‘Je ulipotoka bafuni ulifika pale kitandani na kushika
chochote?’ akaulizwa.
‘Hapana, nilipotoka pale na kuangalia pale kitandani na
kumuona yule mwanamke alivyokuwa kalala, na kifuani kunavuja damu,sikutaka hata
kumsogelea’akasema.
‘Sasa ulijuaje kuwa amekufa?’ akaulizwa.
‘Kwa jinsi alivyokuwa katoa macho, na ulimi umetokeza nje,
ilikuwa dalili kwangu kuwa keshakufa’akasema.
‘Uliposikia mlio ulichukua muda gani hadi kutoka bafuni?’
akaulizwa.
‘Niliposikia huoo mlio cha kwanza nilitulia nikiwaza ni kitu
gani, ndioakili yangu ilinituma kabisa kuwa ni mlio wa bunduki, lakini umetokwa
wapi, …na baaadaye nikachukua taulo na kujifuta maji, kwani
nilikwuanimeshamaliza kuoga, na kutoka nje haraka, na wakati natoka’hapo
akatulia.
‘Ongea, wakati unatoka ilikwuaje?’ akaulizwa.
‘Nakumbuka kulikuwa na mhudumu ambaye nilimwambai anisubiri
,kama nikihitaji kitu, nilihisi ndio yeye, ingawaje sina uhakika, alifungua
mlangi akitoka na kufunga’akasema.
‘Mlango upi?’ akaulizwa.
‘Pale hotelini chumba nilichokuwepo kina sehemu ya mapumziko
na chumba cha kulala, sasa yule binti alikuwa chumba cha mapumziko, na ukitoka
bafuni, unaweza ukapitia mlango wa kuingia chumba cha mapumziko au ukatokea
chumbani. Mimi nilitokea chumba cha mapumziko kwakuchanganyikiwa’akasema.
‘Huyu muhudumu, wakati anatoka, alikuwa kashika
nini?’akaulizwa.
‘Sikuweza kumwangali vyema , lakini kwa kumbukumbu zangu,
alikuwa kashikilia lile sinia la vinywaji, na alikuwa naye kachanganyikwia,
nahisi ni kwasababu ya kusikia mlio wa bunduki’akasema.
‘Je ukiwa bafuni huwezi kusikia sauti za watu wakiongea nje,
chumbani au sehemu ya kupumzikia?’ akaulizwa.
‘Unaweza kusikia,na kwa muda huo kulikuwa na sauti ya
runinga, ambayo ilikuwa bado haijazimwa, alikuwa akiangalai yule mhudumu, na
kwa ndani chumbani halikadhalika, kulikuwa na sauti ya runinga alikwua
akiangalia huyo mwenzangu, kwahiyo sauti zilikuwa nyingi, sio rahisi kugundua kuwa
ni nani anaongea na anaongea kitu gani’akasema.
‘Sauti ya runinga na sauti za watu zipo tofauti, …’akasema
mwanadada.
‘Kwa vile sikuwa na mawazoo ya kusikiliza nini kinaongewa
kwa muda huo, kwanza nilikuwa na mawazo ya familia yangu, pili hizo sauti ni nyingi,
na tatu mambo ya kisiasa ylikuwa yakipita kichwani, kwahiyo nisingelikuwa na
mawazo mengine, hata kama kulikuwa na watu wanaongea’akasema.
‘Hukusikia mlangoo ukifungwa na kufunguliwa ?’ akaulizwa.
‘Hilo nakumbuka nilisikia,nakumbuka sana, na ulikuwa mlango
wa nje, ambao ulikuwa ukiufungua au kufunga hutoa sauti tofauti na mlango wa
kuingia chumbani.’kasema.
Mwanadada alipomuhoji mke wa muheshimiwa alibakia mdomo wazi
kwa muda, hakuamini;
‘Ina maana wewe ulikuwepo siku hiyo ya tukio, na mumeo
hajui?’ akaulizwa.
‘Ndio mimi nilikuwepo hapo, na …nilifikahapo nikiwa sijijui
kwasababu ya ulevi, na zaidi nilikuwa nimechukau bastola, ya rafiki
yangu,’akasema.
‘Mamamamaaa….ok, je hiyo bastola anayo bado huyo rafiki yako?’
akaulizwa.
‘Sina uhakika huo?’ akasema.
Mwanadada alipofuatilia kumbukumbu za polisi aligundua kuwa
bastola iliyomua huyo marehemu sio hiyo anayomiliki huyo mke wa adui wa
muheshimiwa, na hapo akawa na ahueni kuwa mke wa muheshimiwa sio yeye aliyeua.
‘Naomba tafadhali usije kumwambia mume wangu kuwa mimi
nilikuwepo siku hiyo, yalipotokea hayo mauaji,’akasema mke wamuheshimiwa’
‘Kwanini,?’ akaulizwa.
‘Mimi katikamaisha yangu sijawahi kufanya kitu kama
hicho,naheshimu sana ndoa yangu,nilifanya hivyo kwasababu ya shinikizo la huyo
rafiki yangu…na jinsi nilivyoona kule na kushuhudia mwenyewe kuwa kweli mume
wangu ana nyumba ndogo, mimi sioni umuhimu wa kuwa mke wake, nasubiri akipona
tu, naomba talaka yangu…’akasema.‘
‘Hapana hilo sio jambo jema,kwanza tumalizane ni hili, ili
tuone jinsi gani ya kuwasafisha na tukio hili,na ikibidi kufika mhakamani,
hatuna jinsi,inabidi ijulikane tu kuwa ulikuwepo’akasema wakili mwanadada,
‘Lakini nitajitahidi kama huhitaji kujulikana, ….’akasema
huku akiwaza jinsi gani ya kufanya ili kweli huyo mwanamke asijulikane kuwa
alikuwepo huko.
Wakili mwanadada baada ya kusikiliza maelezo ya wanafamilia
hawa kila mmoja kwa wakati wake, alifika ofisini kwake na kuanza kufikiri jinsi
gani ya kuwaokoa hawa watu, kwani sio tu mambo ya kisiasa, lakinii kuna maswala
ya ndoa, ambayo imeshaingai doa.
Kila siku anapopata kazi mpya ambayo mara nyingi inahusiana
na ndoa za watu, anakuta ndani yake kuna mauaji, na mauaji yenyewe yameweka
kinamna ambayo sio rahisi kumgundua muuaji, na yule ambaya anashikiliwa na
polisi utakuta hahusiki kabisa na mauaji hayo.
Alimuwaza huyu mwanaume ambaya kwa sasa hali yake bado sioo
nzuri, na ameshauriwa na dakitari asimuulize maswali ambayo yanaweza kumtia
wasiwasi mgonjwa. Lakini maelezo machache aliyopata yamemfanya agundue kuwa
kinachoendelea hapo na mambo ya mlungula, kuwa ili mambo yaishe akubalaine na
matakwa yao.
*********
‘Mimi nii wakili wa familia ya muheshimiwa, nimekuja hapa
kwa maswali machache yanayohisiana na watejawangu’akasema wakili mwanadada.
‘Maswali gani hayo, mimi sina mahusiano na hiyo familia?’
mke wa jamaa akauliza kwa wasiwasi.
‘Ndio , najua huna mahusiano na hawa watu,na mumeo ni adui
mkubwa wa hiyo familia, hata hivyo, ni vyema tukajua kuwa sisi wanawake ndio
tunaotakiwa kuwajenga waume zetu wawe na roho nzuri.Uadui na chuki sio silka
njema ya maisha, kwani adui yako wa leo anaweza akawa msaada kwako kesho’akasema
wakili mwanadada na yule mwanamke akawa ktulia.
‘Kwa kukumbusha tu, Unakumbuka siku ile ulipomchukua mke wa
muheshimiwa, na kwenda naye huko Dodoma, kwa minajili ya wewe kutaka
kumuonyesha ushahidi kuwa mume wake ana nyumba ndogo, na kwenye safari ile
kulitokea mauaji…?.’akauliza wakili mwanadada.
‘Mimi, …hapana, labda umekosea, sijawahi kuondoka na huyo mwanamke. Hivi mimi
nitoke na mtu wa familia hiyo hadi huko Dodoma, unafikiriaje, wale ni maadui
wetu wakubwa. Ndio, nakumbuka kuwa nilikutana na huyo mwanamke nikampa liftil kiubinadamu tu, lakini kuondoka
naye, hilo silijui’akasema yule mwanamke akionyesha wasiwasi.
‘Usiharakishe kukana, najua kwanini unasema hivyo, lakini
kama nilivyokwisha kukutambushakuwa mimi ni wakili wao, na walishakufahamisha
hilo nasikia ukakata simu,…ukweli ni kuwa mlikuwa naye, na wewe ndiye
uliyemshawishi, hili usilikatae, ninachoka hapa ni mimi na wewe tusaidiane, ili
kulimaliza hili tatizo,…’akasema wakili mwanadada.
‘Mimi nimekuambia sihusiki, kama unahitaji lolote nenda
polisi, wao wanajua zaidi, lakini mimi sihusiki kwa lolote, na sitasema lolote,
natumai umenielewa, maana hivi sasa ninasafari zangu, siwezi kukaa hapa
kusikiliza tuhuma ambazo hazina tija kwangu’akasema.
‘Ushahidi upo, kuwa mliondoka naye, na gari mlilokodi
linajulikana na hawo mliowakodi wameshathibitisha hilo, sasa mimi sioni kwanini
ukatae, na kwenda polisi sio hoja, wao watakuja kwa wakati wao, maana hiyo kesi
imefufuliwa upya.
Yule mwanamke akashituka kidogo na kuangalia chini, kama
anawaza jambo, lakini hakusema kitu.
‘Mimi ninachotaka ni kuwasaida nyie, hasa akina mama.Najua
hayo yalitokea kwasababu ya nia njema, ya kuwalinda waume zenu, na mlihitaji
ushahidi, na katika kufanya hilo ndio mkajikuta mumeingia kwenye mataizo, sasa
naomba tusaidiane hili swala muondakane na huu mzigo.
‘Mimi sijahitaji msaada wako, kwanza nina wakili wangu, kama
ni maswala ya kisheria , basi nitapanga siku mkutane naye, ‘akasema.
‘Hilo halina shida, tutakutaka ikibidi, lakini kwanini
twende kote huko, mimi nimekuja kwa kuomba msaada wako uli kuliweka hili swala
vyema, unakumbuka siku ile usiku , siku ambayo mauaji hayo yalitokea, unamkumbuka
yule binti wa tajiri wa ile hoteli ambaye ndiye unayemtumia kupata taarifa za
mumeo, alikuambia nini? Akaulizwa.
‘Binti gani huyo, ?’ akauliza kwa haraka na kuonyesha
wasiwasi.
‘Hakukuambia kuwa kuna mtu anataka kumkomesha, na ukamwambia utamsaidia, je ulimsaida vipi, ?’ akaulizwa.
‘Wewe tatizo lako unasikiliza maneno ya watu, lakini hayana
nafasi kisheria’akasema.
‘Yalikifika mahakamani yana nafasi, hebu kumbuka vyema siku
ile , yule mwanamke alivyokuwa, jinsi alivyokunywa kupitiliza na wewe ukawa
unamsaidia, je alipotokapale alikwenda wapi,na unakumbuka yale maneno aliyosema
hadi mkaanza kuzozana, hebu kumbuke vyema’akasema wakili mwanadada.
Yule mwanamke akakunja uso akiwa kama anawaza jambo ndipo
akakumbuka tukio lile ambalo yeye hakuwa amelitilia manani, kumbe…..
********
‘Rafiki yangu naomba msaada wako, ?’ akakumbuka siku ile
walipokuwa wakiongea na huyo binti ambaye ni mmoja wa viongozi wa hiyo hoteli.
