Kilikuwa kipindi cha mapumziko, tukawa tunapata chakula cha
mchana,na chakula hicho tulipatia hapo hapo, kuna mgahawa upo kwa nje ya hiyo
mahakama. Mimi na wakili mwanadada tulikuwa tumekaa pamoja,mbali kidogo na wenzetu,
tukawa tunaongea pole pole,
‘Nimekuona…’akaanza kwa utani.
‘Umeniona, kwa vipi?’ nikamuuliza.
‘Mhh,maana macho yako yalikuwa hayabanduki kwa Yule
mwanadada, rafiki ya mke wa wakili wetu mkuu, inaonekana mmh….’akasema wakili
mwnadada.
‘Unajua ni kwa vile tulikuwa tumekaa huku
tumeangaliana,….’nikajitetea.
‘Hata kama mumekaa huku mumeangaliana, lakini macho yenu
yalikuwa yakiongea mengi. Mbona wengine walikaa hivyo hivyo, lakini sikuona
dalili kama zenu. Unajua yeye tabasamu lilikuwa halimuishi usoni kila kikutupia
macho, kweli ni mrembo, au sio, lakini hata
hivyo mara nyingi, alionekana yupo mbali pengine kwa kukuwaza
wewe….’akasema wakili mwanadada, huku akifungua gazeti, ….
Nikageuza kichwa kumwangali kule alipokaa huyu mwanadada
rafiki wa mke wa wakili mkuu, walikuwa wamekaa pamoja na rafiki yake wakiongea,
ilionekana wazi wameivana, na wakati namtupia jicho, kumbe na yeye alikuwa kageuka
kuniangalia, macho yetu yakakutana tena, kwa haraka nikageuka kumwangalia
wakili mwanadada,ambaye alikuwa akisoma gazeti.
‘Hakuna la maana kwenye gazeti, ni mambo yao ya kila siku, ufisadi, ufisadi….’akasema na kuliweka
gazeti pembeni, akaniangalia, na kunikuta nikigeuka haraka kutoka kumwangalia Yule
mwanadada, nay eye akageuka kumwangalia, akasema huku akitabasamu….
‘Mhh, tuendelee sema…unaona kitu hicho, kimetulia….’akasema
huku akinangalia machoni, yale macho yake ya kawaida, sio yale ya mahakamani.
‘Wewe unasema alikwua na mawazo akiniawaza mimi,kwanini awe
na mawazo ya kuniwaza mimi wakati hanijui,…sizani kama tunajuana…..Labda
alikuwa akimuwaza mtu wake, lakini kwa vile tulipata bahati ya kukaa sehemu
ambayo tunaangaliana ndio maana ikawa hivyo, kwani Yule ni nani…hasa, ndio ni
rafiki ya mke wa wakili, lakini unamjaueje?’ nikauliza.
‘Una uhakika kuwa kweli humjui…..?’ akaniuliza huku
akiniangalia kwa makini, na kabla sijamjibu akasema;
‘Mimi namjua kama unavyomjua wewe…..’akasema.
‘Hapana wewe unamjua zaidi yangu…na kwanini nisema simjui
kama namjua kiuwkeli, ….ila hisa zangu zinanituma kama vile nimewahi kukutana
na sura kama hiyo….hebu niambie ni nani na anakaa wapi?’nikauliza
‘Hiyo itakuwa shutukizo kwako wenzetu wanasema ni `surprise’ kama kweli humjui…., usiwe na
papara, kila kitu kitawekwa wazi,….cha muhimu ni kuhakisha kuwa kesi hii
inafikia kikomo, naona hata hakimu amefurahishwa na utaratibu huu, maana watu
wanakuwa huru kujielezea …’akasema wakili mwanadada akionyesha kuwa na furaha
kubwa.
‘Kesi zingekuwa hivi, mbona mtu usingekuwa na wasi wasi
kusema madhambi yake, maana hapa unakuwa kama unatubu dhambi zako na kuelezea
kiukweli kile ulichokifanya,….’nikasema.
‘Tatizo ni udhaifi wetu wa kibinadamu, mwanadamu alivyo,
ukimpa mwanya wa kujitetea na kuweza kuficha makucha yake, atakana hata lile
alilolifanya makusudi,anaweza akasema kabisa sijanywa supu wakati mdomo una
mabaki ya mafuta ya supu na harufu tele, akadai na mafuta ya losheni. Lakini
hatua kwa hatua kama ikizoeleka watu kusema ukweli, kungekuwa hakuna shida….’akatulia
na kuniangalia na mimi nilitaka kugeuka kumwangalia Yule mwanadada,lakini
nikajizuia
‘Unazani kuwa yote waliyoongea mle ndani ni ukweli, sio
kwamba wengine wametungia ili kuficha ukweli….kweli unamwamini huyo Sokoti, ..?’
nikauliza.
‘Karibu kila kitu ninakijua…nilishafanya uchunguzi wa kina,….ila
kiuhakika bado kuna utata, hasa ni nani alifyatua risasi iliyomuua Kimwana…kuwahoji
hapa ni kutaka kupata uhakika, kama kuna mtu ataongea uwongo, nitambana kwa
maswali, maana nina ushahidi wa kutosha, …hilo usijali, mambo yote waliyoongea
pale yanaonekana niya u kweli, na ukweli ni nani alifatua hiyo risasi utadhihiri
humo humo….’akasema wakili mwanadada.
‘Hapo ndipo unaponichanganya, kama sikosei mwanzoni ulisema
unamjau ni nani aliyemuua Kimwana,sasa unasema huna uhakika,….kwahiyo hujui
kiuhakika kuwa ni nani hasa alimuua Kimwana, inavyoonyesa bado kuna utata…?’
nikauliza.
‘Wewe subiri, kwa vile mambo yote yapo mbele ya mahakama,
utamsikia mwenyewe akijitambulisha,...pale hauna atakaye jificha, ….’akatulia
na kuangalia saa yake, halafu akaniangalia an kuniuliza swali;
‘Kwani wewe unazani ni nani anaweza akawa muuaji wa Kimwana?’akaniuliza
swali.
‘Mpaka hapo ilipofikia sio rahisi kubashiri, maana kila
unayemzania mwisho wa maelezo yake anakana kuwa yeye sio muuaji….mwanzoni wa maelezo
ya Sokoti,nilijua kabisa yeye ndiye muuaji,…lakini kakana kabisa kuwa sio yeye,
labda kama kuna maswali ya kumbana, mapaka akiri kuwa yeye ndiye muuaji,….hata
hivyo, maelezo yake yanaonyesha kabisa kuwa yeye hakushika hiyo bunduki na
kumuua Kimwana, sasa sijui ni nani kwakweli…’nikasema huku nikiwaza
‘Usijali ukweli utadhihiri,….kwa wakili kama mimi hadi hapo
ningeliweza kubashiri kuwa ni nani,licha ya ushahidi nilio nao, ambao mwisho wa
siku kama muuajai atakana nitauweka hadharani,lakini siomahalai pake….’akatulia
na kuangalai saa yake.
‘Naona muda tayari tusogee mahakamani….’akasema na mimi
kabla ya kuinuka nikaangalia kule walipokuwa mke wa wakili na rafiki
yake,nikawaonana wao wakiinuka kuondoka,….na hapo nikapata mwanya wa
kumwangalia Yule mwanadada, rafiki wa mke wa wakili akiwa kasimama, na maumbile
yake, kwakeli kila kitu kwake kilikuwa kizuri. Kweli nilikiri moyoni kuwa
nimempenda Yule mwanadada.
Tulipoingia kwenye kile chumba mambo yaliendelea kama
kawaida na Sokoti alimalizia maelezo yake, na muheshimiwa hakimu akauliza kama
kuna swali la kumuuliza, wakili mwanadada akasema kwasasa hakuna swali, maswali
yatakuja baadaye.
Hakimu akauliza ni nani anayefuata, wakili mwanadada
akamwangalia Yule mwanadada,nesi. Yule
mwanadada nesi akakaunja uso, …..na wakili mwanadada akageuka kumwangalia
muheshimiwa hakimu, akasema;
‘Naona sasa tumsikia mke wa wakili wetu mkuu….’ Alisema wakili
mwadada,na hakimu akaangalia saa yake, na akamuita wakili mwanadada, mkuu wa
kituo, wakateta kwa muda ,halafu akasema;
‘Niliwaita hawa wawili kwasababu ndio walioniletea huu utaratibu,
nimefurahia sana, lakini hata hivyo ninahitajika kwenye kesi nyingine, dakika
tano zijazo, na niliona labda baada ya hiyo kesi tukutane tena, lakini
nimeongea na wenzengu wameona tuiahirishe hadi Kesho asubuhi ambapo nitakuwa
na muda wa kutosha.
Ninachowaomba ni kuwa sote tuhakikishe tumehudhuria, mimi
nawaamini kwasababu nyie wote ni waajiriwa, na mumeaminika, nia na lengo letu
ni kuhakikisha kuwa tunalitatua hili tatizo, tunajisafisha, na tutaona kama
kuna hatua nyingine,… lakini hilo litategemea na nyie wenyewe mtakavyokuwa
wakweli mbele yangu.
‘Kwa maana hiyo tutakutaka kesho asubuhi, saa tatu….’akasema
na kuondoka.
*********
Kesho yake tukafika, na tulipofika tukakutana nje
kusalimiana, na baadaye tukaongozana kuelekea ndani. Mimi kama kawaida nilikuwa
na wakili mwanadada, alikuwa ndiye mtu wangu wa karibu kuliko wengine
waliokuwepo.
Wenzangu wakatangulia kuondoka na sisi tukafuata nyuma yao,
nilimuona yule mwanadada kaamua kuwa mwafrika kweli, kasuka kiafrika, na
kuvalia nguo nyeusi, sikujua ana maana kuvaa hivyo, maana kila mtu anahulka
yake katika mavazi yake, huenda ndivyo alivyoona inapendeza kwake, na kweli
elipendeza.
Tukaingia hadi sehemu ya mapokezi, pale kulikuwa na viti,
wengine alikaa, lakini yule mwanadada rafiki wa wakili, akasimama nyuma ya kiti
na kuwa kama kajiegemeza huku kaweka mkono kidevuni, na walionekana walikuwa
wakiongea jambo Fulani la kufurahisha, na wakati tunakuja muelekeo huo
waliokuwa wapo wapo, tukawa tunangaliana huku bado akiwa na lile tabasamu
mdomoni, sijui alifanya hivyo makusi ili aniangalie au ilitokea hivyo tu…ila
moyo wangu ulizidi kuvutika kwake
Macho yetu yalipokutana na yeye, akazidisha lile tabasamu,…
huenda ilitokea hivyo kwasababu alikuw akiongea na mwenzake kwani hata mwenzake
alikuwa akitabasamu hivyo hivyo, na hapo nikahisi jambo ambalo sikuwa na
uhakika nalo, ….akili ikawa inanicheza na kusema haiwezekani, …sio yeye,mbona
kabadilika hivyo, haiwezekani….
Na mara akaja askari na kutuambia kuwa tumebadilishiwa chumba, maana kile tulichokuwa
tukikitumia kinatumiwa na watu wengine, kwahiyo sisi tukaambiwa tuingie kwenye
ukumbi wa mahakama kwani kwa muda huo ulikuwa hautumiki. Ilitisha kidogo
kuingizwa sehemu hiyo, kwani ilikuwa kama kweli mtu anahukumiwa.
‘Samahanini tutatumia humu ndani, lakini sio kwamba kweli
mtu anahukumiwa, utaratibu wetu ni ule ule, kama mwanzo….’akasema hakimu. Na kwa
kuanza tunamuomba mke wa wakili mkuu apite mbele tuendelee na zoezi letu
Mke wa wakili mkuu akiwa kavalia sare na rafiki yake, na
kudhihirisha kweli wanafanana utafikiri mapacha, akainuka haraka na kwenda
sehemu ya kizimba, hakimu akasema asiiingie mle ndani yeye akae kwenye kiti
kilichokuwa pale mbele..akakaa bila wasiwasi, alionyesha kujiamini, hana
wasiwasi…
Kwanza macho yake yalitua kwa mume wake., mume waka
akatabasamu na kutikisa kichwa, akionyesha kumpa uhakika kuwa yupo pamoja na
yeye kwa lolote atakalosema. Na baadaye akazungusha kichwa na kumwangalia
wakili mwanadada, naye akatabasamu na lakini hakutikisa kichwa kama alivyofanya
mume wake. Na halafu akamtupia jicho kwa haraka, mwanadada nesi, mwanadada nesi
akamwangalia kwa dharau.
Nilishangaa, kama hawa ni ndugu kwanini kuna kamauhasama
uliojificha, wanagombea nini,….au ndio kama alivyosema kuwa wakili mkuu
walikuwa mchumba wa mwanzo wa huyo nesi, lakini hata kama ni hivyo,mbona mke wa
wakili, kama inavyojulikana ndiye aliyemsaidia kutafuta kazi huku Dar.
Nikamwangalia Yule mwanadada,ambaye alikuwa kakunja uso kwa
hasira,na mara na yeye akaniangalia, na kwa ajabu kabisa katabasamu. Lile
tabasamu,yale macho, yakanifanaya moyo wangu ushituke. Sijui kwanini,
nikajikuta kichwa kikihangaika kukumbuka jambo,lakini sikuweza kugundua ni
nini.
‘Hebu tueleze kwa kifupi wewe ni nani, na maisha yako na
mumeo…..’alianza wakili mwanadada baada ya maelezo ya mwanzo ya utambulisho,
ambayo aliulizwa na muhushimwa hakimu.
‘Kama nilivyosema awali, mimi ni mke wa wakili mkuu, na
nilizaliwa huko Ulaya, licha ya kuwa makazi yetu ni Kenya, na nawashukuru sana
wazazi wangu kuwa baada ya kunizaa ni pacha mwenzangu, tulipelekwa kwa babu
babu na bibi, waliokuwa wakiishi Kenya. Babu na bibi wao ni Watanzania ile
kwasababu ya biashara, walijiukuta maisha yao wakiwa zaidi Kenya kuliko
Tanzania.
‘Pacha mwenzangu yupo Kenya,…nilikuja kuishi huku kwasababu
ya mwenzangu, ….’hapo akatulia na kumwangalia mumewe, halafu akaongezea kwa
kusema; `nina maana mume wangu…’akatulia na mumewe akatabasamu.
‘Maisha yangu na mume wangu mwanzoni yalikuwa mazuri, lakini
nakiri moyoni kuwa jinsi majukumu ya akzi yalivyoongezeka ndivyo mapenzi yetu
yalivyoanza kuingia doa. Nilijikuta natumia muda mwingi kazini, na kama
mnavyojua kazi zetu, za udakitari, kukutana na watu,kwenda hapa na pale,
kuwahudumia wagonjwa walio mahututi, na hata kusaidia katika upasuaji,kuzalisha,..yaanai
unarudi nyumbani upo hoi.
‘Ikawa nikirudi nyumbani nimechoka, nab ado majukumu ya
nyumbani yanakusubiri, kama ujuavyo, mke ni pamoja na majukumu ya nyumbani,
hata kama una mfanyakazi bado unawajibika na mambo yote ya nyumbani. Tofauti na
akina baba , na hasa akina baba wengine ambao wakirudi nyumbani , hawagusi
kitu, zaidi ya kusubiri kutengewa chakula, maji ya kuoga….’akatulia na
kumwangalia mume wake.
Mume wake alionekana kusema kitu mdomoni,lakini hakutoa
sauti.
‘Je mume wako hakuwa akikusaidia majukumu ya nyumbani,kama
vile kuosha vyombo, kufua na hata kupika…?’ akauliza wakili mwanadada, na
wakili mkuu akajikuta akicheka, na kutikisa kichwa.
‘Kama unavyoona akitikisa kichwa, yeye anajua kuwa hizosio
kazi zake, ni kazi za mwanamke,na mimi sikujali sana kuhusu hayo, nilijua hali
halisi yetu sisi Waafrika,licha ya kuwa kwa kiasi kikubwa tulikulia Ulaya
tukaona jinsi wenzetu wanavyoishi huko, jinsi baba na mama walivyokuwa
wakiishi,lakini bado tulikuwa tunajua milana desturi zetu sisi kama waafrika….’akatulia.
‘Nawashukuru sana baba na mama waliokuja kuliona hilo na
kuwa mara kwa mara walikuwa wakiturudisha nyumba ni kuishi na babu na bibi, na
pia washukuru sana babu na bibi ambao walijibidisha sana kutufundisha maisha ya
mwanamke wa kiafrika, anavyotakiwa awe, hilo lilinisaidia sana vinginevyo,
sijui kama ningeliweza kuishi na mwenzangu.
‘Na mwenzako ukiwa na maana gani?’akauliza hakimu.
‘Nikiwa na maana mume wangu….’akasema
‘Uwe muwazi ….endelea…’akasema hakimu.
‘Nakiri kuwa ilifikia mahali maji yakazidi unga, nikawa
sitimizi baadhi ya majukumu yanayonihusu, lakini sio kwamba niliamua moja
kwamojakuwa sitaki,nilimwambiamwenzangu kuwa nimechoka,au sijisikii, lakini
mwenzagu hakupenda kauli hiyo, na alikuwa akinisema sana, na hata ikafikia
hatua ya kujibisha na hata kupigana….
‘Yeye alisema nini, ulipomwambia kuwa umechoka, au hujisikii…?’
akauliza wakili mwanadada.
‘Alisema hiyo ni kazi yangu, na mimi kama mke wake ,hataki
kusiki kauli hiyo, kwasababuu kanioa, na ukiolewa,yote yanayokustahili kama
mwanamke,ni lazima uyatimize,na kama naona kuwa nachoka kazini, niache kazi….’akasema.
‘Kwanini hukuacha kazi..?’ akaulizwa.
‘Jamani,mimi wazazi wangu walipoteza pesanyingi sana
kunisomesha, ili niwe dakitari, na hata mimi mwenyewe ni kazi ambayo naipenda,
na pia napenda sana kuhudumia wagonjwa,ni kitu ambacho kipo kwenye damu.
Udakitari licha ya kuwa ni kazi,lakini ni wito, ukiwa na huowiti, sizani kwamba
utajisikai vyema kuona mgonjwa yupo hapo usimuhudumie…..’akatulia.
‘Ilifikia hatua nikawanajiuliza ni nani aliye bora,mume
wangu au wagonjwa ninaowahudumia, nikajikuta sipati
jibu,ilakukicha,nakumbukakuwa kuna wagonjwa wananisubiri, kuwa akina mama
wanahiji kusaidia katika kujifungua, kuna…..hapo akili inahama na mbio
nakimbilia hospitalini na kumwavha mume wangu akiwa hana raha,….inaniuma lakini
nitafanyaje.
‘Wewe ni muumini wa dini , na unajua nini kuhusu ndoa….?’ Akauliza wakili mwanadada.
‘Ndio najua hilo, kuwa mume wako ni seheumu ya mwili wako,
najua kuwa kila mmoja anatakiwa amtimizie matakwa mwenzake,bila kukataa, labda
uwe na sababu maalumu, na mimi nilikuwa na sababu maalumu, kama mwenzangu
angelikuwa na ubinadamu, hebu nikuulize wewe kama wakili, je kuna kesi ipo
mbele yako, na mara mume wako akaupigia simu kuwa anakuhitaji, utakatisha hiyo
kesi ukamtimizie matakwa yake?’ akauliza.
‘Hapo unazungumza mtu yupo kazini,lakini wewe ulikuwa ukimkatalia mwenzako
wakati upo nyumbani, huhudumii waginjwa, upo huru kufanya yake anayohitaji mume
wako. Ukamkatalia kwa sababu ya kuchoka,na kutojisikia, huoni hilo ni kosa,?’
akauliza wakili mwanadada.
‘Ndio ni kosa,….lakini nimeshajieleza kwake kuwa nimechoka
na sijisikii anipe muda..sio kwamba nilifanya kiburi na kumkatalia bila sababu…mwili
wa binadamu ukichoka hauna jinsi, hata kama utavuta hisia namna gani, utaishia
kuwa gogo, na sijui kama mtashibishana,….mimi najua hayo, kwasababu ni
dakitari, na pia nimekulia katika mazingira ambayo baba na mama yangu walikuwa
wakisaidia watu wenye matatizo ya namna hiyo , na kwahiyo sikuwa nafanya
makusudi….’akasema.
‘Hebu nikuulize mara ngapi kwa wiki au kwa mwezi uliweza
kuwa na nafasi na mume wako?’ akaulizwa.
‘Kwa wiki ni mara moja au mara mbili…kama unavyojua mimi
nafanya kazi sehemu ambayo nahitajika karibu kila siku….’akajitetea.
‘Ina maana kwa wiki nzima au mwenzi mzima, ulikuw hauna
nafasi na mume wako, ni mara moja au mara mbili tu?’akauliza wakili mwanadada.
‘Hapana….wakati mwingine zaidi ya mara mbili,..lakini
kiuhakika ni mara moja au mara mbili kwa wiki ndipo naweza kusema nakuwa na
nafasi na mume wangu…hata hivyo bado una majukumu ya nyumbani,kazi za nyumbani
zinakusubiria, minguo imajazana,…..ooh, sijui niseme nini….,lakini mwenzangu
yeye alihitaji karibu kila siku…atimiziwe haja yake….’akasema na watu wakacheka.
Na wakili mkuu akatikisa kichwa kama vile kutamba kuwa yeye
ni mwanaume halisi…..
Muda umeisha na sehemu hii ni muhimu sana kutokana na kisa
chetu. Hebu niwaulize, mke huyu alikuwa na makosa, …..? jibuni hata kimiya
kimiya sio mbaya. Tukijaliwa tukutane sehemu ijayo.
WAZO LA LEO: Kukosoana kupo, na hata kuelekezana, lakini
tunapofanya hivyo tusikimbilie kulaumu pale mwenzako anapokosea, maana mara
nyingi ni wepesi sana kuona makosa ya mwenzako kuliko kuona makosa yako.
Tunasahau kuwa tunaponyosha kidole kimoja kwa mwenzako kuna vidole vitatu
vinakuelekea wewe.
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
Mtoto huyoooo, m3 bwana unajua kuturusha roho, unatuwekea oicha za warembo, sasa huyo ndiye nani? Hata hivyo nakuaminia mkuu
Hebu nikuulize haya ni ya kweli na kama ni ya kweli, unapata wapi muda wa kuyaandika, maana sio mchezo? ni swali tu!
Kusema ukweli huyo mwanamke hana makosa, hayo ni makosa ya mumewe, huwezi kumuachia mwenzio afanye kila kitu achoke hoi kama punda kisha utegemee akuhudumie na wewe. Yeye angekuwa na ubinadamu angelimsaidia mwenzie!
Post a Comment