Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, May 20, 2011

Tunaikumbuka hii?


`The break news;
                   This is Radio from Tanzania! It was reported from Mwanza that the steamer
                   MV.Bukoba has sank, and many efforts has being given to rescue the
                   passenger! It was reported that more than 600 people were on board!
                We would keep on report as the news coming, thanks…'


 Nani analikumbuka tukio hili. Mimi kipindi hicho nilikuwa wapi vile, ....lakini wakati nipo shule nilibahatika kuandika kisa hiki(kama kitabu), nilijaribu kuandika kwa kimombo...ni muda mrefu kidogo, na kimombo chenyewe kilikuwa cha shule,...siunajua tena, lugha ya watu hii.  Ilikuwa siku kama ya kesho kama sikosei, tarehe ngapi vile,..tarehe 21-5-1996.
Nimefikiri sana nikaona ni bora nikitoe hicho kisa kwa kiswahili fasaha, badala ya lugha ya watu, au sio...ili tukumbuke kidogo kisa chenyewe...Nilikiita kisa hiki `best friends'.
 Hebu angalia nilivyooanza kisa chenyewe, msinicheke kwa kimombo hicho, ila kwa minajili ya kumbukumbu tu! Someni kidogo....!


           BEST FRIENDS

                                         
                                                        INTRODUCTION

                `The break news;
                   This is Radio from Tanzania! It was reported from Mwanza that the steamer
                   MV.Bukoba has sank, and many efforts has being given to rescue the
                   passenger! It was reported that more than 600 people were on board!
                We would keep on report as the news coming, thanks…'


 The water was slowly dropping from the water tape and water lightly hit her head like a rain! And the water washed out the soap bubbles which were already covered her body like a shining decorated dress! The feelings of pleasures penetrated inside of her mind and sent her in romantic pleasures, in another world of lovers, between a wife and husband!

  She slowly passing her soft hands around her body to smoothen the oils soap on her body, and this created a chilling feeling, a romantic feelings on her outer skin! She let the water   from the tape run over her body, as she ran her fingertips in gentle circles around all her body. And her mind accepted it by send her back when they were playing with water, when they were washing each other with her beloved husband! This feeling washed out all tiredness of a busy day!

 She has been busy with a daily domestic task, cleaning out the surroundings, washing out the clothes and dealt with other domestic duties and after she exhausted with a planned tasks, she thrown out her working clothes and run with a pieces of khanga into her bathing room!

 It was when she raise her hand on her head to clear out the soap-oil inside her long wet hairs, and at the sometimes with another hand put back the soap in its place! It was when the chilling feeling of pleasure reached in it’s a place where she could not proceed, it's when….

Then the news heard! The news from the radio, which penetrated inside her brain, it was like a vibrated shock from the electricity!

 And for a few minutes all her mind sized to work, her body freezing!

 The soap slept out her hand before it has lying in its place and dropped down in flowing water from the water tape! She tried to clear out her mind to assimilate that news, but she was not sure on what she heard, she tried to recall the date…Yes it was the day her husband was supposed to travel with MV. Bukoba…

 She switched off the water tape if she could hear the news again, but what she heard was something else! Is it trues, what she heard? She asked herself


 Without another second thought, she took her khanga from the hanging! And covered her body without make sure that she had cleared the soap bubbles on her body, without make sure that she had covered well her body, without…

She ran out from the bathing room to her sitting room, and therein she met her brother-in law, Mr. Maneno!

He was heard too, she knew for sure, perhaps he could tell her more, but he was as puzzled as she was…


                                           ***************
Kilikuwa kitabu kizima kama kingehakikiwa na kuwekwa ki-kitabu, na ni kisa kirefu kidogo. Tukimaliza kisa chetu kilichopo hewani tutaangalia kama upo uwezekana huo, wa kukiweka hewani. Maana nilikiandika na kukitelekeza tu...Mwasemaje wapendwa?

Ila nawaomba Watanzania wenzangu tusisahau tukio hili kubwa sana, nalilinganisha tukio hili kama lile la Titanic , ingawaje huwezi kiukweli kulilinganisha na hilo tukio, kwani lile lilikuwa kubwa sana. Na wakati naaandika hicho kisa nilikuwa sajaiona hiyo picha ya Titanic, ...msije mkasema niliibia, hapana inafanana kidogo, tu kwasababu inahusiana na mpenzi aliyekuwa mhanga wa hilo tukio, akamwacha mkewe nyumbani, na ilisadikiwa kuwa alikufa....je ilikuwaje, mmmmh, ngoja nikumbuke vyema, kwani hata sehemu nilipokuhifadhi hicho kitabu ....kwenye floppy disk...hutaamini!
 Je ni nani wanalikumbuka tukio hilo au jamaa zake walikuwemo?
 Ni wazo tu kama hamtojali?

Ni mimi: emu-three

4 comments :

Lulu said...

mimi naikumbuka sana sababu, siku hiyo ya tarehe 21/5/96 mdogo wangu R. Kakuru alinipigia simu akiwa mwanza akasema kuwa alikuwa amekwenda bandarini kuwapokea wifi na mdogo wangu ambaye ni dada yake na Kakuru lakini kapata habari kuwa meli imezama. Hapo ni saa mbili asubuhi! Niliwasha Radio call nikaweka online sehemu zote mpaka SOS lakini nilijibiwa kuwa mpaka serikali ya Tanzania iombe msaada ndo SOS itaweza kuingilia. Nilikuwa Dodoma. Nilipiga simu Kisumu, port Bell lakini wapi. Nilikuwa na bahati sababu nilikuwa Admin. kwenye shirika lenye uhusihano na ubarozi wa Uhoranzi hivyo nilikuwa na nyenzo zote za kutuma habari.

Ilipofika saa saba mawasiliano nchi nzima yaligoma. kumbuka kipindi kile hakukuwa na Mobile phones hivyo TTCL ililemewa ila nilishajua kuwa mdogo wangu, wifi na watoto wao watatu walikuwa kwenye meli.

Tulifika Mwanza Alhamisi na tayari miili ya mdogo wangu na mtoto wake wa kike ilipatikana siku hiyohiyo ya J. nne lakini wifi na watoto wake wawili (mke wa R. miili yao haikupatikana mpaka sasa). Kupata jeneza ilibidi nihimili vishindo vya polisi. walinionyesha mpaka bunduki ili nisiende kule nyuma kuchagua sanduku. Nilisema piga kwani hao walioko majini waliomba, basi polisi mmoja alisema mwache tu. Nilikwenda nikachagua sanduku la kutosha maiti mbili nikiwa na mme wangu mpenzi na kaka yangu pamoja na wadogo zangu watatu. Tulisafiri usiku toka Mwanza kwenda kijijini Ibwera na tulifika saa 8 usiku. Kesho yake wakati tunajiandaa kuzika akapitishwa maiti mmoja ambaye alishatoa harufu, watu aliacha msiba wetu ili wamlaze yule ambaye alihitaji msaada mapema na likuwa jirani yetu. Baadaye watu walirudi tukamalizia kuwalaza mdogo wangu na bintiye. Kuanzia siku hiyo mama alipoteza kumbukumbu na hawezi kukumbuka chochote ambacho kilitokea baada ya 21/5/96 lakini matukio ya nyuma yote anayo.

emu-three said...

Pole sana Lulu na nashukuru sana kwa kuwa nasi kwenye blog hii! Ubarikiwe sana kwa moyo wako wa upendo

Anonymous said...

E.B. Chibuga anasema:- Nina hakika bado hatujajifunza kutokana na tukio hili, maana majuzi nilisikia watu wakilalamikia MV Clarias, nikasikia tena bandari ya musoma imeharibika na inahatarisha usalama wa watumiaji, ingawa bado tunaendelea kuitumia..

SIMON KITURURU said...

Rafiki yangu alikuwa melini na kibahati bahati aliponea chupuchupu!:-(

R.I.P Marehemu!

Na twasubiri kisa hiki hapa kijiweni mkuu M3