanaswa na kuhifadhiwa,…unatakiwa uwe makini. Na sijui mumeo anajua nini kuhusu hii safari, natumai hujamwambia lolote kuwa utasafiri kwenda huko kwenye vikao vyao….’akasema.

‘Mimi nilimwambia nitasafiri kwenda Morogoro kupeleka mizigo, na kama inawezekana naweza kusogea mbele kidogo, lakini sikumwambia mbele wapi, kama ulivyonielekeza siku ile.

‘Mizigo yenyewe ndio hii tu,….mbona?’ akaniuliza .

‘Ipo  nje kwenye gari, hii nimekuja kukuonyesha kuwa kama na yenyewe inafaa twende nayo, au kama haifaii nitaiacha hapo kwako’nikasema.

‘Inafaa….twende nayo tu, biashara nyingine unajaribu, huwezi jua’akasema huku akiingalia vile vitu nilivyokuja navyo

‘Safi kabisa…vinafaa,…unajua, ni bora sana kuchukua tahadhari, maana safari ni hatua lolote linaweza kutokea, na utashindwa jinsi gani ya kujitetea likitokea jambo la hatari, hatuombei mbaya, lakini yote hutokea, au sio...'akaniuliza na kabla sijajubu lolote akasema;

Hapo, umefanya vyema kuwambia kuwa huenda tukasogea mbele kidogo.Sasa angalizo, nii kuwa hatutakiwi kuongea lolote kuhusu hayo yanayotupeleka huko, tukitoka humu ndani, mazungumzo yetu, tukitoka humu ndani yatakuwa kuhusu biashara, hadi tutakapofika huko, na hata tukifika huko mazunguzo yetu ni hayo hayo….sisi ni wafanya biashara, hiyo ndiyo nembo yetu…unielewe kwa makini’akaniambia.

‘Lakini mimi bado nina wasiwasi….’nikamwambia.

‘Wasiwasi wa nini…usiwe muoga, uwoga hujenga magonjwa kama shinikizo la damu ….uwe jasiri, hasa unapokuwa katika maisha ya ndoa, ukiogopa wenzako watachukua huo udhaifu wako na kufanya mambo yao. Sikiliza, hayo unayokwenda kuyafanya ni kwa ajili ya misha yako ya baadaye, …’akaniambia.

‘Lakini nakuapia, kama unanitega kwa lolote sitakusamehe hadi kufa,, na sijui nitakufanya nini’nikasema kwa hasira.

‘Hilo utajionea mwenyewe , wewe tukifika huko, utaniambia…..Na sikiliza,  mimi nataka unitambue kama dada yako, na ukikwama kwa lolote, niambie, nitakusadia, na hili nataka ulichukuliea kama sehemu ya malipo yangu kwako, maana ulikubali kuniachia huyu mtu,licha ya kuwa sasa najuta ,lakini yote ni majaliwa.

‘Sawa haya twende , maana kwa sasa sina jinsi, …’nikamwambia.

‘Wewe utakuja kuniambia, …ila nakukanya tena, tunaondoka hapa kama wafanyabiashara, na tukifika huko kazi yetu kubwa ni kutafuta wateja, mimi nawafahamu, kunasehemu tunaweka mizigo yetu , ni sehemu tumekodi, mimi mwenyewe nina duka alngu kubwa tu…’akaniambia.

‘Mwenzangu upo mbali kweli..’nikamwambia nikijaribu kuondoa mawazo.

‘Ni kuhangaika, na kinachohitajika ni ujasiri, ..ukithubutu, utaweza, lakini ukiweka unyinge na kusema sitaweza, na kweli hutaweza. Mimi nimejifunza mengi ndani ya ndoa, na nilishajifunza mengi kabla ya ndoa, kwahiyo maisha nayajua vyema…’akaniambia.

‘Hongera’nikasema.

‘Hongera haisadiii, kinachotakiwa na wewe ujifunze, kwani kuna leo nakesho, angalai wajane wengi wanavyoteseka, kwasababu walijipweteka, wakijua kuwa kila kitu kitatoka kwa mume, sasa mume huyo hayupo, huenda kafariki au ameachika, anashindwa maisha, …hilo tunatakiwa tuwe makini nalo’akaniambia.

