Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, June 26, 2012

Hujafa hujaumbika-58 hitimisho-16
 Mume wangu akabadilika kabisa, halali nyumbani,akija nyumbani anakuja kubadili nguo tu na kuondoka zake, na hataki umuulize wapi anakwenda na kama atakuja kulala nyumbani anakuwa kalewa, kiasi cha kutokujitambua,naishia kumfulia na kumhudumia, kiujumla akawa sio Yule mume niliyamjua tena.

‘Baya zaidi akaanza kuwaharibu mabinti niliokuja kuishia nao hapo nyumbani, na hata kumbaka mtoto ambaye tulimlea wenyewe kama mtoto wetu wa kufikia. Nilianza kumuogopa kuwa sasa sio binadmu wa kawaida. Nilijaribu kukaa ili aniambia tatizo lipo wapi, nikianzakumuulizahayoinakuwa ndioya sababu ya kuondoka hapo nyumbani, anakuwa kama anakuskiliza,..akisikia unaingia hoja hiyo anageuzakichwa pembeni halafu anainuka nakuondoka....akirudi hapo siyo yeye tena, ukimuuliza ni kupiga...na mimi skukbali kupigwa kirahisi tunapigana....

Nikamtafutia dakitari wa kumshauri , lakini hakutaka hata kuongea na yeye. Anasema yeye haumwi hahitaji dakitari.Ikafikia hatua nikakata tamaa kabisa, lakini siku nilipoongea na mama yangu kwa simu na kuniasa kuwa namtia aibu, kuwa mimi ni mke, na huyo ni mume wangu, nisikubali kushindwa. Hapo ndipo nillipojua kuwa kama mwanamke sitakiwi kukata tamaa, nilichohitajika kufanya ni kuangalia wapi nilipokosea. Na hapo ndipo wazo la kufanya jambo likanijia,….’akatulia na kumwangalia mume wake.

‘Jambo gani hilo, ….?’ Akaulizwa na hakimu.

‘Kwanza mimi ni msomi, na usomi wenyewe ni wa udakitari, itakuwa ni aibu kuwa nakosana mume wangu kwasababu zinazohusu mwili, na maumbile ya kibinadam, mimi ndiye nilitakiwa kuwasaidia wale walioshindwa,au wenye matatizo ya ndoa zaoo kutokana na maumbila afya na hisa…

‘Nilichofanya kwanza ni kutafuta utafiti, kuwa kweli mume wangu ana wanawake wan je,…hili nikathibitisha kuwa ni kweli, ana wanawake wa nje, kwahiyo hao nikajua kuwa nina kazi ngumu, kwani huyu mume kakiuka sheria za ndoa, pili ataniletea magonjwa.

‘Je ulikuwa na uhakika gani, au utafiti wako huo uliufanya kwa vipi,….?’ Akaulizwa swali.

‘Ilikuwa kazi nzito,maana sikutaka nijuliane kuwa nina tatizo kama hilo, kwangu ilikuwa ni aibu, lakini sikuwa na njia nyingine, kutokana na majukumu ya akzi yangu, muda mwingi nipi kazini, kwahiyo nikatafiti hadi nikagundua kuwa yupi mtu wanayemuamini sana, ambaye pia ni mtaalamu wa maswala ya ndoa ushauri na pia anajihusisha na kusoma nyota za watu.

‘Mimi nilikwenda kwake sio kwa kutazamiwa nyota au nini, mimi nilichotaka ni yeye kunisaida kuwajua hawo wanawake wanaotembea na mume wangu ni nani…na nilipofika kwake nikajikuta namuelezea kila kitu na yeye akasema kuwa ni kazi ndogo tu, nimpe wiki moja atanipa majibu yangu….’

‘Ni nani huyo mtaalamu, yupo humu ndani?’ akaulizwa.

‘Ndio mtaalamu mwenyewe ni Sokoti….’akasema.

‘Wewe ulimwamini je ?’ akaulizwa.

‘Nilimwamini kwa kusikia kwa watu wengi kuwa kweli anajua mambo hayo, na ukitaka kujua mume wako anatemeba na nani atakutafutia…’akasema.

‘Kwahiyo nilipokuja wiki moja baadaye kweli nilikuta kila kitu, akawa na taarifa ya wanawake wanotemeba na mume wangu na picha za matukio mabli mblai zinazoonyesha yeye akiwa na wanawake hawo, na zilikuwa wazi asingeliweza kunikatalia kwa vyovyote vile.

‘Nikajaribu kuongea naye kila mara, ili tulimalize hilo tatizo, maana haina haja ….nilimwambia kama kaona mimi simfai na basi tuachane kwa wema,…yeye akasema anaju kuoa lakini hajui kuacha, ….nikaona baso labda nitafute njia nyingine…nikakutana tena na huyo mtaalamu akanishauri mambo mengi,lakini mimi nikajiwa na wazo moja ambalo ndilo nililoona ni la maana….’akamwangalia Sokoti ambaye kwa muda ule alikuwa kainamisha kichwa chini.

‘Nilitaka kufanya utafiti wa kisayansi, nikata kujua hawo wanaomzuzua mume wangu wapoje, wana nini ambacho mimi sina. Hili nikaona ni jambo jema, maana utafiti wa kimaandishi hakusaidia kitu, nilsoma vitabu vingi nikajaribu nazaria mbali mbali lakini mwenzangu alikuwa kama vile hayupo. Sasa nifanyeje, nimkimbie, nikaona haizwezakani,…nitapambana kikike, kwani mume ni wangu…

Nilichofanya nikufungua shule, shule ya maswala ya ndoa na matatizo yake, …..mtaniuliza maswali mengi kuwa kama mimi nimeshindwa kuihudumia ndoa yangu nitawezaje kuwafundisha wengine. Kama nilivyosema kuwa nilitaka kutatua tatizo langu kitsayansi, sio kutumia nguvu, lengo langu ni kukutana na hawo wanawake na kujua undani wao, ….si kuwa na jambo jingine zaidi.Ila sikutaka nijulikane kabisa, kuwa mimi ndiye nimeanzisha kitu kama hicho.

Aliyenisaidia hili ni bwana Sokoti, na akawa kama ananialika mimi niwe nitoa mada za ndoa na matatizo yake. Na nilimwambi kuwa afanye kila juhudu awapate hawo wanawake wanaotemba na mume wangu, Ilikuwa kwake kazi rahisi, kama alivyoelezea mwenyewe. Na nikakutana na hawo mabinti, na moja ya mambo niliyokuwa nikiyafanya humo ni kumita kila mwanafunzi na kumhoji, kiundani ….

‘Ulikuwa ukiwahoji vitu gani?’akaulizwa

‘Kwanza niliwajenga kujiamini, na kuniamini na kuwa karibu na mimi kama mama yao, ndio maana ya jina mama docta kwangu mimi, sio mama docta kama ilie ya wazazi wangu. Nilichofanya  nikujitahidi kuvaa kimama, nakujibadili kabisa kiasi kwamba hata wao walikuwa hawaijui sura yangu, nalikuwa navaa miwani mikubwa ya kuficha sura na sura yenyewe nilibadili kinamna, haikuwa rahisi mtu kunijua. Nikawa navaa mawigi ya nywele ndefu, …

Nilipowajengea kujiamini, nikaanza kuwahoji mambo ya ndani, kuhusu mahusiano yao na wanaume, hili lilifanyika kila baada ya darasa la mahusiano nahisia,…ukumbuke kuwa hapo kwenye hiyo shule tulitafuta wakufunzi mbali mbali wanaojua sana kuhusu maumbile, hisia na nyendo za mwanadamu. Kwahiyo ilikuwa ni shule iliyojitosheleza…

‘Kufanya hivyo ni gharama, pesa ulipatia wapi, maana ulitakiwa kuwalipa hawo watu…?’ akaulizwa.

‘Mwanzoni ilinipa shida sana, lakini bwana Sokoti alisema yeye ana jua jinsii ya kuzipata pesa, hasa kutoka kwa hawo wanaume wanaotembea na hwo mabinti, …skiutaka kujua undani zaidi nikamuachia yeye hayo majukumu. Na nilishangaa kweli, maana hawo wakufunzi, walikuwa wakilipwa mishahara mikubwa kuliko hata mshahara wangu wa kazini. Sikujali mwanzoni……’akatulia na kumwangalia hakimu ambaye alionekana akiwaza kitu.

‘Hukuwahi kumuuliza huyo bwana Sokoti, au kufanya uchunguzi wako kujua ni wapi alipokuwa akipata hiyo pesa?’ akaulizwa.

‘Mwanzoni tulipokuwa tukiwekeana mikataba, yeye aliniambai pesa zitatoka kwa hawo hawo wanaume wanaotembea nje ya ndoa, na hili nimuachie yeye, na yeye alisema jambo hilo nilasiri, haitakiwi kujulikana na hata mimi hakutaka kuniambia,sikujali hilo na sikuwa na haja ya kutafanya utafiti wowote, ilimradinilichokuwa nakitaka kimefanikiwa, na nilijiandaa kwa hatua nyingine….

‘Kwanza nilijaribu kufanya yale niliojifunza kwa hawo mabinti kwamume wangu, lakini haikufua dafu, mume wangu alikuwa kama vile keshanitoa moyoni mwake, alinioana kama mtu baki, hasa katika maswala ya mhusiano, tukawa hatujuani hata kutengana katika vyumba, hasa pale tunapokosana. Kila mtu akawa analala kwenye chumba chake.

Akilini mwangu nilikuwa nikiyasiki yale maneno ya hawa mabinti, niliokuwa nikiwafunda, maana walikuwa wakisema wazi wazi kuwa wanawapenda wanaume waliooa, kwani kwanza wana pesa napili wake zao hawajui mapenzi na ni wavivu…hawaki kujifunza jinsi gani ya kuboresha ndoa ndoa,…wanaonawamefika …kwaoo kamawlivyodai,kuwa mume huyo anakuwa kama mtu mwenye njaa, na alihitaji chakula…nyumbani kipo lakini hakina ladha, wakija kwao wanakipata kikiwa kimeandaliwa kwa uzuri zaidi…..

Ndio kwao ilikuwa ni rahisi maana hawana kazi, hawana majukumu yoyote, walichojua wao ni kujiremba, kujifunza mbinu mpya za mapenzi, na pia kwa vile walishapata mafunzo ya maumbie ya binadamu na hisa zake,…basi ikawa ndio kama wamepuliziwa madawa ya kuwaongezea ujuzi. Mimi kila ninapowafundisha nilikuwa nikijaribu kuwakanya kuhusu wanaume waliopo kwenye ndoa kuwa hawo sio vyema kuwa na mahusiano nawo, lakini ilionekana kama kumpigia gita mbuzi…

‘Wakati najiandaa kwa hatua ya pili, nikajikuta nipo kwenye mikono ya polisi, kuwa wamegundua kuwa mimi ndiye niliyekuwa nikimiliki hiyo shule, ambayo inatoa wanawake wanaojiuza na kutengeneza video za kuhujumu wanaume, ambao wanakuja kuhujumiwa kwa kudaiwa pesa nyingi, ili wasije wakazalilika na hizo video.

Nilishituka kwa kweli na niliwapinga sana, na niliona kabla mambo hayo hayajakuwa mabaya zaidi ni bora nijitoe kabisa katika mambo haya, nikakutana Sokoti, yeye hakujali na alisema hakuna ushahidi kama huo ,polisi wanakisia tu,na kwa vile tulikuwa na mwanasheria akasema atalisimamia hilo, na kweli lilimalizwa kinamna.

Hata hivyo nikaamua kuvunja hiyo shule, ingawaje nilisikia kuwa ilikuwa bado inaendelea, na mimi sikutaka kuumiza kichwa change tena, nilikuwanayangu makubwa zaidi ya hayo. Sikukubali kushidwa kuhusu mume wangu, na kila siku hasira, chuki na wivu vikawa vinazidi akilini mwangu, na ikafika hatua nikaona lazima ni fanye jambo.

Nikajaribu kukutana na huyu mwanadada, aliyeuliwa, ….Kimwana, na kila nilipokutana naye alikuwa akiniambia mipango yake kuwa sasa anajiandaa kujenga nyumba ya kifahari, na kununua gari, nilipomuuliza pesa atapatia wapi , akaniambia ni kwa wanaume waliokosamapenzi kwa wake zao…iliniuma sana,…

Hapa naelezea kirahisi lakini kwa Yule aliyeolewa akafanyiwa kitu kama hivyo ndiye anayeweza kuhisi ni maumivuu gani unayoyapata pale uanposalitiwa na mume wake, halafu eti kwa sababu hujui mapenzi….
Hasira chuki , na hata kufikai hatua ya kutaka kulipiza kisasi ikanitanda akilini, kwa ujumla ule moyo wa kibinadamu ukanitoka, nikaanza kuingiwa na wazo jingine….’hapo akatulia.

`Wazo gani hilo?’

‘Kwanza nilitaka kuiharibu ndoa yangu, pili nikataka na mimi nitafute mume wan je…lakini hayo mawili nikaona hayana faida kwangu, haitasaidi kitu, hatimaye nikaoan ni bora kuwaondoa hawa wanawake wanaotembea na mume wangu…maana bila wao mume wangu singeliniacha….chuki , hasira vikatawala ubongo wangu na hatimaye nikatamani kuua….

‘Ulitaka kuwaua wanawake wote waliotembea na mume wako?’ akaulizwa.

‘Sijui, kwakwelikwahli niliyokuwa nayo kwamuda ule,siwezi hata kuelezea,…kwani kiukweli kwa  muda ule hata kama ningelikuwa na bomu, halafu niwaone hawo wanawake wapo sehemu moja ningewadondoshe hilo bomu, niwaanamize kabisa..lakini hasira na chuki zilimlenga mtu mmoja tu, yeye nilimuona kuwa ndio kila kitu, na ndiye mbaya wanguna kuliko wote, huyo ndiye nilitaka awe wa kwanza kuioanja hasira yangu, nimtoe kabisa duniani….’akatulia.

‘Ni nani huyo?akaulizwa.

‘Ni Kimwana….’aliposema hivyo mume wake akashitukana kumtolea macho,…hata hakimu akamwangalia kwa wasiwasi, …..


Je huyu mama alifanyeje? Tuzidi kuwepo.

WAZO LA LEO: Tunapokosa na tukapata mtu wa kutukosa, tukubali kosa, maana sote ni binadamu, hatuwezi tukawa sahihi kila wakati. Mshukuru sana Yule aliyegundua hilo kosa akakusahihisa hata kama kwakufanya hivyo ilikuuma sana. Tukumbuke kuwa kufanya kosa sio kosa ila kulirudia kosa ndio kosa.


Ni mimi: emu-three

3 comments :

Anonymous said...

Kama movie

Anonymous said...

Nasubiri kwa hamu sehemu ijayo

Anonymous said...

Na wewe leo umeamua kimiya kimiya, au ?