Kwakweli mshituko uliotokea kwenye hiyo familia ulikuwa
mkubwa sana, ulikuwa ni msiba mkubwa, na ulitokea pasi na matarajio, japokuwa
msiba hauna hodi, Wake za marehemu na watoto walilia hadi kuzimia....…..
Msiba huo ulivuruga msimamo wa familia ukizingatia kuwa ndugu
huyo ndiye aliyekuwa kichwa cha familia, na yeye aliweza kuiunganisha hiyo
familia kuwa kitu kimoja na kuhakikisha kuwa mila na desturi zao zinafuatwa….japokuwa mara nnyingi alitumia ubabe, na wanasema kwa
ubabe wake ndio maana alifanikiwa, kuwaunganisha wote….
Pamoja na ubabe wake,
watu wengi walimpenda sana, kwani wakati wa furaha alikuwa mtu wa furaha, na
wakati wa kazi ilikuwa ni kazi..hakutaka mzaha, na ukiangalia ndivyo
inavyotakiwa katika jamii zetu za sasa, uwe mtu wa kati na kati,…...
‘Hili limetokea, kama familia tunatakiwa tuwe kitu
kimoja….’akasema mzee wao ambaye ndiye baba peke yake aliyekuwa kabakia kwenye
hizo familia, na alitakiwa kushika hatamu kwa muda, hadi hapo watakapomkubali
ndugu mwingine kushika uongozi wa familia.
‘Kinachohitajika kwasasa na muhimu sana, kama desturi za
mila yetu, ni kumzika jamaa yetu haraka iwezekanavyo….’akasema mzee mmoja wao, katika
ukoo lakini hakuwa mwanandugu wa moja kwa moja, na yeye kama mzee wa jamii,
akatoa ushauri wake,na watu wakaitikia kwa kichwa.
‘Mimi siafiki hilo la kuzikwa kwa haraka….’akasema wakili
mwanadada aliyekuwepo hapo kwenye msiba.
‘Kwanini unasema hivyo?’ akauliza huyo mzee na kwanini ukadakia
kusema, wanawake, hawatakiwi kudakia dakia mmbo, kwanza tulia mtapata nafasi ….wewe
kwanza ni nani kwenye hii familia?’ akahoji kuonyesha alikuwa ahmfahamu vyema.
‘Samahani mzee kwa kudakia, mimi ni mwanasheria, na itakuwa sio vyema, mimi nipo hapa, mambo yaende au tudai mambo kinyume na sheria, za nchi na taratibu zake, pia tutakuwa tunaficha ubaya kama umetendeka….kiutaratibu,
kwanza inabidi tutambue ukweli wa kifo cha marehemu....’akasema na yule mzee
akamwangalia yule mwanadada kwa macho makali.
‘Usituletee mambo yenu ya mjini, mtu keshakufa hata akikaa
mwezi, utafufuka, au hata mkimchunguza ndio atazindukana, siku yake ilishafika
na asingeliweza kuishi kama ahadi yake imeshafika…cha muhimu ni kumsitiri ..’akasema
huyo mzee akiwaangalia watu.
‘Hilo sio tatizo mzee wetu, kuzikwa atazikwa, lakini cha
muhimu ni kujirizisha je kweli amekufa au ameuwawa…maana huyu mtu hali yake
ilikuwa njema kabisa,…akiwa pale hospitalini, hakuonyesha dalili za kuumwa,
kilichomfanya akafikia hali ile ni kuwa aligoma kula, na walipomuwekea dripu a
maji, hali yake ikwa njema, na akakubali kula….akawa hana tatizo tena , mara
gahfla, tunasikia kafa, kwanini kitokee kifo cha ghafla hivyo, kwanini
hamjiulizi hilo swali..?’ akauliza mwanadada.
‘Hiyo ni kweli, maana mimi mwenyewe niliongea naye, jana, na
alionekana hana matatizo yoyote na akasema yupo tayari kusimama mahakamani
kujitetea maana anaamini yeye hana hatia, na yupo tayari kuyafichua maovu
yote…’nikasema nikichangia.
‘Na wewe ndio usiongee kabisa, maana marehemu alikuwa akikulaumu sana…na haya
yanayotokea kwasasa tutakulamu wewe…’akasema huyo mzee akininyoshea kidole kwa
hasira.
‘Kunilaumu kwangu ni kawaida, maana tulikuwa tunasigishana
kwenye mambo ya kawaida, na hilo ni la kawaida kwa wanadamu, lakini tukumbuke
kuwa mimi sikuwa nafanya hayo kwa nia mbaya, nilifany ahayo kudai haki yangu ,
na ndio maana tulipofikia mahali hatuelewani, nikaamua kwenda mahakamani. Mbona
mara ya mwishi nilipobahatika kuongea na marehemu, alinipoongeza kwa hilo na
hata kunisfia kuwa nimekuwa jasiri, na nastahili kuwepo kwenye kundi lake la
wanafamilia..’nikasema.
‘Usijitetee kabisa, na wala hufai kukaa kwenye familia hii,
umekuwa gundu, …tena balaa mkubwa, hujioni, mumeo kafa, sasa huyu ndugu yetu
ambaye alijaribu kukuweka sawa naye huyo kafa, hatujui ni nani atafuatia,…angalia
msiba mingi inayotokea hapa, ukichunguza sana, unaambiwa imetokana na wewe na
hawo unaoishi nao……angalia mwenyewe
tangu uingie kwenye familia hii ni matatizo, inakuwa kama wewe ndiye
unaitafuna hii familia,..’akasema huyo mzee ambaye watu walimwangalia tu, maana
wengi wao hawakuwepo hapo kiakili, msiba ulikuwa umewafika kiukweli.
‘Sio kweli…huyu mwanamama namsifia sana, yeye amekuja kuleta
mageuzi makubwa kwenye hii familia, hata marehemu, alisema hivyo, ila yeye
alikiri kuwa pamoja na hayo huwa hakubali kushindwa na mwanamke ndio maana alikuwa
anajitutumua, ..japokuwa moyoni alishafikia sehemu akakubali yaishe,
ila,…nahisi kuna shinikizo lilikuwa nyuma yake….’akasema mmoja wa wake zake.
‘Mimi sikubaliani na hilo kamwe,…ili hali iwe shwari kwenye
hii familia, huyu mwanamke na watu wake waondoke,…yeye amekuwa kipingamizi hapa
kwetu, ….hili kama wanafamilia, inabidi tuliseme na kulikemea, kama alivyokuwa marehemu,
lisema kwenye kikao , tena mara nyingi, yule ambaye hataweza kusimama na sisi sio
mwenzetu…sasa inakuwaje tumkubali wakati marehemu alimkataa…’akasema huyo mzee.
‘Marehemu hakuwa amefikia hatua ya kumkataa…’akasema mkewe
mwingine, lakini hakuweza kuongea zaidi akawa analia.
‘Huu sio muda wa kulumbana, tupo kwenye majonzi, kwanza
tufikirie jinsi gani ya mazishi, mkumbuke huyu mtu ni mkubwa kwenye familia hii,
kwahiyo watu watakuwa ni wengi sana…..kwahiyo gharama yake ni kubwa, siku hizi
mfiwa badala ya kulia kufiwa, analia pia kuwa anahitajika kuwalisha
waombolezaji,…analia na gharama,… sijui dunia hii ya sasa imekuwaje..zamani mtu
akifiwa , kila anayekuja kwenye msiba anakuja na kitu, vyakula, nyama…kuni,
maji….lakini sasa ni kufaa kufaana,…badala ya mfiwa kusaidiwa, anajikuta kwenye
wakati mgumu, wa kufikiria jinsi gani ya kuwalisha watu watakaofika kwenye
msiba…..’akalalamika huyo mzee.
‘Mzee usijali hilo tutajipanga vyema …ndio maisha yetu,
hatuna jinsi, sisi kama wanandugu tutwajibika kukamuana, na kila takayekuja kwenye
msiba, ni lazima atoe mchango, tutaweka vijana kila kona kukusanya michango,
vinginevyo hatutaweza kuwalisha watu….’akasema mchangiaji.
‘Na lini tutamzika marehemu….?’ Akauliza mmoja wapo.
‘Kwa taarifa za polisi, wamesema kuna watu wamelalamika kuwa
marehemu kapewa sumu..hakufa kifo cha kawaida, kwahiyo mpaka uchunguzi
ufanyike….’akasema huyo mzee.
‘Ni nani huyo aliyelalamika, …..kwasababu wanandugu ni sisi,
ni nani tumjue, ambaye kachukua jukumu bila ya sisi kujua,…., anataka mwili wa
ndugu yetu uchezewe, tusikubali kabisa…’aaksema yule mzee wa mwanzo.
‘Hilo halina mjadala mzee, ilimradi limeshafika polisi,
hakuna jinsi,…, ni kazi ya polisi na wameshamzuia, mpaka wamafanyie
uchunguzi….’akasema huyo mzee.
‘Kwanini …kwanini,…mbona kila siku mnaleta mambo mapya,…na
haya ndiyo yanaharibu baraka, kiujumla hilo halipo kwenye mila zetu,….tunaweza
kugundua bila ya kumchana chana marehemu, tukalizuie, ndugu yetu hawezi kwenda
kuchezewa chezewa na visu..’akasema huyo mzee.
‘Nimeshakuambia kuwa hilo halipo kwenye mamlaka yetu,
ukumbuke kuwa huyo walikuwa naye, na wanawajibika kwa hilo, ..wao wameshindwa
kumlinda…kwahiyo wanataka kujirizisha, na kama ikigundulikana kuwa kafa kwa
sumu basi wao watawajibika iweje mtu aliyekuwa kwenye mikono yao, alishwe sumu,
pia sisi kama wanafamilia tutamtafuta huyo mtu kwa njia zote, na
atawajibika….akasema mzazi wa hiyo familia aliyebakia.
‘Oh, sasa hilo ni tatizo….mtazua mengine yasiyo na msingi….haya
fanyeni mtakavyo, …..’akasema huyo mzee na akamgeukiwa mzee mwenzake waliyekuwa
naye, wakawa wanaongea chini kwa chini kwa kunong’ona,.
‘Na kwanini wewe unapinga hayo, hayo ni kwa manufaa yetu,
tujue ni nani alikuwa nyuma na hilo…’akasema ndugu mmoja wa marehemu.
‘Aaah, mimi sipingi kwa nia mbaya, ila naona kama sio halali
ndugu yetu kuchanwa chanwa tena….mnatafuta nini keshakufa basi, …tumuombee huko
aendapo, hakuna cha zaidi tutakachokipata….sasa kama hamnisikilizi mawazo yangu
, naona niondoke, nitakuja baadaye’akasema huyo mzee, akamgeukia mwenzake, na
wote wawili wakaondoka.
Wakili mwanadada akasogea pembeni na kupiga simu polisi, ….
**********
Tukiwa na wakili mwanadada kwenye msiba, tulianza kuongea
maswala mbali mbali, na mara tukajikuta tukimuongelea mdogo wake marehemu,
yaani mchumba wake mwanadada wakili. Mazungumzo haya yalianza tu pale mdogo mtu
ambaye alikuwa hana nguvu kabisa alipofika kutusalimia na kutaka kujua kama
kuna kitu chochote kinahitajika.
Kwa muda mfupi ndugu huyu alikuwa amekonda, , kiujumla msiba
huo ulimchukua kupita kiasi, na kwa mtizamo wa hiyo familia yeye ndiye alitakiwa
kuwa kiongozi wa hiyo familia japokuwa walikuwepo kaka zake wengine, ambao
hawana uwezo wa nafasi hiyo, lakini kwa vile ni wakubwa wanaweza kuleta
kipingamizi, na hiyo itamfanya huyo mwanasheria kuwa na wakati mgumu.
‘Yeye alipendekezwa na marehemu kuwa anastahili kuishika
nafasi hiyo kama yeye akiondoka, na hata kipindi akiwa hai, pale panapotokea
kikao na kama kaka yake hayupo, huyu ndiye aliywkuwa akikaimu nafasi yake.
‘Namuonea huruma sana mchumba wako, ataiweza kweli hii
familia, maana ni kubwa na ina ubishi, na migawanyiko ya chini kwa chini, na
ilivyo, ili uiweze hii familia inahitajia mtu mbabe, na huyu shemeji yako sio
mbabe, anatumia busara tu…na elimu yake tu…?’ nikaanza kuongea na wakili
mwanadada.
‘Sema aliyekuwaa mchumba wangu…’akasema wakili mwanadada akisisitizia hayo maneno `aliyekuwa mchumba wangu, na huku
akimtizama huyo mchumba wake, ambaye alikuwa kakaa kwenye kiti, upande
waliokuwepo wanaume huku kajiinamia.
‘Ina maana mlishafikia hatua ya kuvunja uchumba wenu?’
nikamuuliza.
‘Mhh, we acha tu,…ilibidi iwe hivyo, ili nimpe nafasi ya
kuchagua…?’ akasema wakili mwanadada.
‘Nafsi ya kuchagua?...kuchagua nini tena?’ nikamuuliza na
hapo akageuka na kuniangalia huku akijaribu kutabasamu.
‘Kati yangu mimi au wewe…’akasema huku akikaa vizuri, na
baadaye akageuka kumwangalia huyo mchumba wake. K wa hali ile ilionyesha wazi
anampenda sana mchumba wake, na alitamani aende akakae naye karibu ili aweze
kumliwaza, …, lakini kulikuwa na msimamo fulani ambao alishauweka akilini mwake
na hakutaka aonekane tofauti...
‘Huwezi ukasema hivyo, maana mimi sina ulazima kwake, na
wala sina urafiki naye, wewe ni mchumba wake, na ulitakiwa usimame naye bega
kwa bega, upiganie penzi lenu, na ukisema hivyo, kuwa ulimpa nafasi ya kuchagua
mimi au wewe, unakosea kabisa…kwasababu mimi sijakubaliana naye kwa hilo…’nikasema.
‘Lakini mila na desturi zinamlazimisha afanye hivyo,
marehemu ndugu yake yaani mume wako, walikubaliana hilo, na aliwahi kunielezea
hata kabla mume wako hajafariki, na kipindi hicho nilichukulia kama mzaha tu,
na nilimwambai kimzaha kuwa , nitafurahi sana nikiwa na mwenzangu kama mke
mwenza…’akasema.
‘Ina maana upo tayari kuishi uke wenza?’ nikamuuliza kwa
mshangao.
‘Tulikuwa tukiongea kama mzaha na sikujua kuwa inaweza ikatokea
hivyo, imekuwa kama lisemwalo laja…mimi siogopi uke wenza, ….ila kwana kuwe na
makubaliano ya dhati, na kama inabidi iwe hivyo, lakini kwa hali hii ya sasa,
sioni kwamba kuna ulazima huo, pili kama uonavyo, yeye, hajawahi kuoa….’akatulia
na kugeuka kuniangalia.
‘Ni kweli hata mimi hilo nimeliona….’nikasema kwa sauti ya
unyonge.
‘Sasa atawezaje kuishi na wake, kama mke mmoja hajawahi
kuishi naye, hawaoni kuwa wanamtwika mzigo mzito ambao hajawahi kuwa na uzoefu
nao, ….na kwanini uke wenza?’ akawa kama anauliza.
‘Mimi sijui…’nikasema nikimwangalia huyo mchumba wake, na
wakati huo alikuwa kainua kichwa na kutuangalia, sikujuwa alikuwa akiwaza nini,
na akatoa leso yake kujifuta usoni, ….
‘Kuna sababu za kimsingi, kama zipo mimi sizipingi,…kuwa
mjane alizoea kuishi na mume, na sasa mume wake keshafariki, na hana uwezo wa
kuishi peke yake..tunaweza kusema hilo linaweza kuwepo, kama njia ya kumsaidia
mjane…lakini sio lazima, ….cha muhimu kwanza ni kumpa muda huyo mjane,
ajitambue, ajipime, na akubaliane na hiyo hali….sio kulazimishana…kama atapenda
kurithiwa, basi ni hiayari yake….’akatulia.
‘Kumbe wewe unakubaliana na hizo mila za kurithiana?’
nikamuuliza.
‘Wanasema ukifika kwa wenye chongo, inakubidi ufumbe jicho
lako…kiukweli moyoni, sikubaliani nalo, lakini ukitaka kuondoa ubinafsi, na
kuweka upendo mbele kuwa mwenzako keshafiwa, na hana jinsi, atasaidiwaje
kijamii, maana hakuna mtu atakaye weza kumsaidia mtu baki…wewe ukishafiwa na
mumeo, kama huna wazazi, kama huna ndugu, hata kama wapo, utakuwa ni mzigo sana
kwao,….kwahiyo tufanyeje,…tusaidiane, na atasaidiwa vipi kwa urahisi ….wao
waliona hivyo kuwa arithiwe, sikati hilo, kwasababu huyo mjane akiwa na mtu
akatambulikana kuwa huyu ni mumewe atasaidiwa bila masharti …ukiwaza sana hilo
na kuondoa ubinafs, …inabidi ukubali…..’akasema.
‘Kwahiyo kwa hali kama yangu , mfano ningekubali kurithiwa,
ulikuwa tayari kuishi na mchumba wako…yaani uolewe na mimi niwe mke mwenza wako…kwanza
kipi kitangulie hata sijui?’ nikauliza na kuguna kama nacheka.
‘Hilo lipo wazi, hajaoa, kwahiyo kwanza kazi kubwa ni
ilikuwa ni kwake, kutafuta mke anayemfaa aoe kwanza, ….mimi nilimsomesha hilo,
kuwa hajawahi kuoa, haiwezekani akimbilie kurithi, hana uzoefu wowote na
mke..tunamtendea isivyo haki, …ndio maana nikimwambia tuvunje uchumba wetu
kwanza, ili apate muda wa kutafakari hilo, mimi
au wewe, ….’akatulia.
‘Yeye alisemaje?’ nikamuuliza kutaka kujua zaidi.
‘Mhhh, aseme nini, na yeye huku anataka na kwako anataka….nilimuona
hana maana, hana msimamo, na mimi tabia yangu ni kuwa sipendi kuburuzwa hasa
pale ninapoona kuwa nipo kwenye msimamo sahihi….mimi sijamkatalia mila zao, na
nilijitahidi sana kujifunza mila zao kwa vile nilikuwa nampenda…’akasema na
kumwangalia mchumba wake, na niliposikia hilo neno `kumpenda’ nikajikuta
nikihisi vibaya, sijui kwanini.
‘Kwahiyo kumbe kweli unampenda mchumba wako, na kilichotokea
kinakuuma sana…na kwa namna moja au nyingine, unaniona mimi kama mpinzani?’
nikamuuliza.
‘Nikuambie ukweli..nasema hivi na tunaongea kwa vile sisi ni
marafiki, …kiukweli nampenda sana, lakini mimi msimamo wangu ni kuwa sitapenda
kama hakuna upendo, sitaolewa, kwasababu kuna kuolewa,sitayumbishwa kwa vile
yeye ni mume, na anachotaka yeye ni lazima kiwe hata kama hakina maana, hata
kama sio sahihi kwa vile yeye ni mume,
basi tukubali, tuje tuumie sote…nilishamwambia hivyo,na nilimuona akiwa hana
raha na msimamo wangu huo…kazoea amri za kwao, kuwa mume akisema keshasema, sio
kwangu, kama ni sahihi haina shida, na sitapinga tu ilimradi kupinga, nitapima
yale anayoyataka, na tukae tukubaliena kama mke na mume..’akatulia.
‘Yeye kama wanaume wengine ambao msimamo wao ni kuwa
mwanaume ni kila kitu, watu kama hawo ukiangalia kwa makini, hawajui kabisa, nini
maana ya upendo, nini maana ya uchumba, nini maana ya ndoa…wanachojua wao, ni
tafsiri ya mume kuwa mmiliki wa mke, na kama unamiliki kitu, ina maana hicho
kitu hakina nafasi ya kujietetea…’akatulia kama vie anayapima hayo
aliyoyaongea.
‘Kwangu mimi hilo halipo..na kiukweli wanaume wa namna hiyo, wanakosea, mke ni
binadamu , na anayo nafasi sawa na mume..wakioana, wanatakiwa kuwa kichwa
kimoja…..wakae waongee wajadiliane wakubaliane, lakini sio kulazimishana kusiko
na msingi…kila jambo wewe unatakiwa useme, sawa mume wangu, nikukate sikio sawa
mume wangu…haiwezekani.’akatulia.
‘Ngoja nikuulize wewe na yeye mlianza anzaje, maana
inavyoonekana kwa wengi, wanaona kama hamuendani kivile?’ nikamuuliza na yeye
akacheka, halafu akashika shavu, na kuanza kuelezea, jinsi gani walivyokutana
na huyo mchumba wake..
‘Sikujua kabisa kuwa nitakuja kumpenda mchumba wangu kiasi
hicho….lakini upendo ulitokea tu pale aliponiokoa nikiwa kwenye kundi la midume
miwili iliyotaka unibaka…..’akaanza kuelezea kisa chake na mchumba wake….
NB: Sehemu ijayo, tutagusia kidogo, jinsi mwanadada huyo
alivyotokea kupendana na mchumba wake, je ilikuwa ni bahati mbaya, au kweli
kuna upendo ndani yake, na je hawa wanawake wawili, watakuabalina kuishi uke
wenza, ….
Je na wewe unasemaje. Najua ndugu yangu utasema `chesive, harikaa, ni kini icho…’ lkn zipo mila na desturi,….wanafanya hivyo,
na wanaishi,….je zimefanikiwa,… je wewe unasemaje, …
WAZO LA LEO:Maisha
yana mambo mengi, na hutaweza kuyafahamu yote, cha muhimu, unapokutana na mwenzako,
hasa wale wanaojikuta kuwa na wapenzi, na huenda kukutana huko ni kwa mjini mjini, hatujuani, wewe hujui kabisa mila na desuri zao, na pia huenda mila na desturi zenu zikawa tofauti kabisa.
Ni vyema, ukafanya utafiti, ukamjua mwenzako kabla
hujachukua maamuzi ya kuishi naye kama mke na mume. Watumieni wazazi wenu au watu
wazima kuzijua taratibu, mila na desturi za mwenza wako, japokuwa mke na mume,
ni familia ambayo sio lazima iwe tegemezi na mila za wazazi wao…, nyie ndio
mtapanga jinsi gani ya kuishi lakini hamuwezi mkajitenga kabisa na familia za wazazi wenu, au sio…
Ni mimi:
emu-three
9 comments :
ukewenza mwanzo ni mzuri bt mkizoeana sidhani km mtakuwa na maelewano tena ila na wanaume nao wanachngia wake zao kuishi kwa ubaya kwa kupenda sehemu moja, kwa upande wangu binafsi siupendi ukewenza.
Hongera sana ndugu wa mimi kwa kazi nzuri...Mungu azidi kukubariki kila iitwapo leo..kuna mafunzo meengi sana kupitia kazi/maandiko yako.
Naungana nawe kabisa na Wazo la leo.
Pamoja daima.
Tha we eho he mtwi wngu, asikubali ukewenza kabisa bora akae na msimamo wake huo huo tang lini mapenzi yakagawanyika❓tuthiishane aha.
Tha we eho he mtwi wngu, asikubali ukewenza kabisa bora akae na msimamo wake huo huo tang lini mapenzi yakagawanyika❓tuthiishane aha.
Nyaaa,
shamballa beads wholesale uk
workforce . Most of these beloved a that your particular pleasantly surprised about apparent products are virtually assortment of are really a number of replications . in the with these types of number of rooting just after
WordPress can be a very well-liked CMS with in depth usages to get a array of web-sites and strong online applications. Being an open source CMS, it has gradually been becoming the choice of additional customers and webmasters about the globe. At present, webmasters and users favor WordPress conversion solutions to obtain a well-designed and totally functional web-site. The WordPress theme conversion just isn't a simple activity and calls for massive technical knowledge and sound domain skills. In the absence of those two important things, the conversion will not be a trusted, economical and helpful proposition. It has been offering top-class WordPress conversion solutions to let users meet their varied requirements. With WordPress already capturing markets and generating inroads into others' share, this organization is steadily increasing to deliver the most beneficial of WordPress conversion services to clients. Getting a strong and straightforward CMS implies it becomes rather quick process to handle web-sites and taking the most effective out of it.
The majority of us are familiar with the physical benefits of massage therapy. And, all of us know expertise first hand throughout our every day interactions, the unavoidable stresses of life. The majority of customers that seek out massage therapy typically do so to help alleviate the physical manifestation of their accumulated anxiety. And, it really is definitely properly warranted sought right after, as constant massage therapy aids to lessen your overall degree of physical discomfort, stiffness discomfort. In addition, it assists to raise the array of motion with the key joints inside your physique. Educated, intuitive skilled hands perform out the accumulated knots, tensions muscular adhesions that create more than time.
I'm also treated to views in the comfort of my garden space: a peep over the dividing wall reveals acres in the aforementioned rice fields. I have a private outdoor fish pond with stepping stones for the front door from the villa, and an open-air bathroom containing a bathtub shrouded within a mosquito net.
David Yurman replica jewelry is an excellent way for people with tight budgets to practical experience the luxury and design and style for which David Yurman is recognized. You'll find high-quality replicas in the marketplace which are just as lovely as the originals. Nobody would ever know it was not a genuine David Yurman piece.
il drago non è altro che Envy. Nel frattempo, un'altra associazione sta tramando nell'ombra: la Thule Society, capeggiata da Karl Haushofer. Questa associazione è alla ricerca della chiave di
Related information:
[url=http://crystalbeadsr7t9.unblog.fr ]crystal beads bulk
[/url]
[url=http://cheapshamballabeads.webs.com ]cheap shamballa beads
[/url]
Kaka m3, nakuonea huruma sana kwa juhudi yako hii , japokuwa kwa kweli tunafaidika, tunga vitabu jasho lako lisiende bure. Pia naona ajabu matangazo ya biashara yanawekwa kwenye blog zisizo na tija, na blog kama hizi hawaweki ni kwanini... Mungu atakujali tu ka kazi ya mikono yako
This will create a smooth, professional refinish on the bathtub.
What are the benefits of having a bathtub refinishing. Usually, the bathtub refinishing
kit that you purchased will have several chemicals that you will need to
effectively resurface your bathroom tub.
Also visit my web page: bathroom remodeling
Take your time and effort so that you'll be able to be assured that you have found the most effective automotive tools and equipment on your current needs. Bath tub liners come inside a variety of colors and resist chipping and scratches. If you intend on using a granite countertop installed, first choose the right.
Here is my webpage; bathtub resurfacing
Post a Comment