‘Jibu
maswali yangu kama wewe ni wakili unayejiamni, ...kama huna hatia mbona
unaogopa,kuyajibu maswali yangu ...’akasema mpelelezi
‘Nimeshakujibu
maswali yako yote muhimu kwa sasa, hasa yale ninayostahili kukujibu kwa hapa,
kama kuna maswali zaidi ya hayo nione ofisini kwangu, au kama unaona nina kosa
nishitaki, mimi nitakuja kujieleza huko kituoni, lakini hayo uyafanye kwa
kufuata utaratibu, sio kihuni huni tu,...’akasema na kuanza kuondoka, na
mpelelezi akamuendea na kumshika begani
Yule
wakili akatulia na taratibu akageuza kichwa kukabiliana na huyo mpelelezi, na
nilijua kitakachofuata hapo ni ngumi,...
‘Usiondoke
mimi sijamalizana na wewe...mu-he-shi-miwa, ’akasema mpelelezi na yule wakili
akageuka mzima mzima huku akiusogeza mkono wa mpelelezi pembeni na kusema;
‘Naona
sasa unataka kunipanda kichwani, nimeshakuambia kuwa kama unataka kuongea na
mimi kisheria, fuata utaratibu, mimi ni mtu nineyeheshimika, mimi ni wakili, na
ninajua sheria ni nini, ...usitake tuharibiane....’akasema
‘Nakufahamu
sana, na ndio maana nyafanya hayo..na kama unakubaliana na mimi kuwa na mimi ni
mpelelezi ninayefahamu kazi yangu vyema, tulia uyajibu maswali
yangu....’akasema mpelelezi.
‘Nimeshakuambia
fuata utaratibu, ili nijibu maswali yako kisheria, njoo ofisini kwangu au
nifungulieni mashitaka, na mimi nitafika kituoni, na kuja kuyajibu maswali yenu
ambayo mnataka kuniuliza, lakini kwa utartibu uliokubalika kisheria, lakini
hapa tunaongea kama wapiti njia tu...’akasema
‘Sasa
mimi ninakushika kwa kosa la kuhusika na mauaji ya mlinzi, ninakushuku wewe
kuwa unahusika, na nataka nifanye uchunguzi wa kina bila kuingiliwa, kwahiyo
ili niweze kufanya hayo ni lazima ushikiliwe ...’akasema na mara nikamuona
mpelelezi akitoa pingu aliyokuwa kaiweka nyuma,...
‘Eti
nini.....’akasema wakili sasa akibadilika na kuwa mkali na muda huo mkuu wa
hapo gerezani akawa anawasogelea akijua sasa hali sio shwari tena...
Tuendelee ni kisa chetu
***********
Mkuu wa kituo hicho cha magereza alipoona hali inataka
kuwa mbaya, akawasogeela wale watu wawili ambao kila mmoja aliashaanza
kutunisha misuli tayari kwa mapambano, na kabla yule mkuu hajawafikia mara wakaingia askari polisi wawili wakiwa
wameshikilia pingu mikononi, wakasimama kusubiri amri , na yule mkuu wa gereza
alipowaona akasema
‘Mpelelei hebu kwanza tuongee ofisini, na wewe wakili
tulia hapo hapo….’akasema na kuwaangalia wale askari polisi, alitaka kusema
neno lakini akaghairi, akamshika mkono mpelelezi na kuondoka naye
‘Askari hakikisha huyu mtu hasogezi mguu, na hapigi simu
, huyu mtu anatakiwa kushikiliwa, tukimuachia ataharibu ushahidi kama ilivyo
kawaida yake, mapaka anafika hapa hakujua kuwa mimi nafahamu mipango yake yote,
kwahiyo ukimpa nafasi akatoka humu atakwenda kuharibu kilakitu…’akasema
mpelelezi
‘Hizo ni hasira zako, mimi sihusiki na lolote, siwezi
kufanya kama unavyosema wewe,mimi naijua vyema sheria na wote wanajua nipo
sahihi wakati wote,….huyu mkuu wa hapa anafahamu kuwa sijui lolote,
nimeshaongea naye, na yeye akanihoji kwa utaalamu wake amegundua kabisa kuwa mimi
sihusiki na lolote…wewe na mihasira yako unashindwa kutumia akili…’akasema huyo
wakili
‘Basi, basi….hebu tukaongee kwanza ofisini kwangu,
nataka uniweke sawa...’akasema na wakaondoka kuelekea ofisini kwa huyo mkuu, ilipita muda, baadaye wakarudi na
mkuu huyo alikuwa na mfuko wa plastiki sikujua ni wa nini kwa wakati ule.
‘Mkuu kama nilivyokuambia huyu mtu hawezi kuachiliwa, huyu ni mtu
hatari kuliko unavyofikiria wewe mkuu, huyu sasa hivi anawekwa pingu tunaondoka
naye hadi kituo cha polisi, au wewe umshikilie hapa hadi tukamlishe uchunguzi
wetu….’akasema mpelelezi,
‘Mkuu lakini huyu ni wakili hawezi kukimbia mimi naona
tumuachie halafu yeye mwenyewe atakuja huko kituoni, mimi namfahamu
sana…’akasema askari mmoja,nampelelezi akamuangalia yule askari kwa makini,
halafu akasema;
‘Huyu haachliwi,ni kama mkuu wa kituo hiki yupo tayari
kubeba dhamana hiyo, sawa anaweza kushikiliwa hapa hapa gerezani, maana hatujui
huko mbele kuna watu gani wa kumsaidia, najua huyu mtu ana watu kila
mahali,hata ndani ya vijana wetu wa kipolisi….’akasema mpelelezi.
‘Sawa mimi nakubali kubeba hiyo dhamana ,nitamshikilia
hapa kituoni, lakini kwa masaa ysiyozidi 24,…’akasema yule mkuu akiangalia saa
yake.
‘Unafanya makosa makubwa sana mpelelezi, siamini kuwa ni
wewe, mimi nilikuwa nakuheshimu sana, lakini kwa hili, tutafikishana mbali
nitahakikisha nitakushitaki kwa kunidhalilisha, na kunisingizia uwongo huwezi kunishutumu kwa jambo ambalo
sijalifanya, na kilakitu kipo wazi , huu sio utaratibu wa kikazi, na kwahili ni
lazima likomeshwe na watu kama nyie hamfai kwenye kazi kama hizo.....’akasema
‘Wewe ndio unafaa, eeh,...usipoteze pumzi yako kwa
vitisho, fanya unalotaka, lakini ni lazima uwajibike, ili haki
itendeke...’akasema mpelelezi.
‘Nakuonya, hizo hasira zako zitakupeleka kubaya, na
nakuhakikishia hili jambo litafika mbali…’akasema yule wakili
‘Usijali,…nimeshajiandaa kwa hilo, tutakutana huko huko
mbali unapopaamini wewe….’akasema mpelelezi kwa kujiamini na yule mkuu akasema;
‘Naona tumelewana, sawa wakili, wewe utabakia hapa , ili
watu wa usalama wafanye uchunguzi wao, na kama watamaliza mapema, basi wewe
utaruhusiwa kuondoka, wao wanatimiza wajibu wao wa kikazi , sio kwa nia ya
kukomoana….’akasema yule mkuu na mara mpelelezi akamsogelea yule wakili, na
kumuambia;
‘Nipe simu yako…’akasema mpelelezi
‘Siwezi kukupa simu yangu…kwanini nikupe simu
yangu?’akasema huyo wakili kwa hasira na mpelelezi akamgeukia mkuu wa kituo
‘Chukua simu yake hatutaki mawasiliano yoyote kutoka
kwake kuanzia sasa hivi, najua ana watu wake watafanya hiyo kazi, lakini kwa
hivi sasa ni vyema kuchukua vitu vyake vyote alivyo navyo vyenye kutilia
mashaka, hasa vya mawasiliani..,hii ni
amri ya polisi….’akasema mpelelezi na yulemkuu akamuangalia wakili , na
kusema;
‘Bora utii sheria, natumai unalielewa hilo muheshimiwa
wakili, mtu ukishikiliwa unatakiwa utoe vitu vyote kwa polisi, ikiwemo simu…na
ukiondoka utakabidhiwa vitu vyako.’akasema huyo mkuu, na wakili akatulia kwa
muda akionyesha hasira, halafu akaitoa simu yake na ilionekana kama anataka
kufanya kitu kwenye simu yake,lakini mpelelezi akmuwahi na kusema
‘Acha ujanja wako…..’akasema mpelelezi akiwa keshamfikia
akitaka kuichukua ile simu mikononi mwa huyo wakili , na yule wakili akasema;
‘Nilikuwa naizima simu yangu na kuangalia muda wa tukio
hili, sina wasiwasi na lolote lile, mnaweza kuchukua kila kitu,lakini nataka
kila jambo lililofanyika hapa liwekwe kwenye kumbukumbu....’akasema
‘Hiyo ni kazi ya mkuu wa hapa, anajua kazi yake hatuwezi
kumfundidha ila ninachotaka mimi ni wewe kukabakia hapa, bila kuleta ujanja wa
kuwasiliana na watu wako, ambao wanaweza kuharibu ushahidi...’akasema
‘Hata hivyo kwa vile umenishuku, ni lazima nimpata
wakili , kwani mimi siwezi kujiwakili mwenyewe,...hiyo ni haki yangu
kisheria...’akasema
‘Utafanya hilo kwa wakati muafaka, kila kitu utapewa kwa
mujibu wa sheria, sasa hivi tunakushikilia ili tuweze kupata ushahidi
...’akasema mpelelezi
‘Sawa, nakusikiliza wewe bosi....’akasema wakili huyo
akikunja uso wa hasira, na kutulia akimuangalia yule mkuu wa hicho kituo cha
magereza, na yule mkuu, akamsogelea na kuichukua ile simu, akampekua na kutoa
kifaa kingine kidogo, nahisi ni cha kuchukulia mawasiliano...akakiangalia na
mpelelezi akasogea na kukiangalia
‘Na hiki ulikuja nacho kwa kazi gani?’ akauliza
‘Hayo maswali nitayajibu nikiwa na wakili
wangu....’akasema, na mpelelezi akakiangalia na kutafuta sehemu ya kuzimia,
kwani ilionekana chombo hicho kilikuwa kikichukua sauti ya maongezi yote
yaliyotokea hapo, akamwambia mkuu,
‘Mkuu, samahani sio kwamba nakupa amri, lakini kwa vile
huyu mtu haniamini, basi nataka wewe ufanye hiyo kazi, hivyo vitu vyote ni
ushahidi, ni vyema ukaviweka kwenye chombo maalumu, na hakikisha havigusi
tena...’akasema na yule mkuu akageuka kumuagalia askari wake mmoja aliyekuwepo
hapo, akasema;
‘Fanya hiyo kazi, mpekue na toa kila kitu alicho nacho
uweke kwenye huu mfuko...’akasema huyo mkuu, na yule askari wake, akafanya hiyo
kazi,
‘Huwezi
kunifanyia hivyo, ..sio haki kabisa,na mkuu unaona alichokifanya huyu mtu,
ametumia nguvu kuninyang’anya mali yangu,na hiyo simu yangu ina mambo yangu ya kikazi, natakiwa
niwasiliane nao muda wowote, hivi
ikitokea mteja wangu ananihitaji kwa haraka atajuaje kuwa nipo sehemu
nisiyoweza kumfikia, hamjui umuhimu wangu ehe…’akasema akitaka kumsogelea huyo
mpelelezi,na wale askari wakawa wamemuwahi na kusimama kati kati yao..
‘Huna ujanja wakili,….ni lazima safari hii upambane na
nguvu ya dola, niliwahi kukuambia kuwa siku za mwizi ni arubaini,usijifanye
kutumia sheria kwa masilahi yako…hakuna aliye juu ya sheria,wewe na wenzako mjue
mwisho wenu umefika, na bora mtubu madhambi yenu, ili tuokeo muda, kwani sasa
hivi, ni lazima haki ipatikane….’akasema
‘Haki, ni nani hajui hiyo haki, hiyo ndio kazi yangu ya
kuitafuta haki kwa watu , kwa jamii,leo hii unanituhumu,…sitakubali hili lililotokea
hapa na mkuu wa hiki kituo ni shahidi, ni lazima lifike kwa vyombo vya sheria,
mkuu umeona yote yaliyotokea hapa, hili
ni lazima litafika mahakamani….’akasema wakili, na mkuu akamshika mkono huyo
wakili na kusema;
‘Twende …..tuwaache hawa watu wakatimize wajibu
wao...usiwe na shaka, ni tarataibu za kawaida tu, kama huna tatizo hakuna
shaka, .....’akasema, na huyo mpelelezi akawaangalia wakiondoka, na yeye
akawageukia wale maaskari na kusema
‘Mimi sipaamini mahali hapa….chukueni
zamu,kuhakikisha huyu mtu hatoki,
….’akasema na kuchukua simu yake, na akawa anaongea na mtu akasema;
‘Upo leo zamu, ..okey safi kabisa,kuna vijana wangu
wawili mtasaidiana nao, kama utahitajia huo msaada, vinginevyo ni kuwa kuna
jamaa ,yule wakili aliyekuwa akimtetea mlinzi, ndio…yes, ameuwawa, ...'akasikiliza halafu akasema
'Mhh, oooh, na wewe
ulimuona eeh, jana usiku eeh, okey, usijali yote hayo nimeshaambiwa....sasa
kama upo zamu leo, hakikisha huyu wakili akiingizwa sehemu atakayokaa,
muhakikishe hana kitu mfukoni,...’akasema na kusogea mabli kidogo ili tusikia
anachoongea, na mimi nikajisogeza sikutaak kitu kinipite.
‘Hakikisheni analala usiku kucha….ndio, msijali,fanyeni
muwezavyo, anaweza kutumia mbinu nyingine....nafahamu kuna watu wake watakuwa
wameshahisi hilo, na hata hawa watu wetu
wanaweza wakafanya hiyo kazi kumsaidia, kila mahali ana watu...’akasema na
kusikiliza simu kwa makini, halafu akasema;
‘Okey, hilo nakuachia wewe…’akasema halafu
akawageukia,maaskari, akatulia akiwaangalia, akamgeukia yule aaskari
aliyemtetea huyo wakili na kutaka kumuambia kitu lakini akaghairi na kunigeukia
mimi akasema;
‘Tunaweza
kuondoka, nina kazi nyingi sana leo,….’akasema na mimi nikamfuatilia nyuma na
tulipofika kwenye magari yetu, akawa anawasiliana na watu wake, alikuwa akitoa
amri;
‘Wale watu wote, washikiliwe, ...ndio wafikishwe
kituoni, waambiwe kuna maswali wanahitajika kuulizwa basi, msiwape nafasi hiyo
, kama ni wakili wao atakuja huko huko kituoni, msiwape nafasi ya kujitetea,
hiyo ni amri....’akasema halafu akatulia na baadaye akapiga simu sehemu
nyingine.
‘Hao watu wakichukuliwa fanyeni upekuzi wa haraka, kila
kitu chenye ushahidi, kama tulivyoongea hakikisheni mnakiwakilisha kwenye
chumba chetu, yaah, nimeshapata hicho kibali, msijali,....’akasema.
Baadaye wakati anaingia kwenye gari lake nikamuuliza
‘Mkuu una uhakika na unachokifanya, huyu wakili nasikia
ni mkorofi sana, ukimchezea, ni lazima
akuweke ndani, nasikia hakubali kushindwa kirahisi,nina uhakika akitoka hapa
atakuchukulia hatua…’nikamwambia mpelelezi
‘Usiwe na shaka na maamuzi yangu,ninamfahamu sanahuyu
jamaa lakini ni vyema tukafanya hivyo ili niweze kukamlisha uchunguzi
wangu,huyu jamaa amekuwa kikwazo kwangu kila ninapotaka habari fulani kwa watu,
ninajikuta napambana naye, yeye wateja wake wengi ni watu ninaowashuku,…na ili
nifanikiwe kwa uchunguzi wangu ni lazima hili lifanyike….’akasema
‘Lakini huna uhakikakuwa yeye anahusika na kifo cha
mlinzi?’ nikamuuliza
‘Uhakika nitaupata tu, kuna vigezo vingi vinamshuku, na
mimi sitaki kupoteza hiyo nafasi, kuna kitu nataka kuthibitisha,usiwe na
wasiwasi,ninachohitajia ni huyu mtu asiachiwe, vinginevyo kazi yangu itakuwa
ngumu sana, hawa watu wana mbinu za kila namna…sasa hivi watu wake watakuwa
wakimtafuta hawajui kuwa na yeye yupo kituoni, lakini watakuwa kwenye vituo
tofauti tofauti..hakuna mawasiliano hapo’akasema mpelelezi
‘Lakini huna uhakika kuwa huyo wakili anahusika na
mauaji ya mlinzi…?’nikamuuliza
‘Niwe na uhakika nisiwe na uhakika,lakini jamaa huyu
anahusika na kifo cha mlinzi, kuna jambo nataka kulicheza, ni swala la muda,
nina imani hadi kesho nitakuwa nimeshafanikiwa, na itabakia kazi ya kuwakilisha
ushahidi wote mahakamani, kama mdada angelikuwepo, isingelisumbua hivi, hata
hivyo hakijaharibika kitu….’akasema mpelelezi na kuanza kuondoka,na yulemkuu
akasema
‘Mdada angesaidia nini?’ nikamuuliza
‘Yeye ana ushahid muhimu sana, zikiwemo hizo nyaraka za
siri, na uchunguzi wote aliokuwa nao mzee, kauchukua yeye, sijui anampelekea
nani, au ana ajenda gani ya siri na kundi hili. Hii inanifanya nimshuku sana
huyu, japokuwa mzee anasema huyo dada hahusiki...lakini kwa nini mzee
anamtetea....’akawa anasema.
‘Labda mdada alikwua akimfanyia kazi zake...’nikasema
‘Hapana, mdada na mzee hawaelewani kabisa, hasa kipindi
hiki cha nyuma, mzee anamshuku mdada kuwa anatumiwa na watu ambao wanamshuku
mzee vibaya, lakini hawajulikani hao watu ni akina nani, na wana masilahi
gani....’akasema mpelelezi
‘Inawezekana wewe na mzee mnamshuku mdada kuwa yupo
kwenye hilo kundi kisiri au?’ nikauliza
‘Hapo sijui...inawezekana, uwezekano ni mkubwa sana, na
wewe unatakiwa unisaidie kwa hilo, tukifika kwako nataka uniambie kila kitu
unachokijua kuhusu mdada, vinginevyo na wewe utashikirishwa kwenye washukiwa,
sasa hivi sina urafiki na mtu, sasa hivi ni kazi tu...’akasema mpelelezi
akiniangalia kuwa uso wa kiaskari.
‘Mhh, hata mimi mkuu...!’ nikasema huku nikijua sasa
mambo yameiva, na mdada hayupo tena, ina maana nisiposhirikiana na mpelelezi,
nitaweza kuyabeba madhambi ya mdada, lakini mdada amekwenda wapi, mbona ameamua
kunisaliti...
‘Kama mdada kafanya hivyo sitamsamehe, ni lazima
nimtafute, sijui yupo wapi, huenda huko alipo anachekelea kuwa kaniweza, mmh, lakini hata hivyo ooh ....kweli moyo wangu hautakuwa na raha bila ya
kumuona mdada,...’nikasema na huku moyoni nikikiri kuwa kweli nampenda mdada,
na sijui nitawezaje tena kuficha madhambi yake.
Na mara nilisikia honi ikipigwa
kuashiria kuwa mpelelezi ananisubiri ili
tuongezane na yeye ili nikamuambia ukweli wote kuhusu mdada...
NB: Haya haya umekucha,
WAZO
LA LEO:Muda ni kitu muhimu sana, wengi wetu tunakipuuzia, muda
ni mtaji aliotujalia mwenyezimungu, na tulitakiwa tuhakikishe kuwa kila sehemu
ya muda inaleta tija, na hasa kwa matendo mema.
Hebu angalia watu wanavyopteza muda kwa maongezi
kijiweni, au kwa kufanya yale yasiyonufaisha jamiii. Tukumbuke kuwa muda kamwe
haurudi nyuma, kila mlio wa sekunde, ni kuashiria kuwa muda unasonga mbele,
uhai unapungua, na kama hakuna faida ujue ni hasara inaingia,
Jiulize, je wewe unakwenda
na huo muda, je wewe umafanyia nini na
mtaji huo muda, jiulize sana , maana kazi ya mtaji ni kuzalisha, tena kwa
faida, kama sio faida ni hasara. Kumbuka kuwa muda kamwe hautakusubiri wewe,
ufanyie kazi huo mtaji ili usije ukajuta wakati huna muda tena wa kuishi hapa
duniani.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Hello, yοu useԀ to compoose amazing articles, Ƅut the
immeԀiate paѕt feԝ posts haѵe alreaԁy been sorta lackluster...
I miss уour incrediblpe writing. Ƥast ɑ few posts arе
only a little from ϲourse!
Feel free to surf to myy blog - healthy cat r7 weight diagram; ,
Hi! I understand this is somewhat off-topic
however I had to ask. Does running a well-established website like yours take a massive amount work?
I'm completely new to operating a blog however I do write in my journal on a daily basis.
I'd like to start a blog so I can easily share my own experience and
feelings online. Please let me know if you have any suggestions
or tips for new aspiring bloggers. Appreciate it!
Feel free to surf to my website :: senior moving assistance
Post a Comment