Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, February 25, 2010

Leo kwake kesho kwako

Jana alitutembelea mama mmoja, yeye sasa ni mjane, mumewe keshatangulia mbele za haki. Alikuwa keshamaliza taratibu za eda, kwahiyo alikuwa akijaribu kujiweka katika hali ya kawaida, lakini alikuwa bado mwingi wa majonzi. Tuliongea naye ili kujua maendeleo yake na jinsi gani alivyo na jamaa wa mume wake, kwani sasa hivi mke akifiwa kama hakuwa na mahusiano mema na ndugu za mume wake kabla, huwa anaishia kunyanyaswa, na hunenda akadhuumiwa hata kila kidogo alichowahi kuchuma na mumewe.


‘Jamani kufiwa, usikie kwa mwenzako, hakuna jinsi kwasababu ni jambo lipo nje ya uwezo wa kibinadamu, lakini ni mtihani..’ alisema Yule mama ingawaje tuliona kama anataka kuanza kulia.

‘Ni kweli, hilo ni la kumshukuru mola kwani yote hupanga yeye, nafikiri hujapata manyanyaso yoyote mapaka sasa.

‘Kwaweli sijaanza, ila kama wasengekuja watu wa dini na kuyaweka mambo sawa, ningeishia kubaya. Kwanza yaliletwa mambo ya kimila, eti nijengewe kajijumba ka kinamna, humo nilale hata bila mkeka, chini, hakuna cha neti wala shuka…nilitamani hata mimi nijifie nimfuate mume wangu. Nashukuru mlvyokuja kututemblea siku ila na wale watu wa dini na kuyakataza hayo mambo kuwa ni mambo ya kimila, dini inayakataza kabisa. Mtu umefiwa, una majonzi, bado uzidi kuteswa, hayo yametoka wapi?’

Wakati anaongea hayo nikakumbuka jinsi gani mtu akifiwa anavyoteseka, sio kwa majonzi tu, ila gharama zake! Mimi karibuni nimefiwa na ndugu zangu , baba mdogo na mama mdogo. Misiba hii ilifululiza, kiasi kwamba tulibaki tukijiuliza nini kulikoni. Yote tulijua ni mapenzi ya muumba, ila kilichotuweka katika kuwaza zaidi ni hizi taratibu zinazotungwa sasa hivi na jamii. Si za kidini ila inakuwa ni taratibu zinazichipuka, na huishia kumuumiza mfiwa badala ya kumsaidia.

Siku hizi mtu ukifiwa, ujiandae kama unaandaa harusi, hata harusi inanafuu zake kwasababu kunapita kamati watu wanachangishana, lakini sasa hivi ukifiwa inabidi mkope , inabidi mchangishane wanandugu ili muweze kuwalisha wanakuja kuwapa pole. Nimejionea nilivyofiwa, kwani misiba iliongazana, kwahiyo hali ilikuwa tete kiuwezo. Ilifika wale waliokuja kutupa pole kuanza kulalamika kuwa mbona mnatupikia maharage, sie hatuli hiki tunataka hiki, tunataka nyama..huu sio utani, ila kweli watu wanadhamiria kuwa kwenye misiba siku hizi ni sehemu ya kupunguzia bajeti.

‘Kuna msiba kwa jirani, naona siku tatu tutahamishia bajeti yetu kwa jirani, mji huu usipojua kuishi utakufa njaa’ nilimsikia jamaa mmoja akisema. Nilimuangalia bila kummaliza. Kweli unahamishia bajeti yako huko, changia basi kiasi angalau nusu ya hiyo bajeti yako, lakini ukifika hapa hutoi chochote na kama ukitoa ni kiasi ambacho hata robo kilo hainunui. Huko tunakoenda ni kubaya….

Nilimugeukia Yule mama ili nisikie nini anachosema, nilimuonea huruma sana, kwani anasema hata rambirambi alizopewa kutoka huko mwanaume wake anapofanyia shughuli zake ameambiwa zitolewe ili zifanyiwe hitimisho la msiba. Hili hitimisho nalo ni sherehe siku hizi. Watu wameacha taratibi za kidini wanafanya yao. Hapo kunahitajika maandalizi ya hali ya juu watu wale na kunywa mpaka sare zinashonwa, picha za video zinachukuliwa ili ziwekwe kumbukumbu. Ni sawa, lakini hayo yafanywe na michango yetu sio kuwakamua wale wafiwa.

Mama huyu analalamika kuwa sasa hivi hana hata hela ya kula kwani hizo hela za rambirambi zilishachukuliwa muda, na alitegemea kuwa angalau angeanzishia kibiashara, kwasababu kipindi mume wake anafariki alikuwa ndio kachishwa kazi, na kunzisha kijibiashara kidogo kwahiyo hata akiba walikuwa hawana. Siunajua tena makapuni kama wamekulipa sana ni mshahara mmoja, zaidi ni kile kiinua mgongo chako.

Nafikiri ipo haja kwa viongozi wa dini kulikemea hili, kwani linavyoachiwa linaendelea kukua na kuwa kitu kingine kabisa. Itafika mtu akifiwa badala ya kulia uchungu na huzuni ya kufiwa, atalia ukata na jinsi gani atakavyowahudumiwa wanaokuja kumpa pole. Tumuogope mungu na tuwe na huruma na wafiwa, ni bora tujenge taratibu njema kuwa mfiwa akifiwa taratibu zote ziwe nje ya mfuko wake. Tumsaidie huyu kwasababu ana majonzi, ana pengo, na huenda kama ni mjane anajukumu la kuihudumia familia aliyoachiwa. Tumuogope mungu jamani, kwani leo kwake kesho kwako!

From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Hii ni kweli, inakera kuona badala watu kuja kutoa pole wanakuja kuongeza matatizo. Tuonane huruma