Mwenyekiti akaangalia kule sauti ilipotokea, kwanza alihisi sauti
ni ya mtu mwingine kabisa, kwani sauti ile ilikuwa ndogo zaidi tofauti na sauti liyotambulikana, na ilionekana ya kuchoka,.., lakini
alipoangalia pale ilipotokea akafahamu huyo mtoa sauti ni nani…
Na kwa muda ule wajumbe wote walikuwa wamegeuze vichwa vyao, kumuangalia mume wa familia na sasa wakageuza vichwa kumuangalia huyo aliyetoa sauti, ili kuwa na uhakika kuwa ni yeye au ni sauti ya mtu mwingine, hata yule aliyekaa karibu naye alifanya hivyo. Ilikuwa sio sauti yake ya kawaida...
Na wakati huo huo, mume wa familia alikuwa bado kasimama kama kapigwa ganzi, kama kaamrishwa 'simama!' akatii..., akaganda, lakini bado akiwa katizama huko mlangoni, ni kama vile anatafakari sauti hiyo ni ya nani....
Mwenyekiti akakohoa halafu akasema;
‘Najua wewe ulitaka kuongea awali, nikakuzuia, ...ili mwenzako amalizie maelezo yake, na ingawaje bado kama alivyodai, lakini sio mbaya, ...'akatulia mwenyekiti akiteta na mke wake kidogo.
'Sio mbaya kama tutampa nafasi ... 'akasema akigeuka huku na kule
'Lakini niliona kabla ya kuendelea tufanye hicho nilichokitaka kwanza,...kupeana nafasi ya kukiri kosa, kutubu nk..., maana vyovyote
iwavyo, sisi ni wanafamilia, sisi ni wanandugu, na zaidi ya hayo sisi sote ni
wanadamu, tunatakiwa tusameheane, lakini utasamehewa vipi kama mwenyewe hujakiri kosa au sio..., ndio maana nikajaribu kumpa nafasi hiyo mume wa familia..’akasema
mwenyekiti.
Mume wa familia alikuwa bado kaganda tu...
'Je mimi sikutimiza wajibu wangu..?' akauliza mwenyekiti na wajumbe wakaguna na ikawa kama sauti ya kuguna guna tu.., hakuna kilichosikika,
'Kiukweli nimelitimiza hilo, na nini kimetokea,..mumeona wenyewe, mume wa familia anataka kukimbia, kama alivyofanya mdogo wake, maji hufuata mkondo...'akasema na hapo wajumbe wakacheka kidogo
‘Lakini ndugu yangu mkwe wangu, mjumbe wa hiki kikao , mume wa familia,... hilo, unalotaka kulifanya unajisumbua bure, huwezi kuondoka hapa...'akasema mwenyekiti.
Hapo mume wa familia akageuka na kuanza kusema kwa hasira...
'Ninani anaweza kunizuia...mimi sio mfungwa, mimi sijashikiliwa na polisi hapa..mimi nipo hapa kwa hiari yangu mwenyewe, na ninaweza kuondoka kwa hiari yangu mwe-nye-we..'akasema mume wa familia, na mwenyekiti akageuka kumuangalia yule aliyetoa sauti, na hakusema neno, aliyesema neno ni huyu ...aliyetoa sauti awali.
'Mimi nitafanya hivyo, ...'sauti ikasema na mume wa familia akamgeukia kama kushtuka vile, lakini hakusema neno, alionyesha uso wa kutahayari tu, kama haamini hicho anachokisikia. Na huyo msemaji akasema;
'Ndugu mwenyekiti, huyu mtu hawezi kufanya mnavyotaka nyie, maana akifanya hivyo ndoto yake yote itayeyuka..nafahamu hilo, ...kiukweli kufanya hivyo inahitajia ujasiri, imani na utashi ulio sahihi, ukizingatia kuwa mikakati mingi ya miaka mingi ilishafanyika, na..kiukweli...hataweza kukiri kosa, ...'sauti ikasema.
'Kwanini..sijaelewa...?' akauliza mwenyekiti.
'Kwanini hawezi kufanya hivyo...eeh, kwanza anaogoa huenda atakiuka yale tuliyokubaliana mimi na yeye, lakini hilo sio kweli, ..' akatulia kidogo.
'Sio kweli kwa maana alishakiuka hayo tayari...hata hivyo, ukweli upo wazi, kama
ingelikuwa ni mtu wa kutubu na kuomba msamaha angeshalifanya hilo mapema na mkewe...'akatulia
'Mimi nina imani mke wa familia kwa upendo wake na huruma zake angelimsamehe tu, nina uhakika na hilo, lakini wapi, sikio la kufa halisikii dawa, sasa labda, nasemea labda, huenda mwenzetu huyu bado anasubiria ushahidi, bado anajiamini kuwa hayo aliyoyafanya hakuna anayeweza kuyazuia,...
'Sasa kwa vile anahitajia mashahidi, basi mimi ni shahidi,..na akitaka ushahidi utatolewa, au sio ..’akasema huyo mzungumzaji mpya, akimuangalia muongeaji wa kwanza, na huyo muongeaji wa kwanza akatikisa kichwa kukubali.
Hapo sauti ya mume wa familia ikatokea sasa kwa jaziba, ikisema;
‘Ina maana hata wewe, unaungana na huyo mzandiki, ..hata wewe unataka kunisaliti mimi..' akasema sasa akiweka kidole mdomoni kama kuzuia kuongea zaidi...’
Sasa mume wa familia alikwua kasimama akiwaangalia wajumbe, lakini akiwa kainamisha kichwa chini. Na wajumbe wakasubiria kauli
ya huyo mzungumzaji mpya ambaye bado alikuwa hajapewa kibali rasmi cha kuongea;
‘Rudi ukae mume wa familia, …’aliyesema sasa hivi alikuwa ni mwenyekiti, na
mume wa familia akawa bado kasimama pale pale karibu na mlango, sio karibu ya kuweza kuushika ule mlango, lakini karibu ya kuukaribia, lakini akiwa kawageukiwa wajumbe.
‘Hiki kikao ni rasmi, na baada ya hiki kikao, kitakachofuatia ni
polisi kufika hapa kufanya kazi yao, unavyokimbia hivyo unatupa wasiwasi, kuwa huenda ndio wewe unayetafutwa na polisi..’akasema mwenyekiti
‘Kwa kosa gani..?’ akauliza mume wa familia kama anashangaa, akawa anageuza kichwa kwa kujiiba kumuangalia mwenyekiti
‘Hilo swali watalijibu wao, hao polis sio mimi..mimi sijui..., ila
kwa taarifa yao waliyotupatia ni hivyo, kuwa sisi sote tuliopo hapa kwenye hiki kikao tupo chini ya
ulinzi, sikutaka kuwaambia hilo kabla ..hata tunavyozungumza hivi sasa,
tunafuatilia kama nilivyowaambia awali, polisi wametuzingira,.. je unafahamu wapi alipo huyo mdogo wako aliyetoroka hapa na kukimbia,..?’ akaulizwa
‘S-s-sijui, ina maana wameshamkamata…?’ akauliza sasa akionyesha uso wa kushangaa na kama kuogopa fulani hivi
‘Na wewe ukitoka hapo nje, utafanyiwa hivyo hivyo, kwahiyo ni bora
urudi ukae kwenye kiti chako ili uwe miongoni mwetu na hata likitokea la
kukamatwa tutajua sisi ni wanafamilia kwahiyo tutaangalia jinsi gani ya kusaidiana kama wanafamilia…’akaambiwa
'Hahaha, kama wanafamilia, ...hahaha, usinione mimi kama mtoto mdogo mwenyekiti, hapa mnachotafuta ni ushahidi wa kutufunga, bila hata ya kutaka zaidi kutoka kwangu, ukweli halisi ninao mimi...mnazunguka tu,..nia ni nini, kuhakikisha nadidimia na kuzama kuzimu,...niende nikawa hohehahe kule kijijini, hiyo ndio furaha yako,..maana ukitaka kumuua mbwa kwanza si lazima umuite majina mabaya au sio, ndicho ulichokitaka, haya sasa fanya utakavyo,...'akasema akinyosha mikono kama ya kusalimu amri.
'Mjumbe usipoteze muda, maana hata useme nini, haya yatafanyika tu,..kikao kitaendelea na wewe utakuwepo, upende usipende, ukitaka kwa hiari yako,..sawa kakae, ila kama unataka nguvu itumike sawa ..sisi tutawaachia wenye mamlaka,...'akasema mwenyekiti.
'Haina haja ya nguvu ndugu mwenyekiti,...mwenyewe atakaa tu,kwasababu mimi ndiye mtu wake wa karibu, mimi ndiye ninayweza kumrejesha akae...sasa kama anataka kuondoka ondoke tuone,... uniache mimi nikamatwe na polis, si ndio pendo lake hilo, si ndivyo alivyotaka au sio, haya ondoka bwana...'akasema mzungumzaji
Sasa taratibu mume wa familia akageuka kuangalia mlangoni kama kweli anataka kuondoka, halafu akiwa kama anarudi kinyume nyume,...huku akiongea, kwa sauti ya huzuni akasema;
‘Kumbuka tulipotoka, kumbuka ahadi yetu, kumbuka mimi na wewe ni
nani, usije kunisaliti tafadhali, nakuomba …’akasema..na sasa akiwa kageuka kumuangalia huyo mzungumzaji.
Mzungumzaji alikuwa kimia, na kitendo kile cha kukaa kimia, kilimfanya mume wa familia, sasa atembee kwa haraka hadi pale alipokaa huyo mzungumzaji mtarajiwa, ili mwendoo wa hatua kadhaa, maana zilikuwa za hasira kama vile anataka kwenda kufanya jambo.
Ili ufike pale kwa huyo mzungumzaji, inabidi umpite docta, kwahiyo alipofika pale
alipokaa docta akasita, akageuza kichwa kumuangalia docta, na docta akawa anamuangalia,
wakaangaliana, na docta akatikisa kichwa cha kusikitika, na mume wa familia,
akainamisha kichwa chini, ..halafu baadae akainua kichwa na kusema;
'Samahani docta...'akasema hivyo, halafu akamgeukia huyo mzungumzaji..
‘Ni kweli hata wewe unataka kuungana na mzungumzaji wa kwanza,
kuyathibitisha maneno yake ya uwongo, maneno aliyoyatunga ili kujihami,...au , hata siamini,…..?’ akauliza...hapo akiwa anazungumza kwa sauti ya chini, kama vile hataki wengine wasikie, lakini ni sauati ya kusikika na watu.
Mdada akatikisa kichwa kukubali.
Kutikisa kichwa huko kuashiria kukubali, kulimfanya mume wa
familia kuinamisha kichwa upande, hakuweza kuamini hayo,…hakuamini huyo mdada
anaweza kuwa kama alivyoita yeye, 'kumsaliti..', sasa wakawa wanaangaliana, mume wa familia, akasema;
‘Ina maana ni kweli, unataka kufanya hivyo,... hapana siamini haya, wamekupa nini hawa
watu,....haiwezekani, usidanganyike mpe---'hapo akasita na kumuangalia docta, halafu akaendelea kuongea
'Hizo ni hadaa zao hao watu, hawatakujali baada
ya hapa, nakuambia ukweli, na ilivyo, baada ya hapa huenda ukaishia jela, huenda mimi na wewe tukaishia jela, maana hata mimi najua hilo ...’akasema huku akionyesha uso wa kukata tamaa, na huzuni, lakini shahidi huyu
mpya akasema;
‘Hapa sio swala la mimi kukusaliti, tatizo ni kwamba nyani haoni
kundule,…na kama ni ubaya , ubaya huo umeuanza wewe, na haijalishi kama
nitaongea au nitakaa kimiya, lakini ni bora niongee ili ukweli ujulikane kwa
manufaa ya wengi, kabla mambo hayajaharibika zaidi, hawa ndio wataweza kutetea au kukuangamiza..’akasema shahidi huyo mpya.
Mume wa familia taratibu akarudi kwenye kiti chake na kukaa, alikaa karibu yangu na hakutaka hata kuniangalia mimi machoni, na aliyeweza kumsemesha alikuwa wakili wake akawa anamuongelesha jambo, yeye akamuashiria kwa mkono anyamaze,
na wakili wake akafanya hivyo.
'Je mwenyekiti nianze...?' akauliza mzungumzaji, na mwenyekiti akaniangalia mimi, na kusema neno, mwenyekiti akatikisa kichwa kukubali, hakutoa sauti...
Mzungumzaji mpya akasema;
‘Naongea haya nikiwa nimeshaongea na mume wangu...kwahiyo nina kibali rasmi japokuwa awali alionekana kunizuia, alifanya hivyo, akiwa bado haamini, lakini baada ya haya mazungumzo, ataamini...haina shaka kwa hilo...’alianza kuongea
mzungumzaji
‘Endelea kuongea na kuruhusu sasa rasmi,...nilikuwa napata ushauri kutoka kwa msaidizi wangu hapa... ila nakuomba kama
alivyofanya mwenzako na wewe iwe hivyo hivyo, …’akasema mwenyekiti.
***********
‘Mhh…kama ni hivyo utanifanya nishindwe kufikisha ujumbe ninaotaka
kuufikisha hapa, kiukamilifu wake, na kwa hivyo ukweli utashindwa kubainika, na mimi sitaki ukweli uje kupotoshwa na watu wengine hasa hao maadui wasionitakia mimi mema,...’akasema
‘Jitahidi kufanya hivyo …’akasema mwenyekiti.
‘Sawa nitajitahidi kufanya hivyo…’akasema shahidi
‘Mimi namwambia mume wa familia kuwa hatima yangu na mume wangu imeshajulikana, kwahiyo kwangu hakuna cha ajabu, tatizo ni yeye na mke wake..'akasema na sasa akamuangalia mume wa familia akisema
'Kama wewe umeshindwa kuukubali ukweli, kama wewe umeshindwa kukaa na mke wako mkaongea mmkayayamaliza, ukasubiria kitu kama hiki, ujue wewe una matatizo, tena matatizo makubwa,...maana haya yasingelijulikana na kila mtu,..na kwa kufanya hivyo, wewe unashinwa kuwajibika kama mume, na huo sio ujasiri,na huo sio upendo wa kweli..na kwahiyo , wewe ndiye msaliti
wa kwanza…’akasema mzungumzaji na mwenyekiti akatabasamu.
‘Mimi nimeteseka sana, ..hujui ni kiasi gani nilivyoteseka,
nimekuwa katika wakati mgumu sana, hujui tu, nimekuwa nikijiuliza je hili
ninalofanya ni sahihi, unaishi na mume ndani hakufahamu, unawalinda watu hawakujali , unafanya mambo, kiukweli mimi…imekuwa ikiniumiza
sana..’akasema
‘Sasa ni wakati wa kujitakasa, …'akasema akimuangalia mume wa familia, na mume a familia akawa sasa kakunja uso kuonyeha hasira.
'Mume wa familia hebu jiulize hivi haya mpaka lini, ..au bado ulikuwa na ndoto za ushindi,...kwanini
tuendelee kuishi katika maisha haya ya sintofahamu, ya kudanganyana, maisha ya
kuigiza, ...mimi bwana nimeamua, ni heri kusema ukweli, ili haki itendeke, hata
kama nitakosa kila kitu, lakini nitakuwa nimepata kitu cha kudumu, ..ambacho ni haki na ukweli.
Mume wa familia hapo akainua kichwa na kumuangalia mzungumzaji
halafu akageuka kwa mwenyekiti, halafu akainamisha kichwa chini hakuniangalia
mimi bado.
‘Wewe unanifahamu sana mimi nilivyo, jinsi gani ninavyokupenda,
unafahamu sana jinsi nilivyojitolea kwa ajili yako, jinsi gani nilivyoweza
kuvumilia, na kuyafanya yale ambayo sikupenda kuyafanya yote hayo niliyafanya
kwa ajili yako..’akatulia
‘Hata huko kujizalilisha nilifanya hivyo kwa ajili yako kukulinda
wewe na familia yako.., hebu niambie ni mapenzi gani unayoyataka,kutoka kwangu, je mimi ni
tofauti na hawo wanawake wote uliwahi kutembea nao…’akawa kama anajiuliza
‘Sio lazima unijibu, lakini ukweli upo wazi, ..lakini kwanini, je
ina maana mimi sikutakiwa nipate raha, sikutakiwa niwe na amani, ina maana mimi
sio binadamu kamilifu,..na zaidi ina
maana mimi ni nani kwako!...’hapo akatulia
Mume wa familia akageuza kichwa na kumuangalia muongeaji, sasa
wakawa wanaangaliana, na muongeaji akaendelea kuongea…
‘Au ina maana mimi ni njia ya kufanikisha starehe zako tu…,
hapana, nasema sasa iwe basi, iwavyo na iwe, na kama kweli ulinipenda kwa
ukweli basi turudi kijijini, tukaanze maisha mapya, kama hilo litawezekana,..lakini haliwezekani au sio,..unajua ni kwanini haliwezekani, su sio.......’akatulia na wakawa wanaangaliana.
Mume wa familia akasema;
‘Sikiliza, sikiliza mpendwa,...usiendelee tafadhali, unajua jinsi gani
unavyonitesa moyoni…unayoongea hapa hayataweza kukusaidia wewe au mimi, hayo sana sana yanazidi kutuumbua tu, na hayo ni furaha ya mkizi…’akasema mume wa familia.
‘Mimi ninajua ninachokifanya, na nafahamu njia sahihi ya kunifanya mimi
niwe na amani ni kusema huu ukweli,…’akasema mdada.
‘Hahaha, ukweli, haya fungua hilo bakuli uone kama utafanikiwa...unawafahamu
hawa watu, unavyoongea hivyo unawapa faida, ya kutufukuzilia mbali, haya
utaondoka na nini sasa, wao wanachotaka ni ....uwaambie huo wanaouita ni
ukweli, ili wapate ushahidi, na mwisho wa siku waweze kutumia huo ushahidi
kukutimua, au kukutia kitanzini…’akasema mume wa familia
‘Kwangu mimi siogopi kutiwa kitanzi, au kukosa haki yoyote, mimi
nina imani kama nina haki yangu hiyo haki nitakuja kuipata tu, lakini sio
nitumie ujanja kuipata wakati haijatambulikana kuwa ni haki yangu, ni kweli
ujana na utoto ulitudanganya sana, na sote tulikuwa na ndoto hiyo, lakini kwa
jinsi umri unavyokwenda, tunajifunza.
‘Namshukuru sana bosi wangu na wale wote walionijenga,
wakanisomesha wakanifanya nibadilike na kuujua ukweli wa maisha,..nashindwa
kuelewa kwanini wewe mwenzangu ulisoma na bado hukubadilika, ina maana hiyo elimu ilikusaidia nini, maana wewe umesoma au sio...,
na sio elimu ndogo, hiyo elimu yako imekufundisha nini, kwanini uhadaike, kwanini ukubali kudanganywa, hapana mimi siwezi kurudia uchafu.
‘Sasa sikiliza wewe mume wa familia,… hakuna ukweli zaidi ya
ukweli unaoufahamu wewe mwenyewe, ukweli ni mkataba wako wewe na mwenyezimungu wako,…jiulize hayo unayoyafanya ni sahihi, je
ungelifanyiwa wewe ungelifurahi, ..ukifika hapo kama ni muungwana utageuka nyuma,.....’akasema.
‘Siamini…’akasema mume wa familia
‘Huwezi kuamini, maana mimi sio yule mdada wa kijijini tena,
japokuwa moyo wangu wa upendo kwako upo pale pale,…ninachoweza kukuambia ni hivi, mimi
sitaki chochote kutoka kwao, nimerizika na maisha yangu na umasikini wangu, ninajua ni vipi nitapata halali yangu, na kazi niliyotaka kuifanya nimemaliza, …’akatulia
'Hahaha, utaimalizia jela...'akasema mume wa familia akicheka kwa kukata tamaa
‘Tatizo hunifahamu mimi ni nani kwa sasa, mimi siogopi kwenda jela, kama kweli nilitenda
kosa na likadhihirika kuwa ni kosa, kwanini niogope kwenda jela, ….kama
niliogopa kwenda jela kwanni nilifanya hayo yanayompeleka mtu jela, huo ndio unafiki, …uliousema
wewe..sasa je mimi na wewe, ni nani anatakwia kuitwa hivyo.
‘Sikiliza wewe mtu, baada ya kusikia hayo yote uliyoyafanya wewe,
ambayo nilikuwa nayasikia tu, sikuwa nimeyafuatilia kabla, sio kwamba
nilishindwa kufanya hivyo hapana, muda ulikuwa hautoshi tu, kuwalinda, na kuyafanya hayo ya kuhakiki ukweli huo,..kwa namna nyingine, nilijua ni katika kuyaweka maisha yako yawe bora zaidi,
lakini ya kwako yamezidi mpaka,..’akatulia
‘Je uliyafanya kwa mujibi wa kazi yako, hapana, je uliyafanya kwa
nia njema ya kuinua maisha yako na katika kufanya hivyo, ilibidi ifanyike
hivyo, kwa nia njema hapana, je ulifanya hayo kwa vipi basi, jibu rahisi ni tamaa, au
utasingizia nini…kiukweli umeniumiza sana…’akamuangalia mume wa familia
‘Hivi wewe upoje, unadiriki hadi kubaka bint wako wa kazi,
unamfahamu vyema yule binti, amatokea wapi, ..binti wa watu alikuwa akihitajia
sana msaada wenu, jamani, yule sio sawa na, na…binti yako, je hayo yangelitokea
kwa bint yako ungelifurahia, kiukweli kitendi hicho kimeniuma sana…
‘Sasa mambo kama hayo mimi
nikae kimia tu, niendelee kuumia tu moyoni, sawa, labda utasema mbona wewe
umefanya hivi na vile, ..mimi niliyoyafanya ni katika uwajibikaji wangu, kazi
zangu…na kila jambo naweza kulitetea kuwa nililifanya kwa minajili
gani..japokuwa nimekiuka sheria za ndoa, na hayo nimeshaongea na mume wangu.
Je wewe uliwahi kukaa na mke wako ukamuelezea yote, ukweli,
kwanini unayafanya hayo, au ulimtegemea marehemu ndio akuongoze au sio, haya
keshakuongoza, sasa hivi hayupo duniani, utamtegemea nani sasa...ni huyo wakili wako,
hizo pesa zako..kiukweli hadi hapa ni lazima niuseme ukweli wote..na mke wako
ataamua, lakini ukweli ni ukweli tu....’akatulia kidogo, akimuangalia mke wa
familia.
‘Mke wa familia kwanza nikuombe msamaha kwa haya yote yaliyotokea
, pamoja na hayo, mimi nimekuwa nikifanya kazi zako kwa kupitia kwa …rafiki
yako, nimekuwa mtiifu kwako, bila hata ya wewe kunifahamu, ..na zaidi hata mume wangu mwenyewe alikuwa hajui hilo..'akatulia
'Nia na madhumuni yangu ilikuwa
kukulinda wewe na mabaya, kwa vile wewe unaishi na mtu ninayempenda, sikutaka
nyia kama familia yake yawakute mabaya, ndio ilikuwa kazi yangu, na katika kufanikisha hayo nilipitia changamoto nyingi tu,..kuna muda nakaa nalia,..siolii machozi, nalia ndani ya nafsi yangu.....je huo wema ni
nani anaufahamu..’akatulia akigeuka kumuangalia mwenyekiti
Halafu ndio akamgeukia mume wa familia, mume wa familia bado
alikuwa akimuangalia mdada huyo kwa mshangao, kama haamini hayo …
‘ Mimi nilishakuambia toka awali, njia tunayopitia sio sahihi,
ukanikatalia, ukamsikiliza marehemu, ukisema yeye ni msomi anayeona mbali, je
hicho alichofanya ndio kuona mbali huko,...'akasema
Mume wa familia akanyosha mkono kama kumzuia, na yeye akasema
'Usinizui,... naanza kuelezea sasa, je kuna
haja ya kuyaficha haya, hapana ni lazima kila kitu kiwe wazi, unasikia wewe
mume wa familia, ...?’ akawa kama anauliza lakini ilionekana kuwa hakutaka
kujibiwa akaendelea kusema;
‘Mimi nilitumai kuwa umeshajifunza, kwa hayo yaliyotokea, kama
kweli ulikuwa na nia njema, kama sio kunitumia, nichakae,na baadaye uendelee
kuzaa na wanawake wa kila namna.Kama kweli unanipenda…sasa nakuambia hivi..,
turudi kwetu kijijini tukajipange upya, tuachane na maisha yasiyona
mpangilio..’akasema na mume wa familia akatikisa kichwa kama kukataa.
‘Unaona eeh, unakataa, kwanini…, hebu angalia, alichokuwa akikihangaika
Makabrasha kipo wapi, kapata nini na sasa yupo wapi sasa hivi..,je wewe una
uhakika gani na maisha ya kesho na kesho kutwa, kuwa wewe utakuwa mjanja kuliko
huyo aliyemkatiza maisha huyo mtaalamu wako, kama ni mtaalamu kweli mbona
kashindwa kutetea uhai wake ...’akatulia akiwa anamwangalia mume wangu.
‘Mimi nimechoka, siwezi tena kuvumilia, siwezi tena kutumikia
watu.., yaliyotokea yametokea, na yaliyofanyika yamefanyika, hakuna faida
iliyopatikana, sana sana ni kujiweka kwenye maisha ya utata....mimi na mume
wangu tumeshaelewana, na anajua ni nini cha kufanya, baada ya hapa, anaweza
kutoa kauli yake au vyovyote atakavyotaka, mimi sio stahili yake, ...akubali
sikubali huo ndio ukweli,....’akageuka kumwangalia mume wake
Mume wake alikuwa kainamisha kichwa chini tu, na taratibu
muongeaji huyo akamshika mgongoni docta, na docta akashtuka ni kama vile
alikuwa mbali kabisa.
‘Pole sana docta,..unisamehe tu…’akasema hivyo na hapo docta
akainua kichwa na kumuangalia muongeaji, lakini hakusema neno.
********
‘Hivi ni nani anaweza kuyafanya haya yote niliyoyafanya, wakati
mwenzake, anastarehe, na wanawake tofauti-tofauti, anazaa watoto, mimi mpaka sasa
sina mtoto hata mmoja, eti kutimiza ahadi na mipango isiyofikilika, hivi ni
nani, ataweza kuvumilia hayo yote uliyoyafanya mimi kuwalinda wana ndoa hao
huku roho ikiniuma
Hahaha…, ina maana mimi nimeumbwa na moyo wa jiwe, niweze
kuyavumilia hayo yote, sina wivu, sina tamaa, … je hivyo ndivyo
tulivyokubaliana mimi na wewe mume wa familia, tulikubaliana kila mtu aaishi na
mwenza wake kwa heshima na adabu mengine tumuachie mungu au sio...’akamwangalia
mume wa familia, ambaye alikuwa naye amemwangalia kwa macho ya kukata tamaa.
Mume wa familia akageuka kuwaangalia watu, na akiwa kama vile mtu
anayeogopa au kutaka kukimbia, aligeuka huku na kule, halafu akamwangalia
muongeaji na kwa sauti ya unyonge akasema;
‘Sikiliza nikuambie, hapo panatosha usiendelee, utania kwa kihoro, kwanini unarudia rudia huko…haya
yatakwisha tu, na mambo yatakuwa sawa, usiogope vitisho vya hawa watu,
usilainike kwa propaganda zao, mbona mambo yapo shwari tu,...’akasema
‘Hahaha bao tu unajidanganya au sio, nimerudia rudia haya ili yakuguse ili usema imetosha, nakiri kosa, nimejirudi, kumbe naongea na jiwe…’akasema mdada
‘Wewe nisikilize kwanza, usianze kuongea ovyo....utaumbuka,
watakufunga hawa watu, hawana ubinadamu hawa.....’akaongea na kukatiza maneno ni kama vile kaongea
sichokuwa kakidhamiria kukiongea.
