Kesi ya hukumu iliahirishwa eti kwa vile wahusika wengi
wakuu walitakiwa kuwemo kwenye kesi hii nyingine ambayo ilitakiwa kusikilizwa
kwenye mahakama hii ya juu,. Sisi hatukujali hilo kwani tulijua matokea yake
yatakuwaje, na wenzetu waliposikia kuwa kesi hiyo imeahirishwa wakashangilia na
kudai kuwa hakimu anaogopa kaona haki haijatenda itakiwavyo.
‘Nyie mlitaka haki gani, kwani ushahidi uliotolewa
mahakamani hamjauafiki, je ina maana mwanamke akishaolewa hana haki, yaana hata
haki yake aliyochuma mwenyewe haitambulikani?’ wakaulizwa.
‘Mwanamke akishaolewa bwanaaa, hana haki tena,haki zote
zinakuwa mikononi mwa mume wake….’akasema mwanamume mmoja.
‘Nikuulize wapi inasema hivyo?’ akaulizwa.
‘Mila na desturi zetu zinasema hivyo, maana mke alikuwa
mikononi mwa wazazi wake, sasa yupo mikononi mwa mwanaume, yule mwanamume anakuwa
ni mzazi wake na ana mamlaka na huyo mke na kila kitu chake…’akasema huyo
mwanaume.
‘Hebu tukuulize wewe , unafahamu ni nini maana ya ndoa, …?’
akaulizwa.
‘Ndoa ni muingiliano wa mke na mume kisheria,…kwa utaratibu
maalumu baada ya kukubaliana, na kupendana?’ akasema.
‘Hutujasikia maneno yanayothibistisha kauli yako ya mwanzo, kuwa ndoa ni kuchukuliwa mke na haki zake zote
ziwe mikononi mwa mume…tulitaka kusikia hayo maneno kwenye tafsiri yako ya
maana ya ndoa, mabona hakuna kitu kama hicho…..?’akasema mwanamke mmoja kama
anauliza.
‘Huwezi ukafafanua kila kitu kwenye tafsiri ya ndoa, mengine
nayakuta huko huko, yapo kwenyeyanakutakana na mila na desturi….mwanamke
akishaolewa anaiingia kwenye mila za mume, kama kulikuwa na sheria kuwa mke
akabidhi mali yake kwa mume, inabidi afanye hivyo, huoni mume anatoa mahari….’akasema
huyo mwanamke.
‘Kwani mahari ina maana gani?’ akaulizwa.
‘Mahari mmmh, hapo hapo?’….akawa naye kama anauliza halafu
akasema;
‘Mahari ndiyo kisithibitisho kuwa mume anamchukua mke, na
kummiliki, …umeshamlipia mharai, wewe hujiulizi kwanini anayelipa mahari ni
mwanaume na sio mwanamke..’akatulia kidogo, akawa kama anatafakari jambo.
‘Mimi nijuavyo, ….mahari ni zawadi ya mume kwa mke, mengine,
ni hizo mila na desturi ambazo ukichunguza sana ndani yake ni taratibu za mfumo
dume, ambao lengo lake lilikuwa kumfanya mwanamke kama kitu, kinachonunuliwa,
thamani yake ni hayo mahari…lakini dini, zikaja na kuliondoa hilo,…hata hivyo
bado wanajamii wengi, wanapofikia sehemu ya matakwa yao, wanashikilia upande wa
mila zaidi kuliko dini inavyosema…’akasema mwanadini mmoja.
‘Hebu tusaidie wewe mtaalamu wa dini , ni kweli kuwa mke
akiolewa, hana haki ya mali yake,…kama kachuma yeye mwenyewe, inakuwa ni mali
ya mume wake, au ukoo wa mume wake?’ akaulizwa.
‘Mke na mume wanapoona wanakuwa kitu kimoja, na wanapochuma
mali zao zinakuwa ni zao , yaani za familia yao, lakini hata hivyo, mume na mke
wanaweza kila mmoja akawa na shughuli zake, kila mmoja anazalisha, na kukawa na
makubaliano kuwa huyu anamiliki hiki na huyu kile, ndio maana akifa mmojawapo,
kuna kurithi zile mali, mke akifa mume anarithii mali ya mkewe , …kuonyesha
kuwa mke naye anaweza akawa anamiliki mali…’akasema huyo mtaalamu.
‘Ina maana mke ana haki ya kumiliki mali, kama kaichuma
yeye, ndio swali letu hapo? Akaulizwa tena hilo swali kuonyesha kuwa jibu lake
halikuwatosheleza watu, na yeye akachukua kitabu chake alichokuwa nacho na
kuanza kusoma maneno haya;
’Ilivyo
ni kuwa mwanamke ana haki ya kumiliki mali na kujipatia fedha, na mume hana
haki ya kutenga mikono kwa kile alichojichumia mwanamke. Na wakati huo huo ni
wajibu wa mume kubeba gharama zote za matunzo ya familia. Mume anapaswa
kumtunza mkewe, watoto wake pamoja na wafanyakazi wa ndani na kununua vyombo
vya ndani n.k..’’
‘Lakini wewe mtaalamu, sisi tujuavyo ni
kuwa mke anapoolewa na mume, anakuwa kama kakabidhiwa kwa mzazi
mwingine,..kwahiyo hana haki tena ya kudai, kumiliki..’akasema yule mwanamume
kutetea maneno yake;
`Unajua watu wanasahau….’akasema huku
akitulia kuonyesha anasoma kitu kwenye kitabu chake halafu akasema;
‘Hebu niwaelezee hapa, kwenye wajibu wa
mzazi kwa mtoto, mzazi anatakiwa kumtunza mtoto wake na kumpa huduma zote,….hata
kama yule mtoto anakazi, anazalisha, lakini kama bado yupo kwenye umri wa
kuitwa mtoto, bado mzazi anawajibu naye, wa kumpa huduma na haki za mtoto….kama huyo mtoto anahitajia,na
hawezi kusema kuwa kwa vile mtoto ni wangu, basi hata kile anachokichuma ni
mali ya mzazi…au sio’akasema huyo mtalaamu.
‘Kwahiyo jibu tulolihitajia hapa ni
kuwa, mke ana haki ya kuchuma, kumiliki mali,…hata kama yupo kwenye miliki ya
mume, na mali yake haiwezi kulazimishwa iwe sehemu ya mali ya mume…na mume bado
anastahili kumtunza huyo mkewe, na kumgharimia…na hastahili kudai mchango kwa
mke, labda mke mwenyewe apende….ndivyo hivyo ilivyo kidini’akasema huyo
mtalaamu.
‘Huo ni uonevu..kwanini mke apendelewe
kiasi hicho, ina maana mimi nimuoe, nitoe
mahari, nije nimgharamie, bado na mali anayochuma nisiwe na haki nayo….haiwezekani
mtaalamu, wewe umepata wapi hayo maneno, isije ikawa ndio nyie mnazua?’
akauliza huyo mwanaume.
‘Nikuulize na wewe hayoo ya kwako
unayodai kuwa mume ana haki ya kila kitu kwa mke umeyapata wapi…mimi nazungumza
kama mtaalamu wa dini, na sijasimamia dini gani, lakini kwa ujumla wake ndio
huo….dini zimekuja kumkomboa mwanamke, kuwakomboa watumwa, kuwakomboa wanadamu
kwa ujumla, maana mwanadamu kwa ujumla ana ubinafsi,…’ akatulia akiangalia watu
waliokuwa wakimsikiliza.
‘Ukimuachia afanye apendavyo mwenye nguvu
atakuwa ndiye mwenye haki ya kila kitu na mnyonge atakuwa wa kudhulumiwa tu…na
hili linakwenda hadi kwa wanawake…wanawake, wamekuwa wakidhulumia sana toka
enzi za mambu zetu…, kuonewa na kuonekana kama kitu…wengine wakitoa sababu za
mahari kama kisingizio...eti kwa vile mwanaume anatoa mahari, basi mke hana
haki tena…sio kweli..’akasema huyo mtaalamu
‘Kuhusu mahari, ilivyo ni kuwa mahari hailipwi kwa mwanamke kama
vile unavyonunua kitu, au ili mwanamke aje kwa mume kama vile kuuza mwili wake.
Mahari ni haki ya mke kimaumbile, na sio haki ya wazazi kama wengine
wafanyavyo, …hii ni hali ya mume kumuonyesha mke kuwa anampenda na wamekubaliana,
…na mahari inaweza ikawa kwa kiasi chochote au kitu chochote,atakachotamke mke…’akasema
huyo mtaalamu.
‘Sasa wewe mtaalamu, kwa kesi kama hii,
inavyoonyesha ni kuwa mwanamke alipata pesa, akiwa ndani ya ndoa, na akajenga
nyumba na duka,..wakati huo mumewe yupo jela, na mumewe alipotoka, akahisi kuwa
nyumba ile na duka, ni kutokana na pesa zake alichokuwa akihisi kuwa huenda
mkewe alikuja kumuiibia….uone utata wake, na marehemu hayupo, angejitetea
mwenyewe, kwahiyo mke anaweza akabuni mbinu za hadaa….’akawa anauliza huyo
mwanaume kwa maelezo.
‘Hilo kwanza tuwaachie mahakama wenyewe,
sisi kama wataalamu wa dini tuna utaratibu wetu, kama kesi hiyo ingelifika
kwetu, basi tungelihukumu kwa mujibu wa taratibu zetu za dini, ..na hizi
zinajulikana, kama nilivyosema awali kuwa mke ana haki ya kumiliki, kuzalisha,
na mali hiyo aliyoichuma, hailazimishwi kuwa mali ya mume wake,….labda wao
wenyewe wakubaliane, sio kwa kulazimishana, na mke mwenyewe akubali, kwa utashi
wake…kwahiyo kutokana na kesi hiyo, sitaki niingilie huko…tusubirini hukumu za
sheria za nchi.’akasema huyo mtaalamu.
‘Ndio maana hakimu kasepa, kaogopa kuwa
ataleta migongano, maana mila zinasema hivi, dini vile, sheria za nchi hivi,
tutashika lipii..’akawa analalamika huyo mwanaume.
‘Mimi sizani kama mila na desturi
zinasema mke asiwe na haki ya kuzalisha au kumiliki…chunguzeni kwa makini hilo,
hizo taratibu zinawekwa na wanafamilia na jamii zao, ili kukidhi matakwa yao,…mila
za mababu zetu zilikuwa na hekima zake, na wazee wetu hawakuwa na nia ya
kumkandamiza mwanamke, kihivyo, bali ni baadhi ya watu waliokuja baadaye na
kuchomeka mambo yao kwa manufaa yao…’akasema mzee mmoja.
‘Ina maana ni kweli kuwa mke
anaruhusiwa kumiliki mali akiwa ndani ya ndoa, na mali hiyo isiwe kwenye
mamlaka ya mume kwa taratibu za kimila?’ akaulizwa.
‘Unajua kuna kitu kidogo mnakisahau
hapo, ndoa ni makubalianao ya mke na mume…hawa watu wakiishi kama ndoa
inavyotakiwa, wakapendana, wakawa wanashauriana, wanakubaliana, mbona hilo jibu
lake lipo wazi, tatizo mke na mume wanaishi kama wabia…yaani mke kaja kwa mume,
lakini bado ana ubinfasi wake, na mume halikadhalika ana ubnafsi wake, ile hali
ya ndoa kuwa ni kuwaunganisha mke na mume haipo..ndoa haijatendewa haki yake…’akasema
huyo mzee.
‘Mzee unaongea sana..sisi swali letu ni
hilo kuwa mke kimila akiwa ndani ya ndoa anastahili kumiliki mali aliyoichuma
wakiwa pamoja na mkewe….?’ Akauliza huyo mwanaume tena.
‘Tatizo lenu vijana, mnataka sana
kumeza,…lakini huwezi kumeza, bila kutafuna, na huwezei kutafuta bila kukipata
hicho kitu na kukiweka mdomoni,…hapo ndipo kwenye tatizo, ili uelewe jambo,
usikimbilie kumeza tu, ….nina maana kuwa msipende sana kukimbilia hitimisho la
jambo, jaribuni sana kuangalia mzizi, chanzo, sababu…ili hata ukila kile kitu
ujue kitakuwa na mafanikio gani kwenye mwili wako…isije ikawa ni sumu..’akasema
huyo mzee.
‘Haya tunakusikiliza mzee, maana hawa
wazee bwana, wana maneno ya ndani, hawajui kuwa sisi vijana akili zetu zina
pupa, tunachotaka ni kujua,…sio kwanini, kwasababu gani, kiini chake ni nini,
tunapoteza muda, tuna haraka na maisha…’akasema huyo kijana.
‘Kijana wewe umeoa?’ akaulizwa.
‘Nimeoa, juzi tu…’akasema.
‘Je kabla ya kuoa, ulijuaje taratibu za
ndoa, jinsi gani mtaishi na mkeo, na kwanini unatakiwa kuoa?’ akauliza huyo
mzee.
‘Kwani hiyo inahitajia shule, hilo lipo
kiasili, ukifikia muda wa kuoa, unatakiwa uoe, mambo mengina yanakuja yenyewe…’akasema.
‘Hilo ndilo tatizo, …na chanzo cha yote
haya ni hilo tatizo. Wewe kijana ni dereva, ulijuaje kuendesha gari lako,
ulijuaje taratibu za barabarani,?’ akuliza mzee.
‘Nilijifunza, kwanza nilienda kusoma
VETA, na..na..’akasita kidogo, halafu akasema;
‘Kwanini unauliza hivyo, kwani hilo
unalouliza linahusianaje na maswala ya ndoa?’ akauliza huyo mwanaume.
‘Huo ni mfano, kuwa kila jambo lina
elimu yake, huwezi kufanya jambo fulani bila kujua undani wake, ..usomee kwanza
kitu fulani ili uwe mtaalamu wake. Huwezi kuwa mwanandoa mpaka uoe, na huwezi
kuoa bila kujua kwanini unaoa, ..ndoa ni makubaliano ya hiari kati ya mke na
mume,…hayo makubaliano lazima yajulikane, …’akasema huyo mzee, watu sasa wakawa
wanakuja kusmsikiliza huyo mzee, na kuwa kundi kubwa.
‘Sio tu mumekutana , mkapendana basi
hiyo iwe ndio elimu…kupendana ni muhimu, lakini sio kigezo cha kuingia kwenye
ndoa moja kwa moja, …lazima kwanza kila mmoja kwa wakati wake ajitahidi kusomea
undoa, muijue ndoa ni nini, ina nini ndani yake kutegemeana na imani zenu, je
ikiwa hivi na vile tutafanyaje, mimi nina uhakika kuwa mkifanya hivyo,
hamtakuwa na matatizi kwenye ndoa zenu….’akasema huyo mzee.
‘Sasa mzee mimi nina kosa gani, maana
hakuna shule ya ndoa..ipo wapi hiyo shule?’ akauliza.
‘Shule sio lazima iwepo, kuwa kuna
jengo,..sio lazima, walimu wenu hawo mnaowajua nyie walimu wa mambo hayo
wanaweza kuwa ni mashangazi na wajomba, mabibi na mababu, hata wazazi wenu,…na
zaidi ya hayo wapo wakufunzi wakubwa ambao nii viongozi wenu wa dini…’akasema
‘Labda tutawalaumu sana viongozi wa
dini, ambao, mtu akija kwao kutaka kufunga ndoa, hawachukui muda kuwadadisi
hawa watu uelewa wao wa ndoa…inahitajika wafanye hivyo, kuwe ni muda wa
kuelimishana, kuhakikisha kuwa wamepima afya zao…huenda haya yanafanyika kwenye
majumba ya ibada, lakini sio wote wanaoingia huko….’akasema huyo mzee.
‘Wazee kama nyie tunawahitajia sana…..sasa
tutafanyaje mzee, maana kama unavyoona, watu wamegombana na sasa wamefikishana hadi
mahakamani…na mengi yametokea kwa ajili ya hilo…?’
akaulizwa.
‘Jamii , inatakiwa ijue hilo, kuwa ndoa
, maisha ya mume na mke, ndio…..chanzo za jamii, kama tutaiweka sawa hii jamii
kuanzia hapo…hatutakuwa na tatizo, ..wengi wanafikiria kusoma ni kilele cha
kila kitu , lakini tukumbuke katika kusoma kila mtu anasomea jambo lake, ambalo
kabisa halihusiani na maisha yao ya ndoa…sasa hii ndoa itajulikanaje….ni lazima
jamii yenyewe ielewe hili, hili sio jukumu la serikali…ni jukumu la mzazi, ni
jukumu la jamii….’akasema mzee.
‘Mimi ninachowashangaa, inapofikia
kipindi cha maandalizi ya harusi, kikubwa mnachoangalia ni shughuli
itafanyikaje..magahrama kibao, kwanini hili la kumuelimisha huyu mwanandoa
msiliweke kwenye ratiba zenu,….kuwa huyo, mke au mume, naye aambiwe kuwa
anahitajika kuhudhuria kisomo, kipindi kile wapo kwenye michakato ya maandalizi
ya hiyo ndoa…kuna hicho mnachokiita kitchen
party, hivi huko mnajifunza nini….wengi mnaifanya hiyo kama sehemu ya
miradi, kupeana zawadi,…’ akasema hivyo na akina mama wakacheka.
‘Ukweli ulivyo , huenda aliyekuwa
kabuni hilo alikuwa na maana nzuri tu, lakini sasa wajanja wamechukulia hilo
kama ni sehemu ya burudani, kuwezeshana, anayejua kupamba haya, apate chake,
kupika haya apate chake,…hamna kusudio hasa la kuelewa nini maana ya ndoa...kwasabbu
kitu hicho huwezi kukielimisha kwa siku moja…hebu anzisheni hili kwenye jamii…..na
hili lingepewa wakina mama, ambao mnajua kuongea sana, japokuwa kwenye ndoa
zenu hamfanyi hivyo…..’watu wakacheka.
‘Lakini pia ni muhimu sana, mambo haya
wakahusishwa wataalmu wa dini, ni muhimu
sana, maana wanndoa wanjengwa kuishii kiimani zao, na wataogopa kuetendeana
mabaya, kwani wakati wote mungu anawaona…mimi nina imani tukifanya hivyo jamii
itaondoakana na maattizo mengi.
‘Kuna watu wanasema nyie kila saa
mnazungumizia ndoa, ndoa,badala ya
maendelea, kiukweli maendelea bila amani ya moyoni, maendelea bila upendo,
hayaji….maendeleo huanzia nyumbani, jamii iliyojipanga vyema kimaadili, ndiyo
inayoweza kuleta maendeleo, maana kutakuwepo na amani, huruma, uaminifu…uhodari
wa kuchapa kazi hakuna kutegeana, na vitu kama hivyo, na hivyo huanzia kwenye
mke na mume, kwenye ndoa…..’akasema huyo mzee
`Keeesiiiii….’ Kelele za kuashiria kuwa
muda wa kusikiliza kesi umefika, na hapo watu wakakimbilia ndani na huku wakimshukuru
huyo mzee kwa hekima zake.
********
‘Msijali,..’akasema
wakili mwanadada tukiwa kwenye mahakama ya juu, kusubria kusoma kwa kesi ya mauaji yaliyokuwa yakitokea mara kwa mara
hapo kijijini. Na mshitakiwa mkuu, akiwa ni shemeji yangu mkubwa, na
wakaingizwa washitakiwa hawo, lakini shemeji mkubwa hakuonekana, tukafikiria
huenda anaumwa….
‘Kesi ya hukumu
imeahirishwa , kwa vile hakimu kahamishiwa, na mwenzake aliyetakiwa kuja
kushika nafasi yake ana dharura, na ukumbuke pia, anahitajika kuipitia kabla
hajakubaliana na maamuzi ya mwenzake,….’akasema wakili mwanadada.
‘Hata hivyo ni heri kwetu, maana wahusika wakuu ni wale
wale, …tunahitajika pia kwenye kesi hii hapa, hili litatusaidia sana, maana
kufanikiwa kwa kesi hii kunasaidia sana,…kwanza kwa uelewi wa watu kuhusu
kadhia nzima hii ya kudai haki za mke hazitambuliwi pale mke anapochuma akiwa
ndani ya ndoa…lakini pili, ni hili la wanaume wengine kuchukua sheria mikononi
mwao, na kuwafanya wanawake ni kama kitu tu…ukikasirika unapiga…’akatulia.
‘Na tatu ambalo ni baya sana, ni hizi imani za kishirikiana,
….hili sasa linakuwa ni tatizo,..kwanini watu wanafikia hatua hiyo,..kweli
linaingia akilini, mzazi wako, eti amloge mwanao,amloge mjukuu wake, au
shangazi yake….kwanini tunakosa huruma kwa wazee wetu hawa…..’akasema wakili
mwanadada.
‘Hili ni tatizo, na tusipolifungia njuga,sheria ikasimama
kidete, na kutoa hukumu kali kwa watu kama hawa, basi, laana zitatuandama, ….huwezi
ukaishi bila wazee, na bila wao, sisi tusingelikuwepo, tunahitajika, kuwatunza,
kuwahehimu, na kujaribu kuwahudumia, ,…maana hali zao zinazidi kuwa duni kila
siku, na mabadiliko ya kimaumbile hayakwepeki, mengine yanatokana na hali duni….’akasema.
‘Mfano, wengine wanasema eti dalili za mchawi zipo kwenye
macho yake, eti kwa vile wanatembea usiku…na vitu kama hivyo, unasahau kuwa
huyo mama, anaishi kwenye nyumba duni, anapika kwa kuni, nyumba hiyo haipitishi
hewa, ….macho yanaathirika na moshi…unafikiri macho, yake yatakuwaje, unafikiri
ngozi yake ya mwili itakuwaje kwa hali kama hiyo, kaz I ngumu za suluba, hana
muda wa kujipaka hata mafuta…’akajionyesha kama vila anajipka mafuta.
‘Huyu mtu kwa hali yake hiyo kutokana na suluba hiyo,
unakuja kumuita mchawi,…hili kweli ni tatizo kubwa, na linasabishwa na adui
ujinga…’akasema mwanadada.
‘Sasa ni kazi ya sheria, ni kazi ya jamii, ni kazi ya kila
mmoja, viongozi wa dini nk, kulibadili hili, na kwenye katiba inatakiwa hili
liwekwe wazi jinsi gani ya kuwalea wazee wetu….wazee watafutiwe njia ya
kulelewa, na kuthaminiwa, wenzetu ulaya, wazee wana sehemu zao..lakini sisi bado
tunahitajia kukaa na wazee wetu, …kinachohitajai ni jinsi gani ya kuwahudumia,
hata ikibidi kukatwa kodi kwa ajili ya kuwahudumia wazee,
‘Kweli hili la kukatwa kodi kwa wazee hawa ni muhimu sana,
na inastahili kabisa tufanye hivi maana leo yeye kesho na wewe utazeeka, wazee,
wanaongezeka, na wanaachwa hivi hivi, baada ya kunyinywa kwenye kazi zisisoza
na maslahi, na kuhudumia watoto, ambao baadaye wanakuja kuwaita wazee hawo
wachawi….’akasema wakili mwanadada.
‘Sasa kwenye kesi yetu hii, tunahitajika kutoa ushahidi,
mimi mwenyewe nitakuwa nawasaidia mashahidi, ….ili haki itendeke,….nawakata
mseme ukweli ilivyokuwa, jinsi gani mnavyotendewa huko majumbani, hadi ikafikia
hatua hiyo….’akasema wakili mwanadada.
‘Kama mlivyoona, bado mauji yanaendelea, hatukutarajia hilo
tukio chanzo chake ni ndani ya jamii yetu kwasababu ya mambo ya kurithi, mambo
ya mali ….za kifamilia, na wajanja wamelichukua na kuingiza mambo yao kiujanja na hii nikuthibitisha kuwa kuna kundi, lenye
mipango, na huenda linamizizi mahali, kuna wafadhili, na humu kwenye jamii
kunatumika kama sehemu ya kueneza sumu zao.
‘Mimi matarajio yangu, jinsi kesi inavyokwenda, tutagundua
mengi, ….sitaki kusema mengi, ila ninahisi kuna mhusika mkuu aliyejificha na
hajakamatwa, huyo wanayesema ni muhusika mkuu, huenda ni chambo tu,na nahisi,
huenda hakuwa yeye….ngoja tutaona ndani ya ulingo huu…..’ akasema akionyesha
mbele ya mahakama,
‘Na mimi nitajitahidi kadri ya uweo wangu kumfichua kwa
kutumia silaha ya maswali na majibu…’akasema wakili mwanadada.
Na wakati mwanadada huyu anaendelea kuongea mimi akili yangu
ikawa inakumbuka tukio zima lilotokea, karibuni,…siku ile alipokuja shemeji, na
kunishawishi twende kumuona kaka yake, ambaye kagoma kula, japokuwa
nilijitahidi kukataa, lakini moyo wa huruma ukanijia, na kwa muda baba wa
kufikia alikuwa hayupo, nikaona, sio ubinadamu, basi tukaondoka na shemeji yangu
huyo hadi huko mahabusu alipokuwa kawekwa shemeji mkubwa, na tulipofika tulimkuta
akiwa kwenye hali mbaya sana.
‘Tangu afike hapa leo
siku ya ngapi vile….., hajala kitu, kagoma kabisa kula….’akasema mlinzi wa
hapo, na hapo mdogo mtu akamsogelea kaka yake pale alipokuwa kakaa, …akiwa hana
nguvu kabisa, akamuinua huku akiwa na chakula mkononi, akitaka kumlisha, na
yeye akawa anagoma, na baadaye mdogo mtu akakta tamaa, na kuniangali mimi kuwa
ninaweza kusaidia akasema;
‘Kaka kula kidogo, huyu hapa shemeji yako, kasema yupo
tayari kukusaidia….’akasema na ndugu yake huyo aliposikia akitajwa shemeji yake
akainua uso, na kuniangalia, na mara nikaona machozi yakianza kumtoka,nikashangaa
kulikoni, halafu kwa sauti ya shida akasema
‘Shemji hatimaye
umefika, kuniona nikifa au ….hata hivyo nisamehe sana,….ila nasema, na ninakiri
moyoni, sina kosa, nilifanya hayo niliyoyafanya kwa nia njema kabisa,
nikiangalia pande zote,sijui nilikosea nini, lakini nina imani, ipo siku
mtagundua hayo, na mtanikumbuka, …mimi tena basi….’akatoa hauli hiyo na hakuweza
kusema neno jingine, akafumba macho….na kuelegea kabisa, wakajaribu kumfunua
mdomo wamlishe kwa nguvu, lakini ikashindikana kabisa.
‘Oh, sasa hili tatizo,….’akasema mdogo mtu, huku mimi
nikikumbuka kauli ya huyo shemeji mdogo, akisema kuhusu kaka yake kumwambia
baba yangu wa kufikia;
‘Mzee hio silipingi,…maana kila mmoja
anastahili kufanya hivyo, akiona kadhulumiwa, lakini tunachohitajika kwa sasa
ni kumsaidia huyu ndugu yetu, kupata hiyo dhamana, mimi namfahamu sana kaka
yangu, hataweza kuvumilia kukaa rumande siku mbili, kama atandelea kubakia huko
rumande,….hatutakuja kuelewana naye tena…..tutakuwa tumejenga uhasama wa kudumu’akasema.
Hali ya kaka yake huyo siku hiyo ilizidi kuwa mbaya, ikabidi
akimbizwe hospitalini, na alipofika huko akawekewa mipira ya kuongeza maji, na
lishe….hali yake iliendelea vyema baadaye, na leo alitarajiwa kufika
mahakamani, lakini cha ajabu hakuonekana kwenye kundi la washitakiwa.
Kabla hatupata muda wa kuulizana, na mara akaja shemeji
mdogo, akiwa kavalia tofauti na jinsi
anavyovaa, kavalia kinyumbani zaidi, …huwa mara nyingi anakuwa kwenye suti na
tai shingoni, lakini leo kavaa fulana na cha ajabu macho yalionekana kuvimba, akionyesha kuwa alikuwa akilia. Mimi mwili
ukaanza kunisisimuka, maana mwanaume akilia ujue kuna jambo….
‘Vipi kuna nini tena…?’ nikauliza huku nikisimama kumkabisli
shemeji yangu huyo, yeye akasema kwa sauti ya uchungu;
‘Shemeji kwanini humkunisikiliza, kwanini
hamkutaka kunielewa, niliwaambia kuwa ninamfahamu sana kaka yangu,hakuwa na
kosa,nyie ndio mngeliweza kumuokoa, nikawasisitiza sana ….angalieni sasa
ilivyotokea,…kaka yangu hayupo tena duniani….’akasema
na kuangusha kilioa kama mtoto mdogo…na kesi ikaahirishwa.
NB: Ilikuwaje hapo…..
WAZO LA LEO:
Huenda wakati sasa umefika kabla ya ndoa, wanandoa wahudhurie kisomo cha ndoa,
ili kuziokoa ndoa nyingi zinazolega lega. Wapo wanandoa wanaishi kwa jina la
mume na mke, lakini ukichunguza undani wake, uhalisia wake haupo, na huenda
ndoa hiyo haipo tena. Je hatuoni kuwa chanzo cha kuvunjika kwa amani huanzia
ndani ya jamii, jamii iliyotokana na mke na mume. Hawa wawili wakiishi kwa
amani, upendo, na ushirikiano, ndio wanaoweza kuzaa matunda mema, ya watoto,
ambao watakuja kulelewa kwa maadili
mema. Ni wazo muhimu la leo
Ni mimi:
emu-three
5 comments :
Acha aende na roho mbaya zake naona wanaangalia upande wao tu.
Acha aende na roho mbaya zake naona wanaangalia upande wao tu.
Wamemnyanyasa sn dada wawatu kipindi kafiwa namumewe sasa mungu ndo anawalipia yoote
Ndugu yangu Nancy, hivi kule kwetu, akina mama(wajane) wanafanyiwa hivi?
Hakuna kitu kama hicho wala hizo mila zao zisizo na haki hatufuatiliagi, sisi ni watu wastarabu sana ndio mn inaniuma km nafanyiwa Mimi yaani.
Post a Comment