Wakati wakili mkuu akiwa anaongea mawazo yangu yalikuwa kwa huyo
mwanadada mwingine, aliyekuja na mke wa wakili, ambaye alikuwa kakaa sambamba
na mimi na kwahiyo tulikuwa
tunaangaliana. Kitu nilichogundua ni kuwa yeye alikuwa akiniangalia kile
anapogundua kuwa nimeangalia pembeni, na nikiwa namuangalia ananikwepa
tusiangaliane usoni.
Nilipata mwanya wa kumchunguza, na kuiangalai sura yake,
angalau kwa kujiiba, sikutaka agundue kuwa namchunguza, na kila hatua iliyopita
nafsi yangu ilinituma nimuangalia , na kuna kama kitu kilikuwa kikinivuta
kufanya huvyo, nimuangalai yeye, na wengine mle ndani ilikuwa kama vila hawapo.
Mara tukakutanisha macho,…tukaangaliana kwa sekunde chache,
na yeye kwa haraka akaangalia pembeni, nikamchunguza alivyo, moyoni, nikasema
`kweli huyu mwanadada ni mrembo,…ni nani mume wake au mchumba wake,kama ndivyo
alivyo, sura nzuri na upole na hapo anaoekana mwingi wa aibu kudhihirisha ile
sifa ya mke,basi inawezekana akawa mke mwema.
Nafsi yangu ikawa imeenda mbali zaidi ikijiuliza, kama kweli
nikipata muda wa kuongea naye ninaweza nikawa rafiki yake, lakini safari hii
sikutaka kufanya makosa ya kumpata mke mwema. Nilitaka
nikipata mke,awe kweli mke aliyekamilika, ….na safari hii,sidanganyiki…nikamwangalia
Yule mwanadada tukajikuta tunaangaliana, …mbona nafsi yangu inavutika kwa huyu mwanadada, kama vile namjua siku nyingi...nikajiuliza bila majibu.
‘Tuambie kama sio
wewe uliyemuua Kimwana atakuwa ni nani?’ swali likanigutusha katika lindi la
mawazo, nikiwa naangaliana na yule mwanadada, naye akawa kama vile kagutuka
toka katika mawao kamayangu.
‘Kwakwelii sijui maana nilipofika maeneo yale nikiwa na
lengo la kuingia na kukutana naye, nikakuta kun awatu wameshafika kabla yangu,
nikaona nimewahiwa, lakini nilijibanzakwenye jingo moja,nikiwa na maana ya
kumsubiria huyo Kimwana, nilishadhamiria kweli kumfanya lolote, …’akasema.
‘Kumfanya nini, lolote lipi, fafanua….’akauliza hakimu.
‘Kwa hasira niliyo kuwa nayo ,nilishafikia hatua ya
kumuua….’akasema.
‘Ehe endelea…’akasema Muheshimiwa hakimu.
Wakati nimejibanza pale nilisikia kitu kama chupa,
…ikivunjika, au…ni mlio wa kugonga kiyoo, lakini sio mkali sana…na nikasikia
kitu kama yowe…nikashituka, na haikupita muda, nikaona mtu akitoka kwenye
jingo, akikimbilia nje, na kuwaita walinzi ….Niliuona akiwa na wasiwasi,
nikajua kuna jambo limetokea huko ndani.
Baadaye sana, nikaona askari wakija,…
.
‘Ina maana mauaji yalishafanyika,….>’akauliza mkuu, kama vile
hakubaliana na maneno ya huyo wakiliimkuu.
‘Ndio, niliona baadaye askari wakitoka na machela wakiwa
wamebeba mtu, sikujua ni nani kwa wakati ule. Nilipoona hiyo ,hali nikaona
niondoke hapoo haraka,kwani hata hivyo nilishachelewa sana , na sikutarajia kuchelewa
hivyo, na kuchelewa kwangu kungelimuweka huyu mwanadada kwenye matatizo.
‘Nikarudi hopsitalini na huyu mwanadada akiniwekea zile
dripu na kuanadika muda amba unglinilinda kwa lolote likitokea…
‘Sasa kwanini bado uwe na wasiwasi wa kuandika muda…wakati
umsema hujamuua wewe, ulikuwa ukijihami nini tena?’ akauliza mkuu.
‘Huwezi jua, kwa hali kama hiyo, lolote linaweza kutokea,
niliamua kuchukua tahadahari zote, hata
hivyo kwa mudaule hatukuwa tunajau lolote…’akasema.
‘Mlijua muda gani kuwa Kimwana kauwawa?’ akauliza hakimu?
‘Nilipofika hapo hospitalini, huyu mwanadada akaondoka, na
baadaye akarudi ,akiwa na uso wa wasi wasi, akaniangalia akiwa na hasira,
nikamuuliza kwanini ananikasirikia, akasema hakujua kuwa mimi ni muuaji.
‘Nimemuua nani?’ nikamuuliza.
‘Umemuua Kimwana….’akasema.
‘Eti nini…kumbe, …nilijua tu…’nikasema.
‘Ina maana ulivyoondoka mkiwa mumepanga na huyo
mwanadada,kuwauondoke,haikuwa mumepanga kuwa unakwenda kufanya mauaji?’
akauliza Mkuu.
‘Hapana, sikumwambia lengo langu moja kwa moja, ilanahisi
alikuwa anajua…nilihocmuambia ni kuwa nakwenda kufanya uchunguzi, ambao utaweza
kuwagundua wabaya wangu, na kukomesha hayo mambo, sikumweleza wazi lango langu,
maana kama ningelimuelezea, angelinikatalia….’akasema.
‘Yeye alisemaje, au alikushauri nini?’ akauliza wakili
mwanadada, ambaye muda mwingi alikuwa katulia.
‘Alisema ….’akatulia na kumwangalia mwanadada ambaye
alionekana hana raha, akawaahamuangalii wakili mkuu, na wakaili mkuu akasema.
‘Aliniambia `Najua unakwenda kwa Malaya wangu….’akasema na
kugeuka kumwangalia mkewe ambaye alikuwa anamwangalia kwa makini.
‘Hebu nikuulize swali , ulipokwena huko ulikuwa na silaha
yoyote?’ akauliza wakili mwanadada.
‘Ndio , lakini sikutoka nayo hapo hospitalini,....njia
ya kwena huko nilipokwenda, ilikuwa lazima nipitie nyumbani kwangu, nilifika nyumbani
kwangu na kuchukua silaha…na pikipiki ....’akasema.
‘Silaha gani ulichukua....?’ akauliza mkuu.
‘Nilichukua bastola….’akasema.
‘Kwani nyumbani kwako kulikuwa na silaha nyingine, ambayo
ungeliweza kuichukua,na kwanini ukachukua bastola,..?’ akauliza mkuu, ambaye
anajua kuwa huyo jamaa ana miliki silaha zaidi ya moja.
‘Ndio nina silaha nyingine nyumbani na zote namiliki
kisheria…’akasema.
‘Silaha hizo unazitumia kwa shughuli gani?’akaulizwa.
‘Kutokana na kazi yangu, niliona nimilki silaha,hata hivyo
mimi napenda sana kuwinda, kwahiyo nina silhana kubwa,ambayo unaweza kuua
mnyama ukiwa mbali…’akasema.
‘Ni wanyama tu,…sio na binadamu..?’akauliza mkuu na wakili
mkuu akamwangaliakwa jicho lua kushangaa, lakini baadaye akasema.
‘Hpana sikuchukua kwa kazi hiyo, ….’akatulia naona hilo
swali lilimkwaza kidogo, na hakimu akamwangalia wakili mwanadada, na kusema.
‘Kwani maswali mengine kwa huyu mtu, au tusikilize mtu
mwingine?’
‘Mimi naona yeye akae kando kwanza , tumsikilize Sokoti,
kwani naye,…’akasema wakili mwanadada.
*********
Sokoti aliposikia hivyo, akawa kama kashituliwa toka usingizini...akamwangalia hakimu akiwa katoa macho ya uwoga, wasiwasi
aliokuwa nao hakuweza kuufichika, akamwanagalia tena muheshimiwa hakimu, na baadaye
akamgeukia wakili mwanadada.Wakili mwanadada akamwangalia usoni,....kwa macho yale ya uwakili,.... na Sokoti,
akajitahidi kumwangalia pia,lakini baadaye akainama chini na kusema;
‘Mimi najua wengi mnaniona kama mkosaji mkuu, kuwa ndiye
niliyesababisha haya yote, lakini naweza kupinga hilo kwa sababu nyingi tu,
kwanza sio mimi niliyepanga kuanzisha kitu kama hicho, …’akatulia.
‘Nani alipanga kuanzisha kitu kamahicho?’ akauliza hakimu.
‘Alikuja mke wa wakili mkuu, kuniambia kuwa anataka
kumdhibiti mumewe ambaya ana uhakika kuwa anatembea nje ya ndoa,….’akasema na
kumwangalia mke wa wakili mkuu, mke wa wakili mkuu, alikuwa katulia kimiya,
nawakili mkuu mwenyewe akashikwa na mshangao, akamwangalia mkewe, na baadaye
akamwangalia huyo jamaa anayeongea.
‘Akaniambia kuwa nitafute mbinu ambazoninaweza kukusanya matendo ya mume wangu, ili apate ushahidi nakutokana na huo ushahidi ataweza kumkomesha huyo mumewe, na pia kuwakomesha hao anaotembea
nao….’akatulia.
‘Mlikuwa na maana gani kukomesha,….?’akauliza hakimu..
‘Tukiwa na ushahidi tungeliweza kufanya lolote, kwa mfano
ushidi huo, tungemtishia kuwa tutaupeleka kazini kwake, na …’akatulia.
‘Na …na nini,sema hapa ni sehemu ya kuweka kilakitu
wazi,sisi hapa ni watu ambao tutapima jemambo yaliyotokea yanaweza kuwekwa
vipi, maana mambomengine,kuyaweka hadharani inaweza isiwe vyema, ndio maana
moja wapo ya kuitana hapa..naomba mnielewe hilo,kwahiyo usiogope kuongea loloe
hapa….utalindwa,kamainabidi kuwa hivyo…’akasema hakimu.
‘Na pia tungemtishia kuwa tutaupeleka ukweni na kwa wazazi
wake..’akasema.
‘Wewe ulifanyeje , yaani hapo ni makubaliano kuwa muanzishe
kitu kama hicho, ukakubali namkaanzisha ulianzishaje,?’ akaulizwa.
‘Baadaya kupata wazo hilo,nikakumbuka mambo yangu yaliyokuwa
kichwani, na nikakumbuka kuwa nikiwa na mashineya kuchukulia mikanda ya video
ya watu wakitenda mambo yao……naweza nikapaat pesa nyingi tu…’akasema.
‘Mambo gani,nimekuambia hapaunatakiwa uweke kila kitu
hadharani…’akaambiwa.
‘Niligundua kuwa kanda zenyewe za matendo ya ngono,
zinapendwa sana, na biashara nzuri, hilo la kwanza,lakini pia tunaweza
tukazitumia kuwatishia watu kama hawa,wanaokwenda kinyume na ndoa zao, tukapata
pesa,na hilo liliwezekana, na hatukuhitaji tena kufanay biashara ya hizo kanda,…..’akasema.
‘Kwa kiingereza wanaita `blackmail’…’akatulia.
‘Fafanua hapo, nini ulichokusudia hapo, …’akaambiwa.
‘Yaani ukishaitengeneza hiyo kanda, unampeleka mlengwa, na
kumuonyesha kuwa tumgeundua siri zako na siri zako ndio hizi hapa, sasa ili
tusizifikishe kwa mkeo, au kazini kwako au kwa mkweo.Ili tusifanye hivyo
unatakiwa uinunue hiyo kanda, na hapo tunataja thamani kubwa ya hiyo kanda,…’akasema
‘Kiasi gani…?’akaulizwa.
‘Milioni kumi,tano,tunaangalia kiasi ulichonacho, …tunachoafanya
ni kujua pesa yako iliyopo benki, au kama una mradi utaoweza kuingiza pesaya
haraka…..hatutaji pesa bila kujua nini ulichonacho…’akasema.
‘Ndivyo mlivyokuwa mumepanga na mke wa wakili?’ akauliza
wakili mwanadada.
‘Hapana, yeye alitaka nitafute ushahidi nimpatie, halafu
yeye atajua nini cha kifanya, hayo mengine ya blackmail, yalikuwa yangu a kundi
langu, yeye alikuwa hajui kabisa…’akasema.
‘Hizo kanda mlizipataje, yaani mlifanyaje m[aka mkawa
mnaweza kupata hizo kanda..’akaulizwa.
‘Kazi hiyo ilipangwa kwa umakini kidogo, kwani kabla ya
kufikia hapo tuliwatayarisha wasichana, wasichana hawo ndio waliokuwa
wakitembea sana na wanaume wa watu, na hasa tuliwalenga wale wanaotembea na
hawa watu tunaowahitaji, …..’akatulia.
‘Mnaowahitaji na nani, na kundi au na wewe na mke wakili?’akaulizwa.
‘Kwanza ilikuwa ni wale ambao mke wa wakili alijua wanatemba
na mumewe, lakini sisi tulikuja kuongezea watu wetu ambao alikuwa hawajui….yeye
alitaka hawo wanaotembea na mumewe tuwapate , aoangee nao, na ili kufanikiwa
hilo tukaanzisha kitu kama shule ya kuwafunda wasichana, …’akatulia.
‘Kufunda mimi najau ni kuwatayarisha wasischana kwa ajili ya
ndoa zao , nyinyi mlikuwa hamna lengo hilo?’ akaulizwa.
‘Sisi hatukuwa na lengo hilo,ila mafunzoo ni hayo, na ssi
tulikwenda kiundani zaidi, kisayansi. Tulikuwa na wataalamu wanaojua mtu, mke
au mume yupoje, hisia zao, hulka na
mienendo yao. Hii shule iliwasaidia kuwajua wanaume, na udhaifu wao. Na
kwahiyo kama msichana anamtakamwanaume Fulani, inakuwa rahisi kwake
kumnasa..ilikuwa hivyo,nakweli tulifanikiwa…’akasema.
‘Kwa vipi mlifanikiwa…?’akaulizwa.
‘Tuligundua kuwa wanandoa wengi hawajui ndoa zao, ….utakuta
mke na mume wapo ndani ya ndoa, lakini nini ndoa, hawajui,….kuna udhaifu mwingi
ndani ya ndoa, usione watu wanatembea na kujinad kuwa wao ni mke na mume,….lakini
ukiingiakiundani kuna matatizo. Na tatizo kubwa ni jinsii gani ya kushibishana
kwenye ndoa,…sio tendo lenyewe tu, lakini ukaribu, kuwa tayari, kukubali kuwa
wao ni kitu kimoja,…wengi hawajui hilo….’akasema.
‘Kwa udhaifi huoni rahisi sis kupenyeza mambo yetu, huyo
mume tunamkamtaisha mtu anyejua hayo, …mume akikutana na mtu kama huyo anaona
kapaat asali…basi mambo yanakwenda hivyo, …cha muhimu ni kuwa kila tendo
linalotendeka sisi tuna liweka kwenye kanda zetu….’akasema.
‘Kwa vipi?’akaulizwa.
Kwanza hawa watu wetu tunaowatuma wanakuwa na saa na simu,
hivyo vyote vina vyombo vyetu, ambavyo vinatuwezesha kuwaona kweney mashine
niliyokuwa nayo sehemu ya siri, Ni mashine yenye nguvu sana, inachukua tukio na
kutengeneza mikanda, safi kabisa, napia tunaweza kubadilibaadhi ya matukio,…..’akasema.
‘Mnabadili vipi..
‘Kama huyu mtu anakuw akichwa ngumu, tunaweza kuigeuza ile
picha,ikaonyesha matendo kinyume na maumbile…au kuleta picha ya mtu mwingine
ambaye ataweza kuogopa zaidi, ….ni rahis kwa mashie hiyo..nakweli wengi
tuliwapata na bahati mbaya wengine walishindwa kuvumilia wakajikuta wakipoteza
fahamu..na hata…’akatulia.
‘Na hata kupoteza maisha, lakini sio lengo letu hilo,
hatukutaka kupoteza misha ya watu…’akajitetea.
‘Na je ina maana mke wa wakili hakuwa anajua hayo mliyokuwa
mkifanya,….?’akaulizwa.
‘Kwakweli sizani kuwa alikuwa akijua, ….labda kama alikuja
kugundua baadaye....maana baadaye alisema anavunja hilo kundi,....hakujua kuwa kuna kundi analolijua yeye na kundi langu la siri,...kwakweli hilo kundi la siri, lilikuwa na watu wangu ambao hakuwajua yeye ilikuwa siri kubwa sana,…’akasema.
‘Nani mwingine kati ya sisi humu ndani aliyekuwa akijua hayo...au ndio unaogopa kutoa siri, haa hakuna siri, tutakuja kukuamuru uwataje wote, waliokuwa kwenye hilo kundi, ila sasa nataka kujua kati ya sisi hapa ni nani yupo kwenye hilo kundi la siri ?’akaulizwa.
Sokoti akageuka nakuwaangalia mmoja mmoja kama vile alikuwa
akiwatambua kwa mara ya kwanza, na alipofika kwa Yule mwanadadaakatulia, Yule mwanadada
akakunja uso kwa hasira. Sokoti akasema;
'Mtu ambaye alikuwa anajua ni....hapa hakuna, ila....'akasita na kumwangalia huyo mwanadada tena.
'Sema ukweli maana sisi tunajau ila tunataka kusikia kweney kinywa chako, una uhakika kuwa tuliopo humu hakuna yupo kwenye hilokundi lako la siri,....?' akauliza wakili mwanadada.
'Huyu mwanadada yupo, yeye ni mmoja
wakundi letu, katika kitengo cha upepelezi….’akasema na Yule mwanadada akasema;
‘Unikome, mimi sikuwa mmoja wakundi lenu, mimi ulinirubuni
tu kwa kazi zako,....kufuatilia mambo yako, mimi naona hapa naonewa tu, kila mtu ananinyoshea kidole mimi, …kama
ni hivyo mimi naone nijiondokee,....’akasema na kuanza kuondoka.
NB. JE NINI KILIENDELEA. Tusichoke, tunamalizia, maana naona wengi sasa ni kimiya kimiya, haina shida, tutafika tu. Najua kuna makosa mengi ya kiuandishi,huenda herufi zimapandana tusameheane kwa hilo, ilimradi maana inajulikana.
WAZO LA LEO:
Tunaambiwa kuwa sifa za mnafiki ni tatu, kuwa mtu huyo akizungumza husema
uongo, pili akiahidi jambo hatekelezi,na tatu haaminiki . Swali je ni nani hana
sifa hizi…
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
kesi yenye utata lakini mwisho kila kitu kitajulikana. Tusubiri kweli na tuone itakuwaje...Wazo la leo kwa kweli kwa vile sisi ni binadamu na kila binadamu ana mapungufu basi katika hayo matatu lazima mtu atakuwa nayo sifa moja au mbili au zote tatu. Pamoja Daima.
Kiukweli kwa maelezo hayo ya wazo la leo hakuna amaye sio mnafiki, -maana utaishije, angalia simu tunazotumia uongo kila muda.
Kazini ukichelewa inabidi udanganye,iliukope inabidi udanganye.
Haya umekopa unadaiwa, hulipi kwa wakati,-maana hapo huaminiki.
Unapewa dhamana za watu unadokoa kidogo, halafu unafuta kiaina-tutaishije, nayo ndiyo maisha,kwahiyo ukiitwa mnafiki usikate.
Tupo pamoja mkuu, napenda sana mawazo yako!
Mmmhh ndugu wa mimi, Hongera sana, kweli moto huu si wakitoto.
Kazi hii kama mimi ningeiandika hata wiki na zaidi.kweli kila mtu na karama zake.Mungu azidi kukubariki sana.Ndugu wa mimi Pamoja Daima!!!!
Post a Comment