Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, July 12, 2012

Hujafa hujaumbika-67 Hitimisho 25‘Hebu niamie ulijuaje kuwa muuaji ni nani kati ya hawo wawili unaowahisi…wawili eeh, maana wengine hawana sifa hizo….?’ nikamuuliza wakili mwanadada akiwa kachoka, baada ya kutokea mahakamani.  Kesi hii ilibidi ifunguliwe baada ya nesi kugoma kutoa maelezo yake siku ile.

‘Mimi nimeshasemasitaongea lolote,ninachotaka ni haki itendeke ,maana nimeshagundua ujanja wa wakili mwanadada, nia na lengolake ni kutuchimba ili mwisho wa siku apate anachotaka, sasa mimi nimeshituka, na hali ilivyo hapa haki haitatendeka….’akasema nesi baada ya kushikiliwa na polisi.

‘Haki gani unayoitaka, maana hapa ni mazungumzo tu, hatujamnyoseha mtu kidole…’akasema hakimu.

‘Mimi sio mtoto mdogo, na msinione kuwa sina akili ya kuwaza mbali, hali ilivyo hapa inaashiriakuwakuna kitu kinatafutwa, na nahisi ukweli utajificha na mnataka kunikamatisha mimi hayo mauaji, ili munilazimishe nikubali …hapana, maana kesi ipo wazi, mimi nawashangaa, hawo akina dada wawili wana sababu zote, na kauli yao, vietndo vyao,…mnashindwa kuwahoji vyema mnaning’angania mimi….’akasema kwa hasira.

‘Kila mtu alipewa nafasi yake, nab ado tulikuwa tunaendelea, hiyoisikupe shida, na unaweza ukatusaidia kuwauliza maswali, huenda tukajifunza kitu kutoka kwako….’akasema wakili mwanadada.

‘Mimi sio kazi yangu, ila kamaingelikuwa mimi nisingeliwaachia hawo akina dada kirahisi hivyo, waan kila sababu ya kuwa ndio wauawaji…’akasema.

‘Kwa vipi hebu tuambie wewe….?’ Akaulizwa.

‘Kwa vipi  unaniuliza mimi kwa vipi ,wakati wamejieelzea wenyewe, walichukua bunduki ambayo ndioyo iliyotumika kumuua Kimwana, hamjasema kuwa risasi iliyotoka hapo ndio iliyomuua Kimwana?’ akauliza.

‘Sawa ndio iliyomuua Kimwana, lakini uliwasikia wakisema sio wao waliofyatua hiyo risasi, walikimbia na wakiwa mafichoni, mtu mwingine akaja akaitumia hiyo bunduki…’akaseam wakili mwanadada.

‘Toka lini muuaji akakubali kuwa kaua, hata kamakweli kaua, sio rahisi kukubali moja moja kwa moja, maana ukikubali hukumu inatolewa mara moja, na hukumu yake haina mashamaha, ni kuwa umeua kwa kukusudia,…sasa ulitarajia wao wakubali kirahisi hivyo…’akasema nesi.

‘Ndio maana hata wewe hukubali kirahisi ….’akasema wakili mwanadada.

‘Nimesema ndio maana wao wanajaribu kupinga, na kupindisha maneno, lakini vielelezo, kama bunduki, kauli yao kuwa walifika na wakaielekeza hiyo bunduki kumlenga Kimwana,….sasa hapo mnataka nini, ‘akasema huku akitabasamu.

‘Unaweza ukalnga lakini usifyatue risasi, ‘akasema wakili mwanadada.

‘Naona uan maslahi na hawo watu, wewe sasa nakuona ni wakili wao, unawalinda, na ndio maana naona hii ni ksei ya ngedeer imepelekewa nyani, sioni kama kuna uhalalai hapa, naomba kwanza nimuone wakili wangu, na pili hii kesi ipelekeni mahakamani maana njua huko haki itatendeka.’akasema na kutulia.

‘Tukimshitaki nani, kama muuaji?’akaulizwa.

‘Hapa mumemshitaki nani, ninavyoona hapa mimi mumenishikilia kama mkosaji, na ndio maana nataka tuipeleke hii kesi mahakamani, na kama ikithibitika kuwa mimi sio mkosaji kesi itawageukia, ni liazima nikushitaki wewe kwa kunichafulia jina langu….’akasema kwa hasira.

‘Lakini hakuna aliayekushitaki wewe, hakuna aliyekunyoshea kidoela wewe hapa tunaongea, tuanasikiliza maelezo ambayo yatatusaidi kujau ukweli wa hikikifo, bado hatujamnyoshea mtu kidole…’akasema hakimu.

‘Na pia kwenye hiyo kesi, naomna awepo hakimu mwingine….’akasema huku akimwangalia yule hakimu kwa macho yaliyojaa chuki.

‘Hili litafanyika usiwe na shaka kabisa,….ila kwanza tumalize mazungumzo yetu hapa ndani…’akasema hakimu.

‘Mimi msimamo wangu ni ule ule kuwa sitaongea lolote mpaka wakili wangu awepo…’akasema.

‘Basi mimi ninatia kibali kuwa ukamatwe , hadi hapo kesho tutakaposikiliza kesi yako,na mimi sio hakimu nitakayesikiliza kesi yenu, hilo nakuthibitishia….’akasema hakimu.

‘Kukamatwa, kwakosa gani?’ akauliza kwa hamaki.

‘Atakayekukamata atakuambia kwanini unakamatwa, kwa hivi sasa upo chini ya ulinzi, na wakili mkuu, mke wako na rafiki yake, Sokoti na kundi lake, wote mpo chini ya ulinzi…’akasema askari ambaye alifika, muda huo huo akiwa kashikilia kibali cha kuwakamata hao aliowataja.

Kesi ikafunguliwa, na kesho yake wakafikishwa mahakamani.

*********
  Wakili mwanadada akiwa kakaa kwenye sofa lake aliegemeza kichwa chake na akawa kama anawaza jambo , …baadaye akasema;

‘Ukiwa katika kazi hii ya uwakili, au kazi nyingine yoyote, ambayo unaifanya kama wito, yaani unahisi ile kazi kama sehemu yako ya maisha, na unaipenda kazi yako bilkujali maslahi yake….mambo mengine yanakuja kinamna ya kipekee kabisa, lakini hata hivyo, kilichosaidia sana, ni yale mahojiano tuliyoyafanya, …nilishagundua kuwa kwa njia ya mahojiano ndipo utagundua udhaifu wa kila mtu,  …’akasema na kutulia.

‘Kwahiyo kumbe lengo lako lilikuwasio kusaidia bali ni kuchimba watu ili ujueukweli?’ nikamuuliza.

‘Lengolangu toka awali lilikuwa kusaidia, na hata nilipomuona yule hakimu siku nilipomuomba hivyo,nilimuelezea wazi kuwa kuna watu wamejikuta kwenye matatizo,ambayo sio kusudio lao,nilimuomba kuwa awasilikilze maana wao wenyewe wamekubali kukiri makosa yao, na kama kuna uawekano kesi hiii iishie kwakushikana mikono, maana kosa lilitokea hadi kufikia mauji ni kwa bahati mbaya…’akasema wakili mwanadada.

‘Hakimu akakubali kwa maelezo yak ohayo?’nikamuuliza.

‘Hkukubali kabisa, hasa nilipomwambi ainahusiana namauaji ya Kimwana, ila ilibid nimshawishi sana kuwa kama hatasikiliza maneno ya hawo wahusika, kesi kama hiyo inaweza ikachukua muda mrefu na mwisho wasiku hata muuaji hataweza kupatikana,…’akasema.

‘Hakimu akasemaje?’ nikamuuliza.

‘Baadaye sana akakubali nakusema yeye atakuja kama msikilizaji tu,hataweza kutoa maamuzii yoyote, na hata baada ya kusyasikiliza hayo maelezoya mwanzo hatakubali kuiskiliza hiyo kesi tena, ataomba hakimu mwingine aisikilize, ….’akasema wakili mwanadada.

‘Kwanini sasa, wakati yeye ndiye uliyemuoma asikilize maelezo na yeye ndiye atjua ukweli upo wapi?’nikauliza kwa kushangaa.

‘Nilimuambia kwakusikilizamalezo yao, tunaweza kufuchua kilekilichojificha, na kama kuna uwezekano wa kusamehe, baadhi ya watu ambao walijikuta wakiingizwa kwenye kesi hiyo bila kujijua anaweza yeye kama hakimu akatoa shauri hilo kwa hakimu mwenzake…’akasema wakili mwanadada.

‘Lakini huoni hapo ni kama unaingilia mambo ya hakimu?’ nikamuuliza.

‘Mimi ni wakili,na mtetezi wa watu,na mimi ninatetea haki, ninapoonakuwa kuna watu wanaonewa, na hawana hatia, nitatumia kila njia kuhakikisha haki inatendeka, na ndivyo nilivyofanya na nitakavyofanya, kuhakikisha kuwa haki inatendeka, na wale wasio na hatia wanapewahaki yao….’akasema.

‘Mimi bado sijaelewa maana hata huko mahakamani sijaweza kufika, ilikuwaje leo?’ nikamuuliza.

‘Leo hakimu mwenyewe aliniita baada ya kusikilizwa kesi ya leo, akanishika mkono kwa kunipongeza, …sikuamini, maana ni muda sasa tumekuwa tukisumbuliwa na hizi kesi, na mwisho wa siku tunaondoka hakimu akiwa kakasirika, kuwa tunamletea kesi zisizokamilika lakini safari hii alinipa sifa nyingi….

‘Kwahiyo kesi imekwisha na muuaji keshajulikana ?’ nikamuuliza.

‘Kesi haijaishha, ila muuaji  keshajulikana , mwisho wa siku alikuja kukubali mwenyewe..’akasema.

‘Mimi bado sijamjua ni yupi hasa ambaye kaja kukubali mwenywe kuwa ndiye aliyemuua Kimwana, maana wameshikwa wengi kuhusiana na hiyo kesi, na ukasema wawili ndio wahusika wakuu,…na leo unasema huyo mmoja keshakubali kuwa yeye ndiye aliyeua, ni nani na ilikuwaje?

‘Nitakuhadithia tu, usiwe na munkari, ila niligundua kuwa mtu huwa anajishuku mwenyewe, hasa unapomwaga damu ya mtu, ile damu itakuandama tu, na wewe mwenyewe utajikuta nafsini ukijaulumu, kwani binadamu sio mnyama, hajaumbwa kuwa na roho ya kinyama, ila hasira zinapokita kwenye nafsi, pake ile hali ya kibinadamu inaondoka kwa muda….’akatulia kama anawaza jambo .

‘Kwahi unataka kusema kuwa muuaji aliua kwasababu ya hasira, ….mbona hujaniambia ni nani, maana hamu yangu hapa ni kumjua huyo muuaji…’nikasema kwa hamasa.

‘Na hilo ndio kosa,ambalo hata wenzetu wa usalama wanalifanya, kukimbilia kumshuku mtu kuwa yeye ndiye kafanya, yeye ndiye kaua,….hitimisho mara nyingi sio njia sahihi, njia sahihi ni kujua chanzo cha jambo, …kiini cha jambo, sababu ya jambo, na ukilijua hilo, hutakuwa an shaka na hitimisho lako…sijui hapo unanielewa…?’ akaniangalia kwa makini.

‘Lakini hayo tulishayajua , …na tukajua sifa za muuaji wa Kimwana zipoje, na nikiangalia kwa makini, kwawale wahusika pale, yupo Sokoti, maana yeye ni kiongozi na ana mamlaka, nlakini nikagundua kuwa hana shabaha,…kwahiyo yeye namuondoa, nikamchukua, …..eeh, wakili mkuu, nikagundua kuwa licha ya kuwa ana shabaha, ana sababu , lakini hana mamlaka kwenye hilo kundi…..haya hwa akina dada wawili, wote wana shabaha, wanasababu na wana ….ndio wana amri, wangelwieza kuamrisha…..lakini, walikataa, sasa huyu nesi, …..ilikuwaje kwake?’

‘Ndio maana nikakuambia usikimbilie kuataka kunjau huyo mtu, hebu jua kiini cha tukio zima, huyo mtu anaweza akawa na shabaha, anaweza akawa na amri, anaweza akawa na sifa nyingine, lakini kwanini ilifikia hadi huko,…ni wivu wa mapenzi,…au sio’akasema wakili mwanadada.

‘Ndio kama ni wivu wa mapenzi karibu wote wanao huo wivu, na hasa hawa akina dada wawili ambao walikuwa na haki, hasa mke wa wakili mkuu, yeye mume wake alichukuliwa na Kimwana…’akasema.

‘Umesahau kuwa hata wewe ulichukuliwa na Kimwana…’akasema huku akicheka.

‘Ndio nilichukuliwa na Kimwana, lakini nani kati ya wale ambaye atanionea wivu mimi, mke wa wakili mkuu, sina mahusiano naye, rafiki yake, mapaka sasa sijamjua, nesi, ndio kasema alinipenda,lakini sikuwahi kuwa na mahusiano na yeye….’akasema.

‘Nesi alikupenda sana, nay eye akakutana na mtu aliyekupenda zaidi, kwahiyo akaona njia ya kukupata wewe ni kuua njiwa wawili kwa jiwe moja, ….’akasema na kuniangalia kwa makini.

‘Kwa vipi, kama alinipenda, lakini mimi sijawahi kuonegea naye, na wala  sina hisia naye kabisa,….hata kama ni mzuri, lakini hajaigusa nafsi yangu, hawezi akachukua maamuzi yake, eti kwasababu ya wivu, sitamuelewa hata siku moja…’nikasema.

‘Mapenzi ni kitu cha ajabu sana, nina uhakika kama ungelikaa na huyo dada siku tatu tu ungeishia kumpenda na kusema huyu ndiye niliyekuwa nikimataka, ..kwasababuu kwanza yeye ni mjanja, pili umri umekwenda na anahitaji sana mtu wa kuishi naye na anayajua mapenzi, …na anawajau wanume, kilichotakiwa ni kupata muda wa kukaa na wewe, hicho ndicho alichokuwa akikitafuta….’akasema.

‘Mhh, sijui na wala sina uhakika na hilo, ….’nikasema huku nikijaribu kuivuta sura ya huyo nesi, kuona kama kweli ananiingia kwenye nafsi yangu hadi nije nimpende ,sikuweza kuingiwa na hisia zozote nikaema;

‘Hapana sina mvuto naye, wa kihivyo, lakini siwezi jua maana sijawahi kukaa naye kwa karibu na nafsi yangu ikatulia kwa ajili yake,hata hivyo, kwanini yeye umshikilie kama mhusika mkuu, na inavyojulikana yeye aliachwa hospitalini,na wakili mkuu kathibitisha hilo,….’nikasema.

‘Kesho fika mahakamani,utasikia mwenyewe akitoa kauli yake ni kwanini ilifikia hatua hiyo, …’akasema wakili mwanadada.

‘Ina maana kumbe hajakubali kidhahiri..!?’ nikauliza kwa mshangao.

‘Keshoo hiyo, nakuhakikishai kila kitu kitawekwa hadharani,….’akasema na kuinuka, hasa pale alipoaangalia saa yake, huwa huyu dada anajali sana muda na mimi alishaniweka njia panda,nilikwa na maswali mengi ya kumuuliza hasa kuhusu huyo rafiki wa mke wa wakili mkuu.

‘Sasa mbona unaniacha njia panda,vipi kuhusu rafiki wa mke wa wakili mkuu ,ni nani,unajue kila maranamuwaza yeye, sijui kwanini,inafiki hatua naanza kumhisi kuwa anaweza kuwa mtu ninayemjua?’ nikamuuliza.

‘Kama mpaka sasa hujamjua, sitaweza kukusaidia kwa hilo, nakumbuka siku ile ulitaka nikukutanishe na yeye muongee,ukashindwa, na sasa bado unamuwaza, unataka nikusaidieje , nikakutongozee, ….’akasema na kucheka.

‘Sio hivyo,nia na lengo langu ni kutaka kumjua ni nani’nikasema huku nikigeuka pembeni ni kikwepa kumwanglia na nikaweka kidevu changu kwenye sofa kama kujiegemeza, na huku nikiwaza mbali,nikimuwaza mwanadada, ambaye keshaiteka nafsi yangu. Wakili mwanadada akawa ananiangalia kwa huruma, na aliponioana nimegukia upande mwingine kama kumkwepa akasema;

‘Kumjua kuwa ni nani…..kwanini….kwanini utake kumjua yeye peke yake….! Na unauliza kuwa yeye ni nani mbona jibu hilo lipo wazi, yeye ni rafiki wa mke wa wakili mkuu, au jina lake unalihitaji, pale , hautukutaka kutajana majina, mana tulikuwa na maeleo ya awali, lakini kama unahitaji jina alke, j, basi nitakutajia….’akasema wakili mwanadada.

‘Jina lake ni nani…?’ nikauliza na kumgeukiwa kwa haraka, nikiwa na hamasa ya kulijua hilo jina.

‘Jina lake halisi ni Tausi binti Maringo…’akasema na kunifanya moyo wangu ushituke, kwa kulisikia hilo jina.

‘Unasema anaitwa nani?’…nikauliza kwa mshngao huku nimesimama, nikiwa nimemkodolea macho wakili mwanadada.

‘Ukitaka zaidi kesho fika mahakamani,huenda ukapata muda wa kuongea naye, na safari hii usiniangushe, tafadhali…mimi sikujua kuwa hata mwanaume kiwembe kama wewe inafika mahali unajiuma uma kwa mwanamke,…hahaha,kumbe mapenzi ni kitu cha ajabu sana,….’akasema huku akiniangalia kwa uso uliojaa tabasamu.

‘Hilo jina nalifahamu,….mmmh, lakini,….lakini siwezi kuwa na uhakika kuwa ni yeye au sio yeye, maana hawafanani, ….lakini mmh, sura inakuja inatoka…au ndio maana namuwaza sana yeye, inawezakana kweli akawa ndio yeye,….lakini mbona kabadilika kiasi hicho?’ Nikauliza huku nikiwa natembea kama vile nataka kutoka nje.

‘Sasa unakwenda wapi, mbona hatujapanga mipangalio ya kesho?’ akaniuliza.

‘Lazima nikamuone kwanza….’nikasema

‘Ukamuone nani?’ akaniuliza.

‘Tausi binti Maringo…’nikasema.

‘Kwani unahisi ni nani huyo?’ akaniliza.

‘Siwezi kusema mpaka niongee na yeye mwenyewe niisikie kauli yake mwenyewe,…kani dhaman yao imekubaliwa’nikasema.

‘Ndio maana nikasema kwa hali aliyo nayo leo, anahitaji kupumzika, maana dhaman yao ilikubaliwa, niliwaacha wakimalizia mambo ya kiofisini, nilijua watakuwa wameruhusiwa, na sina uhakika, kama …’akaantulia na kuangalai saa yake.

‘Kama ni hivyo….ngoja nikawafuate huko huko nikuje imefikia wapi’nikasema.

‘Utamuona tu, kamasio leo hata kesho,….lakini leo hii, nahisi hutaweza kuongea naye vyema, maana hali aliyo nayo, baaada ya kesi ya leo ,nakauli aliyoisikia toka kwa huyo nesi imemchanganya sana, ingawaje alikuja kuniulizia kwanini huonekani mahakamani…kiujumla ana hamu sana ya kukutana na wewe, safari hii kaniomba yeye mwenyewe kuwa anataka kuongea na wewe….’akasema na kutabasamu.

‘Mbona hukuniambia..ooh, tafadhali naomba nikamuone hii leo…’nikasema na moyoni nilishaahidi kuwa vyovyote iwavyo lazima niende nikamuone,….na mara mlango ukagongwa, na nimuda ule ule nilikuwa nimeshafika mlangoni, nikiwa tayari nimeshanyosha mkono kuufungaua huko mlango,

‘Karibu , fungua…’akasema wakili mwanadada.

Mlango ukafunguliwa,…na moyo wangu wangu ukalipuka paah,….mwili ukafa ganzi, ….nikajikuta nikitoa macho bila kupepesa, …..
  
NB: sehemu hii nimeiandika kwa harakasana leo asubuhi, sijapata muda wa kuipitia huenda ikawa namakosa ya hapa na pale, lakini najua itaeleweka, kama kuna maksoa nifahamishe ili niyarekebishe.

Hapa nilipo ninaanza kuwaza kisa kipya, sijui kama kuna kisa tulikikatizia tukiendeleze au nitoke na kisa kingine kipya,....

WAZO LA LEO: Mara nyingi kila mtu hujiona yeye kuwa sahihi, na yeye ndiye mwenye kazi nyingi sana, yeye ndiye mwenye shida nyingi sana, yeyendiye....kuliko wengine, lakini kumbe huenda wengine ni zaidi yake. 

Ni vyema tukaangalia wenzetu kuwa na wao ni banadamu kama wewe, ulicho nacho, shida uliyo nayo, na wao wanaweza kuwa kama wewe na huenda zaidi yao,..


Ni mimi: emu-three

4 comments :

Anonymous said...

Upo mkuu?

emu-three said...

Nipo mkuu, ila leo mambo ya foleni, jembe na yaliyo juu ya uwezo wangu nimejikuta nikishindwa kufanya lolote! Tuombe mungu, huenda wikiendi hii nikafanya kile kinachoitwa hitimisho.
Hata hivyo nahis kesho niseiku maalumu kwablog hii,...sinauhakika ngoja nichunguze!

Subira said...

Mimi nashauri usiandike kisa kingine chochote kirefu mpaka utoe vitabu viwili kwanza. Kwa sababu unatakiwa uwe busy na manuscript zako kuhakikisha ziko tayari kwa vitabu. Angalia jinsi ya kuandaa manuscript, andaa hizo manuscript, ukiwa tayari nitafute tupublish kitabu kimoja baada ya kingine.

Mimi najitolea kuwa "Meneja" wako wa muda, ninakupa mpaka mwezi wa 9, manuscript ya vitabu vyote viwili iwe tayari, kisa kilichopita pamoja na hiki. In the meantime weka visa vifupi fupi tu, vya kuisha leo leo au within a week.

Manuscript ya kwanza ikiwa tayari unajua wapi pa kunipata utanipa taarifa. Maana nimeona namimi nifanye kama Wakili mwanadada hahahaaa!!

emu-three said...

Nashukuru sana Subira kwa wazo lako hilo, na mungu akuzidishie kwa moyo wako huo ....nitakutafuta , tumuombe mungu atupe uhai, nami nitaanza kuifanya hiyo kazi.