Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, January 2, 2014

Mkuki ni kwa Nguruwe-57

  
  Sauti iliyosikika, iliwafanya wajumbe wageuze vichwa vyao, kungalia ni nani aliyeongea hayo maneno, kwani wengi wa wajumbe walikuwa wakimwangalia mume wa familia, ambaye alikuwa akitembea kuelekea mlango wakutokea, akionyesha kuondoka nje ya kikao, lakini hata yeye aliposikia hiyo sauti,  akasimama kama mtu aliyegandishwa, na taratibu akageuka kichwa, kumwangalia huyo aliyetoa hiyo sauti, na macho yake yakakutana na huyo aliyetoa sauti, na kuuliza;

‘Na wewe pia, unataka kunisaliti...?’ akauliza mume wangu wafamilia huku akionyesha uso wa kushangaa na kutahayari, na watu wote wakageuka na kumwangalia huyo aliyeongea, ambaye alishaulizwa swali na mwenyekiti, kuwa je yupo tayari kuthibitisha hayo aliyokwisha kuzungumza shahidi aliyepita, na yeye akatikisa kichwa kuashiria kukubali...

Kutikisa kichwa huko kuashiria kukubali, kulimfanya mume wa familia kuinamisha kichwa upande, hakuweza kuamini kuwa huyo naye angemsaliti, kama alivyoita kusaliti, huku akiwa ameangaliana na huyo shahidi mpya, mume wa familia, akasema;

‘Na wewe pia ....haiwezekani, usidanganyike, na hadaa za hawa watu, ...’akasema huku akionyesha uso wa kukata tamaa, na huzuni, lakini shahidi huyu mpya akasema;

‘Hapa sio swala la mimi kukusaliti, tatizo ni kwamba nyani haoni kundule,na kama ni ubaya , umeuanza wewe, na haijalishi kama nitaongea au nitakaa kimiya, lakini ni bora niongee ili ukweli ujulikane kwa manufaa ya wengi....’akasema shahidi huyo mpya.

‘Naongea haya nikiwa nimeshaongea na mume wangu, na hatima yangu na mume wangu imeshajulikana, hakuna cha ajabu, tatizo ni wewe na mke wako, lakini kwanini tuendelee kuishi katika maisha haya ya sintofahamu, ya kudanganyana, ...mimi bwana nimeamua, ni heri kusema ukweli, ili haki itendeke, hata kama nitakosa kila kitu, lakini nitakuwa nimepaat kitu cha kudumu, ..ambacho ni haki na ukweli.

‘Wewe unanifahamu sana mimi nilivyo, jinsi gani ninavyokupenda, unafahamu sana jinsi nilivyojitolea kwa ajili yako, jinsi gani nilivyoweza kuvumilia, na kuyafanya yale ambayo sikupenda kuyafanya yote hayo niliyafanya kwa ajili yako, hebu niambie ni mapenzi gani unayoyataka,kutoka kwangu, je mimi ni tofauti na hawo wanawake wote uliwahi kutembea nao, ina maana mimi ni nani kwako, mimi ni njia ya kufanikisha starehe zako, hapana, nasema sasa basi, kama unanipenda kwa ukweli basi turudi kijijini, tukaanze maisha mapya, kama hilo litawezekana....’akatulia na wakawa wanaangaliana.

‘Sikiliza wewe, mbona unaharibu,  funga hilo bakuli lako...unawafahamu hawa watu, unavyoongea hivyo unawapa faidia, na haitakusaidia lolote, wao wanachotaka ni ....uwaambie huo wanaouita ni ukweli, ili mwisho wa siku waweze kukutia kitanzi shingoni, ukose haki zako zote...sikiliza, hakuna ukweli, ukweli ni mkataba wangu, ukweli, ni kuwa mimi ni mume wa halali,....usiongee sana...sanasana utaishia jela, hakuna atakayekumini.....’akasema.

‘Mimi sitaki chochote kutoka kwao, nimerizika na maisha yangu na umasikini wangu, na hivi sasa siogopi kwenda jela tena , baada ya kusikia hayo yote uliyoyafanya wewe, ambayo nilikuwa nayasikia tu, sikuwa nimeyafuatilia kabla,..hata huyobinti wenu wa kazi, ...kwakweli umezidi , na ni bora niseme ukweli uamue moja, ni yupo aliye halali kwako, mkeo, sasa hakutaki tena, ni nani atakeyakutaka kwa tabia zako chafu, huyo umeshamkosa, kabakia, rafiki wa mkeo, naye, sijui,...una mfanyakazi wako wa ndani,...hivi wewe unanionaje mimi....eeh...

‘ Mimi nilishakuambia toka awali, njia tunayopitia sio sahihi, ukanikatalia, ukamsikiliza marehemu, ukisema yeye ni msomi anayeona mbali, je hicho alichofanya ndio kuona mbali, ...?’ akawa kama anauliza lakini ilionekana kuwa hakutaka kujibiwa akaendelea kusema;

‘Mimi nilitumai kuwa umeshajifunza, kwa hayo yaliyotokea, kama kweli ulikuwa na nia njema, kama sio kunitumia, nichakae,na baadaye uendelee kuzaa na wanawake wa kila namna.Kama kweli unanipenda,  turudi kwetu kijijini tukajipange upya, tuachane na maisha yasiyona mpangilio, hebu angalia, alichokuwa akikihangaika Makabrasha kipo  wapi, kapata nini na sasa yupo wapi,je wewe una uhakika gani na maisha ya kesho na kesho kutwa, kuwa wewe utakuwa mjanja kuliko huyo aliyemkatiza maisha mtaalamu wako,  ...’akatulia akiwa anamwangalia mume wangu.

‘Mimi nimechoka, siwezi tena kuvumilia, siwezi tena kutumika, yaliyotokea yametokea, na yaliyofanyika yamefanyika, hakuna faida iliyopatikana, san a sana ni kujiweka kwenye maisha ya utata....mimi nimeshamwambia mume wangu kuwa aniache, mimi sio stahili yake, ...akubali sikubali huo ndio ukweli,....’akageuka kumwangalia mume wake, ambaye alikuwa kainama chini, akiwa kashikilia kichwa.

‘Hivi ni nani anaweza kuyafanya haya yote niliyoyafanya, wakati mwenzake, anastarehe, na wanawake tofauti-tofauti, anazaa watoto, mimi mpaka sasa sina mtoto hata mmoja, eti kutimiza ahdi na mipango isiyofikilika, hivi ni nani, ataweza kuvumilia hayo yote uliyoyafanya, ina maana mimi nimeumbwa na moyo wa jiwe, niweze kuyavumilia hayo yote, je hivyo ndivyo tulivyokubaliana...’akamwangalia mume wa familia, ambaye alikuwa naye amemwangalia kwa macho ya kukata tamaa.

Mume wa familia akageuka kuwaangalia watu, na akiwa kama vile mtu anayeogopa au kutaka kukimbia, aligeuka huku na kule, halafu akamwangalia muongeaji na kwa sauto ya unyonge akasema;

‘Sikiliza nikuambie, mambo yatajiweka sawa, usiogope vitisho vya hawa watu, usilainike kwa propaganda zao, mbona mambo yapo shwari tu,...nisikilize kwanza, usianze kuongea ovyo....utaumbuka, watakufunga hawa watu, hawana ubinadamu hawa.....’akawa anaongea , na sasa akawa akimsogelea  huyo shahidi mpya,na watu wote wakawa kimiya wakiwasikiliza wao, na mume wa familia alipomkaribia huyu shahidi mpya, akasimama, wakawa wameangaliana, lakini muongeaji, akageuka kumwangalia mwenyekiti na kusema;

‘Nimesema nipo tayari kuthibitisha hayo aliyoongea mwenzangu, kwani mimi ndiye niliyekuwepo toka mwanzo hadi mwisho wa mipango yote hiyo, japokuwa sio kwa kuitunga, lakini kwa kutumiwa.Mimi nafahamu mipango yote toka kijijini hadi kuja hapa Dar, mimi namfahamu marehemu, kuliko mtu yoyoye humu ndani, na mimi namfahamu mume wa familia kuliko watu wote humu ndani, kwahiyo ni wajibu wangu kulimaliza hili moja kwa moja, ...’akasema 

Mwenyekiti akatabasamu, na bila kusema neno, akamwangalia muongeaji, akisubiria kusikia ni kitu gani, ataongea huyu shahidi mpya
.
Mume wa familia akanyosha mkono kutaka kumshika huyo muongeaji, lakini huyo muongeaji, akauona ule mkono na kuusukuma mbali na..na hapo mume wa familia,akasema kwa sauti ya ukali;

‘Hivi wewe umechanganyikiwa unataka kusema nini, ....’akasema mume wangu akimsogelea huyo muongeaji, na muongeaji akamsukuma pembeni, na kumwangalia mwenyekiti, kama vile anaomba msaada, na mwenyekiti akasema;

‘Mume wa familia, kaa chini, ....mpe nafasi shahidi wetu asema ukweli, wewe huna mamlaka ya kumzuia shahidi wetu huyo, ukweli tumeshaujau kabla,a yeye anauthibitisha tu, hata ukijaribu kumzuia haitasiaidia kitu, mimi namfahamu yeye kama ninavyokufahamu wewe, kwahiyo sogea pembeni, muachae mwenzako aongee....’akasema mwenyekiti.

Mume wa familia, akabakia akiwa kaduwaa, hakujua afanye nini tena, akakaa kwenye kiti kilichokuwa karibu na huyo muongeaji, huku akiwa kainamisha kichwa chini kama alivyokuwa kainamisha kichwa rafki yake, ..

********

‘Kila jambo lina mwanzo na mwsho wake, mimi nimeona mwisho wa haya yote ni hapa, na hakuna jingine ila nikuelezea ukweli, na nyie mtaamua ,mtakalolifanya....lakini nawashauri, kuwa muwe makini na mamauzi yenu, msikimbilie polisi,, kama mtakimbilia polisi, mnaweza msifanikiwe, kwani huko kote niliwahi kupitia, nikakatishwa tamaa, ndio maana nikaamua kufanya nionavyo mimi....’akasema.

‘Ili kupata ukweli,na kumlnda yule asiyependeka,  nilijitolea maisha yangu, hata kuzalilika,.., nikaamua kuwa na adui yangu, uso kwa uso, hata kulala naye kitanda kimoja, ili ...eti kumlinda mpenzi wangu, jamani, ....hivi ni binadamu gani angaliweza kuyafanya haya yote, kwa ajili ya mtu kama huyu...nimakata tamaa, ndio maana nimeamua niseme ukweli, ili jamii isikie, na watakaojifunza wajifunze, ..

‘Hapa nilipo natafutwa, sio na polisi tu, ..bali na wale wanaotaka ukweli huu usilijulikane,..na mimi ushaidi wangu nitaugawa sehemu mbili, ya kwanza, ni historia na chimbuko la haya, na pili, jinsi mauaji ya ya amrehemu yalivyofanyika....’akasema na hapo mume wa familai akainua kichwa na kumwangalai mwenzake, kwa macho yaliyojaa chuki.

‘Kwanini niwaaambie nyie, badala ya kwenda polisi, ...kwasababu, jamii ndiyo inahitajia ukweli kwanza, na sheria, itachukua mkondo wake, baadaye, kama watathibitisha kuwa mimi ni mkosaji, ..jamii ndio yenye mamlaka,na ukificha ukweli kwao, unaikosea, na bora kusema ukweli kwa wale uliowakosea, kuliko kuiacha sheria ambayo huenda, ikakutaka ufiche ukweli....’akatulia.

‘Kuna watu wananitafuta ili waniue,...ili siri isivuje, ili ...mwisho wa siku ukweli usijulikane, na yatakayofuata baadaye, ni mfarakano, wa familia hii, na watu ambao watakuja na madai mengine mapya,wameshajipanga,hamyajui hayo...ndio maana kijana aliyetoka, alipoona hamtaki kumskiliza,a akaona njia bora ni kwenda kutafuta sehemu ya kujificha, lakini utajificha mpala lini,....’akatulia huku akiwa kamwangalia mwenyekiti, na mwenyekiti akawa anamwangalia bila kupepesa macho,

‘Ndugu mwenyekiti, mimi ndiye mpenzi wa asili wa mume wa familia...’aliposema hivyo watu wakahema, na wengine wakaguna.

‘Mume wangu anafahamu hili, na huenda yalitokea hivyo wengi wakifikiria huenda tulilifanya hilo kwa kulipizana kisasi, kati ya mume wa familia na rafiki yake, hayo wanayajua wao, lakini kiundani smimi na mwenzangu, yaani mume wa familia na mimi tulifahamu ni kitu gani tunakifanya, ...’akasema na kugeuka kumwangalia mume wa familia ambaye alikuwa hataki hata kumwangalia.

‘Nafahamu, kikweli kuwa wazazi wa familia ya mke wa familia, wanatufahamu sana, lakini sio kiundani kihivyo, ...ndio maana ndoa zetu hazikubarikiwa,kwa  upande wa mume wangu na kwa upande wa mke wa familia, wote walipinga sana hizi ndoa zetu, sio kosa lao, wanatuhamu, wanafahamu chimbuko letu,japokuwa kama mambo yangekwenda vyema, kusingelikuwa na ubaya kwa ndoa hizo....’akasema na kuinama chini kama anayesoma kitu.

‘Ina maana masikini hatakiwi kumuona tajiri, au tajiri hatakiwi kuolewa na masikini, hii sio halali, upendo wa kweli hauangaliii maisha ya kifedha, ...umasikini kisiwe kikwaza ya kuwanyima watu haki zao, za kupendana, ...nasema haya, kwa wale waliobarikiwa, na huenda hata sisi kama mambo yangelikuwa sawasawa, kama kusingelikuwa na ajenda za siri, kama ilivyokuwa kwenye ndoa zetu. Mimi na mume wangu tungelikuwa tunaishi kwa raha na amani....

‘Mimi na mwenzangu tumezaliwa kwenye familia za kimasikini, familia duni, iliyogubikwa na mitihani ya kila namna, sitaweza kuisema , ila ninachoweza kusema hapa  ni kuwa mimi natoka kijiji karibu na kijiji cha mume wa familia, wote mnalifahamu hilo, na familia zetu ni zile familia zalili sana huko kijijini, na huena ndizo familia za kutolewa mifano, kuwa ni familia duni, ni nani angakubali kuolewa au kuoa kwenye familia kama hizo, inayobakia ni ndoto za Alianacha, kuwa siku moja nitamuoa, au kuolewa na binti  mfalme, au mtoto wa mfalme,...

‘Lakini kwa mipango iliyopangwa, na makubaliano, kati yangu na mwenza wangu, tukajikuta sote tukiingia 
kwenye familia zenye uwezo, japokuwa kiundani mimi na mwenzangu tunapendana sana, pendo la asili, ambalo tuliwahi kulifunga kwenye hanaki la umasikini....baaa ya kuvikana pete ya uzalili, na umasikini, tulikaa na kujadili, 

Mjadala ulikuwa wa kulalamika, ...ina maana sisi tutakuja kuishi kama walivyoishi wazazi wetu, ina maana watoto wetu watakuja kuzalilika, na kuishi maisha ya umasikini kama tulivyourithi kwa wazazi wetu, tukasema hapana, ..tufanye jambo, dau yetu ichanganyike na damu ya kitajiri, ili .....oh..’hapo akatulia kwa muda akiwa kainamisha kichwa chini kama anawaza jambo, na alipoinua kichwa machozi yalionekana machoni, akasema;.

‘Samhani mimi sio mtu wa kulia lia ovyo,..haya yamenitoka tu kwa bahati mbaya,...hayatarudia tena...’akasema na kufuta yale machozi, akaendelea kuongea;

‘Tulijadili sana, jinsi gani ya kuwapata matajiri, je inawezekana kweli, mimi niolewe na tajiri, utawezaje kumshawishi tajiri kuja kunioa mimi, au utawezaje kumshawishi binti wa geti kali kuja kuolewa na mlalahoi kama mwenzangu alivyokuwa...huwezi kulazimisha pendo, au sio, lakini bahati nzuri ikatokea kama dhamira zetu zilivyokuwa, kila mmoja akapata tarajio lake kwa nyakati tofauti, huena ilitokea hivyo ili iwe sababu ya watu kujifunza....

‘Wa kwanza kumpata mwenza ilikuwa ni mimi, nikampata mume mwenye uwezo, na nikamwambia mwenzangu kuwa nimempata mume mwenye uwezo sasa tufanya nini, ..mwenzangu akapagawa na kukasirika, wivu ukamjaa, siunawafahamu wanaume kwa wivu, akasema haiwezekani, akawa kasahau makubaliani yetu, na wakati tunapingana, tukiwa tumenuniana siku mbili tatu,, mwenzangu akiwa hataki hata kuongea na mimi akakutana na binti wa kitajiri kwa mazingira yaliyokwisha kuelezewa..wakajikuta wame...mtamalizia wenyewe..’akacheka kidogo.

Haraka akaja kwangu na kuniambia kuwa hata yeye kampata mwanamke, tajiri, kwahiyo tupange mipango yetu,....mwenzangu kwa haraka, akamwelezea mshauri wake. Yeye alikuwa na jamaa mmoja ambaye alimuamini sana, akawa ndiye mshauri wake, jamaa anayejiita msomi. Na huyo jamaa alipoambiwa hivyo, akamwambia mwenzangu ampe huyo jamaa muda wa kulifanyia hilo kazi.

‘Mnafahamu hiyi ni bahat kubwa sana, sasa umasikini bai-bai, kama mtafuata masharti yangu, mtafanikiwa lakini mkiwa wajinga, makajianganay kuwa ..ooh, nimeolewa, ooh, nimemuoa, tajiri, mtakufa masiki...’hiyo ilikuwa kauli ya huyo mshauri wetu, nikaona hapo tumefika.

Baada ya siku mbili, huyo mshauri akaja na mikakati ya jinsi gani ya kufanya....

Ilitakiwa tuolewe lakini kwa lengo moja la ndoa...ili tupate haki za ndoa, maana kiukweli mimi na mwenzangu tunapendana, hata nikiwa na mume wangu kitandani namuwaza mwenzangu,nahisi hata yeye ilikuwa hivyo hivyo, kama nafsi yangu hainidanganyi..kwahiyo ndoa zetu zikawa kama seehmu ya kuchuma, kuwekeza kwa baadaye....na tukifanikiwa basi tutafute njia ya kujitoa kwenye hizo ndoa ili tuje kuoana ....’akacheka kidogo hapo.

‘Hivi kweli inakuja akilini..lakini ndivyo mikakati ilivyopangwa na huyo mshauri, kuna mambo mengi tulikubaliana, kuwa tujizuie kupata watoto,ili watoto wasije kwua kisingizio, au tukutane kisiri tupate mimba, na hizo mimba tuwabambikie waliotuoa......ndivyo mikakati ilivyokuwa hivyo.

‘Jingine kubwa ilikuwa, kutafiti undani wa familia tulizoolewa, tujua ni jinsi gani walivyopata utajiri, na tuweze kugundua nyaraka zitakazotuwezesha sisi  kutwalia mali na kuishia, tukizipata hizo nyaraak tumpe mtaalamu, yeye atajua jinsi gani ya kuzigushi...kinamna, yeye ni mtoto wa majini.

Asikudanganye mtu, ukishaolewa au kuoa, akili yako yote inakuwa kwenye ndoa yako, ndoa inanoga,a sikuambie mtu, hasa kama umeingia kwenye sehemu unayopata kila kitu, ndoto, na mipango tuliyopanga ikayeyuka, na kila tukikutana kila mmoja anakuwa na dharura, hana muda wa kuliongelea hilo, haat huyo mshauri tukawa tunampiga chenga, na hilo zoezi likafa, na kila mmoja akawa na malengo na ndoa yake.

Ni kweli moyoni bado kila mmoja alikuwa akimkumbuka mwenzake, lakini ki hali halisi, ni nani angekubali kuachia hali aliyo nayo, akarudi kwenye umasikini, hakuna, tulipokutana tena, akiwemo mshauri wetu, tukalibainisha hilo wazi kuwa ile mipango ya awali isitishwe, kwani haiwezekani. Kila mmoja karizika na ndoa yake.

Kauli hizo zikamkatisha tamaa mshauri wetu akatuona sisi ni wasaliti, akatuona sisi hatuna maana, na akaapa kuzisambaratisha ndoa zetu, na kusema hazitadumu, maana tumeolewa au kuoa, kwa ajili ya mali tu, na sio kwa ajili ya upendo.

‘Nyie mtaona, sizani kama ndoa zenu zitadumu,...’ikawa kiapo chake.dhidi yetu

Ndoa ya mwenzangu ilianza kuonyesha nyufa, baada ya kuzaa watoto wawili, na katika makubaliano yetu ya awali ilitakiwa mtu asizae, kwani ukizaa watoto watakuwa vikwazo, mwenzangu yeye akazihirisha wazi kuwa yeye hayupo tena kwenye makubaliano yetu, na hata nilipoongea naye, alionyesha kutokunijali tena, nikafahamu kuwa penzi letu la asili limeshavunjika, kwahiyo mimi nijipange kivyangu.

Baada ya mwenzangu kupata watoto wawili, nikaona mambo yanageuka, na mara mwenzangu akaja kunikumbushia ile mipango yetu, nikashangaa, na kumuuliza iweje sasa, na wakati yeye ana familia yenye watoto tayari, akasema, hana raha kwenye ndoa yake, anaishi tu kwa vile ni sehemu yenye utajiri, lakini ndoa yake anaiona kama jela. Ohoo nikakumbuka ule usemi usemao, utasema hakifai, au hakitoshi kwa vile unacho, wakati ulipokuwa huna, ulikitamani.....sasa ndio yakawa kwa mwenzangu.

‘Sasa unataka tufanye nini?’ nikamuuliza

‘Tumtafute Makabrasha atusaidie,..’akasema

‘Hapana, achana kabisa na huyo mtu, huyo mtu sio mtu mwema, atakuangamiza, na kukuacha ukiumia,...’nikamwambia,na kweli mwanzoni akanisikiliza, kumbe mwenzangu alishaingia kwenye mambo mengine ya ndani, akawa hawezi kuvumilia, akaanza kutembea na mfanyakazi wao wa ndani, ..hayo alinificha kabisa, sikuyafahamu hadi huyo binti alipofika huko kijijini na mambi yakanifikia, nikamuuliza mwenzangu akanikatalia

Nikakutana na Makabrasha, na yeye akajifanya hajui, lolote, kumbe mwenzetu alishapata upenvyo wa kuingiza mambo yake, akawa kapata nafasi ya kupata taarifa zetu za ndani, na aliyewezesha hayo ni binti huyo huyo aliyebakwa na mume wa familia,na mimi sikuyajua hayo, na nisingeliweza kujiingiza huko, kama isngelikuwa kazi yangu niliyokuwa nimeajiriwa nayo, na alijua ili aweze mambo yake,  ni vyema anidhibiti mimi kwanza.

Makabrasha alinifahamu toka siku nyingi, na alijua kuwa mimi sio mwepesi kuingilika kama alivyokuwa mume wa famila, na alinifahamu kuwa mimi ni mpinzani wake, kwahiyo akaona aniweke kwenye makucha yake kwanza, alichofanya ni kufuatlia nyendo zangu, kila ninalolifanya yupo nyuma yangu, na alinipatia kwenye kazi nilizokuwa nikipewa.

Kuna akzi nyingine ilibidi ujifanya wewe ni changudoa, na unabidi wakati mwingine ujitolee kufany hata yale ualiyoyafanya, yeye akachukua kumbukumbu za matukio hayo, kama kinga yake, ujue kazi hiyo nilikuwa naifanya hata mume wangu hajui, ...yeye alijua nafanya kazi za akwaida ninazozifanya kila siku, kumbe mwenzake nilikuwa na kazi za ushushu

Ukumbuke kuwa mimi na mpenzi wangu wa zamani pendo letu lilikuwa lipo pale pale, kwahiyo siku mume wa familia akikazika, anakuja kwako, namliwaza, hapo Makabrasha akapaat ushahidi wa kutosha, wa kunifanya mimi nifanye kile anachokitaka, nikawa mtumwa wake

Makabrasha, alipoona pia kuwa hayo alivyoyachukua kwangu hayampi mwanya wa kuyafanya yale anayoyataka yeye, akaamua kuingia ndani zaidi, ndio akagundua yale yaliyokuwa yakiendelea ndani ya familia ya mume wangu, mpaka akafikia kiwango cha kugundua hiyo mikatana ya siri kati ay mume wa familia na mkewe. Alipoligundua hilo, akaanza kutoa vitisho kwa mume wa familia, kwanza alifanya hivyo akiwa akjificha, lakini baadaye aakjitokeza wazi kuwa yeye ndoiye yupo nyumba ya hayo yote.

Siku hiyo akatuita kikao mimi na mume wa familia, na kuongea na yake ya kuyafanya hayo yote, na akasema kwa vile amegundua kuwa ndoa ya mume wa familia na mkewe haipo kwenye msimamo mwema, hiyo ni kuashiria kuwa siku yoyote ndoa hiyo inaweza kuwa marehemu, kwahiyo kabla ay hayo yote, inabidi upanhgwe mpango wa kuyamiliki makapuni yote,..

Mume wa family alipinga sana, lakini alipoonyeshwa madhila yake, alivyombaka mfanaykazi wa ndani, alipokuwa akitembea na mimi alivyokuwa kaitembea na rafiki wa mke wa famila, ikaonekana kuwa hataweza kusamehewa kwa makosa yote hayo, kinachotakiwa ni kwanza ni kuubadili mkataba wa hiari katio ya wawili hawa,..

Je hilo lingefanyika vipi, ikabidi atafutwe mtu wa ndani, mtu anayeweza kusaidia, hilo, akafikiriwa rafiki wa mke wa familia, lakini ikaonekana hataiweza hiyo kazi, kwa vile ana majukumu mengine, yeye alitakiwa baadaye awe ni kiongozi muhimu kwenye makampuni ambayo Makabrasha atakuja kuyamiliki, kiongozi wa usalama. Alipofikishiwa hii taarifa, kama ilivyotegemewa akakataa, na japokuwa alipewa hivyo vitisho, lakini yeye hakuogopa, ikabuniwa njia nyingine, ...akaitwa, na mtoto akatekwa nyara.

Tukirudi nyuma, ile ajali ya mume wa familia, ilitokea katika harakati za kubadili mikataba, kutoka ya zamani na kuwekwa mikataba mipya ya kugushi, na hayo yote yaliwekewa muda maalumu, mume wa familia, kwa kujisahau akaenda kumtembelea rafiki wa mke wa familia, nia na lengo ni kumjulisha mipango ambayo yao na kumpa matumaini kuwa mipango hiyo ingemsaidia huyo rafiki wa mke wa familia.

Alipofika huko akashangaa kumuona mke wa familia ambaye alijua kuwa yupo kazini, na kwa muda huo akapokea ujumbe wa simu ukamuhimiza kuwa mkataba wa zamani, mmoja uliopo kwenye nyumba ya familia unahitajika haraka,ili zoezi likamilike, akakumbuka kuwa aliusahau kwenye sofa wakati anausoma, kwahiyo akakurupuka mbio .....

Mkataba huo, ulikuwa nakala ambayo mke wa familia alikuwa akiuutumia, na alikuwa kauandika andika, huo ulitakiwa ili kukamilisha zoezi zima, kwahiyo akatoka pale mbio, kurudi nyumbani kabla mke wake hajarudi nyumbani. Kwanini ilikuwa ni kwa haraka hivyo, ni kwasababu mume wa familia alijua kuwa mke wake atakuwa yupo kazini, kumkuta pale akajua kuwa akitoka hapo anaelekea nyumbani, na akirudi nyumbani zoezi litakwama, wasiwasi, na vitisho, vya Makabrasha vikamchanganya, akakanyaga mafuta kupita kiasi na ajali ikatokea.

Makabrasha anaifahamu kazi yake vyema, kwenye kucheka atacheka, kwenye kazi, vitisho, atakutisha kweli,...alijipanga vyema,kwahiyo huo ujumbe aliomtumia mume wa familia uliambatana na picha mbaya ya uchafu waje...akaonywa kuwa, kila kitu kikichelewa nakala moja moja ya ya mchafu yake itakuwa ikitumwa kwa mke wa familia, na wazazi wa mke wa familia,...

Bahati,ikatokea hiyo ajali....ajali hiyo ingechelewesha mambo mengi, lakini kwa Makabrasha ikaonekana ni bahati nyingine nzuri, tunaweza kusema kwake ilikuwa ni bahati nzuri, japokuwa ni ajali, ajali hiyo ikatumiwa kama kisingizio cha kufanikisha mambo mengi kama malivyoona, na kama alivyoelezea  mwenzangu aliyetangulia.

Kuna mtu  ambaye alitumiwa kama tarishi, wa kuzunguka huku na kule , akipewa maagizo na kupeleka hiki na kile huyu ni mdogo wa mume wa familia, yeye kwa asilimia kubwa hakufahamu , na hakutakiwa afahamu ni kitu gani kinachoendelea, kazi yale ilikuwa kumtii kaka yake,na kaka yake, alikuwa akipewa amri na Makabrasha.

 Kuna mtu mwingine ambaye alikuwa kinara wa hayo yote, akiwa kama msaidizi wa Makabrasha, ambaye hadi sasa watu hawajamgundua,  mtu huyu ni hatari hata kuliko baba mtu, huyo ni mtoto wake, ambaye ni wakili, huyo ni mtoto wa nyoka. Yeye aliweza kupenya kwenye sehemu mbali mbali na kupata taarifa nyeti. 

Watu hawajiulizi ni kwanini alikuja kuwekwa wa tatu kwenye mirathi, wakati hata ndani ya familia alikuwa ahjulikani sana.

Mipango ilipokamilika na mikataba halali iliyokuwemo kabla ikaibiwa, na kuwekwa mikataba iliyogushiwa, na kilichobakia ulikuwa mkataba mpya ambao ulionyesha dhamira ya Makabrasha, na huo ulileta sintofahamu, lakini kwa vile Makabrasha alishajiandaa kwa hilo, akatoa vitisho vyake, na mume wa familia akasalimu amri.

Kilichoweza kusaidia ni nakala hiyo ya kwenye mtandao, kama angelifikira hilo mapema, angaliuondoa, kwani Makabrasha ahshindwi kitu, kwani wahusika wote walishawekwa kwenye makucha ya ,Makabrasha, na ilipohakikishwa kuwa kila kitu kimekwenda sawa, Makabrasha akaanza makeke yake, hakutosheka, na kile alichopata, akataka sasa kumuliki kampuni kwa kiwango kikuwa cha hisa,..

Yeye akatayarisha mkataba wa makubaliano kati yake na wamiliki wa makapuni na yakimuweka yeye kuwa kama mumiliki wa hisa nyingi kwenye kampuni ya mume wa familia,kama alivyozoanisha kwenye huo mkataba, - kwa makubaliano , na haikuishia hapo, ukatayarishwa mkataba mwingine ambao mali yangu ikiwemo hospitali ya mume wangu yeye awe na hisa na nayo yalishafikia hatua ya mwisho, na kama kikao kile cha kusaini huo mkataba kingelipita basi ungelisikia makali yake, lakini hakikufanikiwa kwani ndio siku Makabrasha aliuwawa...’akasema na kutulia, mwenyekiti alipoona mungumzaji katulia akamuuliza.

‘Kwahiyo kutokana na malezo yako,wewe uliamua kumuua Makabrasha ili kutokuwezesha huo mkataba usainiwe,ndivyo unavyotaka kusema hivyo ’ akauliza mwenyekiti akionyesha kushangaa na kutokuamini.

‘Kifo cha Makabrasha ni tukio ambalo halikutarajiwa,...nitalielezea kwenye sehemu hii ya pili, lakini kwanza nawaomba kitu kimoja...’akasita kidogo, na kuchukau leso kufuta jasho, na baadaye akasema;

‘Kitu gani unachotuomba, ..?’ akauliza mwenyekiti

‘Ni hivi...’akaanza kuelezea shahidi huyu,

NB: Je itakuwaje, tuanze kuingia kwenye hitimiskho

WAZO LA LEO:Kila mtu ana ndoto zake, na ndoto nyingine ni za kufikirika tu, hatuwezi kupanga kununua gari , kujenga nyumba, au kufanya jambo kubwa wakati uwezo huo hatuna. Tunaweza kuweka malengo hayo, kwa mipangilio ya kimaisha, lakini  hatuwezi kulazimisha yale yaliyo juu ya uweze wetu, tupange kutokana na uwezo na kipato chetu. Zaidi ya hapo tutaingiwa na tamaa mbaya, ambayo mwisho wake hauna heri kwetu.

Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Kwakweli dunia ina mambo,najifunza mengi kutokana na kisa hiki,NAKUSHUKURU SANA