Kama ilivyotarajiwa mahakamani kulijaa watu wengi, lakini
sio kama ilivyokuwa kwenye siku ya kesi liyopita, siku hiyo kwa walio wengi ilionekana
siku hiyo kama hitimisho, japokuwa mshitakiwa mkuu wa mauaji alikuwa hayupo.
Watu wengine
waliofika siku ile, siku ya kesi iliyopita waliogopa kufika leo,wakikumbuka
tukio lililotokea siku ile, na wengine wapya wakajitokeza ili na wao wamuone
huyo mdada, aliyeweza kuwafukuza watu wote mahaamani, ...
‘Huyo mdada yupo wapi ,mbona mimi sijamuona, mimi
nimekuja kwa ajili yake tu,.....’akasema mtu mmoja
‘Wewe usiseme hayo, tuombe mungu isitokee tena kama siku
ile, maana siku hiyo sitaisahau unaniona na unene wangu huo, lakini siku ile
nilikimbia , karibu nivunjike mbavu
maana nilikwenda nikagonga kwenye mti, kwa vile nilikuwa nakimbua huku nageuka
nyuma kuangalia nyuma kuhakikisha kuwa kweli huyo mdada hajanifuata mimi.
‘Hahahaha, ama kweli nyie watu waoga, ina maana mnaogopa
mashetani, mimi siogopi kamwe, ningelikuwepo ningemsomea akatulia, unayakaripia
hayo madude hali inatulia, tatizo nyie mnakimbilia kuogopa..’akasema na mara
kukatokea kitu kimedondoka, yule yule aliyekuwa akimcheka mwenzake kuwa ni
muoga, ndiye aliyekuwa wa kwanza kutaka kukimbia
‘Oh, ni mjuzi kadondoka toka juu ya paa, unakimbia nini
sasa, wewe si umesema huogopi kitu...’akasema mwenzake
‘Yaani mawazo yangu yalishakwenda huko mbali nikajua
huyo mdada kafika kaanza purukushani lake, nikawa napiga mahesabu ya kuwahi
mlangoni....lakini siogopi...’akasema
Ndio hali ilivokuwa kwa siku hiyo mwenye mwana abebe
mbereko na asiye na mwana aeleke jiwe, muda wa mahakama ukafika, wahusika kila
mtu kwa nafasi yake, na sehemu ya washitakiwa kuliokena watu wameongezeka, sio
mtu mmoja tu, ni zaidi ya sita,na wengi wao ni watu mashuhuri tu, waheshimiwa..
Hakimu alifika, na kesi hiyo ikatajwa kwa mujibu wa
utaratibu, na mwendesha mashitaka akaanza kutoa maelezo;
‘Japokuwa mtuhumiwa wetu namba moja hayupo, ameuwawa,
lakini katika kesi hiyo, kama tulivyowahi kusema awali, kuna watu wengine
walioshirikiana naye, japokuwa sio moja kwa moja...’akasema
‘Ndugu muheshimiwa hakimu, kesi hii inagubikwa na kundi
haramu , lililojijengea utawala haramu na kujipanga kinamna,...kama tutakavyokuja
kuelezea hapa..’akaendelea kutoa maelezo marefu na mwisho hakimu akauliza
‘Tuna kesi ya mauaji, je kutokana na maelezo yako,
inaonyesha hiyo ni kesi nyingine, na washitakiwa wengine..’akasema hakimu
‘Hapana muheshimiwa hakimu, kesi ni hiyo hiyo, ila
wahusika wameongezeka, na chanzo cha mauji hayo kinatokana na hawa wahusika,
kwa pamoja, waliandaa mbinu ya kuhalalisha taratibu zao, wakapandikiza watu
kila idara, ili tu waweze kufanikisha malengo yao wakiwa na lengo la kutengeneza dunia yao haramu kwa mikono yao..
‘Katika wahusika hao, kila mmoja alitakiwa kukubali amri
moja, na kama yupo mwanachama atakayesaliti,baada ya kujiunga, alipatikana na
adhabu ya kifo, kama tutakavyokuja kuelezea kwa ushahidi, na leo tuna shahidi
wetu ambaye aliweza kulibaini hili, baada ya kufanya uchunguzi wa kina,
tutaonyesha hayo hatua kwa hatua,...’akasema
Mawakili wa utetezi walikuwa wengi, na kila mmoja
alikuwa na hamu ya kutoa pingamizi lakini kwa vile hakimu alikuwa akihojiana na
muendesha mashitaka, wao ikawabidi wakae kimiya.
‘Mshitakiwa mkuu ameuwawa, na hiyo ni kesi nyingine, je
kuuwawa kwake kunahusiana na hili kundi?’ akauliza hakimu.
‘Ndio muheshimiwa hakimu, kama nilivyosema, katika kundi
hili waliweka sheria, kuwa ukijiunga, hutakiwi kutoka, au hata kama hujajiunga
lakini wao kwa namna moja au nyingine, wamakupa kazi yao, na ukaonekana
kujua,...au kukiuka yale waliyokuagiza, wanakuua,..japokuwa mlinzi aliyuwawa,
hakuwa ndani ya kundi moja kwa moja, lakini yeye alitumiwa na kundi bila hata
yeye kujijiua...’akasema
‘Haya tusipoteze muda, tuanze ....unasema utamsimamisha
shahidi wako, aitwe ili tuanze, na upande wa utetezi mpo tayari...?’ akauliza
‘Tupo tayari muheshimiwa hakimu, ila tuna pingamizi kuwa
mshitakiwa mkuu hayupo, na ameuwawa, ina maana kesi yake haipo , hatuwezi
kumshitaki marehemu, sisi tulitaraji isomwe kesi nyingine, kuhusu wateja wetu
hawa, ambao wamesingiziwa mambo ambayo hawayajui kabisa,...’akasema na hakimu
akageuka kumuangalia muendesha mashitaka, ambaye alisimama akasema;
‘Katika kesi hiyo, tuliainisha awali kuwa kuna wahusika
wengine, ambao walikuwa hawajakamatwa kutokana na sababu mbalimbali, na sasa
ndio hawa wamekamatwa, kwahiyo kesi ni ile ile, nab ado wapo wengine, kama
orodha itakavyokuja kukabidhiwa mahakama hii tukufu, wapo wameshakimbia, lakini
mkono wa sheria ni mrafu....’akasema muendesha mashitaka, kukatokea ubishani wa
kitaalamu hadi hakimu akaingilia kati
‘Mimi naona kesi ni hiyo hiyo tuendelee, kama itaonekana
ni kesi mpya, hatutasita kuliangalia hilo, lakini kama ni kundi ambalo
limejumuika kwa pamoja na wao wakawa wahusika waliosababisha kifo cha marehemu,
kesi ni hiyo hiyo..tuendelee na kesi yetu, shahidi aitwe...’akasema hakimu, na
shahidi akaitwa
Wakati shahidi huyo anatoka kutoka chumba cha mashahidi,
mimi nilikuwa nimekaa mle ndani ya mahakama, sikuwa nimeambiwa nikae chumba cha
mashahidi nikajua kuwa mimi sitaitwa kama shahidi, kama nilivyokuwa nimejua
hivyo...
Nilihangaika kuangalia huku na kule kuwa labda ninaweza
kumuona mdada, lakini hakukuwa na dalili yake, ilionyesha wazi kuwa binti huyu
kashikiliwa kama alivyosema mpelelezi, au huenda sasa ni maiti...nikakumbuka
mazungumzo yangu na huyo mpelelezi.
***********
Kikao changu na mpelelezi kilinifunua akili, na hata
baada ya hicho kikao, nilianza kuogopa kila mtu, nilikujua sasa nipo hatarani
zaidi ya nilivyokuwa nawazia,....sasa nilianza kuogopa kuwa wakati wote naweza
kuuwawa...
Kikao changu na mpelelezi kilionekana ni kikao cha
kunilazimisha niongee kila kitu ninachokifahamu kuhusu mdada, sikuweza kukwepa,
na ilinibdii niongee hata yale aliyonikataza mdada, sikuwa na jinsi....
‘Leo nataka uniambie kila kitu, kuhusu mdada, jinsi
mlivyojuana naye na yote aliyokutendea, na jinsi gani mlivyoweza kushirikiana
....’akasema
‘Lakini mkuu, nilishakuelezea kila kitu mengine ni
maswala binafsi, hivi wewe unaweza kuelezea mambo yako na mkeo, au na ...?’
nikamuuliza
‘Usikwepe swali, hata hivyo huyo sio mke wako, mimi
nafahamu mambo gani ni ya siri na mambo gani sio ya siri, sijasema uelezee
mambo yenu ya mapenzi, natake unielezee mambo ambayo yanamgusa mdada katika
shughuli zake, ...cha muhimu ni ukweli, huna jinsi nyingine, hapa unacheza na
muda, na ni hatari usipoweka wazi...’akasema
‘Ok, mimi na mdada tulikutana kazini, na kutokana na
ucheshi wake tukazoeana,kiukweli nilipomuona kwa mara ya kwanza tu moyo wangu
ulishituka sana, sijui ....lakini ndio hivyo,mapenzi labda...’nikatulia na
mpelelezi akawa kimiya
‘Mdada alianza kunizoesha mambo ambayo mimi sikuwa na
tabia nayo kabla, ujana damu inachemka, nikavutika kirahisi tu...., kwake yeye
alisema ananitoa ushamba, akanishawishi hadi nikaanza kulewa, nilifikia hatua
nikawa mlevi kweli....lakini siwezi kumlaumu kwa hilo, kipindi hicho nilikuwa
na matatizo mengine binafsi...’nikasema kama kumtetea mdada
‘Mdada akaanza kunifundisha jinsi ya kupata pesa, kwa
njia nisizozipenda, kama nilivyokuambia kuwa kipindi hicho nilikua na matatizo
binafsi na moja ya tatizo hilo ni kukwama kipesa, nilihitajika nijijenga
haraka, ili niweze kumuona mchumba wangu ambaye kwa muda huo alikuwa na mtoto,
mshahara wangu hakuweza hilo, japokuwa nilikuwa najua baadaye kwa muajiri wangu
huyo ningeweza kupata maendeleo, lakini swala la muda, likanikwaza.
‘Kutokana na shinikizo la wazazi wa binti, nilitakiwa
niwajibike, ...nionyeshe kuwa kweli, nitaweza kumlea huyo binti na mtoto wake
kama nilivyoahidi, kwahiyo nilijituma, nikawa silali, na kila simu iliyotoka
huko nyumbani, ilikuwa ikinitishia amani....wanakuwa kama wananishinikiza niwe
tajiri wa haraka haraka, kitu ambacho sio rahisi...
‘Alivyotokea mdada na mapendekezo yake hayo, sikuweza
kuyakubali moja kwa moja, maana mimi ni muoga sana kwa wizi, lakini kwa hali
iliyokuwepo, niliona kama mtu aliyekuja kunikoa...’nikasema
‘Tamaa za pupa zikanijia japo kwa tahadhari, kwani kazi
yangu ilikuwa inanihukumu, kwahiyo japokuwa moyo uliona huenda, nikafanikiwa ,
huenda na mimi naweza kukubali,hata hivyo mimi sikufanya, yaani sikukubali,
mdada ndiye aliyefanya kila kitu..’nikasema kwa kujihamu na kujitetea.
‘Mdada ndiye aliyebuni stakabadhi za uwongo,hadi
akafanikiwa kupata pesa nyingi tu, na kunigawia, na mimi sikuwa na jinsi
nikazikubali, na kuanza kujijenga, angalau nikawa nimejionyesha kijijini kuwa
naweza kummudu mtoto wa watu...
‘Jambo moja likazaa jingine, nikawa mfuasi wa mdada,
japokuwa nilikuwa naumia sana moyoni, japokuwa nilikuwa sipendi, lakini kila
alilolitaka mdada nikawa nalifanya, nikikataa yeye ananitishia kuwa atayaelezea
machafu yangu kwa baba mkwe, kwa...’nikatulia
‘Machafu gani hayo...?’ akauliza mpelelezi na hapo
akanifanya nianze kuhisi uwoga na wasiwasi, maana mambo kama haya sikutaka
kabisa yaje kujulikana, lakini sikuwa na jinsi
‘Mdada aliwahi kuchukua picha za uchi, alinilewesha na
kuweza kuchukua picha kama hizo kwa nia ya kunilazimisha ili nifanya kila
anachokitaka yeye, kwahiyo ikawa ndio fimbo ya kunichapia kila nilipotaka
kukataa...
‘Je hayo uliyafanya kwa sababu ya kutaka utajiri, au
kwasababu ya mapenzi au kwasababu ya hivyo vitisho?’ akauliza
‘Mhh, siwezi kusema moja kwa moja kuwa ni kwasababu hii
au ile, ila kila aliponilazimsiah mdada, sikuweza kupinga,...ilionekana kama
kanijaza kitu kwenye ubongo wangu na kuwa goigoi..sikujielewa kabisa, labda ni
kwa vile nilimpenda, labda..ni vitisho, hata sielewi...’nikasema
‘Je kwenye mauaji
ya mtoza ushuru, mdada ndiye aliyakufundisha kuvaa ndevu,akakuambia ufanye hivi
na vile,...maana bado nahisi kuna mengi hujaniambia kuhusiana na kadhia
hiyo..?’ akaniuliza
‘Ni kweli yeye ndiye aliyenilekeza kila
kitu,...akanivalisha hizo ndevu, ..na hata siku ile niliyokuita kuwa nina
ushahidi waliokuwa wakiutafuta polisi, yeye ndiye aliyenibadili na kunifanua
nionekane kama mwanamke, na ndio nikaweza kuufikisha ule mzigo pale
nilipokuelekeza...’nikasema na mpelelezi akawa kama anawaza jambo.
‘Kwa maelezo hayo, nahisi mdada, ...mmh, okey nimeelewa,
na hadi sasa hujafahamu wapi mdada alipoelekea?’ akaniuliza baada ya kutoa
maelezo mengi aliyoyahitajia
‘Kwakweli sifahamu nimeonana na mdogo wake, na hata
mdogo wake hafahamu wapi alipoelekea mdada, naona kama kakimbia
nchi...’nikasema
‘Hawezi kufanya hivyo...tutampata tu, ...’akasema
mpelelezi huku akiwaza jambo, baaadaye akaniuliza
‘Wewe na mzee, mlikuja kuongea na kukubaliana baadaye?’
akaniuliza
‘Hapana, ...maongezi yetu na mzee baada ya kuanza kuumwa
yamekuwa kwa kupitia watu waliosema wametumwa na yeye na kwa bahati mbaya kila
nikifika kwake, nakutana na shangazi, shangazi ambaye hatuivani
kabisa...’nikasema
‘Kwenye nyumba uliyokuwa umepanga, yule mwenye nyumba, unamfahamu
vyema?’ akaniuliza
‘Namfahamu tu kama mwenye nyumba , kwani ana nini?’
nikamuuliza
‘Hili kundi lina mbinu sana, kila mahali wana watu wao,
wewe ulianza kutayarishwa toka upo huko kijijini,...lakini kama chambo, sio
kuingizwa ndani ya kundi moja kwa moja,na pale ulipofanya hayo machafu kwa huyo
mzee, ikaonekana huo ndio wakati muafaka, unaweza sasa kuwekwa kwenye ndoana,
‘Wewe ulipokuja hapa mjini ukiwa umetuma maombi yako,
wenzako walishajipanga, utafikia wapi, utaajiriwa wapi na utakutana na nani,
lakini hujijua, kwasababu wewe ni chambo tu, na hukutakiwa ufahamu lolote,....’akasema
‘Haiwezekani...’nikasema
‘Hata nyumba hiyo, uliyopanga ilishapangiliwa , mle
kulikuwa na vifaa maalumu, na mwenye nyumba, alikuwa mlinzi wa
kukuchunguza...’akasema
‘Sio kweli...’nikasema
‘Huyo mzee hakutakiwa kulala,..yule ni askari
aliyefukuzwa kwa makosa ya jinai, walimfunga baadaye akaachiwa kwa
msamaha,baadaye watu hao wakamfuata na kumuweka kwenye kazi maalumu, hata
hivyo, hata yeye hajui kuwa yupo kwenye kundi hilo haramu, anatumiwa tu...na
yeye atakuwa mmoja wa mashahidi,...tumeficha mahali, maana akionekana
atauwawa.....’akasema
‘Mhh, kumbe.....’nikasema
‘Hukuona huyo mzee, akikufuatilia, yeye alitakiwa kila
ukitoka awe nyuma yako, alikuwa akijibadili kinamna, leo anavaa hivi kesho
hivi, na usingeliweza kumtambua, na alipokuona na mdada, akashituka, akapeleka
taarifa, akaambiwa mdada hata tatizo yeye aendelee na kazi yake..’akasema
‘Ohh...mbona sikuwahi kumuona yeye akiongea na
mdada...’nikasema
‘Mzee alikuwa na kazi yake maalumu, na mdada alipewa
kazi yake tofauti, lakini wao hawakujua wanafanya kazi kwenye kundi, mdada ni
mjanja, alikuja kugundua kuwa huenda alivyotegemea sio, yeye alihisi labda
anafanya kazi ya usalama wa taifa..kumbe yeye ni chamabo wa kundi, kama
ulivyokuwa mlindi na wewe ulishaanza kuingizwa kinamna, kama chambo...’akasema
mpelelezi
‘Mbona sielewi kwa vipi?’ nikauliza
‘Yote utayapata huko mahakamani,ila mengi hyawezi
kuwekwa wazi kwa sasa, sipendi siasa, siasa imeingizwa hapo, na hutaamini,
tangu mwanzo nimekuwa na kazi kubwa sana ya kuwashawishi hao watu,lakini wao
walitaka hili tatizo lizimwe kia-ina...’akasema
‘Oh, kwanini....?’ nikauliza
‘Kwanini, wewe huoni, kila mahali watu wao wapo, ni nani
asiyehusika, huwezi kujua, na masilahi ya watu yapo mbele...hakuna mwenye
huruma tena na jamii, wachache wanaojitia kipaumbele, wanakuja kupewa kitu
kidogo, wananyamaza, angalia mangapi yanafanyika sasa, ambayo yanaathiri jamii,
hali ngumu za uchumi, vitu vinapandishwa bei ....’akatulia
‘Wapangaji bei ni nani...ni hao hao wenye masilahi yao,
...sio rahisi kupambana na hili kundi ndio maana siasa inaingizwa, na
sijui...mimi nitatizmia wajibu wangu, halafu nitakaa pembeni, nione ni hatua
gani itachukuliwa...’akasema
‘Wewe huogopi kufa...?’ nikamuuliza
‘Kufa kila mtu atakufa,..kifo hakiogopi kwa namna
hiyo,...na mimi nimejifunza kazi za kifo, kazi zetu ni kifo muda wowote,
kwahiyo hata uogope vipi, ipo siku utakufa kwa sababu unapambana na watu
waliodhamiria kuua....’akasema
‘Oh, mimi sipendi kabisa kazi zenu...’nikasema
‘Na ndio maana wamekuchukua kama chambo tu...sasa kesho
mimi.nikimaliza kutoa ushahidi wangu, wewe na mdada, na baba mwenye nyumba wako
mnaweza kuitwa kutoa ushahid kuthibistiha haya niliyoyaelezea, nina ushahidi wa
kila namna, lakini huenda, watakawataka kuthibitisha, japokuwa kiusalama
inaweza isiwe hivyo....cha muhimu kwa sasa ni kuhakikisha kuwamdada yupo hai au
wameshamuua...’akasema
‘Una maana gani, umajuaje hayo, umewasiliana na mdada?’
nikauliza maswali mengi kwa mkupuo
‘Mdada ametekwa nyara,hilo halijathibistishwa rasmi,
lakini kama walivyo na watu wao kwenye watu wetu, hata sisi tuna watu wetu
kwenye kundi lao, ila watu wetu hawajawa na uhakika wapi mdada alipofichwa,
walimkamata wakati anapeleka ushahidi wake kwa mtu aliyemtuma, lakini akiwa
njiani akashituka, sijui kwa vipi, alihisi huyo mtu anayempelekea sio mtu wa
usalama kama alivyokuwa akijua awali,..’akasema
‘Mdada alipogundua hilo, akataka kuficha kila kitu,
lakini huyo mtu wake, akamshitukia, kwani alipofika huko alimuambia huyo mtu
kuwa ushahidi aliokuwa nao umeibiwa...’akasema
‘Mhh, mungu wangu, atakuwa salama kweli...?’ nikauliza
nikianza kujiona msaliti...
‘Mwanzoni nilijua labda ni mbinu za mdada, maana kundi
hili lina mbinu nyingi tu...lakini baadaye tulipofuatilia na watu wangu wa
ndani ya hilo kundi, tulikuja kugundua ukweli..kiujumla mdada yupo matatani, wamemshitukia kuwa ana
sura mbili...
‘Unasema nini?’
nikasema kwa hamaki, maana niliona kama mpelelezi anataka mdada afe,
‘Kundi hilo kama walikuchukua kama mtu wao, wakaja kugundua
kuwa umewasaliti wanakupoteza kabisa,....wanaweza kukupoteza kinamna, wana
mbinu za kila namna...’akasema
‘Mbinu gani?’
nikauliza
‘Ni za kijasusi zaidi, ina maana mdada akitoka hapo
salama, inabidi apate dakitari wa hali ya juu kumchunguza...ni tatizo kwakweli,...’akasema
‘Sasa...?’ nikauliza
‘Tangu mwanzo nimekuwa nikiwataka munieleze ukweli,
lakini imekuwa ni kazi ngumu sana kupata ukweli, nilipogundua hilo..ikanibidi
nitumie njia za zaida...unafahamu haya tunawakanya sana watu, kuwa wasiingiwe
na tamaa ya kujiunga na makundi haya yenye mlengo wa kimataifa,...lakini wengi kwa
tamaa zao wanahisi ni kitu rahisi tu, wataingia na kutajirika, sio rahisi
hivyo, kwao ukiingia ni lazima uwe na faida kwao....’akasema
‘Lakini mdada ni mtu aliyealimika, sizani kama aliingia
kichwa kichwa kwa kurubuniwa....na mimi nimekuwa nikimuamini sana anaweza
kujilinda...’nikasema
‘Wewe unazungumzia elimu yetu ya hapa hapa, hao watu ,sio
watu wa elimu ndogo, ni lazima kwanza uwe na akili ya ziada, hiyo ndio sifa ya
kuingizwa kwenye kundi lao. Katika uchunguzi wangu, nilikuja kugundua kuwa wote
waliopo kwenye hilo kundi wana kipaji, wana elimu, na akili zao ni zile akili
za hali ya juu (IQ),...
'Sasa mtu kama mdada, ana kipaji hicho, lakini kwa vile
hakuwa nao mapemda, na walitaka kumtumia kijuu-juu bila kujijua, huenda baadaye
wangelimuingiza ndani zaidi, na walipogundua kuwa mdada kaweza kuchukua nyaraka
zao muhimu, wakaanza kumuandama, na mdada akajaribu kuwazidi ujanja,kama asipo
wapa hivyo vitu watamtesa sana, na ni lazima tavitoa tu mateso yao ni hali ya
juu...’akasema
‘Sasa nyie watu wa usalama mumefanya nini cha kumsaidia
mdada...?’ nikauliza
‘Sisi kama watu wa usalama, bado tunamtafuta hatujui wapi
alikofichwa, ni kazi nzito kidogo ikizingatiwa kuwa hawa watu ni watu hatari na
wanajua ni nini wanachokifanya, hawasiti kutoa roho ya mtu...’akatulia aliposikia
ujumbe wa simu ukiingia kwenye simu yake, akausoma, halafu akanigeukia na
kuniambia;
‘Tutakutana mahakamani, uwe makini...kuna walinzi
watakuwa wanahakikisha usalama wako, ...sasa hivi sitaki kupoteza mashahidi
wengine, wewe na mdada ni watu muhimu kwangu, mtakuwa mashahidi wangu wakubwa,
ila usije kuongea na mtu yoyote kuhusiana na haya niliyokuambia, huwezi kujua
ni nani unayemuambia....’akasema.
‘Lakini mdada ni mmoja wa washitakiwa, kutokana na
maelezo yako, na kama ulivyosema, huenda yeye anahusika na hilo kundi au
nimekosea...?’nikamuuliza
‘Kama alivyo mdada, ni kama ulivyo wewe, mdada na ujanja
wake hakujua kuwa anatumiwa na hilo kundi, watu hao walikuja kumsoma mdada,
wakagundua kuwa ana ujasiri, ana kipaji, lakini pia ana hasira za kisasi kwa
madhila aliyokutana nayo,wakatumia udhaifu wake,wakatumia matatizo yake, kwa
manufaa yao ...’akatulia kidogo
‘Na kwa jinsi walivyojipanga, hata dakitari aliyekuwa
akimtibia mdada ni mtu wao, huyo dakitari ni mmoja wa kundi hilo wa kimiya
kimiya....unaona hapo, siwezi kukuelezea kila kitu mengi utayasikia
mahakamani...’akasema akionyesha wasiwasi
‘Oh, hata dakitari wake...!’nikasema kwa mshangao na
yeye akatabasamu na kusema;
‘Mpaka sasa dakitari wake hajafahamu kuwa
keshagundulikana, labda aje kuambiwa na watu wao walipandikizwa ndani ya kundi
letu, hata hivyo mimi sijamwambia mtu mwingine, zaidi ya vijana wangu
ninaowaamini sana, ambao wananifanyia kazi zangu...
‘Mmm, mbona hatari, kwa hali kama hii utamuamini nani...’nikasema
‘Nimekuwa nikimfuatilia sana huyu dakitari, kwa jinsi
alivyo karibu na mdada, na mdada akawa ufungua wangu wa kufinikisha kwa watu
wengi bila ya yeye kufahamu kuwa namfuatilia, na baadaya akaja kugundua, ndio
hapo tukaanza kukosana mimi nay eye..
‘Sasa huyo dakitari wake, ni mmoja wa kundi, mdada
halijui hilo,...na hata hao tuliowakamata ni kama chambo tu, ni dagaa tu, wapo
samaki na mapapa, kwa ujumla kuna kundi kubwa la watu, wataalamu, madakitari, wanasiasa,
wakufunzi....waheshimiwa...’akatulia
‘Sasa mtawezeje kuwakamata watu wote hao na kwa ushahidi
gani...?’ nikauliza
‘Muda utasema cha muhimu ni kuliweka wazi hili jambo mahakamani,
nafahamu ni kazi kubwa sana,kwani hilo kundi ni mti mkubwa wenye matawi mengi
sana, na baya zaidi shina la mti huo halipo hapa nchini, lakini...muda
utasema....’akasema huku akiangalia saa yake.
Mpelelezi akawa ameshapita kwenye kizimba tayari kwa
kuanza kutoa ushahidi wake,....
NB: Haya ushahidi huoooo
WAZO
LA LEO:Matabaka katika jamii ndio chanzo cha matatizo,
viongozi, watawala, mabosi, mara nyingi wanashindwa kuliona hili, wakitegemea,
ile kauli ya mwenye kisu kikali ndiye mla nyama.
Angalia sasa hivi elimu inatolewa kimatabaka, na
halikadhalika makazini, watu wanaajiriwa kimatabaka, na hata mishahara hutolewa
kimatabaka, kwahiyo hata nyoyo za watu zinajikuta zina hisia za kimtabaka, hapo
unategemea nini, na ni nini chanzo cha haya yote. Chanzo cha haya yote ni
ukosefu wa hekima ya uongozi, wa kujenga jamii inayopewa haki yake bila ubaguzi.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Hellօ, you uyilized to write brilliant articles, neѵertheless, tɦe last few posts Һave bеen sora
poor... I lose your tremendous composing. Ρast a feѡ plасes
aree only a little from track!
mү blog ... cat health bladder problems blood in urine
Post a Comment