‘Siku moja nikiwa kwenye mgahawa mmoja, nikiwa nimeshaingiwa
na ibilisi…’akawa anaelezea mke wakili mkuu, huku akionyesha wazi hasira
alizokuwa nazo.
‘Nilianza kuwaza jinsi gani nitafanya pale nitakapomuona
mume wangu na hawo machangu-doa.Hapo o nilishazamiria kuwa nikimuona mmoja wa
hawo wanawake nitavaana naye hadharani, nilijua kuwa mume wangu anapenda kufika
hapo. …lakini hakutokea siku hiyo.
Jamani wivu unaweza ukakutuma ku-ua ,wivu unaweza ukakutoa katika
akili ya kibidamu na kuwa na akili ya mnyama mkali, hilo nimejifunza,
…sikuamini kuwa ningelikuwa na dhamira hiyo kabla, mwanzoni mtu akiniambia
hivyo, kuwa unaweza ukaua kwa ajili ya mapenzi nilikuwa sikubaliani nalo…..
Nikiwa pale mgahawani , hasira zikiwa zimenipanda, mara
nikamuona mwanadada mmoja akifika pale, akaagiza vitu, akafungiwa kwenye mfuko,
na kuanza kuondoka…mimi kwa ile hasira,nizania kuwa huenda ni mmoja wa wanawake
wa mume wangu. Lakini cha ajabu…. miwani kama vile anaficha macho, na alikuwa
na ywele nyingi kama zile nilizozoea kuvaa wakati ninatoa darasa, nikashangaa,
ni nani huyu ananiigiza mimi uvwaaji wangu….
Nikaona nimfuatilie,….nikamfuatilia kwa nyuma hadi akaingia
hospitali iliyopo hapo jirani,….nikamsubiri hapo nje kuwa akitoka niongee na
yeye, lakini hakuweza kutokea tena, nikakata tamaa, na wakati nataka kuondoka,
mara nikashikwa begakwa nyuma, nilipogeuka nikakutana na sura ambayo
niliikumbuka kwa mbali.
‘Wewe ni nani mbona kama nakufahamu?’ nikamuuliza.
‘Wewe si binti wa mama Docta, mliozaliwa mapacha…siku hizi
umekuwa mpelelezi nini…? ’akaniuliza kwa utani.
‘Oooh, nimekukumbuka kumbe wewe ni mama docta mtarajiwa…ina
maana ni wewe uliyekuwa umevaa vile…..’nikabakia kushangaa.
‘Bado tu unalikumbuka hilo jina…mama docta mtarajiwa…..!’
akasema kwa kushngaa. Mama docta mtarajiwa ndilo jina tulilokuwa tukimuita yeye
akiwa huko kwenye shule ya mama. Kwakweli nilifurahi sana kumuona yeye,maana
nimepata mtu atayenisaidia katika mazila niliyo nayo. Nikamuomba tukaongee , na
kwa muda ule alikuwa kavaa sare za kidakitari, akasema nimsubiri hapo akabadili
nguo.
‘Alirudi baaada ya muda, alikuwa kama siyo yule dada
niliyekutana naye kabla, alikuwa mrembo, msichana mdogo, ….na umbo lake la
kuvutia lilionekana dhahiri, nikasema moyoni kweli kuna wanawake wazuri, ….
‘Kweli wewe ni mrembo, mume wako kama ana wivu atakuwa
anapata shida sana, maana …mmh, umejaliwa, hivi nikuulize wanaume wa barabarani
hawakusumbui, maana sipati picha, najaribu kuwaza, jinsi gani hawo wanaume
wanavyoumia shingo kwa kugeuka kukuangalia….na unafanyeje mpaka uonekana
mschana mdogo, tofauti na vile nilivyouona awali…’nikamtania na yeye akawa
anatabasamu, kinyume na wanawake wengine ambao kama ungewapaoa sifa kama hizo
kingeanguka kicheko.
‘Simpaka nimpate huyo mume, mimi hapa nilipo nawachukia
wanaume wote duniani,na wala sitaki kabisa kuolewa tena,….na nimegundua kuwa
kwa vile sipo na mume, bado naonekana msichana…eti msicahana mdogo, mimi sio
msichna mdogo,,….’akasema huku akijaribu kujiangalia .
‘Kweli unaonekana msichana mdogo….’nikamhakikishia.
‘Mimi niseme ukweli,…nipo kwenye ndoa, na ndoa yangu ilikuwa
moja tu…..’akasema huku akionyesha kidole hewani kimoja. Aliposema hivyo
akaniacha hoi,maana nilijua huyu ndiye mwalimu wa kutibu ndoa za watu, lakini hiyo
kauli yake ikanifanya nishituke, ina maana ….
‘Mbona sikuelewi, wewe si mwalimu wa ndoa za watu, ….ina
maana yale yote uliyokuwa ukiwafundisha wanafunzi wako ilikuwa ni kugeresha,
ina maana hata wewe umeshindwa kutatua matatizo ya ndoa yako, ilikuwaje tena
uwe mwalimu au dakitari wa kutibu ndoa za watu…..?’ nikamuuliza.
‘Ndio hapo ule usemi wa wahenga usemeo mganga hajigangi, unapoonekana
wazi, na pia ujue kuwa penye miti mingi hakuna wajenzi. ….’akaniangalia machoni kama, na mimi nikacheka nikiwa
simuamini hichoanachoniambia, maana kama ungeliwahi kuhudhuria moja ya darasa
lake ungelisema huyo hatakuwa na matatizo na ndoa yake abadani. Baadaye akasema
kuniambia mimi;
‘Mimi ndio najua mengi kuhusu ndoa za watu kinadharia, na
kivitendo ni kupitia kwa wale niliowahi kuishi naoo au kusikia au kutoa
ushuhuda…na kwa ujumla najua sana jinsi gani ya kuwasaidia watu waliopo kwenye
matatio ya ndoa, lakini cha ajabu ,…..’akatulia hapo huku akikuna kichwa kama
vile anaona aibu kutamka hayo maneno, nilimwangali huku bado natabasamu,
kuonyeshakuwa siamini hayo maneno yake, na yeye akaendeleakunimabi hivi;
‘Mimi nimeshindwa kutatua matatizo niliyo nayo, ya ndoa
yangu iliyoyeyuka toka huko mwaka arubaini na kenda ….na sijui kama nitaweza tena
kuirudisha…maana mambohubadilika, na maisha hayarudi nyuma, mimi sio yule wa
siku zile,…na huenda hata mwenyewe keshanisahau maanasiyekuwepo na alke halipo,
na kwavile tuliishi mbali mbaliikawa fimbo ya mbali haiuwi nyoka, unasikia sana
mpendwa…’akawa ananisimulia kwa kwakiswahili cha Mombasa.
‘Siamini hayo unayoniambia…’nikamwambia wazawazi.
‘Amini usiamini ndivyo ilivyo, toka lini kitanda
usiichokilalia ukajua kunguni wake, na hata hivyo siri ya mtungu aijuaye ni
kata, hutaweza kuingia kwenye nafsi yangu ukajua nini kilichonisibu hadi
kufikia hapo, na mara nyingi sitaku kumsimulia mtu yoyote, zaidi alijua mama
yako mpendwa wangu, na sasa najikuta nikifunua siri yangu kwako….’akasema huku
machozi yakiwa yanamlenga lenga. Kwa kweli hapoi name nikshikwa nasimanzi ….
‘Hivi ina maana sisi wanawake ni watu wa kuteseka, ina maana
gani ya ndoa kama kila ninayeoongea naye hanisimulii jema, bali na mteso ndani
ya ndoa, ….’nikajikuta nikisema hivyo mbeel yake, yeye akanishika bega huku
akiwa haniangalii machoni, akasema;
‘Sio kweli, sio kweli kuwa wanawake wote wapo kweye mashaka,
ni kwasababu umekutana na wale waliopo kwenye mashaka, hata hivyo ndoa au
mapenzi ni kama safari ndani ya bahari ,kuna kupanda na kushuka, na pia huwezi
kukosa vipingamizi, ndio maana inaitwa ndoa,….n-doa,….niliwahi kuwaeelzea
wanafunzi wangu kuwa haya maneno tunayatumia tu, lakini hebu jaribu
kuyakokotoa, utagundua kuwa mpangilio wake unawezaukakupa siri fulani
iliyoficha.
‘Siri hiyo inaweza ikawakweli inajulikana kwa huyo
aliyeligundua hilo neno, au asijue kabisa, anayejua mwenyewe ni muumba, kwahiyo
kila neno, kila jambo hebu tujaribu kulitafakari kiundani, wenzetu wanasema
uliangalia katikati ya mstari….sasa ngalia hili neno ndoa, limetanguliwa na
neno `n’…hili linaweza likawa na maana `no’ ambayo ni hapana, au kwa Kiswahili likawa
na maana ya `na’…halfu angali neno lililofuatitia
`doa’…
‘Kwahiyo kwa tafasiri ya katikati ya mstari ni kuwa ndoa ni
kitu kilitakiwa kiwe hakina doa, au kinaweza kikawa na doa…yote yanawezekana.
Kwa mtaji huo unatakiwa ukubali vyovyote iwavyo na ujua kuwa yote ni majaliwa,
na huenda kukatokea jambo likakuuma sana, unatakiw aukubaki ukweli, kuwa huenda kutokea hivyo, ni kwa manufaa yako, lakini …lakini….’hapo alinyamaza
kwa muda akionekana anakwazwana jambo alilotaka kuliongea, na mimi nikashindwa kujizua nikamuuliza.
‘Lakini nini….?’ Nikamuuliza.
‘Usikate tamaa,.... hasa unapokuwa umeshafunga ndoa,….pigania
ndoa yako hadi mwisho, maana ilishaandikwa kwenye vitabu vya mungu kuwa wewe ni mke wake na
yeye ni mume wako, usipopigania wenzako watajitwalia kirahisi, wapo watu
wanasubiri huo mwanya, na sio wote wenye simile, wenye subira,…sijui uninielewa…ndio nikasema lakini, ina maana lakini umfnya juhudi gani kuitetea ndoa yako, ukikubali kirahisi, basi ....lakini ni vyema usikubali kirahisi kama...bado unampenda, kama.....hiyo kama uitizame mara mbili.....’akanimbia.
‘Unajua nilipofika hapa Dar, nilikuwa na matarajio mengi,
kuwa huenda nitamkuta,.... huenda lile tonge nililifinyanga nitaweza kulifikisha
kinywani, lakini …mungu wangu, sikuamini nilichokikuta, nikawaza sana, ina
maana yale yote yalikuwa hayana maana…ina maana unaweza ukapenda, usipendwe,
ina maana mimi nina kasoro, ina maana mimi sio mzuri, mbona wengi wananimbia
huo wimbo kuwa wewe ni mrembo,kwanini yeye asione hivyo….’ Huyu mke wa wakili
alipofikia hapa akamwangali rafiki yake ambaye alikuwa kifuatilia hayo
mazeungumzo huku akitabasamu.
‘Aliniambia kuwa
alipofika hapa Dar, aliyoyakuta yalimfanya akate tama, alisema hivi;.
‘Yaani nimekata tamaa kabisaa, na kuzidi kuwachukia wanaume,
na zaidi nimejikuta nikiwachukia hata hawo wanawake waliomfanya yule
niliyempenda asinikumbuke tena…lakini dhamira ikawa inaniambai kwanini nikubali kirahisi, kwani hawa watu waachiwe hivi hivi kirahisi maana huenda ukasalimu amri, na bado ukapata mwingine wakaja kumchukua pia....lazima lifanyike jambo.....’akasema na mimi hapo nikasema moyoni,kumbe
sipo peke yangu.
‘Hebu niambie ni nini kimekusibu, maana naona matatizo yako yanaweza
yakawa ni sawa na matatizo yangu..?’anikamuuliza.
‘Sizani kuwa matatizo yako yanafanana na matatizo yangu,....ni mtizamo ti wa kifikira, na kila mtu anaumia kutoka na yake yaliyomsibu..... maana wewe kama
sikosei upo ndani ya ndoa…..’akaniambia huku akiangalia pete iliyopo kidoleni
kwangu,na mimi nikainua mkono ili auone vyema, akaendelea kusema hivi;
‘Wewe inaonyesha kuwa una mume tayari na labda mnaonana kila
siku,…kama ni matatizo ni yaleya vikombe vilivyopo kabatini havikosi kugongana,
au sio,…..,lakini mimi ndoa yangu ilipotea zamani sana, nikiwa mdogo,..na
nimekuwa nikiitafuta hadi leo bila mafanikio….’akaniambia.
‘Oooh, tangu ukiwa mdogo, kwa vipi, sasa wewe unaleta
vichekesho,…ina maana ulikuwa na mchumba ukiwa mdogo…mdogo kiasi gani,….?’
nikamuuliza.
‘Hayo tuyaache maana yananitonesha moyo wangu, hebu niambie,
wewe upo hospitali gani maana mama yako aliniambia upo huku unafanya kazi
kwenye hospitali za serikali, nilijaribu kukutafuta lakini sikuweza kukupata,
nikakata tamaa, upo hospitali gani?’ akaniuliza huyo mwandada.
‘Na tuliongea mengi kuhusu maisha yetu ya kazi,lakini
mwenzangu hakutaka kabisa tuongee kuhusu maswala ya ndoa yake tena hasa
kumuhusu yeye..kitu kilichonivunja nguvu. Nanikajua kuwa masahibu yake ni
makubwa huenda ni makubwa kuliko ya kwangu….hapo hasira zikaanza kushuka.
*******
Siku zilivyozidi kwenda ndivyo tulivyozidi kuzoeana na hatua
kwa hatua akawa ananisimulia mambo yake, lakini hakuwahi kunitaji huyo mume
wake ni nani na sasa hivi yupo wapi, amesema hiyo ni siri yake mpaka hapo
atakapoona haina haja tena,….
‘Hebu tuambie kuhusu wewe na Kimwana mlizoeaan vipi, na hadi
kufikia hatua ya kumchukia …?’ akaulizwa.
`Kimwana alikuwa mcheshi sana, muongeaji na mjanja
sana,ukichanganya na uzuri wake, ujuzi wa mambo ya mahusiano,….basi wanaume
wakawa wanakuja kwake kama mbwa anavyojipeleka kwa mbwa mwitu, na kila
alichotaka alikipata. Na aliwahi kuniambia kuwa amegundu kuwa mwanzoni alikuwa
akiogopa bure, kumbe anaweza akawa mtu mashuhuri sana, tajiri wa kuogopwa…..
‘Nikamuuliza kwa vipi, yeye akasema kwa kupitia kwa matajiri
waume za watu, za wanawake wasiojua kuwatunza waumezao,…atahakikisha kila
mwanaume atakayemtaka, anamkwangua hadi senti yake ya mwisho, na kwa muda alisema
kuwa kaolewa kiujanja na keshapata nyumba,lakini alikuwa akitaka kuiuza,…
‘Nikiiuza najenga nyumba kubwa ya kifahari, na kama sio huyo
mume anayejifanya wa sheri, basi atakuwa mume mwingineatakayeimalizia hiyo
nyumba, sina shida ya pesa..lakini huyo mwingien hana pesa, ….nitahakikisha
huyo wa sheria anamucha mke wake anakuja kwangu,. Tatizo ni huyu mume
aliyenioa…nataka kuachana naye, lakini naona kama nimempenda, na mimi sitaku
kupenda.
Na kaja huyu mume wa mtu, mtu wa sheria, nikaona lazima na
yeye awe katika mkoba wangu, maana huwezi jua, unaweza ukakwama mahali
ukahitaji sehemu ya kuehemea, kisheria,… namuhitaji huyo mume kwasababu moja
kubwa, ni wakili, na katika mapenzi,hachoki, na pia anaelekea kila
unavyompeleka, na mwepesi kutoa pesa zake, ila wakati mwingine ana hasira,
anaasili ya hasira, sasa hilo litanifanya nikosane naye, mimi sipendi kabisa
kuburuzwa….
‘Anaitwa nani…?’ nikamuuliza.
‘Wenyewe waanmuita, Mkuu wa wakili,…ni bwege fulani hivi,
…wenyewe wanamuona mtu mashuhuri sana…lakini kwangu si lolote, yupo uchi, hana lolote zaidi ya pesa zake,
….na shida yake kubwa, ana njaa ya mapenzi, mkewe anaonekana si lolotekama alivyo yeye, ...inaonekana kabisa, mkewe hajui kazi..hajui kuishi na mume..., sasa
kakutana na mtaalamu, atakoma ubishi!...heheheee...’ akaniambia na kucheka kwa dharau. Hasira chuki vikanitanda,na
alipoona nipo kimiya..akshituka na kuniangalia, na kama nisengekuwa nimevaa hayo mawani makubwa yanayofunika sehemu kubwa ya uso, angeligundua jinsi nilivyobadilika sura..... akaniuliza.
‘Unamfahamu nni huyo mtu….?’ akaniuliza.
‘Labda ….sijui kama namjua…’nikasema huku nikimeza hasira,
nikimeza wivu, chuki….nikamwangalia yulebinti hadi yeye akahisi vibaya.
‘Inaonekana kama unamjua huyo mwanaume, maana kila ukiniuliza
kuhusu yeye unakuwa kama mtu aliyepigwa na ganzi,….’akanimabia.
‘Hapana ni mshangao maana nilitarajia kuwa wewe ni mrembo na
unaweza ukampata mume yoyote, lakini cha jabu unakimbilia waume za watu,huoni
kuwa unajipotezea muda wako, utaolewa lini’nikamwambia.
‘Hivi sasa nipo kwenye ndoa, lakini ndoa ya kimtego, maana
kile nilichokitaka kwa huyo mume nimeshakipata, sasa nahitaji talaka yangu,sina
muda naye, na nasikia ana kesi kibao,sasa huoni kuwa hakuna uaslama hapo,
niachane naye nijue mambo yangu yataendaje, sina shida naye tena….’haya maneno
aliniambia kipindi ambacho nimeshajitoa kwenye hilo kundi.
`Kwa ujumla katika wanafunzi wote, huyu Kimwana nilizoea na
naye sana,na kila mara nilikuwa nikiongea naye nikiwa na hamu ya kujua zaidi
kuhusu yeye, na kwanini wanaume wawe wanampenda yeye sana kuliko wengine, maana
sura sio tija, lakini kuna jambp jingine,……
Nilipomdadisi sana,aliniambia kuwa yeye katika jambo alilokuwa
akilitia mkazo sana anapokutana na mume, ni kuhakikisha kuwa anampagawisha mwanaume
kwa ujuzi wa hali ya juu,…hapo hafanyo utani maana yupo kazini na kama
alivyosema, hawezi kumlisha mume wake chakula cha aina moja tu, lazima kila
siku anakuja na mapishi mapya….chachandu na kila aina ya kuongeza ladha….
Huyu kwake ni rahisi…ndivyo nilivyoona hivyo,au kujitetea
hivyo kwenye nafsi, kuwa yeye hayo aliyachukulia kama kazi yake, hakuwa na majukumu
yoyote, alikuwa na muda wakutosha, na licha ya utundu wake, lakini pia alikuwa akihakikihsa
kuwa anamjua vyema mume atakayekutana naye,amejifunza mengo kuhusu wanaume…na
hapo nikajua kuwa huyu ndiye adui yangu mkubwa.
‘Unamfahamu Kimwana….?’nikamuuliza huyo rafiki yangu
tuliyekutana naye…
‘Nani asiyemfahamu malaya Yule…namchukia sana yule
mwanamke,na kama ningelimpatia nafasi , ningeutoa ubongo wake…kwa mkono wangu…’akaniambia
mwenzangu huyo
‘Kumbe tupo pamoja, hata mimi nawaza hivyo hivyo….na hapa
nilipo natafuta mwanya ,nikimpatia tu, nahakikisha naitoa roho
yake,….’nikamwambia huyo mwenzangu.
‘Hiyo kazi rahisi, kuna mwanadada mmoja kaniambia kuwa yeye
yupo tayari kunisaidia maana na yeye kachukuliwa mume wake, na baya zaidialipta
mume mwingine na huyu mwanadada akamchukulia tena, na akapata mume mwingine na
bado akaja kuporwa na mtu huyo huyo,kwahiyo amemuona kuwa huyo ni adui yake
mkubwa…..
`Hiyo kali, maana kila nikiwaza naona kumbe yangu yanaweza
yakawa yana nafuu,… sasa amesema atakusaidia vipi? nikamuuliza.
‘Kasema yeye anajua nini cha kufanya, anachohitaji ni
silaha…na angelipenda silaha inayoweza kuua kwa mbali…’akaniambia na mimi nikakumbuka
silaha ya mume wangu ya kuwindia…
‘Silaha….mmh, ikihitajika sio tatizo hasa kwa huyo mchukua
waume za watu, nipo tayari kuitoa, nikihakikisha kuwa itafanya akzi hiyo.
‘Huyo mwanadada,kazamiria kweli…,..lakini tatizo ni jinsi
gani , baada ya hilo tukio tutakavyoweza kujinasua kwenye mikono ya sheria
maana hpo tutakuwa wengi, watu watatu hakuna siri tena hapo…’akaniambia
‘Unamwamini vipi huyo mwanadada,asije akawa askari….?’
nikamuuliza
‘Chamuhimu ni siri ,…. hata hivyo huyo mwanadada simwamini
moja kwa moja, ….’akaniambia
‘Kama humuamini kwanini tena umtafutie silaha, anaweza akatugeuka
nayo,mimi hapo nashauri tuachane naye, tutafute mbinu nyingine…’nikamshauri.
‘Mbinu gani?’nikamuuliza.
‘Kwani sisi hatuna mikono, tunajua kutumia silaha, tuna
shabaha, tunaweza hata kumuwinda kwa mbali,….’
‘Hiyo ni sawa, ngoja nifanye uchunguzi Fulani ukikamilika
nitakuarifu….’akaniambia, na baada ya siku mbili tukakutana tena.
‘Ule uchunguzi umekamilika, na nimegundua mengi ya huyo
Kimwana, kumbe yupo hapa hapa Dar, hajakimbia kama walivyodai watu,
….’akaniambia.
‘Kwani alikuwa amekimbia,…?’ nikamuuliza.
‘Si anatafutwa na polisi, kwa mikasa yake hiyo, na kumbe
watu wengi, wanamtafuta kwa hayo aliyoyafanya, sijui anashiriiana na nani
…namjua jamaa mmoja,lakini yeye kakataa kata kata kuwa hamtumii Kimwana kwa
mambo hayo machafu….’nikamwambia.
‘Ehe niambie tufanyeje sasa, maana siku zinakwenda na hasira
inaweza ikaisha,….’nikamwambia.
‘Ni hivi , huyu Kimwana ana jengo kubwa, ambalo
analimalizia, ….kwa pesa za mazambi yake, ni jengo zuri na lipo maeneo ya huko
Mbezi, na karibu yake, sio mbali sana na nyumba yake, kuna jengo jingine lipo mkabala na hilo, ukiwa
kwenye hilo jenga mbalo lipo juu kidogo unaweza kuona kilal kitu kwenye nyumba
hiyo ya Kimwana. Aliniambia kuwa keshafika hapo na kufanya uchunguzi akaona
inafaa,….
‘Kweli wewe umezamiria….utanipeleka nikapaone,….’nikamwambia
na kweli siku moja tukafika na kupakagua name nikakubali kuwa ni sehemu
nzuri,na inafaa…na bahati nzuri, siku hiyo hata Kimwana mwenyewe alikuwepo hapo, na tuliweza kumuone
vyema tukiwa kwenye hilo jengo la pili.Ni bahati mbaya siku hiyo hatukuja na
silaha, maana kama ingelikuwepo tungefanya mambo yetu….yaani kila nikumuona
huyo binti hasira zilikuwa zikinipanda…..
‘Kwa umbali ule unatakiwa uwe na shabaha…’nikamwambia, yeye
hakunijibu kitu, na nilipoona katulia nikasema;
‘Na yalemdirisha ni ya viyoo, yana matundu makubwa kama
urembo na tunaweza kupenyeza risasi bila kuvunja hilo dirisha…au shabaha zako
umezisahau, unakumbuka yale mazoezi ya mama ya kulenga shabaha…?’ nikamuuliza.
‘Nakumbuka sana, na hilo nilishaliona, na jambo jingine,
ufanye juhudi, hiyo silaha iwe na kitu cha kuzuia sauti, ….siunajua hilo, kuwa
unaweza ukapiga risasi na sauti isitoke kama imewekewa kiwambo cha kuzuia
sauti….’akaniambia.
‘Hilo najua, kipindi napendana namume wangu, alishanionyesha
hilo tukiwinda, na vyote hivyo vipo, usiwe na sahaka.Cha muhimu ni kutafiti
lini atafika, aua anafika muda gani…’nikamwambia…’nikamwambia.
‘Hilo nitalifanyia kazi,mimi namtumia huyo mwanadada
ingawaje simwamini, lakini kila ninachohitaji kuhusu Kimwana,
ananitafutia,….hampeni Kimwana kama nini, yeye mwenyewe anadai kwamacho ya
wengi,watu wanahisi kuwa yeye ni rafiki wa Kimwana, lakini kiundani ya nafsi
yake, Kimwana ni adui yake mkubwa….na yeye alikuwa akitafuta mwanya wa
kummaliza.
‘Basi kumbe tupo wengi, lakini jambo kamahili tukiwa wengi
zaidi ni hatari…’nikasema,na kumwangalia mwenzangu ambaye muda mwingi
alionekana kuwa na mawazo nikasema tena…
‘Mimi kwa sasa sijali,…iwavyo na iwe, huyu mtu hafai,
atatumalizia waume zetu….’nikamwambia.
‘Arubaini zake zimeshafika, na kwa vile ana maadui wengi,
itakuwa vigumu sana kwa sisi kujulikana…’akaniambia, na niligundua kuwa
mwenzangu ana mawazo ya nini kitatokea baada ya hapo, kinyume na mimi ambaye
nilikuwa na dhamira moja tu ya kumuondoa huyu binti aitwaye Kimwana….
Basi tulipokutana kesho yake, mwenzangu akanipa taarifa kuwa
ameshagundua lini Kimwana atakuwepo kwenye jingo, …na mimi nitayarishe hiyo
silaha, bila ya mume wangu kujua,….tukapanga tukutane wapi, hatukutaak
kuonekana pamoja….
Kumbe Kimwana alikuwa akifika hapo kamakujificha, na huwa
haki kwa muda, kwani wengi hawajui kuwa
hiyo ni nyumba yake, kwa kipindi hicho , polisi walikuwa wametulia kumtafuta
polisi…
Mwenzangu alikuwa mwepesi sana kuzipata habari za Kimwana na
kila nikimuuliza anasema kuwa kutoka kwa huyo mwanadada ambaye anajua karibu
kila kitu, kumuhusu Kimwana.….
‘Mwanadada gani huyo, …ni askari, au anafanya kazi
gani….?’nikaona nimuulize.
‘Mwanadada huyo ni nesi….’akaniambia, na kuendelea kunieelzea
kuwa, huyo mwanadada, pamoja na kazi yake ya unesi, lakini pia anajua mambo yaa
upepelezi…’akaniambia hivyo na mimi nikashituka kidogo, maana kuna mtu
ninayemfahamu ana sifa hizo.
Nikawa namdadisi , … ili nimjue huyo mwanadada
anayemuongelea, hata ikibidi aniambie jina la huyo mwanadada. Lakini
hakukubali, alichoniambia ni kuwa,kwa hivi sasa ni bora nisimjue kabisa, kwani
yeye alishaahidi kwa huyo mwanadada kuwa hatamuambia yoyote kuhusu yeye, kwani
hataki kujulikana, kwani ana ajira yake inayojulikana, hata hivyo kwa vile
anatusaidia basi haina haja ya kumjua zaidi ya hapo….’alipofika hapo akatulia
kwa muda, kama vile kamaliza au anasubiri swali.
‘Habu nikuulize….’muheshimiwa hakimu akasema huku
akimwangalai wakili mwanadada, kuataak kujua kama ana swali lolote kabla
hajauliza swali lake, na alipomuona huyu wakili yupo kimiya,akasema
‘Huyo rafiki yako ni nani,maana umeelezea kwa kirefu na nilitarajia
labda utamtaja jina lake,lakini hujafanya hivyo , huyo rafiki yako ni nani,na
je yupo humu ndani….?’akauliza hakimu.
‘Ndio yupo humu ndani ni …ni, huyo hapo,…’akamuonyeshea yule
dada rafiki yake, na wote wakageuka kumwangalia yule mwanadada, na yule dada
alitabasamu bila wasiwasi, na cha ajabu,… akageuka kuniangalia mimi akiwa na
tabasamu mdomoni, ...’
Nilimwangalia na macho yetu yakagongana, na kwaharaka
nikaangalia chini, huku nikiwa siamini
fikira zangu, …kuna kitu kinanijia , lakini nashindwa kukihakiki, na hata
hivyo,…kutokana na hayo maelezo tuliyoyasikia kutoka kwa mke wa wakili, ….huyu
ni mmoja wa wauwaji,….sikudhania kuwa binti mzuri kama huyo anaweza kuwa
muuaji, hapana, sio yeye huyo anayekuja kwenye akili yangu….nikajikuta nikisema
kwa sauti
‘Hapana haiwezekani, sio yeye…’na wote wakageuka kuniangalia
mimi.
NB. Ngoja tuishie hapa kwa leo....nikijiuliza hivi kweli mapenzi yanaweza kumfikisha mtu hadi afikie kuua...?
WAZOLA LEO: Usijiwekee
mipaka katika hisia na dhamira yako, kuwa hiki hukipendi,au hiki unakipenda, hiki
kibaya kwangu na hiki kizuri kwangu, na ya kuwa kila mtu atakuwa kama zilivyo
hisia zako….Hapana ukubali ukweli kuwa hisia hotofautiana kati ya mtu na mtu.
Na tukumbuke kuwa kila jema halikosi kasoro, na hata baya kwako, lawezakuwa likawa
jema kwa mwenzako.
Ni mimi:
emu-three
7 comments :
Na wewe m3 kwa vimwana, unachagua wazuri wazuri, ndio unawaweka hapo, kazi nzuri, iliyoenda shule, sina zaidi maana sifa nyingi unaweza ukashidwa kuweka sehemu ijayo.
Hongera kaka, upo juu
Hongera kaka, upo juu
Hongera kaka, upo juu
hongera mzee
Pamoja sana Ambiere!Bado niko nyuma kidogo sijafikia hii ya hitimisho lakini!
Wadau wasio na jina tupo pamoja ,na Ambiere,nashukuruni sana usijali ww ni ndugu yangu,....
Na wadau wengine wote, hata wale wa kimiya-kimiya kidogo kidogo tutafika. Tupo pamoja!
Post a Comment