Simba alikuwa katulia pembeni, akiwa katunisha misuli yake,
na meno makali yalionekana wazi, yakiashiria kuwa yapo tayari kukatakata
vipande vya nyama kwa yoyote itakayoingia kinywani mwake. Kwa mbwembwe, akayataraza makucha yake kwenye
nyasi, na nyasi zikakatika katika vipande, bila kujali kuwa hizo nyasi ndizo
zinazomuwezesha kuishi kwenye hali bora.
Upande wa pili walikuwepo wanyama wengine, ambao wengi wao ndio
chakula cha simba, waliona wakutane wajadiliane jinsi gani watakavyoweza
kupambana na huyo simba, kwani wao wamekuwa kitoweo cha mnyama huyo, ambaye
kila kukicha alikuwa akiwashukia na kuwararua bila huruma.
Mnyama wa kwanza akasema; ‘Jamani hivi kwa umoja wetu
tunashindwaje kumdhibiti huyu simba, akija hapa tunajikusanya kwa pamoja,
tunamkabili huyu adui yetu.?’
‘Tatizo wengi wetu kama unavyotuona ni wanyonge, hatuna
nguvu,…lakini pia hata tukikaa pamoja,
watoto wetu wanachezacheza ovyo, na kama unavyomuona akitukosa sisi
anawakimbilia watoto wetu, ….’akasema mnyama mwingine.
‘Kwahiyo tufanyeje?’ akauliza mmoja wa wanyama.
‘Hatuna jinsi, sisi wanyonge, iliyobakia kwetu ni kula nyasi
kwa wingi, ..tukila nyasi kwa wingi , tutakuwa na miili mikubwa , kama hawo
wanyama wengine wanaogopewa na simba, tunaimani kuwa huyu simba atatuogopa na sisi…’akatoa maoni
mmoja wa wanyama hao na kweli maoni hayo yakaonekana yana maana kwao.
Wanyama wale wakawa wanafuata mawazo hayo ya mnyama mwenzao
ya kula majani kwa wingi, na kweli majani yakawa yanaliwa kwa wingi, na matokeo yake ni kuwa mbuga za majani zikawa
kama vichaka, …., na matokea yake mvua zikawa haba, kwani kama ujuavyo mvua
zinatokana na miti na majani, na miti na
majani yamekuwa yakitafunwa na hawa wanyama kwa fujo, bila kujali hiyo athari.
Simba, akawa anameza mate kwa tamaa, japokuwa hakuweza kuwala
wanyama wakubwa kama ilivyo kawaida yake, kwa vile walikuwa wakimpa shida,
lakini aliweza kuwala watoto wao walionona…kwake yeye, hajali kwani japokuwa
anawakosa wanyama wakubwa, lakini bado vipo vitoto, vilivyonona.
Haya ndio maisha yetu, ….Serikali, ipo ikisubiri kodi za
wafanyabiashara, bila wao shughuli zao haziwezi kwenda, wafanyabiashara hawa na
wawekezaji, kila kukicha wanabuni mbinu mbali mbali ili waweze kujiendesha kwa
faida, na hata kukwepa kodi. Na kila
wakiona wamekwama, sehemu ya kukimbilia na kuwabana walaji kwa kupandisha
nauli, au bei za vitu vyao.
Leo wafanaybisahara wa usafiri, wameona ili kuweza kumudu
gharama za usafiri, ni kupandisha nauli, wanayempandishia nauli ni mwananchi, …sio
serikali , ambayo wengi wanainyoshea kidole. Kwani wao ndio walioweka kodi
kwenye vipuri, wao ndio wanaotakiwa kuweka miundo mbinu ziwe bora, wao ndio
wasimamizi wa shughuli mbali mbali za kuwewezesah kwenye huduma zao.
Lakini badala ya kumkabili huyo serikali,….kwa kulipa kodi
ipasavyo,au kwa kumgomea huyu serikali kuwa wasilipe kodi kwani kado zao hazifanyi yale yanayostahili kwao….wao wanamgeukia mlaji, mtumiaji, kwa kisingizio kuwa, hata
mzalishaji, anapoona gharama zake ni kubwa, atakachofanya ni kupandiha bei
bidhaa zake ili aweze kupata faidi.
Wengine wameshau kabisa wao ni watoa huduma
, na haingelihitjaji sana kuwa na faida kubwa ukijilingaisha na makampuni, kama hawapati fadia, mbona kila kituo wanatoa pesa za bure kwa wapiga debe ambao hata kazi ya kupiga debe hawajaifanya, na hata kuweka wale wanaoitwa `maday-worker' huku madereva halisi wakikimbilia nyumba ndogo,..... Ndio
maana wakapewa mbinu za kujibadili na kuwa makampuni, ili wazipate hizo faida
nono, kama hawo....!
Kwa mtaji huu wao wanataka kunona , ili waweze kuwa
makampuni makubwa, ili serikali iwaogope, kama wanyama wanavyomuogopa simba, bila
kujali kuwa wanyemkomoa sio serikali, ni mwananchi….oh ama kweli, wakipambana
mafahali wawili mwisho wa siku zinazoumia ni nyasi.
Kwanini kila jambo linalowakwaza hawa wafanyabiashara ,
makampuni, madakitari, nk, hasira zao wanazipeleka kwa wananchi? Swali hilo
likaulizwa na wanyonge kwenye daladala.
‘Kwani serikali ni nani?’ akauliza mzee mmoja
‘Serikali ni wewe na mimi, lakini kuna watendaji ambao
wameajiriwa kwa ajili ya kuwezesha hizo shughuli, hawo ndio serikali, na kwa
maneno mengine, serikali ni wale watu walioajiriwa na wananchi kwa ajili ya
kusimamia shughuli zao…’akasema mzee mwingine.
‘Kwahiyo ndio maana makampuni, wafanyabiashara, madakitari,
wakikwama wanagoma, na wanayemgomea ni mwajiri wa hawa wanaoitwa serikali.
Tusilalamike, kosa ni letu sote wananchi, kwa vile tumewaajiri watu wasio na
masilahi na wao.
‘Tatizo jingine ni kuwa, watendaji hawa walioajiriwa kama
serikali ndio hawo hawo wafanyabishara, ndio hawo hawo wenye hisa kwenye
makampuni mbalimbali, ndio hawo hawo wawekezaji kwenye usafiri, nk, je hapo
unategemea nini, ….
Unategemea kuwa huyu mfanyabishara atawatetea wananchi, ili
yeye apate hasara, haiwezeani, Na hapo ndio unakumbuka busara za wazee wetu
walioliona hilo, kuwa mtendaji wa serikali hahitajiki kuwa hisa mbili, huko
serikalini na huyo huyo ni mfanyabiashara, muwekezaji,….
Muda umefika, kwenu nyie, waajiri wa serikali, kuchambua
pumba na mchele, ….na hilo linawezekana, tuhakikishe wale tunaowaajiri kweli
wana maslahi na sie,…kwani ukiangalia mali yake kama kigezo cha kumuajiri, siku
akiwa madarakani, hatakuangalia wewe, yeye ataangalia mali yake kwanza.
‘Chagueni viongozi bora, kwa maslahi yenu…vinginevyo,
tutabakia kulia kila siku…..vinginevyo, tutageuzwa kuwa majani, wa kutafunwa
huku wenzetu wananona, …..wakimuogopa Simba, Simba ambaye sisi tunaweza
kumdhibiti, kwani anaishi kwenye mapori yetu, au sio
Swali ni nani wakumfunga paka kengele?
NB: Kisa chetu kinaendelea bado naweka mambo sawa, lakini nimeona niitoe hii kwenye diary yangu,
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Tumekupata mkuu,lkn wao watakusikia?
I absolutely love your blog.. Great colors & theme. Did you create this website yourself?
Please reply back as I'm wanting to create my very own website and would like to know where you got this from or what the theme is called. Thanks!
Also visit my web page ... landing page
Post a Comment