‘Hebu niamie ulijuaje kuwa muuaji ni nani kati ya hawo
wawili unaowahisi…wawili eeh, maana wengine hawana sifa hizo….?’ nikamuuliza
wakili mwanadada akiwa kachoka, baada ya kutokea mahakamani. Kesi hii ilibidi ifunguliwe baada ya nesi
kugoma kutoa maelezo yake siku ile.
‘Mimi nimeshasemasitaongea lolote,ninachotaka ni haki
itendeke ,maana nimeshagundua ujanja wa wakili mwanadada, nia na lengolake ni
kutuchimba ili mwisho wa siku apate anachotaka, sasa mimi nimeshituka, na hali
ilivyo hapa haki haitatendeka….’akasema nesi baada ya kushikiliwa na polisi.
‘Haki gani unayoitaka, maana hapa ni mazungumzo tu,
hatujamnyoseha mtu kidole…’akasema hakimu.
‘Mimi sio mtoto mdogo, na msinione kuwa sina akili ya kuwaza
mbali, hali ilivyo hapa inaashiriakuwakuna kitu kinatafutwa, na nahisi ukweli
utajificha na mnataka kunikamatisha mimi hayo mauaji, ili munilazimishe
nikubali …hapana, maana kesi ipo wazi, mimi nawashangaa, hawo akina dada wawili
wana sababu zote, na kauli yao, vietndo vyao,…mnashindwa kuwahoji vyema mnaning’angania
mimi….’akasema kwa hasira.
‘Kila mtu alipewa nafasi yake, nab ado tulikuwa tunaendelea,
hiyoisikupe shida, na unaweza ukatusaidia kuwauliza maswali, huenda tukajifunza
kitu kutoka kwako….’akasema wakili mwanadada.
‘Mimi sio kazi yangu, ila kamaingelikuwa mimi
nisingeliwaachia hawo akina dada kirahisi hivyo, waan kila sababu ya kuwa ndio
wauawaji…’akasema.
‘Kwa vipi hebu tuambie wewe….?’ Akaulizwa.
‘Kwa vipi unaniuliza
mimi kwa vipi ,wakati wamejieelzea wenyewe, walichukua bunduki ambayo ndioyo
iliyotumika kumuua Kimwana, hamjasema kuwa risasi iliyotoka hapo ndio iliyomuua
Kimwana?’ akauliza.
‘Sawa ndio iliyomuua Kimwana, lakini uliwasikia wakisema sio
wao waliofyatua hiyo risasi, walikimbia na wakiwa mafichoni, mtu mwingine akaja
akaitumia hiyo bunduki…’akaseam wakili mwanadada.
‘Toka lini muuaji akakubali kuwa kaua, hata kamakweli kaua,
sio rahisi kukubali moja moja kwa moja, maana ukikubali hukumu inatolewa mara
moja, na hukumu yake haina mashamaha, ni kuwa umeua kwa kukusudia,…sasa ulitarajia
wao wakubali kirahisi hivyo…’akasema nesi.
‘Ndio maana hata wewe hukubali kirahisi ….’akasema wakili
mwanadada.
‘Nimesema ndio maana wao wanajaribu kupinga, na kupindisha
maneno, lakini vielelezo, kama bunduki, kauli yao kuwa walifika na wakaielekeza
hiyo bunduki kumlenga Kimwana,….sasa hapo mnataka nini, ‘akasema huku
akitabasamu.
‘Unaweza ukalnga lakini usifyatue risasi, ‘akasema wakili
mwanadada.
‘Naona uan maslahi na hawo watu, wewe sasa nakuona ni wakili
wao, unawalinda, na ndio maana naona hii ni ksei ya ngedeer imepelekewa nyani,
sioni kama kuna uhalalai hapa, naomba kwanza nimuone wakili wangu, na pili hii
kesi ipelekeni mahakamani maana njua huko haki itatendeka.’akasema na kutulia.
‘Tukimshitaki nani, kama muuaji?’akaulizwa.
‘Hapa mumemshitaki nani, ninavyoona hapa mimi mumenishikilia
kama mkosaji, na ndio maana nataka tuipeleke hii kesi mahakamani, na kama
ikithibitika kuwa mimi sio mkosaji kesi itawageukia, ni liazima nikushitaki
wewe kwa kunichafulia jina langu….’akasema kwa hasira.
‘Lakini hakuna aliayekushitaki wewe, hakuna aliyekunyoshea
kidoela wewe hapa tunaongea, tuanasikiliza maelezo ambayo yatatusaidi kujau
ukweli wa hikikifo, bado hatujamnyoshea mtu kidole…’akasema hakimu.
‘Na pia kwenye hiyo kesi, naomna awepo hakimu mwingine….’akasema
huku akimwangalia yule hakimu kwa macho yaliyojaa chuki.
‘Hili litafanyika usiwe na shaka kabisa,….ila kwanza
tumalize mazungumzo yetu hapa ndani…’akasema hakimu.
‘Mimi msimamo wangu ni ule ule kuwa sitaongea lolote mpaka
wakili wangu awepo…’akasema.
‘Basi mimi ninatia kibali kuwa ukamatwe , hadi hapo kesho
tutakaposikiliza kesi yako,na mimi sio hakimu nitakayesikiliza kesi yenu, hilo
nakuthibitishia….’akasema hakimu.
‘Kukamatwa, kwakosa gani?’ akauliza kwa hamaki.
‘Atakayekukamata atakuambia kwanini unakamatwa, kwa hivi
sasa upo chini ya ulinzi, na wakili mkuu, mke wako na rafiki yake, Sokoti na
kundi lake, wote mpo chini ya ulinzi…’akasema askari ambaye alifika, muda huo
huo akiwa kashikilia kibali cha kuwakamata hao aliowataja.
Kesi ikafunguliwa, na kesho yake wakafikishwa mahakamani.
*********
Wakili mwanadada
akiwa kakaa kwenye sofa lake aliegemeza kichwa chake na akawa kama anawaza
jambo , …baadaye akasema;
‘Ukiwa katika kazi hii ya uwakili, au kazi nyingine yoyote,
ambayo unaifanya kama wito, yaani unahisi ile kazi kama sehemu yako ya maisha, na
unaipenda kazi yako bilkujali maslahi yake….mambo mengine yanakuja kinamna ya kipekee
kabisa, lakini hata hivyo, kilichosaidia sana, ni yale mahojiano tuliyoyafanya,
…nilishagundua kuwa kwa njia ya mahojiano ndipo utagundua udhaifu wa kila mtu, …’akasema na kutulia.
‘Kwahiyo kumbe lengo lako lilikuwasio kusaidia bali ni
kuchimba watu ili ujueukweli?’ nikamuuliza.
‘Lengolangu toka awali lilikuwa kusaidia, na hata
nilipomuona yule hakimu siku nilipomuomba hivyo,nilimuelezea wazi kuwa kuna
watu wamejikuta kwenye matatizo,ambayo sio kusudio lao,nilimuomba kuwa
awasilikilze maana wao wenyewe wamekubali kukiri makosa yao, na kama kuna
uawekano kesi hiii iishie kwakushikana mikono, maana kosa lilitokea hadi
kufikia mauji ni kwa bahati mbaya…’akasema wakili mwanadada.
‘Hakimu akakubali kwa maelezo yak ohayo?’nikamuuliza.
‘Hkukubali kabisa, hasa nilipomwambi ainahusiana namauaji ya
Kimwana, ila ilibid nimshawishi sana kuwa kama hatasikiliza maneno ya hawo
wahusika, kesi kama hiyo inaweza ikachukua muda mrefu na mwisho wasiku hata
muuaji hataweza kupatikana,…’akasema.
‘Hakimu akasemaje?’ nikamuuliza.
‘Baadaye sana akakubali nakusema yeye atakuja kama
msikilizaji tu,hataweza kutoa maamuzii yoyote, na hata baada ya kusyasikiliza
hayo maelezoya mwanzo hatakubali kuiskiliza hiyo kesi tena, ataomba hakimu
mwingine aisikilize, ….’akasema wakili mwanadada.
‘Kwanini sasa, wakati yeye ndiye uliyemuoma asikilize
maelezo na yeye ndiye atjua ukweli upo wapi?’nikauliza kwa kushangaa.
‘Nilimuambia kwakusikilizamalezo yao, tunaweza kufuchua
kilekilichojificha, na kama kuna uwezekano wa kusamehe, baadhi ya watu ambao
walijikuta wakiingizwa kwenye kesi hiyo bila kujijua anaweza yeye kama hakimu
akatoa shauri hilo kwa hakimu mwenzake…’akasema wakili mwanadada.
‘Lakini huoni hapo ni kama unaingilia mambo ya hakimu?’
nikamuuliza.
‘Mimi ni wakili,na mtetezi wa watu,na mimi ninatetea haki,
ninapoonakuwa kuna watu wanaonewa, na hawana hatia, nitatumia kila njia
kuhakikisha haki inatendeka, na ndivyo nilivyofanya na nitakavyofanya,
kuhakikisha kuwa haki inatendeka, na wale wasio na hatia wanapewahaki yao….’akasema.
‘Mimi bado sijaelewa maana hata huko mahakamani sijaweza kufika,
ilikuwaje leo?’ nikamuuliza.
‘Leo hakimu mwenyewe aliniita baada ya kusikilizwa kesi ya
leo, akanishika mkono kwa kunipongeza, …sikuamini, maana ni muda sasa tumekuwa
tukisumbuliwa na hizi kesi, na mwisho wa siku tunaondoka hakimu akiwa
kakasirika, kuwa tunamletea kesi zisizokamilika lakini safari hii alinipa sifa
nyingi….
‘Kwahiyo kesi imekwisha na muuaji keshajulikana ?’
nikamuuliza.
‘Kesi haijaishha, ila muuaji keshajulikana , mwisho wa siku alikuja
kukubali mwenyewe..’akasema.
‘Mimi bado sijamjua ni yupi hasa ambaye kaja kukubali
mwenywe kuwa ndiye aliyemuua Kimwana, maana wameshikwa wengi kuhusiana na hiyo
kesi, na ukasema wawili ndio wahusika wakuu,…na leo unasema huyo mmoja
keshakubali kuwa yeye ndiye aliyeua, ni nani na ilikuwaje?
‘Nitakuhadithia tu, usiwe na munkari, ila niligundua kuwa
mtu huwa anajishuku mwenyewe, hasa unapomwaga damu ya mtu, ile damu itakuandama
tu, na wewe mwenyewe utajikuta nafsini ukijaulumu, kwani binadamu sio mnyama,
hajaumbwa kuwa na roho ya kinyama, ila hasira zinapokita kwenye nafsi, pake ile
hali ya kibinadamu inaondoka kwa muda….’akatulia kama anawaza jambo .
‘Kwahi unataka kusema kuwa muuaji aliua kwasababu ya hasira,
….mbona hujaniambia ni nani, maana hamu yangu hapa ni kumjua huyo muuaji…’nikasema
kwa hamasa.
‘Na hilo ndio kosa,ambalo hata wenzetu wa usalama
wanalifanya, kukimbilia kumshuku mtu kuwa yeye ndiye kafanya, yeye ndiye kaua,….hitimisho
mara nyingi sio njia sahihi, njia sahihi ni kujua chanzo cha jambo, …kiini cha
jambo, sababu ya jambo, na ukilijua hilo, hutakuwa an shaka na hitimisho lako…sijui
hapo unanielewa…?’ akaniangalia kwa makini.
‘Lakini hayo tulishayajua , …na tukajua sifa za muuaji wa
Kimwana zipoje, na nikiangalia kwa makini, kwawale wahusika pale, yupo Sokoti,
maana yeye ni kiongozi na ana mamlaka, nlakini nikagundua kuwa hana shabaha,…kwahiyo
yeye namuondoa, nikamchukua, …..eeh, wakili mkuu, nikagundua kuwa licha ya kuwa
ana shabaha, ana sababu , lakini hana mamlaka kwenye hilo kundi…..haya hwa
akina dada wawili, wote wana shabaha, wanasababu na wana ….ndio wana amri,
wangelwieza kuamrisha…..lakini, walikataa, sasa huyu nesi, …..ilikuwaje kwake?’
‘Ndio maana nikakuambia usikimbilie kuataka kunjau huyo mtu,
hebu jua kiini cha tukio zima, huyo mtu anaweza akawa na shabaha, anaweza akawa
na amri, anaweza akawa na sifa nyingine, lakini kwanini ilifikia hadi huko,…ni
wivu wa mapenzi,…au sio’akasema wakili mwanadada.
‘Ndio kama ni wivu wa mapenzi karibu wote wanao huo wivu, na
hasa hawa akina dada wawili ambao walikuwa na haki, hasa mke wa wakili mkuu,
yeye mume wake alichukuliwa na Kimwana…’akasema.
‘Umesahau kuwa hata wewe ulichukuliwa na Kimwana…’akasema
huku akicheka.
‘Ndio nilichukuliwa na Kimwana, lakini nani kati ya wale
ambaye atanionea wivu mimi, mke wa wakili mkuu, sina mahusiano naye, rafiki
yake, mapaka sasa sijamjua, nesi, ndio kasema alinipenda,lakini sikuwahi kuwa
na mahusiano na yeye….’akasema.
‘Nesi alikupenda sana, nay eye akakutana na mtu aliyekupenda
zaidi, kwahiyo akaona njia ya kukupata wewe ni kuua njiwa wawili kwa jiwe moja,
….’akasema na kuniangalia kwa makini.
‘Kwa vipi, kama alinipenda, lakini mimi sijawahi kuonegea
naye, na wala sina hisia naye kabisa,….hata
kama ni mzuri, lakini hajaigusa nafsi yangu, hawezi akachukua maamuzi yake, eti
kwasababu ya wivu, sitamuelewa hata siku moja…’nikasema.
‘Mapenzi ni kitu cha ajabu sana, nina uhakika kama ungelikaa
na huyo dada siku tatu tu ungeishia kumpenda na kusema huyu ndiye niliyekuwa
nikimataka, ..kwasababuu kwanza yeye ni mjanja, pili umri umekwenda na
anahitaji sana mtu wa kuishi naye na anayajua mapenzi, …na anawajau wanume,
kilichotakiwa ni kupata muda wa kukaa na wewe, hicho ndicho alichokuwa
akikitafuta….’akasema.
‘Mhh, sijui na wala sina uhakika na hilo, ….’nikasema huku
nikijaribu kuivuta sura ya huyo nesi, kuona kama kweli ananiingia kwenye nafsi
yangu hadi nije nimpende ,sikuweza kuingiwa na hisia zozote nikaema;
‘Hapana sina mvuto naye, wa kihivyo, lakini siwezi jua maana
sijawahi kukaa naye kwa karibu na nafsi yangu ikatulia kwa ajili yake,hata
hivyo, kwanini yeye umshikilie kama mhusika mkuu, na inavyojulikana yeye
aliachwa hospitalini,na wakili mkuu kathibitisha hilo,….’nikasema.
‘Kesho fika mahakamani,utasikia mwenyewe akitoa kauli yake
ni kwanini ilifikia hatua hiyo, …’akasema wakili mwanadada.
‘Ina maana kumbe hajakubali kidhahiri..!?’ nikauliza kwa
mshangao.
‘Keshoo hiyo, nakuhakikishai kila kitu kitawekwa hadharani,….’akasema
na kuinuka, hasa pale alipoaangalia saa yake, huwa huyu dada anajali sana muda
na mimi alishaniweka njia panda,nilikwa na maswali mengi ya kumuuliza hasa
kuhusu huyo rafiki wa mke wa wakili mkuu.
‘Sasa mbona unaniacha njia panda,vipi kuhusu rafiki wa mke
wa wakili mkuu ,ni nani,unajue kila maranamuwaza yeye, sijui kwanini,inafiki
hatua naanza kumhisi kuwa anaweza kuwa mtu ninayemjua?’ nikamuuliza.
‘Kama mpaka sasa hujamjua, sitaweza kukusaidia kwa hilo,
nakumbuka siku ile ulitaka nikukutanishe na yeye muongee,ukashindwa, na sasa
bado unamuwaza, unataka nikusaidieje , nikakutongozee, ….’akasema na kucheka.
‘Sio hivyo,nia na lengo langu ni kutaka kumjua ni nani’nikasema
huku nikigeuka pembeni ni kikwepa kumwanglia na nikaweka kidevu changu kwenye sofa
kama kujiegemeza, na huku nikiwaza mbali,nikimuwaza mwanadada, ambaye
keshaiteka nafsi yangu. Wakili mwanadada akawa ananiangalia kwa huruma, na
aliponioana nimegukia upande mwingine kama kumkwepa akasema;
‘Kumjua kuwa ni nani…..kwanini….kwanini utake kumjua yeye
peke yake….! Na unauliza kuwa yeye ni nani mbona jibu hilo lipo wazi, yeye ni
rafiki wa mke wa wakili mkuu, au jina lake unalihitaji, pale , hautukutaka
kutajana majina, mana tulikuwa na maeleo ya awali, lakini kama unahitaji jina
alke, j, basi nitakutajia….’akasema wakili mwanadada.
‘Jina lake ni nani…?’ nikauliza na kumgeukiwa kwa haraka,
nikiwa na hamasa ya kulijua hilo jina.
‘Jina lake halisi ni Tausi binti Maringo…’akasema na
kunifanya moyo wangu ushituke, kwa kulisikia hilo jina.
‘Unasema anaitwa nani?’…nikauliza kwa mshngao huku
nimesimama, nikiwa nimemkodolea macho wakili mwanadada.
‘Ukitaka zaidi kesho fika mahakamani,huenda ukapata muda wa
kuongea naye, na safari hii usiniangushe, tafadhali…mimi sikujua kuwa hata
mwanaume kiwembe kama wewe inafika mahali unajiuma uma kwa mwanamke,…hahaha,kumbe
mapenzi ni kitu cha ajabu sana,….’akasema huku akiniangalia kwa uso uliojaa
tabasamu.
‘Hilo jina nalifahamu,….mmmh, lakini,….lakini siwezi kuwa na
uhakika kuwa ni yeye au sio yeye, maana hawafanani, ….lakini mmh, sura inakuja
inatoka…au ndio maana namuwaza sana yeye, inawezakana kweli akawa ndio yeye,….lakini
mbona kabadilika kiasi hicho?’ Nikauliza huku nikiwa natembea kama vile nataka kutoka
nje.
‘Sasa unakwenda wapi, mbona hatujapanga mipangalio ya kesho?’
akaniuliza.
‘Lazima nikamuone kwanza….’nikasema
‘Ukamuone nani?’ akaniuliza.
‘Tausi binti Maringo…’nikasema.
‘Kwani unahisi ni nani huyo?’ akaniliza.
‘Siwezi kusema mpaka niongee na yeye mwenyewe niisikie kauli
yake mwenyewe,…kani dhaman yao imekubaliwa’nikasema.
‘Ndio maana nikasema kwa hali aliyo nayo leo, anahitaji
kupumzika, maana dhaman yao ilikubaliwa, niliwaacha wakimalizia mambo ya
kiofisini, nilijua watakuwa wameruhusiwa, na sina uhakika, kama …’akaantulia na
kuangalai saa yake.
‘Kama ni hivyo….ngoja nikawafuate huko huko nikuje imefikia
wapi’nikasema.
‘Utamuona tu, kamasio leo hata kesho,….lakini leo hii,
nahisi hutaweza kuongea naye vyema, maana hali aliyo nayo, baaada ya kesi ya
leo ,nakauli aliyoisikia toka kwa huyo nesi imemchanganya sana, ingawaje
alikuja kuniulizia kwanini huonekani mahakamani…kiujumla ana hamu sana ya
kukutana na wewe, safari hii kaniomba yeye mwenyewe kuwa anataka kuongea na
wewe….’akasema na kutabasamu.
‘Mbona hukuniambia..ooh, tafadhali naomba nikamuone hii leo…’nikasema
na moyoni nilishaahidi kuwa vyovyote iwavyo lazima niende nikamuone,….na mara
mlango ukagongwa, na nimuda ule ule nilikuwa nimeshafika mlangoni, nikiwa
tayari nimeshanyosha mkono kuufungaua huko mlango,
‘Karibu , fungua…’akasema wakili mwanadada.
Mlango ukafunguliwa,…na moyo wangu wangu ukalipuka paah,….mwili
ukafa ganzi, ….nikajikuta nikitoa macho bila kupepesa, …..
NB: sehemu hii nimeiandika kwa harakasana leo asubuhi, sijapata muda wa kuipitia huenda ikawa namakosa ya hapa na pale, lakini najua itaeleweka, kama kuna maksoa nifahamishe ili niyarekebishe.
Hapa nilipo ninaanza kuwaza kisa kipya, sijui kama kuna kisa tulikikatizia tukiendeleze au nitoke na kisa kingine kipya,....
WAZO LA LEO: Mara nyingi kila mtu hujiona yeye kuwa sahihi, na yeye ndiye mwenye kazi nyingi sana, yeye ndiye mwenye shida nyingi sana, yeyendiye....kuliko wengine, lakini kumbe huenda wengine ni zaidi yake.
Ni vyema tukaangalia wenzetu kuwa na wao ni banadamu kama wewe, ulicho nacho, shida uliyo nayo, na wao wanaweza kuwa kama wewe na huenda zaidi yao,..
Ni mimi:
emu-three
4 comments :
Upo mkuu?
Nipo mkuu, ila leo mambo ya foleni, jembe na yaliyo juu ya uwezo wangu nimejikuta nikishindwa kufanya lolote! Tuombe mungu, huenda wikiendi hii nikafanya kile kinachoitwa hitimisho.
Hata hivyo nahis kesho niseiku maalumu kwablog hii,...sinauhakika ngoja nichunguze!
Mimi nashauri usiandike kisa kingine chochote kirefu mpaka utoe vitabu viwili kwanza. Kwa sababu unatakiwa uwe busy na manuscript zako kuhakikisha ziko tayari kwa vitabu. Angalia jinsi ya kuandaa manuscript, andaa hizo manuscript, ukiwa tayari nitafute tupublish kitabu kimoja baada ya kingine.
Mimi najitolea kuwa "Meneja" wako wa muda, ninakupa mpaka mwezi wa 9, manuscript ya vitabu vyote viwili iwe tayari, kisa kilichopita pamoja na hiki. In the meantime weka visa vifupi fupi tu, vya kuisha leo leo au within a week.
Manuscript ya kwanza ikiwa tayari unajua wapi pa kunipata utanipa taarifa. Maana nimeona namimi nifanye kama Wakili mwanadada hahahaaa!!
Nashukuru sana Subira kwa wazo lako hilo, na mungu akuzidishie kwa moyo wako huo ....nitakutafuta , tumuombe mungu atupe uhai, nami nitaanza kuifanya hiyo kazi.
Post a Comment