Na mara mjamaa akasimama,
sasa akatembea hadi pale aliposimama huyo mdada muongeaji, akanyosha mkono
kumshika huyo mdada mkono, na kusema;
‘Haya simama twende tukaongea kwanza mimi na wewe, tuyamalize haya
mambo, ukiendelea kuongea hapa, utaharibu kila kitu..’akasema
Mwenyekiti wakati huo alikuwa akiangalia matendo hayo kama
anaangalia picha ya kuigiza, huku akitabasamu au kutikisa kichwa, hakutaka
kuingilia kwanza.
‘Sikiliza mtu wangu,…mimi na wewe tumetoka mbali, ina maana yale
yote tuliyowahi kupanga ndio iwe mwisho wake hivi..tutakwendaje kijijini,
tutaishije huko, kwanza mimi ni mume wa mtu, wewe ni mke wa mtu, hulijui hilo,
tulia na maisha yaendelee..’akasema mume wa familia, ni kama vile
kachanganyikiwa.
‘Nimesema nipo tayari kuthibitisha hayo aliyoongea mwenzangu,
kwani mimi ndiye niliyekuwepo toka mwanzo hadi mwisho wa mipango yote hiyo,
japokuwa sio kwa kuitunga, lakini kwa kutumiwa.Mimi nafahamu mipango yote toka
kijijini hadi kuja hapa Dar, mimi namfahamu marehemu, kuliko mtu yoyoye humu
ndani, na mimi namfahamu mume wa familia kuliko watu yoyote humu ndani, kwahiyo
mimi nawajibika kulimaliza hili jambo moja kwa moja, ...’akasema
‘Mume wa familia tafadhali rudi kwenye kiti chako, tusipotezeane
muda..’hiyo sasa ilikuwa kauli ya mwenyekiti, na mume wa familia akiwa kakata
tamaa akageuka kumuangalia mwenyekiti, na hakutaka hata kuniangalia mimi.
Mwenyekiti akawa anawaangalia wawili hao kwa hamasa kubwa, alikuwa
akitaka kusikia mengi kutoka kwa huyo muongeaji, na alifahamu huyo shahidi
ataongea kile alichotaka kukusikia, na iwe mwisho wa kikao, wamalize kazi
.
Mume wa familia akanyosha mkono kutaka kumshika huyo muongeaji,
lakini huyo muongeaji, akauona ule mkono na kuusukuma mbali na..na hapo mume wa
familia,akasema kwa sauti ya ukali;
‘Hivi wewe umechanganyikiwa unataka kuwapa nini hawa watu faida,
unataka kujizalilisha au kunizalilisha mimi, hayo yaliyosemwa bado hayatoshi
....’akasema mume wangu akimsogelea huyo muongeaji, na muongeaji akamsukuma
pembeni, na kumwangalia mwenyekiti, kama vile anaomba msaada, na mwenyekiti
akasema;
‘Mume wa familia, nimeshakuamuru, urudi sehemu yako, ....mpe
nafasi shahidi wetu asema ukweli, tumekupatia sana wewe nafasi uongee lakini
ukakaidi, kwa sasa hivi huna mamlaka ya kumzuia shahidi wetu huyo…’akasema
mwenyekiti.
‘Mwenyekiti nilikuwa naomba nafasi tuongee na huyu mtu kabla
hajaanza kuongea, tafadhali..’akasema akiwa kama anaomba.
‘Nafasi hiyo haipo tena, huyu sasa hivi ni shahidi wa muongeaji
aliyetangulia, wewe si ulitaka shahidi na ushahidi, sasa subiria huo ushahidi
ufanye kazi…kwa hivi sasa tunachohitajia ni ushahidi wa ukweli uliotanguliwa
kuelezewa, hata ukijaribu kumzuia haitasiaidia kitu, mimi namfahamu yeye kama
ninavyokufahamu wewe, kwahiyo sogea pembeni, muachae mwenzako
aongee....’akasema mwenyekiti.
Mume wa familia, akabakia akiwa kaduwaa, hakujua afanye nini tena,
akakaa kwenye kiti kilichokuwa karibu na huyo muongeaji, hakurudi kwenye kiti
chake, akawa kaka huku kainamisha kichwa chini kama alivyokuwa kainamisha
kichwa rafiki yake docta, ..
********
‘Kila jambo lina mwanzo na mwsho wake, mimi nimeona mwisho wa haya
yote ni hapa, na hakuna jingine ila nikuelezea ukweli, na nyie mtaamua
,mtakalolifanya....’akasema muongeaji.
‘Lakini ndugu mwenyekiti mimi nawaomba , muwe makini na mamauzi
yenu, msikimbilie polisi,, kama mtakimbilia polisi, mnaweza msifanikiwe, kwani
huko kote niliwahi kupitia, nikakatishwa tamaa, ndio maana nikaamua kufanya
nionavyo mimi, na sitaweza kuacha kuusema huu ukweli kwenu, hata kama nitakuwa
nimekiuka utaratibu wa polisi....’akasema.
‘Ili kupata ukweli,na kumlinda yule asiyependeka,
nilijitolea maisha yangu, hata kuzalilika,.., nikaamua kuwa na adui yangu, uso
kwa uso, hata kulala naye kitanda kimoja, ili niupate huo ukweli, hii ni moja
ya kazi zangu msije kunidhania vibaya, wanaojua ukweli wa kazi zangu
hawataniona ni mtu wa ajabu,…haha, samahani kwa kauli hiyo,...eti kumlinda
mpenzi wangu, jamani, ....hivi ni binadamu gani angaliweza kuyafanya haya yote,
kwa ajili ya mtu kama huyu...nimakata tamaa, ndio maana nimeamua niseme ukweli,
ili jamii isikie, na watakaojifunza wajifunze, ..’akasema
‘Hapa nilipo natafutwa na polis, ndio mimi natafutwa na polisi au
sio, sitafutwi na polis tu,, ..bali hata wale wanaotaka ukweli huu
usilijulikane,..na mimi ushaidi wangu nitaugawa sehemu mbili, kama alivyofanya
mwenzangu aliyetangulia
‘Sehemu ya kwanza ni lazima nielezee historia na chimbuko la haya,
na pili, jinsi mauaji ya ya amrehemu yalivyofanyika, haya ni lazima niyaelezee
ili haki itendeke, ni kazi kwako wewe mtetezi wa wanyonge ulifanye hili kama
kweli ndivyo ulivyo,....’akasema na kumuangalia mwenyekiti.
Mwenyekiti akwa anamuangalia huyu muonegaji bila kusema neno.
Aliposema hivyo mume wa familai akainua kichwa na kumwangalia huyu
mdada, kwa uso uliokata tamaa, lakini hapo hapo akionyesha ishara ya
chuki..lakini hakwua na jinsi, afanye nini sasa….
‘Kwanini niwaaambie nyie, badala ya kwenda polisi, ...kwasababu,
jamii ndiyo inahitajia ukweli kwanza, na sheria, itachukua mkondo wake,
baadaye, kama watathibitisha kuwa mimi ni mkosaji sawa…’akatulia hapo
‘Mimi nina-amini jamii ndio yenye mamlaka,na ukificha ukweli kwao,
unaikosea, na bora kusema ukweli kwa wale uliowakosea, kuliko kuiacha sheria
ambayo huenda, ikakutaka ufiche ukweli, sheria ambayo wakati mwingine wenye
mali wanaweza kupata mawakili wakafanya haki iwe batili, watendaji ambao
wanaojali masilahi zaidi kuliko haki, nawaogopa sana hao watu....’akatulia.
‘Kuna watu wananitafuta ili waniue,...ili siri isivuje, ili ukweli
usiwe bayana, na hata hii ajenda ya kusema maswala ya mauaji ya Makabrasha
yasiongelewe hapa, ni moja ya ajenda zao,…hamjui tu…’akasema na mwenyekiti
akatikisa kichwa kama kukataa hilo.
‘Sasa kwanini tufiche ukweli, kwanini kama familia tusiuone huo
ukweli, ili mwisho wa siku kila mtu atoke hapa akiwa huru, kwanini tusujue
ukweli ili familia zilizofarakana ziwe na amani, ili wenye haki wapate haki
yao, na wenye kuwajibika wakawajibike..’akatulia
Mfano mnzuri ni kwa huyo kijana wetu aliyetaka kuusema ukweli
hapa, hamjui ni kwanini alikimbia, ..aliona hata angelisema ukweli wote
msingelimuamini, maana mumeshahukumu kutokana na propaganda za aliopanga haya
yote yatokee, lakini atakimbilia wapi, eeh, niambie, najua baada ya hapa
wengine tutaandamwa, lakini mpaka lini,....’akatulia huku akiwa kamwangalia
mwenyekiti, na mwenyekiti akawa anamwangalia bila kupepesa macho,
‘Ndugu mwenyekiti, mimi ndiye mpenzi wa asili wa mume wa
familia...’aliposema hivyo watu wakahema, na wengine wakaguna. Najua wengi
walikuwa wakijiuliza hilo au wakitaka waupate ukweli halisi, ukweli ndio huo…
‘Mume wangu alikuwa halifahamu hilo, kiundani wake, na huenda yalitokea hivyo wengine watafaikiria
kuwa huenda yaliyotokea yalifanyika kama kulipizana kisasi, kati ya mume wa
familia na rafiki yake, hayo wanayajua hao watakaoongea hivyo, lakini undani wa
hayo yote ulikuwa kati yangu mimi na huyu bwana hapa..mume wa familia.
...’akasema na kugeuka kumwangalia mume wa familia ambaye alikuwa hataki hata
kumwangalia.
‘Nafahamu, kikweli kuwa wazazi wa familia ya mke wa familia,
wanatufahamu sana, lakini sio kiundani kihivyo, wao wanatufahamu kutokana na
historia za mababa zetu, na walijua kuwa hata sisi hatutaweza kubadilika, au
sio..
Yawezekana kutokana na hulka ya mtu, kiukweli hata ndoa yangu na
docta haikubarikiwa kivile, hata upande wa mume wa familia ilikuwa hivyo hivyo
tu, na wahanga wa haya ni watu wasio na hatia kama mke wa familia na docta..wao
walitaka kubadili hilo kuwa yawezekana, kuwa watu wanaweza kubadilika, sasa je
yawezekana hilo……….’akasema na kuinama chini kama anayesoma kitu.
Wengi wanajiuliza ni kwanin
matajiri wasitake watoto wao kuolewa na masikini, ni kwanini..kiukweli hii sio
halali, upendo wa kweli hauangaliii maisha ya kifedha, ...umasikini kisiwe
kikwaza ya kuwanyima watu haki zao, za kupendana, ..’akatulia
Naombeni msinichoke maana baada ya hapa huenda tusikutane tena,
huenda mtaniona kwenye kizimba cha mahakama, au mtanisikia nimefungwa
au..nimeuliwa yote yawezekana maana sisi kama sisi hatuna haki,..toka lini
masikini akawa na haki…mmh. Nina imani kama isingelikuwa hizo ajenda za siri,
kuwa kuna watu walikuwa wakilisubiria hili , ili wapike fitina na kufanikisha
malengo yao huenda maisha yanegliendelea…. Mimi na mume wangu tungelikuwa
tunaishi kwa raha na amani....
Sasa ni hivii, ngoja niwaambie kidogo historia za maisha yangu
yalipotokea…
**********
‘Mimi na mwenzangu tumezaliwa kwenye familia za kimasikini,
familia duni, iliyogubikwa na mitihani ya kila namna, sitaweza kuisema , ila
ninachoweza kusema hapa ni kuwa mimi natoka kijiji karibu na kijiji cha
mume wa familia, wote mnalifahamu hilo, na familia zetu ni zile familia zalili sana
huko kijijini.
Na huena ndizo familia za kutolewa mifano, kuwa ni familia duni, zalili
, enye tabia mbaya,…ni nani angakubali kuolewa au kuoa kwenye familia kama
hizo, inayobakia ni ndoto za Alianacha, kuwa siku moja nitamuoa, au kuolewa na
binti mfalme, au mtoto wa mfalme,...na ndio ilikuwa ndoto yangu na
mwenzangu!
‘Lakini kwa mipango iliyopangwa, na makubaliano, kati yangu na
mwenza wangu, tukajikuta sote tukiingia kwenye familia zenye uwezo,
kutokana na zile njozi zetu,.. japokuwa kiundani mimi na mwenzangu tunapendana
sana, pendo la asili, ambalo tuliwahi kulifunga kwenye handaki la umasikini....baada
ya kuvikana pete ya uzalili, na umasikini, tulikaa na kujadili hili, hivi sisi
mpaka lini.
Mjadala ulikuwa wa kulalamika, ...ina maana sisi tutakuja kuishi
kama walivyoishi wazazi wetu, ina maana watoto wetu watakuja kuzalilika, na
kuishi maisha ya umasikini kama tulivyourithi kwa wazazi wetu, tukasema hapana,
..
Hapana sasa tufanyeja wakati kweli tunapendana,..tufanye nini ili
nafsi zetu zije kufurahia, tukaota ndoto, tukamuomba mungu, …tukasubiria ndoto
hiyo ya aalinacha,.....oh..’hapo akatulia kwa muda akiwa kainamisha kichwa
chini kama anawaza jambo, na alipoinua kichwa machozi yalionekana machoni,
akasema;.
‘Samahani mimi sio mtu wa kulia lia ovyo, huwa nalia moyoni, na
ukiona machozi yananitoka usoni, ujue kuna jambo nzito kuliko uzito wenyewe,..haya
yamenitoka tu kwa bahati mbaya,...hayatarudia tena...’akasema na kufuta yale
machozi, akaendelea kuongea;
‘Tulijadili sana, jinsi gani ya kuwapata matajiri, je inawezekana
kweli, mimi niolewe na tajiri, utawezaje kumshawishi tajiri kuja kunioa mimi,
au utawezaje kumshawishi binti wa geti kali kuja kuolewa na mlalahoi kama
mwenzangu alivyokuwa...huwezi kulazimisha pendo, au sio, lakini bahati nzuri
ikatokea kama dhamira zetu zilivyokuwa, kila mmoja akapata tarajio lake kwa
nyakati tofauti, huena ilitokea hivyo ili iwe sababu ya watu kujifunza....
‘Wa kwanza kumpata mwenza ilikuwa ni mimi, nikampata mume mwenye
uwezo, na nikamwambia mwenzangu kuwa nimempata mume mwenye uwezo sasa tufanya
nini,..’akageuka kumuangalia mume wa familia.
‘Mwenzangu akapagawa na kukasirika, wivu ukamjaa, siunawafahamu
wanaume kwa wivu, akasema haiwezekani, akawa kasahau makubaliani yetu, na
wakati tunapingana, tukiwa tumenuniana siku mbili tatu,, mwenzangu akiwa hataki
hata kuongea na mimi akakutana na binti wa kitajiri kwa mazingira yaliyokwisha
kuelezewa huko nyuma..wakajikuta wame...mtamalizia wenyewe..’akacheka kidogo.
Haraka akaja kwangu na kuniambia kuwa hata yeye kampata mwanamke,
tajiri, kwahiyo tupange mipango yetu,....mwenzangu kwa haraka, akamwelezea
mshauri wake…mnamfahamu eeh…?’ akauliza na ajumbe wakaguna tu.
‘Mshauri wake, ni jamaa mmoja msomi, kijiji kizima wanamfahamu
msomi wa hadi nje ya nchi. Na huyo jamaa alipoambiwa hivyo, akamwambia
mwenzangu ampe huyo jamaa muda wa kulifanyia hilo kazi. Akalisafiria hatujui
huko alifanya nini, alikutana na nani, …alipokuja akaongea na mume wa familia,
walichoongea wanakifahamu wenyewe.
Basi siku yake akatuita, na kutuweka kikao, akasema;
‘Mnafahamu hiyi ni bahati kubwa sana, sasa umasikini bai-bai, kama
mtafuata masharti yangu, mtafanikiwa lakini mkiwa wajinga, makajikanganya kuwa
..ooh, nimeolewa, ooh, nimemuoa, tajiri, mtakufa na umasikini wenu, kaeni
mkijua kwa tajiri hakuna urafiki wa kudumu...’hiyo ilikuwa kauli ya huyo
mshauri wetu, nikaona hapo tumefika.
Sasa ngojeni kuna mambo yanafanyiwa kazi, ..hiki ni kipindi cha
kujiandaa na kampeni, kwahiyo tuvute muda kwanza, mimi nikajiuliza kampeni na
mapenzi yetu yanahusikanaje,…sikumuuliza ila tulimkubalia tu..
Baada ya muda akasema anasafiri na akija atakuja na mambo mazuri,
na pesa za maandalizi ya harudi, ili na sisi tuonekane tumeolewa, au kuoa, sio
kuchukuliwa kama mzigo tu..tukakubali, …
Baada ya siku mbili, huyo mshauri akaja na mikakati ya jinsi gani
ya kufanya....
NB: Tuishie hapa kwa muda
WAZO LA LEO: Ukweli unauma, lakini ukweli ni njia ya
kujisafishia njia ya uhalali wa mafanikio, tusiogope kuongea ukweli hata kama
katika kuongea huo ukweli utajiumiza hata wewe mwenyewe. Ukweli ni haki, na
haki yataka ukweli.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment