‘Hayo sasa tutakuja kuyaongea akifika muhusika, ambaye ataweka kila kitu
sawa….unajua mke wangu nataka kila kitu sasa kiwe kwa namna ambayo, hakuna mtu
ataumia,..nafanya haya kama mume wa familia….
‘….Je ni kweli una mtoto nje…na ni nani
huyo…?’ ,
Wakati anataka kujibu swali hilo mara…wakaingia madocta na nyuma yao,
akaingia mtu, mtu ambaye alinifanya nipandwe na hasira, ..
Ni nani huyu…
Tuendelee na kisa chetu…
**************
Ungeliniona nilivyokuwa nimeshikwa na butwaa ndio ungelifahamu
haya ninayokuambia hivi sasa…, maana akili yangu ilishahamanika, niliposikia
mume wangu kama vile anataka kukubali au kukataa kuwa ana mtoto nje ya ndoa, na
huo ndio ungelikuwa ni shahidi wangu mkubwa, ama kwa heri au kwa shari..
Kiukweli hadi muda huo nilishaamua moja, kama ni kweli hayo
wanayoyazungumza watu basi mkataba ungelifanya kazi yake,..ama kama ni uwongo,
kuna mambo mengi yangelinifanya nianza kukosana na marafiki zangu kuwa wao
wanataka kuivunja ndoa yangui…ila nilichohitajia kwangu kikubwa ni ‘ushahidi..’
Kauli ya mume wangu ingelikuwa ni ushahidi tosha, wa kumaliza
matatizo haya yote kichwani mwangu,angekuwa mkweli, huenda ningeliumia, lakini
mwisho yangelifikia muafaka, lakini kwanini hataki kuniambia ukweli, hapa
nabakia na swali kubwa kichwani, je ni
kweli mume wangu kafanya hivyo, ina maana alisahau huo mkataba, na sikuwezi
kupata jibu hilo, maana mbele yangu kulitokea tatizo jingine…
Mawazo yangu yalikatishwa na huyo jamaa, aliyeingia, kumuona yeye
tu, nilijua kuna tatizo, na tatizo hilo sio dogo,…hapo akili ilishtuka, na
kuharibu mawazo yote niliyokuwa nayo kichwani…!
Cha ajabu hata baada ya wale wengine kuingia ndani, wao waliingia
na moja kwa moja wakaja pale tulipo kwa mgonjwa, ambapo mimi nilikuwa nimesimama
karibu naye, lakini huyo jamaa yeye baada ya kuingia alipiga hatua moja ,
mbili, halafu akasimama karibu na mlango, na mbali kabisa kutoka pale
tulipokuwepo sisi, hakusogea ..
Nilibakia nimeduwaa, nikimkodolea macho huyo jamaa, kiukweli sikutatarajia
kumuona huyu mtu tena katika maisha yangu…baada ya tukio lililotokea huko nyuma
baina yangu mimi na yeye,..na nakumbuka kwa mara ya mwisho nilipokutana naye,
hatukuachana vizuri kabisa, nikakumbuka kauli yangu kwake;
‘Sitaki kuja kuonana na wewe tena, …sikutaki kabisa na ukumbuke
hili, siku nikija kukutana na wewe tena, nitahakikisha nakufungulia mashitaka
ya utapeli, na uwongo, na nitahakikisha, unakwenda ndani, na ukitoka jela,
hutajishughulisha tena na utapeli wako huo….’nikamuambia hivyo kwa hasira.
‘Na pia nakutahadharisha,..mimi nitakuwa nakufuatilia, hatua kwa
hatua,…mimi nakuonya uwe mbali kabisa na mume wangu..unanisikia wewe tapeli…’nilizidi
kumpa onyo na kwa muda huo hakuwa na cha kusema, bali ni kukaa kimia tu.
‘Kama nikikuona upo karibu na mume wangu, nitahakikisha ninakumaliza
kwa mikono yangu mimi mwenyewe…na nitaanika mabaya yako yote hadharani….’nilimwambia…kiukweli
nilikuwa nimeshamfahamu alivyo na jinsi anavyofanya kazi zake, na ushahidi wote
nilikuwa nao…
‘Samahani sana..ni makosa yalitokea, sitarudia tena….’alijitetea
hivyo
‘Sina haja ya samahani yako, ondoka mbele yangu…’nilimuambia hivyo
tukiwa ofisini kwangu na alitoka haraka na sikuweza kuonana naye tena, mpaka
siku hii ya leo.
Jamaa aliendelea kusimama pale, hakusogea hata hatua moja kuingia
ndani, sasa sikufahamu ni sababu ya kuniogopa, au alikuja kwa malengo yake
binafsi.
Kama kawaida yake, alikuwa kavalia mawani meusi machoni, akificha
unafiki wake, mkononi akiwa kashikilia mkoba wake mweusi, mkoba ambao umekuwa kama
sehemu ya mkono wake, maana popote utakapokutana naye, huo mkoba upo mkononi,
sijui ndani yake kuna nini!
Kwa muda ule mimi nilikuwa nimeshikwa na butwaa, mwili ukinicheza
cheza kwa hasira, mdomoni nikitaka kutamka jambo au kupiga ukelele wa hasira…,
lakini sikuweza kufanya hivyo , nikiheshimu mamlaka ya hapo, kuwa hapo ni
hospitalini.
Lakini pia sikuweza kufanya jambo, nikichelea matatizo ya mume
wangu…kiukweli isingelikuwa hayo mambo mawili, ungelisikia mengine, nahisi
ningelipiga ukele, au kwenda kumvaa huyo jamaa kwa hasira, lakini kwa muda huo na sehemu kaam hiyo,
ilibidi ninywee tu, na kuumia na hasira zangu moyoni
Baadaye nikageuka
kumwangalia mume wangu nisikie anasema nini,...kwani kwa muda huo
alishamalizana kusalimiana na walioingia humo ndani kasoro huyo jamaa.
Mume wangu aliponitupia jicho, akaiona hiyo hali usoni mwangu,
nilishabadilika, hasira zote zilikuwa usoni mwangu, alitarajia kuwa
ningelifanya jambo, la kumvaa huyo jamaa au kuongea kwa hasira, lakini hilo
halikutokea, alishangaa kuniona nimesimama tu, siongei neno, ila uso wangu
ulionyesha kila kitu…
Mume wangu akasema;
‘Mke wangu samahani sana, nafahamu hupendi kabisa kumuona huyo
mtu..na nafahamu ni kutokana na yale yaliyotokea kipindi kile..na hayo
yaliharibu sifa zake..lakini hukutaka kuyafuatilia zaidi kuwa yeye hakuwa na
kosa, kama ni kosa basi labda ungelinilaumu mimi, unanielewa hapo, lakini
hukutaka hata kunisikiliza…’akasema kumtetea huyo jamaa.
‘Mimi namfahamu sana rafiki yangu huyu,…ndio kuna wakati mwingine
anafanya mambo-mambo, lakini sio kwa kupenda yeye, wakati mwingine ni kutokana
na mteja wake anavyotaka yeye…anajulia namna za kuweza kumsaidia mteja
wake,…’akatulia
‘kwa hali kama hiyo, yeye yupo tayari kuingia kwenye hatari, ili
kukidhi matakwa ya mteja wake…na wakati mwingine anahatarisha taaluma yake,
lengi ni kusaidiana, anatufahamu maisha yetu sisi watu wa kawaida, na anafahamu
maisha ya watu wliopo kwenye dhiki..au kukwama kwa namna hii au ile, maana sisi
wanadamu tuna madhaifu yetu…’akaendelea kuongea lakini mimi hayakuniingia
akilini.
‘Kwa namna hiyo na nyingine wale maadui zake, na wasipomtakia
mema, wamefikia kumharibia jina lake…, lakini afanyeje kama mteja wake anataka
hivyo, na kama mtu kaja kumlilia hali, mtu kama huyu anatusaidia sana sisi watu
tuliokwama, ni vyema tukamfahamu hivyo, japokuwa upande wa pili watamsakama
sana…’akatulia
‘Sisemi haya kuwa wewe ulitaka kufanya mabaya, kwa kupitia kwake,
hapana, ila kwa taarifa alizozipata,…’akataka kuendelea mimi nikaonyesha mkono
wa kukataa hayo maelezo yake nikasema
‘Please,..bsi basi inatosha,…mimi sitaki tena kusikia hayo maelezo ya huyo mtu, mimi namfahamu
vilivyo,..hakuna mtu anayeweza kunidanganya lolote, sijafanya makosa …namafahamu..kwahiyo
sijui kaja hapa kufanya nini..’nikasema
‘Mke wangu ..najua wewe hurudi nyuma, unamuamini sana rafiki yako,
au sio…lakini nikuambie kitu,….lakini hayo tuyaache kwanza, maana hayo
yalishapita au sio..’akasema na kutulia kidogo
‘Hata hivyo kutokana na hayo yaliyotokea…eeh, yanaweza kuwa ni
sababu, kwani huko yanapoendea, kunaweza kukazuka sintofahamu eeh..nashindwa
kuelezea kiuwazi zaidi..kisheria, si unajua membo mengine yapo kwenye mkataba,
yanahitajia sheria, na..na..ndio maana, nimeona huyu mtu aje kunisaidia, …,
yeye, ni rafiki yangu wa siku nyingi, namuamini sana kuwa atanisaidia kwa
hilo…’akatulia
‘Kukusaidia, kwani una kosa gani mume wangu…..?’ nikamuuliza sasa
kwa hasira , na hapo mume wangu akaonekana kunywea, lakini kwa haraka akajirekebisha
kuonyesha nafasi yake akasema;
‘Ndio hivyo, makosa yap ndio maana nikakuomba msamaha,..au sio,
lakini haya yatasemwa baadae kwa muda muafaka, ngoja nimalizane na huyo mtu…yeye
nimemuita ili aweze kulisaidia hili…’akamuangalia jamaa
‘Huyu jamaa namuaminia…, yeye anajulia sana mambo ya mikataba hasa
ya kifamilia kama hii ya kwetu ya kienyeji enyeji, iliyotengenezwa kimtego
mtego…na pia ya kikazi, na anaweza kufahamu madhaifu ya mikataba hiyo na lipi
lifanyike ili kuirekebisha, bila kuleta matatizo makubwa, anajua njia zote kwa
jins tunavyotaka sisi umenielewa hapo…’akasema
‘Kwanini unataka kufanya hivyo..?’ nikamuuliza
‘Kama nlivyoanza kukuambia awali, mke wangu..nielewe..sitaki
tuongee sana kabla sijaweka haya mambo vizuri, lakini ni hivi.., huo mkataba wa
kimtego,…una mapungufu mengi, na ..ukifika kwa baba yako, kashapata panga la
kukata mti..na huo mti ni nani, sio mimi kweli..ndio hivyo, sasa nikimalizana
na huyu jamaa, nitakuja kuakuambia kila kitu,... ila kwa hali ilivyo inabidi
kujihami, sipendi kazi zetu zote zionekane hazina maana, …na mume nipo, ni aibu
jamani...ni lazima sasa nishike hatamu…’akasema akitikisa kichwa kama kukubali.
‘Mume wangu unajua unajizalilisha wewe mwenyewe, mambo ya ndani
unamtafuta wakili wa kazi gani, umeua..umafanya kosa gani kubwa kihivyo…’nikasema
‘Hapana, ..sijaua..lakini aheri uneliua, ikajulikana
moja,…nafahamu kabisa mbele ya baba yako, naweza kuonekana kama muuaji
tu….nitazalilika, …na, nitakimbilia kujiua…si umeona hapo…ila mke wangu haya ni
mambo ya kawaida tu,..utakuja kunielewa, wala usipate shida, niachie mimi,
nitayaweka sawa, mwenyewe utakuja kuona…’akasema
‘Sitakuelewa kamwe,…na kwanini unafanya hivyo, kwa hali uliyo
nayo, kwanini hujionei huruma, na kama wewe hujijali, kwanini usiwajali wanaokuhangaikia,
eeh, hili …mume wangu…hapana, hapa kiukweli umevuka mipaka…’akasema
‘Mke wangu, niamini, …si unaniamini,..sasa endelea kufanya hivyo,
utaona manufaa yake, mengine nitakuja kukuambia nyumbani,..huyu mtu sivyo kama
unavyomfikiria wewe, na kutokana na hali zetu kuwa sio nzuri kibiashara, yeye
kajitolea kwa gharama ndogo tu, na haya tutayayamaliza haya mambo kwa haraka
iwezekanavyo...’akasema mume wangu.
‘Mimi, sikuelewi na sitakuelewa, na sipo kabisa na mambo yako,
samahani kama nitakukwaza, ila kwa huyu mtu, sipo tayari kushirikiana naye kwa
lolote lile,…’nikasema huku nikimuangalia docta rafiki ambaye kwa muda huo naye
alikuwa kama kachanganyikiwa.
Wakati huo docta yule
aliyekuwa akimshughulia mgonjwa alishaondoka, na alisema atarudi baadae kutuambia
cha kufanya kama nikuondoka na mgonjwa, au bado anahitajika kuendelea na
matatibabu.
‘Mke wangu…usiwe na wasiwasi kabisa…haya nitayamaliza tu, ngoja
docta aje kama ni kuniruhusu haya, kama ni kuendelea kubakia hapa , sawa ,
lakini kabla ya mimi kuondoka hapa, ni lazima mambo fulani yafanyike ili huyu
mtu aondoke ..na kuanza kazi yake…’akasema
Mimi pale nikakaa kimia,…baadae nikageuka kumwangalia docta. Docta
rafiki, alikuwa bado kakaa kimia, na sasa akimuangalia rafiki yake kwa makini…,
na baadae akaniangalia mimi,..na muda huo ndio na mimi nageuka kumuangalia yeye
nikitaka asaidie kwa hili. Macho yakakutana…
***************
Docta rafiki alipoingoa mara
ya kwanza, alichofanya yeye, baada ya kusalimiana na rafiki yake, alijitenga
pembeni, ..lakini pembeni mwa kitanda kama kutupatia nafasi, na muda mwingi
alikuwa katulia huku kainama chini, kama vile hataki kuingilia mambo yetu,
lakini akiwa tayari kutoa msaada ..na kila alipoona napandisha hasira, alikuwa
akinitupia jicho, la kunipa tahadhari…lakini
kwa muda huo mimi sikujali tena,.., nikamgeukia mume wangu.
‘Mume wangu huko unapokwenda ni kubaya, nakuomba tena tuyaache
haya mambo mpaka upone, tafadhali, usije ukafanya mimi nikaja kuonekana
mbaya…’nikasema
‘Wala usijali mke wangu hakuna baya litatokea,…uwe huru tu..lakini
hili lazima lifanyike…’akasema
‘Hili lipi….weka wazi….na sijui kwanini mume wangu unayafanya haya
yote..ina maana una kosa gani kubwa mpaka unadhamiria kuyafanya haya yote,
wakili, wakili wa nini…sijakuelewa bado…?’ nikamuuliza
‘Wakili ndio…ila kwa sasa usiwe na papara, utakuja kujua kila
kitu…nimeshakuambia dhamira yangu kuwa ni lazima apatikane mtu wa kuyaweka haya
mambo sawa, ya ndoa, mali na kadhalika, kuna mkataba au sio, je upo sawa..sasa
nilazima nimpate mtu sahihi wa kunishauri…na nimeonelea mtu wa ngu sahihi huyo
jamaa…’akasema
Nilitaka kugeuka kumuangalia huyo jamaa, lakini hata kichwa
kikasita kufanya hivyo…nikasema;
‘Mume wangu kwani wewe una wasiwasi gani, mimi nipo kwa ajili
yako, na kama unahisi kuna tatizo, mimi nitasaidiana na wewe kulimaliza hili au
sio,....mimi sioni umuhimu wa kumleta mtu mwingine kwenye mambo yetu ya
nyumbani, tulishasema haya ni yetu wawili, sasa huyu mtu ni wa nini…, jaribu
kujionea huruma wewe mwenyewe kwanza, ....!’nikasema.
‘Mke wangu usione nayafanya haya kwa kuwa labda nimependa, …hapana
nimejikuta sina jinsi, na nikiyaachia, nitakuja kudhalilila…hapana, hapa
ilipofikia ni lazima na mimi nifanye jambo…’akasema
‘Ufanye jambo gani,…weka wazi,…na kama kweli kuna tatizio kubwa
kihivyo, na mpaka haya yote yanatokea, utuambie ili na sisi tuweze
kusaidia,..uliua, hapana, ulifanya nini basi…haya kama ni hivyo, kwanini haya
yafanyike hapa hsopitalini,… basi subiria tutoke hapa, tukifika nyumbani
tutakuja kuayaongea haya vizuri…’nikasema nikijaribu kujishusha
‘Hapana mke wangu tulishaongea yote na huyu mtu, sasa hivi kaja
ili kumalizia hili jambo kwa ujumla wake, …ukitaka unaweza kubakia, kusikiliza
kila tutakachoongea, lakini kama hutapendelea, basi, nitakuja kukuambia
tulichokubaliana,..lakini vyema na wewe ungelikuwepo, maana mim nimekuwa mtu wa kuumwa, umwa,..sasa
lini litafanyika hili,naona sku zinakwenda, na baba yako anazidi kuwa
juu..hulioni hilo, ..ngoja tulimalize hili kabisa leo hii hii,..’akasema
‘Mimi sikubaliani na hilo kabisa, unasikia, wewe kwa vile umeamua
kwa masilahi yako, wewe endelea na huyo mu wako, na mimi usinihusishe kwenye
makubaliano mtakayofanya na huyo…na nasema hivi kama una nia njema na hayo
unayotaka kuyafanya, basi subiria tufike nyumbani kwanza...’nikasema.
‘Mke wangu kwa hatua ilipofikia hatuna jinsi, inabidi tukubaliane
na huyu mtu, vinginevyo, mambo yataharibika, nielewe hivyo, na niamini
hivyo,mwenyewe utakuja kuona....’akasema
‘Tukubaliane na yeye, una maana gani hapo na ni mambo gani hayo
yataharibika…?’ nikamuuliza
‘Ndio nasema utakuja kujua lakini kwa hivi sasa siwezi kukuambia
lolote uniamini tu..’akasema
‘Nakuuliza hivi, kwani huyu mtu ndiye anakulazimisha kufanya
hivyo, au ni kwa utashi wako wewe mwenyewe, niambie kama kuna kitu nyuma ya
pazia, nifanye kazi yangu, huyu mtu mimi hanibabaishi kwa lolote lile, ninamfahamu
sana ni mbabaishaji tu, ni tapeli huyo, utakuja kujutia, umeshachelewa…’nikasema
‘Mke wangu mimi nakupenda sana, na sitaweza kuachana na wewe, hilo nimeahidi , sio bab yako wala kitu gani kitavunja ndoa yetu,.. nafahamu hata wewe unanipenda pia, au sio…?’ akasema kama kuniuliza, sikumjibi
kitu
‘Sasa. kwa ajili ya ndoa yetu, kwa ajili ya maisha yetu na familia yetu, na watoto wetu,...mimi siwezi kukubali mambo mengine yaje kutuingilia,...nafahamu kabisa nikikaa kimiya hilo litatokea, na....sijui itakuwaje
kama likitokea...ni nani wa kualaumiwa kama sio mimi,...hapana mimi siwezi kukaa kimia, ni bora nijitetee mapema,...’akasema na akawa anakunja uso kama
anahisi maumivu fulani.
Nikageuka kumuangalia docta, na docta akawa naye anamuangalia mume wangu kwa mashaka...akageuka kuangalia kule wanapokaa madocta, kulikuwa hakuna mtu, halafu akaniangalia mimi...
‘Mke wangu wewe niamini mimi..na sifanyi hili eti kwa shinikizo la
mtu, kuwa eti labda huyo jamaa kafanya jambo kunirubuni, hapana hakuna kitu kama
hicho, huyo ni rafiki yangu hawezi hata siku moja kunifanyia hivyo, haya yote
nayafanya kwa masilahi ya familia, kwa utashi wangu mimi mwenyewe…’akasema mume
wangu.
‘Sizani kama nitakuelewa, na aah, hata sina hamu tena ya kuendelea
kukaa hapa, mimi nataka kuondoka, kama ..oh, docta alisema tumsubirie, ok, au..?’
nikasema nikiwa nataka kuondoka, nikamuangalia docta rafiki, naye akawa ananiangalia
kwa uso wa kunionya kuwa niwe makini.
‘Mke wangu usiondoke kwanza tafadhali…, maana sizani kama
nitaendelea kulazwa hapa, kiukweli hata mimi mwenyewe nataka kuondoka hapa...,ikibidi
leo hii….docta kaniambia hali yangu imeshatengamaa, sasa nikae hapa kufanya
nini..mambp yangu yanalala,..na ndio maana nimemuita huyu mtu, aanze kunisaidia
yale mambo yanayoweza kuleta madhara kwenye familia...’akasema.
Alipoongea hivyo, nikageuka
kumwangalia docta rafiki. Nilimona kainama vile vile, nikamsogelea pale
aliposimama, na yeye akainua kichwa taratibu na kuniangalia machoni, huku akiwa
nusu kutabasamu na nusu kuonyesha mashaka fulani, lakini bado nilikuwa
sijamuelewa, kuwa yupo na mume wangu au yupo na mimi,mimi nikamwambia kwa sauti
ya chini chini ili mume wangu asisikie;
‘Hivi huyo mtu mumemchukulia wapi,…?’ nikamuuliza
Docta rafiki akamtupia jicho yule jamaa , huku mimi naendelea
kuongea
‘Hivi si nyie mlionionya kuwa hali ya mume wangu haihitajii mambo
ya kugandamizwa kimawazo, sasa hamuoni kuwa kwa hali kama hii tunaweza
kumuathiri mgonjwa, au kuna jambo jingine mumelipanga mimi silifahamu...?’
nikamuuliza
Docta rafiki,..akatulia kama anawaza jambo, halafu, akageuka
kumuangalia mume wangu,…mume wangu alikuwa kainamisha kichwa chini,
hatuangalii, ni kama ananiacha niongee na docta, na hakuwa na wasiwasi na hilo
Docta rafiki, akageuka kumwangalia yule jamaa tena pale
aliposimama karibu na mlango, alikuwa kasimama pale pale, hajasogea hata hatua moja, na vile vile alivyokuwa kasimama awali ni hivyo hivyo.. docta akawa anauangalia kwa makini, tatizo yule jamaa
alikuwa kavalia mawani meusi, kwahiyo huwezi kufahamu ana hisia gani machoni…
Baadae docta akanigeukia na kunitizama machoni, na kwa sauti ndogo
akasema;
‘Mimi sijui kabisa ni kitu gani kinachoendelea hata mimi nimebakia
kuduwaa, mpaka sasa nawaza kuna kitu gani kinachoendelea...sijui kuna tatizo gani kubwa limetokea kwa rafiki yako mpaka kufikia hatua ya kumuita huyo mtu, kiukweli bado
nipo gizani…’akasema
‘Siwezi kuamini hilo…kuwa wewe hujui, rafiki yako hawezi kukuficha,
ninajua wewe unalifahamu hili, mumelipanaga hili, kwa dhumuni fulani, basi niambieni
na mimi, ili niufahamu huo ukweli…’nikasema
‘Ina maana huniamini mimi, ..mimi sijui kitu, muulize mume wako,
hili ni lake yeye mwenyewe, na …kiukweli, limenishtua na mimi…’akasema docta, na
mgonjwa aakinua uso kutuangalia, na docta akasema
‘Tunateta kidogo na mke wako,…samahani lakini…’akasema docta
‘Ongeeni tu , tena ni vizuri,..mshauri afahamu kuwa mimi ni mume wake,..na haya nayafanya kwa ajili ya familia yangu..unajua mimi nataka haya mambo tuyamalize yote leo hii hii, hebu mshauri ili tulimalize hili tatizo..., najua wewe ni rafiki mwema kwetu..’akasema mume wangu.
'Ukisema hivyo unanifanya kama vile nafahamu unachotaka kukifanya....'akasema docta
'Hapana,...simaanishi hivyo, nataka wewe umshauri aakubale yale ninayotaka kuyafanya, kiukweli wewe hujui lolote kuhusu hili, ni mambo ya kifamilia, lakini wewe unaweza kumshauri, akakubaliana na mimi...'akasema
Docta akaniangalia mimi...na mimi nikasema;
‘Nakuapia kama unajua lolote kuhusu hili, mtapambana na mimi….nikitoka
hapa naenda kuongea na baba, tuone hatima ya haya mambo itafikia wapi, maana
kiukweli nimechoka, nimevumilia na kila hatua inakuwa aheri ya jana, na mimi ni
binadamu jamani ….’nikasema
‘Usifanye vitu kwa pupa, najua ukilifikisha kwa baba yako hivi kama lilivyo, utakuwa
umeharibu kila kitu,...tafuta ni nini kinachoendelea kwanza, ili uwe na uhakika, je kama mume wako ana kusudia jambo jema,...huwezi jua, na mwache baba yako afanye kivyake, ipo siku mtakaa meza moja
mtayamaliza, nina uhakika na hilo….’akanishauri docta.
‘Kwanini kwanza mkamruhusu huyu mtu kuingia ndani..hapo ndio
nasema hata wewe unalifahamu hili, sio vizuri mlivyofanya…’nikasema
‘Nikuambie,…huyu mtu alipofika alisema kaitwa na mume wako…nasikia
mapema tu,alimwambia docta kuwa kuna mgeni wake atafika, kwahiyo, akifika
aruhusiwe kuingia, kwani yeye ana mazungumzo muhimu na huyo mtu, ambayo
yanamsumbua kichwa chake...’akasema rafiki wa mume wangu.
‘Na wewe ukakubali kirahisi hivyo..ulitakiwa kwanza uje uongee na
mume wangu, au uniambie mimi ili nikupe ushauri, maana huyo mtu namfahamu sana
mimi…hebu niambie tukianza kuzozana hapa, huoni lolote laweza kutokea, maana
mimi kiukweli sitakubaliana na haya mambo...’mimi nikasema.
‘Mimi nakushauri uvute subira ufahamu wanachotaka kukifanya,…na
mimi nisingeliweza kumzuia huyo mtu, nilijua bado ile hali tete ya mume wako
bado ipo na ukizuia jambo analolitaka yeye,..inaweza ikamuathiri mume wako...’akasema
‘Mhh…siamini, …kuna nini lakini…’nikasema
‘Hata huyo jamaa sisi tulimtahadharisha, kuwa hali ya mume wako
haitaki mawazo mengi kama kaja na mambo yenye utata, ni bora yasubirie, lakini alichotuambia sisi wenyewe tulibakia hatuna
jinsi…’akasema
‘Kasema nini…?’ nikauliza
‘Kasema hiyo hali aliyo nayo mume wako, yeye pekee ndiye anayefahamu jinsi gani ya
kuimaliza, keshaongea na mume wako na keshajua tatizo lipo wapi, kwahiyo yeye,
kaja kumalizia makubaliano, na ana uhakika atayamaliza matatizo yanayomsumbua
mume wako, hebu tuambie sisi hapo tungelifanya nini..’akasema rafiki wa mume
wangu.
‘Huyo ni tapeli mkubwa, anajua kucheza na hisia za watu, ni kama
mchawi fulani hivi..namfahamu sana…nahisi kuna kitu..lakini ngoja tu,
nitakigundua, kwa vyovyote vile, na ataishia kubaya..’nikasema
‘’Usichukulie jaziba…’akasema docta,
‘Wewe subiria uone…nitafanya jambo, ananitambua nilivyo, wewe
subiria uone…’nikasema na sasa nikasogea pale nilipokuwa awali, na kumuinamia
mume wangu…nilimuangalia moja kwa moja usoni, lakini yeye akawa ananikwepa
tusiangaliane machoni…kama ananionea aibu, …sikujali, nikamuuliza;
‘Mume wangu nakuomba tena, huyu mtu aondoke hadi hapo hali yako
itapokuwa salama, kama kuna lolote niachie mimi, nitaongea naye, nahisi kuna
kitu kakufanyia, au kakutisha nacho, huyu mtu ni tapeli, na mimi namjulia,
unaisikia.....’nikamwambia kwa sauti ya chini chini, na yeye akasema;
‘Mke wangu, usiwe na wasiwasi,....mimi nimeshaongea na huyu jamaa,
na sivyo kama unavyofikiria wewe, nahisi uliyoyasikia kwa watu ndiyo
yamekufanya ufikirie hivyo,…sikiliza yeye
kufika kwake hapa ni kwa vile mimi ndiye nimemuita. Na nilishawahi naye kabla…,
na leo, kaja tumalizane…yeye kaja kwa nia njema tu, ya kunisaidia..ya kutusaidia
ili haya mambo yaishe kwa amani. ..na hatakuwa na muda mrefu,…nakuomba uondoe
wasiwasi dhidi yake…’akasema.
Nilikaa kwa muda, nikiyawazia haya, nikainua kichwa kugeuka,
kwangalia docta rafiki wa mume wangu, ambaye alikuwa akituangalia tunavyoongea
na mume wangu, na aliponiona nipo kimiya,akataka kunisogelea nahisi alitaka
kunisihi jambo.
Mimi niliona nisipoteze muda, kwa haraka nikatoka pale na kutembea
hadi pale alipokuwa kasimama jamaa…jamaa alikuwa kasimama vile vila hakujali
kuwa nakuja mbele yake, hadi nilipofika pale aliposimama. Na niliona kama
anataka kusogea nyuma, lakini hakufanya hivyo, akatulia, akisubiria nitafanya
nini….
NB: Sehemu nyingine inakuja soon
WAZO LA LEO: Ukiwa na hasira usifanye jambo kwa pupa,
hakikisha umetuliza hasira yako kwanza kabla ya kuchukua maamuzi, mara nyingi
ndani ya hasira ibilisi hachezi mbali, na hasira inaweza kuwa ni hasara.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment