`Ndugu hakimu, hawa wote ni wahusika wakuu kwa kadhia hii
nzima ambayo ilifikia hadi watu kupoteza uhai wao na wengine sasa wapo
kitandani wameshikwa ni kiharusi. Ni jambo la kusikitisha sana kuwa kuna watu
wanabuni mambo kwa maslahi yao, bila kujali athari zake kwa wengine.
Tumeliona tulionglee hili hapa, kabla hatujasikia uamuzi
wako, kwasababu ni jambo la kijamii, na ni vyema tukawasikiliza hawa wakosaji,
ni kwanini walifikia kutenda haya waliyotenda, na tukapeana nasaha, ili mwisho
wa siku kila mmoja aone ubaya wa hilo jambo, na ajirekebishe, kuliko kumpelea
mtu jela, akasota huko na akitoka hajajifunza lolote.
Mimi katika utafiti wangu nimeona kuwa ni vyema taratibu
kama hizi zikafuata, mkosajai ajue kosa lake akiri na ajute, na apewe
nasaha,ambazo zitamsaidi kuliko kumuhukumu tu. Na pia wakosaji waanpokuwa
jela,ni vyema kukawa na shule nasaha, kwa kila mmoja kutokana na kosa lake
akalishwe chini ajieleze ni kwanini alifikia hatua hii.
Akimaliza kujieleza ,aelezwe madhara yake kwa mwenzake, na
ni nini kwa athari kwa jamii, hili lifanywena watu waliosomea mambo hayo, na
pia watu wa dini, wahusishwe kutoa mambo ya kiroho, ili yamjeneg huyu mtu, na
hata akitumikia kifungo chake ajue ni halali, na akimaliza hatarejea tena.
Angalia wengi waliofungwa, wakirudi uraiani, wanajiona kama
sio binadamu tena,hawajui hata waanzie wapi maisha, na hata wengine kuimba kuwa
ni `ni heri tena warejee jela,..’ ni maneno ya kukata tamaa,ina maana huko jela
kuliko sio chuo chamafunzo,ni sehemu ya kukomoana.
Mimi kwa mtizamo wangu tuanze kubadili mtizamo wa jela, jela
iwe sehemu ya mafunzo, wakifika wahukumiwa, kwanza tujenge imani za hawa
watu,kuwa kufanya kosa ni dhambi, hili lifanywe nawatu wa dini, pili tangalia
makosa yao, kwanini wamefikia hapo, hawa watu wa ushauri nasaha
wawepo,waangalie jinsi gani ya kumshaurii huyu mtu. Halafu kila mtu ana kipaji
chake, humo vipaji viendelezwe na kazi ziendlezwe kama kawaida.
Nimegundua jela nyingi, zinakuwa ni sehemu ya kuharibu watu
kisaikolojia, watu wanaingie humo wanafanyiana uchafu, wanazalilishana,
wanaambukizana amgonjwa, sasa hapa tunakuwa tunafanya nini. Ndugu muheshimiwa,kuna
wau wengine wamehukumumiwa hata kosa hawajafanya, ni kutokana na sababu za
kujieleza, au kutegewamakosa, hawa watu wanaumia sana,na mwisho wa siku
wanajiona hawana thamani katika hii dunia, tutakuja kujibu nini mbele ya
muumba.
Pamoja na kusema hyo, kuna jambo jingine ni vyema
tukaliangalai mapema, hasa kunapotokea jambo, kama la mauaji,au uasi wowote,
imekuwa ni destruri kukimbilia kukamata, kutesa, kuweka watu ndani, na kutoa
hukmu kutokana na vigezo vilivyoonekana, lakini hatuchunguzi haya makosa
kiundani, hili utaliona katika kesi hii,.
Labda tuanze kwa wahusika kujieleza , na tukianzia na
mkosaji , ambaye wote tulimnyoshea kidole yeye, na kutokana na akzi yake,
hakustahili kufikia huko,lakini kwa udhaifu wa kibinadamua akjikuta kifanya hayo
aliyoyafanya, na hili katika utafiti wangu niligndua kuwa limetokana na maswal
ya kindoa, naona tisirejee naomba kwa nafasi yako muheshimiwa tumruhusu mkuu
wetu wajieleze, kwani yeye ndiye anaonekana ndiye mkosaji, je kweli yeye ndiye
mkosaji…
Hakimu akatulia kwanza kwa muda, akafikiri, na baadaye
akauliza;
‘Kwahiyo tunakubaliana kuwa hapa tunasikiliza maelezo ya
mwanzo tu, ambayo baadaye yatatusaidia katika kesi hii, mimi sikupendelea hii
hali,maana ipo kinyume na utaratibu, lakini kutokana na hali ya kesi hii
ilivyo, naona iwe hivyo, ili tusisumbuane tena, na kesi zenu zisizo na ushahidi
wa kutosha…’akasemanakutulia.
‘Kama mnavyojua utaratibu, haya yote yalitakiwa kusikilizwa
mahakamani, hapa inabidi tufanye kama utangulizi wa kujua kuwa kesi ya kujibu
ipo kwa hawa watuhumiwa aua la,..ina maana tunafanya kama mashauri nje a
mhakama, …..sawa maana kwa mtizamo huo alioelezea wakili mwanadada, naona
inaweza ikasaidiahusuani hii kesi ambayo naona inakuwa kama mchezo wakuigiza,
haya wakili wetu mkuu,tuambie, kwanini ulifikia huko ulikofikia.
Wakili mkuu ambaye muda mwingi alikuwa kainamisha kichwa
chini, …..alinua kichwa chake na kuwatizama watu waliopo mle ndani, leo alikuwa
kabadilika,alikuwa, kabadilika na kuonekana Yule wakili anyejulikana,
mtanashati na nguo zake safi kama wakili,
akageuka na kuangalia wote waliohudhuria humo ndani, na wa mwisho kumwangalia
alikuwa mke wake,pale akatulia kidogo, akayapepesa macho, halafu akasema;
‘Kabla ya yote, naomba kwanza nimuombe radhi mke wangu,kuwa
nimemkosea kiasi kikubwa sana, kama hatanisamehe yeye bado hakijafanyika kitu,
na mimi nitakuwa ni mtu wakuangamia tu, ….' akasimama na kwenda kupiga magoti mbele ya mkewe. Na yule mwanadada akakunja uso kwa hasira alipoona wakili mkuu akifanya lile tendo, akageukia dirishani asiwaangalia.
'Mke wangu.mimi nimekuwa mkosaji wa ndoa yangu
mwenyewe,kwasababu ya tamaa zangu za kimwili, …nakuomba unisamehe mke mke, nisamehe, kwa yote, najua umeumia sana
kwa haya yaliyotokea, hata kama nitatoa sababu nyingi zilizonisukuma kufanya
hivyo haitasaidia kitu,…’akamwangalia mke wake kwa macho yaliyogubikwa na machozi.
Mke wake, alimwangalia kwa muda kwa macho yaliyojaa hasira, akasema ;
'Eti nini....nikisamehe wewe...ehe, ehe....'ondoka mbele yangu akaangalia kwa mbele huku akijifanya hamuoni.
Ule moyo uliokuwa umejaa
chuki, hasira na kusalitiwa katika ndoa ukawa unamcheza akilini, alitamanii kutapika maneno
mabaya, lakini akasita, akamwangalia Yule mwanaume na kauli aliyotoa, akageukia
nyuma, na huku akikumbuka yale aliyokuwa kadhamiria moyoni.
Alipoitwa hapo, yeye alikuja na dhamira moja tu, kuwa ndoa haina haja
kwake,alishaona bora aiombe talaka yake, ajue ataishije mwenyewe,hatua hiyo
ilifika hapo pale alipoona ule mkanda wa video uliokuwa kwenye chumba ambacho
mume wake huwa anaweka kumbukumbu zake za siri.Na licha ya kujaraibu kuongea naye, ili ajue nini kinaendelea mume wake akawa hakubali.
Yeye kuwa hana tabia ya kuingi
ingia humo,hakuwa akipenda kuingilia maswala ya mume wake. Lakini siku moja,
Yule binti anayeishi naye alikuja mbele yake akamwambia ;
‘Mama, kule ofisi kwa baba kuna mkanda ambao nahisi una
jambo…’akasema.
‘Jambo gani,na umejuaje hayo,…wewe nilishakukanya kuwa huko
ofisni kwa baba yako hakutakiwi kuingi- ingia, unakumbuka alivyokuwa akisema
kila siku….huo mkandaumejuaje kuwa una jambo….?’akamuuliza kwa hamaki .
‘Mama…nilimuona baba akiuangalia, …nilikwenda humo kwasababu
alinituma sigara….na bahati wakati naingia sikupga hdoi nikaona anauangalia,
nikarudi nyuma haraka, na nikapiga hodi, akazima …nimekuamua kukuambia,
kwasababu, nilitaka kukusaidia wewe, nakushauri sana ukauchukue huo mkanda uone
kilichomo…’akamshauri mama yake wa
kufikia, na kweli mke huyu akavutika na kwenda kuuchukua huo mkanda wa CD, na alichoona
humo, kilimvunja nguvu, hakuamini kuwa mume wake alifikia hatua
hiyo,….alishindwa kuvumilia na nguvu zikamwishia na kudondoka chini.
Wakatii huo huyo binti alikuwa nje,akiosha vyombo, akahitaji
sabuni, akaingia ndani, akamuita mama yake, lakini kulikua kimiya akaona
amfuate huko chumbani kwake, akashituka kumuona yupo chini, kazimia, akahaha na
kuanza kuita;
‘Mama…mama….mungu wangu….’yule binti akawa analia hakujua ni
nini kimefanya iwe hivyo kwa ule, na akili zilipotulia akakumbuk kuwa huenda ni
kwasababau ya ule mkanda aliomshauri auchukua, na wakati ule ulikuwa umefika
mwisho, kwahiyo Yule bintio hakuona nini alichokuwa akiangalai huyo mama yake…,
akaenda pale kwenye `DVD player' na kuangalia, kweli akauona mkanda, akautoa na kuuficha.
Baba mtu akaja kwani ilibidi huyo binti ampigie simu baba
yake huyo wa kufikia, na alipokuja wakamuwahisha hospitalini na haikuchukua
muda hali yake ikawa njema. Na hata alipoulizwa tatizo ni nini,hakusema kitu,
alichoweza kufanya ni kumwangalia mume wake kwa jicho la chuki.Mume wake hakujua
kuwa kuna nini kinaendelea na kwa vile walishakuwa hawaivani, akaona ni kawaida
tu .
Na huyu mke hakukubali akaanza kulifuatili hilo swala
kwa karibu sana licha ya kutoweka kwa ule mkanda ambao alitaka uwe kama ushahidi. Na alichunguza sana bila kujua nani kafanya vile, akili yake ikamshuku Sokoti kuwa huenda ndiye alitengeneza hayo, kinyume na makubaliano yao. Akamuuliza Sokoti ambaye alipinga kuwa hakupanga yale, yeye hata kama angefnay hivyo, kwanza angemuonyesha yeye.
'Mimi nilishafnya kama tulivyopanga, ....huyo atakuwa mtu mwingine...'akajitetea vikali…..na hapo akaona kuwa hilo
alilokuwa kadhamiria huenda likasababisha mambo mabaya, ndipo wakati ule akamwambia Sokoti
kuwa huo mpango waliokuwa wamepanga uvunjike.
Tangu siku ile chuki ikawa imemtanda akilini, na kila anapowaza
ile taswira ya ile ule mkanda na yale matendo aliyoyaona kwenye ile Cd’s, yakawa yanamuandama akilini, na mbaya zaidi mume wake akawa analewa kupita kiasi, akimuuliza anakuwa mkali,.....akaona lazima afanye jambo, akaanza kumuandama Kimwana, amabye naye likuwa akimjibu kijeuri kila alipomuuliza. Ndipo akaweka nadhiri, akasema;
‘Lazima nitafute mbinu za kummaliza huyu mwanamke,halafu tunaachana na huyu mwanaume, naomba talaka yangu, na kurudi kwetu,sina haja ya mume…..sina haja tena na huyu mtu,….lakini lazima nimmalize huyu
mwanamke…..’akajikuta akisema kila mara.
Akageuka kumwangalia huyu mwanaume akiwa kapiga magoti mbele yake, akiomba msamaha huku akitoa
machozi, …akamwangalia kwa muda,…..nasijui kwanini…moyo wa huruma ukamtanda ,
na akajiskia vibaya kwa ilechuki
aliyokuwa nayo, akajikuta akilengwa lengwa na machozi huku akiyakumbuka ya
nyuma, …lakini akaona haina haja, yaliyopita ni ndwele , kinachotakiwa ni
kuganga yajayo, ingawaje hajui hatima ya yote, lakini ni vyema akakiri kuwa
keshamsamehe, akasema;
‘Mimi nimeshakusamehe leo na kesho ahera, lakini …’akataka kusema jambo,nahakimu akaingilia kati
na kusema;
‘Mambo mengine utakuja kuongea zamu yako ikifika, cha muhimu
hapa ni wewe, je umeshamsamehe kwanza, , ….’akasema muheshimiwa hakimu.
‘Mimi nimeshamamehe, ila tu ninachohitaji…...’kabla
hajaongea wakili mwanadada akamtuliza, akijua nini anataka kusema.
‘Wewe tulia tu kwanza, usiwe na papara,…..msikilize
muheshimiwa hakimu ….’
‘Endela kuongea wakili mkuu, mtuhumiwa…maana wewe hapa ndiye
mtuhumiwa mkuu, tunataka tulione hilo, kuwa je unastahili kutuhumiwa,…au la…su
sio?’ akamgeukiwa wakili mwanadada.
Wakili mwanadada akatingisha kichwa kukubali, hakusema neno,
na kumgeukiwa wakili mkuu, ambaye aliaanza kuongea kwasauti ya unyonge;
‘Mimi kutokana na tamaa zangu nilijikuta nikiwa na mahusiano
ya nje ya ndoa,hili kwangu nililiona kama ni sehemu ya sifa ya mwanaume, licha
ya elimu yangu, ….nilikuwa na nyumba ndogo, niliona kama vilekupata chakula
tofauti na kile nilichokizoea, hasa ninapofika kwa mke wangu akasema kuwa
kachoka au hajisikii, basi hapo nilipata kisingizio. Ni kweli mke wangu alikuwa
anachoka kutokana na kazi zao, lakini hilo sikulielewa.
‘Wenzetu wajanja wakaligundua hilo wakatumia uzaifu wangu,
wakatutegea wasichana,na kutuchukua picha mbaya, ambazo walinitishia nazo kuwa
nisipotekeleza matakwa yao watanizalilisha,kwakweli nilipoona zile kanda za
video niliogopa sana, nikijua kabisa zikifika kwa bosi wangu, muajiri wangu,
kazi sina, na pia nitazalilika hasa kwa mke wangu na jamii kwa ujumla….
Mtu pekee niliyemuamini tangu awali ni huyu mwandada sijui kwanini. Kwa
ufupi yeye alikuwa ndiye mpenzi wangu wa awali kabla sijamuoa mke wangu...na ana udugu na mke wangu. ....Cha ajabu ni kuwa yeye nimekuwa nikumwamini sana kuliko hata mke wangu,...sijui
kwanini, maana kila nikiwa nimetatika na jambo, huwa nakwenda kwakwe kupata
ushauri, na yeye amekuwa mtu wangu wa karibu,
kuliko hata mke wangu,maana mke wangu muda mwingi yupo kazini….na maswala kama
haya nisingeliweza kwenda kumuomba yeye ushauri…ningesemaje…
Nilipopatwa na haya matatizo, sikuwa na mtu mwingine wa
kumwamini,mwanzoni nilitulia sikumweleza yoyote, nikajaribu kulimaliza kimiya
kimiya,lakini hawa watu walipozidi kunifuta tena, ndipo maji yakanifika
shingoni, sikuwa na pesa walizohitaji, nikawa kama nimechanganyikiwa na
kutumbukia kwenye kunya pombe kupita kiasi, na hali ilivyokuwa huyu mwanadada
akanigundua, na baada ya kunishawishi sana ni kamwambia hali ilivyo.
‘Hivi kweli wewe unamwamini mkeo?’ akaniuliza.
‘Kwanini unasema hivyo,?’ nikamuuliza.
‘Mimi nahisi kuwa huenda ni mkeo anakufanyia hivyo,
unakumbuka awali nilikuambia kuwa mkeo anakutana na jamaa mmoja,ambaye wengi
wanamtambua kama mtaalamu wa maswala ya mapenzi…’akaniambia.
‘Sasa hayo yanahusiana vipi na hizi picha chafu?’
nikamuuliza.
‘Anaweza akawa kashauriwa hivyo….yule mwanaume simwamini,
…na nilishakuambia kuwa mkeo hakufai…wewe hunisikii,…angalia sasa mwaka wa
ngapi hamna watoto…umeniacha mimi, sasa unaona….’akaniambia huyu mwanadada, na Yule
mwanadada akamwanagalia kwa mshangao,nafikirihakutarajia hayo.
‘Basi naomba ujaribu kunifuatulia hilo,kama ni yeye
anafungamana na haya mambo ,itakuwa ndio mwisho wake wakuishi na mimi…na ….aah,
hayo tuyaache kwanza…’nikamwambia.
‘Alifutailia lakini hakuona ukweli wa hilo, ni wakati huo
hawa jamaa wakazidi kunisakama, na chaajabu kila ninachopanga, wanakijua, ….na
mtu pekee aliyekuwa akiyajua hayo ninayopanga ni huyu mwanadada, ….nilijaribu
kumbana kama anaweza kuwa ndiye anayetoa taarifa zangu, lakini niligundua kuwa
sio yeye, nikahisi kuwa kuna jambo jingine…
Niliamua kufanya mambo yangu menginebilakumuhusisha, lakini
kila nililofanya bado wakawa wanajua na kutoa vitisho vya kila namna,hapo sasa
mawazo msongo na hali ilivyokuwa ikanifanya nipatwe na huo mshituko,
uliosababisha hali yangu kuwa tete…
‘Nilipoona mambo yanazidi kuwa mabaya, nikanona nitumie njia
ambayo ni ya hatari,niliona ni bora kuwamaliza hawa watu mmojabaadaya mwingine,
nilijaribu kutafuta ni nani yupo nyuma ya haya yote, ikawa vigumu, basi nikaona
bora nianze na hawa akina dada ambao walishiriki na mimi hadi mikanda hiyo
mibaya ikatolewa, maana wao watakuwa wanajua, licha ya kuwa kila nilipowahoji,
walisema wao hawajui lolote kuhusiana na hiyo mikanda..
Kutokana na hali yangu kuwa mbaya ,nikaona nitafute msaada,
na hakunamwingine niliyemuamini, nikamtumia huyu mwenzangu….nikamuomba
anisaidie…’akasema na Yule mwanadada akasema kwa hasira;
‘Hivi wewe vipi, ina maana umeamua kunisaliti, ndivyo
tulivyokubaliana hivyo, ina maana unataka kuniingiza kwenye mambo yako….’akasema
kwa sauti ya hasira, na wakili mwanadada akamkatisha kwa kuuliza swali;
‘Akusaidie kwa vipi?’
Mkuu wa wakili akamtizama Yule mwanadada ambaye alikuwa bado
akamuangalai kwa hasira akasogeza mkono kutaka kumshika, lakini Yule mwanadada
akarudi nyuma, kwa hasira na kuukwepa ule mkono, ilionyesha wazi hakutaka
kabisa kuhusishwa au hakutarajia kuwa wakili mkuu angafikia hapo. Wakili mkuu
akaendelea kuongea;
‘Siku hiyo nilikuwa nimetundukiwa madripu ya dawa,lakini
ilikuwa kama ushahidi wa kuficha hayo niliyokuwa nimekusudia kuyafanya. Ndio
nilikuwa anumwa, lakini kwa muda haikuhitajika dawa ya namna hiyo, nikamuomba anipe dawa itakayonipa nguvu,niweze
kuinuka hapo na kwenda kummaliza mwanadada mmoja ambaye niliona ndiye yupo
karibu na hawo watu ingawaje hakutaka kuniambia….
‘Mwanadada yupi huyo…?’ akauliza muheshimiwa hakimu
‘Wote mnamjua , haina haja ya kumtaja kwa sasa…’akasema.
‘Ni vyema ukamtaja, kwani tunataka kuweka haya mambo
sawa…’akasema muheshimwa Hakimu.
‘Ni mwanadada Kimwana….’akasema nakutulia,na wote mle ndani
wakageukiana, lakini wakili mwanadada alikuwa katulia kimiya akisikiliza yale
mazungumzo,
‘Mnaona nilishawaambia kuwa ndio yeye aliye muua Kimwana
mkawa mnanibishiamnoana sasa kakubali mwenyewe….’akasema Mkuu.
‘Sijasema kuwa nimemuua mimi, sikumuua mimi, …..hilo nawaambia
ukweli….’akasema mkuu wa wakili huku akionyesh akwakidole…
‘Aaah,….unapinga tena…’akasema mkuu kwa kuhamaki na
Muheshimiwa hakimu akamtulia mkuu, kwa mkono, kuwa aache mwenzake aendelee
kuelezea.
NB; Kumbe bado mambo yapo, nilijua leo tunamalizia, tuonane
sehemu ijayo ya hitimisho la kisa hiki.
WAZO LA LEO: Urafiki wa kweli hauna msimu, na pendo la zati
hutoka moyoni, nadhahiri yake ni matendo mema. Mpende akupendaye,asiyekupenda,.... kama ni mumeo au mkeo, jitahidi akupende kwa kujiuliza huyo anayempenda ana nini cha zaidi ambacho wewe huna.
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
Duuh, kila ninayemfikiria kuwa ndiye muuaji anachomoa, hapo tunakuachia wewe mkuu. Tupo pamoja, kura yangu ipo, na kama wanaruhusu,nikakupigia mara mia..
Τhe write-uρ has established helpful to us.
It’s very іnformative and you're certainly extremely educated in this region. You have opened up my eyes in order to various views on this particular topic together with intriguing, notable and solid written content.
Feel free to visit my page ... buy viagra
Thank you for sharing your info. I really appreciate your efforts
and I will be waiting for your next post thanks once again.
Feel free to visit my blog ... debtconsolidationinsider.com
Post a Comment