Mume wangu akabadilika kabisa, halali nyumbani,akija
nyumbani anakuja kubadili nguo tu na kuondoka zake, na hataki umuulize wapi anakwenda na kama atakuja kulala nyumbani
anakuwa kalewa, kiasi cha kutokujitambua,naishia kumfulia na kumhudumia,
kiujumla akawa sio Yule mume niliyamjua tena.
‘Baya zaidi akaanza kuwaharibu mabinti niliokuja kuishia
nao hapo nyumbani, na hata kumbaka mtoto ambaye tulimlea wenyewe kama mtoto wetu wa kufikia.
Nilianza kumuogopa kuwa sasa sio binadmu wa kawaida. Nilijaribu kukaa ili aniambia tatizo lipo wapi, nikianzakumuulizahayoinakuwa ndioya sababu ya kuondoka hapo nyumbani, anakuwa kama anakuskiliza,..akisikia unaingia hoja hiyo anageuzakichwa pembeni halafu anainuka nakuondoka....akirudi hapo siyo yeye tena, ukimuuliza ni kupiga...na mimi skukbali kupigwa kirahisi tunapigana....
Nikamtafutia dakitari wa
kumshauri , lakini hakutaka hata kuongea na yeye. Anasema yeye haumwi hahitaji dakitari.Ikafikia hatua nikakata tamaa kabisa, lakini siku nilipoongea
na mama yangu kwa simu na kuniasa kuwa namtia aibu, kuwa mimi ni mke, na huyo
ni mume wangu, nisikubali kushindwa. Hapo ndipo nillipojua kuwa kama mwanamke
sitakiwi kukata tamaa, nilichohitajika kufanya ni kuangalia wapi nilipokosea.
Na hapo ndipo wazo la kufanya jambo likanijia,….’akatulia na kumwangalia mume
wake.
‘Jambo gani hilo, ….?’ Akaulizwa na hakimu.
‘Kwanza mimi ni msomi, na usomi wenyewe ni wa udakitari,
itakuwa ni aibu kuwa nakosana mume wangu kwasababu zinazohusu mwili, na
maumbile ya kibinadam, mimi ndiye nilitakiwa kuwasaidia wale walioshindwa,au
wenye matatizo ya ndoa zaoo kutokana na maumbila afya na hisa…
‘Nilichofanya kwanza ni kutafuta utafiti, kuwa kweli mume
wangu ana wanawake wan je,…hili nikathibitisha kuwa ni kweli, ana wanawake wa
nje, kwahiyo hao nikajua kuwa nina kazi ngumu, kwani huyu mume kakiuka sheria
za ndoa, pili ataniletea magonjwa.
‘Je ulikuwa na uhakika gani, au utafiti wako huo uliufanya
kwa vipi,….?’ Akaulizwa swali.
‘Ilikuwa kazi nzito,maana sikutaka nijuliane kuwa nina
tatizo kama hilo, kwangu ilikuwa ni aibu, lakini sikuwa na njia nyingine,
kutokana na majukumu ya akzi yangu, muda mwingi nipi kazini, kwahiyo nikatafiti
hadi nikagundua kuwa yupi mtu wanayemuamini sana, ambaye pia ni mtaalamu wa
maswala ya ndoa ushauri na pia anajihusisha na kusoma nyota za watu.
‘Mimi nilikwenda kwake sio kwa kutazamiwa nyota au nini,
mimi nilichotaka ni yeye kunisaida kuwajua hawo wanawake wanaotembea na mume
wangu ni nani…na nilipofika kwake nikajikuta namuelezea kila kitu na yeye
akasema kuwa ni kazi ndogo tu, nimpe wiki moja atanipa majibu yangu….’
‘Ni nani huyo mtaalamu, yupo humu ndani?’ akaulizwa.
‘Ndio mtaalamu mwenyewe ni Sokoti….’akasema.
‘Wewe ulimwamini je ?’ akaulizwa.
‘Nilimwamini kwa kusikia kwa watu wengi kuwa kweli anajua mambo
hayo, na ukitaka kujua mume wako anatemeba na nani atakutafutia…’akasema.
‘Kwahiyo nilipokuja wiki moja baadaye kweli nilikuta kila
kitu, akawa na taarifa ya wanawake wanotemeba na mume wangu na picha za matukio
mabli mblai zinazoonyesha yeye akiwa na wanawake hawo, na zilikuwa wazi
asingeliweza kunikatalia kwa vyovyote vile.
‘Nikajaribu kuongea naye kila mara, ili tulimalize hilo
tatizo, maana haina haja ….nilimwambia kama kaona mimi simfai na basi tuachane
kwa wema,…yeye akasema anaju kuoa lakini hajui kuacha, ….nikaona baso labda
nitafute njia nyingine…nikakutana tena na huyo mtaalamu akanishauri mambo mengi,lakini
mimi nikajiwa na wazo moja ambalo ndilo nililoona ni la maana….’akamwangalia
Sokoti ambaye kwa muda ule alikuwa kainamisha kichwa chini.
‘Nilitaka kufanya utafiti wa kisayansi, nikata kujua hawo
wanaomzuzua mume wangu wapoje, wana nini ambacho mimi sina. Hili nikaona ni
jambo jema, maana utafiti wa kimaandishi hakusaidia kitu, nilsoma vitabu vingi
nikajaribu nazaria mbali mbali lakini mwenzangu alikuwa kama vile hayupo. Sasa
nifanyeje, nimkimbie, nikaona haizwezakani,…nitapambana kikike, kwani mume ni
wangu…
Nilichofanya nikufungua shule, shule ya maswala ya ndoa na
matatizo yake, …..mtaniuliza maswali mengi kuwa kama mimi nimeshindwa
kuihudumia ndoa yangu nitawezaje kuwafundisha wengine. Kama nilivyosema kuwa
nilitaka kutatua tatizo langu kitsayansi, sio kutumia nguvu, lengo langu ni
kukutana na hawo wanawake na kujua undani wao, ….si kuwa na jambo jingine
zaidi.Ila sikutaka nijulikane kabisa, kuwa mimi ndiye nimeanzisha kitu kama
hicho.
Aliyenisaidia hili ni bwana Sokoti, na akawa kama ananialika
mimi niwe nitoa mada za ndoa na matatizo yake. Na nilimwambi kuwa afanye kila
juhudu awapate hawo wanawake wanaotemba na mume wangu, Ilikuwa kwake kazi
rahisi, kama alivyoelezea mwenyewe. Na nikakutana na hawo mabinti, na moja ya
mambo niliyokuwa nikiyafanya humo ni kumita kila mwanafunzi na kumhoji,
kiundani ….
‘Ulikuwa ukiwahoji vitu gani?’akaulizwa
‘Kwanza niliwajenga kujiamini, na kuniamini na kuwa karibu
na mimi kama mama yao, ndio maana ya jina mama docta kwangu mimi, sio mama
docta kama ilie ya wazazi wangu. Nilichofanya nikujitahidi kuvaa kimama, nakujibadili kabisa
kiasi kwamba hata wao walikuwa hawaijui sura yangu, nalikuwa navaa miwani
mikubwa ya kuficha sura na sura yenyewe nilibadili kinamna, haikuwa rahisi mtu
kunijua. Nikawa navaa mawigi ya nywele ndefu, …
Nilipowajengea kujiamini, nikaanza kuwahoji mambo ya ndani,
kuhusu mahusiano yao na wanaume, hili lilifanyika kila baada ya darasa la
mahusiano nahisia,…ukumbuke kuwa hapo kwenye hiyo shule tulitafuta wakufunzi
mbali mbali wanaojua sana kuhusu maumbile, hisia na nyendo za mwanadamu.
Kwahiyo ilikuwa ni shule iliyojitosheleza…
‘Kufanya hivyo ni gharama, pesa ulipatia wapi, maana
ulitakiwa kuwalipa hawo watu…?’ akaulizwa.
‘Mwanzoni ilinipa shida sana, lakini bwana Sokoti alisema
yeye ana jua jinsii ya kuzipata pesa, hasa kutoka kwa hawo wanaume wanaotembea
na hwo mabinti, …skiutaka kujua undani zaidi nikamuachia yeye hayo majukumu. Na
nilishangaa kweli, maana hawo wakufunzi, walikuwa wakilipwa mishahara mikubwa
kuliko hata mshahara wangu wa kazini. Sikujali mwanzoni……’akatulia na
kumwangalia hakimu ambaye alionekana akiwaza kitu.
‘Hukuwahi kumuuliza huyo bwana Sokoti, au kufanya uchunguzi
wako kujua ni wapi alipokuwa akipata hiyo pesa?’ akaulizwa.
‘Mwanzoni tulipokuwa tukiwekeana mikataba, yeye aliniambai
pesa zitatoka kwa hawo hawo wanaume wanaotembea nje ya ndoa, na hili nimuachie yeye,
na yeye alisema jambo hilo nilasiri, haitakiwi kujulikana na hata mimi hakutaka
kuniambia,sikujali hilo na sikuwa na haja ya kutafanya utafiti wowote,
ilimradinilichokuwa nakitaka kimefanikiwa, na nilijiandaa kwa hatua nyingine….
‘Kwanza nilijaribu kufanya yale niliojifunza kwa hawo
mabinti kwamume wangu, lakini haikufua dafu, mume wangu alikuwa kama vile
keshanitoa moyoni mwake, alinioana kama mtu baki, hasa katika maswala ya
mhusiano, tukawa hatujuani hata kutengana katika vyumba, hasa pale
tunapokosana. Kila mtu akawa analala kwenye chumba chake.
Akilini mwangu nilikuwa nikiyasiki yale maneno ya hawa
mabinti, niliokuwa nikiwafunda, maana walikuwa wakisema wazi wazi kuwa
wanawapenda wanaume waliooa, kwani kwanza wana pesa napili wake zao hawajui
mapenzi na ni wavivu…hawaki kujifunza jinsi gani ya kuboresha ndoa ndoa,…wanaonawamefika
…kwaoo kamawlivyodai,kuwa mume huyo anakuwa kama mtu mwenye njaa, na alihitaji
chakula…nyumbani kipo lakini hakina ladha, wakija kwao wanakipata kikiwa
kimeandaliwa kwa uzuri zaidi…..
Ndio kwao ilikuwa ni rahisi maana hawana kazi, hawana
majukumu yoyote, walichojua wao ni kujiremba, kujifunza mbinu mpya za mapenzi,
na pia kwa vile walishapata mafunzo ya maumbie ya binadamu na hisa zake,…basi
ikawa ndio kama wamepuliziwa madawa ya kuwaongezea ujuzi. Mimi kila
ninapowafundisha nilikuwa nikijaribu kuwakanya kuhusu wanaume waliopo kwenye
ndoa kuwa hawo sio vyema kuwa na mahusiano nawo, lakini ilionekana kama kumpigia
gita mbuzi…
‘Wakati najiandaa kwa hatua ya pili, nikajikuta nipo kwenye
mikono ya polisi, kuwa wamegundua kuwa mimi ndiye niliyekuwa nikimiliki hiyo
shule, ambayo inatoa wanawake wanaojiuza na kutengeneza video za kuhujumu
wanaume, ambao wanakuja kuhujumiwa kwa kudaiwa pesa nyingi, ili wasije
wakazalilika na hizo video.
Nilishituka kwa kweli na niliwapinga sana, na niliona kabla
mambo hayo hayajakuwa mabaya zaidi ni bora nijitoe kabisa katika mambo haya,
nikakutana Sokoti, yeye hakujali na alisema hakuna ushahidi kama huo ,polisi
wanakisia tu,na kwa vile tulikuwa na mwanasheria akasema atalisimamia hilo, na
kweli lilimalizwa kinamna.
Hata hivyo nikaamua kuvunja hiyo shule, ingawaje nilisikia
kuwa ilikuwa bado inaendelea, na mimi sikutaka kuumiza kichwa change tena,
nilikuwanayangu makubwa zaidi ya hayo. Sikukubali kushidwa kuhusu mume wangu,
na kila siku hasira, chuki na wivu vikawa vinazidi akilini mwangu, na ikafika
hatua nikaona lazima ni fanye jambo.
Nikajaribu kukutana na huyu mwanadada, aliyeuliwa, ….Kimwana,
na kila nilipokutana naye alikuwa akiniambia mipango yake kuwa sasa anajiandaa
kujenga nyumba ya kifahari, na kununua gari, nilipomuuliza pesa atapatia wapi ,
akaniambia ni kwa wanaume waliokosamapenzi kwa wake zao…iliniuma sana,…
Hapa
naelezea kirahisi lakini kwa Yule aliyeolewa akafanyiwa kitu kama hivyo ndiye
anayeweza kuhisi ni maumivuu gani unayoyapata pale uanposalitiwa na mume wake, halafu eti
kwa sababu hujui mapenzi….
Hasira chuki , na hata kufikai hatua ya kutaka kulipiza
kisasi ikanitanda akilini, kwa ujumla ule moyo wa kibinadamu ukanitoka, nikaanza
kuingiwa na wazo jingine….’hapo akatulia.
`Wazo gani hilo?’
‘Kwanza nilitaka kuiharibu ndoa yangu, pili nikataka na mimi
nitafute mume wan je…lakini hayo mawili nikaona hayana faida kwangu, haitasaidi
kitu, hatimaye nikaoan ni bora kuwaondoa hawa wanawake wanaotembea na mume
wangu…maana bila wao mume wangu singeliniacha….chuki , hasira vikatawala ubongo
wangu na hatimaye nikatamani kuua….
‘Ulitaka kuwaua wanawake wote waliotembea na mume wako?’
akaulizwa.
‘Sijui, kwakwelikwahli niliyokuwa nayo kwamuda ule,siwezi hata
kuelezea,…kwani kiukweli kwa muda ule hata
kama ningelikuwa na bomu, halafu niwaone hawo wanawake wapo sehemu moja
ningewadondoshe hilo bomu, niwaanamize kabisa..lakini hasira na chuki
zilimlenga mtu mmoja tu, yeye nilimuona kuwa ndio kila kitu, na ndiye mbaya
wanguna kuliko wote, huyo ndiye nilitaka awe wa kwanza kuioanja hasira yangu,
nimtoe kabisa duniani….’akatulia.
‘Ni nani huyo?akaulizwa.
‘Ni Kimwana….’aliposema hivyo mume wake akashitukana
kumtolea macho,…hata hakimu akamwangalia kwa wasiwasi, …..
Je huyu mama alifanyeje? Tuzidi kuwepo.
WAZO LA LEO: Tunapokosa
na tukapata mtu wa kutukosa, tukubali kosa, maana sote ni binadamu, hatuwezi
tukawa sahihi kila wakati. Mshukuru sana Yule aliyegundua hilo kosa
akakusahihisa hata kama kwakufanya hivyo ilikuuma sana. Tukumbuke kuwa kufanya
kosa sio kosa ila kulirudia kosa ndio kosa.
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
Kama movie
Nasubiri kwa hamu sehemu ijayo
Na wewe leo umeamua kimiya kimiya, au ?
Post a Comment