Sijawahi kufika Dodoma, ilikuwa ni mara yangu ya kwanza, na
ingawaje nilikuwa na mzigo wa kuuza, lakini hilo halikuwa akilini kwangu kabisa,
kwani kichwani kulijaa mawazo , chuki , hasira na wivu. Vitu hivyo vilinifanya
nishikwe na jaziba, ambayo sijawahi kuwa nayo kabla, na kila dakika iliyokuwa ikipita kwangu ilikuwa
kama mtu anayepigilia msumari wa moto kwenye akili yangu, na hasa pale
nilipokuwa nikiikumbuka ile video nilyoiona kwa yule mwanadada.
Niliangalia huku na kule kama ninaweza kumuona mume wangu,
lakini hakukuwa na dalili yoyote, nikageuka kumwangalia mwenzangu ambaye
alikuwa haonyeshi dalili yoyote ya wasiwasi, yeye alishaanza kuongea na wateja
wake. Baadaye akanijia na kunishika bega, akasema;
‘Haya maswala hayataki hasira, na lolote utakaloliona huko
liwe akili kichwani mwako, maana ukitumia nguvu, ukaweka hasira yako mbele,
utakosa kila kitu, hii iwe sehemu ya uchunguzi tu,…kumbuka maelekezo yangu,
huku tumekuja kwa ajili ya biashara na si vinginevyo….haya twende makaoni,….’akaniambia
yule mwanadada, na tukachukua taksii hadi huko makaoni.
‘Lakini mimi bado siamini, maana nimemuliza mume wangu
kakataa kata kata, na hata kuniapia kuwa yeye hawezi kufanya jambo kama hilo,
…’nikakumbuka nilivyomwambia, na huyu mwenzangu hakutaka kunijibu lolote.
Tukiwa kwenye gari simu yake ikaita, akachukua ule mkoba
wake, na hapo nikajikuta nikishikwa na wasiwasi, …ule mkoba, nikakumbuka kile kitu...nikageuka haraka kuangalia nje, na
kuyaondoa hayo mawazo haraka kichwani, sikutaka kuwazia mabaya zaidi.
Nilichofanya ni kuanza kuwaza maisha yangu na mume wangu, ili kuondoa mawazo
hayo mengine kichwani. Kwa ujumla, sikutaka mawazo mengine yaniteke akili
yangu, na ili nifanikiwe hilo nikajikuta nikiwaza siku ile mume wangu
aliporejea toka Dodoma .
Siku ile nilikuwa sina raha , nilikuwa nimeshaanza
kuathiriwa na mawazo, hasa baada ya kupata hizi taarifa kuwa mume wangu naye ni
miongoni mwa hawo wenye nyumna ndogo, …nilijitahidi sana kutokumuonyesha hasira
nilizo kuwa nazo, kwani bado nilikuwa sijaamini. Lakini nahisi aligundua mabadiliko fulani.
*****
‘Mke wangu mpenzi vipi mambo ya hapa, nimekumisi sana, kila
siku huko kwenye kikao nilikuwa nikikuwaza wewe, nilitamani nikatishe kikao
nije nikuone…’akaniambi huku akinikumbatia, na mimi nilikuwa kama mti, mwili mzima ulikuwa wa baridi, na kitendo kile
kilifanya fundo nilililokuwa nalo moyoni litake kupasuka, nikajitahidi
kujifanya na mimi nipo naye, nikasema kinafiki;
‘Hata mimi mume wangu, na nashangaa siku mbili hizi nimekuwa
nikiota kuwa naibiwa, maana nasikia huko Dodoma kuna wanawake warembo, ambao kazi
yao kubwa kuwaburudisha wanasiasa wanaokwenda huko, wakijua kuwa mna pesa
nyingi za kutumia…’nikamwambia.
‘Hayo ni yao, na kama wapo watu wa namna hiyo, wanafanya
hivyo kwa tamaa zao. Siwezi kukukatalia kwasababu watu tunatofautiana, na mambo
kama hayo yapo, lakini kila mmoja ana akili zake, kama una mke unayempenda kama
mimi ninavyo kupenda wewe kwanini nijiingize kwenye tamaa hizo’akaniambia huku
akijaribu kuyakwepamacho yangu.
‘Ni kweli ni tamaa, na tamaa za wanaume hazina mpaka…na
uwongo wenu hauna dini, maana unaweza hata kuapa, wakati ni kweli umefanya
hivyo,…’nikaanza kumwambia, na yeye akageukia dirishani na kusema;
‘Mimi, nifanye mambo hayo…hapana, nani wa kukuzidi wewe,
hilo usidanganyike,na kama kuna mtu kakudanganya hivyo ujue ana lake
jambo’akasema.
‘Mumu wangu nakupenda sana, na sitavumilia kama nitagundua
kuwa una mtu mwingine, na ukumbuke tulipotoka, ukumbuke uliponichukulia, wengi
walinitaka na wewe pekee ndiwe uliyefanikiwa kunichukua, sasa isje ikafika
mahali nikajuta na kusema aheri ningekwenda kwa yule mwingine…’nikamwambia na
niliona akibadilika sura, akasema;
‘Lakini hayo yote yametoka wapi mpenzi wangu, ni nani
mlikutana naye akaanza kukudanganya, ndio maana nakukunya usikae na marafiki,
wengi wa marafiki ni waongo, na wanaweza wakatunga uwongo wenye sawa na ukweli,
ukaamini, na kumbe hakuna kitu….chunga sana mashoga, hawo watu sio wema, na
hawapendi wenzao wakiishi kwa upendo na amani’akaniambia huku akijbaragua kwa
kushika hiki na kile.
‘Mume wangu, dunia sasa hivi haina siri, mambo ya mitandao ,
mambo ya kisasa, yanaweza yakaonyesha kila kitu, zamani wazee wetu walitumia
ramli wakajua ya ghaibu,lakini siku hizi
kuna mitandao, inaweza ikaonyesha kila kitu…upo chumbani kumbe wenzako wameweka
mitambo inaonyesha siri zako,…’nikasema na yeye akaniangalia kwa mashaka.
‘Mke wangu vipi, mbona unanitisha, mbona unakuja na hoja za
kunipa wasiwasi, kuna nini kimetokea hadi ufike kuongea hayo, unataka kusema
nini…..?’akaniuliza akiwa na wasiwasi.
‘Natumai umenielewa, nililotaka kusema ni hilo, kuwa uwongo
una mwisho wake, na mbio za sakafuni maranyingi huishia ukingoni, ukumbuke
tulipotoka, ukumbuke magonjwa, ukumbuke mungu wako, kuwa lolote utakalolifanya
kwa siri, mungu analiona na ipo siku ukweli utadhihiri na kuishia
kuumbuka’nikasema na yeye akatulia kimia.
‘Mume wangu kumbuka alivyosema dakitari kuwa mimi nina
dalili za shinikizo la damu, la kushuka, na nijitahidi sana kutokupata
mishituko au mashinikizo ya mawazo.Na hilo nimejitahidi sana, na mtu wakuweza
kunisadia zaidi ni wewe…nakuomba tafadhali usije ukaniua….’nikasema na yeye
akashika shavu, kuonyesha kuumia kwa namna fulani…
‘Mke wangu ina maana huniamini…?’ akaniuliza
‘Nakuamini ndio maana nakuambia hayo,….’nikasema na baadaye
mazungumzo yalikatishwa na wageni, maana hayo mambo yao ya siasa hayampi mtu
muda wa kuongea na mwenzake, simu, wageni, ilikuwa ni kero.
*******
‘Halloh, mwanadada,ni mimi mke wa kiongozi, nilitaka kukuambia
kuwa mume wangu kaondoka leo asubuhi, kwenye mambo yao ya kisiasa, sasa nimekaa
nakuwaza sana, nikaona ili nisiumie na mawazo, ni bora nijirizishe,…’nikasema
kwenye simu.
‘Hata mimi nina safari ya huko, na umefanya jambo la maana
sana, maana huko kuna biashara msimu huu, nguo zako na vipodozi vinahitajika
sana. Unajua hawa wakubwa, wakifika huko wanahitaji zawadi kwa washikaji zao,
sasa hapo ndipo soko linapozaa matunda, nitakupigia simu nikuelekeze vitu gani
vya kubeba..’akasema huku akikwepa kuongea lolote kuhusu madhumuni ya hiyo
safari.
Baadaya alinipigia simu na kunielekeza nini chakubeba, aina
gani za nguo, vipodozi na bidhaa zingine ambazo alisema zinahitajika sana
huko.Na hata nilipotaka kuongea madhumini ya hiyo safari, yeye alikwepa na
kuongelea maswala ya biashara tu.
Nilipokutana naye aliniambia kwanini hakupenda kuongea
lolote kuhusu madhumuni ya hiyo safari,kwenye simu akaniambia;
‘Kumbuka haya mambo yanahitaji usiri mkubwa, simu siku hizi
zinasikilizwa, na kumbukumbu za mazungumzo zinanaswa na kuhifadhiwa,…unatakiwa
uwe makini. Na sijui mumeo anajua nini kuhusu hii safari, natumai hujamwambia
lolote kuwa utasafiri kwenda huko kwenye vikao vyao….’akasema.
‘Mimi nilimwambia nitasafiri kwenda Morogoro kupeleka mizigo,
na kama inawezekana naweza kusogea mbele kidogo, lakini sikumwambia mbele wapi,
kama ulivyonielekeza siku ile.
‘Mizigo yenyewe ndio hii tu,….mbona?’ akaniuliza .
‘Ipo nje kwenye gari,
hii nimekuja kukuonyesha kuwa kama na yenyewe inafaa twende nayo, au kama
haifaii nitaiacha hapo kwako’nikasema.
‘Inafaa….twende nayo tu, biashara nyingine unajaribu, huwezi
jua’akasema huku akiingalia vile vitu nilivyokuja navyo
‘Safi kabisa…vinafaa,…unajua, ni bora sana kuchukua
tahadhari, maana safari ni hatua lolote linaweza kutokea, na utashindwa jinsi
gani ya kujitetea likitokea jambo la hatari, hatuombei mbaya, lakini yote
hutokea, au sio...'akaniuliza na kabla sijajubu lolote akasema;
Hapo, umefanya vyema kuwambia kuwa huenda tukasogea mbele kidogo.Sasa angalizo, nii kuwa hatutakiwi kuongea lolote kuhusu
hayo yanayotupeleka huko, tukitoka humu ndani, mazungumzo yetu, tukitoka humu
ndani yatakuwa kuhusu biashara, hadi tutakapofika huko, na hata tukifika huko
mazunguzo yetu ni hayo hayo….sisi ni wafanya biashara, hiyo ndiyo nembo yetu…unielewe
kwa makini’akaniambia.
‘Lakini mimi bado nina wasiwasi….’nikamwambia.
‘Wasiwasi wa nini…usiwe muoga, uwoga hujenga magonjwa kama
shinikizo la damu ….uwe jasiri, hasa unapokuwa katika maisha ya ndoa, ukiogopa
wenzako watachukua huo udhaifu wako na kufanya mambo yao. Sikiliza, hayo
unayokwenda kuyafanya ni kwa ajili ya misha yako ya baadaye, …’akaniambia.
‘Lakini nakuapia, kama unanitega kwa lolote sitakusamehe
hadi kufa,, na sijui nitakufanya nini’nikasema kwa hasira.
‘Hilo utajionea mwenyewe , wewe tukifika huko, utaniambia…..Na
sikiliza, mimi nataka unitambue kama
dada yako, na ukikwama kwa lolote, niambie, nitakusadia, na hili nataka
ulichukuliea kama sehemu ya malipo yangu kwako, maana ulikubali kuniachia huyu
mtu,licha ya kuwa sasa najuta ,lakini yote ni majaliwa.
‘Sawa haya twende , maana kwa sasa sina jinsi,
…’nikamwambia.
‘Wewe utakuja kuniambia, …ila nakukanya tena, tunaondoka
hapa kama wafanyabiashara, na tukifika huko kazi yetu kubwa ni kutafuta wateja,
mimi nawafahamu, kunasehemu tunaweka mizigo yetu , ni sehemu tumekodi, mimi
mwenyewe nina duka alngu kubwa tu…’akaniambia.
‘Mwenzangu upo mbali kweli..’nikamwambia nikijaribu kuondoa
mawazo.
‘Ni kuhangaika, na kinachohitajika ni ujasiri, ..ukithubutu,
utaweza, lakini ukiweka unyinge na kusema sitaweza, na kweli hutaweza. Mimi
nimejifunza mengi ndani ya ndoa, na nilishajifunza mengi kabla ya ndoa, kwahiyo
maisha nayajua vyema…’akaniambia.
‘Hongera’nikasema.
‘Hongera haisadiii, kinachotakiwa na wewe ujifunze, kwani
kuna leo nakesho, angalai wajane wengi wanavyoteseka, kwasababu walijipweteka,
wakijua kuwa kila kitu kitatoka kwa mume, sasa mume huyo hayupo, huenda
kafariki au ameachika, anashindwa maisha, …hilo tunatakiwa tuwe makini
nalo’akaniambia.
‘Lakini….
‘Lakini nini tena, sikiliza, kama bado moyo wangu
hujajipanga kwenye hii safari , tafadhali rudi nyumbani kajipange vyema, …mimi
sitaki mtu anayedeka, nataka mtu ngangari, ukifika kule uwe na ujasiri, uwe
makini kwa kila tendo, ujue hutakiwi kujulikana, na kwahiyo uvaaji wako wa huku utakuwa tfauti
na wakule, kuna wanawake kule wanajua jinsi gani ya kukuvalisha na kukuweka
mwili wako uwe kivingine, hayo ni ya huko…’akasema.
‘Una maana gani kusema hivyo.?’nikasema kwa wasiwasi.
‘Wewe ,mwanamke wewe, upo dunia ipi, …kumbuka huko
tunakwenda kama wafanay biashara, na wateja wetu sio wazee,.hata kama kuna
wazee, kule wote wanakuwa ni vijana, sasa watavutika vipi na biashara zako kama
na wewe huan mvuto. Biashara ni pamoja na mtangano yenye mvuto’akasema.
‘Mbona unanitisha…’nikasema na kutaka kuondoka.
‘Hahaha…tatizo lako umefikiria vingine, …nikuambie ukweli,
hakuna kitu kinachouza bidhaa kama matangazo, vitu vya mvuto. Mfano ukiweka
muuzaji mrembo kwenye duka lako, wateja wengi watafika hasa vijana, hasa
matajiri na watu wote hupenda urembo, asikudanganye mtu, na….ndivyo ilivyo,
sasa ukumbuke wewe unakwenda kuuza bidhaa zako, ni lazima uwe katika hali ya
kumvuta mteja…uvaaji wako, taswira, tabasamu..ni siri ya biashara…tukifika huko
hutakiwi uvae kama ulivyovaa hapa…’akaniambia
‘Na pia nataka ujue kuwa tukishakubaliana hapa hakuna
marejeo, maana mipango inapangwa huko, gharama na kila kitu tutalipiwa, na
tukifika tunarejesha pesa ya watu, ….je umenielewa, na upo tayari?’ akaniuliza
‘Sawa nimekuelewa…ni..ni..potayari..’nikamwambia huku bado
moyo ukiwa unasita. Na yeye akaniangaliwa kwa muda, bia kusema neno, baadaye
akageuka na kuanza kupanga panga vitu vyake, na alipokuwa tayari, akatoka nje,
na mimi nikabalia mle ndani nikiweka vitu vyangu sawa, vingine vilikuwa nje
kweney gari nililokuja nalo.
Waakti nipo pale
ndani peke yangu, mara simu yake ikaita,..ilikuwa ndani ya mkoba wake wa
mkononi, mkoba wa bei mbaya, nikawa nauangalia kwa mshangao, …naikaushika,
ulionekana mnzito kidogo, na baadaye moyo ukanituma niufungue ili niichukue
hiyo simu nimpelekee huko nje,…nikaivuta zipu, ukafunguka, ilikuwa zipu kama ya
dhahabu, na wakati nahangaika, mara
nikashika kitu kigumu kikiwa ndani ya huo mkoba…..
Binadamu tulivyo, ukihisi kitu tofauti unakuwa na hamasa ya
kutaka kujua ni kitu gani. Sina tabia ya upekuzi, lakini pale moyo wangu
ukanituma niangalia ni kitu gani hicho. Nikajikuta nikikigusa tena na hata
baadaye nikaamua kukitoa ili nikione ni kitu gani. Ulionekana mnzito, ...!
Nikawa nahangaika kuutoa ule mfuko ili niangalia vyema ni
kitu gani, na kabla sijautoa ule mfuko wote hadi juu, nikajikuta
nikiuachia kwa haraka, kama vile mtu aliyeshika kaa la moto, …moyo wangu ukaenda
mbio,….sijui kwanini. Sikutegemea kuwa huyu mwanadada anaweza kuwa na kitu kama
hiki, nikaogopa….nikajikuta nikitetemeka mwilii mzima kwa uwoga…oh kwanini
niogope, nikajiuliza na kujipa moyo!
‘Vipi nimesikia simu yangu ikiita,….’Sauti toka mlangoni,
ilinipa mshituko wa ajabu , karibu nidondoke, nikauachia ule mfuko kwa haraka
na kujivunga natafuta wapi mlio wa simu hiyo unapotokea, sikugeuka nyuma kumwangalia
huyo mwanadada.Maana ningeligeuka angelinugundua jinsi gani nilivyobadilika kwa
haraka!
‘Samahani nichukulie huo mkoba wangu simu ipo hapo ndani ya huo
mkoba hapo…’akasema huyo mwanadada na mimi nikauinua ule mkoba kwa haraka,huku
nikifikiria jinsi gani ya kuufunga, maana ulikuwa wazi baada ya mimi kuufungua
kwa kiherehere changu …..’ Nikakishika kile kidude cha zipu, na kukivuta
haraka, huku nikigeuka, na mara nikakutana naye….
‘Oh, usifungue mkoba wangu bwana…, huu una mambo yangu yote
humu ndani…’akasema na kuchukua ule mkoba, nafikiri kwa vile mawazo yake
yalikuwa kwenye kuichukua hiyo simu hakujali alipoona ule mkoba upo wazi,
akaitoa ile simu na huku akiongea na simu, akakwa akiniangalia kwa macho ya
mashaka.
Mimi nilijifanya simuoni…
‘Ndio kila kitu kipo tayari, …mambo yamekubali, wewe weka
mipango yote sawa, nakutegemea wewe, usiniangushe,….’akawa anaongea kwenye simu
huku akiufunga ule mkoba wake vizuri, na alipomaliza kuongea na simu
akanigeukia na kuniangalia kwa yale macho ya mashaka, hakusema kitu, nahisi
aligundua kuwa huenda nimeangalia mle ndani mkoba wake.
Safari maalumu ambayo mimi niliita safari ya fumanizi ikaanza
, lakini moyoni sikuwa na amani kabisa,nilitamanii nisiende, kuna kitu kilikuwa
kikinikataza , na mara nyingi ni kihisi
jambo kama hilo, huwa kuna jambo baya litatokea, lakini ….
‘Kila kitu kipo tayari, hoteli na sehemu ya kufikia
imeshaandaliwa, na kuna mtu keshalipia kila kitu,sisi tukifika tunapewa bili na
kumrejeshea huyo jamaa yangu pesa yake aliyotulipia, hii ina maana hakuna tena
mjadala, iliyobakia ni safari, natumai tumeshakubaliana na hilo,….’akasema huku
akiweka mizigo yake vyema.
Nilibakia kimiya nikijiuliza niende au nisiende…na simu
yangu ikaita, na aliyeita alikuwa ni mume wangu , nikaizima , sikutaka kuongea
naye kwa muda huo nilijua angelinigundua kuwa sipo sawa.
‘Niende au nisiende….’nikajiuliza.
NB: Haya ni nini kitatokea , ni safari ya fumanizi, hatujui
ni nini kitatokea.
WAZO LA LEO:Tupendane
na kusaidina kwenye mambo mema,na tuonyane na kukutazana kwenye mambo mabaya,
ili tuwe na jamii yenye upendo na amani.
Ni mimi:
emu-three
5 comments :
What i do not understood is in fact how you're not actually much more well-preferred than you might be right now. You're so intelligent.
You already know therefore considerably in relation to this topic,
made me for my part consider it from so many
various angles. Its like women and men aren't fascinated until it's one thing
to do with Woman gaga! Your individual stuffs outstanding.
All the time handle it up!
My webpage: organic essential oils
safari ya hivyo inataka moyo, poleni sana wanandoa ambao ndoa zenu zinamashaka. ila kikubwa ni kuaminiana na kutimiziana kwa kila hali. ili kuepushiana vishawishi.
``poleni sana wanandoa ambao ndoa zenu zinamashaka''
Ammy wewe hujaolewa nini, maana mm nionavyo kila ndoa ina mashaka, ila watu ni kuvumiliana tu.
Mama Kadogo
Ubarikiwe sana kipaji chako kizidi kukua!
Hi to every body, it's my first pay a visit of this weblog;
this website consists of remarkable and genuinely good information in favor of visitors.
Feel free to surf to my blog post: online backgammon
Post a Comment