‘Lakini….

‘Lakini nini tena, sikiliza, kama bado moyo wangu hujajipanga kwenye hii safari , tafadhali rudi nyumbani kajipange vyema, …mimi sitaki mtu anayedeka, nataka mtu ngangari, ukifika kule uwe na ujasiri, uwe makini kwa kila tendo, ujue hutakiwi kujulikana,  na kwahiyo uvaaji wako wa huku utakuwa tfauti na wakule, kuna wanawake kule wanajua jinsi gani ya kukuvalisha na kukuweka mwili wako uwe kivingine, hayo ni ya huko…’akasema.

‘Una maana gani kusema hivyo.?’nikasema kwa wasiwasi.

‘Wewe ,mwanamke wewe, upo dunia ipi, …kumbuka huko tunakwenda kama wafanay biashara, na wateja wetu sio wazee,.hata kama kuna wazee, kule wote wanakuwa ni vijana, sasa watavutika vipi na biashara zako kama na wewe huan mvuto. Biashara ni pamoja na mtangano yenye mvuto’akasema.

‘Mbona unanitisha…’nikasema na kutaka kuondoka.

‘Hahaha…tatizo lako umefikiria vingine, …nikuambie ukweli, hakuna kitu kinachouza bidhaa kama matangazo, vitu vya mvuto. Mfano ukiweka muuzaji mrembo kwenye duka lako, wateja wengi watafika hasa vijana, hasa matajiri na watu wote hupenda urembo, asikudanganye mtu, na….ndivyo ilivyo, sasa ukumbuke wewe unakwenda kuuza bidhaa zako, ni lazima uwe katika hali ya kumvuta mteja…uvaaji wako, taswira, tabasamu..ni siri ya biashara…tukifika huko hutakiwi uvae kama ulivyovaa hapa…’akaniambia

‘Na pia nataka ujue kuwa tukishakubaliana hapa hakuna marejeo, maana mipango inapangwa huko, gharama na kila kitu tutalipiwa, na tukifika tunarejesha pesa ya watu, ….je umenielewa, na upo tayari?’ akaniuliza

‘Sawa nimekuelewa…ni..ni..potayari..’nikamwambia huku bado moyo ukiwa unasita. Na yeye akaniangaliwa kwa muda, bia kusema neno, baadaye akageuka na kuanza kupanga panga vitu vyake, na alipokuwa tayari, akatoka nje, na mimi nikabalia mle ndani nikiweka vitu vyangu sawa, vingine vilikuwa nje kweney gari nililokuja nalo.

 Waakti nipo pale ndani peke yangu, mara simu yake ikaita,..ilikuwa ndani ya mkoba wake wa mkononi, mkoba wa bei mbaya, nikawa nauangalia kwa mshangao, …naikaushika, ulionekana mnzito kidogo, na baadaye moyo ukanituma niufungue ili niichukue hiyo simu nimpelekee huko nje,…nikaivuta zipu, ukafunguka, ilikuwa zipu kama ya dhahabu,  na wakati nahangaika, mara nikashika kitu kigumu kikiwa ndani ya huo mkoba…..

Binadamu tulivyo, ukihisi kitu tofauti unakuwa na hamasa ya kutaka kujua ni kitu gani. Sina tabia ya upekuzi, lakini pale moyo wangu ukanituma niangalia ni kitu gani hicho. Nikajikuta nikikigusa tena na hata baadaye nikaamua kukitoa ili nikione ni kitu gani. Ulionekana mnzito, ...!

Nikawa nahangaika kuutoa ule mfuko ili niangalia vyema ni kitu gani,   na kabla sijautoa ule mfuko wote hadi juu, nikajikuta nikiuachia kwa haraka, kama vile mtu aliyeshika kaa la moto, …moyo wangu ukaenda mbio,….sijui kwanini. Sikutegemea kuwa huyu mwanadada anaweza kuwa na kitu kama hiki, nikaogopa….nikajikuta nikitetemeka mwilii mzima kwa uwoga…oh kwanini niogope, nikajiuliza na kujipa moyo!

