‘Mwanangu ni bora tu uende ukaishi na mama yako huyu mdogo,
maana maisha ya hapa hutayaweza, kama unavyoona huyu mume wangu ni mlevi
kupindukia, na siku zote amekuwa akiniamurisha nikufukuze hapa nyumbani uende
kwa baba yako, kwani hataweza kulea mtoto wa mtu mwingine, ambaye sio wa kwake,
wakati baba yake yupo, na kama nionavyo watoto wake mwenyewe ni mzigo
kwake’hiyo ilikuwa kauli ya mama yangu siku tunaagana.
Kwangu mimi siku hiyo ilikuwa ya furaha, nikiwa na ndoto
kichwani kuwa naenda Darisalama, mji ambao sifa zake zimeenea kila kona ya
kijiji chetu. Nilijua kuwa ukifika Dar, utapata starehe za kila namna, na
nilijua kuwa kila anayeishi mji huo mashuhuri ni tajiri.
‘Mama nitakwenda na mama mdogo, na nikipata pesa nitakuwa
nakutumia, ili usiteseke tena, najua huko Dar pesa zipo nyingi’nikamwambia huku
nikiwa na furaha tele.Na hata wadogo zangu, watoto wa mama na baba huyo wa
kufikia, wakawa wanalilia na wao waondoke hapo.
‘Mwanangu ninakuasa huko Dar, kuna mitihani yake, sio kweli
kuwa ukifika huko utapata kila kitu, kama ingelikuwa hivyo wote wanaotokea huko
wangelikuwa matajiri, au kila mtu angelikimbilia huko. Cha muhimu mwanangu
ukumbuke maisha haya tuliyo nayo, wewe sasa ni mkubwa, ujua jinsi gani ya
kujichunga, usije ukapatwa na madhara yaliyonikuta mimi. Nakuasamwanangu,
ukaishi vyema na mama yako huyo mdogo, uwe na adabu na umtii, kama mama
yako’akasema mama.
‘Mama sasa kwanini sisi tunaishi hivi, kwani baba yangu yupo
wapi?’ nikamuuliza swali hilo tena, ingawaje nilikuwa nimeapa moyoni kuwa
sitamuuliza swali kama hilo tena, kwani kila nikimuuliza, kilichofuata hapo ni
machozi na siku hiyo mama hatakuwa na raha siku nzima. Sijua kwanini na
hakupenda kabisa kuniambia.
‘Mwanangu nilishakuambia kuwa swali hilo silitaki, kwasababu linanitia
uchungu, linanikumbusha mbali sana, ..na nisingelipenda kukusimulia machungu ya
maisha yangu kwani yatakuumiza tu mwanangu.’akasema mama huku machazi yakianza kumtiririka usoni.
‘Kwanini mama, nikikuuliza hilo swali unalia, kwani kuna
nini kuhusu maisha yako, na baba yangu mzazi, amekufa au yupo hai? Mama mimi
sasa ni binti mkubwa na nina haki ya kujua wapi alipo baba yangu au kwanini
baba alitutelekeza na sisi kuja kuishi na huyu baba asiye na mapenzi kabisa na
mimi, na wewe huna raha kabisa licha ya kuwa unaishi naye?’Nikawa nataka kujua
kulikoni, sikujali tena kama mama atalia au vipi, mama akaangalia huku na kule
kuhakikisha kuwa baba hayupo karibu.
‘Mwanangu, licha ya kuwa baba yako huyu hana mapenzi na
sisi, lakini ndiye aliyeniokoa kipindi ambacho nilikuwa karibu ya kufa. Yeye
alijitolea na kuishi na mimi nikiwa magonjwa karibu ya kufa, kipindi hicho ndio
nimejifungua wewe. Mwanangu, sipendi kabisa kukusimulia maisha yangu, kwani ni
ya uchungu kiasi kwamba hayafai kusimuliwa mtoto kama wewe’akasema mama.
‘Lakini mama mimi sasa sio mtoto, nimeshavunja ungo, na
akili yangu ni ya kiutu uzima, na sasa najiandaa na safari ya kwenda mji mkubwa
duniani, mji wa Darisalama’nikasema huku nikiwa na furaha.
Mama aliniangalia na machoni kukawa kumeshatanda kiwingu cha
machozi, akatulia kwa muda , halafu akasema ;
‘Baba yako nasikia yupo huko Mererani,ni mmoja wa matajiri
wa madini, na anaishi na mke wake, na watoto wao, hanijui tena…‘akasema mama. Na mimi nikaingiwa
na hamu ya kumjua huyo baba yangu, kumbe baba ni tajiri , sasa kwanini sisi
tuteseke na umasikini, nikajiuliza na kumuuliza mama.
‘Mimi sikuwahi kufunga ndoa na baba yako, ..’akatulia mama
kwa muda, huku akiwaza, nahisi alikuwa akivumilia uchungu wa kumbukumbu
zilizopita, na baada ya kufikiri kwa muda, ndio akaanza kunisimulia maisha yake
yaliyopita ambayo ndiyo yaliyosababisha machungu aliyo nayo.
**********
Mwanangu usijisikie vibaya nikisema hivyo, lakini ndivyo
ukweli ulivyo, kuwa kila ninapokuona ninakumbuka machungu yaliyonikuta katika maisha
yangu, hata wakati mwingine nakuona kama wewendiye mkosi wamaisha yangu. Samahani
sana mwanagu kusema hivyo, hata kama ungelikuwa wewe, ukahisi hivyo. Hizo ni
hisia tu mwanangu kutokana na maisha yangu yaliyopita.
Siku mwanangu ulipoingia tumboni kwangu ndipo siku ambayo
kila kitu kinachoitwa raha, amani na upendo vilipotoweka kabisa katika maisiha
yangu. Ilifikia kipindi nina mimba, nikiiangalia hiyo mimba nakulaani, nikisema
sitaki utoke salama, ….unisamehe tu mwanangu ndivyo nilivyokuwa nikiwaza.,
Sikujua haya yote yangelitokea, kwani kipindi hicho nilikuwa
mdogo tu, na siku hiyo ambayo nakumbuka ndiyo siku niliyopata hili doa, ilianzia
siku ile tulipokuwa tukifurahia kumaliza
darasa la saba , ilikuwa siku tuliyokuwa tukisherehekea kumaliza daras ala
saba. Kwangu mimi ilikuwa siku ya pekee sana, kwani ndiyo siku ninaikumbuka sana
kuwa ilikuwa mwisho wa maisha yangu ya ubinadamu.
Siku hiyo, mimi na baba yako, yaani huyo baba aliyenipa
mimba yao, tulikuwa tumetoka kwenye sherehe ya kumaliza darasa la saba, na siku
hiyo tulishajiona tumekuwa na tulikua tukijiita LY, yaani last year. Nilikuwa nimejipamba ipasavyo, na shingoni nimevalisha
shada ya maua, nililovikwa na wazazi wangu.
Shuleni nilikuwa na akili sana, hata zawadi ya mwanafunzi
bora nilipewa mimi, na hata baba yako huyo ambaye tulikuwa darasa moja alikuwa
hanifikii kabisa. Kwahiyo kipindi napewa zawadi yeye alikuwa na wivu wa ndani
kwa ndani, licha ya kunipongeza na kujivunia kuwa ana dada mwenye akili.
Mimi na huyo baba yako tulikuwa marafiki sana, toka utotoni
hadi kufikia darasa la saba, wengi wasiotujua vyema walizania kuwa sisi ni
watoto wa mzazi mmoja, labda sisi ni ndugu, lakini hatukuwa na udugu wowote. Mimi nilikuwa sioni raha,
kama sikumuona baba yako huyo,lazima ili siku ikamilike ni lazima tuonane, kama
sio bombani ni wakati tunakwenda shule.
Baba yako huyo alinipenda kiukweli kwani hakupenda kabisa
nionewe na mtu yoyote, hata kama nimekosa shuleni na mwalimu anataka kuniadhibu,
yeye aliweza kumuomba mwalimu achapwe yeye badili yangu. Na nyumbani kwao
wakila chakula tofauti ambacho labda ni kizuri, atanifichia ahakikishe kaniltea
kidogo, na ikawa hata mimi nafanya hivyo.
Mwanzoni wengi walijua kuwa ni utoto, tukiwa wakubwa hayo
yataisha, lakini haikuwa hivyo,kwani kila umri ulivyozidi kuwa mkubwa ndivyo
mapenzi yetu yalivyozidi. Licha ya kuwa moyoni mwetu, hatukuchukulia kama
mapenzi ya sasa, ya kiukweli, tuliyachukulia kama mapenzi ya dada na kaka.
Mapenzi yasiyotafsiriwa vibaya , na hatukujua zaidi ya kupendana kama kaka na
dada hadi pale tulipofika mwisho wa
darasa la saba.
‘Maua unajua mimi nakupenda kweli, naona tukimaliza darasa
la saba tuoane kabisa, naogopa utakuja kuolewa na mtu mwingine’akaniambi baba yako
huyo.
‘Eti nini tuoane, hivi wewe unajua maana ya kuoana kweli,
unaanza kuleta mambo ya dhambi hapa. Na ujue kuwa kuoana ina maana kubwa
,nijuavyo mimi, mkitaka kuoana mnatakiwa mlipe mahari,muwe na nyumba ya
kuishi,muwe na pesa ya kujitunza wenyewe, sasa sisi bado wadogo,huoni kuwa
unawaza mambo ya kikubwa wakati sisi hatujafikia huko’nikamwambia.
‘Pesa tutatafuta wenyewe, mahari mimi nitatafuta, nitafanya
vibarua hadi nitaipata,, sitapenda kabisa nikukose wewe, ni heri nife kuliko
kukuona unaolewa na mtu mwingine. Au wewe hunipendi?’ akaniuliza Adam, ndilo
jina la baba yako huyo.
‘Mimi nakupenda sana, lakini sikuwa nimewazo huko, nakupenda
kama kaka yangu, hata hivyo ni kweli hata mimi sioni raha nisipokuona, na
nitasikitika sana kama na wewe utamuoa mtu mwingine badala yangu, sijui
nitaishije, lakini tusiwe na haraka ya mambo hayo, tusubiri, kwanza mimi nategemea
kufaulu, na kwenda sekondari’nikasema.
‘Ndio hapo naanza kuogopa,maana mimi sina uhakika wa
kufaulu, natarajia kuwa mfanyabisahara, na ndoto zangu ni kwenda kuchimba
madini Mererani kama alivyo mjomba. Sasa nataka nikiondoka niondoke na
wewe,sitapenda wewe uende sekondari, maana ukifaulu, utakwenda kukutana na
wasomi wenzako na utakuja kunisahau kabisa’akasema.
‘Adam mimi siwezi kabisa kukusahau, nakupenda kama
ninavyoupenda mwili wangu, wewe utaona tu, hata nikifaulu, kama nitakwenda
sekondari ya mbali nitakuwa nikikuandikia barua kila siku. ‘nikamwambia.
‘Hapana kama kweli unanipenda lazima tufunge ndoa, ili hata
ukiondoka nijue wewe ni mke wangu,’akasema.
‘Hilo haliwezekani, sisi bado wadogo,na hata wazazi wetu
wakisikia hayo wataanza kutufikiria vibaya, wao wanajua tunapendana kama kaka
na dada, hayo ni mabaya tusiyaongelee …’nikamwambia.
‘Mimi nina wazo moja,…’akaniambia huku akiona aibu
`Wazo gani?’ nikamuuliza.
‘Ili tudumishe mapenzi yetu, inabidi tuwe wapenzi wa kweli,
na hili litafanikiwa kama ….’
Basi ushawishi ulianzia hapo, ikawa kila tukikutana na baba
yako lazima anishinikize kuwa tufanye mapenzi ya kiutu uzima. Na mimi niliogopa
sana nikijua madhara yake, licha ya kuwa nilikuwa nikimpenda sana baba yako
huyo na sikupenda kabisa nimuuzi.
Siku matokeo ya mitihani yalipotoka, ndipo siku baba yako
huyo aliponishinikiza, na siku hiyo alinichukua hadi kwa jirani mmoja rafiki yake
ambaye alikuwa akionyesha kanda za video, na sijui kuwa walipanga iwe hivyo,
kwani waliweka mikanda mibaya, ambayo baada ya kuiangalia, nilijikuta
nikikubali kufanya alichotaka yeye na hapo nikawa nimeingiza balaa mwilini
mwangu, kwani tendo hilo la siku moja, lilikuwa kama sumu mwilini mwangu,
Siku hiyo sitaisahau maana sikutarajia kuwa matokea yake
yatakuwa hivyo,.nilipiga ukelele wa maumivu, maumivu ambayo, hayakuishia
kuniharibia usichana wangu tu, bali yalikwenda moja kwa moja hadii kuniharibia
maisha yangu.
Ujauzito huo uligunduliwa nikiwa shuleni, kidato cha kwanza,
wakati huo nimeshafika sekondari, na kilikuwa kipindi cha kupimwa wanafunzi
afya zao. Siku hiyo baada ya kupimwa, nilibakai bwenini, nikiwa na wasiwasi,
kwani nilishajihisi vibaya, sikuwa na uhakika wa kuwa nina mimba, lakini ile
hali yangu ya kuumwa umwa,na kujsikia kichefuchefu, na dalili nilizozisikai
kuwa ukiwa hivyo ni dalili za mimba, nikajua tayari.
Mara nikasikia nikiitwa, nikaambiwa naitwa na mwalimu wa
utawala, nikajua sasa mambo ndio hayo. Nikafika kwake, na yeye hakuniambia kuwa
nina tatizo gani, yeye alichosema ni kuwa, marakwa mara wanapofanya uchunguzi
kwa watoto, na kugundua tatizo, huwa inabidi mwalimu akutane na mzazi, kujadili
jinsi gani ya kulitatua hilo tatizo’akasema.
‘Mwalimu kwani mimi nina tatizo gani,maana siishi kuumwa?’
nikamuuliza.
‘Ndio jambo tunalotaka kuongea na wazazi wako, tuone
tutakusaidia vipi, kwahiyo jiandae, tutaondoka pamoja’akaniambia huyu mwalimu. Mimi
moyoni nilijua tu mambo yameshaharibika, na ninavyowajau wazazi wangu, basi
tena, ndio nakwenda kuuwawa.
‘Mwalimi mimi siwezi kwenda nyumbani, baba ataniua mwalimu’nikasema
huku nikianza kupiga piga miguu chini.Mwalimu akaniangalia, nafikiri alitaka
kuniambia nani aliyekutuma kufanya hivyo, lakini akatumia busara ya ualimu, kwa
kunificha, kwani sikuambiwa kwanini narudi nyumbani na mwalimu.
‘Kwani wewe una wasiwasi gani, kwani unahisi kitu kitu gani
kibaya ulichofanya, ?’ akauliza mwalimu na alipoona nipo kimiya akasema;
‘Mimi nataka kwenda kuonana na wazazi wako ili kuwaelezea
hali yako ya kiafya , kama unavyoona akribu kila siku wewe ni mgonjwa, na pia
kuongea nao kuhusu matokea yako ya mitihani, usiwe na wasiwasi hao ni wazazi
wako hawawezi kukua,kwani kila mzazi ana uchungu na mwanae’akasema mwalimu
lakini nilijua anaongea vile kunipa matumaini tu. Kama angelimjua baba yangu
asingelisema hivyo.
Mimi nilipanga kumtoroka tukifika njiani, kwani nilijua
ukali wa baba yangu, …
NB: Je ilikuwaje
WAZO LA LEO:
Jamii njema huanzia kwa watoto, ikiwa na maana kuwa watoto ndio msingi wa
familia , watoto ndio msingi jamii,watoto ndio msingi wa taifa. Tukilijua hili,
ni vyema tukahakikisha kuwa msingi huu ni imara. Je tufanyeje ili msingi huu
uwe imara, ndilo swali analotakiwa kila mzazi kujiuliza.Hii ni
dhamana,..tusifurahie tu kupata watoto, lakini tujua jinsi watoto hawo waatishi
ile kiwe kizazi bora baadaye.
Ni mimi:
emu-three
7 comments :
Nasubiri kusoma ilikuwaje...Nimependa sana wazo la leo hasa hapa "tusifurahie tu kupata watoto, lakini tujue jinsi watoto hao wataishi ili kiwe kizazi bora baadaye".
ndio m3 hujambo ,nakujuwa huwezi kutusahau hata iweje upo nasi,nami nafatilia mkasa mpya ,kwani dunia duara inazunguka na hatujuwi mwisho wake
tuombe kheri
Imekuwaje ndugu inakuja mungu akipenda, nashukuru kuwa tupo sote.
Ndiyo mpendwa Samira kama kawa tupo pamoja,je ww maisha yako hayakuwahi kukutana na mitihani kama hiyo?
Jamani kama kuna ambaye aliwahi kukutana na mitihani kama hii atupe ushahidi ili kisa kikolee utamu.
Karibuni wote kwenye kisa hiki kipya
Haya hayaa! Tupo pamoja mkuu hatua kwa hatua, mpaka mwisho!
Tupo pa1 mkuu, hatua kwa hatua mpaka mwisho!
Nikweli kabisa Ndugu wa mimi,Wazo limetulia.
Mmmhh Kisa hiki Ndugu wa mimi kina mambo mengi sana yaani kinagusa mno.MUNGU azidi kubariki kazi za mikono yako;Pamoja sanaaaaa!!
Gгeat beat ! I ωish to appгentiсe even as
уou аmеnd your web sіte, how can i subscгibe for а blog wеbsite?
The account аided me a apρlicаblе ԁeal.
ӏ have been tiny bіt familіar
of this your broadcаst provideԁ vіbrant clear idea
My website - cincinnati bail bonds
Post a Comment