‘Msaada gani, wewe niambie mimi nitakusaidia kama
inawezekana’akasema.
‘Kuna malaya mmoja anajifanya yeye anaweza kutembea na kila
mwanaume, sasa hivi kanichukulia mtu wangu, ambaye nilishajua ndiye kitega
uchumi changu, na baya zaidi anaongea mbele za watu kuwa kanizidi ujanja’akasema.
‘Malaya gani huyo, achane naye, wanaume wapo wengi, kwani
wewe shida yako ni nini, pesa unazo, maisha mazuri unayo, unataka nini zaidi?’
akaulizwa.
‘Kanizalilisha, kutangaza kuwa mimi silolote kwake, na
kwanini aingilie anga zangu, na hili sio mara ya kwanza, halafu nikuambia
ukweli huyu nii mmoja wa wshikaji wa mumeo’akasema
‘Ni yupi huyo?’akauliza.
‘Yule mwalimu wa kule juu, yule ambaye alikuja wakati
tunajaribu zile nguo akaanza kuongea kiingereza chake kibovu, akasema na y eye anahitaji
nguo kwa ajili ya harusi yake, nikakubonyeza kwa kukuambia achana
naye,umemkumbuka?’ akasema huyo binti.
‘Sasa yule naye anakubabaisha, kwanza ni rafiki yako, na
siuliniambai kuwa ndiye anatembea na muheshimiwa adui wa mume wangu’akasema.
‘Huyo huyo, …ni mshikaji wa mume, anakula huku na huku’akasema.
‘Sasa unataka tumfanye vipi?’ akaulizwa . Yule binti
akapitisha kidole shingoni, kuashiria kuwa anataka kumuua
‘Hayo achana nayo kwa sasa muda utafika wa kuchukua hatua,
watakuja kujimaliza wenyewe, usiwe na papara’akamwambia huyo mwanadada.
‘Muda bado, wakati ananizalilisha, kanichukulia mtu wangu, na
bado ananifuata fuata kwenye maisha yangu, ngoja …leo nikitoka hapa,
nitamuonyesha jambo, kuwa mimi ni askari alikimbia jeshi,…ngoja kuna kitu
nakifuatilia, kikikamlika tu, basi sijui kesho itamkuta…’akasema na wakawa
wanaendelea kunywa, baadaye huyo mwanadada akaondoka, na kuwaacha waoo
wakiendela kunywa.
Kesho yake hakumuona huyo binti hadi anaondokahapo Makaoni.
*********
Baada ya ushawishi mkubwa huyu manamama akakubali kutoa
ushirikiano, na waaksafiri hadi makaoni na huko ukweli ukagundulikana kumbe mauaji
yalipangwa na rafiki wa huyo marehemu, kwasaabbu ya wivu wa kimapenzi
akishirikiana na kundi la adui wa muhehimiwa.
Ilikuja kugundulika kuwa bastola iliyotumika ilikuwa
ikimilikiwa na mwenye hiyo hoteli. Hoteli hiyo ilikuwa na vyombo vya kunasa
matukio yanatokea ndani ya vyumba, na ilipofuatiliwa ikagundulikana kuwa mwanamke aliyefanya mauaji hayo, alikuwa
mpenzi wa mwanzo wa muheshimiwa, lakini hawakudumu naye, baada ya kutokea huyo
marehemu.
Mwanamke huyu alikuja kukutana baadaye na adui wa
muhehimiwa, ambaye alikuwa katika mipango ya kumfuatilia muheshimiwa, wakaungana,
na kwa vile walishachoka na huyo marehemu kuwa anavuja siri zao, wakaona huo
ndio wakati muafaka.
Walichofanya ni kumtumia huyo mwanadada ambaye alikuwa mtu
wa karibu wa mwenye hoteli hiyo kwa upande wa usalama, na akaweza kuiba bastola
ya tajiri wa hiyo hoteli, na siku hiyo ya tukio, mwenye hoteli alikuwa kasafiri
nje ya nchi.
Yule mwanamke kwa vile alikuwa upande wa usalama na anajua
siri zote za hiyo hoteli, na mitambo inavyovyofanya kazi, na siku hiyo akaingia
kwenye hiyo mitambo, na kufuatilia matukio yote hadi alipopata nafasi hiyo
akaitumia. Alichofanya yeye ni kukaa kwenye ile mitambo akawa anamuelekeza mtu , kutoka kwenye kundi la maadui wa
muheshimiwa ambaye, alitumwa kwenda kumaliza kazi.
Siku mwenye hoteli hiyo aliporudi, akakuta mitambo hiyo
haifani kazi, alipoita fundi na kuangalia tatizo limetokea wapi, ndipo
wakagundua kuwa kuna mtu aliiharibu, na mtu wa mwisho kuonekana ikawa ndio huyo
muuaji aliyetumwa na maadui wa muheshimiwa. Ilionyesha dhahiri akiwa kashika
bastola akimlenga huyo mwanamke. Wakakamatwa wote, na baada ya kubwa wakakiri
na kusema kila jambo.
Mambo hayo yalipogundulikana na kufika kwa adui wa
muhehimiwa, aalijaribu kutumia pesa zake kuhonga, lakini haikuwezekana, akazidi
kujichimbia kaburi. Na, siri nyingi za huyu adui wa muheshimiwa zikavuja, wengi
wa marafiki zake wakamsaliti, kwani walishafikia sehemu hawaelewani tena, na alipogundua kuwa mmoja
wa watu waliokuwa wakimfuatilia ni mke wake, hakuamini, mwili ukaanza kuishiwa
nguvu, jasho na moyo kwenda mbio
Katika uchunguzi wa kiserikali iligundulikana kuwa huyo
jamaa ana matatizo mengi kazini na uchunguzi ukabaini kuwa utendaji wake mbovu
umeiingiza serikali hasara nyingi kwenye kitengo chake, kwa kukwepesha makapuni
mengi kutokulipa kodi, kwa masilahi yake binafsi. Hayo yalipowekwa wazi na ushaidi wa kutosha
kutolewa, jamaa akafikishwa mahakamani.
Ikabidi afilisiwe na akaunti zake, ambazo nyingi
alizifungulia nchi za nje, zikafungwa, …jamaa kuona hivyo akajaribu kutoroka
nchini, lakini akabambwa uwanja wa ndege, akiwa kajbadili sura, kuona maji
yamefika shingoni, shinikizo la damu
likapanda, na kiharusi juu. Masikini yale yale yaliyowapata wahasimu wake
yakamgeukia na yeye…mbio hadi ICU.
Mwisho.
NB: Imebidi nifanye hivyo, ….kwa kujaribu kukifupisha hiki kisa,ili tuone nini kilitokea kwa jamaa hawa, natumai ujumbe umefika, kama kuna maoni, ushauri, naomba tuambizane,
na mungu akipenda tutaanza kisa kingine, …
WAZO LA LEO:
Tusipende kutendeana ubaya, kwasababu za kiwivu na chuki binafsi, tujue zamb za
ubaya zitalipwa hapahapa duniani, kwani mbio za sakafuni huishiwa wapi? Naombeni
mnijibu, hata kwa kimiya kimiya sio mbaya ….
Ni mimi:
emu-three
4 comments :
JAMANI, KISA HIKI CHA MWISHO M3 UMENIACHA NJIA PANDA, SIJAKIELEWA VIZURI.
Umekisoma kisa chote toka mwanzo? hebu kisome tena utakielewa vyema, najua nimekifupisha tofauti na utaratibu wangu, lkn sina jinsi. Mambo yapo juu ya uwezo wangu!
Pamoja sana jirani.
Much informative and useful article… I like it personally…
Welcome to my site [url=http://www.about-dogs.zoomshare.com/]www.about-dogs.zoomshare.com[/url].
Post a Comment