Kuna siku nilipita mahali nikakuta mti ambao kwa wanaoujua
historia yake, wanasema ni mti wa zamani sana, hata ukiuangalia, utakuwa mizizi
yake ni mikubwa na shina lake ni imara. Sio huo miti tu, kuna yumba za kihistoria,
kuna huko Bagamoyo na Kilwa, utakuta nyumba kama hizo ambazo zilijengwa miaka
mingi nyuma na bado zipo, ingawaje hatutaki kuziweka katika hali ya uimara
zaidi tena
Vitu kama hivyo vya
kihistoria wanatakiwa watu ambao ni wataalamu wa ujenzi, wakaziboresha katika
mfumo wake ule ule, uliokuwepo, bila kuharibu kitu,hiyo inawezekana, niliona
wenzetu wa Ujerumani, wakijereshea nyumba zao za asili,kama zilivyokuwepo
awali. Na huoni tofauti, au tunashindwa, labda mapaka kuwepo wafadhili,sijui!
Lakini haya yote hayakuwezekana kama kulikuwa hakuna `msingi’
imara wa majengo hayo, au mizizi madhubuti wa miti hiyi. Ukianganlia mifano
hiyo, utaona haina tofauti na maendeleo ya ujenzi, maendeleo ya kimaisha mengi
hutegemea misingi imara iliyowekwa kabla.Kama hakuna misingi imara, hatutaweze
kuendeleza hicho kilichopo, tutakuwa kila siku tunaanza moja.
Tulishuhudia mejengoya gorofa yakidondoka hapa nchini siku
za karibuni, chanzo kilikuwa ni nini? Ni kutokana na kutokuwepo na msingi
imara, ambayoo mtaalamu alitakiwa kuuweka, huenda mtalaamu alitoa tasmiini,
nini kinatakiwa, lakini watelekezaji wakachakachua, nini kilitokea,tuliona
wenyewe.
Nalizungumza hili nikijua kuwa leo watoto wetu wa darasa la
saba wanafanya mitihani, mitihani ya `shule za msingi’ hata jina lenyewe
linajieleza kuwa ni elimu ya msingi. Hii ilionyesha jinsi gani wenzetu
walivyolifikiria hilo kwa makini. Kwani wenzetu waliobuni jina hili waliona
mbali, wakijua kuwa huo ndio msingi wa elimu ya mtoto. Hapo ndipo kulitakiwa
nguvu zote zielekezwe, ujuzi wa hali ya juu utumike, na ili msingi huo uwe
imara, walihitajika `mainjinia’ wa hali ya juu wa kuwekeza msingi huo.
Kwasababu hapo ndio
msingi wa mtoto, ambaye tunatarajia atapanda kama gorofa linavypanda kielimu
had kufika ngazi za juu. Sasa kama huyu mtoto hakujengwa vyema kielimu, kwa
kuwekewa msingi imara, kweli ataweza
kufika huko juu tunapotarajia . Huyu ndiye mtalaamu tunayemtegemea na hapa ndio
msingi wake ulipoanzia, je huyu kweli imwekwa kitaalamu(kitaaluma)
Kwetu sisi msingi wa elimu hatukuuchukulia kama msingi wa
nyumba, tuliona ni sehemu tu ya kujifunza kusoma na kuandika, ambapo mtu wa
kawaida anaweza akasimamia. Ndio maana walimu wake tunachukua wale ambao
hawakufanya vizuri sana kwenye masomo yao, kwani tunachofanya sisi wale
waliofanya vyema kwenye mitahani yao, ndio wanakwenda elimu ya juu. Huo ndio
msingi wa nyumba yetu, ambayo tutarajia
iwe gorofa.
Angalia sasa jinsi mitaala inavyobadilishwa kila siku, ina
maana tangu tupate uhuru hatujaweza kuwa ni mitaala thabiti, hatuna wataalamu
walioweza kuweka mitaala imara ambayo tungeliweza kujivuna kuwa hii ndio
mitaala itakayo jenga nyumba imara ya gorofa. Nasita hata kusema kuwa hapo sasa
pamekuwa ni sehemu ya kujaribia kama ule usemi wa kiongozi wetu wa kichwa cha
mwendawazimu, kila mtu akija anakuja na ufundi wake, unaujaribu labda kama
utafaa. Sio nalaumu, lakni mimi nashindwa tu kuelewa mpaka lini!
Sasa hivi watoto wetu hawo wa shule za msingi, waliingia
kwenye mitihani yao, na utaratibu mwingine mpya, na huo utaratibu tunaujaribu
kama utafaa, baada ya miaka ya mtu mzima wa uhutu bado tunajaribisha, haya
ngoja tuweke huo msingi wa majaribio wagorofaletu la elimu.
Wazazi wenye uchungu na vizazi vyao, wamelalamika na
utaratibu huoo mpya kwasababu,umeletwa muda mfupi kabla ya kufanya mitihani,
hata kama wamejaribiwa, lakini tukumbuke huo ndiomsingi wa elimu, na hilo
tunalotaka kufanya halihitaji majaribio,kwa unyetiulivyo, sijui kama hija yangu
mnaielewa.i lakini ndio hivyo,hatujui ni kwanini ukaletwa huo utaratibu mpya,na
kwanini ukaletwa muda mfupi tu wakati
watoto wanakaribia kufanya mitihani.
Tunaomba ili tufike mbali,sehemu hii tuwekee `mainjinia ‘
ambao wana elimu ya kutosha , wana uchungu na watoto wetu, ili kweli tuweze kuweka
misingi imara, kama kweli tuna nia njema na kizazi chetu kijacha, kama kweli
tuna nia njema ya kuleta maendeleo ya nchi yetu.
Vinginevyo tutaishia kila siku kuanzisha msingi mipya,wakati
wenzetu wanaendeleza magorofa yao. Na
kinachofanyika sasa sio kuweka misingi mipya mimi naona kama vile tunaweka miti
pembeni ili nyumba hiyo, isije ikaanguka!Kwani elimu ya miaka saba
ingelijulikana matunda yake hata kabla ya huo mtihani, tujue mtihani sio tija,
cha lazima ni ile miaka saba iliwekeza nini. Tusije tukawafunza watoto wetu
kucheza kamari ya kubuni, na wenye bahati wakazipatia hizo namba!
Kwa uoni wangu mdogo, hili halitawezekana kama sehemu hiyo
haitafanyiwa utafiti wa kina na kuweka watu wanastahili, wenye elimu ya
`uinjinia’ na pia wawe na uchungu na
watoto wetu. Sehemu hiyo isafishwe kabisa, na kuweka watu makini, wenye uchungu
na watoto wetu.
Tujua kuwa seehmu kubwa ya elimu hiyo ya msingi ambayo haina
matokea mazuri, ni kwa watoto wetu wanaosomea kweney mavumbi, wenzetu watoto
wao wanapelekwa shule za kimataifa je, sisi wakulima, sisi walalahoi, watoto
wetu watakwenda wapi, baaada ya kuwekewa msingi huo wa vijumba vibovuvibovu, ambavyo
kila baada ya mwaka, tunawekewa viraka na miti pembeni ili visianguke.
Wananchi tuamuke na tuhoji,…hili ni letu, na tusipohoji na
kufuatilia mwisho wa siku inakula kwetu, hili ni jukumu letu sote, tusilale na
kuiachia serikali, kwani serikali ni sisi, na hao waliowekwa hapo kusimamia elimu, tunawalipa sisi weyewe kwa kodi zetu, na ili wawajibike vyema tusaidiane nao, na moja ya msaada mkubwa ni kuhoji, kuuliza ili kujua, sio kukaa kimiya na kulalamika pembeini.
Tumuombe mungu awajalie watoto wetu wafanye mitIhani yao
vyema kwa amani na usalama. Kwani wao hawajui ni nini kinachoendelea, matarajio
yao ni kwenda mbali, na kwenda mbali kwako ni elimu hiyo waliyoipata kama
msingi wao. Kama kwelii mabadliko yaliyowekwa yana nia njema, twakuomba mungu
uyabariki, lakini kama yana nia ambayo haitasaidia baadaye, mwenyezimungu
tunaweka kilio chetu mbele yako. Twakuomba utusaidie kwa maslahi ya vizazi
vyetu na taifa letu kwa ujumla . AMIN
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Haya ni muhimu sana kwa mkuu wetu, kuhakikisha hicho kitendo cha wizara, kwanza kinasafishwa, na pili kiwekwe watu wanaostahili.
Tusiangalie uzoefu tu wa mtu, lakini ni vyema tukaangalia`utaalamu'wenye tija, utaifa na uadilifu. Mtu akivurunda tumuondoe.
Lingine kwa maoni yangu ni kuwa tusiweke mtihani wa mwisho kuwa ndio kila kitu kwa mtoto. Mtoto apimwe kila hatua na mtihani wa mwisho uwe ni sehemu ndogo tu ya kuhitimisha.
Ninashangaa sana eti hata hesabu inakuwa ni ya kuchagua, hamjui kuna watu wanabahati ya kukisia, hivi huyu aliyefanya hivyo hajui hesabu nini, maana yeye anafikiri hesabu unachagua kama masomo mengine. Sielewi.
M3 naomba maoni yangu haya uyawasilishe, kwani mimi ni mzazi na nina uchungu na kizazi hiki na nchi yangu.
Post a Comment