Sauti iliyosikika, iliwafanya wajumbe wageuze vichwa vyao, kungalia
ni nani aliyeongea hayo maneno, kwani wengi wa wajumbe walikuwa wakimwangalia
mume wa familia, ambaye alikuwa akitembea kuelekea mlango wakutokea, akionyesha
kuondoka nje ya kikao, lakini hata yeye aliposikia hiyo sauti, akasimama kama mtu aliyegandishwa, na taratibu
akageuka kichwa, kumwangalia huyo aliyetoa hiyo sauti, na macho yake yakakutana
na huyo aliyetoa sauti, na kuuliza;
‘Na wewe pia, unataka kunisaliti...?’ akauliza mume wangu
wafamilia huku akionyesha uso wa kushangaa na kutahayari, na watu wote
wakageuka na kumwangalia huyo aliyeongea, ambaye alishaulizwa swali na
mwenyekiti, kuwa je yupo tayari kuthibitisha hayo aliyokwisha kuzungumza shahidi
aliyepita, na yeye akatikisa kichwa kuashiria kukubali...
Kutikisa kichwa huko kuashiria kukubali, kulimfanya mume wa
familia kuinamisha kichwa upande, hakuweza kuamini kuwa huyo naye angemsaliti,
kama alivyoita kusaliti, huku akiwa ameangaliana na huyo shahidi mpya, mume wa
familia, akasema;
‘Na wewe pia ....haiwezekani, usidanganyike, na hadaa za hawa
watu, ...’akasema huku akionyesha uso wa kukata tamaa, na huzuni, lakini
shahidi huyu mpya akasema;
‘Hapa sio swala la mimi kukusaliti, tatizo ni kwamba nyani
haoni kundule,na kama ni ubaya , umeuanza wewe, na haijalishi kama nitaongea au
nitakaa kimiya, lakini ni bora niongee ili ukweli ujulikane kwa manufaa ya
wengi....’akasema shahidi huyo mpya.
‘Naongea haya nikiwa nimeshaongea na mume wangu, na hatima
yangu na mume wangu imeshajulikana, hakuna cha ajabu, tatizo ni wewe na mke
wako, lakini kwanini tuendelee kuishi katika maisha haya ya sintofahamu, ya kudanganyana, ...mimi bwana nimeamua, ni heri kusema ukweli, ili haki itendeke, hata kama nitakosa kila
kitu, lakini nitakuwa nimepaat kitu cha kudumu, ..ambacho ni haki na ukweli.
‘Wewe unanifahamu sana mimi nilivyo, jinsi gani
ninavyokupenda, unafahamu sana jinsi nilivyojitolea kwa ajili yako, jinsi gani
nilivyoweza kuvumilia, na kuyafanya yale ambayo sikupenda kuyafanya yote hayo
niliyafanya kwa ajili yako, hebu niambie ni mapenzi gani unayoyataka,kutoka
kwangu, je mimi ni tofauti na hawo wanawake wote uliwahi kutembea nao, ina
maana mimi ni nani kwako, mimi ni njia ya kufanikisha starehe zako, hapana,
nasema sasa basi, kama unanipenda kwa ukweli basi turudi kijijini, tukaanze
maisha mapya, kama hilo litawezekana....’akatulia na wakawa wanaangaliana.
‘Sikiliza wewe, mbona unaharibu, funga hilo bakuli lako...unawafahamu hawa
watu, unavyoongea hivyo unawapa faidia, na haitakusaidia lolote, wao wanachotaka
ni ....uwaambie huo wanaouita ni ukweli, ili mwisho wa siku waweze kukutia
kitanzi shingoni, ukose haki zako zote...sikiliza, hakuna ukweli, ukweli ni
mkataba wangu, ukweli, ni kuwa mimi ni mume wa halali,....usiongee sana...sanasana
utaishia jela, hakuna atakayekumini.....’akasema.
‘Mimi sitaki chochote kutoka kwao, nimerizika na maisha
yangu na umasikini wangu, na hivi sasa siogopi kwenda jela tena , baada ya
kusikia hayo yote uliyoyafanya wewe, ambayo nilikuwa nayasikia tu, sikuwa
nimeyafuatilia kabla,..hata huyobinti wenu wa kazi, ...kwakweli umezidi , na ni
bora niseme ukweli uamue moja, ni yupo aliye halali kwako, mkeo, sasa hakutaki
tena, ni nani atakeyakutaka kwa tabia zako chafu, huyo umeshamkosa, kabakia,
rafiki wa mkeo, naye, sijui,...una mfanyakazi wako wa ndani,...hivi wewe
unanionaje mimi....eeh...
‘ Mimi nilishakuambia toka awali, njia tunayopitia sio
sahihi, ukanikatalia, ukamsikiliza marehemu, ukisema yeye ni msomi anayeona
mbali, je hicho alichofanya ndio kuona mbali, ...?’ akawa kama anauliza lakini
ilionekana kuwa hakutaka kujibiwa akaendelea kusema;
‘Mimi nilitumai kuwa umeshajifunza, kwa hayo yaliyotokea, kama
kweli ulikuwa na nia njema, kama sio kunitumia, nichakae,na baadaye uendelee
kuzaa na wanawake wa kila namna.Kama kweli unanipenda, turudi kwetu kijijini tukajipange upya,
tuachane na maisha yasiyona mpangilio, hebu angalia, alichokuwa akikihangaika
Makabrasha kipo wapi, kapata nini na
sasa yupo wapi,je wewe una uhakika gani na maisha ya kesho na kesho kutwa, kuwa
wewe utakuwa mjanja kuliko huyo aliyemkatiza maisha mtaalamu wako, ...’akatulia akiwa anamwangalia mume wangu.
‘Mimi nimechoka, siwezi tena kuvumilia, siwezi tena
kutumika, yaliyotokea yametokea, na yaliyofanyika yamefanyika, hakuna faida
iliyopatikana, san a sana ni kujiweka kwenye maisha ya utata....mimi
nimeshamwambia mume wangu kuwa aniache, mimi sio stahili yake, ...akubali
sikubali huo ndio ukweli,....’akageuka kumwangalia mume wake, ambaye alikuwa
kainama chini, akiwa kashikilia kichwa.
‘Hivi ni nani anaweza kuyafanya haya yote niliyoyafanya,
wakati mwenzake, anastarehe, na wanawake tofauti-tofauti, anazaa watoto, mimi
mpaka sasa sina mtoto hata mmoja, eti kutimiza ahdi na mipango isiyofikilika,
hivi ni nani, ataweza kuvumilia hayo yote uliyoyafanya, ina maana mimi
nimeumbwa na moyo wa jiwe, niweze kuyavumilia hayo yote, je hivyo ndivyo
tulivyokubaliana...’akamwangalia mume wa familia, ambaye alikuwa naye
amemwangalia kwa macho ya kukata tamaa.
Mume wa familia akageuka kuwaangalia watu, na akiwa kama vile mtu anayeogopa au kutaka kukimbia, aligeuka huku na kule, halafu akamwangalia muongeaji na kwa sauto ya unyonge akasema;
‘Sikiliza nikuambie, mambo yatajiweka sawa, usiogope vitisho
vya hawa watu, usilainike kwa propaganda zao, mbona mambo yapo shwari tu,...nisikilize
kwanza, usianze kuongea ovyo....utaumbuka, watakufunga hawa watu, hawana
ubinadamu hawa.....’akawa anaongea , na sasa akawa akimsogelea huyo shahidi mpya,na watu wote wakawa kimiya
wakiwasikiliza wao, na mume wa familia alipomkaribia huyu shahidi mpya,
akasimama, wakawa wameangaliana, lakini muongeaji, akageuka kumwangalia
mwenyekiti na kusema;
‘Nimesema nipo tayari kuthibitisha hayo aliyoongea
mwenzangu, kwani mimi ndiye niliyekuwepo toka mwanzo hadi mwisho wa mipango
yote hiyo, japokuwa sio kwa kuitunga, lakini kwa kutumiwa.Mimi nafahamu mipango
yote toka kijijini hadi kuja hapa Dar, mimi namfahamu marehemu, kuliko mtu
yoyoye humu ndani, na mimi namfahamu mume wa familia kuliko watu wote humu
ndani, kwahiyo ni wajibu wangu kulimaliza hili moja kwa moja, ...’akasema
Mwenyekiti akatabasamu, na bila kusema neno, akamwangalia muongeaji, akisubiria kusikia ni kitu gani, ataongea huyu shahidi mpya
.
Mume wa familia akanyosha mkono kutaka kumshika huyo
muongeaji, lakini huyo muongeaji, akauona ule mkono na kuusukuma mbali na..na
hapo mume wa familia,akasema kwa sauti ya ukali;
‘Hivi wewe umechanganyikiwa unataka kusema nini,
....’akasema mume wangu akimsogelea huyo muongeaji, na muongeaji akamsukuma pembeni,
na kumwangalia mwenyekiti, kama vile anaomba msaada, na mwenyekiti akasema;
‘Mume wa familia, kaa chini, ....mpe nafasi shahidi wetu
asema ukweli, wewe huna mamlaka ya kumzuia shahidi wetu huyo, ukweli
tumeshaujau kabla,a yeye anauthibitisha tu, hata ukijaribu kumzuia haitasiaidia
kitu, mimi namfahamu yeye kama ninavyokufahamu wewe, kwahiyo sogea pembeni,
muachae mwenzako aongee....’akasema mwenyekiti.
Mume wa familia, akabakia akiwa kaduwaa, hakujua afanye nini
tena, akakaa kwenye kiti kilichokuwa karibu na huyo muongeaji, huku akiwa kainamisha
kichwa chini kama alivyokuwa kainamisha kichwa rafki yake, ..
********
‘Kila jambo lina mwanzo na mwsho wake, mimi nimeona mwisho
wa haya yote ni hapa, na hakuna jingine ila nikuelezea ukweli, na nyie mtaamua
,mtakalolifanya....lakini nawashauri, kuwa muwe makini na mamauzi yenu,
msikimbilie polisi,, kama mtakimbilia polisi, mnaweza msifanikiwe, kwani huko
kote niliwahi kupitia, nikakatishwa tamaa, ndio maana nikaamua kufanya nionavyo
mimi....’akasema.
‘Ili kupata ukweli,na kumlnda yule asiyependeka, nilijitolea maisha yangu, hata kuzalilika,..,
nikaamua kuwa na adui yangu, uso kwa uso, hata kulala naye kitanda kimoja, ili
...eti kumlinda mpenzi wangu, jamani, ....hivi ni binadamu gani angaliweza
kuyafanya haya yote, kwa ajili ya mtu kama huyu...nimakata tamaa, ndio maana
nimeamua niseme ukweli, ili jamii isikie, na watakaojifunza wajifunze, ..
‘Hapa nilipo natafutwa, sio na polisi tu, ..bali na wale
wanaotaka ukweli huu usilijulikane,..na mimi ushaidi wangu nitaugawa sehemu
mbili, ya kwanza, ni historia na chimbuko la haya, na pili, jinsi mauaji ya ya
amrehemu yalivyofanyika....’akasema na hapo mume wa familai akainua kichwa na
kumwangalai mwenzake, kwa macho yaliyojaa chuki.
‘Kwanini niwaaambie nyie, badala ya kwenda polisi,
...kwasababu, jamii ndiyo inahitajia ukweli kwanza, na sheria, itachukua mkondo
wake, baadaye, kama watathibitisha kuwa mimi ni mkosaji, ..jamii ndio yenye
mamlaka,na ukificha ukweli kwao, unaikosea, na bora kusema ukweli kwa wale
uliowakosea, kuliko kuiacha sheria ambayo huenda, ikakutaka ufiche
ukweli....’akatulia.
‘Kuna watu wananitafuta ili waniue,...ili siri isivuje, ili
...mwisho wa siku ukweli usijulikane, na yatakayofuata baadaye, ni mfarakano,
wa familia hii, na watu ambao watakuja na madai mengine
mapya,wameshajipanga,hamyajui hayo...ndio maana kijana aliyetoka, alipoona
hamtaki kumskiliza,a akaona njia bora ni kwenda kutafuta sehemu ya kujificha,
lakini utajificha mpala lini,....’akatulia huku akiwa kamwangalia mwenyekiti,
na mwenyekiti akawa anamwangalia bila kupepesa macho,
‘Ndugu mwenyekiti, mimi ndiye mpenzi wa asili wa mume wa
familia...’aliposema hivyo watu wakahema, na wengine wakaguna.
‘Mume wangu anafahamu hili, na huenda yalitokea hivyo wengi
wakifikiria huenda tulilifanya hilo kwa kulipizana kisasi, kati ya mume wa
familia na rafiki yake, hayo wanayajua wao, lakini kiundani smimi na mwenzangu,
yaani mume wa familia na mimi tulifahamu ni kitu gani tunakifanya, ...’akasema
na kugeuka kumwangalia mume wa familia ambaye alikuwa hataki hata kumwangalia.
‘Nafahamu, kikweli kuwa wazazi wa familia ya mke wa familia,
wanatufahamu sana, lakini sio kiundani kihivyo, ...ndio maana ndoa zetu
hazikubarikiwa,kwa upande wa mume wangu
na kwa upande wa mke wa familia, wote walipinga sana hizi ndoa zetu, sio kosa
lao, wanatuhamu, wanafahamu chimbuko letu,japokuwa kama mambo yangekwenda
vyema, kusingelikuwa na ubaya kwa ndoa hizo....’akasema na kuinama chini kama
anayesoma kitu.
‘Ina maana masikini hatakiwi kumuona tajiri, au tajiri
hatakiwi kuolewa na masikini, hii sio halali, upendo wa kweli hauangaliii
maisha ya kifedha, ...umasikini kisiwe kikwaza ya kuwanyima watu haki zao, za
kupendana, ...nasema haya, kwa wale waliobarikiwa, na huenda hata sisi kama
mambo yangelikuwa sawasawa, kama kusingelikuwa na ajenda za siri, kama
ilivyokuwa kwenye ndoa zetu. Mimi na mume wangu tungelikuwa tunaishi kwa raha
na amani....
‘Mimi na mwenzangu tumezaliwa kwenye familia za kimasikini, familia
duni, iliyogubikwa na mitihani ya kila namna, sitaweza kuisema , ila
ninachoweza kusema hapa ni kuwa mimi
natoka kijiji karibu na kijiji cha mume wa familia, wote mnalifahamu hilo, na
familia zetu ni zile familia zalili sana huko kijijini, na huena ndizo familia
za kutolewa mifano, kuwa ni familia duni, ni nani angakubali kuolewa au kuoa
kwenye familia kama hizo, inayobakia ni ndoto za Alianacha, kuwa siku moja
nitamuoa, au kuolewa na binti mfalme, au
mtoto wa mfalme,...
‘Lakini kwa mipango iliyopangwa, na makubaliano, kati yangu
na mwenza wangu, tukajikuta sote tukiingia
kwenye familia zenye uwezo, japokuwa
kiundani mimi na mwenzangu tunapendana sana, pendo la asili, ambalo tuliwahi
kulifunga kwenye hanaki la umasikini....baaa ya kuvikana pete ya uzalili, na
umasikini, tulikaa na kujadili,
Mjadala ulikuwa wa kulalamika, ...ina maana sisi tutakuja kuishi kama walivyoishi
wazazi wetu, ina maana watoto wetu watakuja kuzalilika, na kuishi maisha ya
umasikini kama tulivyourithi kwa wazazi wetu, tukasema hapana, ..tufanye jambo,
dau yetu ichanganyike na damu ya kitajiri, ili .....oh..’hapo akatulia kwa muda
akiwa kainamisha kichwa chini kama anawaza jambo, na alipoinua kichwa machozi
yalionekana machoni, akasema;.
‘Samhani mimi sio mtu wa kulia lia ovyo,..haya yamenitoka tu
kwa bahati mbaya,...hayatarudia tena...’akasema na kufuta yale machozi,
akaendelea kuongea;
‘Tulijadili sana, jinsi gani ya kuwapata matajiri, je
inawezekana kweli, mimi niolewe na tajiri, utawezaje kumshawishi tajiri kuja
kunioa mimi, au utawezaje kumshawishi binti wa geti kali kuja kuolewa na
mlalahoi kama mwenzangu alivyokuwa...huwezi kulazimisha pendo, au sio, lakini
bahati nzuri ikatokea kama dhamira zetu zilivyokuwa, kila mmoja akapata tarajio
lake kwa nyakati tofauti, huena ilitokea hivyo ili iwe sababu ya watu
kujifunza....
‘Wa kwanza kumpata mwenza ilikuwa ni mimi, nikampata mume
mwenye uwezo, na nikamwambia mwenzangu kuwa nimempata mume mwenye uwezo sasa
tufanya nini, ..mwenzangu akapagawa na kukasirika, wivu ukamjaa, siunawafahamu
wanaume kwa wivu, akasema haiwezekani, akawa kasahau makubaliani yetu, na wakati
tunapingana, tukiwa tumenuniana siku mbili tatu,, mwenzangu akiwa hataki hata
kuongea na mimi akakutana na binti wa kitajiri kwa mazingira yaliyokwisha
kuelezewa..wakajikuta wame...mtamalizia wenyewe..’akacheka kidogo.
Haraka akaja kwangu na kuniambia kuwa hata yeye kampata
mwanamke, tajiri, kwahiyo tupange mipango yetu,....mwenzangu kwa haraka,
akamwelezea mshauri wake. Yeye alikuwa na jamaa mmoja ambaye alimuamini sana,
akawa ndiye mshauri wake, jamaa anayejiita msomi. Na huyo jamaa alipoambiwa
hivyo, akamwambia mwenzangu ampe huyo jamaa muda wa kulifanyia hilo kazi.
‘Mnafahamu hiyi ni bahat kubwa sana, sasa umasikini bai-bai,
kama mtafuata masharti yangu, mtafanikiwa lakini mkiwa wajinga, makajianganay
kuwa ..ooh, nimeolewa, ooh, nimemuoa, tajiri, mtakufa masiki...’hiyo ilikuwa
kauli ya huyo mshauri wetu, nikaona hapo tumefika.
Baada ya siku mbili, huyo mshauri akaja na mikakati ya jinsi
gani ya kufanya....
Ilitakiwa tuolewe lakini kwa lengo moja la ndoa...ili tupate
haki za ndoa, maana kiukweli mimi na mwenzangu tunapendana, hata nikiwa na mume
wangu kitandani namuwaza mwenzangu,nahisi hata yeye ilikuwa hivyo hivyo, kama
nafsi yangu hainidanganyi..kwahiyo ndoa zetu zikawa kama seehmu ya kuchuma,
kuwekeza kwa baadaye....na tukifanikiwa basi tutafute njia ya kujitoa kwenye
hizo ndoa ili tuje kuoana ....’akacheka kidogo hapo.
‘Hivi kweli inakuja akilini..lakini ndivyo mikakati
ilivyopangwa na huyo mshauri, kuna mambo mengi tulikubaliana, kuwa tujizuie
kupata watoto,ili watoto wasije kwua kisingizio, au tukutane kisiri tupate
mimba, na hizo mimba tuwabambikie waliotuoa......ndivyo mikakati ilivyokuwa
hivyo.
‘Jingine kubwa ilikuwa, kutafiti undani wa familia
tulizoolewa, tujua ni jinsi gani walivyopata utajiri, na tuweze kugundua
nyaraka zitakazotuwezesha sisi kutwalia
mali na kuishia, tukizipata hizo nyaraak tumpe mtaalamu, yeye atajua jinsi gani
ya kuzigushi...kinamna, yeye ni mtoto wa majini.
Asikudanganye mtu, ukishaolewa au kuoa, akili yako yote
inakuwa kwenye ndoa yako, ndoa inanoga,a sikuambie mtu, hasa kama umeingia
kwenye sehemu unayopata kila kitu, ndoto, na mipango tuliyopanga ikayeyuka, na
kila tukikutana kila mmoja anakuwa na dharura, hana muda wa kuliongelea hilo,
haat huyo mshauri tukawa tunampiga chenga, na hilo zoezi likafa, na kila mmoja
akawa na malengo na ndoa yake.
Ni kweli moyoni bado kila mmoja alikuwa akimkumbuka
mwenzake, lakini ki hali halisi, ni nani angekubali kuachia hali aliyo nayo,
akarudi kwenye umasikini, hakuna, tulipokutana tena, akiwemo mshauri wetu, tukalibainisha
hilo wazi kuwa ile mipango ya awali isitishwe, kwani haiwezekani. Kila mmoja
karizika na ndoa yake.
Kauli hizo zikamkatisha tamaa mshauri wetu akatuona sisi ni
wasaliti, akatuona sisi hatuna maana, na akaapa kuzisambaratisha ndoa zetu, na
kusema hazitadumu, maana tumeolewa au kuoa, kwa ajili ya mali tu, na sio kwa
ajili ya upendo.
‘Nyie mtaona, sizani kama ndoa zenu zitadumu,...’ikawa kiapo
chake.dhidi yetu
Ndoa ya mwenzangu ilianza kuonyesha nyufa, baada ya kuzaa
watoto wawili, na katika makubaliano yetu ya awali ilitakiwa mtu asizae, kwani
ukizaa watoto watakuwa vikwazo, mwenzangu yeye akazihirisha wazi kuwa yeye
hayupo tena kwenye makubaliano yetu, na hata nilipoongea naye, alionyesha
kutokunijali tena, nikafahamu kuwa penzi letu la asili limeshavunjika, kwahiyo
mimi nijipange kivyangu.
Baada ya mwenzangu kupata watoto wawili, nikaona mambo
yanageuka, na mara mwenzangu akaja kunikumbushia ile mipango yetu, nikashangaa,
na kumuuliza iweje sasa, na wakati yeye ana familia yenye watoto tayari,
akasema, hana raha kwenye ndoa yake, anaishi tu kwa vile ni sehemu yenye
utajiri, lakini ndoa yake anaiona kama jela. Ohoo nikakumbuka ule usemi usemao,
utasema hakifai, au hakitoshi kwa vile unacho, wakati ulipokuwa huna,
ulikitamani.....sasa ndio yakawa kwa mwenzangu.
‘Sasa unataka tufanye nini?’ nikamuuliza
‘Tumtafute Makabrasha atusaidie,..’akasema
‘Hapana, achana kabisa na huyo mtu, huyo mtu sio mtu mwema,
atakuangamiza, na kukuacha ukiumia,...’nikamwambia,na kweli mwanzoni
akanisikiliza, kumbe mwenzangu alishaingia kwenye mambo mengine ya ndani, akawa
hawezi kuvumilia, akaanza kutembea na mfanyakazi wao wa ndani, ..hayo
alinificha kabisa, sikuyafahamu hadi huyo binti alipofika huko kijijini na
mambi yakanifikia, nikamuuliza mwenzangu akanikatalia
Nikakutana na Makabrasha, na yeye akajifanya hajui, lolote,
kumbe mwenzetu alishapata upenvyo wa kuingiza mambo yake, akawa kapata nafasi
ya kupata taarifa zetu za ndani, na aliyewezesha hayo ni binti huyo huyo
aliyebakwa na mume wa familia,na mimi sikuyajua hayo, na nisingeliweza
kujiingiza huko, kama isngelikuwa kazi yangu niliyokuwa nimeajiriwa nayo, na
alijua ili aweze mambo yake, ni vyema
anidhibiti mimi kwanza.
Makabrasha alinifahamu toka siku nyingi, na alijua kuwa mimi
sio mwepesi kuingilika kama alivyokuwa mume wa famila, na alinifahamu kuwa mimi
ni mpinzani wake, kwahiyo akaona aniweke kwenye makucha yake kwanza,
alichofanya ni kufuatlia nyendo zangu, kila ninalolifanya yupo nyuma yangu, na
alinipatia kwenye kazi nilizokuwa nikipewa.
Kuna akzi nyingine ilibidi ujifanya wewe ni changudoa, na
unabidi wakati mwingine ujitolee kufany hata yale ualiyoyafanya, yeye akachukua
kumbukumbu za matukio hayo, kama kinga yake, ujue kazi hiyo nilikuwa naifanya
hata mume wangu hajui, ...yeye alijua nafanya kazi za akwaida ninazozifanya
kila siku, kumbe mwenzake nilikuwa na kazi za ushushu
Ukumbuke kuwa mimi na mpenzi wangu wa zamani pendo letu
lilikuwa lipo pale pale, kwahiyo siku mume wa familia akikazika, anakuja kwako,
namliwaza, hapo Makabrasha akapaat ushahidi wa kutosha, wa kunifanya mimi
nifanye kile anachokitaka, nikawa mtumwa wake
Makabrasha, alipoona pia kuwa hayo alivyoyachukua kwangu
hayampi mwanya wa kuyafanya yale anayoyataka yeye, akaamua kuingia ndani zaidi,
ndio akagundua yale yaliyokuwa yakiendelea ndani ya familia ya mume wangu,
mpaka akafikia kiwango cha kugundua hiyo mikatana ya siri kati ay mume wa familia na mkewe. Alipoligundua hilo, akaanza kutoa vitisho kwa mume wa
familia, kwanza alifanya hivyo akiwa akjificha, lakini baadaye aakjitokeza wazi
kuwa yeye ndoiye yupo nyumba ya hayo yote.
Siku hiyo akatuita kikao mimi na mume wa familia, na kuongea
na yake ya kuyafanya hayo yote, na akasema kwa vile amegundua kuwa ndoa ya mume
wa familia na mkewe haipo kwenye msimamo mwema, hiyo ni kuashiria kuwa siku
yoyote ndoa hiyo inaweza kuwa marehemu, kwahiyo kabla ay hayo yote, inabidi
upanhgwe mpango wa kuyamiliki makapuni yote,..
Mume wa family alipinga sana, lakini alipoonyeshwa madhila
yake, alivyombaka mfanaykazi wa ndani, alipokuwa akitembea na mimi alivyokuwa
kaitembea na rafiki wa mke wa famila, ikaonekana kuwa hataweza kusamehewa kwa
makosa yote hayo, kinachotakiwa ni kwanza ni kuubadili mkataba wa hiari katio
ya wawili hawa,..
Je hilo lingefanyika vipi, ikabidi atafutwe mtu wa ndani,
mtu anayeweza kusaidia, hilo, akafikiriwa rafiki wa mke wa familia, lakini
ikaonekana hataiweza hiyo kazi, kwa vile ana majukumu mengine, yeye alitakiwa
baadaye awe ni kiongozi muhimu kwenye makampuni ambayo Makabrasha atakuja
kuyamiliki, kiongozi wa usalama. Alipofikishiwa hii taarifa, kama
ilivyotegemewa akakataa, na japokuwa alipewa hivyo vitisho, lakini yeye
hakuogopa, ikabuniwa njia nyingine, ...akaitwa, na mtoto akatekwa nyara.
Tukirudi nyuma, ile ajali ya mume wa familia, ilitokea
katika harakati za kubadili mikataba, kutoka ya zamani na kuwekwa mikataba
mipya ya kugushi, na hayo yote yaliwekewa muda maalumu, mume wa familia, kwa
kujisahau akaenda kumtembelea rafiki wa mke wa familia, nia na lengo ni
kumjulisha mipango ambayo yao na kumpa matumaini kuwa mipango hiyo ingemsaidia
huyo rafiki wa mke wa familia.
Alipofika huko akashangaa kumuona mke wa familia ambaye
alijua kuwa yupo kazini, na kwa muda huo akapokea ujumbe wa simu ukamuhimiza
kuwa mkataba wa zamani, mmoja uliopo kwenye nyumba ya familia unahitajika
haraka,ili zoezi likamilike, akakumbuka kuwa aliusahau kwenye sofa wakati
anausoma, kwahiyo akakurupuka mbio .....
Mkataba huo, ulikuwa nakala ambayo mke wa familia alikuwa
akiuutumia, na alikuwa kauandika andika, huo ulitakiwa ili kukamilisha zoezi
zima, kwahiyo akatoka pale mbio, kurudi nyumbani kabla mke wake hajarudi
nyumbani. Kwanini ilikuwa ni kwa haraka hivyo, ni kwasababu mume wa familia
alijua kuwa mke wake atakuwa yupo kazini, kumkuta pale akajua kuwa akitoka hapo
anaelekea nyumbani, na akirudi nyumbani zoezi litakwama, wasiwasi, na vitisho,
vya Makabrasha vikamchanganya, akakanyaga mafuta kupita kiasi na ajali ikatokea.
Makabrasha anaifahamu kazi yake vyema, kwenye kucheka
atacheka, kwenye kazi, vitisho, atakutisha kweli,...alijipanga vyema,kwahiyo
huo ujumbe aliomtumia mume wa familia uliambatana na picha mbaya ya uchafu
waje...akaonywa kuwa, kila kitu kikichelewa nakala moja moja ya ya mchafu yake
itakuwa ikitumwa kwa mke wa familia, na wazazi wa mke wa familia,...
Bahati,ikatokea hiyo ajali....ajali hiyo ingechelewesha
mambo mengi, lakini kwa Makabrasha ikaonekana ni bahati nyingine nzuri,
tunaweza kusema kwake ilikuwa ni bahati nzuri, japokuwa ni ajali, ajali hiyo
ikatumiwa kama kisingizio cha kufanikisha mambo mengi kama malivyoona, na kama
alivyoelezea mwenzangu aliyetangulia.
Kuna mtu ambaye
alitumiwa kama tarishi, wa kuzunguka huku na kule , akipewa maagizo na kupeleka
hiki na kile huyu ni mdogo wa mume wa familia, yeye kwa asilimia kubwa
hakufahamu , na hakutakiwa afahamu ni kitu gani kinachoendelea, kazi yale
ilikuwa kumtii kaka yake,na kaka yake, alikuwa akipewa amri na Makabrasha.
Kuna mtu mwingine
ambaye alikuwa kinara wa hayo yote, akiwa kama msaidizi wa Makabrasha, ambaye
hadi sasa watu hawajamgundua, mtu huyu
ni hatari hata kuliko baba mtu, huyo ni mtoto wake, ambaye ni wakili, huyo ni
mtoto wa nyoka. Yeye aliweza kupenya kwenye sehemu mbali mbali na kupata
taarifa nyeti.
Watu hawajiulizi ni kwanini alikuja kuwekwa wa tatu kwenye
mirathi, wakati hata ndani ya familia alikuwa ahjulikani sana.
Mipango ilipokamilika na mikataba halali iliyokuwemo kabla
ikaibiwa, na kuwekwa mikataba iliyogushiwa, na kilichobakia ulikuwa mkataba
mpya ambao ulionyesha dhamira ya Makabrasha, na huo ulileta sintofahamu, lakini
kwa vile Makabrasha alishajiandaa kwa hilo, akatoa vitisho vyake, na mume wa
familia akasalimu amri.
Kilichoweza kusaidia ni nakala hiyo ya kwenye mtandao, kama
angelifikira hilo mapema, angaliuondoa, kwani Makabrasha ahshindwi kitu, kwani
wahusika wote walishawekwa kwenye makucha ya ,Makabrasha, na ilipohakikishwa
kuwa kila kitu kimekwenda sawa, Makabrasha akaanza makeke yake, hakutosheka, na
kile alichopata, akataka sasa kumuliki kampuni kwa kiwango kikuwa cha hisa,..
Yeye akatayarisha mkataba wa makubaliano kati yake na
wamiliki wa makapuni na yakimuweka yeye kuwa kama mumiliki wa hisa nyingi
kwenye kampuni ya mume wa familia,kama alivyozoanisha kwenye huo mkataba, - kwa
makubaliano , na haikuishia hapo, ukatayarishwa mkataba mwingine ambao mali
yangu ikiwemo hospitali ya mume wangu yeye awe na hisa na nayo yalishafikia
hatua ya mwisho, na kama kikao kile cha kusaini huo mkataba kingelipita basi
ungelisikia makali yake, lakini hakikufanikiwa kwani ndio siku Makabrasha
aliuwawa...’akasema na kutulia, mwenyekiti alipoona mungumzaji katulia
akamuuliza.
‘Kwahiyo kutokana na malezo yako,wewe uliamua kumuua
Makabrasha ili kutokuwezesha huo mkataba usainiwe,ndivyo unavyotaka kusema
hivyo ’ akauliza mwenyekiti akionyesha kushangaa na kutokuamini.
‘Kifo cha Makabrasha ni tukio ambalo halikutarajiwa,...nitalielezea
kwenye sehemu hii ya pili, lakini kwanza nawaomba kitu kimoja...’akasita
kidogo, na kuchukau leso kufuta jasho, na baadaye akasema;
‘Kitu gani unachotuomba, ..?’ akauliza mwenyekiti
‘Ni hivi...’akaanza kuelezea shahidi huyu,
NB: Je itakuwaje, tuanze kuingia kwenye hitimiskho
WAZO LA LEO:Kila
mtu ana ndoto zake, na ndoto nyingine ni za kufikirika tu, hatuwezi kupanga
kununua gari , kujenga nyumba, au kufanya jambo kubwa wakati uwezo huo hatuna.
Tunaweza kuweka malengo hayo, kwa mipangilio ya kimaisha, lakini hatuwezi kulazimisha yale yaliyo juu ya uweze
wetu, tupange kutokana na uwezo na kipato chetu. Zaidi ya hapo tutaingiwa na
tamaa mbaya, ambayo mwisho wake hauna heri kwetu.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Kwakweli dunia ina mambo,najifunza mengi kutokana na kisa hiki,NAKUSHUKURU SANA
Post a Comment