Mbio zangu za kisiasa naona ndio zimeishia hapa, maana kama unavyoniona hapa nipo kitandani,
sina hata uwezo wa kusimama jukwaani, niachopigania sasa ni afya yangu, lakini
nitapigaia kwa mikono mitupu, …ndio hapo hapo nazidi kujiumiza, maana kila kitu
nilishakiingiza kwenye mambo ya kisaisa, nikitarajia nitashinda, lakini nianavyo
sasa hizi zimekuwa ni mbio za sakafuni ambazo mwisho wake umeishia hapa
kitandani, sasa hapa nategemea miujiza ya mugu tu..’akasema rafiki yangu kwa
uchungu, huku akiagalia mkono wagu ambao ulikuwa hauna nguvu.
‘Usikate tamaa rafiki yangu, kuumwa sio mwisho wa kuishi,
utapona na unaweza ukaingia jukwaani tena, hayo yote ni majaribio ya kimaisha’nikampa
moyo.
‘Hiyo ni kupeana moyo, kiuzoefu, uapokumbwa na maradhi kama
haya, uwezo unapungua kwa kiasi kikubwa, na wengi hawadumu, nimewaona, na ni
bora ujuachie, …mimi naona niwaachie hawo wezangu ambao wanajiona wana pesa,
kwani kwao pesa sio tatizo’akasema na kukunja uso.
‘Lakini hebu niambie, kwanini ukajiingiza katika mambo
mengine ambayo ulijua kabisa yatakuharibia kisiasa?’ nikamuuliza.
‘Unapokuwa na wenzako na katika mjumuiko wa watu, mara nyingi akili
yako inatekwa na yale yaliyopo, huwezi ukajitenga, na mara nyingi hufikirii
upande mwingine wa shilingi, kwani
unajiuliza mbona wenzako wanafanya ,na baya zaidi ni pale yule ambaye
ulitegemea ndiye muongozaji wako, ndiye anayekushwishi ufanye hivyo. Sikujua
mazara yake yatakuja kuwa hivi. Kwa ujumla nilijiisahau kuwa humo humo kuna
ambao hawakutakii mema, cha ajabu ni kuwa hawo watu ni miongoni mwa wenzako’akasema.
‘Kwahiyo kwa ujumla unataka kusema kuwa umeshindwa, na
umeshajitoa kama alivyokuamrisha huyo adui yako?’ nikamuuliza.
‘Sio kwasababu yake, unaweza uaksema hivyo, kwani hata hivyo,
sina jinsi imebidi, kwani iabidi nijitoe, maana wenzangu huko walipofikia ni
kubaya, …kama wanafikia kutoa kafara za roho za watu kwa ajili ya mambo haya ya
kupita tu, basi,bora mimi nijitoe tu’akasema na mimi nikamwangalia kwa makni nikijiuliza
anasema hivyo kwa sababu ya afya yake au kuna jambo jingine.
‘Ndugu yangu nimepatwa na mitihani mingi sana katika uwanja
huu wa siasa, na sikutegema kuwa leo ningekuwa hapa kitandani, lakini huenda
yote yametokea ili niweze kujifunza ukweli, nanikweli nimejifunza, kuwa
binadamu yupo tayari kuua ili tu ajinufaishe nafasi yake, marafiki , ndugu,
wanafikia hatua hawajali tena urafiki wao au udugu wao, inasikitisha sana,
….’akasita kusema zaidi.
‘Hapo kuna Jambo unanificha, kwani kuna nini kilitokea?’
nikamuuliza.
‘Kuna mauaji yalitokea, na hadi sasa sijamgundua ni nani
hasa aliyefanya hivyo, ila kwa juu, juu ninaweza kusema ni huyo adui yangu
ambaye alifanya mpango huo ili iwe kashfa kwangu, labda ni yeye, lakii
alivyonipigia simu anadai kuwa sio yeye, ila anataka kutumia nafsii hiyo
kuniangamiza kama sitakubali matakwa yake, na wenzake’akasema.
‘Kwahiyo ina maana sio wewe uliyeua, na kwa ujumla hata
polisi hawakuwahi kukushikilia wewe kama mshukiwa?’ akaulizwa.
‘Sijaua, na kushukiwa kupo, ila ndio hivyo mchezo ulichezwa
na mwisho wa siku mambo yakazimwa kinamna,lakini kesi ya kushukiwa bado ipo,
imetulizwa kinamna, na hapa ninavyosema hivi
huenda nikipona hapa naweza kufikishwa mahakamani, kama wenzangu wataamua
kulifuatilia hili swala kama walivyodai’akasema.
‘Kwanini hukufanya uchunguzi binafsi ukagundua I nani yupo
nyuma ya jambo hili, wewe mwenyewe?’akaulizwa.
`Niliamua kufanya hivyo, lakini mwisho wa siku nikajikuta
nagundua mambo mengine ambayo hadi sasa siyaamini, na hata huyu adui yangu
alinikanya kuwa kama nataka kujiletea matatizo zaidi niendelee na uchunguzi
wangu,kwani anadai kuwanitagundua mabaya zaidi ya hayo, sikumuelewa kabisa.
‘Hayo si maneni ya vitisho tu, ungelifanya uchunguzi bila
hata ya yeye kujua kwani haiwezekani?’nikamuuliza.
‘Ndivyo nilivyofanya, lakini utafanyaje uchunguzi wewe mwenyewe
, kama unavyojua ili ujue ni nini kilitokea lazima kuwahoji watu, na hawo
utakaowahoji wanayafikisha hayo maneno kwa jamaa, kwani yeye kwa ajili ya pesa
zake anajulikana sana, kwahiyo imekuwa ni ngumu, na wenzangu walinishauri
nisihangaike na huo uchunguzi, wao wanajua nini la kufanya.
‘Kwani ilikuwaje?’ nikaumuuliza, na yeye akainua kichwa na
kuangalia huku na kule kuhakikisha kuwa hakuna anayetusikiliza , na alipoona
hakuna mtu, akasema;
Siku ile baada ya kutoka kwenye kikao, kama kawaida yetu,
huwa tunakunywa kidogo, na huwezi kunywa peke yako, tukawa na akina dada
wakutuliwaza, maana kazi zetu hizi zina mawazo sana, sasa inabidi unywe kidogo,
na ukinywa, unatakiwa upate mtu wa kukuliwaza,ndivyo hata wenzangu
walivyonishauri, mwazoi nilipinga sana hili swala, lakini ibilisi wa mtu ni mtu
…’akasema na kutulia.
Sikutaka kumuuliza kuwa `hiyo ni lazima au ni tabia tu’
nikanyamaza ni mpe muda wa kujielezea.
‘Tabia hiyo sikuipenda, lakini ilinibidi nijiunge na kundi,
maana nisingejitenga na wenzangu, nilishawishiwa, nikashawishika, nikaonja
asali, na kweli muonja asali haonji mara moja nikawa nami nimelowea, nikawa
kwenye mkumbo.’akasema.
`Basi ilikuwa kila baada ya kikao, ukishakunjwa, na …ni
lazima utafute wa kukuliwaza,labda kiuashauri kwa wenzangu ambao watakutana na
mambo haya kama wana wake, wajitahidi kwenda na wake zao ili kupunguza hii
tabia, lakini wengi hawapendi hilo’akasema
‘Siku hiyo kama kawaida, nilimchukua bibie mmoja, ambaye nilishajenga mazoea naye,
na kweli alinivutia sana ,ukiwa naye, sio tu anakuliwaza, lakini anakupa siri
zamaisha, anakupa mawazo ambayo ukisimama kwenye jukwaa ukiongea, watu
wanakushangilia, …ana kipaji cha kuwasoma watu, na alikua akinipa siri za ndani
ambazo nilikuwa sizijui, namshukuru sana, na kama angelikuwa hai angelinisadia
sana.’akasema na kuangalia huku na kule.
‘Una maana gani kusema kama angelikuwa hai, ina maana yeye
ndiye aliyeuliwa?’ nikamuuliza.
‘Hawa washenzi wasikie hivi hivi tu, hili najua ni njama
zao, walishagundua kuwa huyo mtu wao anatoa siri badala ya kugundua kuwa huyo
mwanadada hafanyi kile walichomuagizia’akasema.
‘Ina maana alikuwa mtu wao?’ nikamuuliza, na y eye akacheka,
na kuangalia tena huku na kule,
‘Kama asingelikuwa mtu wao, sasa hivi ningelikuwa jela, ndio
maana mambo hayo waliyanyamazisha ki-aina. Na yule mwanamke alishaamua kuwa mtu
wagu, nasikitika sana, ……’akasema na kuonyesha kweli kuna jambo lililotokea
ambalo lilimuuma sana.
‘Sasa kwanini hukuwafahamisha polisi wakafuatilia kiundani?’
ikamuuuliza.
‘Kwa hali kama hiyo usingeliweza kuwaambia polisi chochote, ningejichogea
tu, a ukizingatia hali mazingira yenyewe ya siku hiyo’akasema.
‘Sasa hebu niambie, huyo mwanamke aliuliwa au yeye ndiye
aliyehusika katika kufaya mauaji?’nikamuuliza.
‘Mimi nilikuwa naoga, baada ya kujaribu kuwasiliana na mke
wangu nyumbani bila majibu, nikawa sina raha, hata usingizi ukawa haupatikani,
basi, nikamuomba mwenzangu, huyo mwanadada iliyekuwa kuwa sijisikii vyema ngoja
nijimwagie maji kidogo, wakati naoga nikasikia ndio nikasikia mlio wa bunduki,
natoka kule bafuni kuangalia kitandani, …oh, basi tena.
‘Basi tena vipi?’ nikamuuliza.
‘We acha tu
NB: Mambo bado magumu, mengi yapo juu ya uwezo wangu, lakii
itajitahidi nikimalize hiki kisa hata kwa ufupi tu.
WAZO LA LEO: Kuua
ni zambi zambi kubwa sana, sasa hivi watu wanaona ni rahisi tu kuua, utu
umetoweka, ubinadamu haupo tena. Jamani hebu tujiulize tuauwezo gani wa kuumba,
a kuweka rohoo ya mtu, hadi tufikie kuitoahiyo roho ya mt, asiye a hatia, je utakuja kusema nini mbele ya
muumba…,?
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Kaka usivunjike moyo, kaza buti, mungu yupo na wenye kusubiri, na wakatenda mema. Hii ni kazi ya mkono wako, ina baraka,utafanikiwa tu.
Ndugu wa mimi, Kazi nzuri sana,MUNGU yu pamoja yote ni Mapito.kila kitu kitakwenda sawa.MUNGU anatosha.
Pamoja Daima.....
Post a Comment