Mara nyingi baada ya vikao vya chama huwa tunaingia mitaani,
huko tunatafuta hoteli nyingine , tofauti na ile tuliyofikia, na mara nyingi
yanayofanyoka huko, ni siri yetu na hawo wenye hizo hoteli. Kila mtu huwa ana
hoteli yake, ambayo anaiamini. Hayo yote nilijifunza toka kwa wenyeji wa vikao
kama hivyo.
‘Unajua kazi hizi za kisiasa zinahitaji kutulizwa, ….maana
kujibizana kwenye vikao, kimuhemuhe cha kutokujua nini kitatokea, yote hayo
yanaweza yakakupandisha shinikizo la damu, kwahiyo ili kuyakwepa hayo,
tunahitaji viburudisho vya zaida..’akaniambia mzee mmoja.
‘Mbona tumeshakunywa na kula, kuna viburudisho gani zaidi?’
nikauliza.
‘Wewe, pale umekunywa kukiwa hakuna vinurudisho vya
macho,….unajau mungu katujaliwa mapambo ya dunia, ukiyaangalia mweneywe nafasi
inarizika,…hata unywe vipi, hata ule vipi, hata uwe tajiri kiasi gani, hata
upate raha kiasi gani, hujakamilisha marizio ya nafsi yako, kama hujaona hakuna
pambo la dunia, pambo la nafsi….’akasema huyo rafiki yangu.
‘Wewe tatiz la ni mshahiri, au muimba taarabu, pambo gani
hilo, usiniambia kuwa….unanyumba ndogo’nikamwambia nikiwa siamini kuwa mzee
kama huyu anaweza kuwa na haizo tabia.
‘Iiite nyumba ndogo, au vyovyote vile , lakini mimi naita
pambo la moyo, ….ukinywa, ukila, huku yupo mbele yako, au pembeni yako
anakupepea, unasahau dunia yote ya dunia,…unasahau machungu ya vikao, unasahau
malumbano yasiyo na mpangilia kweney vikao, …ukitoka hapo akili
imetulia’akasema.
‘Mmmh, ina maana hata wewe unafanya mambo hayo, huoni kuwa
unahini ndoa yako, na ukijulikana na wajumbe wa kikao si ndio utaharibu jina
lako…’nikasema kwa wasiwasi.
‘Kilammoja anajau hilo, hakuna wa kumdanaganya mwenzako,
mimi namjua kila mmoja na mtu wake, hizo ni siri zetu, kinachotakiwa usiweke
hadharani, ufanya kwa siri, na, ukifika huko utawakuta kila mmoja kajificha
kwenye sehemu yake, hakuna anaymfiuatilia mwenzake,…’akaniambi.
‘Jamani hayo sasa mapya kwangu na sijui kama mimi naweza
kuyafanya, mimi naheshimu ndoa yangu, na namuogopa sana mungu, maana lolote
utakalolifanya kwa siri, ujue mungu yupo..anakuona’nikasema.
‘Sikiliza kijana, wewe si unataka kushinda siasa, wewe
uliniomba kuwa nikufunde kuhusus mambo ya siasa, …’akasema.
‘Lakini hayo sio mambo ya kisiasa, huo ni …u…u’nikashindwa
kutamka hilo nililolitaka kulisema.
‘Unataka kusema kuwa huo ni uchafu, ni uchafu gani unafanya,
wakati ni sehemu ya kutoa kile ulichojaliwa, na unakula na mwenzako ambaye
anakihitaji. Huo ni utu mwema, ubinadamu, …kwanini tule peke yetu, wakati
wenzetu wapo na wao wanahitaji, ….na wanahitaji sana ni hawa akina dada zetu,
mapambo ya dunia..’akasema akiangalia juu kama vila anaona raha fulani.’
‘Mimi hayo siwezi…’nikasema lakini yule mzee alinishika
mkono, name nikamfuata kama vile mtoto anayemfuata baba yake, hadi kwenye
hoteli moja iliyokuwa kando ya mji, huko akaongea na mwenye hoteli, tukapewa
ufunguo, na kwenda chumba cha maalumu.
Huko hatukukaa muda, mara wakaingia mabinti wawili,……
**********
`Mume wangu nampenda sana, na ukizingatiwa jinsi
alivyonipata kwa shida, nilijua kabisa na yeye ananipenda na hakuna atakayeweza
kumhadaa, na sikuwazia hata siku moja kuwa atakuja kunisaliti, ….’akasema mke
wa Kiongozi.
Mke wa kiongozi aliletwa hapo hospitalini akiwa hajitambui,
baada ya kupata mshituko, uliosababisha shinikizo la damu.
‘Vipi imekuwaje tena, wakati uliniambia kuwa ulishapata dawa
ambayo imeondoa hilo tatizo?’ mke wangu akamuuliza mgonjwa.
‘Hata mimi nilijua kuwa hilo tatizo limekwisha, na
ukizingatia kuwa nilishajiweka katika hali ya kurizika na mimi nikawa
najichanganya katika maisha ambayo sikujua kama na mimi nitaweza kuwa nayo,
maisha ambayo hakuna angeliweza kuamini kuwa na mimi nilikuwa nimejihusisha
nayo.
‘Maisha gani tena hayo, ambayo ulijihusisha nayo, na sisi
sote tunakujua kuwa ni mke mwema,….?’ Akamuuliza mke wangu.
‘Haya maisha ya ndoa yasikie tu, usiwaone watu wapo mitaani,
au wanapita njiani wakiwa wameshikana mikono ukawazia kuwa huenda hawana
matatizo yoyote,…..kama sio hili ni lile. …’akasema ankutulia.
‘Kwahiyo na wewe ulishindwa kuvumilia hayo matatizo ndio
shinikizo la damu likakuathiri tena?’ akaulizwa.
‘Wewe ni rafiki yangu, na nimekuwa karibu sana na wewe, na
nilijaribu sana kukuficha mengi ya mimi na mume wangu, kwa vile najua ni wajibu
wangu kama mke kufanya hivyo, lakini haya yaliyonifika yanahitaji mtu wa karibu
wa kunishauri, maana sasa nipo njia panda,…..’akasema akionyesha uso wa kutahayari.
‘Sawa rafiki yangu, najua kweli umefikwa, na nitajitahidi
kukushauri vile niwezavyo, maana mimi mara nyingi najua wewe ndiye wa
kutushauri sisi kwa jinsi ulivyo, kila mtu anapenda tabia zako’akamwambia mke
wangu.
‘Hapo ndipo tunakosea, maana sio kila mtu anakijua, kila mtu
ana uazaifu wake,mimi ninaju hiki na kujitahidi kila niwezavyo, lakini kune
mengine yanashindikana ambayo yule ambaye unayemuona hafai naweza akakupa
ushauri wa maana zaidi, lakini inatakiwa kuangalia ni nani wa kuomba kwake
ushauri, hili nimejifunza, na limekuwa fundisho kwangu…’akatulia na kujinyosha
pale kitandani.
‘Kwani ni nini hasa kikubwa, ….hebu niambie tuone tutafanya
nini?’ akasema mke wangu.
‘Tatizo huenda limeanzia mbali,….lakini mimi nimeinizwa tu
kama chambo bila kujua, na ndio maana naogopa hata kumwaminimtu tena, maana
yuleunayemuona ni rafiki , anaweza akawa adui mkubwa, bila hata yaw ewe kujua,
maana hujui undani wake…’akainuka na kukaa, na kweli alionyesha kuchoka.
‘Matatizo yangu yalianza pale nilipoamua kujichanganya, na
hili tulikubaliana na mume wangu kuwa ili tuweze kuweka misha yangu vyema ni
bora na mimi nijishughulishe, na ili tufanikiwe, nahitaji kusoma kidogo kuhusu
mambo ya biashara , tukakubaliana na nikaingia shule, …..’akaanza kuongea .
Huko shuleni, ni lazima uwe na marafiki ambao watakusaidia
masomo, maana kichwa kilishaanza kushika mambo ya kidunia, sikujau kuwa
nitaingia darasani tena, na ndiponikakutana na yule aliyenisaidia siku ile ya
ndoa…’akajaribu kutabasamu.
‘Ina maana yale yaliyotokea siku ile ya ndoa ulikuwa
ukiyajua,..?’ nikamuuliza.
‘Kiukweli nilikuwa siyajui, nilikuja kuyajua baadaye,…muda
mchache tu pale alipokuja mama mmoja kwenye chumba nilichokuwa nimefungiwa, na huyo
mama ndiye aliyenitoa kile kitambaa machoni, na mdomoni, maana nilifungwa
machine na mdomi, na akanifungua zile kamba zilizokuwa nimefungiwa miguuni.
‘Kwa muda ule sikujua ni nani, maana alivyokuwa kavaa,
ilikuwa sio rahisi kumgundua, alikuwa kajifunga mtandio shingoni, kama tai, kavaa nywele za bandia ndefu, na machoni kavaa
mawani mikubwa meusi, na akawa akijitahidi kuongea kwa sauti ya kuigiza ya
mzungu anayejifunza Kiswahili….’akatulia.
Tofauti na alivyokuja mwanzoni,maana mwanzoni alikuwa mkali,
akiongea kwa vitisho, lakini leo japokuwa alikuwa akiongea kwa laafudhi ile ile,
lakini alikuwa akiongea kwa upole, na alionyesha kunijali,….akanisogelea na
kusema;
‘Jamaa kaingia mkenge, hutaamini kuwa hakujua mpaka
allipofunga ndoa, na wakati alipotaka kumfunua yule binti, shangazi yake
akacheza mchezo , maana hakuwa na jinsi, japokuwa mwanzoni alinipinga sana,
….’akasema huyo mama sikujua ana maana gani.
‘Kwahiyo mpaka wanaondoka hapo, hakujua kuwa kaoa mke
kanyaboya?’ akauliza yule mlinzi akicheka kwa kebehi.
‘Mpaka wanaondoka, …na nasikia hadi wanafika nyumbani kwao
,ambapo kulikuwa nasherehe kubwa, alikuwa hajajua hilo, na kivumbi ilikuwa
wakati wapo ndani…’akasema yule mama huku akicheka.
‘Lete uhondo ilikuwaje?’
Walipofika ndani, ilikuwa ni utambuslisho kwanza kabala
hawajaingi kwenye ukumbi maalumu uliaandaliwa, bwana akawa kasimama akiongea na
wazazi wake, na yule binti, alikuwa kasimama na wapambe wake….muda huo bado kava
lile gauni kubwa, na alikuwa bado kajifuka gubi gubi…‘
‘Aliyechokoza mambo ni shangazi wa bwana harusi, yeye akaenda
na kushika bibi harusi wakaingi wote chumbani, …..na bwana harusi akafuta kwa
nyuma, alisubiri kidogo kablsa ahjaingia ndani, akijua labda bibi harusi
anaandaliwa , kichwani akijenga picha nyingi za kushinda na kumpata binti
mrembo, mara shangazi yake akatoka haraka huku uso ukiwa umebadilika.
Bwana harusi hakujali hilo, yeye akaingi ndani taratibu,,….na
kutupa macho pale kwenye sofa lililokuwa limewekwa hapo chumbani,…akapikicha
macho,…ya kutokuamini, akangalai huku nakule, akimtafuta mrembo wake,…
‘Karibu mume wangu, nipo hapa, hakuna mwingine zaidi yangu…’akasema
yule mwanamke kwa uso uliojaa furaha, na kebehi.
‘Wewe umeingiaje humu ndani, na mke wangu yupo wapi?’
akauliza kwa hasira, huku akingalai huku na kule.
‘Mke wako yupo wapi tena, mbona unanishangaza, mimi ndiye
mke wako halali,…’akasema akimuonyesha ile pete aliyomvalisha pale wakati wanafunga
ndoa.
‘Kumbe ndio maana hukutana nikiangalie wakati nilipotaka kukuangalia,
wakati tunafunga ndoa, ningelijua ningelikufurumua pale mbele ya watu…na leo nitahakikisha
unatoka hapa ukiwa ….’akasema na kumfuata akitaka kumpiga.
Wakati anamsogelea huku akijuta kwanini hakuweza kumfungua pale na kumwangalia, alikumbuka kichwani, jinsi ilivyokuwa, akakumbuka pale
kwenye ndoa, alipojaribu kumfunua,ili amuangalie usoni, lakini binti yule
alikataa, …Yeye mwenyewe kwa kujiamini, kwani alijua kuwa ni yule binti mrembo,
anaona aibu, na kwa vile ndoa imekuwa kama ya kualzimishwa, akasema haina haja
, ilimradi ndoa inafungwa, wataonana mbele kwa mbele.
Ndoa ikafungwa, na vigelegele vikatanda hewani, huku
shangazi wa bibi harusi akiwa haamini kuwa mpango umewezekana, na hadi
wanaondoka pale alikuwa hajaamini, …..
‘Ina maana huyo shangazi wa bibi harusi alikuwa akiyajua
hayo?’ akaulizwa.
‘Nilimweleza huo mpango saa chache tu, kabla hawajafika hawo
waowaji, alipinga vikali, lakini nikamwambi akubali asikubali hilo litafanyika,…hakuwa
na jinsi, hata hivyo ,hata yeye alikuwa kaipnga vikali hiyo ndoa, isifanyike,
lakini waume waliikomalia,…si wameshakula hela za watu…’akasema huyu mama.
‘Basi mambo yaliyofuata hapo ilikuwa kivumbi na jasho, kutupiana
maneno ya jaziba, na baaadaye yule mkewe,..maana ni mkewe tena, akasema;
‘Wewe….tulia kwanza, usiharibu siku yetu muhimu..nikuulize
hivi wewe kila siku nilipokuwa nikikuuliza kuwa kweli unanipenda, ulikuwa ukinijibu
nini….?’ Akauliza yule binti akiwa keshatulia, na alijau jinsi gani ya
kumuingia huyo jamaa, na wakati huo yupo tayari kwa lolote.
‘Yale yalikuwa ni mapenzi ya kudanganyana tu, sikuwa na
mpengo na wewe…..’akasema huyu jamaa akiwa kakakasirika, na alishatayarisha
ngumi, lakini mkono ukawa mnzito.
‘Hivi wewe ulitarajia
nini kwangu, kuwa uuchezee mwili wangu tuuu…eehe, na mwisho wa siku uende kuoa
mke mwingine’ akasema huyu binti akiwa kashika kiuno, hakuogopa, na alikuwa
tayari kupambana.
‘Hatukuwa na makubaliano hayo, wewe ulichohitajia ni pesa
zangu, na ulizipata , na mkataba wetu ukaisha, mambo ya ndoa yalikuwa sio
makubaliano yetu, mimi na wewe’akasema huyu jamaa akiwa kawaka, na ile suti
aliiona inambana.
‘Hiyo haipo, ulisema mwenyewe kuwa mambo yako yakiwa sawa
tutafunga ndoa, unabisha hukusema hivyo,….sasa mimi ni mkeo halali, …naona
mambo yako yameshakamilika, ndio maana ukatayarisha hiyo harusi ….na tukafunga
ndoa, …ugomvi upo wapi,…ukumbuke pale, ulikubali mbele ya mashahidi kuwa upo tayari kuwa
na mimi….kwa raha na shida…kama ulivyotamka siku ile tulipofunga uchumba mimi
na wewe…umesahau…’akasema yule binti akimsogelea kutaka kumkumbatia na yule
jamaa akamsukuma.
‘Mimi hiyo sikubali, utaondoka hapa nyumbani sasa hivi…’alisema
yule mwanaume na kumshika huyo binti mkono, huku akimvutia nje,na watu waliposikia vurumai huki ndani,
mmoja aikabidi agonge mlango kuuliza kuna nini, na kablahajagonga vyema mlango
ukafunguka na jamaa akaonekana akivutana na huyo binti, na shangazi mtu ambaye alishawaita
wazazi wa bwana harusi akaingia ndani na kuanza kuwasuluhisha.
‘Jamani msijaze watu, tulieni, wazee wamekuja tutafute
suluhisho…mkileta vurugu, mtaumbuka wenyewe…’akasema shangazi.
‘Na kweli ataumbuka….mimi ni mkewe halali…’akasema yule
binti.
Baadaye wazee walikutana akiwemo bwana ba bibi harusi,
wakaanza kuhojiwa, na binti akajieleza;
‘Huyu bwana simuelewi, kakubali mwenyewe kufungandoa na
mimi, tangu siku nyingi, na mbele ya wakuu, alikubali kuwa yupo tayari kufunga
ndoa na mimi..’akasema yule binti.
‘Mimi sikujua nii wewe….’akajitetea huyu bwana harusi,
akanyamazishwa. Na hata muda wake wa kujitetea ulipofika, alijikuta akiwa
hawezi hata kuongea, kwa hasira na kutahayari.
‘Baadaye wazee wakatumia busara zao, maana binti alihojiwa na
kuanza kujieleza vyema, kwanini kafanya vile, na ili kuthibitisha kuwa yeye
ndiye aliyekuwa mchumba wake halali, kabla hajamtelekeza, akatoa vielelezo vingi
vya picha kuonyesha kuwa yeye ndiye aliyestahili kuolewa na huyo jamaa, na
jamaa alipoulizwa je, huyu aliwahi kuwa mchumba wake, akasema ndio, lakini
hakuwa tayari kumuoa, kwani alishapata anayependa.
‘Hatukuelewi,kama mlifika hadi kupeana uchumba, ulitarajia
nini..hebu jiweke wewe kweney nafasi yake, hebu jiulize wangapi waliokuwa
wakimtaka, wakawa hawana nafasi hiyo tena, kwasababu ulishamvalisha pete ya
uchumba, halafu baadaye unamtelekeza…hapo hujatuambai kitu, huyu sasa ni mkeo
halali….’akasema mama mmoja.
‘Huyu ndiye bahati yako, haina haja ya vuruga, …’akasema mama
yake mzazi, na wengi wakakubaliana na hilo, na jamaa alipoona hana wa kumtetea
akaondoka hapo nyumbani, na kwenda kusipojulikana, haijulikanai kuwa
atakubaliana na hiyo ndoa, au atafanyaje...lakini tumjuavyo, aatkuwa kwwney baa
anakunywa …..’akamalizia yule mama.
‘Hakwenda polisi kuwafahamisha kuwa mchumba wake katekwa
nyara?’ akaulizwa yule mama.
‘Hawezi kwenda polisi yule, anajua akifnay hivyo ataumbuka
zaidi…’akasema huyu mama na baadaye akamgeukia huyo binti na kusema;
‘Usihofu binti, upo salama, ninachotaka ni wewe usiolewe na
huyo muhuni, …kuolewa na yeye ni kama kumtupia mwewe kifaranga cha kuku, ….yule
namjua vyema, naijua hadi familia yao, naona ajabu baba yako kukubali uolewe na
huyo mtu wakati anawajua fika, lakini najua sio yeye, ila ni sababu ya mkewe,….’akasema
yule mama.
‘Kwani wewe ni nani, na kwanini uwe na uchungu na mimi?’
huyo binti akamuuliza.
‘Hayo utayajua baadaye, ila nimekuja kukutoa wasiwasi, ili
ujue kuwa haya hayakufanyika kwa nia mbaya, na mengine, ni mambo ya kupoteza
muda, ili ijulikane kuwa tumekuteka nyara kwasababu ya kupata pesa, lakini
sivyo hivyo kabisa…’akasema huyo mama.
‘Mbona mimi siwaelewi….’nikasema.
‘Utaelewa tu, ninachokuomba ni wewe kutulia, ndio maana
nimekufungua kila kitu, ili uwe huru, ila nakuomba usifanya jambo jingine
lolote kama la kutoroka, mwenyewe utakuja kufurahi kuwa kweli nimekuokoa kwa
kutaka kupelekwa kusikokufaa kwa tamaa za watu. Najua ni jukumu langu kukufanyia
hivyo….’akasema yule mama, na baadaye akawageukia wale mabaunsa na kuwaambia.
‘Sitaki mumusumbue huyu binti kuanzia sasa, maana lile zoezi
la awali limeshakamilika, hakikisheni mnampa kila anachokihitaji, cha muhimu,
ni usalama wake, mengine nitakuja mwenyewe kuongea naye,…’akasema huyo mama na
kuondoka.
Siku ile nzima sikumuona huyo mama, na niliweza kutembea humo
ndani kwenye hiyo nyumba, niliyokuwa
nimeshikiliwa, sikuruhusiwa kutoka nje, niliweza kuingia chumba kimoja baada ya
kingine, maana ilikuwa ni nyumba kubwa, lakini sikuruhusiwa kabisa kutoka nje,….hata
ilipofika usiku.
Ilipofika usiku nilibakia kuangalia runinga, na baadaye
usingizi uliponijia nikalala , na kesho yake, asubuhi nikiwa nimechoka na yale maisha,
nikaanza kulalamika. Na nilipoona hawanijali, nikaamua kulazimisha kutoka nje,na yule askari
akanizuia, nikamwambia kwa hasira;
‘Mimi nataka kutoka nje, mbona mnanifanyia hivyo jamani,
kwani mimi ni mfungwa hapa?’ nikauliza huku nikijisi kizunguzungu, maana muda
mwingi niliokuwa hapo nilikuwa sijisikii kula,kwahiyo mwili ulikuwa hauna nguvu.
‘Wewe subiri kidogo, utaongea na mama,anakuja sasa hivi
…’akasema huyo mlinzi ambaye
Na kweli haikupita muda, mara mlango ukafunguliwa, na wakati
huo nilikuwa nimeinama chini, nikijizuia kulia, na nilipoinua kichwa na
kuangalia kule mlangoni, ili nimuone huyo aliyeingia, nilibakia nimeduwaa,
nikatoa macho ya kutoamini, na kabla sijasema neno, nikahisi giza likitanda
usoni, ….
NB : Hii ni sehemu ya pili ya kisa chetu, maelezo ya mke wa jamaa, tuzidi kuwepo
WAZO LA LEO: Alipangalo mungu kuwa liwe,huwa...
Ni mimi:
emu-three
6 comments :
Hivi niulize kweli mtu unaweza ukaoa na mkafunga ndoa, bila kwanza ya kuiona sura ya unayemuoa!
Maana pale ukishafunga ndoa, unaambia umfunue umwangalia,lkn hapa kweli, mbona unamfunua baada ya kufunga ndoa, au sio jamani, maana mm sijao?
Unamfunua kwanza unamuona kuwa ni yeye, ndio ufunge ndoa au ndio munafunga ndoa kwanza halafu ndio unapewa ruhusa ya kumfunua usoni na kumwangalia, au unakwenda ndani kumuona kwa Waislamu,baada ya kufunga ndoa? Hapa kweli kuna fundisho, tuwe makini tusije tukaoa kanyaboya.
M3 twashukuru sana kwa kutujali, mm hapa nimepata fundisho, kwa wale tunaotarajia kuoa. Ubarikiwe sana
Kuoa kwa namna hiyo kumepitwa na wakati. Siku hizi mnapimana kwanza weeee, na baadaye ukiona safi, unajua sasa huyu tutaivana, ndio mnafunga ndoa.
Kwahiyo siku ya kufunga ndoa, unamjau mtu unayemuoa,au kukuoa, ipasavyo,hata akijibadili vipi utajua huyu ndio yeye, au sio yeye.
Hawa naona walifunga ndoa usiku, au kwenye kizakiza hivi au ndio hiyop laana ya kulazimisha kuoa, utaoaje mtu hakupendi.
LAKINI KISA KINAVUTIA, TUPE UHONDO M3,INGAWAJE UNATUBANIA KUIONA SURA YAKO!
Mmmmhh kweli Mbio za sakafuni ndugu wamimi,Kazi muruwaa kabisa yaani naishiwa maneno.
Wazo Leo limenigusa sana.
Pamoja Daima!!!
mie hoi, napenda kusoma ila kazi nazo, bosi mkali, mpaka atoke ndo panya tutawale haaahaaaa.. kisa hiki naamini kina mafunzo mengi sana tu. mimi nakuombea tu ufanikiwe kutoa vitabu vya hadithi zilizopita hasa ile akufaae kwa dhiki daah ile ilikuwa funga kazi. kila la kheri mwaya.
raha ya harusi bwana harusi akufunue akuone bi harusi au sio jamani.
wazo tamu kweli......pamoja sana....ila mambo ya kuoana bila kuonana mimi hilo nalipinga kabisa
Post a Comment