‘Kwahiyo
nimpigia simu huyo mpelelezi nimuambie kuwa huo mzigo ninao hapa kwako,au sio?’nikauliza
huku nikitoa simu yangu tayari kwa kumpigia simu mpelelezi, baada ya kuona
mdada anakasirikia, na yeye akasema kwa haraka;
‘Huu
mzigo hautakiwa kabisa kuwa hapa kwangu, nilichofanya mimi nikuuondoa pale
kwako kwa muda ili polisi wasiuone, kwasababu hata hivyo huwezi kujua hao
polisi wana nia gani na huo mzigo, inawezekana ni kundi ambalo linataka
kuhakikisha unafungwa...’akasema
‘Ukumbuke
kuwa mimi niliuchukua kwa nia ya kukuokoa, na hapa nimeshapoteza muda mwingi,
ulitakiwa uwe umeshaondoka,....’akasema akiangalia saa yake.
‘Sasa....?’
akauliza
‘Mimi
nitaurudisha pale kwako,na wewe wasiliana na mpelelezi wako haraka iwezekanavyo
mtafute njia ya kukabidhiana huo mzigo, huo mzigo ni bomu, yeye atajua jinsi
gani ya kufanya,….’akasema na mimi nikawa kimiya akasema kwa ukali;
‘Unanisikia
mpigie kwa wakati wako, sasa hivi utoke humu ndani, umenielewa,au bado una
msimamo wako, ....?’ akauliza
‘Nipo
na wewe, japokwua sipendelei kabisa....’nikasema
‘Sasa
wewe ondoka,huu mzigo utaukuta huko kwako..’akasema mdada akitizama pale
kabatini na kuangalia saa yake na mimi nikainuka kuondoka, na ghafla
nikamuuliza swali
‘Sasa
huo mzigo utafikaje huko kwangu, maana nakuona upo mwenyewe au utawaita vijana
wako….?’nikamuuliza na yeye akawa haniangalii, alikuwa akitizama nje kwa
kupitia dirishani halafu akasema;
‘Hiyo
sio kazi yako,…nimeshakuambia uondoke, usipoteze muda, muda sasa hivi ni
mali....’akasema na mara tukasikia mlango ukigongwa, na mdada akasimama kwa
haraka,na kuelekea pale mlangoni.
Mimi
nikiwa na wasiwasi nikatega sikio kumsikiliza anaongea na nani, kumbe alikuwa
mlinzi wake, akawa anaongea na mlinzi wake, na baadaye nikasikia akisema;
‘Muite
huyo mtu ni mtu wangu ....’akasema mdada na kutoka nje kabisa, nilisikia mlinzi
akisema;
‘Sawa
bosi....’akasema huyo mlinzi na kukawa kimiya kidogo, halafu nikasikia mdada
akiongea na mtu mwingine kwa sauti ya taratibu sikuweza kusikia
wanachozungumza, ulipita muda kidogo, baadaye mdada akarudi ndani na alionekana
hana raha, akasema;
‘Hali
sio shwari kabisa, mambo yameharibika,...’akasema mdada, na safari hii akaja
kukaa karibu na mimi, na alikuwa akiongea kwa sauti ya ndogo kama vile hataki
mtu mwingine asikie, alionyesha ile hali ya kujiamini imemuondoka, ikabidi
nimuulize
‘Kwani
vipi mdada mbona umebadilika ghafla, kuna nini zaidi...?’ nikauliza nikiwa na
wasiwasi na yeye akaniangalia na kusema;
‘Polisi.....’akasema
mdada akiangalia kule kwenye kabati lake.
*********
Tuendelee na kisa chetu kwa kumalizia sehemu hii iliyokuwa imebakia kabla hatujaingia kwenye hitimisho.
‘Wamekuja au?’ nikauliza
‘ Polisi wamefika tena hotelini kwako kufanya upekuzi, na
wamesema watafanya msako huo kila kona na inavyoonekana wamejigawa makundi
mawili, kundi jingine lipo njiani kuja hapa kutafuta huo ushahidi....’akasema
‘kwahiyo kuna mtu kawaambia kuwa huo mzigo ulihamishwa
au wamejuaje mpaka waendelee kuutafuta?’ nikamuuliza
‘Kama kulivyo na watu wangu ndani ya kundi lao, ndivyo
na wao walivyo na watu wao ndani ya kundi langu, na sio rahisi kuwabaini watu
wao...nilijaribu kuwachuja watu wangu lakini sikuambilia kitu, cha muhimu ni
kuwahiana tu,….’akasema mdada na mimi nikamuangalia mdada, ambaye alisimama na
kusema;
‘Kwasasa tunahitajika kufanya jambo la haraka, maana hao
jamaa wapo njiani, hapa hatuna muda wa kupoteza….’akasema mdada akichukua simu
yake kuongea na watu wake.
‘Kwahiyo utafanya nini?’ nikamuuliza nikiangalia
mlangoni nikijua hao askari wanaweza kuja hapo , na mimi sikupenda wanikute
hapo.
‘Mimi nitafanya nini au wewe utafanya nini, hivi huoni
kuwa hili bomu ni kwako…mimi nafanya kukusaidia tu….’akasema akielekea kwenye
kabati akitaka kulifungua, na mara simu yake ikaita, akasikiliza kwa muda,
halafu akageuka kuniangalia huku akiendelea kuongea na simu, na alipomaliza
akasema
‘Mmm, naona uondoke wewe na mzigo wako...’akasema mdada akiwa kashikilia ufunguo wa kabati lake
‘Mdada, nitawezaje kuondoka nao.....na nyie mliokuja nao ndio mnaweza kujua jinsi gani ya kutoka nao, kunipa mimi ni kutaka nishikwe nao...’nikasema
‘Sikiliza nikuambie, wewe kwa sasa mpigie simu mpelelezi mkutane mahali,...ni muhimu sana
mzigo huo ukawa kwa mtu mwaminifu, mimi siwaamini hao polisi ....’akasema
‘Lakini....’nikataka kujitetea, na yeye akasema;
‘Lakini nini, fikiria jinsi ya kufanya, mimi sishindwi
kuurudisha huu mzigo hapo kwako, lakini nina shaka kuwa pale watakuwa
wameshaweka mitego, ukifika tu, watakuwahi, na hapa hautakiwi kabisa uonekane, na wakifika hapa watapekua kila mahali, unaona jinsi ilivyo, ni muhimu huu mzigo utoke hapa haraka iwezekanavyo, na siwezi kuwatumia vijana wangu kwa sasa, watashukiwa...’akasema
‘Sasa....ngoja mimi nimpigie simu mpelelezi...aja hapa kuliko mimi kutoka nao.’nikasema na
mdada akawa anafungua lile kabati
Nilipiga namba ya mpelelezi, na simu ikawa inaita tu, mpelelezi hakupokea hadi ikakatika, na kwa hali ile nikawa nimechanganyikiwa, nikageuka kumuangalia mdada, na mdada akawa ameshafungua kabati lake, akanuliza
‘Vipi....?’ akauliza
‘Hapokei simu, inaita tu.....’nikasema
‘Ngoja tuone tutafanya nini...'akasema mdada, na huku akiwa kashikilia mlango wa lile kabati, alikuwa hajatoa ule mfuko.
'Muda umekwenda sana, na ni muhimu huu mzigo
utoke hapa, na ni lazima ufike mikononi mwa mpelelezi, vinginevyo, ...’akasema
na akageuka kuongea na watu wake, na alipomaliza kuongea na simu akasema;
‘Naona polisi wapo njiani, walitakiwa wawe wameshafika
hapa, lakini cha ajabu kundi hilo limepitia ofisini kwao kwanza, na walifanya
kikao kidogo, halafu wakatoka, na sasa wanakuja huku, nafikiri walikwenda kupata kibali rasimi...'akasema huku kashika kichwa akiwaza
'Kwahiyo?' nikauliza
'Unajua wakati mwingine inabidi ufanya hata yale yasiyofanyika, ili tu uweze kuokoa kitu muhimu, nikuambie ukweli, huu mzigo sasa ni kitu muhimu sana, kwa polisi, wakiupata hatujui lengo lao litakuwaje, lakini kwa mtizamo wa haraka, wewe utakwenda jela....mahabusu...'akasema
'Na wewe?' nikauliza
'Mimi...!?' akasema kama anashangaa na baadaye akasema;
'Mimi usiwe na shaka nami, najua jinsi gani ya kujitetea hofu ni kwako...'akasema kwa kujiamini
'Kwahiyo....'nikasema nikiwa natafuta njia ya kukwepa kuondoka na huo mzigo, kwangu mimi nilishaona ni bomu kubwa sana, na mdada akatabasamu na kusema;
'Sasa tunataka tucheze
mchezo, ...unatakiwa utoke hapa kama mdada, unanielewa,...’akasema
‘Nini, kama nani, mdada usilete mambo yako tena...’nikasema
‘Wewe subiri....’akasema na kuingia chumbani kwake, na
alipotoka akawa katoka na nguo zake za kike, na vipodozi, mawigi, na...
‘Mdada unataka kufanya nini?’ nikauliza nikiangalia vile
vitu alivyobeba,
‘Wewe subiri, ujanja kuwahi,...’akasema na kuanza
kunikarabati usoni....
NB:Je watafanikiwa
WAZO
LA LEO: Wakati wengine wanalia watakula nini, kuna wengine
wanamwaga, kuna wengine wanatumia pesa nyingi tu kwa sherehe ambayo ingefanyika
kwa gharama ya kawaida, yote haya yanafanyika kutokana na utofauti wa kipato, au
kwa kujifaharisha tu.
Haikatazwi kufanya hivyo,kwani hayo ni maamuzi binafasi,
lakini mnaonaje nyie mnaotumia mamilioni ya mapesa, katika bajeti zenu za
harusi, mkaweka fungu la kuwasaidia mayatima, masikini na wasiojiweza, nafikiri
mkifanya hivyo sherehe zenu zitaleta tija sana, na baraka zitaongezeka.
Kwanini
tuweke fungu kubwa kwa vinywaji kula, na sijui nini mwisho wake ni kufuru tu. Jamni
tuwajali mayatima, tuwajali wasiojiweza, hiyo kwetu ni ibada kuliko hizo
sherehe za kufuru.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment