Leo ni leo….nikaingia kwenye mapambano…nikiwa peke yangu!
Nikiwa nimetulia ofisini kwangu nikimalizia kazi mbali mbali, na
mara nyingi unapoanza kazi za mahesabu,kuweka kumbukumbu za mahesabu kwenye
komputa, na kutayarisha taarifa mbali mbali, masaa yanakwenda haraka bila
hata yaw ewe mwenyewe kujitambua, nikawa nimesahau kabisa wajibu wangu
mwingine.
Nilipoangalia saa, ndio nikagundua hilo….nilikuwa nimetumia muda
mwingi sana,...hapo hapo nikaacha kila kitu, na kujiandaa kutoka mle ndani,
niende chumbani kwangu ikibidi nikachukue silaha, ili nikaweza kuwavamia
Makabrasha na mume wa familia.
Kwanza nilitaka kuhakikisha kuwa hawo jamaa bado wanaongea, au mume
wa familia keshaondoka maana muda mwingine ulishakwenda, nikachukua simu kutaka
kupiga, lakini kitu kikanizuia, sikupiga simu.. nikawa sasa nataka kutoka mule
ndani,…hapo ndio nikasikia king’ora cha polisi kwa mbali,
Muda huo moyo wangu unadunda sana,…na ikitokea hivi kama nipo
kwenye mapambani ni ishara ya hatari…na niliposikia hicho king’ora cha polisi
ndio ikawa ni zaidi,…hata hivyo mwanzoni nilijua ni polisi wanapita tu..,
lakini kilipofika maeneo ya kwenye jengo kikasimama hapo, na mimi
nikashituka, nikajua kuna kitu ..kuna jambo, na sio jambo dogo.
Nilichofanya kwa haraka nikumpigia simu mlinzi kumuuliza kuna
nini, na mlinzi akasema hana uhakika
‘Huna uhakika, hilo sio gari la polis limesimama huko, limafuata
nini…?’ nikauliza
‘Ndio na mimi nafuatilia madam…’akasema.
Hapo sasa sikujali nikampigia boso yaani Makabrasha..simu ikawa
inaita bila kupokelewa,…moyoni nikajua kuna tatizo limetokea ofisini kwa
makabrasha, nilitaka kumpigia mtoto wake kwani ndiye mlinzi wa baba yake,
lakini sikupenda afike kwanza, nilijua akifika kila kitu kitaharibika.
Nikawa bado nipo mle ndani, moyo haunitumi kutoka nje…., nikapiga
simu kwa walinzi kama mtoto wa Makabrasha keshafika, huyo mlinzi akasema hana
uhakika, kwani yeye alitoka, na kumuachia mwenzake ulinzi, na huyo mwenzake
ameshaondoka.
Baada ya dakika chache, nikapiga simu tena kwa walinzi
kuulizia kuna nini, wakaniambia kuna tatizo kubwa limetokea ndani ya ofisi ya
Makabrasha, na polisi wameshafika,..
‘Polisi!, tatizo gani la kuwahusisha polisi?, wamekuja kufanya
nini?’ nikauliza maswali mengi kwa haraka bila kujua nauliza nini.
‘Makabrasha kapigwa risasi na hali yake ni mbaya sana, sijui kama
atapona...’akasema huyo mlinzi na aliposema hivyo
‘Kapigwa risasi na nani…!’ nikauliza
‘Hatujui madam…’wakasema
‘Hamjui , huyu mtu aliingiaje ndani na silaha, bila kujulikana…’nikasema
nikiwa nimesahau kila kitu kuwa kama ni wa kulaumiwa ni mimi, niliyezima
mitambo ya kugundua vitu kama hivyo.
Pale mawazo yangu yalinipeleka kuwa liyefanya hivyo ni mume wa
familia, japokuwa Makabrasha siku hiyo nzima alikuwa akikutana na watu mbali mbali,
na wa mwishi ndio alikuwa mume wa familia kutokana na ratibba yake
‘Kama ni yeye amepatia wapi silaha, na aliingia nayo kw vipi,
yawezekana..mungu wangu…’nikajikuta nikisema hivyo…
Nikampigia tena mlinzi mwingine kumuulizia,..sasa nikiwa na sauti
ya kutaka kulia, nikasema;
‘Na nani kafanya hivyo, maana muda mfupi uliopita nilikuwa
nikiongea naye, kwenye simu,haiwezekani..ngoja nikahakikishe....’nikasema na kukata
simu.
Nilitoka mle ndani, nia nikuelekea huko, ili kama mume wa familia
yupo hapo niweza kutoa msaada,lakini nilikuwa nimechelewa, kwani nilipotoa
kichwa kuangalia kwenye korido, nikawaona maaskari. Wanakuja kuelekea chumba
cha Makabrasha.
Kumbe maaskari walishafika, nikarudi ofisini kwangu kwa haraka
kabla hawajaniona,na kujifungia, sikutoka kabisa, na sikutaka kufanya lolote
maana sikujua nikikutana na hao polisi nitasema nini.
Nikawa namuomba munu wangu hayo yanipitilie mbali maana nikihojiwa,
nikasema ni mimi nilizima mitambo ya kuonyesha matukio, nitakuwa hatarini,
kwanini nilifanya hivyo, nk…
Maombo yangu yakajibiwa,…ajabu kabisa siku hiyo hakuna polisi
aliyekuja kunihoji. Walikagua ofisi zote lakini ya kwangu wakaisahay,…baadae
ndio nikasikia kuwa, wameshampata muaaji,...
‘Ni nani huyo..?’ nikauliza, wakanitajia sifa za huyo mtu
aliyekamatwa, na jina lake,..oh...
‘Huyu mdada alifikaje hapa…., alikuja muda gani?’ nikauliza, na
walinzi wakasema alifika hapo muda kabla polisi hawajafika, na inaonekana ndiye
aliyemuua Makabrasha, na polisi
wameshamshika, yupo chini ya ulinzi.
‘Aliingiaje na silaha..?’ nikauliza
‘Hata sisi hatuji Madam, maana mlinzi wa mlango wa kuingilia
anakiri kuwa alimkagua na hakumkuta na silaha yoyote, na mitambo ya hatari
haikuwahi kulia…’akasema na alipotaja mitambo, moyo wangu ukakumbuka jambo,
hapo hapo nikauliza
‘Je yule mgeni wa Makabrasha, mwanaume aliondoka muda gani?’
nikauliza.
‘Alipoondoka tu ndio huyu mdada akaja…baadaye ndio hapo
ikagundulikana kuwa Makabrasha amepigwa risasi...’akasema.
‘Ni nani sasa aligundua hilo?’ nikauliza.
‘Hatujui, hata sisi tuliona ajabu, maana hakuna mlio wowote wa
hatari uliosikika, ina maana mitambo huko juu haifanyi kazi..na akti yetu
hakuna aliyewahi kupanda huko juu, mpaka sasa polisi hawajasema ni nani
aliwapigia simu…!’ akasema.
‘Sawa…tutajua tu..’nikasema
Wazo la haraka ni kwenda kuwasha mitambo ya kunasia matukio, …amoja
na uamkini wangu, siku hiyo nilichanganyikiwa, maana…mawazo yangu yalikuwa kwa
mume wa familia je yupo salama…
‘Je polis wakigundua hilo, kuwa ni mimi nilizima hiyo mitambo
itakuwaje..’hilo nalo lilinisumbua sana…hapo sina ujanja, moja kwa moja
nitashikwa kwa kuhusika na hayo mauaji, hapo nikawa na wakati mgumu.
Nikatafuta upenyo, hadi nikaupata nikatoka pale haraka na kwenda
chumba cha mitambo ili niweze kuweka ile mitambo ON, niliingia kile chumba kwa haraka, nikaendelea ule mtambo...nilipotaka kugusa pale, nikagundua ipo ON tayari.
Unajua nilishituka,..ni kama vile mtu kaona kitu cha kutisha,.. ina maana kuna mtu alikuja akabadili, ...ni nani huyu, hakukuwa na muda wa kufikiri, ni kitendo cha haraka, kama ipo ON, ina maana matukio yote yatakuwa yapo bayana..
Hapo nikavutika nione kilichotokea kwenye ofisi ya Makabrasha, kwa haraka nikavuta droo ya ile komputa, laptop...ila nataka kuivuta mara....nikasikia kitu au mtu, hapo nikageuka kwa haraka kuangalia huku na kule, nilihisi ni mtoto wa Makabrasha kaja,..lakini hakukuwepo na mtu, hata nilipojaribu kuangalia kila sehemu sikuona mtu..ila nina uhakika huyo atakuwa ni mtu tu...
Nikaacha, kile nilichotaka kukifanya, sasa nikawa na wasiwasi kuwa hata polisi wanaweza kunikuta hapo, na ninaweza kuonekana kuwa nilikuwa natafuta njia za kuficha ukweli,...na wakatu nawaza hilo, mara nikasikia watu kama wanakuja mueleko huo nikajua ni polisi…nikatokeza kichwa.
Ni kweli walikuwa
ni polis wanazunguka, hapo, nikaona hakuna usalama tena…nilipoona kuna upenyo
nikatoka kwa haraka na kurudi ofisini kwangu, na kutulia kuwasubiri polisi
wakija kunihoji, nilijua ni lazima watafika kunihoji...lakini hilo halikutokea kabisa siku hiyo.
Muda ule nipo hapo ofisi peke yangu, nikawa namuwazia Makabrasha, sikuamini kuwa huyu mtu anaweza kufa,..ina maana uhai wa mtu ndio hivyo, muda mpo naye ghafla keshapotea, ndio basi tena...nikamuwazia sana, zile tambo zake..kuwa yeye hawezi kufa hivi karibuni maana ana afya..., hata hivyo, kuna muda nilijikuta nikimuwazia kuwa huenda atapona hajafa...lakini kama alipigwa risasi, sijui sehemu gani, na huyo muuaji alidhamiria kumuua, sijui kama atapona!.
Unafahamu mtu hata awe mbaya vipi, linapomfika jambo kama hilo, la
ugonjwa au umauti, hata kama ni ugonjwa tu, huwezi tena kumtakia mabaya, huruma itakuja tu, labda wewe uwe na nfasi mbaya, hapo mimi nikawa naombea apone tu, asife...sio dhamira yangu mtu huyo afe, mimi nilitaka akamatwe afungwe tu, ili haki itendeke, lakini sio kufa...
Kiukweli pamoja na mengine, kuwa alikuwa ni adui yangu na ilifikia
muda natamani hata kumuua, lakini mtu huyo alikuwa na mazuri yake, ukiwa naye, ..na hata kwa jamii,..na kiukweli pamoja na hayo, alishakuwa mtu wangu wa karibu, sasa
nikifikiria kuwa sitamuona tena, hapo kiukweli sikuweza kujizuia, nililia
sana..kumbuka hapo nipo peke yangu…
Sikumbuki nilikaa muda gani
nikilia hivyo,…kuangalia saa muda ukawa umepita sana, kupo kimia, na ile hali iliyozoeleka muda huo huwa nje kumechangamka, lakini siku hiyo ilikua kinyume chake, watu waliondoka, waliobakia ni wachache tu..
Hapo nikapiga simu kwa askari ili nijua kinachoendelea, askari huyo ndiye akaniambia kinachoendelea huko njem...kuwa Makabrasha kakimbizwa hospitalini...
'Ana hali mbaya sana..?' nikauliza
'Sijui Madam, hakuna aliyeweza kumuona, polisi hawaruhusu...'akasema
'Oh, basi, huenda atapona..'nikasema
'Sijui...'akasema huyo askari, na kukata simu
Nikawa hata sijui nifanye nini...kila ninachoshika hakishikiki, ule ujasiri wangu wote ukaondoka, ..nikachukua simu kumpigia mume wa familia, simu haipatikani, nikampigia docta wake ninayemfahamu simu haipatikani, nikampigia simu mume wangu halikadhalika....ikawa n ajabu kwangu, kwanini watu hao muhimu hawapatikani.
Sasa nimetulia, mara simu ya huyo askari niliyekuwa nampigia simu ikaita, nikapokea kwa haraka
'Nipe habari..?' nikauliza
'Makabrasha hatunaye tena duniani..'akasema
'Nini, una uhakika...?' nikauliza
'Ndio ukweli wenyewe, kafariki kwa jeraha la risasi,..uchunguzi bado unaendelea,…’ akasema huyo askari.
Shahidi huyu alipofika hapo akatulia kidogo kama kukumbuka kifo cha mtu huyo. Hata mume wa familia alionekana kuwa mbali zaidi maana sasa alikuwa kashika kichwa kwa mikono kichwa kimeegemea mikono.
Nilipopata taarifa hiyo, sasa akili ndio ikaanza kufanya kazi,
sasa nikaona nitoke hapo haraka nirudi huko chumbani kwangu, niliangaza nje, nilipoona hakuna dalili ya askari haraka nikatembea hadi sehemu ya kushuka chini kulekea chumbani kwangu, karibu nionekane na askari, lakini hakuniona.
Wazo langu kwa muda huo ikiwezekana, nitokea kabisa kwenye
hilo jengo nipotee kabisa, usiku kama huo angaliona nani,..na asubuhi na mapema nisafiri hadi huko kwetu kijijini, maana hata hapo watu humo jengo wananifahamu kwa sura ya bandia, sio ile sura yangu ya asili, kwangu ingelikuwa ni rahisi
kutoka na ingelichukua muda watu kunigundua kuwa ni mimi nilikuwa nafanya kazi
humo.
Nilishajipanga hivyo, lakini nisingeliweza kuondoka haraka hivyo,...bado kuna mambo ya kufanya, kwanza...hapo ndiop nikakumbuka ile silaha...nikawa sasa nipo chumbani, kwa haraka nikainua lile godoro....nilishikwa na butwaa...
Bastola haipo...!
‘Nani kaingia humu na kuichukua bastola…’ nikajikuta nikijiuliza mwenyewe,
hapo nikainua godoro kabisa na kuliweka pembeni, hakuna kitu…
Mawazo ya haraka yakaniambia, bastola hiyo ndio imechukuliwa
kufanyiwa mauaji…miguu yote ikalegea, nikajikuta nakaa sakafuni,..sina la
kufanya, nikaiona jela ilee…
Maana hapo utajitetea nini..ni mimi niliyezima mitambo, bastla
iliyoua nilikuwa nayo mimi, ni kwanini nilikuwa na bastola…nitasema nini kwa
polisi…’hapo akatulia kwa muda, na aliyemzindua ni mwenyekiti,…
‘Bastola haipo imekwenda wapi…hapo tuambie ukweli, nahisi kuna
kitu unatuficha?’ aliyeuliza swali hilo ni mwenyekiti…
‘Mimi sijui mwenyekiti sikujua imekwenda wapi….’akasema msimuliaji
‘Hapo kwakweli sisi hatukuelewi, Ina maana unataka kutuambia kuwa
sio wewe uliyemuua Makabrasha…?’ akauliza mwenyekiti.
‘Mwenyekiti huo ndio ukweli anu, haya niliyosimulia ndivyo
ilivyokuwa,…’akasema
‘Kiukweli inavyoonyesha hadi hapo, ni kuwa wewe na mpenzi wako
ndio mlioshirikiana kumuua, makabrasha,…hadi hapo tu, huna cha kujitetea,…’akasema
mwenyekiti
‘Mwenyekiti ndio maana nikaamua kuwaelezea ilivyotokea, nafahamu
hilo, kuwa haya maelezo yangu ambayo ndio ya ukweli, yanaweza kunifunga, na
mimi nitaonekana kuwa ndiye niliyeua,…lakini huo ndio ukweli, mkweli hana
lawama..’akasema shahidi
‘Hebu nikuulize, hapo ulipokuwa kwenye ofisi na ofisi ya
Makabrasha kuna umbali gani…?’ akauliza
‘Ni ofisi zilishikiana, yaani ni sema ni vyumba viwili vya karibu,
sema ofisi ya Makabrasha ni kubwa, sio kama ilivyokuwa yangu…’akasema
‘Kwahiyo chochote kinachofanyika ofisi kwa Makabrsha hukuweza
kukusikia..?’ akaulizwa
‘Huwezi kusikia kabisa,..alivyoitengeneza ofisi yake ni ‘sound
proof..’ akasema
‘Lakini ungeliweza kutoka kwenye chumba chako kwa haraka na
kufanya mauaji na kurejea ofisi kwako,…au sio…?’ akauliza mwenyekiti.
‘Ungeliweza…siwezi kusema huwezi maana …..ila nasema hivi, mim
sijafanya hivyo,…’akasema
‘Polisi wanasema, wewe ndiye uliyezima mitambo ya kuonyesha
matukio, wewe ulikuwa na bastola, bastola hiyo alikuelekea mdogo wa mume wako
kwa siri..mdogo wa mume wako kalithibitisha, hilo…kwanini ulihitajia silaha
mdogo wa mume wako kasema hajui…’akasema mwenyekiti.
‘Hawezi kujua hilo, maana hakuna aliyemuambia…alichosema ni
sahihi..’akasema shahidi
‘Hadi hapo, sisi kama wanafamilia, unafikiri tunaweza kukuamini..?’
akauliza mwenyekiti
‘Nakumbuka, tangu mwanzo,
kabla sijaongea mimi, wewe ulikuwa ukiamini kuwa aliyefanya hivyo ni mume wa
familia na mdogo wake, au sio , sasa iweje kwa haraka uamini kwua ni mimi
nimeyafanya hayo mauaji,…?’ akauliza shahidi.
‘Ni kutokana na maelezo yako…’akasema mwenyekiti.
‘Kwahiyo ukweli wangu ndio unaokufanya nionekane mimi ni muhalifu,
au sio..kwahiyo mimi nimefanya kosa kuwaelezea huo ukweli, jinsi ilivyokuwa…?’ akauliza shahidi
‘Kutokana na maelezo yako toka mwanzo, inaonyesha ni wewe,
kwasababu silaha iliyotumika kumuua Makabrasha ulikuwa nayo wewe hadi hatua ya
mwisho, na wewe ndiye uliyafahamu wapi silaha hiyo ipo, na wewe ndiye ulizima
mitambo ya kuonyesha matukio, kweli si kweli..?’ akauliza
‘Ndio…’akasema
na wewe umekiri kuwa
ulishafikia sehemu upo tayari hata kumuua, kutokana na hali aliyowatendea,
na..zaidi ulikuwa tayari kufanya lolote kumlinda mpenzi wako, na zaidi wewe
unafahamu kutumia silaha vizuri, kuliko mpenzi wako
..huoni huo ukweli, hapo huwezi kukwepa hilo,..sema ukweli wako,
ili tulimalize hili...’akasema mwenyekiti.
‘Ndugu mwenyekiti,..hayo niliyowasimulia hadi hapo, ndivyo
ilivyokuwa, huo ndio ukweli, wa siku hiyo,...kama mliambiwa vinginevyo ni
uwongo, maana mimi nilikuwepo humo ndani, tatizo, ni kuwa, ni kweli ni mimi
nilizima kitufe cha kuonyesha matukio…’akatulia]
‘Subiri kidogo..ulisema ulipokwenda kuwasha uliona kipo ON…?’
akauliza mwenyekiti
‘Ndio..ndio maana nataka muwe na subira, kwasababu bado nina
maelezo zaidi ya hayo, mkifanya haraka mtauharibu ukweli na nyie ndio ndugu
zangu, mnahitajika muufahamu ukweli kabla sijaingia mikononi mwa polisi..’akasema
‘Sawa sisi tutakusikiliza tu, lakini hadi hapo, hata sisi tuna
wasiwasi na wewe…’akasema mwenyekiti..
‘Wasiwasi wako hadi hapo, unakujaje, kuwa mimi ndiye niliweka
hicho kitufe OFF, kwanini usiwe na wasiwasi kuwa NINANI, aliyekuja kuweka ON,
na kwanini..na aliweka muda gani…?’ akauliza shahidi..
‘Hapo sijui, labda utuambie wewe…’akasema mwenyekiti.
‘Ndio nawakata msiwe na pupa,…maana kumbe baada ya hapo, huenda,
huyo mtu alikuja kuweka ON, baada ya kumaliz hiyo kazi, au sio, kwanini matukio
hayo yasionekana, hadi leo,..je polisi wanayo taarifa ya matukio yaliyotokea
siku hiyo…?’ akauliza
‘Mimi sijui…’akasema mwenyekiti
‘Hawana, ukweli ni kwamba kuna mtu alikuja akaiba video, ya amtuki
ya siku hiyo, ina maana kama ingelikuwepo, ingelionyesha yote yaliyotokea baada
ya kuwekwa ON, nina imani,..kuna kitu hapo…’akatulia
‘Kwanini unasema hivyo…?’ akauliza mwenyekiti.
‘Sikiliza,..mimi niliweka OFF,..akaja mtu mwingine, huyu mtu
mwingine hajui kuwa mimi nimeweka off…ukiwaja kwa haraka, usipoangalia kwa
makini unaweza kuweka ON, ukijua mwenzako kaweka OFF, au ukaweka OFF, ukijua
mwenzako kaweka ON, na ndivyo ilivyotokea…’akasema
‘Una maana gani..?’ akauliza mwenyekiti.
‘Ndugu mwenyekiti…baada ya
kufikiri sana na kupata taabu ya kuliwazia hilo tukio lilivyokuwa, nikaona ni
bora niseme huo ukweli ulivyokuwa, lakini nikijua kabisa, nikielezea huo ukweli
kwa polis kwanza nitakwua mshukiwa namba moja , achilia mbali polisi,yoyote
nitakayemuelezea huu ukweli, jinsi
ilivyokuwa hataamini kuwa sio mimi niliyemuua Makabrasha,
‘Hata mimi…’akasema mwenyekiti
‘Ni sawa, sio kosa lako mwenyekiti,sio kosa la yoyote aliyepo humu
ndani, lakini mimi ninaamini ukweli ndio silaha ya mtu yoyote yule…’akatulia
‘Sawa tuelezee ukweli wote, ndio tunataka sisi..kama wanafamilia..’akasema
mwenyekiti
‘Ukweli wangu ndio huo, nyie ndio kwa mara ya kwanza nimweza
kuwalezea kila kitu kilivyokuwa, bila kukwepesha jambo, maana hapo ningeliweza
kukepesha, hebu jiulize kwanini hadi leo polisi hawajaweza kunikamata…?’
akauliza
‘Walitaka kukukamata mimi ndio nimewazuia…’akasema
‘Sasa ndugu mwenyekitu huo ndio ukweli, ni wajibu wenu, kuukubali
kama ulivyo, au kuungana na polisi, siwezi kuwazuia kwa hilo, lakini ukweli halisi
ndio huo, na sikuwaficha kitu hata kimoja,…ndio maana nilitaka nielezee hatu
kwa hatua…,kama nimewaficha kitu mungu pekee ndiye anayejua zaidi….siwezi
kukumbuka kila kitu au sio…’akasema
Aliposema hivyo mwenyekiti akakuna kichwa kidogo ile yakufikiri
halafu akasema;
‘Mhh,… mimi sijui, lakini nionavyo mimi polisi wakisikia hayo
maelezo yako , moja kwa moja wewe utakuwa mshukiwa namba moja, je hujatuficha
kitu, mimi naomba uwe mkweli ili wakili wetu aweze kukutetea, nipo tayari
kumtoa wakili wangu kwa ajili hiyo…?’ akaniuliza mwenyekiti.
‘Mwenyekiti, pamoja na hayo mimi nimeshaongea na polisi, lakini
nilijua jinsi gani ya kuwaambia..niliwaambia yale niliyoyafanya kama mfanyakazi
wa Marehemu lakini sikuwaambia kuhusu bastola au kuzima mitambo, ili nipate
muda wa kukamilisha upelelezi wangu, ni muhimu sana ili haki iweze kutendeka...’akasema.
Mwenyekiti akaangalia saa yake, na alionekana na maswali mengi ya
kumuuliza huyo shahidi, lakini kabla hajamuuliza huyo shahidi, huyo shahidi
akasema;
‘Mimi imenichukua muda kuliwaza hilo, lakini moyo unanisuta,
na kila nikiwaza sana naona sijatenda uadilifu, na watu wengine wanakamatwa
ovyo, wakishukiwa kwa hayo mauaji,…wakati sio kweli,… na imekwenda, inafikia
hali kama inafifia hivi, kwanini..ina maana kuna mtu anafichwa, ukweli sasa unaanza
kubatilishwa, na kuna watu wengine, wanatarajiwa kukamatwa..na ni baada ya propaganda
potofu..’akatulia
Na wasiwasi wangu ni huo kuwa atakayefuata kwa hivi sasa ni mume
wa familia na mdogo wake, ambaye keshausema ukweli ..na huo ukweli kama kausema
ulivyo, mume wa familia yupo matatani, mimi ndio naanza kuingizwa sasa....ndio
maana nikaona sasa inapokwenda ni kubaya, ni bora nijitokeze mimi mwenyewe,
wasiwasi wangu ni kuwa bado sijamaliza kazi yangu,....'akasema.
'Kwahiyo umeamua kujitokeza kwa vile sasa inaelekea kumgusa mpenzi
wako wa asili..kwahiyo kwa hivi sasa upo tayari kufungwa kwa ajili yake…?'
akauliza mwenye huku akitabsamu kwa utani.
'Hapana, ....mimi kama mpelelezi, hilo nilikuwa nalifanyia kazi,
nilikuwa kwenye uchunguzi binafsi, kumjua ni nani hasa aliye-yafanya hayo
mauaji, maana nashindwa kujua, ni nani mwingine angeliweza kufika hapo na
kuchukua silaha hiyo, ..’akatulia
‘Kwanza kabisa kwenye shuku zangu nilimuwazia mtoto wa Makabrasha,
lakini ukumbuke hadi walinzi walithibitisha kuwa mtu huyu hakuwahi kufika eneo
la jengo hilo…wapo walinzi ninaowaamini sana,… na yeye pamoja na kukosana na
baba yake asingeliweza kumuua baba yake, anampenda sana baba yake, sasa ni nani
mwingine angeliweza kulifanya hilo...'akatulia kidogo, halafu akasema;
'Kiufupi, sikutaka kusema huo ukweli, kabla sijamaliza uchunguzi
wangu, ila ninachotaka kuwaambia hapa ni hivi, ...mimi sijamuua Makabrasha huo
ndio ukweli...na sikuwa na mipango huo, mimi nilikuwa na mipango yangu mingine
kabisa ya kumnasa huyo mtu na kumfikisha kwenye vyombo vya dola, nikiwa na
ushahidi ambao ulikuwa unafichwa na Makabrsha..ili iwe ni mwisho kwa mtu huyu,
na kundi lake haramu, maana yeye anatumiwa tu....’akasema
‘Ushahidi huo unao sasa…?’ akauliza mwenyekiti.
‘Siwezi kukujibu hilo swali kwa hivi sasa…’akasema shahidi
‘Kwanini…?’ akauliza mwenyekiti.
‘Nina maana yangu kama mpelelezi, niamini kwa hilo…’akasema hivyo
‘Sasa kama sio wewe uliyemuua Makabrasha ni nani basi,…maana kwa
muda huo, mweye silaha, na aliyekuwa humo ndani ni wewe?’ akauliza mwenyekiti.
‘Kama mtaniruhusu ninaweza kuongea nionavyo mimi,kutokana na
uchunguzi wangu kiogo nilioufanya, ningelipata muda zaidi eeh, nikaweza
kumalizia uchunguzi wangu, ningelimaliza kazi..lakini naona haraka haraka za
polisi zitafanya nisifanikiwe, na nafahamu ni kwanini..’akasema
Mwenyekiti alisita kumuuliza ni kwanini, akawa anaangalia nje,
halafu shahidi akasema
‘Japo sio sahihi, hata mimi sipendi, je ndugu mwenyekitu upo
tayari niutoe ushahdi mwingine wa ni nani kamuua Makabrasha, kitu ambacho hata
polis hawajaweza kukigundua,..?’ akauliza
‘Hayo ..kwanini usiwaambie polis wenyewe, maana wanasubiria huko
nje…?’ akasema mwenyekiti na watu wakageuka kuangalia huko nje, na kweli askari
walionekana wakiranda randa nje, kuhakikisha hakuna mtu anayetoka.
Shahidi akainamisha kichwa chini, kama anamuomba mungu wake,
halafu akasema
‘Mwenyekiti wewe ndiye unayweza kulisawazisha hili, na ukweli
ukapatikana, wewe ndiye waliyekuamini, au sio…mimi nasema hivi, fanya kile
unachoona ni sahihi, lakini kwangu mimi, …bado nilikuwa na mengi ya kufanya,..unaonaje…
yao…’akasema nakusita, alipoona mwenyekiti akisoma ujumbe wa simu yake
Ilionekana Mwenyekiti yupo
kwenye wakati mgumu. Baadaye mwenyekiti akachukua simu yake akitaka sasa
akitaka kupiga , huku akimwangalia huyo shahidi, na shahidi akageuka pembeni
kumuangalia mume wake, alijua hadi hapo hakuna jinsi, ni lazima mwenyekiti atimize
aajibu wake, hata hivyo nafsi mwake alijua bado hajakamilisha kazi yake.
Shahidi huyo sasa akaniangalia mimi, nahisi alihitajia msaada wangu…
NB: Ni nini kitaendelea.
WAZO LA LEO:
Dhana mbaya haitakiwi, hii ni pamoja na kusengenya, kuwateta watu wengine
vibaya,..hivi vitu sasa hivi vinaonekana ni vya kawaida tu! Watu kutetana,
kuandikana mambo ya aibu, kupiga picha mbaya na kuziweka mitandaoni, kuzusha
uwongo, au propaganda,..au jambo halijathibiti,a u kuruhusiwa kuongea wewe unakuwa wa kwanza kulitangaza... nia wakati wmingine ni kuharibiana majina. Hii ni dhambi kubwa, hebu fikiri
kama ni wewe ungelifanyiwa hivyo ungelifurahi, ukijua kuwa ni uwongo. Inaumiza
sana..je utawezaje kulilipa hilo jeraha la mtu aliyeumia moyoni kutokana na
dhana hizo potofu..Tujiepusheni na tabia hii jamani.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment