‘Haya hebu tuambie jinsi ulivyomuua Kimwana…?’ swali hili
lilimpandisha shinikizo la damu, bwana Sokoti,
akatoa macho ya uwoga, na
alipoanza kuongea akaongea kwa kuhamaki,;
‘Mimi sijamuua Kimwana, muheshimiwa,….’akasema na kutulia.
‘Kama wewe ndiye mratibu wa mambo yote haya, utakataaje kuwa
hukumuua Kimwana…haya tuambia ni nani alimuaa kimwana, au uliratibuje mpamgo
wako huo wakumuua Kimwana…’akasema mkuu.
‘Hebu tueleze mahusianoa yako na Kimwana’ akasema wakili
mwanadada, alipoona mkuu anakimbilia hitimisho mapema. Sokoti akamwangalia mkuu
kwa uso uliotahayari, na alipoona mkuu kamkazia macho akageuka kumwamgalia
hakimu, na hakimu naye alikuwa kamkazia macho, akainama chini .
‘Sokoti hapa tunachohitaji ni ukweli, sio kwamba hatujui huo
ukweli, tunaujua sana, ila tunahitaji uaminifu wenu,…nani mkweli juu ya haya, ukisema
uwongo, utajichingea mwenyewe, semaukweli ili mwiso wa siku upate mashama, na
msema kweli ni mpenzi wa mungu….’akasema wakili mwanadada.
Sokoti akamwangali muheshimiwa hakimu, namuheshimiwa hakimu
akaonyesha uso wa kutabasamu, hapo akaingiwa na ujasiri na kuanza kuongea.
‘Kimwana nilimjua toka kwa rafiki yake ambaye alikuwa ni
dereva wake na mlinzi wake,huyu jamaa alikuwa rafiki yangu wa siku nyingi, na
mipango yake mingi alikuwa akiniambi mimi kabla hata ya haya yote, na mimi kama
rafiki yake, nampa ushauri wa hapa na pale, akifanikiwa haachi kunipa ahsante
yangu. Na hata walivyopanga mipango yao na Kimwana kuwa Kimwana awe anakutana
na matajiri wenye wake zao, na huyo jamaa amtokee na kudai kuwa ni mume wa
Kimwana, nilikuwa najua.
Ilipokuja hii shughuli mpya, ikabidi niongee na huyu dereva,
kuwa atakuwa mtu muhimu sana katika kundi, ila kwanza nilimkanya asimuambie
Kimwana lolote, lakini najua kwa vile walikuwa wapenzi atakuwa alimwambia.
Niliona asimwambia ili Kimwana ahudhurie hilo darasa la mke
wa mkuu, na ionekane kabisa kuwa mimi sijuani na Kimwana, na Kimwana asijua
kabisa kuwa najuana na mke wa wakili mkuu, na hilo lilifanikiwa, na mipango
yangu ikawa inakwenda vyema.
Mimi pamoja na mengine niliwahi kupitia mafunzo ya
upelelezi, lakini nilihitaji mtu mwingine,ila wakati mwingine nilikuwa
nikifanya hiyokazi,nilikuwa silali, nilikuwa na simu yangu ambayo niliitumia
sana, na hata nilipopata hiyo mitambo, nikawa sibanduki ofisini. Mimi nacheza
na simu na mitambo yangu inanisadia.Mitambo hiyo na simu ilikuwa kila kitu
kwangu…..
Ikafika muda tukapanga kuwa Kimwana aoane na mtoto wa
Msomali, lengo letu lilikuwa ni nyumba, kwani nyumba yake ilikuwa sehemu nzuri,
tulikuwa tunaihitaji hiyo sehemu kwa ajili ya mambo yetu, kwahiyo mipango
ikapangwa, na kwa vile Kimwana alikuwa akimjua mke wa Msomali, na hata Msomali
mwenyewe mambo hayakuwa magumu.
Urafiki kati mke wa Msomali ulikuwepo toka huko kijijini,
alichofanya Kimwana ni kujua undani zaidi wa Msomali, hasa kama kweli
wanaivana, na ukiongezea na shule aliyopata toka kwa mke wa wakiili mkuu na
wakufunzi wetu wengine, tukafanikiwa kirahisi.
Msomali akamuacha mkewe na kumuoa kimwana, hiyo ilikuwandoa
ya geresha,kwetu sisi, ilitakiwwa iwe hivyo ili tufanikiwe mambo ya nyumba.
Mwanzoni tulikuwa hatujui kuwa nyumba hiyo ni ya mkopo, na yakuwa Msomali
hajalipa deni la nyumba, kama tungelijua hilo tungelitumia njia nyingine.
Kutokana na udhaifu wa ndoa ya Msomali na mkewe , tukafanikiwa
kumuondoa huyo mke, na Msomali akajua kapata mke anayejua mapenzi, kumbe
ilikuwa kanyaboya. Na baadaye tukagundua kuwa Msomali ni mwepesi kumtumia kwa
mambo yetu mengine, tukamuhadaa, na akawa chambo chetu.
Kitu kingine kilichofanya tumuandame sana Msomali, ni ujio
wa mtu mwigine muhimu sana, huyo alikuja kwangu kama mteja.Kama unavyojua kuwa
mimi ni mtaalamu wa kujua nyota za watu, maswala ya ndoa, na kweli karama hiyo
ninayo,ila nilishindwa kuiendeleza kwasababu
ya tamaa ya pesa.
‘Huyu mtu mwingine muhimu ni nani?’ akaulizwa.
‘Ni huyu…’akasema na kumuonyeshea Yule dada aliyejulikana
kama rafiki ya mke wa wakili. Hapo nikamtupia jicho kuona kama kuna mabadiliko
yoyote usoni, lakini hakuonekana kujali, ilikuwa kama hayupo, alikuwa
anasikiliza tu, na tabasamu kwa mbali hasa pale anaponiangalia mimi.
‘Umuhimu wake ni ni nini? Akaulizwa.
‘Nilijua kwamba ana sifa zile zile alizo nazo mke wa
wakili,yaani yeye ni dakitari na anajua sana maswala hayo ya mahusiano na ni
mwalimu mnzuri, na huyu nilikuja kumuomba awe anakuja kutoa darasa kipindi mke
wa wakili akiwa hayupo, na hata mke wa wakili alipoondoka, yeye akashika nafasi
yake kama mwalimu wa wanandoa.
‘Hili lilifanyika kisiri, hata mke wa wakili alikuwa hajui….nilijua
hivyo,sikujua kuwa hawa watu ni marafiki…’akamwangalia mke wa wakili na huyo
rafiki yake.
Mimi na Kimwana tukaanza kusigishana, maana mafahali wawili
hawakai zizi moja, Kimwana alikuwa natabia yakupenda pesa, tena pesa nyingi, na
tatizo lake hatosheki, na akizishika mkononi ni mchoyo, hatimizi yale masharti
kuwa pesa zote ziwekwe kwenye kundi na baadaye ndipo zigawiwe kutokana na
makubaliano,tabia ambayo hata mimi, licha ya kujihami, nilikuwa nayo.
Yeye alisema ndiye anayefanya kazi nyingi sana, kwahiyo pesa
yote ikae kwakwe, na oia haniamini mimi, hapo tukaanza mgongano, na hata kutishiana
amani. Ikafika hatua sasa tumeshaipata nyumba ya Msomali, yeye akadai kuwa ni ya
kwake,kama mke halali wa Msomali, na pia yeye ndiye aliyefanya mpango na watu
wa mkopo, akalipa salio dogo, na nyumba ikawa yake.
Ni kweli hati na kila kitu kilikuwa kwa jina lake, alkini
hilo tulishpanga toka awali kuwa ni mali ya kundi, hata kama mtu atakuwa kapata
tenda ya jina lake, lakini mwisho wa siku ni mali ya kundi, hilo akalikataa na
kuihodhi nyumba.
Matatizo yakaanza kutokea, kwani baadhi ya watu tuliokuwa
tukiwadai oesa kwa njia hiyo ya `blackmail’ wengine walipata na maafa…mishituko,na
kundi kama shule ikaanza kunyoshewa kidole, na muda huo mke wa wakili
keshajitoa, ina maana muda wowote mimi ningelijulikana kuwa nipo nyuma ya hilo
kundi, ikabidi tubadili baadhi ya mambo ili kujificha…
Nikakutana na watu wangu muhimu, tukaona tuwaondoe hawa
wanawake kiaina, wengine tuliwasahauri warudi kijijini tuwaanzishie miradi, na
wengine tuliwapatia shule nje ya nchi, ili tu kuondoa ushahidi,lakini Kimwana
akagoma kwasaabbu yeye alijiona ndiye mwenye kundi.
Wale waliogoma kama Kimwana tukakubaliana tutafute njia ya vitisho
na wakigoma, ni bora kuwamaliza….’hapo akatulia
‘Kuwamaliza kwa vipi?’ akaulizwa.
‘Hata ikibidi kuwaua,..lakini mwanzoni tulitumia njia ya
vitisho au kuwagongansiha na wale waliowahi kukutana nao tukachukua picha za
video, ili watu hawo watufanyie hiyo kazi ya kuwamaliza, laikini sio kuwapeleka
mahakani, hilo yulikuwa makini nalo sana, nakishindikana tutumie njia ya
kuwamaliza hata kwa kuua….’akasema.
‘Mlifanya hivyo?’akaulizwa.
‘Hayo yalikuwa mawazo tu ya awali, hatukufikia hatua ya
kusema tumuue mtu fulani mwanzoni, kwasababu aliyegoma kuondoka ni Kimwana peke
yake, wengine tulifanikiwa kuwaondoa hapa mjini. Kimwana akawani tatizo, na
tuligundua kuwa huyu atatufanya tugundulike mapema kwa ukaidi wake, kwani
alifikia hatua ya kututishia kuwa atatulipua kwenye usalama.
Nikajadiliana na mkuu wetu wa upelelezi, yeye akasema hiyo
kazi tumuachie yeye kwasababu huyo Kimwana ni mmoja wa maadui zake. Siku hiyo
mimi nilishangaa kwa maneno hayo maana Kimwana na huyu mkuu wetu wa upelelezi
ni marafiki wakubwa, kumbe kiundani ni maadui, na sababu kubwa niliyohisi ni
kugombea wanaume matajiri.
Akamgeukai Yule mwanadada ambaye alikuwa kakaa lakini
kaangalia pembeni, alikuwa kakasirika kwa vile hakuruhusiwa kuondoka, kwahasira
akakaa kwenye kiti huku akiwa kageuka kuangalia mbali na wenzake kama vila
hayupo, na aliposikia maneno hayo, akageuka nakusema.
‘Mimi sikuwa nagombea wanaume matajiri, yeye alinizika pesa
zangu, na pia alikuwa akitembea na wakili mkuu,…wakili mkuu alilikuwa mpenzi
wangu wa siku nyingi, …’akasema na alipomwangali mke wa wakili akashituka ka
kunyamaza.
‘Katika kazi yetu tukagundua kuwa kuna watu wanakuja kwa kasi
na wanaweza wakafichua hili kundi,tukajadilian kuwa watu kama hawo tuwaondoe kwa
haraka, …wa kwanza alikuwa ni Msomali,ambaye mwanzoni tilimdharau,kumbe alikuwa
simba mwenda pole, alikaribia kinamna kutugundua,....siku moja akribu aninase, akiwa na simu yake, akiasiliana na mtu fulani. Huyu tukaona kuwa dawa yake
ni ndogo, ni kuhakikisha kuwa kesi zinamuandama, halafu hapati kazi, na akifika
jela huko kuna watu wetu watammaliza,..
‘Lakini jamaa huyu alikuwa na roho ya paka, maana kila tukijaribu
hili tulikuta anaokoka, na baadaye tukagundua kuwa anaye msaidizi wa karibu ,
ambaye ni wakili mwanadada, huyu naye akawa ni pingamizi kwetu, na tulikuja
kugundua kuwa huyu wakili mwanadada ni tishio kwetu zaidi ya hata Msomali,
tukaona dawa ya huyu mtu ni kummaliza, maana hana mume, na kila mtego wa
kumnasa kama wengine tuliojaribu kwake ulishindikana, tukaona huyu atatuwekea
kiwingu,….tukaandaa mtego wa kumuua.
Siku hiyo tukagundua kuwa anakwenda kumuona Kimwana, mtego
ukatayarishwa, ili ajue kuwa Kimwana yupo huko, na kwa vile alikuwa akimtafuta
Kimwana, tukamwekea mtego , na Kimwana mwenyewe alikuwa hajuihilo, na hata
dereva wake alikuwa hajui hilo, ilikuwa ni siri kati yangu mimi na baadhi ya
watu wangu na mpelelezi wetu .
Mpelelezi wetu ni huyu nesi, na uzuri wake alikuwa keshamdhibiti
wakili mkuu,…na pia anamjua vyema mke wa wakili mkuu, na pia alikuwa akimjua
vyema rafiki wawakili mkuu,….huyu rafiki wa wakili mkuu, kama nilivyosema
alikuwa mtu muhimu kwetu lakini alikuwa hajui….kuwa nay eye uzaifu wake
ulitusaidia mambo fulani. Na mpelelezi
wetu mkuu, aakajenga urafiki naye, na akaahidi kumsaidia mambo yake aliyokuwa
akiyahitaji….
‘Hayo tutayasikia toka kwake yeye mwenyewe, wewe tuelezee
ilikuwaje wew na Kimwana baadaye.
‘Basi mtego ukategwa na kweli wakili mwanadada kama tulivyotarajia
akaenda kumuona Kimwana,mimi nikawasiliana na mpelelezi wangu, yeye akasema
hiyo kazi nimuachie yeye…kwasababu mkuu wa upepelezi anaweza akafanikisha mambo
fulani,hakuniambia mambo gani. Akasema mimi niwasiliane na dereva kumpa maagizo
kuwa ahakikishe kuwa wakili mwanadada hatoki humo ndani akiwa hai.
Tukalipanga hilo kitaalamu, …’akasema.
‘Kitaalamu kwa vipi?’akauliza hakimu.
NB: Muda umekwisha mwenye jembe huyooo, anaingia tukijaliwa
tutaendelea hapo tulipoishia.
WAZO LA LEO: Kusengenya
siku hizi ni fasheni, kila wakutanapo wawili, lazima haitakosa neno la kumsema
mtu Fulani, kuwa yupo hivi, ana lile ,na ubaya wake upo hivi na vile. Ni vyema
tukaacha kupoteza muda kwa kusema watu(kusengeanya), tukautumia huo muda katika
mambo ya maendeleo, kwani kuna msemo usemao kuwa watu wema hujadili mambo na
wabaya hujalidili watu..
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
hongera
Yaani leo umetuacha ferry!! pantoni ile inaishia zake, mpaka jumatatu tena panapo majaaliwa Inshaallah. Kipande hiki kimenoga sana.
Kweli Subira tukijaliwa j3,wikiendi njema, endelea kuipigia kura blog yako hii kila siku
Post a Comment