‘Vipi nimesikia simu yangu ikiita,….’Sauti toka mlangoni, ilinipa mshituko wa ajabu , karibu nidondoke, nikauachia ule mfuko kwa haraka na kujivunga natafuta wapi mlio wa simu hiyo unapotokea, sikugeuka nyuma kumwangalia huyo mwanadada.Maana ningeligeuka angelinugundua jinsi gani nilivyobadilika kwa haraka!

‘Samahani nichukulie huo mkoba wangu simu ipo hapo ndani ya huo mkoba hapo…’akasema huyo mwanadada na mimi nikauinua ule mkoba kwa haraka,huku nikifikiria jinsi gani ya kuufunga, maana ulikuwa wazi baada ya mimi kuufungua kwa kiherehere changu …..’ Nikakishika kile kidude cha zipu, na kukivuta haraka, huku nikigeuka, na mara nikakutana naye….

‘Oh, usifungue mkoba wangu bwana…, huu una mambo yangu yote humu ndani…’akasema na kuchukua ule mkoba, nafikiri kwa vile mawazo yake yalikuwa kwenye kuichukua hiyo simu hakujali alipoona ule mkoba upo wazi, akaitoa ile simu na huku akiongea na simu, akakwa akiniangalia kwa macho ya mashaka.
Mimi nilijifanya simuoni…

‘Ndio kila kitu kipo tayari, …mambo yamekubali, wewe weka mipango yote sawa, nakutegemea wewe, usiniangushe,….’akawa anaongea kwenye simu huku akiufunga ule mkoba wake vizuri, na alipomaliza kuongea na simu akanigeukia na kuniangalia kwa yale macho ya mashaka, hakusema kitu, nahisi aligundua kuwa huenda nimeangalia mle ndani mkoba wake.

Safari maalumu ambayo mimi niliita safari ya fumanizi ikaanza , lakini moyoni sikuwa na amani kabisa,nilitamanii nisiende, kuna kitu kilikuwa kikinikataza ,  na mara nyingi ni kihisi jambo kama hilo, huwa kuna jambo baya litatokea, lakini ….

‘Kila kitu kipo tayari, hoteli na sehemu ya kufikia imeshaandaliwa, na kuna mtu keshalipia kila kitu,sisi tukifika tunapewa bili na kumrejeshea huyo jamaa yangu pesa yake aliyotulipia, hii ina maana hakuna tena mjadala, iliyobakia ni safari, natumai tumeshakubaliana na hilo,….’akasema huku akiweka mizigo yake vyema.

Nilibakia kimiya nikijiuliza niende au nisiende…na simu yangu ikaita, na aliyeita alikuwa ni mume wangu , nikaizima , sikutaka kuongea naye kwa muda huo nilijua angelinigundua kuwa sipo sawa.

‘Niende au nisiende….’nikajiuliza.

NB: Haya ni nini kitatokea , ni safari ya fumanizi, hatujui ni nini kitatokea.

WAZO LA LEO:Tupendane na kusaidina kwenye mambo mema,na tuonyane na kukutazana kwenye mambo mabaya, ili tuwe na jamii yenye upendo na amani.


Ni mimi: emu-three

5 comments :

Anonymous said...

What i do not understood is in fact how you're not actually much more well-preferred than you might be right now. You're so intelligent.

You already know therefore considerably in relation to this topic,
made me for my part consider it from so many
various angles. Its like women and men aren't fascinated until it's one thing
to do with Woman gaga! Your individual stuffs outstanding.
All the time handle it up!
My webpage: organic essential oils

Ammy K said...

safari ya hivyo inataka moyo, poleni sana wanandoa ambao ndoa zenu zinamashaka. ila kikubwa ni kuaminiana na kutimiziana kwa kila hali. ili kuepushiana vishawishi.

Anonymous said...

``poleni sana wanandoa ambao ndoa zenu zinamashaka''
Ammy wewe hujaolewa nini, maana mm nionavyo kila ndoa ina mashaka, ila watu ni kuvumiliana tu.
Mama Kadogo

Anonymous said...

Ubarikiwe sana kipaji chako kizidi kukua!

Anonymous said...

Hi to every body, it's my first pay a visit of this weblog;
this website consists of remarkable and genuinely good information in favor of visitors.


Feel free to surf to my blog post: online backgammon