Watu wote walikuwa
kimiya wakitaka kusikia kauli ya shahidi huyo mpya, hasa pale alipotoa ombi,kwa mwenyekiti, la kuomba
jambo ambalo hakuliweka wazi, na mwenyekiti akiwa na mashaka na huyo shahidi akamuuliza ni ombi gani
hilo,
Tuendelee na kisa chetu..........
‘Kifo cha Makabrasha
ni tukio ambalo halikutarajiwa na wengi, hata mimi sikutarajia kuwa huyo mtu
angeliuliwa kirahisi hivyo,...nitalielezea hili kwa undani zaidi ili kila mtu
apate kuelewa, ila kabla ya kulielezea hili, nina ombi moja kwako mwenyekiti na
washiriki wa kikao hiki...’akasema shahidi.
‘Kitu gani unachotuomba, ..?’ akauliza mwenyekiti na shahidi
huyo akatoka pale alipokuwa amekaa akatembea hadi alipokaa mwenyekiti na kuanza
kumnongoneza jambo, waliongea kwa muda, kwa kunong’onezana, na mwenyekiti akawa
kama anakataa, kwa kutikisa kichwa na alionekana kabisa hataki hayo anayoambiwa
na huyo shahidi,...
Baadaye mwenyekiti akasema , kwa sauti ambayo tulimsikia ;
‘Nitampigia yeye mwenyewe, atajua ni nini la kufanya lakini mimi
sitaki kabisa ...’akasema na akashisha sauti, kwani shahidi alionekana
kutokutaka hayo anayoongea naye yaisisikike, na alipoona mwenyekiti hakubaliani
naye, akasogea kinyume nyume akiwa kama katahayari, hata hivyo, akageuka na
kurudi sehemu yake, na kuanza kuongea;
‘Nafahamu kabisa wote humu ndani nii watu wenye hekima,
akili na utashi wa kufikiri, haya nitakayowaelezea hapa ni mambo ambayo
sikustahili kuwaelezea, ni mambo ambayo nilitakiwa niwaelezee polisi, lakini
kwa ajili ya kuliweka hli jambo sawa, nimeamua kuwalezea, kwani nikiacha kuelezea ilivyokuwa mkitoka
hapa, kila mmoja atatoka na yake, na mwisho wake, nitakamatwa kabla sijamaliza
kile nilichokianza.
Mwenyekiti aliposikia hivyo, akainua simu yake na kumpigia
mtu, na kumfanya shahidi atulie kwanza, na mwenyekiti akawa anaongea na simu
huku akiwa kainama na alikuwa akiongea kwa sauti ndogo, kama vile hataki watu
waliopo humo ndani kusikia anachoongea, na alipomaliza akasema;
‘Samahani kidogo, nilikuwa naweka mambo sawa, ...haya
shahidi unaweza kuendelea na maelezo yako....’akasema mwenyekiti akionyesha kukerwa
na kitu, na shahidi akatulia kwanza akimuangalia mwenyekiti na baadaye akasema;
‘Ni hivi...Makabrasha hayupo peke yake, japokuwa wenzake,
wameamua kujifanya hawahusiki, na hata mimi sikuwahi kuwa na hawo wenzake kwa karibu,ila
niliwahi kusikia wakiongea na Makabrasha wakipanga mipango yao, na kuna watu
wakubwa tu, lakini kwa nafasi yangu siwezi kusema lolote hapa, ila kuna mtu
mmoja ambaye alikuwa akifika mara kwa mara kuonana na Makabrasha, nitakuja
kumuelezea mwishoni kama mambo yakienda sawa ....’akaelezea huyu shahidi.
‘Kwahiyo sio swala dogo kama mnavyolifikiria nyie, ...mimi
nitajitahidi kuelezea upande wa mtu wetu tu, ambaye anatuhusu sana,...huko
kwingine hakuwahusu,...kwa manufaa yenu, na kwa manufaa yangu pia,...kwa wenye
kuelewa wataelewa, na hata mkisikia leo nimekamatwa, au ku-uwawa, mjue jinsi
gani ya kulieleza hili kwa jamii...’akasema kwa sauti ndogo.
‘Mwenyekiti nafahamu toka awali umekuwa makini na swala
hili, nafahamu ni kwanini, na nafahamu kuwa wewe na polisi mnaaminiana sana,
lakini nakupa angalizo, kuwa kumbukumbu nyingine walizokupa wewe, ni za uwongo,
kuna mambo wameyaficha, makusudi, huenda ni katika mbinu zao kwa ajili ya
kufanikisha kazi zao, au ni kwa ajili tu ya kuficha ukweli...mimi huko sitaongelea
sana kuthibitisha hayo....’akasema na mwenyekiti akamwangalia kwa mashaka,
lakini hakusema kitu.
‘Nafahamu kabisa kuwa mwenyekiti hunifahamu undani wangu,ninaishije
hapa Dar, zaidi ya kufahamu kuwa
nimeolewa na docta, na wewe ulikuwa mstari wa mbele kuipinga ndoa yangu, siwezi
kukulaumu sana, ...kwa vile unafahamu sana asili ya huko nilipotoka, na kwa
hekima zenu, haya yanayotokea kama wangeliwasikiliza nyie huenda haya
yasingelitokea. Lakini yote ni maisha....’akasema shahidi.
‘Maisha yangu ya kawaida, licha ya ndoa, wengi wananifahamu
kama mama shughuli, leo nipo hapa kesho nipo kule, hata mshirika wangu hajui
zaidi ya kunitumia kwa manufaa yake...hata mume wangu hajui zaidi ya kunifahamu
kama mama shughuli..’akasema akimgeukia mume wangu na baadaye mume wake.
‘Anayenifahamu vyema, ni rafiki wa mke wa familia, kwani yeye ndiye
aliyekuwa bosi wangu, hata mke wa familia hanifahamu vyema, zaidi ya kuwa ni
jirani yake, na zaidi ya kuniona nikimsaidia rafiki yake kwenye mambo fulani
fulani...nawaambia hivyo, maana kama mambo haya yatakwisha kwa amani, basi
sitaki tena kazi hizi za hatari, mimi nimejipanga kivyangu, maisha ni popote,
hata kijijini inawezekana....
Mimi ninachotaka kuwaelezea ni jinsi gani ilivyotokea, siku
Makabrasha alipouwawa, ...ni kweli nilikuwepo kwenye hilo jengo, ....’akatulia
kidogo akimwangalia mwenyekiti, kama anachelea kuongea jambo, lakini mwenyekiti
akamuashiria aendelee kuongea;
‘Makabrasha alikuwa na maadui wengi, na wengi wao, walifikia
hata kumlaani,na inapofikia hatua wanadamu wenzako wanakulaani, wanatamani hata
ufe, ujue wewe huna thamani tena katika hii dunia, hata kama ni tajiri, lakini
ndani ya mioyo ya watu, wewe ni mfu, ...’akatulia kama anasubiria jambo,
akamwangalia mwenyekiti.
Mwenyekiti alikuwa katulia kama anawaza jambo, lakini
baadaye akachukua simu yake na kumpigia mtu akawa anasikiliza na kuwafanya watu
watulie wakisubiria hata shahidi huyo alionekana mwingi wa wasiwasi , hadi
mwenyekiti alipomaliza kuongea na simu, halafu akaonyeshea kidole guma,
kuashiria mambo yapo shwari..
‘Endelea shahidi uwanja ni wako, nimeshafikisha ujumbe wako.....’akasema
mwenyekiti na shahidi bado akiwa na wasiwasi akasema;.
‘Katika maisha yetu haya, watu wana matatizo yao, wengine
hawajui wataishi vipi, wanahangaika usiku na mchana, ili wapate angalau riziki zao...lakini
maisha ni magumu, usiombe..., watu hawa hawana utulivu wa moyo, wana amani ya
kiwiliwili tu, lakini hawana amani ya moyoni,...ndivyo maisha ya walio wengi
yalivyo, watu kama hawa wanatafuta upenyo litokee jambo watoe hasira
zao...’akasema na kugeuka kumwangalia mume wa familia.
‘Watu wana matatizo yao makazini mwao, wananyonywa,
wanachokifanya hakiliangani kabisa na kile wanachokipata, nguvu kazi yao
inatumika vibaya, ...hakuna anayewajali, wanahangaika, kupata, agalau huduma
muhimu, angalau mahitajio muhimu, lakini kipato chao hakikidhi hata hizo huduma
muhimu.
Wanachokipata ni kama vile wenzetu wanavyosema tonge mdomoni, hata
mdomoni kwenyewe ni kama onja –onja, unategemea huyu mtu atakuwa na amani
kweli...huyu akipata nafasi ya kufanya unyama ataufanya unyama kweli
Watu wana matatizo sana huko kijijini , usione watu wapo
kimiya, mtu analima mvua hakuna, pembejeo hakuna, anatumia jembe la mkono, mtu
huyu kila siku anakatwa kodi, kila anachonunua, ni kodi, akigeuka huku kodi,
mtoto wake wanadaiwa ada, yeye anaumwa magonjwa yasiyohesabika, akienda
hospitalini, hakuna dawa...akanunue, akanunue, na kodi yake imeenda wapi, mtu
kama huyu utasema ana amani , ni kweli ana amani ya kiwiliwili, atavumilia,
lakini moyoni hana amani..na akipata kisingizio cha kufanya ubaya ataufanya
kweli kweli..
Siku tulipoongea na mwenzangu tuliyajadili haya, na
Makabrasha alituambia hayo niliyoyaongea mwanzoni, akasema alipoiona system,...ilivyo, jinsi watu
wanavyokula, wanavyohujumu, wanavyowatesa wenzao, akaona hakuna jingine na yeye
ni lazima atafute njia ya kutumbukiza
mrija wake, ..na yeye aweza kufanya awezavyo, ili naye apate maisha mazuri.
Hizo ndio ndoto zake, kuwa katika hii dunia, ni kila mtu na
hamsini zake, kama una uwezo wa kufanya hivi, na ukapata, basi fanya, kama kuna
sehemu unaweza kuitumia kama ngazi ili na wewe ulipate tunda fanya hivyo, na
yeye akasema atatumia kisomo chake, akili yake, kuhakikisha, anapata kutoka kwa
matajiri, kwani anasema matajiri wengi hawajapata hicho walichokipata kwa njia
za halali, kwa hiyo hata yeye akiwaibia ni halali yake....hizo ndio sera zake.
Alipotuona tumebahatika kuolewa na kuoa kwa watu wenye
uwezo, akasema kama hatutaungana naye, basi na sisi ni wamoja wa watu
wanaohujumu raia, kwahiyo tutakuwa maadui zake...hizo ndio sera zake, na
alichofanya yeye, ni kutumia elimu yake, katika nyanja yake, akachanganya na
ujanja wake wa vitabuni, akabuni njia zinazojulikana kama blackmail.Sijui tafsiri yake ni nini kwa Kiswahili, ....’akasema na
kumwangalia mwenyekiti.
Wakati tupo kijijini tunahangaika na maisha, Makabrasha
alikuwa akifika, anatuweka chini, anatueelzea mambo mengi, aliyoyagundua, na
yanayotendeka, mambo ya kidunia, na utajiri wao, kwakweli hata mimi nilivutika
sana, nikatamani niolewe na mtu mwenye uwezo, ndio maana tuliona na sisi
tutatafute sehemu ya kuuona ubinadamu wetu, na sisi angalau tujue kula wali kwa
uma, angalau na sisi tuweze kuiona dunia, ni kweli mimi nikaolewa na mume
ambaye ana uwezo wake, na mwenzangu akamuoa, binti wa watu, tukajisahau.
Ndipo akatokea huyu jamaa, na ndoto zake, na sera zake,
kwake yeye hilo lilimuuma sana, kwani alishapanga mipango yake, mingi....hutaamini
kutoka na mbinu za huyu mtu, kutokana na kazi yake hiyo aliweza kupata pesa
nyingi tu, na akaanza kujenga nyumba, na sio nyumba, ni gorofa, hadi anaingia
kwenye noa zetu, yeye alishakuwa na mipango ya kumalizia gorofa lake lilitoka
ardhini, kwenda mbinguni.
Watu kama hawa wapo wengi, wanaishi kiujanja ujanja,
wanakuja kwako, wanakupima udhaifu wako, wanakuona una njaa kali, wanaanza
kupenyeza sera zao, na nyie bila kujua, kwa vile mumesahaumia, mumeshteseka,
....mna visasi ndani ya moyo, mnakubali, mnaingia kichwa kichwa, na kufuata
yale anayowaelezea, hamjui mwenzenu kajiapanga vipi, ....
Nimebahatika nikapata ndoa yangu, sawa, ilikuwa ni ndoa
yenye ajenda ya siri, lakini ni ndoa yangu, sawa, ilikuwa nampenda mtu
mwingine, lakini ni ndoa yangu, ambayo huenda asingelikuja huyu mtu ningeliweza
kujifunza nikayasahau ya kale,tukaendelea kuishi hivyo hivyo, kwa kudanganyana,
wengi wanaishi hivyo mpaka umauti unawakuta, ni mke na mume kimwli, lakini kindani mioyo
yao inatamani kwingine...huwezi amini, mume wangu alikuwa kila siku
akinifundisha jinsi gani ya kuishi kwa raha, kama mume na mke, nilikuwa
nikimuitikia kwa kichwa, lakini moyoni nilikuwa na jereha, ..
Haya na mengine mengii yalijenga chuki kwenye moyo wangu,
nakutamani kufanya lolote, kwa yule ambaye namuona ni kikwazo kwangu, lakini
sikufikia hatua ya kutaka kuua, naogopa sana kumwaga damu ya mtu asiye na
hatia, na ikizingatia kuwa mimi nimejifunza uaskari, na moja ya nidhamu ya
uaskari, ni kuua adui, aliyeanishwa kisheria kuwa kweli huyu ni adui yako na anastahili kufanyiwa
hivyo, ....
Nafahamu wengi watanishangaa, nikisema nimejifunza uaskari,
naomba mlielewe hivyo, na mlichukulie hivyo hivyo, ndio maana nikatoa ombii kwenu,
kuwa haya niakayoyaongea hapa, yaishie hapa hapa,, tukitoka hapa, kila mtu na
hamsini zake, hayo mengine waachieni wahusika, wanajua ni nini wanachokifanya,
lakini kama mtu atajitia kidomo domo, ....sawa nitakamatwa, kama mshukiwa, wa
mauaji, lakini je ni kweli nilifanya hivyo...?’ akageuka kuwaangalia watu.
Nafahamu mpaka hapo nimewachanganya, ...mtaelewa tu...’akawa
kama anatabasamu.
‘Sasa naomba nianze maelezo yangu kwa jinsi ilivyokuwa
....akageuka kumwangalia mume wangu ambaye naye alikuwa akimwangalia kwa
hamasa, kama vile haamini kitu gani kinachotokea; kama vile hamuamini huyo
mwanamke kuwa ni yule yule aliyekuwa akimfahamu siku nyingi.
Mume wa familia alikuwa ameshapona muda mrefu tu, lakini kutokana na alivyopanga Makabrasha ,
akatakiwa kuendelea kuigiza kuumwa hadi hapo mipango ya mtu huyo ikamilike,
aliambiwa hilo ni kwa manufaa yake mwenyewe ili asije akaonekana kuwa yupo
kwenye mipango fulani, ili mke wake aendelaa kumpa nafasi , kwani kwa hayo
aliyoyafanya kikatiba yao ya kifamilia, ndoa haipo tena,..sasa asingelweza
kuondoka hivi hivi...ile ndoto yetu ya kijijini isingelikamilika..
Mimi nikawa nimepewa kazi ndani ya ofisi ya Makabrasha,
nikiwa kama muhudumu wake maalumu, lakini nia na lengo lake niwe karibu naye,
nisije nikaharibu mipanglio yake, kwahiyo nikawa napangiwa kazi hata za usiku,
na mume wangu kwa vile alikuwa hajui kinachoendelea yeye alifahamu kuwa nipo
kazini. Aniniruhusu , ananiamini ....
Nilimuandikia na hata kuongea na rafiki wa mke wa familia
kuwa mimi sifanyi kazi naye tena, ikiwa ni moja ya mikakati ya Makabrasha ili
aweze kuniajiri yeye, na hata rafiki wa mke wa familia alipofika, mimi nilikuwa
ndani ya jengo, jengo ambalo analimiliki Makabrasha, na humo kuna mambo mengi
ambayo hayajulikani.
Hadi hapo Makabrasha alikuwa hajanifahamu vyema, zaidi ya
binti wa kimasikini, wa kule kijijini..na alikuwa akifahamu kidogo kuwa nilikuwa natumiwa na rafiki wa mke wa familia,...
Mipango ikiwa inakamilishwa, mikataba imeshabadilishwa, na
mikataba mipya imetayarishwa, na kuwekwa inapostahili, sasa Makabrasha akaanza
kutoa makucha yake, akatayarisha mikataba mipya ambayo itampa yeye nafasi ya
kumiliki makampuni, na mali nyingi, ambazo kwa muda mrefu alikuwa akizimezea
mate, lakini alifanya hivyo kwa mgongo wa mume wa familia. Na mume wa familia,
alikuwa hana nguvu tena, kwani alishawekwa kwenye mikono ya Makabrasha. Akili
yake ya kuwaza mbali ilikuwa imefika kikomo.
‘Nitafanya nini kwa sasa, huyu jamaa ana siri zangu nyingi,
ana mambo yangu mengi, ambayo akimuonyesha mke wangu au wakwe zangu,
nitafukuzwa kama mwizi, kwahiyo inabidi nimkubalie kila kitu...’akaniambia na
mimi nikawa sina njia ya kumsaidia, nikamwambia, kwa usalama wake, akubali tu,
hadi hapo nitakapogundua njia ya kulimaliza hilo.
Mimi nilishaamua kuwa nilimalize hilo, kwani kama
nisipofanya jambo, hali hiyo itaendelea kututesa katika maisha yetu yote,
tutakuwa watumwa wa mtu mmoja, na hata kama tutaendelea kuishi kwenye ndoa
zetu, itakuwa ni ndoa jina tu,..kwa mfano mimi nilitakiwa kumtii huyu mtu kama
mtumwa wake, kila anachokitaka nimfanyie, hata kuzalilika, sasa kulikuwa na
manufaa gani hapo, nikaona nijitolee muhanga, nifanye kazi yangu...sote sisi ni
maaskari kwenye jamii, inapofikia mahali kama hapo, unastahili kuonyesha
uaskari wako...tumia mbinu za medani...shauri lenu..’akasema na kutabasamu.
‘Usijali, mshirika, mimi nitajitolea kwa ajili yako....kama
utanikumbuka sawa, nafanya haya kwa vile nakupenda, japokuwa penzi kwako kwangu
silioni..nimeshakuona kuwa wewe unanitumia ili upate unachokitaka, huna tofauto
na Makabrasha...’nikamwambia.
‘Kwanini unasema hivyo, mimi mbona nakupenda sana, umeshahu tulivyoahidiana kule
kijijini...kwa hali iniliyo nayo, nashindwa kutimiza ahadi zetu, kwani nimewekwa
sehemu ambayo siwezi kukuonyesha kuwa nakupenda, lakini moyoni tupo
pamoja,....huoni sasa naumwa, ugonjwa wa kuigiza, nikipona tu na yeye
akifanikiwa anvyotaka, nitatafuta njia ya kumkomoa, tutarudisha mali yetu yote...’akaniambia
‘Umeshachelewa wewe hupati kitu tena, ...kama huyu jamaa
ataendelea kuwepo duniani, ujue wewe utakuwa mtumwa wake wa kudumu, na hutakuwa
na ndoa yenye furaha tena, ..na sizani kama ndoa yako ipo hai tena, kama
itakuwepo ni kwa huruma tu...’nikamwambia.
‘Sasa tufanye nini?’ akaniuliza
‘Sasa hivi unaniuliza eeh, sasa tufanye nini, kamuulize Makabrasha,ninachoweza kusema niliyo nayo niachie mwenyewe, wewe endelea na Makabrasha wako...’nikamwambia.
‘Hivi wewe unajiamini nini , wewe unafahamu vyema huyu mtu, ...nakuonya kama una jambo dhidi yake, unajitakia matatizo,achana naye huyo mtu....’akasema.
‘Mimi ni askari, ninafahamu ni kitu gani ninachokifanya,
ninachohitajia kwasasa ni silaha tu,...sina silaha,na sitaki kuazima silaha kwa aliyekuwa bosi wangu, nimeshaacha kazi ...’nikamwambia, na yeye abakia kimya akiniangalia kwa macho yaliyojaa mshangao, maana
alikuwa hanifahamu kuwa mwenzake katika kuhangaika na maisha, nilishapitia kozi
za kijeshi,...’akatabasamu.
‘Wewe mwanamke, usije ukajidanganya, ukaangalia sinema ukaigiza, ukafikiri hayo mambo ni rahisi hivyo kwanza nikuulize lini umejifunza kutumia silaha?’ akaniuliza.
‘Mimi nafaham kutumia silaha kama unvyofahamu wewe kutumia kijiko wakati wa kula,...’nikasema kwa mbwembwe
, na yeye akaniangalia kwa macho ya mshangao, nikamwambia;
‘Nipe hiyo silaha uone nitakavyoitumia, hilo kwangu ni dogo
sana, na cha muhimu kwa sasa ni mimi kuipta hiyo silaha, sio jinsi gani ya
kuitumia au kutaka kujua nilijifunza wapi kutumia silaha, mjini hapa, ...cha
muhimu kwa sasa ni muda, tunakimbizana na muda...’nikamwambia.
‘Mhh, haya,... ndio maana kila mara upo na rafiki ya mke
wangu, najua ni yeye kakufundisha, lakini
uwe makini na silaha, mimi sipendi sana kushika shika silaha,...’akasema.
‘Nahitaji sana silaha kipindi kama hiki, lakini sitaki mtu
afahamu kuwa nina silaha,..hasa rafiki wa mke wako, au aliyekuwa bosi wangu, sitaki ajue nina mipango gani ....Nahitaji sana silaha, na tatizo ni muda, ningeenda kuazima kwa watu wangu ninaowafahamu, japokuwa
sipendi iwe hivyo, lakini muda....sina muda kabisa nikitoka hapa kama unavyoona
nina watu wananilinda..wapo hapo nje wananisubiria.’nikamwambia.
‘Kama ni silaha, na ...mimi ninaweza kukupatia silaha,
lakini silaha ya nini, unataka kumuua nani, usiniambia umefikia hatua ya kutaka
kumuua Makabrasha?’ akaniuliza kwa mashaka.
‘Sitaki kumuua mtu yoyote, na sina mpango huo, ila ikibidi...’nikasema
nikiwaza jinsi gani ya kumfamisha mtu kama huyo.
‘Lakini siwezi kufaya kosa kama hilo,la kuua, hapana, kama
ningelitaka kufanya hivyo ningelishafanya mapema sana, ...ila silaha itanisaidia
sana mimi kwa kujihami, muda wake ukifika, nikiwa na silaha, ninakuwa kama nina
wasaidizi watano nyuma yangu, ..’nikamwambia na nikweli nikiwa an silaha,
hunibabaishi.
‘Kuna jambo nataak kulifanya usiku wa leo, na asubuhi yake,
ni muhimu sana niwe na wasaidizi wangu, na wasaidizi wangu ni silaha..kama
nitakuwa sina silaha, sitawezi kufany a kitu, jamaa kajizatiti sana, ana
walinzi, ana mitandao ya ulinzi, kwahiyo hata nikiwa na silaha, itakuwa ni kwa
muda maalumu tu....’nikamwambia.
‘Naona wewe unajitakia matatizo makubwa kwa Makabrasha, na
je huyo mtoto wake, ambaye ni mkorofi utawezaje kumdhibiti vipi maana yule ni kichaa, eti kasomea sheria, mbona haviendani! ...Mimi kwa ushauri wangu,achana nao, mimi
nimeamua tuwape kila wanachokitaka, ili tu ...wasije wakanichafulia jina alngu,
nikafukuzwa, hata hivyo, ...mbona mambo yapo safi, mikataba ile inanipa mamlaka
ya kufanya kila jambo, kama mume wa familia....’akaniambia.
‘Halafu mwisho wake itakuwaje,..hujaliangalia hilo kwa mapana yake, hapo ulipo kwa lolote utakalolifanya kwa sasa, bado upo kwenye matatizo, hasa ya ndoa yako. Ile mikataba mnayojidanganya nayo si chochote silolote,...'akasema.
'Hivi wewe unamfahamu Makabrasha ...?' akaniuliza.
'Namfaahmu sana, ila wewe huifahamu familia uliyo nayo, familia ya mke wako, sio ya kuchezea, kwanini
hamniulizi mimi ambaye nimeifanyia kazi za siri familia hiyo, kwanini mnakuwa wakaidi,
wewe unamfuata Makabrasha, yeye ni jambazi, mwisho wa siku anakuruka, wewe
utaenda jela, yeye kwa vile ni wakili anafahamu jinsi gani ya
kujitetea,....’nikamwambia.
‘Sasa wewe ulitaka mimi nifanye nini kwa hatua kama hii?’
akaniuliza
‘Ni kweli kwa akili zako fupi hukuwa na jinsi nyingine, maana wewe ni kidume,...ni kweli hata hivyo umeshachelewa, kama ungelinisikia toka mwanzo, yote haya
yaasingelifika hapa, tamaa zako za kimwili, na akili fupi ya kufikiri ndio imekufikisha hapo,...sijui
kama kweli haya yataisha kwa amani, na hata yakiisha kwa amani, sijui kama ndoa yako
itakuwepo tena, na baya zaidi unaweza ukaishia jela, wakikuhurumia sana, watakutupa kijijini ukawe
omba omba...’nikamwambia.
‘Thubutu, hilo halitatokea, na likitokea, nitafanya jambo
ambalo halitasahaulika katika familia yao...’akasema
‘Utafanya nini....?’ nikamuuliza
‘Wewe niambie silaha unahitaji ya nini..?’ akaniuliza.
‘Kuna mtoto wake, yeye ndiye namuogoap sana, anataka
kunifanya mimi kama anavyonifanya baba yake, siwezi kuzalilika kiasi hicho,
silaha itanifanya nimdhibiti...’nikamwambia bila kumfafanulia mambo mengine
ambayo niliyapanga kichwani mwangu,sikuwa namuamini sana kwenye mambo hayo ya
kivita..
‘Kama kweli unahitaji silaha, na kama kweli itaweza kusaidia
jambo, mimi nitafanya kila mbinu hadi niipate hiyo silaha,..hiloniachie mimi ,
nitachukua silaha ya mke wangu,nitamtumia mdogo wangu, maana siwezi kutoka hapa
kwa sasa..ila tukubaliane, kuwa silaha hiyo itakuwa inaletwa kwako usiku kama
ukiwa na kazi za usiku, asubhi tunairudisha...au unasemaje?’ akaniuliza.
‘Kama unaweza kuipata hiyo silaha, itasaidia sana, nahitaji kuwa nayo sanasana usiku
wa leo, na asubuhi utakapokwenda kukutana na Makabrasha, baada ya hapo inaweza
isiwe na kazi tena, ...’nikamwambia nay eye akaniangalia kwa mshangao,
hakuamini kuwa mimi ninaweza kutumia silaha.
‘Sikiliza kwa makini, kesho ukifika kuonana na Makabrasha,
ujaribu sana kumchelewesha ili nipate muda wa kusimamisha mitandao yake ya
ulinzi, na ...kwa vile mtoto wake, atakuwa hayupo, ...kama alivyodai, japokuwa
simuamini, ...nitaweza kufanya mengine bila kujulikana, yote inategemeana na
muda, muda ni kitu muhimu kwenye mapambano kama hayo...’nikamwambia.
‘Kwani unataka kufanya nini kitakachosaidia, maana mengi
yameshafanyika, mikataba karibu yote nimeshaisaini kukubali, umebakia huo mmoja
tu,.....na wewe mwenyewe umeshasaini mkataba wako, kilichobakia ni mume wake,
ambaye hatakuwa na kauli ya kubisha,...hivi mume wako umeshaongea naye...?’
akaniuliza.
‘Siwezi kufanya ujinga kama huo, unafikiri mimi ni mjinga
kama wewe...kanisainisha huo mkataba, nimekubali kufanya hivyo, lakini siwezi
kuongea na mume wangu, nafahamu kabisa mume wangu hawezi kukubali, san a sana,
ni kunitafutia njia ya kupewa talaka haraka..ndio maana nahitaji hiyo silaha...’nikamwambia.
‘Kumbe...ni kwa ajili yako, ..kwahiyo mimi haitanisaidia
sana, kwasababu nimeshakubali kila kitu...’akasema kwa shingo upande. Na wakati
huo ujumbe ukaingia kwenye simu kuwa muda wa kuongea na huyo mtu umekwisha
ninasubiriwa nje tuondoke, nililetwa na mlinzi wa Makabrasha, ambaye baadaye
huhakikisha kuwa nimerudi ofisini kwake, au nyumbani kwangu, nilikuwa
nikifuatiliwa kila hatua, ili nisije nikafanya kinyume na makubaliano.
Ujumbe huo ulipoingie kwenye simu yangu niliuosoma, pamoja
na mengine, niliambiwa nisisahau kuwa usiku wa leo kuna kazi, kwahiyo nimuombe
mume wangu. Nilifahamu hilo, na nilishamuaomba mume wangu, lakini moyoni
nilijua usiku huyo utakuwa usiku maalumu, huenda wa mapambano au wa kumaliza
kazi niliyokwisha kuianza, cha muhimu niipate hiyo silaha, ...
‘Je hiyo silaha inaweza kupatikana kwa usiku wa leo, ...?’nikamuuliza nikiwa na
mashaka ya kupatikana hiyo silaha. Na mume wa familia aliniangalia kwa makini,
na wakati ananiangalia mimi akilini nilikuwa nikijiuliza, hata kama ikipatikana hiyo
silaha, ni jinsi gani ya kuiingiza kwenye lile jengo maana jumba lile lina
mitambo ya kunasa matukio na hiyo mitambo ikihisi kuwa mtu ana silaha, kuna
ving’ora vya vya hatari vinalia, na kuna askari wa Makabrasha wasio na akili
nzuri, wakitokea hapo, ni kupiga hata kuua.
‘Hilo niachie mimi, ...silaha itapatikana, na natumai
hutaifanyia jambo la kijinga...’akasema na mimi nikaingiwa na wazo na kusema;
‘Usiku wa leo kuna tafrija kwenye lile jengo, itakuwa ni
nafasi nzuri ya mimi kuweza kuipenyeza hiyo silaha bila kujulikana,..unaonaje?,
kama kweli itapatikana usiku wa leo muda wa saa tano hivi, itakuwa vyema, je
mke wako hawezi kuhisi kuwa silaha haipo?’ nikamuuliza.
‘Mara nyingi haitumii, ipo kwenye kabati lake siku zote,
sijawahi kumuona akiichukua, hata kama kuna tukio la hatari, huwa haichukui,
ipo tu..sizani kama atakuwa na wasiwasi nayo...’akaniambia.
‘Basi wewe jitahidi, mtume mdogo wako,akaichukue ...mimi
nitawasiliana na yeye, nione jinsi gani nitakavyoichukua hiyo silaha, lakini
asifike sehemu ya mapokezi, ..asionekane kabisa kwenye hilo jengo,nitamwelekeza
jinsi gani ya kufanya ...’nikamwambia, na tukakubaliana hivyo...na tulikuwa
tukiongea nje kwenye eneo analochukulia mazoezi ya viungo kwasababu ya matatizo
yake ya ajali.
‘Na kweli usiku ule nikaipata hiyo silaha, silaha iliyokuja
kumuua Makabrasha,...swali ni je niilipata pata vipi hiyo silaha, na
ilitumikaje, nitawaelezea yote hayo...’akasema na kutulia kidogo, akamwangalia
mwenyekiti.
Mwenyekiti alikuwa akiangalia saa, na mara shahidi huyu
akaenda pale alipokaa mwenyekiti wakawa wananong’ona, sikujua wanaongea kitu
gani, lakini walipomaliza kuongea, mwenyekiti alichukua simu na kumpigia mtu,
huku akiwa kamuangalia huyo shahidi kama vile anaogopa jambo kutoka kwa huyo
shahidi.. ...
NB: Je silaha hiyo ilifikaje kwa shahidi, na je ilitumikaje
kumuua Makabrasha na je kwanini shahidi huyu anaongea sana na mwenyekiti,
tukutane sehemu ya tatu ya hitimisho la kisa hiki.
WAZO LA LEO: Kila hila mbaya, ina walakini wake, na mwisho
wa hila mbaya, ni kuumbuana tu.
No comments :
Post a Comment