Mchana ulikuwa wa
pilika pilika, kukutana na wateja, na kugongana katiba bei mpaka unafiki
mahali unauza kitu chako,sikuamini , maana bidhaa nyingi zilinunuliwa kwa baei
kubwa ambayo sikuwahi kuuza kabla, nikagundua kuwa kumbe wenzangu hawa
wanaochukau bidhaa zangu na kuja kuuza huku walikuwa wakipata faida kubwa sana.
‘Unaona ,hiindio biashara, ndio maana hawa wanzetu wakiwa na
kikao huku, tunafanya kile tuwezalo tuje huku, …’akasema mwanadada.
‘Kweli nimeamini, kumbe ndio maaana mpo juu kibiashara,
…mumenifungua macho, safari nyingine sibakia nyuma’nikasema.
‘Muda bado wa kuchuma, pesa, ngoja jamaa watoke kwenye
mikutano yao, ….hawa waliokuja ni wachache tu, ambao wengi walikuja kusikiliza
, wapo ambao wanalipwa marupurupou ya hali ya juuu, wapo bado kwenye kikao,
..’akasema.
‘Ina maana kuna wengine watakuja?’ nikauliza.
‘Kwani umewaona wenyewe
hapa,…saa zao bado, wakaitoka kwenye vikao vyao utawaona, ..’akasema na yeye akaondoka na kuniacha
nikiendelea na kuuza bidhaa zangu…na kila muda nilipokuwa sina mteja, nikawa
namuwaza mume wangu kwani nilikuwa sijajua wapi alipo, na niliogopa kumuuliza
mwenzangu, kutokana na masharti niliyopewa,kuwa tusiongee lolote kuhusiana na
hilo lililonileta hapo.
****
‘Mke wangu kama ulivyosikia , leo ndio kikao maalumu cha
kusikiliza maombi yetu,kwani wamemuweka mtu mwingine kinyume na makubaliano ya
mwanzo,na kwa ajili hiyo tumeweka pingamizi, kwahiyo leo ndio siku ya
kusililizwa hilo pingamizi,…’akanimambia ,mume wangu.
‘Sawa mimi ninakusikiliza wewe, maana najua nini kitafuata
baada ya hayo maelezo yako hayo, lakini ukumbuke kuwa sasa hivi hata biashara
zetu hali ni ngumu sana, hapa nilipo nawaza jinsi gani ya kujikwamua…’nikamwambia
mume wangu.
‘Lakini mke wangu haya si kwa ajili ya maisha yetu ya
baadaye, kwani nafanya haya kwa ajili ya nani kwa sio kwa ajili ya familia…hebu
niambie?’ akaniuliza.
‘Najua hilo, lakini
unaweza ukatumia nguvu nyingi pasipo na sababu, na hapo ukapata vsingizio vya
kufanya mengine yasiyokubalika, lakini mimi sitaki kusema mengi. Ninachoweza
kusema nikukutakia safari njema na mafaniko mema, na ukifika huko usisahau kunisalimia
wote hasa wale wanakutuliza mawazo baada ya kikao..’nikasema na yeye akacheka
akijua kuwa nafanya utani, akaniangalia mara moja na alipoona namtizama
akaangalia pembeni.
‘Hakuna anayeweza kunituliza mawazo zaidi yako mke wangu, ni
kwa vile ni mbali, ilitakiwa tuwe pamoja, au safari twende pamoja?’ akauliza.
‘Kama ulikuwa na lengo hilo ungeliniambia toka mapema, il
niweke mambo yangu vyema,. ..nahisi kuniambia muda kama huu ,na kesho ni safari
ni kunitega….,’nikasema.
‘Sio kukutega mke wangu, najua kuwa kuna mambo yetu ya
biashara ambayo usipokuwepo wewe hayatawezekana, na kama ulivyoniambia jana
kuwa kuna mizigo mingine unapeleka Morogoro, sio mbaya, lakini mimi sipendi
biashara hizi za safari ndefu, …siwi na amani kabisa’akaniambia.
‘Hakuna anayependa mambo kama haya ya kwenda masafa, hata
mimi mwenyewe sipendi safari zako hizo za kila siku kwenda huko kwenye vikao,
lakini hakuna jinsi,..cha muhimu ni kujua wewe ni nani…’nikamwambia.
‘Sawa mke wangu, mimi nakuelewa, ila nilikuwa nauliza ,
ulisema kuwa ukitoka huko Morogoro utangaalia kuwa unaweza kwenda mbeel kidogo,
mbele kidogo wapi, …?’ akaniuliza.
‘Huo mzigo ukiisha, nitarudi huku Dar, ili nichukue
mwingine, lakini kama hautaisha hapo Morogoro, ninaweza kusogea mbele zaidi,
kuwafuta wateja huko walipo,….siku hizi unatakiwa kuwafuata wateja walipo…’nikamwambia,
na kabla hatujaongea zaidi simu yake ikaita, na kama ilivyo kawaida akatoka
nje, na mimi nikapata mwanya wa kumuandalia safari yake, huku nikiwaza mazungumzo yangu ya
mwisho na mwanadada.
********
‘Siku ile baada ya harusi mume wangu alikuwa mtu wa kulewa,
na akirudi nyumbani hujibwaga kitandani, hakuwa na muda na mimi. Nikijaraibu
kumuuliza yeye alidai kuwa hanitambui kama mke wake, kwahiyo niondoke hapo
nyumbani kwake, lakini sikukubali, sikukata tamaa, nikujua mtaka cha mvuguni
sharti ainame. Na jambo jingine lililonitia hamasa ni kuwa wazazi na ndugu zake
walikuwa upande wangu…’akasema mke wa hasimu wa mume wangu.
‘Sisi tupo na wewe hatupendi ndugu yetu amuoe huyu mwanamke
wake aliyemtaka bila ya kutuhusisha sisi, mke ambaye kila mtu anamtaka ni wewe,….wewe
ulitambuslishwa kwetu, na sisi tukakukubali, sasa huyo mwingine katoka wapi,
mke mwenyewe tunasikia ni mshamba wa huko kijijini, sis huyo hatufai,….’alisema
mmoja wandugu za mume wangu.
‘Sisi siku zote tunajua kuwa wewe ndiye mchumba wa kaka
yetu, tulishangaa siku ile alipokuja na kusema anataka kumuoa huyo mshamba,…eti
anadai kuwa huyo ndiye alimpenda na kuna mtu anataka kumuonyesha kuwa yeye ni
zaidi yake’akasema ndugu mwingine. Na hapo nikawa na amani kuwa sipo peke
yangu.
‘Ina maana kutaka kukuoa wewe, ni kutaka kuonyesha kuwa yeye
ni zaidi ya mume wako, sio kwasababu ya mapenzi, maana mimi na yeye tulianza
mapenzi yetu toka zamani, na hadi kufikia kuvalishana pete, na wakati huo
alikuwa akikufahamu, jiulize kwanini hakukuvalisha pete wewe…’akasema.
‘Nikuambai ukweli siku saba za mwanzo zilikuwa za mateso
kwangu, maana huyu jamaa alikuwa akinywa pombe kupita kiasi, na siku nyingine alikuwa
akirudishwa nyumbani akiwa hajiwezi, ikawa kazi yangu kumvua nguo, hata kumuogesha, kwani wakati mwingine
alikuwa kajichafua…kabisa. Yote hayo ilibidi nikubaliane nayo maana naweza
kusema nimejitakia mwenyewe.
Siku ya nane ya mateso, kuzalilika zarau na hata kubigwa
mangumi na mateke, ilileta matokeo yake, siku hiyo mume wangu alirudishwa akiwa
hajiwezi anavuja damu, kaumizwa sana,nilishangaa rafiki zake badala ya
kumpeleka hospitali walimleta nyumbani wakidai kuwa kakataa kupelekwa
hospitalini,eti ana dakitar, ..hapo nikaanza kuogopa,nikai wake, na hata
tulipowauliza imekuwaje, wao hawakutaka kuweka wazi sana, walisema;
‘Mambo ya walevi haya, kapigwa na mwenye mke, kaingilia anga
zisizoingiliwa…’akasema mmojawapo
‘Mwenye mke…?, ina
maana kafumaniwa?’ nikauliza.
‘Ndio maana yake,…. lakini tumeyamaliza,…ni ajali kazini’akasema
huyu rafiki yake naye akionekana bado kalewa. Iliniuma sana, licha ya kuwa
nilijua mambo kama hayo kwa huyu mume wangu yanawezekana kuwepo, lakini baadaye
sikujali nikasema tutabanana hapo hapo, mpaka kieleweke.
Kesho yake asubuhi, wakati namuuguza yale majeraha, baada ya
dakitari kuondoka, tofauti na siku nyingine, alikuwa mpole sana, na aliweza kutulia
nyumbani siku hiyo,labda ni kutokana na yake mjereha, aliona aibu kukutana na
watu akiwa hivyo. Na lipofika mchana nikamuandalia chakula, nikiwa najua kama
kawaida yake,atakipiga teke hicho chakula na kunivurumishia matusi na mateke,
lakini haikuwa hivyo, alikula na baadaye akatulia, na mimi nilipoona hivyi nikaja
na kukaa karibu yake huku najihami.
‘Mke wangu najua nimekukwaza sana….nisamahe ka yote,
ingawaje umejitakia wewe mwenyewe haya yote…’akasema na kwa mara ya kwanza
akatamka hilo neno mke wangu, sikuamini nikageuka kumwangalia huku usoni nikiwa
nimejawa na tabasamu la kutokuamini, na baadaye machzo yakanitoka, sijui ni
kwasababu ya furaha au ni kitu gani.
‘Unasemaje mume wangu, ..?’ nikauliza nikitamani arudie lile
neno ‘mke wangu ‘kwa mara nyingine.
‘Nimefikiria sana, na baadaye nimeona sina jinsi, kwani yule
mwanamke nasikia keshaolewa na yule mshamba mwenzake, hata hivyo, nitahakikisha
nayasambaratisha maisha yao, nitahakikisha hapati raha, na ikiwezekana nitamzalilisha
kila hatua,hadi aje kunipigia magoti…atajua kuwa mimi ni nani’akasema kwa
hasira huku akigonga meza.
Mimi nilimuitikia kama mume wangu, lakini sikutaka hayo
anayoyataka kuyafanya, kwani ukizingatia kuwa hayo yaliyotokea ni kwa manufaa
yangu. Nilichofanya mimi ni kuuma na kupulizia, nikiwa na maana kuwa,
tunayapanga pamoja, lakini tukitoka hapo natafuta njia nyingine ya kuyazuia
kinamna,…
‘Kuna siku kabisa ilipangwa mbinu ambayo mume wako
angalipata ajali, …lakini mimii nikafanya mbinu, na mipango hiyo haukufanikiwa,
na sasa najua kabisa huko Dodoma kuna mipango mingi imepangwa, ambayo mimi
sijaijua vyema, kwani nahisi walinigundua kuwa huenda mimi natoa siri zao ndio
maana walikuwa hawanihusishi tena kwenye mipango yao.
‘Mimi hizi safari za kwenda Dodoma, zikuzipanga hivi hivi
tu, kuwa labda nakuja kumfumania, hapana hayo nilishayapa mgongo, afanya
atakalo, …lakini kuna kitu kinaniuma, na kinanifanay nijione kuwa nahusika, na
huenda isingelikuwa mimi hayo yasingelikuwepo, na ndio maana nimekuwa
nikijitolea kw ahali na mali kuhakikisha natimiza wajibu wangu.
Moja ya lengo langu la kwenda mara kwa mra huko Dodoma, ni
kuwa mlinzi wa mumeo, hutaamini hayo, lakini najitahidi pale ninapoweza, na
nina watu wangu wanaifanay hiyo kazi, sikustahili kukuambia hili,lakiini
imebidi, na nimeapa kuwa nitahakikisha kuwa hakuna mabaya yanayotokea kwa mume wako.Lakini
siku nilipogundua kuwa mume wako kajiingiza kwenye makundi haramu, makundi
ambayo hayana mambo mame,….sikuamini, ….
‘Ina maana kuwa ..’nikaishiwa hata la kuongea.
‘Ndio maana nataka tushirikiane kwa hilo, …lengo letu liwe
moja, ikibidi hawa watu waje kushikana mikono wakubali matokea, yaani mume
wangu na wa kwako waje wakubaliane na …’akasema.
‘Kwa jinsi nimjuavyo mume wangu sizani kama hilo
litafanikiwa’nikasema.
‘Hata mimi nalijua hilo, lakini tutafanyaje …unakumbuka
nilivyokuambia awali, kuwa vyovyote iwavyo, lakini sisi ni wanawake,
tunaunganishwa na uasili wetu, kuwa sisi ni walezi, sisi sio walezi wa watoto
wetu tu, lakini pia ni walezi wa familia, walezi wa waume zetu….’akasema
mwanadada huku nikimshangaa.
‘Najua utashangaa hilo, lakini ukiolewa ujue hilo ni jukumu
lako, jukumu la kuwalea wanaume zetu, tusilikwepe hili jukumu. Tukilikwepa
ndiyo hayo machafu yanapotokea. Najua kabisa tukiwa pamoja na tukawa na lengo
moja, tukajua majukumu yetu, tunaweza kuifanya dunia hii ikawa na amani, lakini
tukiwa kinyume chake, …dunia hii haitakuwa na amani abadani,…’akasema
‘Sijui, nsikuelewi, maana kusema ni sawa, lakini jinsi gani
ya kuwafanya hawa watu wakubaliane na sisi na kazi nyingine kubwa
sana…sijui…hata hivyo sijakubaliana na hayo yako, kuwa mume wangu kajiingiza
kwenye hayo machafu, …nimjuavyo mume wangu hilo haliwezekani. Labda…sijui
wamempa kitu gani..’nikasema nikionyesha kuchanganyikiwa.
‘Ndio maana nikakutaka tuongezane huko ukajionee mwenyewe…
Nilipowaza hayo nikasema lazima nifike huko Dodoma
nikajionee mwenyewe. Haya siku inakwisha, na jioni hiyo inaingia mbona
sijamuona huyo mume wangu, …Na wakati nawaza hilo, nikaona gari likipita na
kusimama mbele yetu, na walioshuka pale walikuwa watu wanne, wanaume wawili na
wanawake wawili, na mmojawapo alikuwa mume wangu, nikasogea pembeni ili
nimuangalia vyema nione wapi anapoelekea.
‘Ukimuona usichukue papara, nipigie simu kwanza,
nitakuonyesha nini cha kufanya..’nikakumbuka hayo maneno, lakini mimi sikusubiri
nikaanza kumfuatilia mume wangu huko anapokwenda…kwani hata hivyokila
nilipokuwa nikimpgia simu mwanadada,ilisema namba hiyo inatumika’
NB. Haya jamani tupo makaoni, tuone nini kitatokea....
WAZO LA LEO: Maneno mengi pekee hayajengi, matendo na
mipango thabiti inayotekelezeka ndiyo mafanikio ya jambo lolote.
Ni mimi:
emu-three
7 comments :
mmmhhh hapa simulizi tamu nasubiri kuona kitatokea!!!
mmmmhhhh kwa kweli yataka moyo mambo ya ndoa na mahusiano kwa ujumla
If sоme one deѕіres to be updated with most
uр-tο-date technolοgies thеn hе
must be paу a viѕit this web page
and bе up tο dаtе еvеryday.
My website : best memory foam mattress
Whаt's up, always i used to check webpage posts here early in the break of day, as i like to gain knowledge of more and more.
My site: same day loans
Hi, І dо think this is аn excellent blog.
І ѕtumbledupon іt ;) I am gοing
to revisit yet again since I bookmarκеd it.
Mοney and freedom іs the greatest way to change, may you be гіch and
continue to helρ οther ρeople.
Also visit my page - instant payday loans
bοokmarked!!, I reаlly liκe your sitе!
Also see my web page :: quick loans
Post a Comment