Kuna siku za nyuma, nilipita mahali nikakuta kuku
wanapigana, na cha ajabu, watu walikuwa pembeni wakishangilia, na kila mmoja
akimpa ushindi mmoja wa kuku wale. Na binadamu tulivyo watu walikusanyika na
kuwazunguka wale kuku huku wakishangilia. Leo nimekuta jambo hilo, lakini cha
ajabu baadaye kwenye hilo kundi la watu, kukatokea mzozano, kuna mmoja akdai
kuwa mwenzake kamsemea mbovu, na badala ya kuangalia wale kuku,ikabidi watu
wageuka kuangalia watu wakikabana na na kurushiana makonde,na kuishia
kuumizana.
‘Jamani mbona mnakuwa kama hawa kuku!’akasema mama mmoja.
‘Na wewe mwanamke, usilete maneno yako ya kejeri hapa, ninaweza kukuchenjia na wewe’akasema
mmoja wa wale waliokuwa wakipigana.
‘Unajua tofauti yetu na hawa kuku, ni kuwa sisi wanadamu
mungu katupa busara na hekima, ili tuweze kuwa na maamuzi sahihi’nikasema.
‘Ni kweli’mmoja akadakia.
‘Sasa hebu angalieni wale kuku, wamepigana mpaka sasa hawana
nguvu, kila mmoja anapepesuka, hebu tujiulize wale kuku walikuwa wakipigania nini,?’
nikauliza.
‘Mmoja kaingia kwenye anga za mwingine, huoni yule mtetea
aliyesimama pembeni, kila mmoja anataka kumuonyesha yule mtetea kuwa yeye ni
zaidi ya mwenzake’akasema bwana mdogo mmoja.
‘Je na hawa waliokuwa wakipigana hapa sasa hivi wanataka
kuonyeshana nini?’ akauliza jamaa mmoja.
‘Hawa naona bangi zinawakera kichwani, waacheni wapigane,
wakiumizana watajifunza, kwani wahenga walisema ndugu wakipigana chukua jembe
ukalime’akasema jamaa mwingine.
‘Hapana, sio vyema watu wakigombana mkawaachia hadi kupigana
na kuumizana. Ni vyema ukiona watu wamekosana, ukawapatanisha, kwani
kupatanisha waliokosana, ni jambo analolipenda sana mwenyezimungu. Na hebu angalia
mataifa yanayogombana, nini kinatokea, kama sio watu kukimbia majumba yao, na kwenda
kuishi ugenini, na ukiangalia sana wanaoumia zaidi ni watoto, wazee na akina
mama. Je hapo kuna heri gani’ akasema mzee mmoja.
‘Kupatanisha waliokosana ni jambo la heri,na kama sote
tutakuwa na mioyo ya kupaatnishana , dunia hii ingelikuwa ni uwanja wa amani na
upendo. Cha ajabu ni kuwa dunia hii imegeuka kuwa uwanja wa fujo kwasababu
tunaona raha watu waigombana, na baadala ya kuwapatanisha sisi tunazidi kuwachonganisha.
‘Hebu angalieni vyombo vingine vya habari, hasa hivyo
vinavyoitwa vya udaku,ni nini wanachokifanya,je kinaleta heri, kama sio
kufarakanisha. Haya angalieni mataifa mengine ambayo badalaya kupatansiha watu
wanazidi kuwachochea, kwa kulalia upande mmoja, nia hasa ni nini kama sio
ubinafsi . Kwa mtaji huo dunia haitakuwa
na heri kamwe, amani na upendo vitakuwa kama msamiati uliosahaulika.
Tupende kupatanishana ili tuwe na heri, na jambo hili mola
pekee ndiye mlipaji, usifanye hivyo kwa jaili ya kujionyesha kwa watu ,au kwa
kutafuta sifa, fanya hivyo kwa ajili ya mola wako ukitarajia heri nyingi baadaye,
na kweli utaziona kuanzia hapa hapa dunia.
Mimi naona ajabu watu wanafarakana , na hata kufikia hatua ya
kununiana, na wanaweza wakaishi hivi hivi masiku kadhaa , na hata miezi, kila
mmoja hataki kuongea na mwenzake, na hutaamini ukiambiwa kuwa hawo ni ndugu
baba na mama mmoja. Na ukichunguza sana, ni sababau ya kufitinishwa. Ndio maana wahenga walisema ni bora hata ya mchawi kuliko mfitinishaji. Hili jamani sio jambo jema na halina heri kwetu.
Tukumbuke kuwa sisi ni wanadamu, sio kuku au wanyama, tuna
akili, na tumepewa hekima na busara, vitu ambavyo ni bure kabisa, havihitaji
kununuliwa. Tutashindwa na kuku, au
wanyama wengine, ambao licha ya kuogombana kwao lakini kesho unaweza ukawakuta wanakula
chakula pamoja na hata kuingia banda moja mahali wanapolala.
Amani duniani
itatengemaa, kama sote tutajitahidi kuwapatanisha wale waliokosana kwa usawa,
bila ya ubaguzi, bila kujali tofauti zao, kwani amani ikivurugika haijali hizo
tofauti, kila mmoja aatingie kwenye hasara.
Ijumaa njema..
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
I dοn't even know how I ended up here, but I thought this post was good. I do not know who you are but definitely you are going to a famous blogger if you aren't alгeadу
;) Cheerѕ!
Also see my webpage: indianapolis emergency vet
ubinafsi ukizidi ndo mambo yanakuwa hivyo...ijumaa njema nawe pia na wote watakaopita hapa..
Post a Comment